UTAKATIFU (HOLINESS)

                   Calvary Pictures | Download Free Images on Unsplash

   UTAKATIFU (HOLINESS)

Katika sehemu hii ya kwanza tutaangalia maeneo matatu;

1) UTAKATIFU KATIKA ROHO (holiness in spirit)

2) UTAKATIFU KATIKA NAFSI (holiness in soul)

3) UTAKATIFU KATIKA MWILI (holiness in body)

 

1) UTAKATIFU KATIKA ROHO 

UTANGULIZI

“1 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu; 2ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; 3yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, 4NA KUDHIHIRISHWA KWA UWEZA KUWA MWANA WA MUNGU, KWA JINSI YA ROHO YA UTAKATIFU, KWA UFUFUO WA WAFU, YESU KRISTO BWANA WETU; 5ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; 6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo;” (Warumi 1:1-6)

4NA KUDHIHIRISHWA KWA UWEZA KUWA MWANA WA MUNGU, KWA JINSI YA ROHO YA UTAKATIFU, KWA UFUFUO WA WAFU, YESU KRISTO BWANA WETU;” (Warumi 1:4)

New King James Version
and declared to be the Son of God with power according to the Spirit of holiness, by the resurrection from the dead” (Romans 1:4)

New American Standard Bible
who was declared the Son of God with power according to the Spirit of holiness by the resurrection from the dead, Jesus Christ our Lord,” (Warumi 1:4)

>> BWANA WETU YESU ALIFANYIKA, NA KISHA KUTAMKWA, NA KUDHIHIRISHWA KUWA NI MWANA WA MUNGU MWENYE NGUVU ZA MUNGU

>> ALIFANYIKA MWANA WA MUNGU HIVYO KWA ILE [Roho ya Utakatifu]

>> ROHO HIYO YA UTAKATIFU NDIYO ILE ILE ILIYOMFUFUA KUTOKA KWA WAFU

Roho ya Utakatifu ndiyo yenye Nguvu za Utakatifu! Nguvu hizi za Utakatifu ndizo zilizozishinda nguvu za dhambi (alipoishi pasipo kutenda dhambi); na pia zikazishinda nguvu za mauti (alipofufuka kutoka kwa wafu).

Lakini kubwa zaidi ni kwamba Bwana wetu Yesu alizaliwa akiwa Mtakatifu kama maandiko yasemavyo:

“34Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? 35Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (Luka 1:34-35)

>> UTUNGAJI MIMBA YA BWANA YESU ULIKUWA HIVI:

1) Roho Mtakatifu atakujilia ju yako

2) Atakapokujilia juu yako huyo Roho Mtakatifu, Nguvu zake Aliye Juu zitakufunika kama kivuli

MATOKEO

3) Kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa, KITAKATIFU, MWANA WA MUNGU

LEO HII, ILI WEWE UNAYESOMA UWE MTAKATIFU NI LAZIMA:

1) AWEPO ROHO MTAKATIFU

2) KILA ALIPO ROHO MTAKATIFU ZIPO NA NGUVU ZAKE ALIYE JUU, BABA YETU WA MBINGUNI; YAANI, HUWEZI KUMTENGANISHA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!(MATENDO 1:8) NGUVU ZA MUNGU NI NGUVU ZA NENO LAKE, AMBAZO ZIMO KWA ROHO WA NENO.

3) LAZIMA UWEPO MTENDA DHAMBI UNAYEZITUBIA DHAMBI ZAKO KWA KUMWAMINI YESU KRISTO, MTAKATIFU, MWANA WA MUNGU, KWA MARA YA KWANZA (UNAOKOKA AU UNAZALIWA MARA YA PILI), BAADA YA KUSOMA AMA KUSIKIA NENO HILI TAKATIFU LA MUNGU LILILOHUBIRIWA AU KUFUNDISHWA KWA ROHO MTAKATIFU [YOHANA 3:3-7)

4) LAZIMA UWE UMESIKIA NENO LA KWELI YA INJILI YA YESU KRISTO, AU UMELISOMA, NA KULIAMINI, NA KULIPOKEA MOYONI MWAKO! YAANI, UMELIFUNGULIA NENO HILO MOYO WAKO, NA KULIRUHUSU LIINGIE NA KUTENDA KILE LILICHOSEMA LITAKITENDA, KWA MAANA IMANI CHANZO CHAKE NI KULISIKIA MOYONI MWAKO/ROHONI MWAKO NENO LA KRISTO (YOHANA 10:17)

5) NDIPOSA MUNGU HUACHILIA NEEMA YAKE YA WOKOVU (SAVING GRACE) KWAKO KWA KUKUSAMEHE DHAMBI ZAKO,  NA KUKUPA UZIMA WA MILELE, KWA SABABU UMEMWAMINI MWANAWE PEKEE YESU KRISTO ALIYEMTUMA ULIMWENGUNI KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KILICHOPOTEA (LUKA 19:10 &TITO 3:3-4)

MUHIMU: KAMA UMEOKOKA WEWE NI MTAKATIFU UNAYEISHI MAISHA YA UTAKASO KUPITIA KUITII KWELI (1 PETRO 1:22a). KILA NENO UNALOLIAMINI LINAENDELEA KUKUTAKASA ROHO, NAFSI, NA MWILI WAKO WOTE KAMA TUTAKAVYOONA!

“22Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.” (Warumi 6:22)

Na tena;

“11Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa” (Ufunuo 22:11)

>> PASIPO UTII WA KWELI (NENO LA MUNGU) HAMNA UTAKASO!! KADIRI UNAVYOZIDI KUONGEZEKA KATIKA UTII, MAANA YAKE UNAONGEZEKA KIIMANI! NA KAMA UNAZIDI KUMWAMINI MUNGU MAANA YAKE UNAZIDI KUHESABIWA HAKI MBELE ZAKE!!

“16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. 17KWA MAANA HAKI YA MUNGU INADHIHIRISHWA NDANI YAKE, TOKA IMANI HATA IMANI; KAMA ILIVYOANDIKWA, MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI.” (Warumi 1:16-17)

>> UNAPOMWAMINI YESU MOYONI MWAKO NA KUHESABIWA HAKI, UKIISHA KUSAMEHEWA DHAMBI ZAKO, NA KUFANYWA HAI MILELE, HUKO NDIKO KUOKOKA; (WARUMI 10:9-10) NA KISHA BAADA YA HAPO UNAENDELEA KUISHI KWA IMANI HIYO TAKATIFU SANA (WARUMI 1:17) MAISHA YAKO YOTE HUKU UKILITII NENO LA MUNGU, (1 PETRO 1:14) LINALOENDELEA KUKUTAKASA!! HAKI AMA UTAKATIFU WA MUNGU UNAZIDI KUDHIHIRISHWA NDANI YAKO KADIRI UNAVYOZIDI KULITII AMA KULITENDA NENO LA MUNGU! NA HII NDIYO MAANA YAKOBO ALISISITIZA WALIOOKOKA WAWE WATENDAJI WA NENO, NAO WATAKUWA HERI (BARIKIWA) KATIKA KUTENDA KWAO KOTE!!(YAKOBO 1:22-25) DALILI KUU Y A MWONGO, AMBAYE HAJAOKOKA, NA WALA SIYO MTAKATIFU, NI KUTOISHI SAWASAWA NA NENO LA MUNGU! YAANI, KUTOISHI MAISHA YA KULITII NENO LA MUNGU! MAANA HAMNA MAISHA NJE YA NENO LA MUNGU! MAISHA YA MTAKATIFU NI KULITENDA NENO! UTAKATIFU WOTE WA MUNGU BABA YETU, NA WA BWANA WETU YESU KRISTO UMEFUNULIWA KWENYE NENO LAKE TULILOLIAMINI TUKAOKOKA, NA TUNALOLIAMINI NA TUNAENDELEA KUTAKASIKA!

Sasa tukirudi hapo juu kidogo tuliona kwamba Yesu ALIZALIWA AKIWA MTAKATIFU!! Ndiyo maana malaika Gabrieli alisema, “? 35..............Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (Luka 1:35)

>> UTAKATIFU WA YESU ULITOKANA NA;

1) NENO LA MUNGU TAKATIFU KWA MKONO WA MALAIKA (LUKA 1:28, 30-33)

NENO HILI KUTOKA KITI CHA ENZI LILIBEBA;

MST 28: SALAMU ZA MUNGU, UFUNUO WA NEEMA ALIYOPEWA MARIAMU NA MUNGU, NA HAKIKISHO KWAMBA BWANA ALIKUWA PAMOJA NAYE,

MST 30: KUONDOLEWA HOFU NA HAKIKISHO LA KWAMBA AMEPATA NEEMA KWA MUNGU,

MST 31:  UJAUZITO WA MARIAMU, UZAZI WAKE, KWAMBA ATAZAA MTOTO MWANAMUME, NA KWAMBA ATAMWITA JINA LAKE YESU,

MST 32: TAARIFA KUTOKA MBINGUNI KWAMBA MTOTO HUYO ATAKUWA MKUU, ATAITWA MWANA WA ALIYE JUU, NAYE ATAPEWA KITI CHA UFALME CHA DAUDI BABA YAKE (KWAMBA ALITOKEA UKOO WA DAUDI),

MST 33: TAARIFA ZAIDI KWAMBA UFALME WAKE HAUTAKUWA NA MWISHO, NA KWAMBA UTAKUWA NI WA MILELE.

>> HILI NDILO NENO LA BWANA KWA MKONO WA MALAIKA KWA BIKIRA MARIAMU; NA NENO LENYEWE LINAONYESHA KWAMBA MTOTO YESU ANGEZALIWA AKIWA MTAKATIFU (MST 32)

MST 34; MARIAMU AKAULIZA NENO LILE LITATIMIZWAJE WAKATI YEYE HAJUI MUME, YAANI NI BIKIRA?

>> NDIPO MARIAMU ALIPOMUULIZA MALAIKA KWAMBA LITATIMIZWAJE NENO LILE MAANA YEYE HAJUI MUME BADO (YAANI, NI BIKIRA?) JIBU NI HILI KWENYE MSTARI WA 35;

“ 35Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (LUKA 1:35)

JIBU;

1) ROHO MTAKATIFU ATAKUJILIA JUU YAKO,

2) NGUVU ZAKE ALIYE JUU ZITAKUFUNIKA KAMA KIVULI,

3) KWA SABABU HIYO YA KWENYE (1) NA (2) NDIPOSA HICHO KITAKACHOZALIWA KITAITWA KITAKATIFU MWANA WA MUNGU,

KITAKATIFU MWANA WA MUNGU (YESU) = {ROHO MTAKATIFU + NGUVU ZAKE} KWENYE ROHO, NAFSI, NA MWILI WA MARIAMU

KUZALIWA KWA YESU KULIHITAJI;

1) NENO LA MUNGU,

2) MOYO UNAOAMINI NA KULIPOKEA NENO LA MUNGU WA BIKIRA MARIAMU

3) ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE

HALI KADHALIKA BIBLIA INAPOSEMA KWA HABARI YA KUZALIWA MARA YA PILI KWA MWANADAMU MTENDA DHAMBI;

“3Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili;” (Yohana 3:3-7)

KINACHOHITAJIKA NI;

1) NENO LA MUNGU LINALOHUBIRIWA AU KUFUNDISHWA KWA NJIA ZOTE

2) MOYO WA MTENDA DHAMBI

3) IMANI YA YESU MOYONI MWA MTENDA DHAMBI (YAANI, ATAKAYEMWAMINI YESU)

4) ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE (NDANI YA NENO, MAHUBIRI, AU MAFUNDISHO YALIYOVUVIWA NAYE (HOLY-SPIRIT-INSPIRED TEACHING OR PREACHING OR TESTIMONY)

5) NEEMA YA WOKOVU INAPATIKANA HAPA KUTOKA KITI CHA ENZI, NA YEYOTE AAMINIYE ANAZALIWA MARA YA PILI ROHO YAKE! (YOHANA 3:6)

>> UNAPOKUWA UMEZALIWA MARA YA PILI, KAMA ILIVYOKUWA KWA YESU, NA WEWE UNAZALIWA UKIWA MTAKATIFU!!! (YOU ARE BORN AGAIN HOLY!!! KUZALIWA MARA YA PILI, AMBAKO NDIKO KUOKOKA NI KUZALIWA KUTAKATIFU (HOLY BIRTH) MAANA WOTE WALIOHUSIKA NI WATAKATIFU!!!

AGENTS OF THE SECOND-BIRTH (WAHUSIKA WAKUU WA KUZALIWA MARA YA PILI)

1) NENO TAKATIFU LA MUNGU

>> NENO NI SAFI SANA NA TAKATIFU LILILOSAFISHWA MARA SABA KWENYE TANURU LA MUNGU (ZABURI 12:6 NA ZABURI 119:140) [THY WORD IS VERY PURE!!)

2) ROHO MTAKATIFU

>> HUYU NI ROHO WA MUNGU ALIYE JUU SANA, MTAKATIFU, MUUMBA WA MBINGU NA NCHI

3) IMANI TAKATIFU YA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU (THE HOLY FAITH OF JESUS)

>> BWANA YESU ALIZALIWA AKIWA NI MTAKATIFU MWANA WA MUNGU, AKAISHI MAISHA MATAKATIFU, AKASHINDA DHAMBI, AKAFANYWA KUWA DHAMBI YA ULIMWENGU (HE WAS MADE THE SIN OF THE WORLD), AKAICHUKUA DHAMBI YA ULIMWENGU (AKIWA NI MWANA-KONDOO WA MUNGU) KWENYE MWILI WAKE ULIOKUWA NI MFANO WA MWILI WA DHAMBI, AKATOLEWA KAMA SADAKA YA DHAMBI (SIN OFFERING), AKAIGONGOMELEA DHAMBI MSALABANI, AKAIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI, ADHABU ILIYOUPASA ULIMWENGU AKAICHUKUA YEYE, AKAFANYA UPATANISHO KWA KULIPA DENI LA DHAMBI, AKAWAWEKA HURU WANADAMU WOTE MBALI NA DHAMBI, AKAUWAWA MWILI WAKE, ROHO YAKE AKAHUISHWA AMBAYO KWA HIYO ALIWAENDEA ROHO WALIOKUWA KIFUNGONI TANGU ZAMANI ZA NUHU, AKAWAHUBIRI, AKAWAONDOA KUZIMU WENYE HAKI WOTE TANGU ZAMANI ZA NUHU, AKAWALETA PAMOJA NAYE PARADISO, MAANA AKAWA AMEMNYANG’ANYA SHETANI FUNGUO ZA MAUTI, NA MAUTI IKABATILIKA (MAUTI IKAFA), AKAFUFUKA KUTOKA KWA WAFU AKIWA AMESHINDA PIA MAUTI, NA KUMNYANG’ANYA SHETANI MAMLAKA YAKE YOTE JUU YA MWANADAMU, AKAWA AMEMHARIBU SHETANI ALIYEKUWA NA NGUVU ZA MAUTI, MAGONJWA , MARADHI, UMASKINI, NA UTUMWA WOTE JUU YA MWANADAMU KWA SABABU YA DHAMBI, AKAMWEKA YEYOTE AMWAMINIYE YEYE HURU MBALI NA DHAMBI, AKAWA AMEWAWEKA HURU WAFUNGWA WOTE WA DHAMBI NA UOVU, UBAYA WOTE, N.K. AKAWA AMEZIHARIBU NGUVU ZOTE ZA UOVU, UBAYA, DHAMBI, MATESO NA UONEVU WA KILA AINA WA SHETANI KWA WANADAMU KWA SABABU YA DHAMBI; AKAWA AMEVUNJA KILA NIRA NA KUONDOA KILA MZIGO MZITO KWA YEYOTE AMWAMINIYE;AKAWA AMETANGAZA UHURU MBALI NA DHAMBI, MBALI NA MAGOMJWA, MBALI NA MATESO YOTE YALIYOSABABISHWA NA DHAMBI!! AKAIANZISHA IMANI TAKATIFU IOKOAYO! IMANI YAKE YESU! YAANI, UNAMWAMINI YEYE TU, NAYE ANAFANYA YOTE ALIYOYAKAMILISHA MSALABANI! KWA KUWA AMEMALIZA YOTE PALE JUU MSALABANI! HAKUNA ALICHOSAZA AMBACHO BADO HAJAKAMILISHA! NDIYO MAANA ALITANGAZA “IMEKWISHA!!” WOTE WAMWAMINIYE YEYE WANAOKOLEWA KUTOKA DHAMBINI, NA WANAPONYWA MAGONJWA YAO YOTE, NA UDHAIFU WAO WOTE! LAKINI PIA WANABATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA MOTO! AMETUPA MAISSHA MAPYA YASIYOHARIBIKA! UZIMA NA KUTOHARIBIKA UMEFUNULIWA! INJILI SASA NI HABARI NJEMA! KWAMBA KUNA TOBA NA MSAMAHA WA DHAMBI VINAHUBIRIWA! UKIAMINI UNAOKOKA! IMANI YA YESU INASAFISHA MOYO KABISA!!! UKIMWAMINI ANAKUPA MAISHA MAPYA YASIYOHARIBIKA, AMBAYO NDIYO UZIMA WA MILELE; UTAKATIFU NI UZIMA WAKE WA MILELE NDANI YA KILA AMWAMINIYE! UTAKATIFU NI MAISHA YAKE YA MILELE NDANI YAKE KILA AAMINIYE! UTAKATIFU NI UHAI WAKE WA MILELE NDANI YA MWAMINI! MTAKATIFU AMESHINDA DHAMBI NA MAUTI! ANAISHI KWA NGUVU ZA NENO TAKATIFU LA MUNGU! MTAKATIFU ANALIISHI NA KULITENDA NENO KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKE!!

“7Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. 8Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; 9WALA HAKUFANYA TOFAUTI KATI YETU SISI NA WAO, AKIWASAFISHA MIOYO YAO KWA IMANI.” (Matendo ya Mitume 15:7-9)

>> ILI UWE MTAKATIFU WAJIBU WAKO NA JUKUMU LAKO NI MOJA TU: KUMWAMINI YESU ALIYETUMWA NA BABA

>> ILI UISHI MAISHA MATAKATIFU, WAJIBU WAKO NA JUKUMU LAKO KUU NI MOJA TU; KUMWAMINI YESU ALIYETUMWA NA BABA.  YAANI, UISHI KWA IMANI YA YESU, MWANA WA MUNGU!!!

“20Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” (Wagalatia 2:20)

>> WATAKATIFU WANAISHI HAPA DUNIANI KWA IMANI YA MWANA WA MUNGU, YESU

>> WANAOOKOKA HUWA WANAZALIWA WAKIWA WATAKATIFU, NA KISHA HUENDELEA KUISHI MAISHA HAYO MATAKATIFU, KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAO, KUPITIA IMANI YAO KWA NENO LILILO HAI LA MUNGU! NENO LI HAI KWAO KWA SABABU YESU AMEFUFUKA NA ANAISHI! YESU NDIYE HILO NENO LA UZIMA! (JESUS IS THE LIVING AND ENDURING WORD OF LIFE!)

UTAKATIFU NI NINI BASI?

>> UTAKATIFU NI MAISHA YA NENO LA MUNGU, AMA MAISHA YA YESU ALIYEFUFUKA KUTOKA KWA WAFU, ANAYOYAISHI MTOTO WA MUNGU ALIYEZALIWA MARA YA PILI KUPITIA IMANI ILIYO HAI KWA YESU KRISTO, ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE, ALIYEMWAMINI, NA KUMPOKEA MOYONI MWAKE, NA SASA ANAISHI KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU YULE YULE, ALIYEKUWAMO NDANI YA YESU, NA ALIYEMFUFUA YESU KUTOKA KWA WAFU, NA NDIYE ANAYEMWEZESHA KWA NGUVU ZAKE, KULIISHI NA KULITENDA NENO LA MUNGU NA MAPENZI YAKE YOTE, SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKE KWENYE MWILI WA DAMU NA NYAMA.

UTAKATIFU UKIFAFANULIWA

1) UTAKATIFU NI MAISHA YA ROHO YA UTAKATIFU NA NGUVU ZAKE ZA NENO LA MUNGU TAKATIFU

2) MAISHA HAYA NDIYO YALE ALIYOYAISHI YESU, NENO LA MUNGU, ALIPOKUWA KWENYE MWILI

3) MTOTO WA MUNGU ALIYEMWAMINI YESU, AMEZALIWA MARA YA PILI AKIWA MTAKATIFU, NA NDIPOSA AMEANZA KUYAISHI MAISHA HAYA YA YESU, AU MAISHA YA NENO LA MUNGU

4) MAISHA HAYA ANAYAISHI KWA IMANI ILE ILE YA MWANA WA MUNGU YESU

5) ANAYAISHI MAISHA HAYA KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE, AKILITENDA NENO LA KRISTO SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKE

6) NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU NI NGUVU ZILE ZILIZOMFUFUA YESU KUTOKA KWA WAFU, NA NDIYO HIZO ZINAZOMWEZESHA AAMINIYE KUISHI MAISHA YA YESU ALIYEFUFUKA

7) MAISHA KATIKA NGUVU ZA UFUFUO WA YESU NI MAISHA YENYE USHINDI JUU YA DHAMBI NA MAUTI, ANAYOYAISHI MWANA WA MUNGU, KWA ROHO WA MUNGU, AKIYATENDA MAPENZI YA MUNGU YOTE YALIYOMO KWENYE NENO LAKE, KWA JINA LA YESU KRISTO ALIYEFUFUKA KUTOKA KWA WAFU; NA SASA ANAKAA NDANI YAKE YEYE AMWAMINIYE AKIMWEZESHA KWA NAMNA ZOTE KUYATENDA YOTE YANAYOMPENDEZA MUNGU NDANI YAKE KRISTO YESU ALIYE BWANA NA MWOKOZI WAKE!!

“ Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminilo jina lake; 13 waliozaliwa,  SI KWA DAMU, WALA SI KWA MAPENZI YA MWILI, WALA SI KWA MAPENZI YA MTU, bali KWA MUNGU.” (Yohana 1:11-13)

>> WATAKATIFU WANAZALIWA WAKIWA WATAKATIFU MAANA MBEGU INAYOWAZAA NI MBEGU TAKATIFU AMBAYO NI NENO LA MUNGU

“ Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.” (1 Petro1:23)

>> Ni roho yako inayozaliwa mara ya pili; “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” (Yohana 3:6)

>> Ni roho yako inayozaliwa mara ya pili; kule kusema kuzaliwa maana yake ni uumbaji mpya! maana mimba inapotungwa kiumbe kinachoumbwa tumboni mwa mama ni kiumbe kipya ambacho hakijawahi kuwepo hapa duniani kabla; kadhalika roho yako ilikufa kwa sababu ya dhambi zako. (Waefeso 2:1) Ni lazima ufufuliwe ili uweze kuwa hai!! Na maandiko yanasema Yesu alipofufuliwa na sisi tulifufuliwa pamoja naye (Waefeso 2:5-6)

>> KUOKOKA NI WEWE KUFUFULIWA KUTOKA KWENYE MAUTI YA KIROHO (SPIRITUAL DEATH)

>> UNAFUFULIWA NA KISHA UNAFANYWA UPYA KAMA MAANDIKO YASEMAVYO;

“ Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;” (Tito 3:4-6)

>> YEYOTE ANAYETAKA KUWA MTOTO WA MUNGU HATAKIWI KUFANYA LOLOTE WALA CHOCHOTE ILI AWE MTAKATIFU, BALI ANATAKIWA KUMWAMINI TU YESU, NA NDIPO ANAZALIWA MARA YA PILI AKIWA MTAKATIFU: YAANI, KAMA WARUMI 1:4 ISEMAVYO; ANAZALIWA KWA NGUVU ZA MUNGU MARA YA PILI, KUWA MWANA WA MUNGU, KWA ROHO MTAKATIFU, KWA KUFUFULIWA KUTOKA KWENYE MAUTI YA KIROHO, NA KUFANYWA UPYA PALE ANAPOMWAMINI YESU!!

>> WEWE NI MTAKATIFU KWA KUZALIWA (YOU ARE HOLY BY SECOND-BIRTH), NA HAUWEZI KAMWE KUWA MTAKATIFU KWA MATENDO MEMA YOYOTE, AU MATENDO YA HAKI YOYOTE! 

Daudi alieleza waziwazi hali ya kiroho ya mwanadamu aliyezaliwa baada ya Adamu!! Na hii ndiyo hali ya wanadamu wote tangu anguko la mwanadamu  dhambini, maana wote walikuwa viunoni mwa Adamu;

“ Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani” (Zaburi 51:5)

>> KILA MWANADAMU ALIUMBWA TUMBONI MWA MAMA YAKE KATIKA HALI YA UOVU

>> MIMBA YA KILA MWANADAMU ILITUNGWA AU ILICHUKULIWA NA MAMA YAKE AKIWA HATIANI

>> HIVYO NI DHAHIRI WANADAMU WOTE HUZALIWA WAKIWA KATIKA HALI YA UOVU NA HATIA MBELE ZA MUNGU

>>HII MAANA YAKE roho ya mwanadamu ni roho ya uovu au roho ya dhambi!!! Ni roho iliyokufa kiroho kwa kuwa haina uhai wa kiroho wa Mungu, au maisha ya kiroho ya Mungu, Aliye Roho!

“ roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa;.................” (Ezekieli 18:20)

“ nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu” (Waefeso 2:1)

“walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mbaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” (Mwanzo 2:17)

>>TANGU ADAMU, WANADAMU WOTE WANAZALIWA WAKIWA WAMEKUFA HAKIKA, MAANA WOTE WAMO DHAMBINI!!!

>> MAITI HAIWEZI KUJIFUFUA KAMWE KWA NAMNA YOYOTE! UNAPOTAFUTA KUWA MTAKATIFU KWA KUFUNGA, KUTOA, KUSALI SANA, KUSOMA BIBLIA, N.K. ILI UWE MTAKATIFU KWA MATENDO HAYO PEKE YAKE, UNAJIDANGANYA MAANA HAUHESABIWI HAKI KAMWE KWA MATENDO YAKO YA HAKI! ISITOSHE UNAYAFANYA HAYO YOTE UKIWA TAYARI WEWE UMEKUFA KIROHO! UNAHITAJI KUFUFULIWA KWANZA ILI UWEZE KUYATENDA HAYO NA MENGINE KAMA HAYO KWA NEEMA YA MUNGU; YAANI, KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE

>> WEWE NI MTAKATIFU roho yako KAMA UMEZALIWA MARA YA PILI

>> NA WEWE NI MTAKATIFU roho yako KAMA UNAISHI NA KUENENDA KWA IMANI YA YESU; YAANI, KAMA UNAISHI KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU; KAMA UNAISHI NA KUENENDA KWA KULITENDA NENO KWA NEEMA YAKE YESU!!! WEWE NI MTAKATIFU KAMA MAISHA YAKO YOTE MSINGI WAKE NI UTII WA NENO LA MUNGU AMBALO NDILO KWELI; KWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKO! KWA MAANA UNAOKOLEWA KWA ROHO MTAKATIFU , NENO LA KRISTO, NA NGUVU ZAKE; NA KISHA UNAENDELEA KUISHI KWA ROHO MTAKATIFU HUYO HUYO NA NGUVU ZAKE, KWA KULITENDA NENO LA MUNGU.

MUHIMU:

>>UNAZALIWA MARA YA PILI roho yako UKIWA MTAKATIFU, KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE, KWA NJIA YA NENO LAKE ULILOLIMINI

>>UNADUMU KATIKA UTAKATIFU KWA NEEMA YAKE, KWA KULITENDA NENO LA MUNGU, KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE AKAAYE NDANI YAKO, KUPITIA IMANI YAKO INAYOZIDI KUONGEZEKA KWA NENO LA MUNGU; AMBALO LINAZIDI KUJAA ROHONI MWAKO (MOYONI MWAKO)

 

UBARIKIWE NA BWANA YESU

TUKUTANE SEHEMU IJAYO

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post