UTAKATIFU KATIKA ROHO-4

 Calvary Wallpapers - Top Free Calvary Backgrounds - WallpaperAccess

UTAKATIFU KATIKA ROHO-4

Kwa kuwa mwanadamu = (roho + nafsi) + mwili, yaani, mwanadamu anaishi kwenye mwili, nimeona ni muhimu kuendelea kidogo na somo hili kuhusu utakatifu katika roho. Nataka niongelee kidogo;

1) Nguvu za Kiroho, na

2) Usemi wa Mtakatifu

Biblia inaongea kwa habari ya Yesu Kristo alipokuwa akikua kwamba, “ Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.” (Luka 2:40)

>> UKUAJI UNAOKUBALIKA KWA MUNGU NDIO HUU TUNAOUONA KWA YESU

1) ALIKUA KWA KUONGEZEKA MIAKA YA KUZALIWA

2) ALIONGEZEKA NGUVU

3) ALIKUWA AMEJAA HEKIMA

4) NEEMA YA MUNGU ILIKUWA JUU YAKE

Biblia inasema pia kwa habari ya Yohana Mbatizaji aliyemtangulia Yesu  ili kumtengenezea njia kwamba, Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake Israeli.” (Luka 1:80)

>> UKUAJI WA YOHANA MBATIZAJI NAYE ULIKUWA UNAFANANA NA ULE WA YESU

1) ALIKUA KWA KUONGEZEKA MIAKA YA KUZALIWA

2) AKAONGEZEKA NGUVU ROHONI

3) AKAKAA MAJANGWANI MPAKA SIKU ALIPOTOKEA KWA ISRAELI

>> WATOTO WETU TULIOOKOKA TUNAPOWAZAA NI LAZIMA NAO WAKUE HIVYO ILI WAWEZE KUMPENDEZA MUNGU NA WANADAMU,  NA KUJA  KUMTUMIKIA MUNGU WAKATI UKIFIKA. LAKINI HII INATEGEMEA HALI YA KIROHO YA WAZAZI JINSI ILIVYO;

“21Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele. (Isaya 59:21)

>> HILI NI AGANO LA MUNGU NA MZAZI; KWAMBA UTAZAA WATOTO AMBAO WATAKUWA NA ROHO ILE ILE YA MUNGU ILIYO JUU YAKO, NA WENYE MANENO YALE YALE YA UZIMA AMBAYO MUNGU AMEYATIA KINYWANI MWAKO. HII INAONYESHA UMUHIMU NA ULAZIMA WA MZAZI KUWA NA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU, NA KUENENDA KWA ROHO HUYO SIKU ZOTE ZA MWILI WAKE. MAANA HIYO NDIYO FAIDA KUU, AMA URITHI PEKEE BORA WA MZAZI KWA MTOTO; KAMA MZAZI HAUJAOKOKA, AU HAUJAJAZWA ROHO MTAKATIFU, AMA UMERUDI NYUMA NA KUPOTEZA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU, TUBU HARAKA, OKOKA, NA UREJEE KWA BWANA YESU; KISHA NAYE ATAKUPA ROHO MTAKATIFU (MATENDO YA MITUME 2:38) MAANA YEYE NDIYE ANAYEBATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA MOTO (MATHAYO 3:11); LAKINI PIA UNAWEZA KUOMBA NA BABA ATAKUPA ROHO MTAKATIFU. (LUKA 11:13); HUU NI

1) URITHI USIOHARIBIKA

2) URITHI WA MILELE

3) URITHI UTAKAOMPA MAISHA MATAKATIFU YA ROHO MTAKATIFU

4) URITHI UTAKAOMPA KUNENA MANENO YA UZIMA KWA HUYO ROHO WA UZIMA, AKIWA NDANI YA YESU KRISTO

5) NA KWA KUWA IMEANDIKWA KINYWA CHA MTU HUNENA YAUJAZAYO MOYO WAKE (MATHAYO 12:34), HII NDIYO MAANA TUTAANGALIA USEMI WA MTAKATIFU KWA MUJIBU WA MAANDIKO

1) NGUVU ZA KIROHO (SPIRITUAL POWER)

Imeandikwa “Mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu” (Matendo 1:8) Kwa hivyo nguvu za Mungu ni Roho, kama vile Mungu Alivyo Roho (Yohana 4:24) Pasipo Roho Mtakatifu hakuna nguvu za Mungu. Nabii Zecharia alisema kwamba SI KWA UWEZA WALA NGUVU BALI NI KWA ROHO WA MUNGU!!! ( Zecharia 4:6) HAKUNA MWANADAMU AWEZAYE KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU PASIPO ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE , AMBAYO TUMEONA KWENYE MASOMO YALIYOTANGULIA KWAMBA NDIYO NEEMA YAKE. Neema hii inapatikana kwa yeyote aaminiye wakati wote, mahali popote ulipo, katika mazingira yoyote uliyomo. (Waebrania 4:16). Mungu anatoa neema yake wakati wowote ukimjia na kumwomba akurehemu na kukupa neema yake hiyo katika uhitaji wowote ulionao. Tena amesema na wewe mwanawe kwamba uje kwake kwa ujasiri wote ili akupe rehema na neema ya kukusaidia katika uhitaji wako wa kuyafanya mapenzi yake. Kwa maana anajua kwamba hauwezi kufanya lolote la kumpendeza pasipo mkono wake au neema yake (Yohana 15:5 c) Kila roho ya andiko ni takatifu kwa maana lile andiko nalo ni takatifu, kama tulivyoona tayari huko nyuma. Anayeweza kukuunganisha na neno la Mungu ni Roho Aliye Mtakatifu, ambaye ndiye mwenye nguvu za utakatifu, unazoongezewa ukiliamini neno hilo takatifu rohoni mwako (moyoni mwako).

>> Ongezeko la nguvu za Mungu linawezekana

1) Pale unapoamini neno au andiko ambalo ulikuwa haujaliamini

2) Kwa kuamini huko andiko hilo linakuwa roho na hivyo uzima/maisha ama uhai rohoni mwako (moyoni mwako) –Yohana 6:63

3) Yaani, unakuwa umeongezewa “roho”!!! Umejazwa “roho”!!! roho hii imetoka kwa neno!!! kama imetoka kwa neno maana yake imetoka kwa Yesu!!! kama imetoka kwa Yesu maana yake imetoka kwa Mungu, maana Yesu ni Jina la Mungu kwenye mwili!!! Hapo mwanzo kulikuwako neno, Naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:1, 14)

4) Kama umeamini au haujaamini hii inaonekana kirahisi pale unapokutana na shetani uso kwa uso kwenye jaribu. Mwitikio wako huwa unakuwaje kwenye jambo lile unalosema umemuamini Bwana  kwalo? Yesu alimjibu shetani, imeandikwa....! Akamshinda kwa upanga mkali wa moto wa Neno lake! (Ufunuo 19:11-16) Je! na wewe unao huo moto rohoni mwako? Maana moto huo ni moto wa Roho Mtakatifu! Ni moto wa Neno uliloliamini ambalo Yeremia anasema; “Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana;.........” (Yeremia 23:29a) Kama Neno ni moto, na roho ya Neno ni moto, na nguvu za hiyo roho ni moto! Mungu wetu ni moto ulao!!! UKISHINDA KWA KULING’ANG’ANIA NENO KWENYE JARIBU LAKO HAPO UNAKUWA UMEJULIKANA;

- KWAMBA KWELI ULIKUWA UMEAMINI

- KWAMBA KWELI NENO LILIKUWA MOYONI MWAKO

- KWAMBA KWELI NENO LILIKUWA ROHO NDANI YAKO

-KWAMBA KWELI NENO LILIKUWA UZIMA/MAISHA/UHAI NDANI YAKO

-KWAMBA KWELI  NGUVU ZA MUNGU, AMBAZO NI NGUVU ZA NENO, AMBAZO NI NGUVU ZA BWANA YESU, ZINATENDA KAZI NDANI YAKO. HAPO UNAMPA MUNGU UTUKUFU!!

>> USHINDI WA MTAKATIFU UPO KWENYE KUAMINI TU PEKE YAKE!!! Maana imeandikwa, “.........na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, HIYO IMANI YETU.” (1 Yohana 5:4b)

>> NI KUAMINI PEKE YAKE KUNAKOKUUNGANISHA NA ROHO YA NENO AMA ROHO WA NENO; NJIA PEKEE YA KUINGIA ROHONI NI IMANI; NA USHINDI WA MTEULE, MTAKATIFU , MWANA WA MUNGU, UKO KWENYE ROHO PEKEE; MAANA ROHO NDIYO INA NGUVU ZA MUNGU ZA KUKUWEZESHA WEWE UAMINIYE KUYAISHI MAISHA YALIYOMO KWENYE ANDIKO/NENO LA MUNGU.

Hivyo anaposema kwenye Warumi 1:16-17 kwamba;

“16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. 17Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.” (Warumi 1:16-17)

>> LAZIMA MTEULE, MTAKATIFU, MWANA WA MUNGU, UENDELEE TOKA IMANI HATA IMANI (FROM FAITH TO FAITH), NA KWA KUFANYA HIVYO;

>> “5 Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,  Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.

6Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka

7 Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.” (Zaburi 84:5-7)

>> HERI (AMEBARIKIWA) MTU YULE AMBAYE NGUVU ZAKE ZATOKA KWA BWANA YESU (KAMA ILIVYOANDIKWA SI KWA UWEZA WALA NGUVU BALI NI KWA ROHO)

>> HUYO HUENDELEA KUTOKA NGUVU HATA NGUVU KADIRI ANADUMU KATIKA IMANI.

Lazima liwepo ongezeko la nguvu katika maisha ya kiroho ya mtoto wa Mungu; ongezeko ambalo linatokana na ongezeko la imani. Neno la Kristo haliwezi kukaa kwa wingi ndani yako kama hauongezeki kiimani. Maana imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo (Warumi 10:17). Kwa kuwa imani kuongezeka maana yake unazidi kujaa roho na uzima kwa Neno la Bwana unaloliamini, kama ilivyoandikwa; “.....maneno hayo niliyowaambia ni roho na tena ni uzima.” (Yohana 6:63)

>> Kila unapoamini unaingiwa na roho ya neno lile uliloliamini rohoni mwako (moyoni mwako) kama nabii asemavyo;

“1 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe. 2 Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami. (Ezekieli 2:1-2)

1) Mwanadamu simama kwa miguu yako, NAMI NITASEMA NAWE

2) NAYE ALIPOSEMA NAMI, roho ikaniingia!!!!

3) roho iliponiingia ikanisimamisha!!!

4) roho hiyo iliponisimamisha NDIPO NIKAMSIKIA YEYE ALIYESEMA NAMI

Hii ndiyo Warumi 10:17! HAPA ROHO MTAKATIFU ANAFUNUA JINSI YA KUMSIKIA YEYE!! KAMA MUNGU AMESEMA NAWE, UKAMSIKIA KWELI, INA MAANA ILE ROHO YA LILE NENO ILISHAKUINGIA. HIYO ROHO YA NENO NDIYO INAYOKUFUNGUA MASIKIO YA KIROHO NA KUKUPA KUISIKIA SAUTI YA ROHO MTAKATIFU, AMBAYO NDIYO SAUTI YA BWANA YESU, AMBAYO NDIYO SAUTI YA BABA YETU WA MBINGUNI; Maana imeandikwa kwamba Roho hatanena kwa shauri lake tu mwenyewe kama anavyojisikia, bali yote atakayoyasikia atayananena.

“13Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana HATANENA KWA SHAURI LAKE MWENYEWE, LAKINI YOTE ATAKAYOYASIKIA ATAYANENA, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.” (Yohana 16:13-15)

>> ROHO MTAKATIFU AKISEMA NAWE HUWA ANASEMA NENO LA MUNGU AMA NENO LA KRISTO

>> ANAPOSEMA NAWE LILE NENO, KAMA UMEUFUNGUA MOYO WAKO KULIPOKEA HILO NENO, NDIPO roho YA LILE NENO HUKUINGIA ROHONI AU MOYONI MWAKO

>> ILE roho IKIKUINGIA LAZIMA IKUBADILISHE ILI UFANANE NAYO, MAANA INAUNGANIKA NA roho YAKO, NANYI MNAKUWA roho moja; UNAKUWA mmoja na Neno. HAPO NDIPO TUNASEMA “UMEMWAMINI YESU, AMA UMEMWAMINI MUNGU.

>> KUAMINI NI KUMSIKIA MUNGU!! KILA UNAPOAMINI, UNAZIDI KUJAA SAUTI YA MUNGU!!

>>HAKUNA ALIYEAMINI, AU ALIYEMSIKIA BWANA HALAFU ASITENDE YALE ALIYOAMBIWA!!! TABIA KUU YA WATOTO WA MUNGU NI UTII WA KWELI!!! AMA UTII WA NENO!!! WANAISHI KWA UTII!!! WANAISHI WAKILITENDA NENO LA MUNGU WALILOLIAMINI!! WANALITENDA NENO HILO KWA NGUVU ZA HILO NENO!!! KUMWAMINI MUNGU NI KUSIKIA NA KUTNDA ALICHOSEMA KWA ROHO NA NGUVU ZAKE! YAANI, KWA NNEMA YAKE!!! HAKUNA ALIYEMSIKIA MUNGU HALAFU ASITENDE ALICHOAMBIWA!!! KWA MAANA, ILI UMSIKIE MUNGU, NI LAZIMA roho yake IKUINGIE KWANZA; roho AMBAYO INATOKA KWENYE LILE NENO LAKE, KAMA ILIVYOANDIKWA “maneno hayo niliyowaambia ni roho na tena ni uzima”(Yohana 6:63)

>> roho ya Mungu kutoka kwenye Neno lake ikikuingia inaunganika nawe katika roho yako, na kukufanya wewe kuwa mmoja na Mungu. Hivyo unatenda katika ushirika na Mungu; na kwa nguvu zake!! kwa Roho wake!! kupitia imani iliyo hai kwa Neno lake!! (IMANI YA YESU)

>> KUMSIKIA ROHO MTAKATIFU KUNAKUJA BAADA YA ROHO KUKUINGIA, NA HUKU NDIKO KUNAITWA KUSIKIA KWA IMANI!!! MAANA UNAMSIKIA KATIKA roho yako NA SIYO KWA MASIKIO YA DAMU NA NYAMA!! Mungu unamsikia katika roho!! Kama amesema samehe, maana yake yake roho yake ya kusamehe ndiyo imesema nawe!!! Kama kasema achilia maana yake roho yake ya kuachilia ndiyo imesema nawe!!! kama kasema toa maana yake roho yake ya utoaji ndiyo imesema nawe!!! kama kasema imba maana yake roho yake ya uimbaji ndiyo imesema nawe!!! kama amesema omba maana yake roho yake ya kuomba ndiyo imesema nawe!!! kama kasema nyenyekea maana yake roho yake ya unyenyekevu ndiyo imesema nawe!!! kama kasema tii maana yake roho yake ya utii ndiyo imesema nawe!!! kama kasema heshimu maana yake roho yake ya kuheshimu ndiyo imesema nawe!!! kama kasema ombea maana yake roho yake ya kuombea ndiyo imesema nawe!!! n.k. n.k.

>> Kwa kuwa hizi zote “roho yake ya ...” ni takatifu maana yake Mungu amenena kwa utakatifu wake!!! (Zaburi 60:6, Zaburi 108:7)

>> kama ulifungua moyo wako kulipokea neno lake maana yake roho ya utakatifu imekuingia! nao ni utakatifu katika eneno la maisha alilosema nawe kama ni ndoa, huduma, kazi ya mikono, mahusiano, n.k.

>> Na kwa kuwa roho hiyo ya neno imeunganika nawe na kuwa roho moja nawe, HII INAMAANISHA WEWE NI MTAKATIFU KAMA YEYE ALIYESEMA NAWE, NA UKAMSIKIA, ALIVYO; HUKU NDIKO KUMWAMINI!

>>UKIUNGANIKA NAYE NDIPO UNAKUWA NA NGUVU KAMA YEYE ALIVYO NA NGUVU, KWA KUWA UMEPOKEA NGUVU KUTOKA KWA ile roho ILIYOKUINGIA PALE ALIPOSEMA NAWE, NA WEWE UKAMSIKIA!!! UNAMSIKIA ROHO MTAKATIFU KWA MASIKIO YA ROHONI AU MOYONI MWAKO!!!

1) SIKILIZA NENO KWA MASIKIO YA NJE

2) FUNGUA MOYO WAKO KWA LILE NENO LIINGIE NDANI YAKO

3) NDIPOSA roho ya lile neno itakuingia NA KUKUSIMAMISHA JUU YA MWAMBA (EZEKIELI 2:2)

4) NDIPO UTAMSIKIA YEYE ALIYESEMA NAWE ROHONI MWAKO

5) UKIMSIKIA MAANA YAKE WEWE NA YEYE NI MMOJA (MMEUNGANIKA KATIKA ROHO); hapa ndipo umeunganika na nguvu zake, hekima yake, ufahamu wake, wema wake, kicho chake, utayari wake, mawazo yake kama tutakavyoona, n.k.

-HAPA NI KAWAIDA KWAMBA UTAYAFANYA MAPENZI YAKE PASIPO KUHIMIZWA KWA MAANA KAMA MAANDIKO YASEMAVYO;

“18Kwa kuwa nimejaa maneno;

Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.” (Ayubu 32:18)

>> ILE ROHO ILIYO NDANI YAKO NDIYO INAYOKUHIMIZA; MWAMINI ALIYEJAA ROHO HAWEZI KUHIMIZWA KUTOKA NJE, BALI ANAHIMIZWA KUTOKA NDANI NA ROHO MTAKATIFU; HUYU AMEJAA MANENO YA UZIMA; AMEJAA ROHO WA UZIMA KUPITIA IMANI YAKE ILIYO HAI KWA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI. ALIYEJAA ROHO HAHIMIZWI kuomba, kutenda mema, kusoma Biblia, kulitenda neno, kusamehe, kuachilia, kukaa na mke wake kwa akili, kumtii mumewe katika mambo yote na kuacha kabisa kuchukua uongozi wa kiroho kutoka kwa mumewe, n.k. ALIYEJAA ROHO NI MTIIFU KWA NENO NA ANALIISHI NENO MAANA MAISHA YAKE YOTE NI KRISTO!!! ANAISHI KWA NGUVU ZA MUNGU!!! ANAENDELEA KUTOKA NGUVU HADI NGUVU KADIRI ANAVYOENDELEA KUTOKA IMANI HADI IMANI!!!

2) USEMI WA MTAKATIFU

Imeandikwa, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; ............... WATASEMA KWA LUGHA MPYA.” (Marko 16:17)

>>Imezoeleka kwamba andiko hili limekuwa likitumika kwa habari ya Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha (Matendo ya Mitume 2:1-4) Lakini leo hii nataka nikuonyeshe maana moja ya kunena kwa lugha mpya kwa mtu aliyeokoka. Aliyeokoka ni yule anayemwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Huyu ni yule ambaye ni mwenye haki wa Mungu anayeishi kwa Imani ya Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa dunia yote. Alipokuwa akiwaambia wanafunzi wake kwamba watakamatwa na kupelekwa mabarazani kushtakiwa, aliwaeleza kwamba wasifikirie fikirie jinsi gani watakavyosema, maana Roho Mtakatifu atawapa saa ile ile nini cha kusema.

“Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.” (Mathayo 10:19-20)

>> KWENYE MASOMO YALIYOTANGULIA TULIONYESHA MUUNGANIKO WA MWAMINI NA ROHO MTAKATIFU KATIKA ROHO KWA MUJIBU WA 1 Kor 6:17 inayosema, “ Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.”

Yaani, (Roho Mtakatifu + roho yako) + nguvu za Roho = WEWE

Hapa kwenye Nguvu za Roho ndipo pana nguvu za ile roho ya andiko/neno uliloliamini, na unalolinena kwa Roho Mtakatifu. Unaweza kuwa unanena kwa roho ya maarifa, au roho ya kumcha Bwana, au roho ya shauri, au roho ya ufahamu, au roho ya hekima, roho ya nguvu, au roho ya ufunuo. Unaweza kuona na pia kunena kwa roho saba za Mungu zilizomo ndani yako kutegemeana na jinsi gani umejaa Roho!! Kumbuka tulisema kujaa Roho kwa Waefeso 5:18 ni kujaa roho kwa neno uliloliamini!! Yaani, unajaa Neno katika roho yako kwa Roho Mtakatifu kupitia imani yako iliyo hai kwa Yesu. Ulibatizwa kwa Roho Mtakatifu ili uendelee kujazwa Roho kupitia Neno la Kristo unaloendelea kuliamini. Ujazo wa Roho Mtakatifu ni endelevu. Mapenzi ya Mungu ni wewe kuendelea kujaa Roho kadiri unavyoendelea kujaa Neno unaloliamini. Hii ni kwa sababu hamna kipimo cha mwisho cha kujaa Roho maana imeandikwa Mungu hamtoi Roho kwa kipimo (Yohana 3:34). Bwana wetu Yesu alijaa Roho Mtakatifu pasipo kipimo (measureless measure!) Na huu ndio mpango wa Mungu kwa Kanisa lake!!! Yaani, wewe uliyejazwa Roho, ambaye umekuwa hekalu la Roho Mtakatifu, ambaye unaendelea kuongezeka kiimani, kwamba ujazwe Roho hadi kikombe chako kufikia kufurika na kumwagika!!! KWA KUJAA ROHO UNAKUWA UMEJAA MANENO YA UZIMA ROHONI MWAKO!!! “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” (Yohana 6:63) KUJAA ROHO NI KUJAA MAISHA YA KRISTO! KUJAA ROHO NI KUJAA UZIMA WA KRISTO! KUJAA ROHO NI KUJAA NGUVU ZA KRISTO! KUJAA ROHO NI KUJAA MAISHA YA NENO! KUJAA ROHO NI KUJAA YESU! KUJAA ROHO NI KUJAA ROHO SABA ZA MUNGU! NDIPOSA UNAPONENA UNAKUWA UNANENA KWA ROHO HUYU MTAKATIFU.

TUTAJUAJE KWAMBA ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAYENENA NDANI YAKO?

“Roho ya BWANA ilinena ndani yangu; Na neno lake likawa ulimini mwangu.” (2 Samueli  23:2)

>> ROHO MTAKATIFU AKINENA NDANI YAKO LAZIMA ATANENA NENO LA MUNGU TU PEKE YAKE; ROHO MTAKATIFU YEYE SIKUZOTE HUNENA;

1) HEKIMA YA NENO

2) MAARIFA YA NENO

3) UFAHAMU WA NENO

4) USHAURI WA NENO

5) KICHO CHA NENO

6) UWEZA WA NENO

7) UFUNUO WA NENO

>> ROHO MTAKATIFU AKINENA NDANI YAKO YEYE SIKUZOTE HUYAFUNUA MAANDIKO (LUKA 24:32) YANAYOMHUSU YESU, ILI UMJUE YESU, UMWELEWE YESU, UMFAHAMU YESU, UMTAMBUE YESU, UMTUKUZE YESU, UMWINUE YESU, UMWABUDU YESU, UMHIMIDI YESU, UMHESHIMU YESU, UMSIFU YESU, UMSHUKURU YESU, UMWAMINI YESU, UMFUATE YESU, UMTII YESU, UJITOE KWA YESU, UMKIMBILIE YESU, UMTUMAINIE YESU, UMTEGEMEE YESU, UMNYENYEKEE YESU, UJIDHILI KWA YESU, UMTANGULIZE YESU, YESU AWE KILA KITU KWAKO, UMWIMBIE YESU, UMTUMIKIE YESU, UISHI KWA AJILI YA YESU PEKE YAKE, UMPENDEZE YESU TU, UMFURAHISHE YESU TU, UYAFANYE MAPENZI YA YESU TU, UMCHEZEE YESU TU, UTEMBEE NA YESU, UFANYE KAZI NA YESU, UFANYE YOTE/UENDE KOTE/UMILIKI VYOTE/UWE VYOTE/UTENDE YOTE NA MAISHA YAKO YOTE KWA AJILI YA YESU!!!

>>HILI NDILO KUSUDI LA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU ILI KINYWA CHAKO KIMLETEE MUNGU UTUKUFU KWA NJIA YA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WA DUNIA YOTE!!!

>>KWA KUWA YESU NDIYE MWENYE KUIANZISHA NA KUIKAMILISHA IMANI YETU (WAEBRANIA 13:2) MANENO YAKE KINYWANI MWETU LAZIMA YAWE NI MANENO YA IMANI KUTOKA KWENYE ROHO WA IMANI ALIYEMO NDANI YETU TULIYEPEWA NA BWANA WETU YESU.KWA KUWA KWA MOYO MTU HUAMINI NA KWA KINYWA MTU HUKIRI....! (WARUMI 10:10)

LUGHA MPYA YA WATEULE, WATAKATIFU, WATOTO WA MUNGU NDANI YA YESU

Imeandikwa, “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena.” (2 Wakorintho 4:13)

>> KAMA KWELI UMEOKOKA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI LAZIMA USEME NA KUNENA KILE TU ULICHOKIAMINI!! KWA KUWA IMEANDIKWA PIA “ Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”(Warumi 10:10)

>> LUGHA YA IMANI NI LUGHA MPYA YA MTU ALIYEAMINI AU ALIYEOKOKA AMA ALIYEZALIWA MARA YA PILI.

>> ALIYEAMINI HUWA ANAONGEA NA KUKIRI KILE ALICHOKIAMINI NA SIYO KILE ANACHOKIONA KWA KUWA YEYE HAENENDI KWA KUONA KAMA MAANDIKO YASEMAVYO;

“(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)” (2 Wakorintho 5:7)

>> wasioamini ndio wanasemaga na kuzungumzia kila iitwapo leo mambo yanayoendelea na yanayoonekana; kila wakati wao huongea matatio tu na kupitisha hukumu zisizo za haki  kama: mambo magumu, mambo mabaya, mambo yanaharibika, hali mbaya, mambo yameharibika, mambo yamekwama, haiwezekani, hii ngumu,  mambo hayaendi, kanisa limepotea; kanisa limerudi nyuma; kanisa linakwenda kuwa dini tu fulani isiyookoa; n.k. USISEME HATAINGIA MBINGUNI AU HAWATAINGIA MBINGUNI UKAISHIA HAPO!! HUO NI UOVU MAANA UMEHUKUMU TAYARI KANA KWAMBA WEWE NI MUNGU!! SEMA HAWATAINGIA AU HATAINGIA MBINGUNI KAMA HATATUBU.....!!!!BWANA WETU YESU SIKUZOTE ALIWEKA OPTION AU KIPENGELE CHA REHEMA KWENYE KAULI ZAKE! UPENDO HAUFUNGI MLANGO MOJA KWA MOJA!!! HAINGII!! HATAINGIA!!! UNAJUAJE KAMA KESHO ATATUBU AU LA??!! KWANZA UNAMWOMBEA? AU ULIMWOMBEA?ULIAMINI ULICHOOMBA?

>> IMANI NI KUWA NA UHAKIKA YA MAMBO YATARAJIWAYO; NI BAYANA YA MAMBO YASIYOONEKANA (Waebrania 11:1)

-ANAYEAMINI ANA UHAKIKA MOYONI MWAKE UTOKAO KWA BWANA ALIYE ROHO KWAMBA YALE YOTE ANAYOYATARAJIA NI HAKIKA LAZIMA AYAPOKEE, AYAONE, YATOKEE, YAWE, NA YATUKIE HALISI KWENYE MWILI. IMANI INAKUPA UHAKIKA WA KESHO (ASSURANCE OF TOMORROW)

>> ANAYEAMINI PIA ANA USHAHIDI AU HATI MILIKI YA MAMBO YALE YASIYOKUWEPO BADO; YAANI, ANAMILIKI YASIYOKUWEPO NA YASIYOONEKANA ROHONI MWAKE, KINYWANI MWAKE, NA AKILINI MWAKE!!! KWA NINI? NI KWA SABABU AMEAMINI!!! ALIOMBA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU, AKAAMINI, AKAPOKEA, NA SASA ANASHUKURU, HUKU AKIMTUKUZA MUNGU KATIKA KUNGOJEA KWAKE KWA MATUMAINI YA UHAKIKA. (HE/SHE IS NOT WAITING IN VAIN)

>> Imeandikwa, “ Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:24)

>> KAMA ULIAMINI MOYONI MWAKO ULIPOKUWA UKISALI NA KUOMBA, LAZIMA UTAKUWA ULIPOKEA HAJA ZAKO MOYONI MWAKO, NA KINYWA CHAKO KITAKIRI KUWA TAYARI UNAZO HAJA ZA MOYO WAKO!! MAANA KWA MOYO MTU HUAMINI HATA KUPATA HAKI, NA KWA KINYWA MTU HUKIRI HATA KUPATA WOKOVU (WARUMI 10:10)

>> ULISALI NA KUOMBA NINI KUHUSU KANISA LA TANZANIA?  WATAKATIFU KWENYE MWILI WA KRISTO? HALI YA KIROHO TANZANIA? TAIFA LETU LA TANZANIA? HUYO NA YULE, NA WALE, NA HAO, NA WAO??!! ULISIMAMA KWENYE MAANDIKO YAPI? NA BAADA YA KUOMBA ULIAMINI NINI? NA KAMA ULIAMINI UNAONGEA NINI LEO?????!!!!! MANENO YA KINYWA CHAKO YANAKUSALITI KWAMBA HUKUAMINI CHOCHOTE NA KWAMBA ULIPOTEZA MUDA TU KWENYE KUOMBA KWAKO, NA HATA KUFUNGA!!! MAANA BADO UNAENENDA KWA KUONA!!!! UNAHUKUMU KWA KUFUATA YALE UNAYOYAONA KWA MACHO NA KUYASIKIA KWA MASIKIO KINYUME NA MAANDIKO, NA PIA KINYUME NA ALIVYOFANYA YESU ALIYEKUWA AMEJAA MACHO SABA AU ROHO SABA!!!

“1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. 2Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA; 3na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;” (Isaya 11:1-3)

>> YESU MWANA WA MUNGU ALITAZAMA KWA MACHO SABA YA MOYONI

>> MACHO HAYA SABA NI MACHO YA IMANI AMBAYO HAYATAZAMI MAMBO, AU VITU, AU HALI, AU MAZINGIRA KWA VILE YANAVYOONEKANA.

>> YESU HAKUHUKUMU WALA KUONYA KWA KUYAFUATA ALIYOYAONA KWA MACHO YAKE, WALA HAKUONYA KWA KUYAFUATA ALIYOYASIKIA KWA MASIKIO YAKE.MACHO NA MASIKIO YA YESU YALIKUWA NI YA MOYONI MWAKE (ROHONI MWAKE)

>> MAPENZI YA MUNGU NI KWAMBA WANAWE WALIO NDANI YA MWANAWE YESU KRISTO NAO WASIHUKUMU WALA WASIONYE KWA KUFUATA YALE WAYAONAYO KWA MACHO YAO NA YALE WAYASIKIAYO KWA MASIKIO YAO. WALIOOKOKA WANATAKIWA KUTOA HUKUMU YA HAKI INAYOTOKANA NA IMANI YA YESU. UNAAMINI KWANZA, UNAOMBA NA KUAMINI, UNAENENDA KWA IMANI; IMANI KWA AJILI YA KANISA, FAMILIA YAKO, UKOO WAKO, UKOO WA MUMEO/MKEO, TAIFA LAKO, N.K. BAADA YA KUAMINI LAZIMA UVIPIGE VITA VYA IMANI KWA AJILI YA HAO WOTE!!! THERE IS NO DELIVERY WITHOUT VICTORY!! (HAMNA KUPOKEA AHADI YA BWANA YOYOTE AU NENO LAKE LOLOTE KUTIMIA PASIPO KUPATA USHINDI KWENYE VITA VYA KIROHO, AMBAVYO NI VITA VILE VIZURI VYA IMANI!!!)

Yuda aliandika; “3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.” (Yuda mst 3)

>> LAZIMA KUISHINDANIA SANA IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU!!

>> SHETANI HAKUBALI KWAMBA WEWE UNAAMINI! HIVYO VITA VYAKE VYOTE NI KUIPINGA IMANI YAKO MTAKATIFU!! UKIWAZA NJE YA NENO ANAKUSHINDA! UKIONGEA KINYUME NA NENO ANAKUSHINDA! UKITENDA KINYUME NA NENO ANAKUSHINDA PIA! UKIHUKUMU KWA KUFUATA UNAYOYAONA KWA MACHO AU UNAYOYASIKIA KWA MASIKIO ANAKUSHINDA! WATEULE WENGI WAMESHINDWA VITA VYA KIROHO, NA HATA WATUMISHI PIA! WANAHITAJI KUKWAMULIWA KWA MAMOMBI NA MAFUNDISHO YENYE UZIMA ILI WAJUE WAMEKUWA WAKITENDA DHAMBI MAANA IMEANDIKWA KWAMBA “....KILA TENDO LISILOTOKA KWENYE IMANI NI DHAMBI!!! (WARUMI 14:23)” MANENO YAKO YASIYO YA IMANI NI DHAMBI!! MAWAZO YAKO YASIYO YA IMANI NAYO NI DHAMBI!! MATENDO YAKO YASIYO YA IMANI NAYO NI DHAMBI!!! MTENDA DHAMBI NI MTUMWA WA SHETANI!!

KAULI ZA ASIYEAMINI

“14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.” (1 Yohana 5:14-15)

Biblia iko wazi hapa kwamba;

1) UKIOMBA KITU SAWASAWA NA MAPENZI YAKE, ANAKUSIKIA (WEWE ULIYEOKOKA)

2) NA UKIJUA KWAMBA ANAKUSIKIA, UOMBACHO CHOCHOTE

3) UNAJUA KWAMBA UNAZO ZILE HAJA ULIZOMWOMBA

>>ANDIKO HILI UKIUNGANISHA NA MARKO 11:24 KWAMBA, “ Yo yote myaombayo mkisali, aminini kwamba mnayapokea, Nayo yatakuwa yenu.” LINAKUPA KUPOKEA NA KUMILIKI KILE ULICHOOMBA KATIKA SALA ZAKO, NA BAADA YA MAOMBI YALE UNAZO HAJA ZOTE ZA MOYO WAKO.

>> KAULI YA KWANZA MAARUFU YA ASIYEAMINI NI HII;

●MUNGU ATAJIBU TU!

●NAMSUBIRI MUNGU ATAJIBU KWA WAKATI WAKE!

●NIMEMWOMBA MUNGU NASUBIRI MAJIBU

>> NI WAPI KWENYE MAANDIKO HAYA MAWILI INAPOONYESHA KWAMBA MUNGU ATAJIBU??!!!

>> IKO WAZI HAPA KWAMBA UNAPOKEA MAJIBU YAKO WAKATI ULE ULE UNAPOSALI NA KUOMBA KWA IMANI (MK 11:24)

>> IKO WAZI PIA KWAMBA UNAPOMWOMBA MUNGU SAWASAWA NA MAPENZI YAKE, KWENYE NENO LAKE, KWA ROHO WAKE, YEYE ANAKUSIKIA; NA KWA KUWA AMEKUSIKIA UNAONDOKA KWENYE MAOMBI UKIWA NA ZILE HAJA ZA MOYO WAKO TAYARI UMEZIPOKEA ROHONI (MOYONI) MWAKO

>> KWA MAANDIKO YOTE MAWILI UNAONDOKA KWENYE MAOMBI NA SALA ZAKO TAYARI UKIWA NA HAJA ZA MOYO WAKO, NA SIYO KWAMBA MUNGU ATAKUJIBU KWA WAKATI WAKE!!!

>> NI LAZIMA UPOKEE KWA IMANI, NA UINGIE KWENYE MAISHA YA SHUKRANI NA KUMPA MUNGU UTUKUFU ALIYEKUTENDEA, AU ALIYEKUPONYA, AMA ALIYELETA UAMSHO, AU ALIYEWAREHEMU NA KUWAPA NEEMA WALE ULIOWAOMBEA; NA ALIYETENDA MAMBO MAKUU SAWASAWA NA AHADI ZAKE ULIZOZIAMINI, NA NENO LAKE ALILOLISEMA AMBALO WEWE UMELIAMINI, N.K.

>>UNAPOKUWA UMEAMINI HIVYO UNAANZA KUTEMBEA KAMA MMOJA ALIYETENDEWA TAYARI, AU ALIYEPOKEA TAYARI, AU ALIYEONA TAYARI, AMA ALIYEPEWA TAYARI, AMA KAMA MMOJA ANAYEJUA IMEKUWA TAYARI, N.K. YAANI, UNAISHI UKIWA NA MAJIBU YA MAOMBI, SALA, NA DUA ZAKO. HII INAONDOA UHITAJI WOTE MAISHANI MWAKO KWA NEEMA YAKO.

>> SASA KAMA UMEAMINI KWA NINI UNALALAMIKA? KAMA UMEAMINI KWA NINI UNASIKITIKA? KAMA UMEAMINI KWA NINI UNANUNG’UNIKA? KAMA UMEAMINI KWA AJILI YAKE AU KWA AJILI YAO KWA NINI UNAHUKUMU KWAMBA HAWATAINGIA MBINGUNI? KAMA UNAVIPIGA VITA VYA IMANI KWA AJILI YAO KWA NINI UNAWAHUKUMU? KAMA ULIPOOMBA AU KUOMBEWA ULIPOKEA UPONYAJI, KWA NINI UNASEMA UNAUMWA BADALA YA KUMSHUKURU MUNGU KWAMBA KWA KUPIGWA KWAKE YESU WEWE UMEPONA??!! KAMA UMEAMINI KWA NINI UNADAI TALAKA? KWA NINI UNAJUTA KUOANA NAYE? KAMA UMEAMINI KWA NINI UNAONGEA KINYUME NA KWELI? MANENO YAKO YANAKUSALITI KWAMBA WEWE NI MUOVU TU USIYEAMINI NENO LA MUNGU NA NDIYO MAANA UNAONGEA YALE TU UNAYOYAONA NA KUYASIKIA. HII NI KWA SABABU MOYONI MWAKO HAUNA NENO LA MUNGU ULILOLIAMINI KUHUSU HAYO UNAYOYASEMA NA KUYAHUBIRI!!! HAUMWAMINI YESU!!! NA KAMA ULIMWAMINI, BASI UJUE UMEACHA KUENENDA KWA IMANI NA SASA UNAENNENDA KWA KUONA. LUGHA YA MTEULE NI KWAMBA “IMEKWISHA!!” BWANA AMETENDA! NIMEPONA NAMSHUKURU MUNGU! KANISA LINAONGEZEKA KILA SIKU KWA WALE WANAOOKOLEWA! WANANGU WANAMCHA BWANA, NAO NI HODARI KATIKA BWANA NA KATIKA UWEZA WA NGUVU ZAKE!!! IBRAHIMU BABA YETU WA IMANI HAKUENENDA KAMA WEWE!! YEYE HAKUANGALIA UMRI WAKE ULIOKWISHA KUSOGEA SANA MPAKA MIAKA MIA, NA WALA HAKUTAZAMA UZEE WA SARA MAANA NAYE ALIKUWA BIBI KIZEE SASA. AKAWA AKISEMA “MIMI NI BABA WA MATAIFA MENGI!!” MIMI NINA WATOTO WENGI KAMA MCHANGA WA BAHARI NA KAMA NYOTA ZA MBINGUNI!!! N.K. IBRAHIMU HAKUTAZAMA HALI ZA MACHO ZINAZOKATISHA TAMAA NA KURUDISHA NYUMA KIIMANI!! HEBU MSIKILIZE ROHO MTAKATIFU KWENYE NENO HILI;

“16Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; 17(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. 18Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 19Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. 20Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; 21huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. 22Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki. 23Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; 24bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; 25ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.” (Warumi 4:16-25)

1) LUGHA YA MUNGU INAYOFUNULIWA HAPA NI LUGHA YA IMANI: “YAANI, KUYATAJA YASIYOKUWAKO KANA KWAMBA YAMEKUWAKO”

>> LUGHA MPYA YA MTAKATIFU , MWANA WA MUNGU NI KUYATAJA, AU KUYATAMKA, AMA KUYANENA, AU KUYAKIRI, AU KUYATANGAZA, AMA KUYASEMA, AMA KUYASHUHUDIA YASIYOKUWAKO KANA KWAMBA YAMEKUWAKO KWA KUWA TU UMEMUAMINI YESU. HII NI LUGHA AMBAYO MSINGI WAKE NI LILE NENO LA MSALABA, IMEKWISHA!!! (YOHANA 19:3O)

>> HII MAANA YAKE UNAYAONA YASIYOONEKANA, UNAYASIKIA YASIYOSIKIKA,UNAYAMILIKI YASIYOONEKANA BADO NA YASIYOKUWEKO,  NA MWISHO WAKE NI KUYATENDA YASIYOWEZEKANA KIBINADAMU BAADA YA KUONGEZEWA NEEMA YAKE KAMA TULIVYOONA KWENYE MASOMO HAYA YALIYOTANGULIA.

>> BABU IBRAHIMU ALIENDELEA KUYATAJA YASIYOKUWAKO KANA KWAMBA YAMEKUWAKO MPAKA ISAK A AKAZALIWA!!! KISHA YAKOBO, KISHA WALE KUMI NA MBILI, NA MMOJA WAO YUDA, AMBAYE KATIKA UZAO WAKE AMETOKEA KRISTO YESU MWANA WA DAUDI,  NA KWA YEYE IBRAHIMU AMEJIPATIA WATOTO WENGI KAMA MCHANGA WA BAHARI, NA KAMA NYOTA ZA MBINGUNI.

>> IMANI YA YESU INAKAMILISHA NA KUTIMIZA YASIYOWEZEKANA. LAKINI LAZIMA AWEPO MMOJA ANAYEAMINI AMBAYE, KAMA IBRAHIMU,

2) ATAAMINI KWA KUTARAJIA YALE YASIYOWEZA KUTARAJIWA (MST 18) ILI NENO LA MUNGU LITIMIZWE NA BWANA YESU APATE KUTUKUZWA KWA YEYE.

3) YULE AMBAYE ATAYAONDOA MACHO YAKE KWENYE HALI NGUMU, HALI MBAYA, MWILI UNAOUGUA, MAUMIVU ALIYONAYO, MATESO ANAYOYAPITIA, MAMBO YANAYOHARIBIKA, MAMBO YALIYOKWAMA, MAMBO AMBAYO HAYAENDI, N.K. HALAFU AKAITAZAMA AHADI YA BWANA YESU

-HATASITA KWA KUTOAMINI  KWA MFANO WA IBRAHIMU

-HATAZIFUATA FIKRA ZAKE ZINAZOISHIA KWENYE YALE YANAYOONEKANA

-AMBAYE ATATIWA NGUVU KWA IMANI KAMA ILIVYOKUWA KWA IBRAHIMU.

- TENA ATATIWA NGUVU HIVYO HUKU AKIJUA HAKIKA KWAMBA MUNGU HAWEZI KUDANGANYA, NA WALA HAWEZI KUSHINDWA KUFANYA NENO LOLOTE, BILA KUJALI HALI NI MBAYA KIASI GANI. YEYE ATATEMBEA TU NA SAUTI YA MUNGU PEKE YAKE, ILIYOMO MOYONI MWAKE (ROHONI MWAKE,) KUTOKA KWENYE ILE ROHO YA IMANI ILIYOMO NDANI YAKE KUPITIA LILE NENO ALILOLIAMINI.

>> HUYU NDIYE MTAKATIFU ANAYEMWAMINI MUNGU PASIPO KUYUMBAYUMBA WALA KUSITASITA, WALA KURUDI NYUMA, WALA MANUNG’UNIKO, WALA KUKATA TAMAA, WALA KUVUNJIKA MOYO, WALA YOYOTE KAMA HAYO.

Kumbuka utahukumiwa sawasawa na maneno yako, na utahesabiwa haki kutokana na maneno yako pia.

“34Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 35Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. 36Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” (Mathayo 12:34-37)

44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka. 45Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka. 46Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 48Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.” (Yohana 12:44-50)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post