UTAKATIFU KATIKA ROHO-3

 

UTAKATIFU KATIKA ROHO-3

UTANGULIZI

Nilipokuwa nikifanya bidii kuandika kwa habari ya utakatifu katika nafsi niliona moyoni mwangu imenilazimu kuendelea kuandika kuhusu utakatifu katika roho; maana hayo ndiyo maisha yetu, ukizingatia kwamba sisi ni roho, tuna nafsi, na tunaishi kwenye mwili. Lakini pia chochote tunachofanya nafsini, na kwa miili yetu huwa kinafanywa kwa roho fulani: hakuna tendo linalofanywa pasipo roho fulani kuwa nyuma yake. Tendo linatendwa rohoni kwanza kabla halijatendwa mwilini.

Mfano Biblia inasema, “11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

14Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 15Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.” (1Yohana 3:11-12, 14-15)

>> KAINI ALISHAMUUA ABEL NDUGUYE MOYONI MWAKE KWA CHUKI YAKE, SIKU NYINGI KABLA HAJATEKELEZA MAUAJI YALE KWENYE MWILI. KWA HIYO ALIUA KIROHO KABLA HAJAUA KIMWILI.

Bwana wetu Yesu alisema, “27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:27-28)

>> UKIMTAZAMA MWANAMKE KWA KUMTAMANI UMEKWISHA KUZINI NAYE MOYONI MWAKO. YAANI, UMEZINI MOYONI/ROHONI MWAKO KABLA HUJAZINI MWILINI.

>> DHAMBI HUWA INATENDWA ROHONI AU MOYONI MWAKO KWA ULE TU UWEPO WA ILE roho ya dhambi MOYONI (ROHONI MWAKO)

>> TABIA YA roho NI KWAMBA HUWA INASEMA MANENO YAKE, INAWAZA MAWAZO YAKE, NA INATENDA MATENDO YAKE WAKATI WOTE! ROHO MTAKATIFU HUWA ANAONGEA MAWAZO YAKE NA MANENO YAKE, WAKATI WOTE! ROHO ZA SHETANI NAZO HUWA ZINAONGEA MAWAZO YAKE NA MANENO YAKE WAKATI WOTE! UKIPITA MAHALI PENYE ROHO FULANI YA UOVU HUWA UTAYASIKIA MAWAZO YAKE HIYO ROHO. ROHO HUWA INARUSHA MAWAZO WAKATI WOTE! MAWAZO YA ROHO HUWA NDIO USHAWISHI WA HIYO ROHO. SIYO TU KUYASIKIA BALI UTAYAONA KATIKA ROHO MAWAZO NA MATENDO YA HIYO ROHO YA UOVU KWA NAMNA MBALIMBALI. MUNGU ASHUKURIWE, ATUPAYE KUSHINDA KILA SIKU KWA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI YESU.( (1 Wakorintho 15:57) TUNAYO MAMLAKA YA KUZIKEMEA, KUZIFUNGA, KUZIKATAA, KUZIVUNJA, KUZING’OA HIZO ROHO, NA KUHARIBU KAZI ZAKE ZOTE. KWA KUWA MWANA WA MUNGU ALIDHIHIRISHWA ILI KUZIVUNJA HIZO KAZI ZA SHETANI ZOTE.(1 Yohana 3:8) NA HII NDIYO MAANA TUMEAGIZWA KWA NENO LA BWANA KUVAA SILAHA ZOTE ZA VITA ILI KUWEZA KUZIPINGA HILA ZA HIZO ROHO CHAFU NA OVU ZA SHETANI NA KUUTUNZA UTAKATIFU WETU.

“10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;” (Waefeso 6:10-18)

>> SIONGELEI VITA VYA KIROHO ILA NATAKA UZINGATIE MSTARI WA 18; “KWA SALA ZOTE NA MAOMBI MKISALI KILA WAKATI KATIKA ROHO, MKIKESHA KWA JAMBO HILO NA KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE.”

>> .... “KILA WAKATI KATIKA ROHO”....... “MKIKESHA”........... “NA KUDUMU”........!! HAYA NI MANENO MAKUU YANAYOONYESHA KWAMBA HAKUNA WAKATI UNAPOTAKIWA KUACHA KUWA KATIKA ROHO AMA KUENENDA KATIKA ROHO!!!! KWA KUWA ADUI ANASHAMBULIA WAKATI WOTE!! ANARUSHA MISHALE YA MOTO WAKATI WOTE! HAKUNA ROHO INAYOPUMZIKA, AMA KULALA, AU KUSINZIA. ROHO HUWA HAICHOKI, HAILALI, NA WALA HAISINZII! HIVYO NI LAZIMA KUKESHA NA KUENENDA KWA ROHO.

MAELEZO HAYA YAMEKUWA NI YA MUHIMU ILI KUONYESHA UMUHIMU WA KUENENDA KATIKA ROHO

KUISHI NA KUENENDA KWA ROHO

Biblia inasema,

>> “16Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.” (Wagalatia 5:16)

>> “25Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” (Wagalatia 5:25)

>>  WATAKATIFU WALIONUNULIWA KWA DAMU YA YESU HUISHI NA KUENENDA KWA ROHO

>> WANAPOENENDA KWA ROHO HAWAWEZI KAMWE KUZITIMIZA TAMAA ZA MWILI

>> WANAPOISHI KWA ROHO HUWA WANAYATENDA MAPENZI YA ROHO YALIYO SAWASAWA NA NENO LA KRISTO

Kuenenda kwa Roho Mtakatifu ni kuenenda kwa neema yake Kristo. Na kama tulivyoona katika somo lililotangulia huko ni kuenenda kwa Roho Mtakatifu na Nguvu zake, sawasawa na Neno la Uzima, kupitia imani yako iliyo hai kwa Yesu Kristo aliyefufuka kutoka kwa wafu.

Tunaweza kuonyesha kwa kielelezo mtiririko wa kuenenda kwa Roho Mtakatifu kwa mwana wa Mungu jinsi kulivyo ili kurahisisha uelewa wetu wa jambo hili muhimu katika maisha yetu ya kiroho .

LAZIMA LIWEPO NENO AU ANDIKO LILILOTANGULIA KUHUBIRIWA, KUFUNDISHWA, AU KUSOMWA.

   

   

LAZIMA NENO AU ANDIKO HILO LIAMINIWE NA KUPOKELEWA MOYONI

 

ANDIKO AU NENO HILO LINAKAA SASA MOYONI KAMA ROHO BAADA YA KUAMINIWA NA KUPOKELEWA MOYONI. YAANI, ROHO YA HILO NENO AU ANDIKO

 

KWA KUWA NENO LA KRISTO NI ROHO NA TENA NI UZIMA (YOHANA 6:63); SASA MWAMINI ANA UZIMA, AU UHAI, AMA MAISHA YA HIYO ROHO, AMA HILO NENO

SASA MWAMINI ANALIISHI NENO HILO ALILOLIAMINI KWA NGUVU ZA HIYO ROHO YA HILO ANDIKO LILILOMO MOYONI MWAKE. HUYU NDIYE MWENYE KULITENDA NENO. HUYU NDIYE ANA ILE “IMEANDIKWA...” YA YESU (MATHAYO 4:4, 7, 10) MOYONI MWAKE, INAYOMPA USHINDI KWENYE VITA VYOTE, MAANA NI UPANGA WA ROHO KINYWANI MWAKE. (WAEFESO 6:17)

HUYU NDIYE AMBAYE HAISHI KWA MKATE TU, BALI ANAISHI KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA BWANA ( MATHAYO 4:4)

>> Kuenenda kwa Roho maana yake huyo Roho Mtakatifu “133 Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako,

Uovu usije ukanimiliki.” (Zaburi 119:133) ANAZIELEKEZA HATUA ZAKO KWA NENO LAKE, NA UOVU HAUWEZI KAMWE KUKUMILIKI!!!

-HII MAANA YAKE NI KWAMBA ANAZIONGOZA HATUA ZA MOYO WAKO; HATUA ZA MOYO WAKO NI YALE MAKUSUDIO NA MAAZIMIO YA MOYO WAKO; YAANI, KULE KUNIA KWAKO AMA KUTAKA KWAKO KUTENDA!! ANAKUPA KUFANYA HAYO KWA ILE ROHO YA NENO ILIYOMO MOYONI MWAKO AU KATIKA ROHO YAKO NA NGUVU ZAKE. HIVYO UNAKUSUDIA AU KUAZIMIA AMA KUNIA KULITENDA NENO, NA UNALITENDA KWA NGUVU ZA HIYO ROHO YA HILO ANDIKO AU NENO UNALOKUSUDIA KULITENDA. NDIYO MAANA PAULO AKAANDIKA, “13Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” (Wafilipi 2:13)

>> ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAKUPA KUTAKA, KUNIA, AMA KUKUSUDIA NDANI YA NENO, AU KATIKA NENO, AMA SAWASAWA NA NENO

>> NA KISHA ROHO HUYO HUYO NDIYE ANAYEKUPA KUTENDA (KUKUONGOZA KUTENDA) YALE ULIYOKUSUDIA MOYONI MWAKO

>> ROHO HUWA ANAFANYA HAYO KWA KADIRI YA VILE ULIVYOJAA ROHO YA NENO!!! MAANA ANAPOSEMA NENO LA KRISTO LIKAE KWA WINGI MOYONI MWAKO (WAKOLOSAI 3:16), ANAMAANISHA ULIAMINI NENO KWA WINGI MOYONI MWAKO ILI UJAE ROHO KWA HILO NENO! KWA MAANA KWA MOYO MTU HUAMINI (WARUMI 10:10) KULE.NENO KUKAA KWA WINGI MOYONI MWAKO SIYO TU KUJAA MAANDIKO ULIYOYAKARIRI KICHWANI MWAKO!! BALI UNAJAA ROHO, ROHONI MWAKO, KWA HAYO MANDIKO, MAANA ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA!!! (2 WAKORINTHO 3:6)

“18Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;” (Efe 5:18)

“...............BALI MJAZWE ROHO” (Efe 5:18)

>> AMINI NENO.......JAA ROHO YA NENO.....AMINI NENO..........JAA ROHO YA NENO.......!!! JAA ROHO MTAKATIFU WA BIBLIA MPAKA NDANI YAKO KUWE NA NURU TUPU NA PASIWEPO GIZA ENEO LOLOTE KAMA ALIVYOSEMA BWANA WETU YESU.

“34 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza. 35Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza. 36Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa mwanga wake.” (Luka 11:35-36)

>> JICHO ANALOONGELEA BWANA YESU HAPA NI LILE JICHO LA MOYONI; JICHO LA MOYONI NI ILE ROHO YAKO MWANADAMU; KAMA UKIWA NA MOYO SAFI MAANA YAKE MACHO YAKO YAKO SAFI (PURE EYES ARE THERE WHEN THERE IS A PURE HEART); MOYO UKIWA SAFI MAANA YAKE ROHO YAKO NI SAFI (PURE SPIRIT/holy spirit) UTAKATIFU WAKO UNAANZA KATIKA ROHO YAKO. ROHO YAKO (JICHO LAKO) IKIWA SAFI NDIPO MWILI WAKO WOTE UTAKUWA SAFI; KUMBUKA MWANADAMU = [(ROHO +NAFSI) + MWILI] ROHO ISIPOKUWA SAFI , NAFSI YAKO HAIWEZI KUWA SAFI, NA MWILI WAKO HAUWEZI KUWA SAFI PIA;

Biblia inasema pia;

“27Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA;

Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.”  (Mithali 20:27)

>>PUMZI YA MWANADAMU NI TAA YA BWANA! THE PURER YOU ARE, THE BRIGHTER YOU SHINE!! (KADIRI ULIVYO SAFI ZAIDI, VIVYO HIVYO UTAANGAZA ZAIDI ULIMWENGUNI)

>> NURU AU MWANGAZA HAPA NI ULE WA UTUKUFU WA MUNGU ALIYEMO NDANI YAKO KWA ROHO MTAKATIFU; UTUKUFU MAANA YAKE NI UTAKATIFU WA PENDO LAKE MUNGU!! (THE HOLINESS OF HIS LOVE!!!)

>> MUNGU ANATAKA UANGAZE KWA NURU YA UZIMA ULIOMO ROHONI MWAKO, KAMA ILIVYOANDIKWA, “NDANI YAKE (NENO) NDIMO ULIMOKUWA UZIMA, NAO ULE UZIMA ULIKUWA NURU YA WATU.” (YOHANA 1:4)

>> UNAANGAZA KWA KADIRI YA NURU ULIYONAYO YA UTAKATIFU WA BWANA! GIZA MWILINI WAKO NI KWENYE MAENEO YALE USIYOMWAMINI BWANA BADO, NA HIVYO UNA GIZA BADO NDANI YAKO. NDIYO MAANA YESU ANASEMA;

“35Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza. 36 Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa mwanga wake.” (Luka 11:35-36)

>> KAMA HAKI YA MUNGU HAIDHIHIRISHWI NDANI YAKO TOKA IMANI HATA IMANI KAMA MAANDIKO YASEMAVYO (WARUMI 1:17),  INA MAANA HAUONGEZEKI KIIMANI; NA KAMA HAUONGEZEKI KIIMANI HAUONGEZEKI KWA NENO LINALOKAA MOYONI MWAKO KWA IMANI; HII MAANA YAKE HAUJAI ROHO; NA KWA KUWA ROHO YAKO NI TAA YA BWANA INA MAANA MWANGA ULIO NDANI YAKO HAUONGEZEKI; NA KAMA MWANGA WAKO HAUONGEZEKI INA MAANA UMEDUMAA NA HOUNGEZEKI KATIKA UTAKATIFU WA BWANA; YAANI, HAUMZALII MUNGU MATUNDA; HUU NI UTASA KIROHO; USIPOANGALIA MWANGA ULIO NDANI YAKO UNAWEZA KUZIMIKA NA GIZA KUTAWALA. BWANA WETU YESU AMETOA TAHADHARI. LAZIMA UHAKIKISHE KWAMBA KILA SEHEMU KATIKA MWILI WAKO IWE NA NURU; NA UNAFANYA HIVYO KWA KUITII KWELI AMBAYO ULIKUWA HAUJAITII KABLA;

“MKIISHA KUJITAKASA ROHO ZENU KWA KUITII KWELI......” (1 PETRO 1:22)

HUKO NDIKO KUJITAKASA; YAANI, KUHAKIKISHA KWAMBA HAUNA SEHEMU ILIYO NA GIZA; KUJITAKASA NI KUHAKIKISHA KWAMBA MWANGA UMEENEA KATIKA MWILI WAKO WOTE! MAISHA YA UTAKASO NI MAISHA YA KUHAKIKISHA KWAMBA UNAONDOA GIZA KATIKA ROHO, NAFSI, NA MWILI WAKO WOTE; IMANI YA YESU NDIYO INAYOSAFISHA MOYO (MATENDO YA MITUME 15:9) USAFI WA MOYO NDIO USAFI WA ROHO YAKO; KUJITAKASA NI KUONDOA UCHAFU WA ROHO, UCHAFU WA NAFSI; NA UCHAFU WA MWILI.UCHAFU NDIO UNAOLETA GIZA.

“ Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho huku tukitimiza utakatifu katika kumcha bwana.” (2 Wakorintho 7:1)

>> NENO LA MUNGU LINAPOTUJIA KWA ROHO MTAKATIFU SISI TULIOOKOKA LINATUTAKA TUJITAKASE AU KUFUA MAVAZI YETU KAMA MAANDIKO YASEMAVYO;

“”Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” (Ufunuo 22:14)

>> KUJITAKASA NI KUFUA MAVAZI YAKO ILI YAZIDI KUWA SAFI, NA UZIDI KUFANANA NA BWANA WETU YESU KRISTO; MWISHO WA UTAKASO WETU NI KUINGIA KATIKA MALANGO YA YERUSALEMU WA MBINGUNI, ULE MJI WA WATAKATIFU TULIOANDALIWA WATEULE, WATAKATIFU, WANA WA MUNGU. USIJIONE UMEJUA KILA KITU ETI KWA SABABU YA HUDUMA, AU UPAKO, AU UMRI WA WOKOVU, AU CHEO KANISANI, N.K.

Wengi utakuta ni wachafu kwenye vinywa vyao; ni wasengenyaji, walalamikaji, waongo, wasingiziaji, wazushi, wabishi, n.k. Wengine wanapenda fedha, wanatoa rushwa, wanapokea rushwa, wanashitakiana ndugu kwa ndugu mahakamani kwa sababu ya fedha, wanagombea vyeo hata kupelekana mahakamani, wanapeana talaka kwenye ndoa, wanasemana vibaya; Wengine wanasalitiana ndugu katika Kristo, wanapenda kuwa wa kwanza, bado ni wabinafsi, ni wachoyo, ni wabahili; Wengine bado ni wezi, ni wazinzi; wengine wamerudi nyuma, wamepoa, wameigeukia dunia, wanapenda anasa, hawapendi suluhu, wanachukiana, wanabaguana, wanadharauliana; wengine bado wana ukabila, wana ubaguzi wa rangi, wana madaraja ya waliosoma na wasiosoma, wenye pesa na wasio na pesa, walio navyo na wasio navyo, n.k. LAKINI WATU HAWA WALIMWAMINI YESU; IMEKUWAJE MPAKA WAKAFIKIA KUWA WAOVU KIASI HIKI??? WALIACHA KUMWAMINI MUNGU! WALIACHA KUISHI NA KUENENDA KWA IMANI; WAKAMHUZUNISHA ROHO MTAKATIFU; WAKADHARAU NA KUYAPUUZA MAONYO; WAKAZIDI KUHARIBIKIWA MAANA WAKAFIKIA SASA KUMPINGA ROHO MTAKATIFU; WENGINE WAMEKWENDA MBALI ZAIDI MPAKA KUFIKIA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU, INGAWA SI WENGI; WENGI WAMEMWACHA YESU, ILA NEEMA YAKE BADO INGALIPO, MAANA REHEMA ZAKE HAZIKOMI!!! UNAWEZA KUTUBU NA KURUDI KWA ROHO MTAKATIFU NA NENO LAKE, NA NGUVU ZAKE!!

>> UAMSHO UNATOKEA PALE MTENDA DHAMBI ANAPOACHA KUJIHESABIA HAKI, AKATUBU KWA KUMAANISHA KUZIACHA DHAMBI; AKAAMUA KUMRUDIA BWANA YESU ALIYEMWACHA KWA KULIACHA NA KULIPUUZA NENO; AKATUBU NA KUANZA TENA KUENENDA KWA ROHO MTAKATIFU NA KUIPA DUNIA KISOGO; MAANA WENGI WAMEMWACHA BWANA YESU NA KUIPENDA DUNIA HII MBOVU YA SASA (WAGALATIA 1:4) INAYOWAYAWAYA KAMA MACHELA NA KULEWALEWA KAMA MLEVI (ISAYA 24:1-20)

NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO IKO HIVI;

1) NENO LA KRISTO HUPELEKEA>>> (2) IMANI YA KRISTO AMBAYO HUPELEKEA>>> (3) NEEMA YA KRISTO AMBAYO HUPELEKEA>>> (4) MAISHA YA KRISTO NDANI YAKO MWAMINI

>> Kila andiko ni takatifu; kila roho ya andiko ni takatifu; kila unapojaa roho ya andiko unazidi kujaa utakatifu wa Kristo  kupitia lile andiko; utakatifu wa andiko ni nguvu na maisha ya lile andiko uliloliamini; hiyo roho na nguvu zake hukuwezesha wewe kuishi na kutenda kama vile andiko lisemavyo; roho ya andiko ndiyo inayokufananisha na Yesu; ukiamini roho inaingia ndani yako na kuunganika na roho yako. Yaani, ile roho inakuwa sehemu ya wewe kwa sababu wewe ni roho, na ile nayo ni roho. Hivyo nguvu za Roho Mtakatifu ndizo zinazounganisha roho yako na roho ya hilo andiko. Ukiunganika na andiko unakuwa roho moja na andiko au neno. Unakuwa mmoja na Yesu. Unakuwa mmoja na Neno. Unapoongea neno unakuwa unaongea kana kwamba unasoma kilichoandikwa kwenye kibao cha moyo wako. Roho Mtakatifu hukusaidia kunena neno lake ambalo limo moyoni mwako au rohoni mwako.

>> (Roho Mtakatifu + roho yako) + roho ya andiko + nguvu za roho ya andiko) = ALIYE NDANI YAKO NI MKUU KULIKO YEYE ALIYE KATIKA DUNIA HII (1 Yohana 4:4)

>> Ile roho ya andiko ndiyo inayokunenepesha roho yako na kukutia nguvu.

>> Roho Mtakatifu + roho yako = WEWE

>> Hivyo [WEWE + roho ya andiko na nguvu zake ]= ALIYE NDANI YAKO NI MKUU KULIKO ALIYE WA DUNI A HII

>> (roho ya andiko na nguvu zake) = Imani na ndiyo unayoipata wewe kutoka kwenye neno la Mungu ulilolisoma au ulilolisikia na kuliamini. Kama Waebrania asemavyo.

“ Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, KWA SABABU HALIKUCHANGANYIKA NA IMANI NDANI YAO WALIOSIKIA.” (Waebrania 4:2)

>> YAANI, WALILISIKIA NENO LAKINI HALIKUWAFAA KWA NAMNA YOYOTE! KWA NINI?

>> KWA SABABU HALIKUCHANGANYIKA NA IMANI NDANI YAO WALIOSIKIA!! KUMBE NI LAZIMA NENO LILE UNALOLISIKIA LICHANGANYIKE NA IMANI NDANI YAKO!!!

Hapo  juu tumesema; WEWE + roho ya andiko na nguvu zake = Aliye ndani yako ni Mkuu kuliko yeye aliye wa dunia hii. Tukasema, Imani = roho ya andiko na nguvu zake, na sasa tukichukua neno IMANI badala ya roho ya andiko na nguvu zake tunapata;

[WEWE + IMANI = ALIYE NDANI YAKO NI MKUU KULIKO WA DUNIA HII] HAPA NDIPO WAEBRANIA 4:2 INATIMIA. YAANI, LILE NENO LIMECHANGANYIKA NA IMANI NDANI YAKO WEWE ULIYEAMINI!

WEWE ULIYEAMINI: Roho ameunganika na roho yako, na lile neno uliloliamini limekuwa roho ndani yako; na kama tulivyosema nguvu za Mungu, au hata za adui, sikuzote  zimo kwenye roho. Kwa hiyo tukisema roho ya andiko basi ni pamoja na nguvu zake. KWA HIYO NI WEWE NA IMANI MOYONI MWAKO= UTUKUFU WA MUNGU KUONEKANA NA KUDHIHIRIKA

WEWE + IMANI MOYONI MWAKO = UTUKUFU WA MUNGU KUDHIHIRIKA

“Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” (Yohana 11:40)

>> UNAPOAMINI UNAUNGANIKA NA NENO NA NGUVU ZAKE, NA UNAUNGANIKA PIA NA MAKUSUDI, MALENGO, NA NIA YA HIYO ROHO YA HILO NENO; HIVYO NGUVU ZAKE HIZO ZINAKUPELEKEA WEWE KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU YOTE YALIYOMO KWENYE HILO NENO; MAPENZI AMBAYO SASA YAMEKUWA NI YAKO WEWE; HIVI NDIVYO UNAVYOLITENDA NENO!!! UKIAMINI NI LAZIMA ULITENDE NENO. HUWEZI KUAMINI HALAFU USILITENDE NENO. HAKUNA ANAYEAMINI HALAFU ASILITENDE NENO LA MUNGU. KAMA HULITENDI NENO LA MUNGU, MAANA YAKE HAUAMINI!!! NA KULITENDA NENO KUNAANZA KATIKA ROHO SIKUZOTE. KANUNI NI KWAMBA LAZIMA UTENDE KATIKA ROHO KWANZA KABLA HUJATENDA KATIKA MWILI. AMINI TU!!!!

 

TUKUTANE KATIKA SEHEMU IJAYO YA SOMO HILI

UBARIKIWE SANA NA BWANA YESU.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post