20 Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli.
Wafilipi 2:20
21 Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.
Wafilipi 2:21
● MAANA WOTE WANATAFUTA VYAO WENYEWE , SIVYO VYA KRISTO YESU! Malengo yao, mipango yao, makusudi yao, n.k. VYAO, YAO, NA SI VYA YESU AU YA YESU. Hawa ndio humaliza mwaka kwa sala nyingi na maombi eti Mungu awafanikishe katika yale waliyoyapanga na kuyakusudia wao!! Je! huwa wanajibiwa??!!
James 4:3 (NLT) And even when you ask, you don’t get it because your motives are all wrong—you want only what will give you pleasure.
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Yakobo 4:3
1. Wanaomba lakini hawapati.
2. Hawapati kwa sababu wanaomba vibaya. Kivipi?
3. Wanaomba ili wavitumie kwa tamaa zao. Wanaomba KIUBINAFSI ( SELFISHLY) na WANATAWALIWA NA TAMAA
B: MALENGO YA MUNGU KWA MWAKA MPYA
Maandiko yanasema kwa habari za Yesu Kristo Mwokozi wetu ya kwamba:
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
2 Wakorintho 5:15
● YESU KRISTO BWANA WETU ALIKUFA KWA AJILI YETU, AU BADALA YETU, AU MAHALI PETU PALE JUU MSALABANI
● KWA KUFANYA HIVYO ALIKUWA AMEIBEBA YEYE NA KUISTAHIMILI HUKUMU AU ADHABU YA DHAMBI ZETU SISI MAANA YEYE HAKUTENDA DHAMBI
● HIVYO GHADHABU YA MUNGU IKAWA IMETEKELEZWA JUU YA MWANAWE PEKEE YESU NA SISI WANADAMU TUKAWA TUMEEPUSHWA NA HUKUMU HIYO YA KUTISHA
● ALIFANYA HIVYO KWA KUWA YEYE NI UPENDO! HAIKUWEZEKANA MAUTI IMSHIKE NA HIVYO ALIFUFUKA!
● AKAWA AMEIHARIBU MAUTI ILIYOKUWA IMETAWALA TANGU ADAMU!
● AKAWA PIA AMEMHARIBU IBILISI ALIYEKUWA NA NGUVU YA MAUTI NA KUTUWEKA HURU SISI TULIOKUWA TUMEFUNGWA MAISHA YETU NA HOFU YA MAUTI!!!
● DAMU ALIYOIMWAGA MSALABANI ILIKUWA NI DAMU YA MWANAKONDOO WA MUNGU ALIYEICHUKUA DHAMBI YA ULIMWENGU! DAMU HII YA THAMANI NDIYO INAYOTUSAFISHA MIOYO YETU PALE TUNAPOMWAMINI NA KISHA KUMPOKEA MIOYONI MWETU KAMA BWANA NA MWOKOZI WETU, TUKIISHA KUZIUNGAMA NA KUZITUBIA DHAMBI ZETU ZOTE KWAKE YESU.
● TUKO HURU SASA MBALI NA DHAMBI NA TU MALI YAKE MAANA AMETUTUNUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE! Yohana 1:29, Warumi 5:6-21, 2 Wakorintho 5: 17-21, Waebrania 2:14-15, Waebrania 9:14,
SISI TULIOMWAMINI YESU NI MALI YAKE NA TUNAISHI KWA AJILI YAKE YEYE TU!
14 Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;
2 Wakorintho 5:14
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
2 Wakorintho 5:15
>> YESU ALIKUFA KWA AJILI YA WOTE WENYE MWILI
>> WALE WANAOMWAMINI ANAKUWA AMEWALIPIA DENI LA DHAMBI ZAO!! MAANA IMEANDIKWA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI (WARUMI 6:23)
18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
1 Petro 1:18
19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
1 Petro 1:19
20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;
1 Petro 1:20
● BEI ALIYOTUNUNULIA YESU KUTOKA MAUTINI, KUTOKA KUZIMU, KUTOKA GIZANI, KUTOKA DHAMBINI N.K. NI DAMU YAKE MWENYEWE!! ALIUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YETU ILI ATUPE MAISHA MAPYA YASIYOHARIBIKA AU UZIMA WA MILELE!!
7 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.
Yohana 10:7
9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
Yohana 10:9
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Yohana 10:10
11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Yohana 10:11
17 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
Yohana 10:17
18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Yohana 10:18
Kama sisi ni wake lazima tuishi kwa ajili yake!! Hatuna mipango yetu wenyewe bali mipango yake! Hatuna mawazo yetu wenyewe bali mawazo yake! Hatuna maneno yetu wenyewe bali maneno yake! Hatuna matendo yetu wenyewe bali matendo yake! Hatupo kuyafanya mapenzi yetu wenyewe bali mapenzi yake yaliyomo kwenye neno lake!!!
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
Isaya 55:8
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Isaya 55:9
10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
Isaya 55:10
11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Isaya 55:11
12 Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
Isaya 55:12
>> Hatuwezi kwenda pasipo uongozi wake, ruksa yake, na kibali chake! Tunaongozwa na Roho wake Mtakatifu (Rum 8:14) maana tu watoto wake tuliozaliwa mara ya pili (Yohana 3:3-7&Tito 3:3-7)!! Tunaishi kwa kila neno litokalo katika kinywa chake (Mathayo 4:4), na tu watendaji wa neno (Yakobo 1:22-25)! Maisha yetu yamo kwenye neno lake (Yohana 1:4)! TUMEZALIWA MARA YA PILI KWA NENO NA TUNAISHI KWA NENO LAKE HILO! NA PASIPO YEYE HATUWEZI NENO LOLOTE
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Yohana 15:5
>> SISI TUMO NDANI YAKE NA YEYE YUMO NDANI YETU!! LAKE LOLOTE NI LETU!!
10 Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.
1 Samweli 3:10
>> SIKU ZOTE TUNAMSIKILIZA NA KUMTII YEYE! AKISEMA TUNATENDA!! WAKATI WOTE MA MAHALI POTE TUNAMWABUDU NA MAISHA YETU YANAMPENDEZA YEYE YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU!!! GLORY! HALLELUJAH!
Tags
MAFUNDISHO