MAOMBI 7 MUHIMU YA MAISHA YAKO YA KIROHO WEWE UAMINIYE
1) OMBI LA KWANZA
“15 Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, 16siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, 17Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; 18macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 19na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; 20aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” (Waefeso 1:15-23)
1A: MUNGU AKUPE ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE
1B: MACHO YA MOYO WAKO YATIWE NURU (MACHO YA KIROHO YA MOYONI)
1C: ULIJUE TUMAINI LA WITO WAKE JINSI LILIVYO
1D: UUJUE UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE KATIKA WATAKATIFU JINSI ULIVYO
1E: UUJUE PIA UBORA WA UKUU WA UWEZA WAKE NDANI YETU TUAMINIO JINSI ULIVYO
1F: UBORA HUO WA UKUU WA UWEZA WAKE NDANI YETU TUAMINIO NI KWA KADIRI YA UTENDAJI WA NGUVU ZA UWEZA WAKE ALIOTENDA KATIKA KRISTO ALIPOMFUFUA KATIKA WAFU AKAMWEKA MKONO WAKE WA KUUME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (THE EXCELLENCE OF THE GREATNESS OF THE RESURRECTION POWER OF JESUS CHRIST; THE POWER THAT IS INDESCRIBABLY SO MUCH GREATER THAN ALL OTHER POWERS PUT TOGETHER)
1G: HAPO ALIPOKETI KRISTO YESU BWANA WETU NI JUU SANA KULIKO UFALME WOTE, NA MAMLAKA, NA NGUVU, NA USULTANI/MILKI (DOMINION), NA KILA JINA/CHEO LITAJWALO, WALA SI ULIMWENGUNI HUMU TU, BALI NI KATIKA ULE UJAO PIA [EXALTED POSITION OF THE SAINTS IN CHRIST JESUS-NAFASI YA JUU SANA TULIPOINULIWA WATAKATIFU WAKE NDANI YA KRISTO YESU NA PAMOJA NAYE (WAEFESO 2:6)]
MUHIMU: HAPA NI JUU SANA KULIKO SHETANI, MASHETANI YOTE, MAJINI, MAPEPO YOTE, UFALME WOTE WA GIZA, MAJESHI YOTE YA SHETANI, NA NGUVU ZAKE ZOTE
1H: KATIKA KUKETISHWA KWETU HUKO (WAEFESO 2:6) PAMOJA NAYE MKONO WA KUUME WA BABA, ALIVITIA VITU VYOTE (VYENYE UHAI NA VISIVYO NA UHAI, YAANI, UUMBAJI WOTE) CHINI YA MIGUU YAKE; NA KISHA AKAMFANYA YEYE KUWA KICHWA JUU YA VITU VYOTE, KWA AJILI YA KANISA NDILO MWILI WAKE, UKAMILIFU WAKE ANAYEKAMILIKA KWA VYOTE KATIKA VYOTE.
MUHIMU: MUNGU, NDANI YAKE KRISTO YESU, AMETUTIISHIA KANISA UFALME WA GIZA WOTE, PAMOJA NA VITU VYOTE VILIVYOUMBWA, CHINI YA MIGUU YETU, YAANI, SISI TULIOMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WETU, SISI AMBAO NDILO KANISA LAKE!
>> JIOMBEE WEWE MWENYEWE, OMBEA MKEO/MUMEO, WAOMBEE WANAO, MBEA KANISA, WAOMBEE WASHIRIKA ULIOWEKWA KUWALISHA NA KUWACHUNGA, MWOMBEE MCHUNGAJI WAKO, OMBA MAOMBI HAYA SIKUZOTE!!! OMBA KILA SIKU, KILA WIKI, KILA MWEZI, NA KILA MWAKA!!! UKIFIKISHA MIAKKADHAA UTAONA MATOKEO YA AJABU, MAANA HAYA NI MAPENZI YA MUNGU MWENYEWE, NA ROHO MTAKATIFU MWENYEWE NDIYE ALIYEYATOA!
2) OMBI LA PILI
“14Kwa hiyo nampigia Baba magoti, 15ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, 16awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 17Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; 18ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 19na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.” (Waefeso 3:14-19)
2A: MUNGU AKUJALIE, KWA KADIRI YA UTAJIRI WA UTUKUFU WAKE, KUFANYWA IMARA KWA NGUVU (STRENGTHENED WITH POWER), KWA KAZI YA ROHO WAKE MTAKATIFU, AKAAYE NDANI YAKO.
2B: MUNGU AKUJALIE KWAMBA KRISTO AKAE MOYONI MWAKO KWA IMANI, UKIWA NA SHINA NA MSINGI KATIKA UPENDO (ROOTED AND GROUNDED IN LOVE).
2C: KRISTO AKIKAA HIVYO MOYONI MWAKO KAMA KWENYE 2B, NDIPOSA MUNGU AKUPE KUFAHAMU PAMOJA NA WATAKATIFU WOTE JINSI ULIVYO UPANA, NA UREFU, NA KIMO, NA KINA (KNOWING THE SPIRITUAL DIMENSIONS OF LOVE); NA KUUJUA UPENDO WAKE KRISTO, UPITAO UFAHAMU KWA JINSI ULIVYO MWINGI.
2D: KATIKA KUUJUA HIVYO UPENDO WAKE KRISTO(2C), NDIPO MUNGU AKUPE KUTIMILIKA NA KUKAMILIKA KATIKA UKAMILIFU NA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU
>> KUUJUA PENDO NA KUUISHI NDIKO KUMJUA MUNGU MAANA MUNGU NI UPENDO (1 YOHANA 4:8); KULIJUA NA KULIISHI PENDO LAKE NI UKAMILIFU MAANA UPENDO NDIO KIFUNGO CHA UKAMILIFU (WAKOLOSAI 3:14)
>> OMBA, JIOMBEE, MUOMBEE, NA UWAOMBEE FAMILIA YAKO, KANISA LA MAHALI PAMOJA, NA MWILI WOTE WA KRISTO MPAKA KANISA LIRUDI KUISHI HIVI NA KUWA NA USHUHUDA HUU DUNIANI WA UPENDO;
“34Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. 35Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi” (Yohana 13:34-35)
-KAMA KUNA UAMSHO UNATAKIWA NI UAMSHO WA PENDO LAKE KRISTO NDANI YA MIOYO ILIYOJAA CHUKI NA UBINAFSI MAKANISANI NA KWENYE JAMII PIA, KIASI KWAMBA DUNIA HAIONI KUTIMIZWA KWA YOHANA 13:34-35 WAZIWAZI PASIPO MASHAKA YOYOTE MAISHANI MWETU!
3) OMBI LA TATU
“9Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; 10mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; 11hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.” (Wafilipi 1:9)
3A: MUNGU AKUPE NEEMA KWAMBA PENDO LAKE LILILOMO NDANI YAKO LIZIDI KUWA JINGI SANA KATIKA HEKIMA NA UFAHAMU WOTE
3B: KWAMBA KWA KUONGEZEKA HUKO KWA PENDO LAKO, UPATE KUYAKUBALI YALIYO MEMA (KUMBUKA MUNGU ALIUMBA KILA KITU KIKIWA NI CHEMA SANA- MWANZO 1:31)
3C: KWA KUYAKUBALI YALE YALIYO MEMA TU, UKAPATE KUWA NA MOYO SAFI, BILA KOSA, MPAKA SIKU YA KRISTO (LOVE IS PURE, AND PURITY IS BLAMELESSNESS BEFORE GOD)
3D: HAYO YOTE YATENDEKE NDANI YAKO HUKU UMEJAZWA MATUNDA YA HAKI, KWA NJIA YA YESU KRISTO, KWA UTUKUFU NA SIFA YA MUNGU
>> PENDO LA MUNGU NI TAKATIFU, NA HIVYO KUJAA PENDO LAKE NI KUJAA UTAKATIFU WAKE ILI KUWA HIVI;
“3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 4 KAMA VILE ALIVYOTUCHAGUA KATIKA YEYE KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU, ILI TUWE WATAKATIFU, WATU WASIO NA HATIA MBELE ZAKE KATIKA PENDO.” (Waefeso 1:3-4)
>> NI MPANGO WA MUNGU TANGU KABLA YA UUMBAJI KWAMBA TUJE KUWA WATAKATIFU, WATU WASIO NA HATIA WALA LAWAMA MBELE ZAKE KATIKA PENDO! HIVYO LAZIMA TUOMBEANE! JIOMBEE, MUOMBEE MKEO/MUMEO, MWANAO/WANAO, WAOMBEE WATAKATIFU WOTE, LIOMBEE KANISA, MUOMBEE MCHUNGAJI WAKO, WAZEE WA KANISA, MASHEMASI, NA VIONGOZI WOTE!!!
4) OMBI LA NNE
“11 Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu. 12Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; 13apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.” (1 Wathesalonike 3:11-13)
4A: MUNGU AWAONGEZE NA KUWAZIDISHA KATIKA UPENDO NINYI KWA NINYI (KANISA, FAMILIA, WATUMISHI, VIONGOZI, N.K.), NA KWA WATU WOTE PIA
4B: MUNGU BABA YETU NA BWANA WETU YESU KRISTO, APATE KUIFANYA MIOYO YENU IWE BILA LAWAMA KATIKA UTAKATIFU MBELE ZAKE WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA WETU YESU PAMOJA NA WATAKATIFU WAKE!
>> JIBU LA OMBI HILI MAANA YAKE WEWE KANISA UTAKUWA TAYARI KUMLAKI BWANA YESU MAWINGUNI AKIRUDI WAKATI WOWOTE, MAANA U MTAKATIFU USIYE NA LAWAMA YOYOTE MBELE ZAKE KATIKA PENDO LAKE! KWA MAANA PENDO LAKE NI UTUKUFU WA UTAKATIFU WAKE WOTE!!
“7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” (1 Yohana 4:7-8)
5) OMBI LA TANO
“20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, 21 awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.”
5A: MUNGU WA AMANI ALIYEMFUFUA YESU KUTOKA KWA WAFU AWAFANYE NINYI (KANISA, NDOA, FAMILIA, VIONGOZI, WATUMISHI, WATAKATIFU, WASHIRIKA, N.K.) KUWA WAKAMILIFU KATIKA KILA TENDO JEMA
5B: KATIKA UKAMILIFU HUO KWENYE KILA TENDO JEMA, MUNGU AKUPE NEEMA YA KUYAFANYA MAPENZI YAKE NA KUMPENDEZA YEYE
5C: KATIKA KUYAFANYA KWAKO HUKO MAPENZI YAKE, MUNGU AFANYE NDANI YAKO KILA LIPENDEZALO MBELE ZAKE, KWA YESU KRISTO BWANA WETU!
>> KAZI NJEMA ALIYOIANZA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO (Wafilipi 1:6) INAENDELEA HAPA KUELEKEA UKAMILIFU NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA WETU
6) OMBI LA SITA
“9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; 10mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; 11mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;” (Wakolosai 1:9-11)
FANYA MAOMBI NA DUA KWA AJILI YAKO NA WOTE UWAPENDAO;
6A: KWAMBA WOTE MJAZWE MAARIFA YA MAPENZI YAKE (KNOWLEDGE OF HIS WILL) KATIKA HEKIMA YOTE NA UFAHAMU WA ROHONI,
6B: ILI UENENDE KAMA ULIVYO WAJIBU WAKO KWA BWANA YESU,
6C: KATIKA KUENENDA HUKO KAMA ULIVYO WAJIBU WAKO KWA BWANA, UMPENDEZE KABISA (PLEASING HIM FULLY),
6D: KATIKA KUMPENDEZA HUKO BWANA KABISA, UMZALIE MATUNDA KATIKA KILA KAZI NJEMA (BEARING FRUIT UNTO EVERY GOOD WORK),
6E: NA KATIKA KUZAA HUKO MATUNDA, UZIDI/UONGEZEKE KATIKA MAARIFA YA MUNGU,
6F: UKIWA UNAWEZESHWA KWA UWEZO WOTE KATIKA MAMBO YOTE,
6G: UPATE KUWA NA SABURI YA KILA NAMNA, NA UVUMILIVU, PAMOJA NA FURAHA.
Kumbuka Biblia inasema, kwa habari ya saburi,
“2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” (Yakobo 1:2-4)
>> KULE KWENYE WAKOLOSAI ANASEMA ‘SABURI YA KILA NAMNA’! NA HAPA YAKOBO ANASEMA SABURI INA KAZI KAMILIFU (PERFECT WORK), YA KUKUFANYA WEWE UWE MKAMILIFU NA MTIMILIFU,USIYEPUNGUKIWA NA NENO LOLOTE!
JAMES 1:4/YAKOBO 1:4
New International Version
Let perseverance finish its work so that you may be mature and complete, not
lacking anything.
New Living Translation
So let it grow, for when your endurance is fully developed, you will be perfect
and complete, needing nothing.
English Standard Version
And let steadfastness have its full effect, that you may be perfect and
complete, lacking in nothing.
>> SABURI YA KILA NAMNA, UVUMILIVU, PAMOJA NA FURAHA NI UKAMILIFU WA MTAKATIFU
>> NA HII NDIYO KAZI ANAYOIFANYA ROHO MTAKATIFU KATIKA UTU WA NDANI KWA MTU ALIYEOKOKA; NA SIYO TU ALIYEOKOKA, BALI YULE ALIYEOKOKA MWENYE KUUTAFUTA UFALME WA MUNGU KWANZA NA HAKI YAKE; YULE MWENYE KUONGOZWA NA ROHO; YULE MWENYE NJAA NA KIU YA HAKI; YULE MWENYE KUYAFIKIRI NA KUYATAFUTA YALE YALIYO JUU, KRISTO ALIKO, AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU; YULE MWENYE KUIFUATA ROHO NA SIYO MWILI; YULE MWENYE KUISHI NA KUENENDA KWA ROHO; YULE MWENYE KUYATANGULIZA, NA KUYATAFUTA SIKUZOTE MAMBO YA ROHO HUKU AKIMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI; YULE ANAYEENENDA KATIKA KWELI YOTE; YULE AMBAYE NI MGENI, MPITAJI, NA MSAFIRI HAPA DUNIANI; YULE AMBAYE NI BIKIRA SAFI WA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU; YULE ANAYEUCHUCHUMILIA UKAMILIFU NDANI YA KRISTO YESU BWANA; YULE AMBAYE HATAKI KITU KINGINE COCHOTE ISIPOKUWA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU YOTE KAMA YALIVYOFUNULIWA KATIKA NENO LAKE; YULE AMBAYE KUFANIKIWA KWAKE NI KUFANIKIWA KWA NENO LA MUNGU NA SIYO VINGINEVYO, NA HIVYO NI KUFANIKIWA KWA MAPENZI YA MUNGU KATIKA NENO LAKE!!!
>>MTU WA NAMNA HII NDIYE AMBAYE ATAOMBA SAWASAWA NA MAOMBI YALIYOFUNULIWA HUMU, SIKUZOTE, NA KAMWE HATAACHA MPAKA AONE KANISA LINAENENDA SAWASAWA NA MAJIBU YA MAOMBI HAYA!
7) OMBI LA SABA
“8Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; 9tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; 10ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.” (Wafilipi 3:8-10)
MST 8: MUNGU AKUPE KUONA KWAMBA HAKUNA KITU CHOCHOTE AU JAMBO LOLOTE DUNIANI HAPA LENYE UMUHIMU SAWA NA ‘KUMJUA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI’ YAANI, KUMJUA MKRISTO KUWE MOYONI MWAKO NI MUHIMU KULIKO CHOCHOTE DUNIANI KINACHOWEZA KUITWA MUHIMU![THIS IS YOUR PERSONAL AND INTIMATE KNOWLEDGE OF THE LORD JESUS]
MST 8: MUNGU AKUPE UTAYARI MOYONI NA AKILINI MWAKO WA KUPATA HASARA YA MAMBO YOTE!!!!! TENA UPATE HASARA HIYO YA MAMBO YOTE UKIYAHESABU KUWA KAMA KINYESI, KWA LENGO LA KUMPATA KRISTO!!!!!
MST 9: MUNGU AKUPE KUITAFUTA HAKI YAKE ILE ITOKAYO KWENYE IMANI, NA SIYO HAKI ILE ITOKAYO KWA SHERIA/TORATI, AU MATENDO YA SHERIA, AMA MATENDO YA HAKI!! BALI NI HAKI ILE ITOKANAYO NA KUMWAMINI MUNGU TU KABLA HUJATENDA LOLOTE! MAANA UKIMWAMINI MUNGU YEYE HUKUPA NEEMA YA KUYATENDA MAPENZI YAKE YALIYOMO KWENYE NENO LAKE ULILOLIAMINI! MAANA IMEANDIKWA;
“13Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” (Wafilipi 2:13)
>> LENGO NI KUKUONDOLEA NA KUKUEPUSHA NA MAJIVUNO KWAMBA WEWE NDIYE UMETENDA/UMEFANYA HAYO, NA HIVYO KUBEBA UTUKUFU WA MUNGU KWA KUJIHESABIA HAKI. MAANA HAUHESABIWI HAKI KWA KUWA UMETOA SANA, UMEFUNGA SANA, UMEHUDHURIA IBADA ZOTE MWAKA MZIMA, UMETOA MICHANGO YOTE, N.K. BALI UNAHESABIWA HAKI KWA SABABU ULIMWAMINI ALIPOSEMA NENO LAKE!!! HAKI MBELE ZA MUNGU, AU UTAKATIFU WAKE, HAUPATIKANI KWA NJIA YA MATENDO YAKO! BALI UNAFANYWA KUWA MTAKATIFU KWA KUZALIWA MARA YA PILI KWA NEEMA YAKE, PALE UNAPOHUISHWA ROHO YAKO NA KUFANYWA UPYA KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE, KUPITIA IMANI YAKO KWA KRISTO YESU BWANA WETU.
MST 10: “..ILI NIMJUE YEYE, NA UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE, NA USHIRIKA WA MATESO YAKE, NIKIFANANISHWA NA KUFA KWAKE; 11 ILI NIPATE KWA NJIA YO YOTE KUIFIKIA KIYAMA YA WAFU.”
10A: MUNGU AKUPE KUMJUA YESU KRISTO KIBINAFSI (UHUSIANO BINAFSI WA WEWE NA YEYE)
10B: AKUPE NA KUUJUA PIA UWEZA AMA NGUVU ZILIZOMFUFUA KUTOKA KWA WAFU UKIWA KWENYE MWILI WA DAMU NA NYAMA; KWAMBA UNATENDA KAZI KWA JINSI GANI KINYUME NA UPINZANI WA MWILI, SHETANI, NA DUNIA! YAANI, UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE NI NGUVU ZILE ZILE ZILIZOMFUFUA YESU NA KUKUPA KUISHI MAISHA MAPYA ZIKIWA ZINAKUWEZESHA KUYAISHI MAISHA YALE YALE YA YESU KWA KUWA UMEFUFULIWA PAMOJA NAYE (WAEFESO 2:6), NA SASA UKO HAI NDANI YAKE, KWA AJILI YAKE, PAMOJA NAYE, KWA NJIA YAKE, NA KWA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA JINA LAKE.
10C: AKUPE PIA KUUJUA USHIRIKA WA MATESO YAKE KATIKA MAISHA YAKO NDANI YA MWILI HUU UNAOHARIBIKA JINSI ULIVYO; KWAMBA JINSI GANI UNAWEZA KUSTAHIMILI MATESO YOTE KWA AJILI YA KRISTO KATIKA MWILI
10D: BWANA AKUPE PIA KUJUA KULE KUFANANISHWA NA KUFA KWAKE UKIWA UNAISHI KATIKA MWILI, ILI IONEKANE DHAHIRI NI KWA JINSI GANI NA KWA KIWANGO GANI UMEIFIA DHAMBI NA TAMAA ZENYE KUDANGANYA ZA MWILI NA ZA DUNIA HII
10E: ILI NIPATE KWA NJIA YO YOTE KUIFIKIA KIYAMA YA WAFU. KIYAMA YA WAFU NI UFUFUO WA WAFU (RESURRECTION OF THE DEAD)
-MAISHA YA UKRISTO/WOKOVU NI MAISHA YALE YALE ALIYOISHI BWANA WETU YESU KWA MIAKA MITATU NA NUSU KABLA YA KUSULUBIWA, KUFA, NA KUFUFUKA!
-BWANA WETU YESU ALIISHI MAISHA YAKE KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU ALIYEKUWEMO NDANI YAKE
-ROHO HUYO HUYO AMEKUSUDIWA KATIKA MPANGO WA MUNGU AJE KUKAA NDANI YAKO PALE UNAPOMWAMINI YESU, NA KUOKOKA, NA KUBATIZWA MAJI MENGI, NA KISHA KUMPOKEA ROHO HUYO (MATENDO YA MITUME 2:38-39)
- MAISHA KATIKA NGUVU ZA MUNGU NI MAISHA YA KULIISHI NA KULITENDA NENO LA MUNGU! NA HAYA NDIYO MAISHA ALIYOISHI YESU, NA PIA NDIYO MAISHA ANAYOISHI MKRISTO/MTOTO WA MUNGU/ ALIYEOKOKA/ ALIYEZALIWA MARA YA PILI/ ALIYEMWAMINI YESU/ ALIYEMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE!!! NI MAISHA YA KUONGOZWA NA KUTAWALIWA NA ROHO MTAKATIFU UNAYEMPOKEA BAADA YA KUOKOKA (MATENDO YA MITUME 2:1-4 &19:1-7)
>>“1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.” (Matendo 2:1-4)
>>“37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.” (Matendo 2:38-39)
>> “1Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. 7Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.” (Matendo 19:1-7)
>> NI MPANGO WA MUNGU WEWE ULIYEAMINI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU; UNAWEZA PIA KUOMBA MUNGU ATIMIZE AHADI YAKE YA ROHO MTAKATIFU KWAKO; UNAWEZA PIA KUOMBEWA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU WAKATI WOWOTE; UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU SASA, NA KUANZA KUSEMA KWA LUGHA NYINGINE KAMA ROHO MTAKATIFU ATAKAVYOKUJALIA KUTAMKA!
SALA YA KUOKOKA
“EE BWANA YESU! NAAMINI KWAMBA WEWE NI MWANA WA MUNGU, NA KWAMBA ULIKUFA MSALABANI KWA AJILI YA DHAMBI ZANGU; NAAMINI DAMU YAKO ULIYOIMWAGA MSALBANI DIYO PEKEE INAYOOSHA DHAMBI ZA MWANADAMU; NAOMBA UNIOSHE DHAMBI ZANGU ZOTE SASA EE YESU; INGIA MOYONI MWANGU SASA; NINAKUPA MOYO WANGU NA MAISHA YANGU, MIMI NA NYUMBA YANGU; NIOSHE, NITAKASE, NISAFISHE, NISAMEHE YESU; NIMEAMUA KUKUPOKEA KUANZIA SASA UWE BWANA NA MWOKOZI WANGU BINAFSI PAMOJA NA NYUMBA YANGU; NIPOKEE UNIFUNDISHE, ILI NIYAFANYE MAPENZI YAKO SIKUZOTE ZA MAISHA YANGU, MIMI NA NYUMBA YANGU’ ASANTE KWA KUNIOKOA MIMI NA NYUMBA YANGU; NI KWA JINA LAKO YESU NIMEOMBA”
SALA YA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU
“BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU, NINAKUSHUKURU KWA WOKOVU WAKO MKUU. ASANTE KWA KUNISAFISHA MOYO WANGU NA DHAMBI ZOTE KWA DAMU YA YESU KRISTO. MIMI NI MWANAO SASA MAANA NIMEOKOKA; ULISEMA HAUTANIACHA YATIMA BALI UTANIPA ROHO WAKO AKAE NDANI YANGU HATA MILELE; ULISEMA PIA KWAMBA NIKITUBU DHAMBI ZANGU, NIKABATIZWA, NITAPATA ONDOLEO LA DHAMBI, NA KISHA NITAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU. ULISEMA PIA HAO WANAOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU HAO NDIO WANA WA MUNGU; KWA KUWA MIMI NI MWANAO, NINAPOKEA SASSA ROHO MTAKATIFU KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI; NINAPOKEA ROHO MTAKATIFU NA NINAANZA KUSEMA KWA LUGHA NYINGINE SASA KAMA ROHO ANAVYONIWEZESHA KATIKA JINA LA YESU, KARIBU ROHO MTAKATIFU............!!!”
>>UKIFIKA HAPO MWISHONI FUNGUA KINYWA CHAKO ANZA KUSEMA KWA LUGHA NYINGINE KAMA ROHO ATAKAVYOKUJALIA KUTAMKA! UTATAMKA MANENO MAGENI USIYOYAJUA, LAKINI USIZUIE KUNENA KWA LUGHA! ENDELEA KUOMBA KWA LUGHA USIACHE! JIUNGE NA WALIOOKOKA UENDELEE KUJIFUNZA KUHUSU WOKOVU NA ROHO MTAKATIFU!!! UBARIKIWE NA BWANA YESU!