UTAKATIFU KATIKA ROHO-2
JINSI YA KUISHI MAISHA MATAKATIFU
Tumetoka kuona kwenye utangulizi wetu kwamba unapookoka unakuwa umezaliwa ukiwa mtakatifu. Tuliona Daudi akitufundisha pia kwamba, sababu kwa nini alitenda dhambi, ni kwamba ;
1) ALIUMBWA TUMBONI MWA MAMA YAKE KATIKA HALI YA UOVU; NA
2) MAMA YAKE ALICHUKUA, AU KUBEBA MIMBA YA DAUDI AKIWA HATIANI MBELE ZA MUNGU.
>> Hii ni Zaburi ya 51:5 “ Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.”
Na kwenye zaburi ya 58:3 anasema; “ Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea wakisema uongo.”
1) WASIO HAKI WAKO HIVYO TANGU MATUMBONI MWA MAMA ZAO
>> Hii maana yake roho ya kutoamini na ya kutomcha Mungu ziliingia na kuanza kuwatumikisha dhambini tokea tumboni. Yesu aliposema atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yohana 8:34) alimaanisha utumwa wa dhambi ulianzia tumboni mwa mama yako. Yaani, mimba yako ilitungishwa na roho ya dhambi! Maandiko yanasema roho itendayo dhambi imekufa (Ezekieli 18:4,20) Hii ina maana mama mjamzito mtenda dhambi roho yake imekufa, kwa maana haina uhai wa Mungu au uzima wa Mungu, ama maisha ya Mungu ndani yake! Hii inamaanisha roho yake imefarakana na Mungu kama ilivyo kwa wanadamu wote watendao dhambi. Hivyo anapobeba ujauzito ile mimba inayotungwa huwa inatungwa katika hali hiyo ya mauti, yaani, hali ya kutokuwa na uhai wa kiroho inayotokana na kutokuwa katika uhusiano mzuri na Mungu Mtakatifu aliye Roho! Ukimwamini na kumtii Mungu Mtakatifu Yeye anakufanya uwe hai; ukimwasi na kumkataa unakuwa mfu kwa maana roho yako imekufa! Kuokoka ni kufanywa hai tena au kupewa maisha mapya baada ya kutubu na kuiamini Injili! (Marko 1:15) Hii ina maana unahuishwa, ama unafanywa hai tena, au unafufuliwa kutoka kwenye mauti ya kiroho na kuwa hai tena roho yako.
2) WASIO HAKI WAMEJITENGA TANGU KUZALIWA
>> Kutokuwa mwenye haki ni kuwa mtenda dhambi usiyemwamini wala kumcha Mungu wala kumtumainia kwa namna yoyote! Tangu Anguko la Adamu wanadamu wote wanazaliwa wakiwa ni WASIO HAKI mbele za Mungu! JUHUDI AU BIDII YOYOTE LEO YA KIIMANI, AU KIDINI, AU KIMADHAHEBU, ISIYOKUBALI KUOKOKA NA KUWA KIUMBE KIPYA MWENYE MOYO MPYA NA ROHO MPYA, KWA KUMWAMINI YESU KRISTO PEKEE, HAISAIDII KUMTOA DHAMBINI NA MAUTINI MWANADAMU AWAYE YOTE MAANA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI (WARUMI 6:23a) KWA MAANA KUSUDI LA AGANO JIPYA NI KULETA ULIMWENGUNI VIUMBE WAPYA KUPITIA IMANI YA YESU KRISTO ALIYEKUFA AKAFUFUKA KWA AJILI YAO !!
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” (2 Wakorintho 5:17)
Imeandikwa pia;
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi;nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.Nami nitawapa ninyi moyo mpya,nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.” (Ezekieli 36:25-26)
>>AGANO JIPYA LIMEKUSUDIWA KULETA VIUMBE WAPYA WENYE MIOYO MIPYA NA ROHO MPYA [Kiumbe kipya = moyo mpya + roho mpya] YA KALE YAMEPITA TAZAMA, YAMEKUWA MAPYA
>> MAISHA YA KALE YA KUTAWALIWA NA DHAMBI NA KUISHI KWENYE UASI WA KWELI YAMEPITA, NA SASA YAMEKUWA MAPYA! MAISHA MAPYA YA UTAKATIFU, HAKI, NA KWELI!!!
BWANA WETU YESU AMEKUJA KULETA BADILIKO LA KWELI LA MOYO KWA KUKUPA ROHO MPYA!! YAANI, AMEKUJA KUKUBADILISHA WEWE MWANADAMU AMBAYE NI roho mwenye nafsi na unaishi kwenye mwili!!! [Mwanadamu = (roho +nafsi) + mwili]
>> HII NI HATUA YA KWANZA YA KUKUPA MOYO MPYA NA ROHO MPYA AMBAPO SASA UMEKUWA KIUMBE KIPYA, MTAKATIFU MWANA WA MUNGU!!! ULIYEZALIWA MARA YA PILI KWA MAJI NA ROHO (YOHANA 3:3-7)
>> HATUA YA PILI BAADA YA KUFANYWA KUWA KIUMBE KIPYA NI KUUNGANISHWA NA BWANA MUNGU MWENYEZI MWENYEWE KATIKA ROHO KWA NJIA YA YESU KRISTO
“Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.” (1 Wakorintho 6:17)
>> Unaungwa na Bwana Yesu na kuwa roho moja naye pale UNAPOMPOKEA ROHO MTAKATIFU KWENYE UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NA MOTO (Mathayo 3:11) Biblia inasema, “LAKINI MTAPOKEA NGUVU AKISHA KUWAJILIA JUU YENU ROHO MTAKATIFU...........” (Matendo ya Mitume 1:8)
Na tena;
“Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.” (Matendo ya Mitume 2:38)
>> NABII EZEKIELI NAYE ALITABIRI KWAMBA MUNGU ANGETIA ROHO YAKE NDANI YA WATEULE WAKE
“26Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” (Ezekiel 36:26-27)
>>MST 26: KUZALIWA MARA YA PILI
>>MST 27: KUUNGANISHWA NA ROHO WA MUNGU ALIYE MTAKATIFU (1 Kor 6:17)
>>YAANI, SASA roho yako wewe uliyeokoka kwa kuzaliwa mara ya pili INAUNGANISHWA NA Roho Mtakatifu ama Roho wa Kristo! (i.e. roho + Roho = wewe na Bwana ni mmoja, au roho moja; Kihisabati inakuwa, 1+ 1 = 1)
>> MUUNGANIKO HUU NI WA MUHIMU SANA ILI KUKUWEZESHA WEWE KUISHI MAISHA MAPYA YA UTAKATIFU KATIKA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU KAMA ILIVYOANDIKWA, “ Akajibu akaniambia, akisema,Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, SI KWA UWEZO, WALA SI KWA NGUVU, BALI NI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA MAJESHI.” (Zekaria 4:6)
>> SI KWA UWEZO WAKO WALA NGUVU ZAKO MWANADAMU; BALI NI KWA ROHO YANGU.......! ASEMA BWANA WA MAJESHI! (ROHO WA MUNGU)
>> MAISHA MAPYA YA ULIYEOKOKA UNAISHI SI KWA UWEZO WAKO WALA NGUVU ZAKO MWANADAMU, BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE! IMEANDIKWA, MTAPOKEA NGUVU, AKISHA KUWAJILIA JUU YENU ROHO MTAKATIFU!! (MDO 1:8) HIZI NI NGUVU ZA MUNGU ZA KUKUWEZESHA KUISHI SAWASAWA NA MAPENZI YAKE MUNGU BABA YETU, NA KRISTO YESU BWANA WETU!
UNAISHIJE BASI MAISHA MATAKATIFU? (HOW DO YOU LIVE A HOLY LIFE?)
Pale bustanini Edeni Mungu alitangulia kuumba kila kitu atakachokihitaji mwanadamu kabla hajamuumba.
1) Aliumba mahali pazuri pa kuishi (bustani yote)
2) Aliumba vyakula vyote vya kula huyo mtu
3) Alitengeneza mazingira mazuri na nchi njema yenye rutuba, yenye madini, yenye uwiano mzuri wa asili (balance of nature), yenye maji safi, hewa safi, majani safi, miti safi, wanyama wazuri wa kila namna, mandhari nzuri ya kuvutia, maua na mimea ya aina zote mingi na ya kuvutia, n.k.
4) Akamuumba mwanamume na kumweka bustanini ILI AILIME NA KUITUNZA! Yaani, akampa jukumu la kufanya au kazi ya kufanya bustanini.
5) Akampa neno la Mungu la kumuongoza maisha yake bustanini, kwamba nini afanye na nini asifanye. Na matokeo ya uasi yangekuwa ni yapi.
6) Akatengeneza ushirika kati yake Yeye Mungu na huyo mwanadmu katika majukumu yale yaliyohitaji mmwanadamu kutumia uwezo ambao Mungu alikuwa ameuweka ndani yake (unlocking the human potential); Akamletea mfano wanyama awape majina na majina aliyowapa ndiyo yakawa majina yake. Hapa anamfundisha kuishi sawasawa na majukumu na baraka za kitabu cha Mwanzo 1: 26-28. “26Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
7) Kisha akamfanyia mssaidizi wa kufanana naye ili aje kumsaidia Adamu katika makusudi yale yaliyompelekea Mungu kumuumba mwanadamu na kumweka juu ya kazi za mikono yake. Kumwabudu, kumtumikia, kuyafanya mapenzi yake, kuumba familia pamoja naye, kumiliki, kutawala, na kutiisha uumbaji wote wakiwa kama mwili mmoja, katika ushirika na Roho wa Mungu, na kumpa Mungu utukufu wote, sifa, shukrani, na heshima.
>> Maana alikuwa pia na tabia ya kuja bustanini wakati wa jua kupunga kuongea na Adamu (Mwanzo 3:8)
8) Mwanadamu alipoasi sauti ya Bwana ambayo ndiyo neno lake ushirika huu ulivunjika maana alikufa kiroho, na ili uwe na ushirika na Mungu lazima uwe hai kiroho; Hivyo Adamu akajificha kutoka katika uwepo wa Mungu (Mwanzo 3:8-11). Laana ikaingia, dhambi ikaingia, taabu zikaingia, masumbufu ya maisha nayo yakaingia. Mwanadamu akaanza kujisumbukia yeye mwenyewe na kujihangaikia yeye mwenyewe!
- Adamu akajishonea mavazi ya majani ya miti baada ya kujikuta uchi. (Mwanzo 3:7)
-Ardhi ikalaaniwa kwa ajili ya dhambi zake (Mwanzo 3:17)
-Kula kwa uchungu kukaingia (Mwanzo 3:17)
- Laana ya Mungu ikaharibi mazingira yaliyokuwa mazuri, ya kupendeza, na ya kuvutia; miiba na michongoma ikaanza kuota (Mwanzo 3:18)
- Akaanza kula mboga za kondeni na siyo bustanini tena (Mwanzo 3:18)
- Akaanza kula kwa jasho tofauti na ilivyokuwa Edeni kwenye uwepo wa Mungu alikokuwa anakula bila jasho (Mwanzo 3:19) Kula huku kwa jasho kulitamkwa kutaendelea mpaka atakaporudi mavumbini alikotwaliwa mwili wake (Mwanzo 3: 19) Kifo cha mwili kikaingia hapa Na siyo kifu tu peke yake bali mwili kuchoka, kuugua, na kuzeeka pia maana ndizo sababu zinazopelekea mwili huu kurudi mavumbini ulikotoka!
- Mahangaiko, masumbuko, kutaabika, na kuteseka ili kula na kunywa vikaingia kwa wingi!
TANGU HAPO MWANADAMU HAMTUMAINII MUNGU TENA, HANA USHIRIKA NA MUNGU TENA, HAOMBI MSAADA KWA MUNGU TENA, HANA MPANGO NA MUNGU TENA, HAMWAMINI MUNGU TENA, ANAISHI KWENYE UADUI NA MUNGU, ANAJITUMAINIA YEYE MWENYEWE UWEZO NA NGUVU ZAKE KUTOKANA NA ELIMU, PESA, AKILI, CHEO, NAFASI, WATU ALIONAO ANAOWATEGEMEA, MALI ALIZONAZO, N.K. HIZI ZOTE NDIZO JUMLA YA UWEZO NA NGUVU ZAKE MWANADAMU ALIYEASI!!!
>> ALICHOFANYA MWANADMU MTENDA DHAMBI NI SAWA NA KUKATAA NG’OMBE WA MAZIWA NA KWENDA KUGOMBANIA, NA KUTAFUTA SANA, MAZIWA YANAYOTOKA KWA YULE NG’OMBE!!! NI MFANO WA KUKATAA KIWANDA CHA PESA NA KWENDA KUZITAFUTA SANA PESA, NA KUZIGOMBANIA HIZO PESA ZINAZOZALISHWA NA KIWANDA ALICHOKIKATAA!!! NI SAWA NA KUKATAA KISIMA CHA MAJI NA KWENDA KUYATAFUTA MAJI, NA KUYAGOMBANIA SANA MAJI YANAYOTOKA KWENYE KILE KISIMA ALICHOKIKATAA!!
>> MWANADAMU MTENDA DHAMBI AMEMKATAA MUNGU WA MILELE, ASIYE NA UHARIBIFU, ANAYEISHI MILELE, AMBAYE BARAKA ZAKE NI ZA MILELE, NA SASA AMEGEUKIA VITU VISIVYO NA UHAI, VINAVYOHARIBIKA, VYA MUDA MFUPI HAPA DUNIANI, NA VISIVYOWEZA KUOKOA KABISA. AMEGEUKIA SANAMU HIZO NA ANAABUDU MIUNGU ISIYOSEMA, WALA ISIYOWEZA KUOKOA, WALA KUMPA UZIMA AU KUMPONYA.
AMEMKATAA MUNGU;
-MUUMBA WA MBINGU NA NCHI NA VYOTE VILIVYOMO
-AMBAYE MBINGU NA NCHI NA VYOTE VILIVYOMO NI MALI YAKE
-AMBAYE ANAWEZA YOTE NA HAKUNA NENO GUMU LOLOTE ASILOLIWEZA
-AMBAYE ANA NGUVU ZOTE ZILIZO KUBWA MNO, NA ZA AJABU, ZINAZOTISHA KULIKO CHOCHOTE ALICHOKIUMBA, MFANO SHETANI NA MAJESHI YAKE, NA SILAHA ZAKE ZOTE ZILIZOPO, ZILIZOKUWEPO, NA ZITAKAZOKUWEPO.
-AMBAYE NI MPOLE, MWINGI WA HURUMA NA REHEMA, YEYE AMBAYE NDIYE UPENDO MWENYEWE, SI MWEPESI WA HASIRA, ANASAMEHE NA KUSAHAU DHAMBI NA MAKOSA YOTE, ANAPONYA MAGONJWA, MARADHI, NA UDHAIFU WOTE, NI FURAHA YAKE NA MAPENZI YAKE KUSAIDIA.
-YEYE AMBAYE HANA UPENDELEO, HACHOKI, HAMDHARAU MTU AWAYE YOTE, HALALI WALA HASINZII MLINZI WA YAKOBO, YEYE AMBAYE AMEANDAA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA KWA AJILI YA WATAKATIFU WAKE WALIOMWAMINI YESU.
-YEYE AMBAYE HANA MFANO WAKE MAANA HAWEZI KUFANANISHWA NA YEYOTE AU CHOCHOTE!
>> MUNGU WA NAMNA HII AMBAYE HUWEZI KUMALIZA KUMWELEZEA KUANZIA SASA MPAKA UTAKAPOZEEKA KABISA NA KUAGA DUNIA, NDIYE ALIYEMTUMA MWANAWE PEKEE ULIMWENGUNI ILI WEWE, UKIMWAMINI, AKUSAMEHE DHAMBI ZAKO ZOTE UTAKAPOZITUBIA KWA KUMAANISHA KUZIACHA, AKUPE UZIMA WA MILELE KWA KUKUZAA MARA YA PILI KWA NJIA YA MWANAWE YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WA DUNIA YOTE!!!
>> YEYE ANAKUSAMEHE HALAFU HAKUMBUKI TENA KABISA DHAMBI NA UOVU WAKO WOTE, KISHA ANAKUPA ROHO WAKE AKAE NDANI YAKO HATA MILELE; WALA HAISHII HAPO, BALI ANAKUFUNDISHA SASA MAISHA YAKO YOTE JINSI YA KUISHI NA KUENENDA KWA UTAKATIFU, HAKI, NA KWELI; UKIMPENDEZA YEYE SIKUZOTE NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE SIKU ZOTE, KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKO KAMA ILIVYOANDIKWA KWENYE ZEKARIA 4:6 KWAMBA, “..........SI KWA UWEZO WALA NGUVU BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU”
NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO
A: UTAKATIFU ULIOUPOKEA ULIPOZALIWA MARA YA PILI ULIUPOKEA KWA NEEMA!! HII NI NEEMA IOKOAYO (SAVING GRACE)
“ 8KWA MAANA MMEOKOLEWA KWA NEEMA , KWA NJIA YA IMANI; AMBAYO HIYO HAIKUTOKANA NA NAFSI ZENU, NI KIPAWA CHA MUNGU; 9 WALA SI KWA MATENDO, MTU AWAYE YOTE ASIJE AKAJISIFU. 10 MAANA TU KAZI YAKE, TULIUMBWA KATIKA KRISTO YESU, TUTENDE MATENDO MEMA, AMBAYO TOKEA AWALI MUNGU ALIYATENGENEZA ILI TUENENDE NAYO.” (Waefeso 2:8-10)
-NEEMA MAANA YAKE HUKUSTAHILI LAKINI MUNGU MWENYEWE NDIYE ALIYEAMUA NA KISHA AKAKUCHAGUA YEYE MWENYEWE KWA MAPENZI YAKE; YAANI, AMEKUSTAHILISHA WEWE AMBAYE HUKUSTAHILI (GOD’S UNMERITED FAVOUR) KWA MAANA HAPAKUWEPO KIGEZO CHA WEWE KUPEWA HIYO NEEMA LAKINI MUNGU KWA UPENDO WAKE MKUU KWA WANADAMU AKAKUCHAGUA WEWE ULIYEOKOKA; HAUKUFANYA LOLOTE ILI UOKOKE MAANA YESU ALIKAMILISHA KAZI YOTE YA UPATANISHO NA UKOMBOZI PALE JUU MSALABANI; NA NDIYO MAANA ALISEMA IMEKWISHA! AKIMAANISHA ASITOKEE YEYOTE MWINGINE AKAJA NA KUSEMA KUNA KITU CHA KUONGEZEA KWENYE KAZI YA UKOMBOZI; KUFANYA HIVYO NI KUUKANA MSALABA NA KURUHUSU MAPEPO YAKUINGIE MAANA UNAMKANA YEYE ALIYEKUFA AKAFUFUKA KUTOKA KWA WAFU. UKOMBOZI WA DAMU YA YESU NI MKAMILIFU. DENI LA DHAMBI LIMELIPWA. HATI YA MASHITAKA DHIDI YETU TUAMINIO IMEFUTWA; HUKUMU YA DHAMBI AMA ADHABU YA DHAMBI IMETEKELEZWA JUU YAKE ILI MWANADAMU USIINGIE HUKUMUNI. UPONYAJI WA MAGONJWA UMENUNULIWA KWA DAMU YAKE; MAGONJWA, UDHAIFU, NA MARADHI YOTE HAYAWEZI TENA KWA NAMNA YOYOTE KUMTESA YEYOTE AAMINIYE. LAANA ZOTE ZIMEBATILISHWA; BARAKA ZOTE ZIMEACHILIWA; NA ZOTE ZINAPOKELEWA KWA IMANI. ALIYEOKOKA AMESAMEHEWA DHAMBI ZAKE ZOTE, NI MTAKATIFU, ANA UZIMA WA MILELE, AMEPONA MAGONJWA NA MARADHI YOTE NA HAUMWI MAANA KWA KUPIGWA KWAKE YESU YEYE AMEPONA!!! ANAWEZA KUSHAMBULIWA NA ROHO ZA MARADHI AU MAGONJWA , LAKINI KAMA ILIVYOANDIKWA KWAMBA “BASI MTIINI MUNGU MPINGENI SHETANI NAYE ATAWAKIMBIA” (YAKOBO 4:7) MAGONJWA YAKIJA TUNA MAMLAKA YA KUYAKATAA, KUYAPINGA, NA KUZIKEMEA NA KUZIFUNGA ZILE roho za magonjwa, udhaifu, na maradhi zote!! KILA TUNAPOSHAMBULIWA KWA DALILI ZOZOTE “TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA,” PAULO ALIANDIKA. HAKUNA ALICHOSAZA BWANA WETU YESU, USIDANGANYWE! NA HAKUNA SIRI YA AJABU YOYOTE; ANACHOTAKA BWANA YESU NI WEWE KUMWAMINI TU!!!! UKIAMINI MUNGU ANAKUPA NEEMA!!! FAITH PRECEEDS GRACE! IMANI HUTANGULIA KABLA YA NEEMA! NEEMA NI NINI? TUNAELEKEA KULIJIBU HILI SWALI MUDA MFUPI UJAO!!
B: NA MAISHA UNAYOYAISHI BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI UKIWA MTAKATIFU, UNAYAISHI NAYO KWA NEEMA YA KRISTO!! HII NI NEEMA YA KUISHI KWAYO (LIVING GRACE)
Biblia inasema, “11Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.” (Tito 2:11-14)
1) NEEMA YA MUNGU IWAOKOAYO WANADAMU WOTE IMEFUNULIWA. NEEMA HIYO TULIIPOKEA KWA MKONO WA YESU KRISTO
“14Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, UTUKUFU KAMA WA MWANA PEKEE ATOKAYE KWA BABA; AMEJAA NEEMA NA KWELI. 15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 KWA KUWA KATIKA UTIMILIFU WAKE SISI SOTE TULIPOKEA, NA NEEMA JUU YA NEEMA. 17 KWA KUWA TORATI ILITOLEWA KWA MKONO WA MUSA; NEEMA NA KWELI ZILIKUJA KWA MKONO WA YESU KRISTO.” (Yohana 1:14-17)
2) NEEMA HII ILIYOKUJA KWA MKONO WA YESU KRISTO NDIYO INAYOKUOKOA UKIMWAMINI YESU, NDIYO INAYOMFUNDISHA MWAMINI ALIYEMPA MAISHA YAKE YESU, KWA KUOKOKA, JINSI YA KUISHI NA KUENENDA NDANI YA YESU.
>> ANDIKO LA TITO LINASEMA NEEMA HII YA BWANA WETU YESU KRISTO
A) INAOKOA KUTOKA DHAMBINI UKIAMINI
B) NAYO INAMFUNDISHA MWAMINI AU MTOTO WA MUNGU ALIYEOKOKA MAMBO MAWILI;
B1: KUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA, NA
B2: >> KUISHI KWA KIASI (SELF-CONTROLLED LIVING)
>> KUISHI KWA HAKI (RIGHTEOUS LIVING)
>> KUISHI KWA UTAUWA (GODLY LIVING)
Neema hii ni ile ile iliyoanzia kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. BWANA YESU ALIISHI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE! Na wakati wote wa huduma yake alikuwa akisisitiza kwamba si Yeye aliyekuwa akizifanya kazi zote isipokuwa ni Baba yake akaaye ndani yake. Baba wa Yesu ni Roho Mtakatifu (Luka 1:35) Naye ndiye anayehusika kwa kuzaliwa kwetu mara ya pili tunapomwamini Yesu. Yaani, ndiye anayetuzaa mara ya pili kwa nguvu zake mwenyewe kupitia mbegu ya neno takatifu la Mungu tuliloliamini.
“3Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 4Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, ALITUOKOA; 5 SI KWA SABABU YA MATENDO YA HAKI TULIYOYATENDA SISI; BALI KWA REHEMA YAKE, KWA KUOSHWA KWA KUZALIWA KWA PILI NA KUFANYWA UPYA NA ROHO MTAKATIFU; 6AMBAYE ALITUMWAGIA KWA WINGI, KWA NJIA YA YESU KRISTO MWOKOZI WETU; 7ILI TUKIHESABIWA HAKI KWA NEEMA YAKE, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.” (Tito 3:3-7)
>> ROHO MTAKATIFU NDIYE MWALIMU ( YOHANA 14:26) WA MAISHA YALIYO SAWASAWA NA NENO KAMA ALIVYOISHI YESU.
>> ANAKUFUNDISHA JINSI GANI YA KUISHI NA KUENENDA KAMA YESU ALIVYOENENDA.
>> KWA KUWA YESU ALIISHI NA KUENENDA KWA NGUVU ZA MUNGU, ROHO MTAKATIFU HUYU NI YULE YULE ALIYEKUWEMO NDANI YA YESU, NAYE NDIYE ANAYEKUJALIA NGUVU ZAKE ILI UISHI MAISHA MATAKATIFU YALE YALE ALIYOYAISHI YESU ALIPOKUWA KWENYE MWILI.
>> KAMA ZECHARIA ALIVYOSEMA SI KWA UWEZO WALA NGUVU (ZECHARIA 4:6), BASI AGANO JIPYA LOTE LIMETULETEA MAISHA KATIKA NGUVU ZA MUNGU, KWA ROHO MTAKATIFU, KUPITIA IMANI YA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU.
>> WANA WA MUNGU WANAISHI KAMA YESU WALIYEMWAMINI ALIVYOISHI, KWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU (WARUMI 8:14)
“6Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” (1 Yohana 2:6)
>> ILI UISHI KAMA YESU LAZIMA UISHI KWA IMANI YA YESU!!!! MAISHA YA IMANI YANAKUFANYA UISHI KWA NENO LA KRISTO!
“20Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” (Wagalatia 2:20)
NA BIBLIA INASEMA;
“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” (Yohana 6:63)
>> Neno la Mungu ni roho, tena ni uzima! Ili neno la Mungu likuletee manufaa ni lazima neno hilo liwe roho ndani yako. Unapoamini neno la Mungu huwa linakaa moyoni mwako kama roho. Yaani, neno uliloliamini linaunganika na roho yako! Yaani, ile roho ya andiko inaunganika na roho yako! Mfano,
>neno la maombi lina roho ya maombi -neno la ukarimu lina roho ya ukarimu
>neno la utoaji lina roho ya utoaji -neno la uchaji Mungu lina roho ya kumcha Bwana
>neno la huruma lina roho ya huruma -neno la hekima lina roho ya hekima
>neno la furaha lina roho ya furaha -neno la maarifa lina roho ya maarifa
>neno la imani lina roho ya imani -neno la bidii lina roho ya bidii
>neno la upendo lina roho ya upendo -neno la amani lina roho ya amani
>neno la nguvu lina roho ya nguvu -neno la uvumilivu lina roho ya uvumilivu
>neno la upole lina roho ya upole -neno la utakatifu lina roho ya utakatifu
>neno la unyenyekevu lina roho ya unyenyekevu -neno la kufunga lina roho ya kufunga
>neno la utii lina roho ya utii -neno la kujikana lina roho ya kujikana
> la neno la uaminifu lina roho ya uaminifu -neno la utakaso lina roho ya utakaso
>neno la umoja lina roho ya umoja, -neno la wema lina roho ya wema n.k. n.k.
>> KILA UNAPOSOMA ANDIKO MAANA YAKE KUNA ROHO YA HILO ANDIKO UTAIPOKEA KAMA UKILIAMINI
>> USIPOLIAMINI NENO LA MUNGU, HUWA LINABAKI KAMA ANDIKO TU LINALOUA NA WALA HALIWEZI KUKUHUISHA
2 WAKORINTHO 3:6
“6Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.”
>> ANDIKO LINAUA KWA SABABU ULE UZIMA ULIOMO NDANI YAKE HAUMO KWENYE ANDIKO TU LENYEWE, BALI UMO KWENYE ROHO YA HILO ANDIKO, NA WEWE HAUWEZI KUUPATA HUO UZIMA USIPOLIAMINI, HATA KAMA UMELIKARIRI KICHWANI; ANDIKO LINAKAA MOYONI AU ROHONI MWAKO KAMA “roho” UNAPOLIAMINI; NA HAPO NDIPO LINAPOKUPA UZIMA AU UHAI AMA MAISHA YALIYOMO KWENYE HILO ANDIKO KWENYE ROHO YAKO.
>> Hapo juu tumesema NENO LA.... LINA ROHO YA HILO NENO! NA KWENYE YOHANA 6:63 HAPO JUU TUMESOMA KWAMBA ROHO NDIYO INAYOTIA UZIMA [IT IS THE SPIRIT WHICH GIVES LIFE........ ( WHICH QUICKENS)] NA YOHANA 1:4 INASEMA, “NDANI YAKE NDIMO ULIMOKUWEMO UZIMA....). UZIMA, UHAI, AU MAISHA YA YESU YAMO KWENYE NENO LA MUNGU, NAYO NDIYO MAISHA YETU TULIOAMINI!! HII NDIYO SABABU YA KUSEMA YESU NDIYE UHAI WETU , AU YESU NDIYE MAISHA YETU, AU YESU NDIYE UZIMA WETU! (Wakolosai 3;4)
>>Kwenye 1 Wakorintho 15:45 Biblia inasema, “45Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.” (1 Wakorintho 15:45)
>>YESU NDIYE ADAMU WA MWISHO! A LIFE- GIVING SPIRIT (ROHO ANAYEHUISHA, AU ROHO ANAYETIA UZIMA, AMA ROHO WA UZIMA) YESU LEO TUNAMTAMBUA KATIKA ROHO KAMA ROHO ANAYEHUISHA! YAANI, YESU NDIYE ANAYETUPA UZIMA WAKE, AMA UHAI WAKE, AMA MAISHA YAKE YEYE MWENYEWE YALIYOMO KWENYE NENO LAKE NDANI YA ROHO ZETU PALE TUNAPOLIAMINI NENO LAKE!! ILE roho ya neno au roho ya andiko imetoka kwa Yesu mwenyewe ambaye ni neno! Nayo inakuja kwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu pale tunapoliamini neno lake!! Kwa kuwa Yesu ni Roho wa Uzima leo, maana yake tunapoamini neno la uzima Yeye ndiye hutupatia uzima uliomo kwenye neno lake tuliloliamini; kwa kuwa imeandikwa Roho ndiye atiaye uzima.......! (Yohana 6:63)
>> Usipoamini hauwezi kulitenda neno kwa kuwa bado unakuwa umebaki katika andiko na si katika roho!!! Hata ukifanya lolote haliwezi kumpendeza Mungu kwa kuwa umefanya kwa nguvu na uweza wako mwenyewe. Nguvu za Mungu zimo kwenye roho!!!Ile roho ya hilo andiko au hilo neno ndiyo yenye nguvu za hilo andiko. Mfano roho ya maombi ndiyo yenye nguvu za maombi; roho ya utoaji ndiyo yenye nguvu za Mungu za utoaji; roho ya kusamehe ndiyo yenye nguvu za Mungu za kusamehe! Zile nguvu ndizo zinazokuwezesha KUIYAISHI MAISHA YA HILO ANDIKO AU NENO!! Hii ndiyo inaitwa neema ya Kristo inayotufundisha na kutuwezesha kuyatenda mapenzi ya Mungu yaliyomo kwenye neno lake!!!
[NEEMA YA KRISTO = ROHO MTAKATIFU + NGUVU ZAKE]
“38habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.” (Matendo ya Mitume 10:38)
>> [ MAFUTA YA YESU = ROHO MTAKATIFU + NGUVU ZA HUYO ROHO]
Mafuta haya yakiwa ndani yetu ndiyo yanakuwa ni neema yake katika maisha yetu mapya ndani yake!
“20Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.
“27Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.” (1 Yohana 2:20,27)
>> MTOTO WA MUNGU AMETIWA MAFUTA NAYE KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KUPITIA IMANI YAKE ILIYO HAI KWA YESU
>> MAFUTA HAYA YANAKAA NDANI YAKE SIKU ZAKE ZOTE KUMFUNDISHA NA KUMWEZESHA KULIISHI NA KULITENDA NENO LA KRISTO
>> Roho Mtakatifu na nguvu zake ndiyo Neema ya Kristo kwetu, na ndiyo mafuta yake kwetu!!! Roho ni Roho wa Neno! Nguvu zake ni Nguvu za Neno! Roho na Nguvu zake humwezesha mtoto wa Mungu kulitenda neno licha ya upinzani wa mwili, nguvu za giza za shetani, na ulimwengu huu wa sasa. KULITENDA NENO KUNA UPINZANI! LAKINI BWANA WETU YESU ALITUSHINDIA! NASI TUNATEMBEA KWA USHINDI WAKE WA MSALABA! NENO LAKE NDIYO TAA YETU NA MWANGA WA NJIA YETU! YEYE MWENYEWE NDIYE NJIA! TITO 2:11 ALISEMA NEEMA YAKE INATUFUNDISHA,
1) KUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA KIDUNIA
2) NA KUTUFUNDISHA KUISHI KWA KIASI, HAKI, NA UTAUWA.
>> Maisha yetu ni maisha ya uanafunzi; tunajifunza na kufundishwa UTII WA KWELI; Mafundisho yetu ni katika maisha halisi ya kila siku. Ukifaulu kutendea kazi neno ndipo unamzalia Mungu matunda yakaayo, nawe unakuwa mwanafunzi wa Yesu kweli kweli.
“1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.” (Yohana 15:1-8)
>> HUWEZI KUSAMEHE PASIPO NGUVU ZA ROHO YA KUSAMEHE, ILIYOMO ROHONI MWAKO BAADA YA KUAMINI NENO LA KUSAMEHE.
>> HUWEZI KUKATAA UBAYA PASIPO NGUVU ZA KUKATAA UBAYA ZA ROHO YA KUKATAA UBAYA, ULIYONAYO BAADA YA KUAMINI ANDIKO LA KUKATAA UBAYA.
>> HUWEZI KUPAMBANUA PASIPO NGUVU ZA KUPAMBANUA ZA ROHO YA KUPAMBANUA, ILIYOMO NDANI YAKO BAADA YA KUAMINI NENO LA KUPAMBANUA
>> HUWEZI KUJITAKASA PASIPO NGUVU ZA ROHO YA UTAKASO ILIYOMO NDANI YAKO, KUTOKANA NA KUAMINI KWAKO NENO LA UTAKASO.
>> HUWEZI KUMCHA MUNGU PASIPO NGUVU ZA ROHO YA KUMCHA MUNGU ILIYOMO NDANI YAKO BAADA YA WEWE KUAMINI NA KULIPOKEA NENO LA KUMCHA BWANA.
>> HUWEZI KUTOA SADAKA GHALI (SACRIFICIAL GIVING) PASIPO NGUVU ZA ROHO YA UTOAJI HUO BAADA YA KUAMINI KWAKO NENO LA UTOAJI WA AINA HIYO! MFANO, KUMTOA MWANAO PEKEE, AU KUUZA VYOTE ULIVYONAVYO, NA KUWAPA MASKINI, UPATE KUWA NA HAZINA MBINGUNI, NA KISHA UJE KUMFUATA YESU!!!
KUISHI KWA IMANI NI KUENENDA KWA ROHO MTAKATIFU WA NENO ANAYEKUWEZESHA KUTENDA KAZI KWA ROHO YA NENO KILA LINAPOHITAJIKA KUTUMIWA, NENO LILE ULILOLIAMINI, AMBALO LIMEKUWA ROHO NDANI YAKO. YAANI, LIMEUNGANIKA NA ROHO YAKO! NEEMA YA KRISTO NI “ILE ROHO YA NENO....!” YENYE “NGUVU ZA LILE NENO....” INAYOKUWEZESHA “KUISHI MAISHA YA LILE NENO...!”
HII NDIYO NEEMA YA KRISTO:
NEEMA = [ROHO YA NENO....! + NGUVU YA NENO...!] INAYOZAA “MAISHA YA LILE NENO!!
>> MAISHA YA LILE NENO NI KAMA KUSAMEHE, KUACHILIA, KUOMBA, KUTOA, KUJIDHILI, KUJIKANA, KUMCHA BWANA, KUJITENGA NA UOVU, KUREHEMU, KULIA NA WANAOLIA, KUWAHESABU NDUGU ZAKO KATIKA KRISTO KUWA BORA KULIKO NAFSI YAKO, KUJISHUSHA, KUNYENYEKEA CHINI YA MAMLAKA ZILIZOPO KUANZIA NGAZI YA NDOA, FAMILIA, KANISA, SHULENI, CHUONI, KAZINI, NA NGAZI YA TAIFA, KUENENDA KWA UPENDO WA KRISTO, KUKATAA UBAYA WA KILA NAMNA WA KIDUNIA, KUTOIFUATISHA NAMNA YA DUNIA HII, KUWAHESHIMU WANAOSTAHILI HESHIMA, KUMZALIA MUNGU MATUNDA YAKAAYO, KUMZALIA MUNGU MATUNDA YAPASAYO TOBA, KUJITOA, KUUTOA UHAI WAKO KWA AJILI YA HAO NDUGU, KUUCHUKUA UDHAIFU WA HAO WASIO NA NGUVU, KUWAPENDA MAADUI ZAKO, KUWAOMBEA WANAOKUONEA, KUTOLIP KISASI CHA NAMNA YOYOTE, KUTOLIPA BAYA KWA BAYA, KUUSHINDA UBAYA KWA WEMA, N.K. N.K.
>> MAZINGIRA NA HALI ZIKITOKEA ZA WEWE KULITENDA NENO KATIKA NAMNA MOJAWAPO YA HIZI NA NYINGINEZO NYINGI ZILIZOMO KWENYE MAANDIKO, KAMA LILE NENO HALIMO MOYONI MWAKO, LAZIMA UANGUKE! MAANA IMEANDIKWA;
“24 Basi KILA ASIKIAYE HAYO MANENO YANGU, NA KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26NA KILA ASIKIAYE HAYO MANENO YANGU ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.” (Mathayo 7:24-27)
>> NYUMBA YAKO YA KIROHO HAIWEZI KUSIMAMA KAMA HAUNA NENO MOYONI MWAKO ULILOLIAMINI AMBALO LIMEKAA KAMA ROHO NDANI YAKO, NA HIVYO LIMEKUPA UZIMA AU MAISHA YA HILO NENO ROHONI MWAKO!!! MAANA IMEANDIKWA, “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyokuambia ni roho, tena ni uzima.”(Yohana 6:63)
>> KILA UNAPOAMINI ANDIKO LOLOTE AU NENO LOLOTE HUWA HALIBAKI TENA KAMA ANDIKO; BALI LINAKUWA NI ROHO, NA PIA NI UZIMA ROHONI MWAKO.
>>HAPA NDIPO TUNASEMA WEWE UMEUNGANIKA NA BWANA YESU KATIKA ROHO (1 KOR 6:17) YAANI,
- umekuwa roho moja na Bwana, (one spirit with the Lord)
- au umekuwa mmoja na neno (one with the Word)
- ama umekuwa mmoja na Yesu (one with Jesus)
1) MIMI NI MTAKATIFU KWA KUWA NI ROHO MOJA NA BWANA YESU
2) MIMI NI MTAKATIFU KWA KUWA NI MMOJA NA NENO LAKE
3) MIMI NI MTAKATIFU KWA KUWA NI MMOJA NA YESU
>> ALIYENIONA MIMI AMEMUONA YESU; ALIYENISIKIA MIMI AMEMSIKIA YESU; ALIYENIPA MIMI AMEMPA YESU; ALIYENITENDEA MIMI AMEMTENDEA YESU: ALIYENIZUNGUMZIA MIMI AMEMZUNGUMZIA YESU; YESU YU HAI NDANI YANGU!
“20Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” (Wagalatia 2:20)
>> NIMESULUBIWA PAMOJA NA KRISTO
>> NIKAFA NA KUZIKWA PAMOJA NAYE
>> NIKAFUFULIWA PAMOJA NAYE
>> NINAISHI NDANI YAKE
>> SI MIMI TENA NINAYEISHI, BALI KRISTO YU HAI NDANI YANGU
>> MAISHA YANGU KATIKA MWILI HUU NINAISHI KWA IMANI YA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU, ALIYENIPENDA, AKAJITOA NAFSI YAKE KWA AJILI YANGU
>> [ (Roho wa Kristo + roho yangu) + Nguvu zake] = MIMI NDANI YAKE
>> [ (Roho Mtakatifu + Nguvu zake) + roho yangu] = NEEMA YAKE NDANI YANGU
.>> Roho Mtakatifu + Nguvu zake + roho yangu = MAISHA YANGU KWA NEEMA YAKE NDANI YAKE
Mpaka hapa hii inatosha kujenga msingi wa fundisho lifuatalo la UTAKATIFU KATIKA NAFSI; UTAKATIFU KATIKA ROHO UNATOSHA KWA SASA INGAWA KUNA MENGI MNO YA KUFUNDISHA, UBARIKIWE NA BWANA YESU.