TATIZO SIYO HILO, AU HAO, AU YEYE, TATIZO NI WEWE!! (YOU ARE THE PROBLEM, NOT HIM, OR THEM, OR THAT!!)
"1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako." (Mathayo 7:1-5)
1) Tatizo siyo bia au pombe nyingine yoyote inayonuka au kunukia, BALI TATIZO NI ile roho ya ulevi iliyomo rohoni mwako wewe mnywa pombe iliyokufunga na inayokutumikisha kwenye ulevi, na huwezi toka humo mpaka utubu na kumwamini Yesu akuweke huru!! (Yohana 8:36)
“1OLE WA TAJI YA KIBURI YA WALEVI wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la HAO WALIOSHINDWA NA DIVAI! 2Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama dhoruba ya maji mengi yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono. 3TAJI YA KIBURI YA WALEVI WA EFRAIMU ITAKANYAGWA KWA MIGUU; 4na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa hari, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake. 5Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji ya fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake. 6Naye atakuwa roho ya hukumu kwake yeye aketiye ili ahukumu; naye atakuwa nguvu kwao wageuzao nyuma vita langoni. 7LAKINI HAWA NAO WAMEKOSA KWA DIVAI, WAMEPOTEA KWA KILEO; KUHANI NA NABII WAMEKOSA KWA KILEO, WAMEMEZWA KWA DIVAI, WAMEPOTEA KWA KILEO; HUKOSA KATIKA MAONO, HUJIKWAA KATIKA HUKUMU. 8Maana meza zote zimejaa matapiko na uchafu, hapana mahali palipo safi. 9Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini.” (Isaya 28:1-9)
“ 9 Au hamjui ya kuwa WADHALIMU HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, WALA WALEVI, wala watukananji, wala wanyang’anyi.” (1 Wakorintho 6:9-10)
>> HAWA WOTE NA WENGINE KAMA HAWA SEHEMU YAO NI ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI, KAMA HAWATATUBU NA KUIAMINI INJILI KWA KUMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAO!!
2) Tatizo siyo mwanamke mwenye sura nzuri, au maumbile mazuri au sauti nzuri au aliyevaa nusu uchi, BALI TATIZO NI ile roho ya uzinzi iliyomo ndani yako inayokutumikisha kwenye uzinzi maana huwezi kujinasua mpaka umruhusu Yesu akunasue pale utakapomwamini na kutubu, akakusamehe na kukuondolea hiyo roho ya shetani!!
“4Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui BWANA.” (Hosea 5:4)
“2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. 3Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? 4Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. 5Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito.” (2 Samueli 11:2-5)
>> TATIZO HALIKUWA UMBILE ZURI SANA LA BATH-SEBA LINALOVUTIA NA KUPENDEZA MACHO, BALI TATIZO LILIKUWA NI ILE DHAMBI YA UZINZI ILIYOKUWEMO NDANI YAKE DAUDI. DAUDI ALIKUWA ANA DHAMBI AMBAYO HAJAITUBIA! DHAMBI, KAMA HUJAITUBIA, HUWA HAIONDOKI! HUWEZI KUSAMEHEWA DHAMBI AMBAYO HUJAITUBIA! KUJITAKASA NI MAISHA YA KUZITUBIA NA KUZIACHA DHAMBI ZILE ZIKUZINGAZO UPESI KAMA MAANDIKO YASEMAVYO (WAEBRANIA 12:1), KWA KULIAMINI NA KULITENDA ANDIKO HUSIKA LINALOKUWEKA HURU MBALI NA DHAMBI HIZO MAHUSUSI! HEBU MSIKIE DAUDI ANAPOTUBIA UZINZI WAKE (SOMA ZABURI YOTE YA 51), NA KWENYE ZABURI YA 119 DAUDI ANAPELEKA OMBI HILI, KWA ROHO MTAKATIFU, ILI ASIANGUKE TENA KWENYE DHAMBI YA UZINZI. ANASEMA;
“ Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.” ((Zaburi 119:37)
>> Kwa jibu la ombi hili maana yake Daudi hawezi tena kumwangalia mwanamke mrembo wa aina yoyote kwa kumtamani, maana macho yake yamegeuzwa na hivyo hawezi kutazama tena visivyofaa!! Ayubu naye katika kumcha kwake Mungu anafanya agano na macho yake la kutomzama binti au mwanamke yeyote kwa kumtamani!!!
“ Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?” (Ayubu 31:1) Anachomaanisha hapa Ayubu na hata Daudi ni kuwa; “ Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, NA MOYO WANGU KUYAANDAMA MACHO YANGU” (Ayubu 31:7) Moyo wa Ayubu haukuandamana na macho wake! Yaani, hakumtazama kamwe mwanamke awaye yote KWA TAMAA YA MOYO WAKE!! Ambayo ni uzinzi! Ndiyo maana Yesu alisema, “ lakini mimi nawaambia, kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:28)
>> TATIZO SIYO MWANAMKE YEYOTE ANAYEVUTIA AU MREMBO AU ALIYEVAA MAVAZI YA KIKAHABA, BALI TATIZO NI ILE roho ya uzinzi iliyomo moyoni mwako AMBAYO HAITAKUACHA MPAKA UTUBU, UMWAMINI YESU, NA KUOKOKA KUTOKA KWENYE UTUMWA WA NA KIFUNGO CHA DHAMBI ZAKO!!!
3) Tatizo siyo chochote kinachovutia macho, au kinachopendeza macho, au kinachoonekana ni cha kifahari saaaana, BALI TATIZO ni ile roho ya tamaa ya macho uliyonayo inachokutumikisha kwenye kila namna ya tamaa kiasi kwamba kila kitu kizuri au kinachovutia na kupendeza macho cha dunia hii unakitaka wewe, na hata ukikipata hiki unakitaka kingine, na kingine, na kile, na kile!!! Tamaa kamwe haishibi ndugu mpendwa maana kuzimu kamwe haishibi mpaka itakapokumeza ukapotea milele iwapo hautaamua kutubu na kuokoka kwa kumpokea Yesu atakayekuweka huru kweli kweli!!(Yohana 8:36)
“15Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.” (1 Yohana 2:15-17)
“10Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza. Hayo pia ni ubatili. 11Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?” (Mhubiri 5:10-11)
>>MPENDA FEDHA KAMWE HAUWEZI KUTOSHEKA NA KIASI CHOCHOTE CHA FEDHA UTAKACHOKIPATA! MAANA UNA MOYO WA KUPENDA FEDHA! UNAABUDU SANAMU INAYOITWA FEDHA! mungu WAKO NI mungu fedha! KADIRI UNAVYOPATA FEDHA UNALIMBIKIZA NA KUJIWEKEA HAZINA DUNIANI KINYUME NA MANENO YENYE UZIMA YA BWANA WETU YESU KRISTO ALIYESEMA, “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; KWA KUWA HAZINA YAKO ILIPO, NDIPO UTAKAPOKUWAPO NA MOYO WAKO.” (Mathayo 6:19-21)
>> HAKUNA MWANADAMU AWAYE YOTE AMBAYE ATAJIWEKEA HAZINA YAKE HAPA ULIMWENGUNI HALAFU MOYO WAKE UKAWA KWA MUNGU! HAZINA YAKO ILIPO NDIPO UTAKAPOKUWA NA MOYO WAKO! JAZA MAPESA BENKI HAPA DUNIANI NA MOYO WAKO UTAKUWA KWENYE HAZINA YAKO HUKO KWENYE MABENKI! HUWEZI KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI! BALI UNAABUDU mungu PESA NA MALI!! HUWEZI KUWA NA MUNGU MOYONI MWAKO!!! HAZINA YAKO ILIPO NDIPO UTAKAPOKUWAPO NA MOYO WAKO!!
>> KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI NI KUTAWANYA KWA KUSAIDIA MASKINI NA WAHITAJI; NI KUWA TAJIRI WA MATENDO MEMA!NI KUUZA VYOTE ULIVYONAVYO NA KUWAPA MASKINI, KISHA UNAKUWA NA HAZINA MBINGUNI, NA NDIPO UNAKUJA KUMFUATA YESU KWENYE NJIA NYEMBAMBA! MTENDA DHAMBI AKISIKIA HAYA MARA MOJA ANAANZA KUFIKIRIA KUWA ATAKUWA MASKINI NA KUPOTEZA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI WAKE, KWA KUWA MOYONI MWAKE HAMWAMINI MUNGU WALA KUMCHA ALIYESEMA;
“ Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo kilichojaa, kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” (Luka 6:38)
>> Mwabudu sanamu uliyejiwekea hazina duniani huamini hili; huamini kama imeandikwa;
“Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.” ( Marko 4:24)
>>Mwabudu sanamu anapohitajika kutenda mema kwa kutumia akiba aliyojiwekea nafsi yake, yeye husema sina fedha!!! Amesahau kwamba imeandikwa, “ Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.” (Marko 4:25) Ndugu mwabudu sanamu mbinguni hutaingia usipotubu, na hata akiba uliyojiwekea hapa duniani, halafu unakiri huna kitu, nayo utanyang’anywa!!! Kwa maana unaposema huna huo ni uongo na ibada ya sanamu kwa kuwa moyo wa utoaji huna! upendo wa Mungu huna! huruma za Yesu huna! bali umejaa upendo wa fedha, mali, na utajiri! Hakika ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko wewe kuingia kwenye ufalme wa Mungu, katika hali ya kuabudu miungu uliyonayo! (mungu pesa, mungu mali, na mungu utajiri!! )Unaweza kutubu na kumpa Yesu moyo wako akuoshe dhambi zako na sanamu zako zote ili umwabudu Yeye katika Roho na Kweli ukiwa na uzima wa milele rohoni mwako.
Luka 18:18-25
“18 Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele? 19Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu. 20Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako. 21Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu. 22Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate. 23Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi. 24Yesu alipoona vile alisema, Kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu! 25KWA MAANA NI VYEPESI NGAMIA KUPITA KATIKA TUNDU LA SINDANO KULIKO TAJIRI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU.” ( Luka 18:18-25)
>>IBADA YA SANAMU ILIMFANYA AUKOSE UFALME WA MUNGU! MAANA KWA KUTOIFAHAMU KWELI, ALIPOAMBIWA (1) AUZE VYOTE ALIVYONAVYO, (2) AWAPE MASKINI, (3) KISHA AWE NA HAZINA MBINGUNI, ALIFIKIRI ATAFILISIKA!HAKUONA KWAMBA ALIKUWA ANATAJIRIKA KATIKA MUNGU, KWA MAANA ANGEPOKEA UTAJIRI WA VITU VISIVYOHARIBIKA NA VYENYE UMILELE, HUKU AKIWA NA UZIMA WA MILELE, NA PIA MUNGU ANGEKUWA AMEJAA MOYONI MWAKE, NA KWAMBA MWISHO WAKE ANGEZIDISHIWA VITU VILE VILE ALIVYOVITOA MAANA SASA ANGEKUWA AMEJIFUNZA KUVITUMIA VYOTE KWA AJILI YA YESU, KANISA LAKE, NA UFALME WAKE, NA HIVYO KUTAJIRIKA KWA MATENDO MEMA, NA ANGEKUWA SASA ANALIMBIKIZA MALI, FEDHA, NA UTAJIRI MBINGUNI, HUKU AKIMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI! KUKUBALI KUUZA MALI ULIZONAZO NA KUWAPA MASKINI NI KUWEKWA HURU KUTOKA KWENYE IBADA YA SANAMU NA KUHAMISHA MOYO KUTOKA KWENYE UHARIBIFU WA TAMAA ZENYE KUDANGANYA, NA KUUHAMISHIA MOYO HUO KWA MUNGU BABA YETU WA MBINGUNI!! UNAPOTEZA ILI KUPATA! UNATAWANYA ILI KUKUSANYA!
4) Tatizo siyo kwamba unachopata ni kidogo, hilo siyo tatizo lako la msingi , BALI TATIZO ni hiyo roho uliyonayo ya kutoridhika na kile ukipatacho kwa kuwa una tamaa ya mali, fedha, na utajiri moyoni mwako; hivyo huwezi kuridhika wala kutosheka na chochote upatacho maishani mwako! Laiti ungetubu na kumwamini Yesu angekusamehe na kukutoa kwenye kifungo cha tamaa na kukupa amani, inayotokana na kuridhika (contentment) ambako angekufundisha Yeye mwenyewe . Ndipo ungetosheka na kuridhika kwanza na Yeye Mwenyewe Jehovah Al-Shaddai maana hakika Anatosha!!Kisha ungeridhika na kile ukipatacho ambacho Yeye angekupa akili njema ya kukidhibiti, na angekuongeza kidogo kidogo hatua kwa hatua mpaka mwisho wako ungeongezeka sana kiroho, kiakili, kihisia, kimwili, kifedha, kimali na vitu, na mwisho kijamii.
“3 Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa, 4amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya; 5na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. 6 WALAKINI UTAUWA PAMOJA NA KURIDHIKA NI FAIDA KUBWA. 7 KWA MAANA HATUKUJA NA KITU DUNIANI, TENA HATUWEZI KUTOKA NA KITU; 8 ILA TUKIWA NA CHAKULA NA NGUO TUTARIDHIKA NA VITU HIVYO. 9LAKINI HAO WATAKAO KUWA NA MALI HUANGUKA KATIKA MAJARIBU NA TANZI, NA TAMAA NYINGI ZISIZO NA MAANA, ZENYE KUDHURU, ZIWATOSAZO WANADAMU KATIKA UPOTEVU NA UHARIBIFU. 10MAANA SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; AMBAYO WENGINE HALI WAKIITAMANI HIYO WAMEFARAKANA NA IMANI, NA KUJICHOMA KWA MAUMIVU MENGI. (1 Timotheo 6:3-10)
Vita Vizuri vya Imani
>> “11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole. 12 Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.” (1 Timotheo 6:11)
>>“11 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;
Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.” (Mithali 13:10)
>>NAMNA MOJA YA KUJIJUA KWAMBA UNA TAMAA YA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI NI KULE KUTAKA NA KUPENDA KWAKO UTAJIRI WA HARAKA HARAKA. FEDHA YA HARAKA HARAKA, NA MALI ZA HARAKA HARAKA! HIYO HAITOKI KWA MUNGU BALI KWA IBILISI, SHETANI, BABA WA UONGO! HARAKA HARAKA YAKO HII NI HARAKA YA KUJIWAHISHA KUZIMU NA JEHANAMU IWAPO HAUTATUBU NA KUOKOKA!
>> MAPENZI YA MUNGU, UTARATIBU WA MUNGU, NJIA YA MUNGU, NENO LA MUNGU, NA MPANGO WA MUNGU NI KUCHUMA KIDOGO KIDOGO, NA NDIPO YEYE MWENYEWE ATAKUZIDISHIA NA KUKUONGEZA HUKU AKIFANYA HILI HAPA;
“Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.” (Zaburi 32:8)
>> LAZIMA UJIFUNZE VITA VYA IMANI ILI KUPOKEA USHINDI WA YESU WA MSALABA DHIDI YA NGUVU ZA GIZA ZINAZOPINGA WATU WATEULE, WATAKATIFU WA MUNGU KUINULIWA NA KUTAJIRIKA KIFEDHA NA KIMALI: ATAKUFUNDISHA JINSI YA KUVIPIGA VITA VIZURI VYA IMANI, ATAKUFUNDISHA JINSI YA KUKWEPA KUINGIA KATIKA MTEGO WA KUWEKA HAZINA DUNIANI NA KUABUDU SANAMU PESA, ATAKUFUNDISHA JINSI YA KUWEKA HAZINA MBINGUNI, ATAKUJAZA UPENDO WAKE NA HURUMA ZAKE, ATAKUFUNDISHA JINSI YA KUTAJIRIKA KWA MATENDO MEMA BADALA YA KUTAJIRIKA KWA VITU VITATU VINAVYOHARIBIKA; FEDHA, MALI, NA UTAJIRI. ATAKUFUNDISHA JINSI YA KUUZA VYOTE ULIVYONAVYO, NA KUWEKA HAZINA MBINGUNI KWA KUWAPA MASKINI, NA KISHA KUMFUATA YESU UKIWA NA MOYO SAFI. ATAKUFUNDISHA UTAKATIFU KATIKA PESA, MALI, NA UTAJIRIJINSI ULIVYO; ATAKUFUNDISHA KUTAFUTA, NA ATAKUJAZA, UTAJIRI WA KWELI USIOHARIBIKA NA JINSI YA KUJITAJIRISHA KATIKA MUNGU!
>>“1 Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” (Mwanzo 15:1)
>> BWANA MUNGU MWENYEZI MWENYEWE NDIYE NGAO YAKO, NA THAWABU YAKO KUBWA SANA! HAKIKA YESU ANATOSHA KAMA UKIMWAMINI NA KUMTUMAINI!!
5) Tatizo siyo kwamba Kanisa limerudi nyuma na kupoa kama unavyosema, BALI TATIZO ni hiyo roho uliyonayo ambayo Yesu aliiita unafiki (Mathayo 7:1-5) inayotazama sikuzote vibanzi vya wengine na kujifanya kutaka kuviondoa huku wewe mwenyewe una boriti machoni mwako ambayo huiongelei, na wala hutaki kuishughulikia hata kidogo!
BORITI YAKO:
>> HUOMBEI WENGINE NA WALA HUWABEBEI MIZIGO YAO KAMA BIBLIA INAVYOAGIZA NA WALA HUNA ROHO YA UPOLE INAYOTAKIWA KUWAREJEZA WALE WALIOGHAFILIKA KATIKA MAKOSA MBALIMBALI
Wagalatia 6:1-2
“1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho MREJEZENI UPYA MTU kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.” (Wagalatia 6:1-2)
NA TENA;
>> “19 Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na MTU MWINGINE AKAMREJEZA; 20jueni ya kuwa yeye AMREJEZAYE MWENYE DHAMBI hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.” (Yakobo 5:19-20)
-HUNA MOYO WA KUREJEZA WATAKATIFU WALIOPOTEA MBALI NA KWELI; UNACHOFANYA NI KUWASEMA VIBAYA NA KUENEZA HABARI ZAO MBAYA ZA KUANGUKA NA KUJITIA UNASIKITIKA KWAMBA KWELI HIZI NI NYAKATI MBAYA MAANA WATU WANAPOTOKA NA KUANGUKA MNO! HUOMBI, HUOMBEI, HUWATAFUTI WALIORUDI NYUMA AU WALIOACHA IMANI, NA WALA HUWAFUATI KUONGEA NAO, HUNA MACHOZI KWA AJILI YAO, NA KAZI YAKO NI KUHARIBU SIFA ZAO! HUWAJIBIKI KWA YESU NA WALA HUNA UTII WA KWELI NDANI YAKO! HAPO AMESEMA “MTU WA KWENU AKIPOTEA..!” WANGAPI WAMEPOTEA KWENU? HALAFU AKASEMA NA “...MTU MWINGINE AKAMREJEZA!” WEWE UMEREJEZA WANGAPI? UNA MACHO MAKAVU YASIYOLILIA WENGINE KAMA VILE ULIVYO MKAVU KIROHO USIYE NA MAFUTA YA ROHO NA NDIYO MAANA KINYWA CHAKO KINAMTUMIKIA SHETANI KWENYE UTUMISHI WA KUCHAFUA WENGINE WALIOJIKWAA KINYUME NA KRISTO!!!
>> “16Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.” (1 Yohana 5:16)
-UNAONA WANGAPI? NA UMEONA WANGAPI WANATENDA DHAMBI ISIYO YA MAUTI (AMBAYO NI KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU) HALAFU HUKUOMBA??? BADALA YAKE UKAPATA, SIYO JAMBO LA KUOMBEA, (PRAYER POINT) BALI WEWE ULIPATA JAMBO LA KUONGELEA/KUSENGENYA (GOSSIPING POINT). BIBLIA HAIKUSEMA HAPA KWAMBA UKIMUONA NDUGUYO KATIKA KRISTO AU MTUMISHI AU MTOTO WA MUNGU YEYOTE ANATENDA DHAMBI KWAMBA UTAKWENDA KUONGEA/UTAANZA KUSAMBAZA KWA KINYWA CHAKO, AU KWA VIDEO, AU KWA NAMNA YOYOTE!!! BIBLIA IMESEMA UTAFUMBA KINYWA KWA WANADAMU NA BADALA YAKE UTAKIFUMBUA KINYWA KWA MUNGU BABA YETU WA MBINGUNI!! KWA HIYO TATIZO NI WAOVU WENGI KAMA WEWE WASIOOMBA BALI WANAOONGEA TU MABAYA YA WENGINE WAMEJAA MAKANISANI!!!NA WALA HAKUNA MWOMBEZI MPAKA GHADHABU YA MUNGU INASHUKA!!!
“ 12 Kwa maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi, na maovu yetu tumeyajua; 13 katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena jeuri na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni. 14 Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia. 15Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki.16AKAONA YA KUWA HAPANA MTU, AKASTAAJABU KWA KUWA HAPANA MWOMBEZI; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu;na haki yake ndiyo iliyomsaidia.” ( Isaya 59:12-16)
>> “1Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. 2Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe. 3Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.” (Warumi 15:1-3)
-KWA KUWA WEWE NI MTENDA DHAMBI MBINAFSI SANA UNAYEDAI KUMJUA MUNGU NA KULITAJA JINA LA BWANA YESU, NDIYO MAANA HUNA MOYO WA (au roho ya ) KUWACHUKULIA WENGINE UDHAIFU WAO! SIKUZOTE UNAOMBA KIBINAFSI TU UNAPOJIOMBEA MWENYEWE TU NA MAMBO YAKO! UKIFUNGA NA KUOMBA UJUE LIMEKUFIKA SHINGONI!! SIKUZOTE UNAJIPENDEZA WEWE MWENYEWE NA KAULI MBIU YAKO NI KWAMBA SIKU ZA MWISHO HIZI KILA MTU AUBEBE MZIGO WAKE!! UKIOMBEA KANISA UNAOMBEA KUSANYIKO LAKO TU! HUZINGATII KABISA KWAMBA ROHO MTAKATIFU AMEAGIZA KWAMBA KILA MTU ALIYEOKOKA AMPENDEZE JIRANI YAKE APATE WEMA AKAJENGWE KAMA KRISTO ALIVYOFANYA, KWA KUWA YEYE KRISTO HAKUJIPENDEZA MWENYEWE ( WARUMI 15:1-3)!!! HUNA MOYO WA UPENDO AMBAO UNGEKUSUKUMA KUWAOMBEA WENGINE NA KUBEBA MADHAIFU YAO! WALIO WA ROHONI NI WAOMBEZI NA WABEBA MIZIGO YA WENGINE PAMOJA NA MADHAIFU YAO MBELE ZA MUNGU! HURUMA NA UPENDO WA KRISTO HUWASUKUMA KUFANYA HIVYO! WEWE HUFANYI HIVYO KWA KUWA NI MUOVU MMOJA HIVI NA MBINAFSI AMBAYE HUJATUBU KIKWELI KWELI NA WALA HUNA UPENDO NA HURUMA ZAKE KRISTO! UJAPOSEMA UMEOKOKA LAKINI LAZIMA UTUBU NA KUOKOKA KWELI KWELI ILI USTAHILI KUINGIA KWENYE UFALME WAKE ATAKAPOKUJA MAWINGUNI KULICHUKUA KANISA!
>> BORITI YAKO NI KUBWA MNO LAKINI CHUKUA HAYO MACHACHE ILI UTUBU NA KUSIMAMA KATIKA KWELI NA UANZE KUMCHA MUNGU KIKWELIKWELI NA KUACHA KUJIDANGANYA HALAFU UKAJIKUTA JEHANAMU SIKU MOJA AMBAKO UTALIA NA KUSAGA MENO MILELE!
5) Tatizo siyo milima (matatizo) iliyomo maishani mwako unayokutana nayo kwenye mwendo wako wa imani ya Yesu, BALI TATIZO ni hiyo roho uliyonayo ya kutoamini Neno la Mungu wala humwamini Kristo Mwokozi ambaye ndiye suluhisho la matatizo yako yote na pia ndiye jibu la maswali yako yote kupitia Roho wake Mtakatifu, Neno lake takatifu, na Nguvu zake!! Biblia imesema waziwazi;
“21Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. 22Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. 23Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.” (Marko 11:21-23)
-TATIZO SIYO MILIMA!! MILIMA INAWAKILISHA MATATIZO MAKUBWA MNO KAMA MLIMA MKUBWA AMBAO HUWEZI HATA KUWA NA WAZO LA KUUHAMISHA WEWE MWANADAMU! MLIMA HAUWEZI KUHAMISHWA NA WALA HAUHAMISHIKI! BWANA YESU HAPA ANAONGELEA DHAHIRI MAMBO MAGUMU YASIYOWEZEKANA KIBINADAMU!!! SASA MAMBO HAYA YASIYOWEZEKANA KIBINADAMU YANAWEZEKANA KWA IMANI YA YESU! YANAWEZEKANA KWAKO WEWE UNAYEMWAMINI YESU KWELI KWELI!! MAANA IMEANDIKWA,
“23Yesu akamwambia, Ukiweza! YOTE YAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE.” (Marko 9:23)
-SASA WEWE BADALA YA KUMWAMINI MUNGU UNALALAMIKA, UNALAUMU, UNAKOSOA, UNANUNG’UNIKA, UNAHUKUMU, UNAKATA TAMAA, UNAVUNJIKA MOYO, UNAHAHA NA KUSUMBUKA HUKO NA KULE, UNATAMKA MANENO YA HOVYO KUTOKANA NA YALE UNAYOYAONA NA KUYASIKIA, HUNA TUMAINI, HUONYESHI KUTOA TUMAINI LOLOTE, HUNA NENO LA FARAJA WALA MATUMAINI MOYONI MWAKO, YAANI, WEWE HAUMWAMINI YESU!!! HAUMWAMINI MUNGU!! HAUMWAMINI NENO!!! NA NDIYO MAANA KINYWA CHAKO SIKUZOTE KINAONGEA NA KUNENA KULE KUTOAMINI KULIKOJAA MOYONI MWAKO. MAANA, LAITI UNGEKUWA UNAAMINI UNGEKUWA UMEIAMBIA MILIMA YOTE ING,OKE NA KWENDA KUTUPWA BAHARINI! UNGEKUWA UMEONDOA MATATIZO NA CHANGAMOTO ZOTE KWENYE HUDUMA YAKO, KANISANI UNAKOSHIRIKI, KWENYE NDOA YAKO, KWA WANAO, KWA MUMEO, KWA MKEO, KAZINI KWAKO, SHULENI AU CHUONI KWAKO, KAZINI KWAKO, KWENYE BIASHARA YAKO, KILIMO CHAKO, NA KAZI YOTE YA MIKONO YAKO; KWENYE TAIFA LAKO UNGEKUWA UMEHAMISHA MILIMA YOTE YA KIUCHUMI, KISIASA, KIFEDHA, KIUTAWALA, KIUNGOZI, KISHERIA, KIKATIBA, KIELIMU, KIAFYA, NA KWENYE SEKTA ZOTE NA NYANJA ZOTE ZA MAISHA!!! KINACHOTAKIWA NI WEWE KUMWAMINI MUNGU NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU! MAANA UNAPOAMINI, UNAKUWA NA MAJIBU YOTE KUPITIA NENO LAKE NA AHADI ZAKE ZILIZOMO KWENYE BIBLIA TAKATIFU. LAKINI PIA ULE USHIRIKA ULIO NAO NA YESU KWA ROHO WAKE UNGEPELEKEA WEWE KUJULISHWA SIRI NYINGI KUHUSU WATU, KANISA, TAIFA, NA KILA KITU KAMA APENDAVYO ROHO! HIVYO UNGETEMBEA HAPA DUNIANI UKIWA HURU, USIYE NA HOFU WALA MASHAKA YOYOTE , MWENYE FURAHA, AMANI, NA MATUMAINI SIKU ZOTE, UNAYEJUA UMETOKA WAPI, UKO WAPI , NA UNAKWENDA WAPI!!! UNAYEYAJUA MAMBO YAJAYO AMBAYO ROHO MTAKATIFU AMEKUJULISHA KAMA ALIVYOSEMA YESU INGEKUWA PALE AJAPO HUYO ROHO MOYONI MWAKO UNAPOMPOKEA; “13Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, NA MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI YAKE. 14Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.” (Yohana 16:13-14)
-KWA MUJIBU WA BIBLIA KUTOAMINI NI DHAMBI
“16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ILI KILA MTU AMWAMINIYE ASIPOTEE, BALI AWE NA UZIMA WA MILELE. 17Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18AMWAMINIYE YEYE HAHUKUMIWI; ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA; KWA SABABU HAKULIAMINI JINA LA MWANA PEKEE WA MUNGU.” (Yohana 3:16-18)
-UNAPOKOSA KUAMINI UNAKUWA UNATENDA DHAMBI! UNAONGEA DHAMBI! NA UNAWAZA DHAMBI!!! UNAISHI HUKU HUKUMU YA MUNGU IKIWA JUU YAKO!!
“23Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.” (Warumi 14:23)
>> MATATIZO UNAYOYAHUBIRI, UNAYOYASEMA, UNAYOYATABIRI, UNAYOYATARAJIA, NA UNAYOYAZUNGUMZA KILA SIKU KUHUSU KANISA, MKEO. MUMEO, WANAO, NDUGUZO, TAIFA, N.K. NI MILIMA ILIYOMO MAISHANI MWAKO WEWE USIYEMWAMINI YESU HUKU UNASEMA UMEOKOKA AU UNAMTUMIKIA MUNGU! MOYONI MWAKO HUMWAMINI MUNGU!! NA HII NDIYO MAANA UNAONA MILIMA, UNAONGEA MILIMA, UNATABIRI MILIMA, N.K. MTENDA DHAMBI HAWEZI KUSABABISHA DHAMBI ZIISHE MOYONI MWA MTENDA DHAMBI! NDIYO MAANA DHAMBI BADO INATAWALA KWENYE HIYO UNAYOIITA HUDUMA, MAANA WEWE MWENYEWE KILA SIKU UNASEMA HALI NI MBAYA! AU UNAMAANISHA HALI NI MBAYA WAPI??!! KWA WENGINE ??!! KWAKO VIPI??!! UNGEKUWA MTAKATIFU UNGEKUWA UMEWABEBA HAO WENGINE NA KUWAOMBEA NA KUMWAMINI MUNGU KWA AJILI YAO, NA HIVYO KUHAMISHA MILIMA YOTE MAISHANI MWAO NA KWENYE HUDUMA ZAO!!! MILIMA INAHAMA UNAPOKUWA UMEOMBA, UMEAMINI, NA UNAPOKUWA UMEMKABIDHI BWANA MUNGU MWENYEZI AISHUGHULIKIE! (1 PETRO 5:6-7) NAWE UNAKUWA NA UHAKIKA ANAISHUGHULIKIA, NA HUKU UNAJUA KWAMBA YEYE SIKU ZOTE HUWA HAANZI NA KUISHIA KATI KATI!! (WAFILIPI 1:6) NA WEWE ULIOMBA SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE (1 Yohana 5:14-15) NA HIVYO ULIPOKEA HAJA ZOTE ULIZOMWOMBA MAANA ALIKUSIKIA! UNAWEZAJE KUIONA MILIMA BAADA YA HAPO? HALI MBAYA UNAYOISEMA NI HALI MBAYA ULIYONAYO KIROHO!!! MAMBO MAGUMU UNAYOYAONA NA KUYASEMA NI UGUMU WA MOYO WAKO KUMWAMINI MUNGU! MAANA MUNGU AMESEMA YEYE NI MUNGU WA WOTE WENYE MWILI, NA HAKUNA NENO LOLOTE GUMU ASILOLIWEZA (YEREMIA 32;17). NA KWENYE ISAYA ANAULIZA, “BWANA WA MAJESHI ASEMA HIVI, INGAWA HILI NI NENO LILILO GUMU MBELE YA MACHO YA MABAKI YA WATU HAWA KATIKA SIKU HIZO, JE! LIWE NENO GUMU MBELE YA MACHO YANGU? ASEMA BWANA WA MAJESHI.” (ZECHARIA 8:6) MAMBO UNAYOYAONA YANAHARIBIKA NI MAISHA YAKO YANAYOHARIBIWA NA SHETANI ULIYEMPA NAFASI MOYONI MWAKO (WAEFESO 4:27 NA YOHANA 10:10) KWA KUTOKUAMINI KWAKO. MAANA IMEANDIKWA PIA KWAMBA “AONAVYO MTU NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO.....” (MITHALI 23:7) TUBU UMWAMINI YESU!!
6) Tatizo siyo huyo (mkeo, mumeo, bosi wako, mfanyakazi mwenzako, mwajiri wako, mzazi wako, mwanao, kiongozi wako, rafiki wako, mfanyabiashara mwenzako, n.k.) uliyegombana naye, usiyeongea naye, uliyefarakana naye, uliyetengana naye, uliyekorofishana naye, n.k. BALI TATIZO ni roho ya ubinafsi na chuki uliyonayo wewe moyoni mwako, na kukosa kwako upendo wa Mungu moyoni mwako! Na kwa kuwa imani hutenda kazi kwa upendo (Wagalatia 5:6) wewe huwezi kumwamini Mungu, maana hauliamini pendo lake Baba! Yesu ni upendo wa Mungu kwa ulimwengu wote!Biblia imeeleza wazi sifa na tabia za upendo;
“4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; (1 Kor 13:4)
>> WEWE KWA KUWA HAUMWAMINI YESU, HAUNA ROHO YA UVUMILIVU (MOYO WA UVUMILIVU) KUTOKA KWA YESU; UMESHINDWA NA HAUWEZI KUVUMILIA KAMA YESU ALIVYOVUMILIA. UVUMILIVU WA YESU UKIWA NDANI YAKO UNAYO SILAHA KUBWA SANA YA KULINDA NA KUDUMISHA MAHUSIANO YAKO! KUKOSA KWAKO UVUMILIVU WA KIMUNGU NDIKO KUMEPELEKEA KUVUNJIKA KWA NDOA YAKO NA/AU MAHUSIANO YAKO MENGINE!
“5haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;” (1 Kor 13:5)
>> UPENDO WA MUNGU HAUKOSI KUWA NA ADABU (HAUNA JEURI); JEURI YAKO IMEVUNJA NA KUHARIBU MAHUSIANO YAKO MENGI SANA!
>> UPENDO WA MUNGU HAUTAFUTI MAMBO YAKE; HAUNA UBINAFSI! HAUTAFUTI FAIDA YAKE BINAFSI; HAUJIANGALII WENYEWE TU; HAUJITANGULIZI WENYEWE; HAUJITAFUTII MANUFAA YAKE TU; HAUTAFUTI HESHIMA YAKE TU; HAUTAFUTI UTUKUFU WAKE TU; HAUTAFUTI SHUKRANI ZAKE TU; HAUTAFUTI SIFA ZAKE TU; HAUJIKWEZI; HAUJIINUI; HAUWADHARAU WENGINE; HAUJIANGALII WENYEWE TU;HAUJINUFAISHI WENYEWE TU; HAUJIFIKIRII WENYEWE TU; HAUJIWAZII WENYEWE TU; HAUJIPANGII MIPANGO YAKE BINAFSI TU; HAUJIWEKEI AKIBA YAKE TU; HAUJISUMBUKII WENYEWE TU;HAUJIFURAHISHI NA KUJIPENDEZA WENYEWE TU;........UPENDO HAUTAFUTI MAMBO YAKE! LAKINI WEWE, KWA SEHEMU KUBWA MAOVU HAYA NDIYO MAISHA YAKO, HUKU UKIWAKWAZA, UKIWAUDHI, UKIWAUMIZA, UKIWAONEA, UKIWATESA, UKIWASUMBUA, UKIWAELEMEA, UKIWAPUNJA, UKIWADHULUMU, UKIWATUMIKISHA MNO, NA UKIWAKWAZA WENGINE NA KUWATENDEA MABAYA; UKISHINDWA KABISA KUWATENDEA HAKI!!! KWA KUWA HUWAPENDI! UNAWACHUKIA! UMEJAA UBINAFSI! MAHUSIANO MENGI UMESABABISHA YAVUNJIKE HALAFU UNATANGAZA UBAYA WAO HAO ULIOWATENDEA UBAYA! UNATAKA WAO NDIO WAONEKANE WABAYA! UNATANGAZA UBAYA WAO ILI UFICHE UOVU WAKO;HAUWAJALI WATU, HAUJALI HISIA ZAO, HAUJALI MAISHA YAO, HAUFIKIRII KABISA FAIDA NA MANUFAA YAO! UPENDO HAUTAFUTI MAMBO YAKE!! KWA HIYO TATIZO SIYO WAO, BALI DHAMBI ZAKO! CHUKI YAKO NA UBINAFSI WAKO! TUBU NA UMWAMINI YESU, UPOKEE PENDO LAKE, UANZE KUISHI NA KUENENDA KATIKA PENDO LAKE!!OKOKA HALAFU UJAZWE ROHO WAKE MTAKATIFU ILI UISHI KWA SIFA NA UTUKUFU WAKE!
>>UPENDO HAUONI UCHUNGU: MOYONI MWAKO UMEJAA UCHUNGU NA CHUKI! UCHUNGU MOYONI NI CHUKI! CHUKI NI HASIRA NA GHADHABU ILIYOHIFADHIWA MOYONI! UCHUNGU NI KISASI KILICHOHIFADHIWA MOYONI; UCHUNGU NI UADUI MOYONI! UCHUNGU NI UGOMVI MOYONI! USIPOKUWA NA UPENDO WA MUNGU LAZIMA MOYO WAKO UNA CHUKI! CHUKI NI MAUTI MOYONI MWAKO! UMEKUFA KIROHO! HAUONGEI NA WATU! HAUSALIMIANI NAO! UNA UADUI NAO! HUO NI UOVU! HIYO NI MAUTI! YESU ALISEMA WAPENDE ADUI ZAKO! TATIZO SIYO WAO, BALI WEWE USIYEITII KWELI!!!
●“13 N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. 14Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. 15Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. 16Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.” (Yakobo 3:13-16)
● “14Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 15Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.” (1 Yohana 3:14-15)
● “. 30Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. 31Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;” (Waefeso 4:30)
● “9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako,
Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.” (Mhubiri 7:9)
>> UCHUNGU NI HASIRA NA GHADHABU VILIVYOHIFADHIWA MOYONI MWAKO KAMA UCHUNGU!! HUNA AMANI YA YESU! UOVU NA UBAYA UMO MOYONI MWAKO! UNA HASIRA ZA HARAKA HARAKA NA ZA MRIPUKO MAANA UMELIMBIKIZA MAHASIRA NA UCHUNGU MOYONI! WEWE NDIYE CHANZO CHA KUVUNJIKA MAHUSIANO!!! WEWE NA KAMWE SIYO YEYE!! AU WAO!!
● “18Mtu wa hasira huchochea ugomvi;
Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.”(Mithali 15:18)
● “22Mtu wa hasira huchochea ugomvi;
Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.” (Mithali 29:22)
>> CHANZO CHA MAGOMVI NI HIYO MIHASIRA YAKO!!
● “19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; 20kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.” (Yakobo 1:19-20)
>> HASIRA YAKO MWANADAMU KAMWE HAIWEZI KUITENDA HAKI YA MUNGU KAMA ANDIKO LISEMAVYO HAPO JUU; NA HAPA NAPO ANASEMA, “17KILA LISILO LA HAKI NI DHAMBI, na dhambi iko isiyo ya mauti.” (1 Yohana 5:17) HIVYO UNAWEZA KUONA HAPA KUWA SIKU ZOTE HASIRA ITAKUPELEKEA KUTENDA DHAMBI! NA HASIRA IKIKUTAWALA UNAKUWA KWENYE KIFUNGO CHA UOVU!!!
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu,
Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9Maana watenda mabaya wataharibiwa,
Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.” (Zaburi 37:8-9)
“5haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;” (1 Kor 13:5)
>> UPENDO HAUHESABU MABAYA! WEWE MWENYE CHUKI UMEWEKA KUMBUKUMBU YA MABAYA ULIYOTENDEWA NA BADO KILA UNAPOTENDWA MABAYA UNAWEKA KUMBUKUMBUKU! HII NI KWA SABABU HAUNA MOYO WA KUSAMEHE ALIONAO YESU! UKIWA NDANI YA YESU UNAKUWA NA NEEMA YA KUSAMEHE KAMA YESU ANAVYOSAMEHE! SABINI MARA SABA KWA SIKU! YEYE ALITUOSHA DHAMBI ZETU NA KUTUSAMEHE, NA WALA HAZIKUMBUKI DHAMBI HIZO! “17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.” ( Waebrania 10:17)
>> KUMBUKUMBU YA MABAYA MOYONI MWAKO NI VISASI NA CHUKI VILIVYOHIFADHIWA MOYONI! HUU NI UOVU NA UBAYA MOYONI AMBAO LAZIMA UTAMDHURU MWAANADAMU MWINGINE! UPENDO HAUWEKI MOYONI ORODHA NDEFU YA MABAYA ULIYOTENDEWA NYAKATI MBALIMBALI ZILIZOPITA! CHUKI NDIYO HAISAHAU MABAYA ULIYOTENDEWA BALI INAHESABU; ALINETENDA HIVI, AKANITENDA VILE, AMERUDIA HILI, N.K. HAKUNA UHUSIANO WAKO UTAKAODUMU KAMA UNAWEKA MOYONI KILA UBAYA UNAOTENDEWA! LAKINI PIA HAUWEZI KUWA NA AFYA NJEMA YA KIROHO, KIHISIA NA KIMWILI KAMA UMEJAA KUMBUKUMBU YA MABAYA MOYONI!KAMA UKO HIVI TUBIA UOVU HUO NA UMWAMINI YESU ATAKUWEKA HURU MBALI NA KIFUNGO HICHO CHA UOVU!
“6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.” (1 Wakorintho 13:6-7)
>> KUNA WENGINE HUDHANI KUWA NA UPENDO WA MUNGU MAANA YAKE KUACHILIA UOVU, KURIDHIA UOVU, KUJIZUIA KUKEMEA UOVU, KUTETEA UOVU, KUFICHA UOVU, KUFUMBIA MACHO UOVU, NA MAMBO KAMA HAYO! HUO WOTE SIYO UPENDO NI CHUKI! MFANO MZAZI ASIYEMKEMEA, WALA KUMKARIPIA, WALA KUMWADHIBU MTOTO HUYO ANAMCHUKIA MTOTO WAKE NA WALA HAMPENDI! NA ANAMHARIBU MTOTO WAKE YEYE MWENYEWE! IMEANDIKWA;
“24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;
Bali yeye ampendaye humrudi mapema.” (Mithali 13:24)
>> UPENDO HAUFURAHII UDHALIMU BALI HUFURAHI PAMOJA NA KWELI!! UPENDO UNA HEKIMA, NGUVU, NA MAARIFA YOTE YA KUONDOA UOVU NA KUKOMESHA KABISA DHAMBI NDANI YA MOYO WA MWANADAMU. UPENDO WA MUNGU NI UTUKUFU WA UTAKATIFU WAKE. MUNGU NI UPENDO (1 Yohana 4:8) NA PIA NI MTAKATIFU (1 Petro 1:16). IMEANDIKWA PIA KWAMBA MUNGU NI ROHO (Yohana 4:24) HIVYO TUNAONA HAPA KWAMBA MUNGU NI ROHO WA UPENDO ALIYE MTAKATIFU SANA! LOVE IS HOLY! (UPENDO NI MTAKATIFU!) PALIPO NA UPENDO WA KWELI WA MUNGU DHAMBI HAIWEZI KUSHAMIRI!! DHAMBI INASHAMIRI PALE PENYE CHUKI, UBAYA, UBINAFSI, NA UOVU WA KILA NAMNA!
Mstari wa saba wa sura hii ya kumi na tatu ya kitabu cha Wakorintho wa kwanza inahitimisha kipengele hiki kinachoonyesha kwamba tatizo siyo mtu mwingine, bali kwamba tatizo ni wewe uliyeshindwa KUMPENDA KAMA YESU ALIVYOKUPENDA!! Hapa anasema UPENDO WA MUNGU UKIWA NDANI YAKO; [ 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.]
1) UNAVUMILIA YOTE
2) UNAAMINI YOTE
3) UNATUMAINI YOTE
4) UNASTAHIMILI YOTE
>> HAKUNA NENO GUMU KWA UPENDO, HAKUNA MTU MGUMU KWA UPENDO, HAKUNA MWANADAMU MGUMU KWA UPENDO, HAKUNA HALI NGUMU KWA UPENDO, HAKUNA MAZINGIRA MAGUMU KWA UPENDO! UPENDO UNASHINDA YOTE!!! BIBLIA IKISEMA ‘YOTE’ INAMAANISHA UNAWEZA KUVUMILIA MAKWAZO YOTE, MAUDHI YOTE, MACHUKIZO YOTE, UONEVU WOTE, KUTENDWA MABAYA KOTE, N.K. IKIWA NI MAPENZI YA MUNGU, KAMA UPENDO HUO UKIWEMO NDANI YAKO!! SASA HUWEZI KUWA NA SABABU YA KWELI YA KUVUNJA UHUSIANO, AU KUMPA MKEO TALAKA, AU KUMKIMBIA MUMEO, KAMA UPENDO WA MUNGU UKIWA NDANI YAKO!! YESU ALIVUMILIA YOTE KWA AJILI YAKO ILI UOKOKE; YESU ALIAMINI YOTE KWA AJILI YAKO ILI UOKOKE! YESU ALITUMAINI YOTE KWA AJILI YAKO ILI WEWE UOKOKE! YESU ALISTAHIMILI YOTE KWA AJILI YAKO ILI WEWE UOKOKE! KAMA UNAMPENDA UTAVUMILIA YOTE KUTOKA KWAKE, UTAAMINI YOTE KUTOKA KWAKE, UTATUMAINI YOTE KUTOKA KWAKE, NA UTASTAHIMILI YOTE KUTOKA KWAKE HUYO MWANADAMU ALIYEUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU! NAONGEA NA WEWE ULIYEPOKEA PENDO LAKE ULILOLIAMINI PALE ULIPOOKOKA! KAMA HAUFANYI HIVYO INAONYESHA WAZIWAZI KWAMBA HAUKUOKOKA KIKWELI KWELI! NA SASA NI SAA YAKO YA KUOKOKA KIKWELI KWELI UPOKEE UPENDO WA MUNGU MOYONI MWAKO!!!
7) Tatizo siyo wanao unaosema wameharibika na wana tabia mbaya, BALI TATIZO ni wewe mwenyewe ambaye una matatizo mawili.
1) “6Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” (Mithali 22:6)
>> Ulishindwa kumlea huyo mwanao au kuwalea hao wanao katika njia iwapasayo ambayo Biblia inasema HAWATAIACHA HATA WATAKAPOKUWA WATU WAZIMA! Ulishindwa kuwalea katika adabu njema na maonyo ya Bwana kwa kuwa wewe mwenyewe haumwamini Yesu ambaye ndiye NJIA, KWELI, NA UZIMA, na mtu hawezi kwenda kwa Mungu isipokuwa ni kwa kupitia Yeye (Yohana 14:6)
>> Ni kweli uliikosa njia pale mwanzo ya kumlea mwanao au hao wanao kwa kuwa wewe mwenyewe haukuwa unatembea kwenye njia hiyo! Lakini hata sasa bado unaweza kumgeukia Yesu, ukamwamini, naye akaiponya nyumba yako isishuke jehanamu yote pamoja na wewe mwenyewe!
2) Tatizo lako la sasa ni KUTOMWAMINI YESU ambaye anaweza kuiokoa nyumba yako!!!
Biblia inasema,
“30kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 31WAKAMWAMBIA, MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO. 32Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. 33Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. 34Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.” (Matendo ya Mitume 16:30-34)
MST 31
1) MWAMINI BWANA YESU,
2) NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO.
>> UKIMWAMINI LEO BWANA YESU ATAKUOKOA
>> LAKINI HATAKUOKOA WEWE PEKE YAKO,
>> BALI ATAKUOKOA WEWE PAMOJA NA NYUMBA YAKO
NEEMA YA BWANA YESU IMEFUNULIWA KWAKO MUME, KWAKO BABA, KWAKO MAMA, KWAKO MKE, PAMOJA NA NYUMBA YAKO! KAMA ILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA SIKU ZA LUTU, MUNGU ATAKUOKOA WEWE NA NYUMBA YAKO, YAANI MKEO/MUMEO, WANAO, NDUGUZO, NA JAMAA ZAKO WOTE! MUNGU HUWA HABADILIKI! ALIFANYA HIVI ZAMANI ZA AKINA LUTU NA NUHU NA LEO KATIKA AGANO JIPYA AMETOA NEEMA MAALUMU YA WOKOVU, UPONYAJI, NA BARAKA, KWAKO NA NYUMBA YAKO! Rahabu yule kahaba aliokoka na upanga wa Yoshua kwa maana alimwamini Mungu wa Israeli kwa kuwaficha wale wapelelezi wawili ili wasikamatwe walipokuwa wakisakwa (Yoshua 2:3-6);Hii ni kwa sababu alijua Mungu wa Israeli anakwenda kuutia mkononi mwa Joshua ule mji! Rahabu aliamini katika nguvu za Mungu wa Israeli akaokoka yeye na nyumba yake!
“17Na mji huu utakuwa wakfu kwa BWANA, mji wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma.” (Yoshua 6:17)
“22Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia. 23Basi wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli.” (Yoshua 6:22-23)
>> IMANI YA RAHABU ILILETA WOKOVU KWA “.....wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia;” (MST23)
HUU BADO NI MPANGO WA MUNGU KUKUOKOA WEWE, NA WATU WOTE WA NYUMBANI MWAKO, KUTOKA KWENYE UTUMWA WA DHAMBI, NGUVU ZA GIZA, MAUTI YA KIROHO, NA ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI! KUOKOKA NI KUFANYWA KUWA KIUMBE KIPYA ROHONI MWAKO NA NAFSINI MWAKO, (2 WAKORINTHO 5:17) NA MWILI WAKO KUPONYWA MAGONJWA, MARADHI, NA UDHAIFU WOTE (Mathayo 8:17 & 1 Petro 2:24) NA KUTAKASWA KWA AJILI YA YESU KRISTO KUKAA NDANI YAKE! MWILI WAKO UNAKUWA HEKALU LA ROHO MTAKATIFU AMBALO NDILO KANISA!! ( 1 Wakorintho 3:16-17 & Waefeso 1: 22-23)
“1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.” (Mathayo 7:1-5)