KICHO CHA MKE KWA MUME
Kicho ni hali ya hofu kama tafsiri ya kamusi isemavyo, na katika mambo ya Mungu kicho ni hofu ya Mungu ama uchaji Mungu. Kuishi maisha ya uchaji Mungu ni kuishi maisha yenye kicho kitakatifu!!! Biblia ilitangulia kutabiri kwamba Mungu angekuja kufanya Agano Jipya na wanadamu muda mrefu kabla ya kuja Yesu; kwa kupitia Nabii Yeremia Roho Mtakatifu alifunua mpango wa Mungu kuja kuwaokoa wanadamu na kuwasaidia kuishi wakiyafanya mapenzi yake. Namna pekee ya kuishi ukiyafanya mapenzi ya Mungu duniani ni KUWA NA KICHO CHAKE MWENYEWE MOYONI MWAKO! Yeremia aliandika,
“39nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao; 40nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache.” (Yer 32:40)
- …….. NAMI NITATIA KICHO CHANGU MIOYONI MWAO, ILI WASINIACHE!!
Mungu alikuwa amekusudia kufanya Agano Jipya na nyumba ya Israeli maana Agano la mwanzo/la kale walikuwa wamelivunja (Yer 31:31-34).
Sasa hapa anasema atatia kicho chake ndani yao (mioyoni mwao), na Mungu ambaye ni Roho (Yoh 4:24) chochote atoacho hutoa kupitia Neno lake, ambalo ni Roho, na tena ni Uzima (Yoh 6:63). Neno la Mungu ni roho, na hicho akupacho hukupa wewe katika roho kupitia Imani yako kwa Neno lake! Ndiyo kusema hiki kicho ni roho pia, nayo huitwa ‘roho ya kumcha Bwana’! Kwa hiyo ndani ya Kristo Mungu ameweka ndani ya waaminio/waliookoka/watoto wake/waliozaliwa mara ya pili, roho yake mwenyewe ya kicho, na hivyo hawa waaminio kamwe hawawezi kumwacha!! Hii haimaanishi kwamba hawakosei bali huwa wakikosea/wakitenda dhambi/wakirudi nyuma, mioyo yao bado huwa inamtaka Yesu, na hivyo huwa wanatubu na kuziacha dhambi, na kumrudia Kristo Bwana na Mwokozi wetu Yesu!! Hii ni kwa sababu pia ndani ya mioyo yao Yesu ameweka roho ya toba! Ndipo Biblia inasema wana mioyo iliyotubu;
“15 Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu” (Isa 57:15)
-‘yeye aliye na roho iliyotubu’, ‘mioyo yao waliotubu’
-Anayeamini ametubu hata kabla hajakosea na kutubu maana kutubu kwake siyo mpaka umuone amepiga magoti analia akiomba rehema, bali ile roho ya toba moyoni mwake inamfanya awe aliyetubu tayari: yaani, anayetubu, atakayetubu, anayependa kutubu, anayetaka kutubu, aliyekubali kutubu, aliye mwepesi kutubu, mwenye moyo wa toba na mwenye maisha ya toba; na hivyo Mungu anamuona ametubu maana TOBA IMO NDANI YAKE TAYARI! Mungu ameweka toba moyoni mwake kupitia ile roho ya toba ambayo ndiyo inayomwezesha, inayomshawishi, inayomwongoza na inayomfanya atubu siku zake zote za mwili wa udongo!!! Tunachosema ni kwamba ukiokoka unakuwa kiumbe kipya ndani ya Yesu (2 Kor 5:17), na upya unaoongelewa ni huu hapa:
“Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda” (Eze 36:26-27)
KIUMBE KIPYA (2 KOR 5:17)= MOYO MPYA + ROHO MPYA (EZE 36:26-27) |
KUOKOKA MAANA YAKE YESU ANAKUPA MOYO MPYA WENYE ROHO MPYA ALIYE MTAKATIFU!!! Huyu ni Roho wa Neno/Kristo ambaye unapoamini Neno lake anaachilia neema maishani/moyoni mwako yenye kukuwezesha kulitenda hilo Neno, neema ambayo ndiyo roho ya hilo Neno yenye nguvu za Mungu zinazotenda kazi ndani yako kukuwezesha kuyafanya mapenzi yake!!!i.e kuitenda kweli.
KICHO CHA MKE KWA MUME?!
Biblia inasema, “30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.” (Mithali 31:30)
Hili neno ‘upendeleo’ kwa tafsiri za Biblia za kiingereza limetumika neno ‘charm’; yaani, uchangamfu wenye mvuto. Na hapa Biblia inasema,
-uchangamfu huo wenye mvuto wa mwanamke unadanganya wengi!!!
-uzuri wa mwanamke nao si mali kitu!!!
-BALI MWANAMKE AMCHAYE BWANA NDIYE ATAKAYESIFIWA KUANZIA MBINGUNI MPAKA KWA MWANADAMU
-Yaani, sifa za kweli na za maana huenda kwa mwanamke mcha Mungu! huyo ndiye mwenye sifa za kweli mbele za Mungu kwa sababu wazuri ni wengi lakini ni watenda dhambi tu! Wenye uchangamfu unaovutia ni wengi lakini nao ni waovu tu!sifa zote wanazozipata hazina maana mbele za Mungu kama HAWANA KICHO MIOYONI MWAO!!! Na huu ndio mtazamo wa Mungu kwamba wewe mwanamke sifa zozote unazozipata kwa watu kuhusiana na muonekano wako au kuongea kwako, au uchangamfu wako, au kuvutia kwako, kama hauna kicho moyoni mwako, ni bure kabisa kama maandiko yasemavyo;
“22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe,
Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.” (Mith 11:22)
“Good
News Translation
Beauty in a woman without good judgment is like a gold ring in a pig's snout.” (Prov
11:22)
-Akili inayoongelewa hapa ni ile akili itokayo kwa Mungu! Akili ya kuenenda kwa kicho katika njia zako zote! Ndoa, familia, kazi, biashara, mahusiano n.k. Sasa kama haumchi Mungu uzuri wote ni bure! Hatua ya kwanza ya mahusiano bora katika ndoa yanayompendeza Mungu ni uchaji Mungu! Uchaji Mungu wa mtoto wa Mungu aliyeokoka na kujazwa Roho Mtakatifu, na anayeenenda kwa huyo Roho maishani mwake!
>> “14Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.” (Rum 8:14)
>> “16Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” (Gal 5:16)
>>KICHO CHA MKE KWA MUME KINAANZIA KWENYE KUMCHA KWAKE MUNGU<<
1)“Kwa rehema na kweli uovu husafishwa;
Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu” (Mith 16:6)
-KWA KUMCHA BWANA WATU HUJIEPUSHA NA UOVU
2) “Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu” (Mith 1:7)
-KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA KUPOKEA MAARIFA YA MUNGU (anakupa roho ya maarifa/spirit of knowledge of God)
3) “Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;
Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu” (Mith 9:10)
-KUMCHA BWANA NI MWANZO WA KUPOKEA HEKIMA YA MUNGU (anakupa roho ya hekima/spirit of wisdom)
NINI MAANA YA KUMCHA BWANA?
“Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;
Kiburi na majivuno, na njia mbovu,
Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.” (Mith 8:13)
-NI KUCHUKIA UOVU
-NI KUCHUKIA KIBURI
-NI KUCHUKIA MAJIVUNO
-NI KUCHUKIA NJIA MBOVU (EVIL WAYS)
-NI KUCHUKIA KINYWA CHA UKAIDI
Mithali 31:30 inasema mke mwema , kwa hiyo, anasifika/anasifiwa kwa kuchukia uovu, kiburi, majivuno, na njia zote mbovu; na anachukia pia kinywa cha ukaidi! Huu ndio uchaji Mungu wake!
“New
International Version
Therefore, since we have these promises, dear friends, let us purify ourselves
from everything that contaminates body and spirit, perfecting holiness out of
reverence for God.” (2 Cor 7:1)
“Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.” (2 Kor 7:1)
UTAKATIFU UNAKAMILISHWA NA KUMCHA BWANA! KWA KUMCHA BWANA UNAISHI MAISHA YA KUJITAKASA ROHO, NAFSI NA MWILI!
Biblia inasema,
“ Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2wakiutazama mwenendo wenu safi, NA WA HOFU.” (1 Pet 3:1-2)
-ENYI WAKE WATIINI WAUME ZENU
-ILI KAMA WAPO WASIOAMINI (WASIOOKOKA)
-WAVUTWE (SHOULD BE WON OVER) KWA MWENENDO WA WAKE ZAO PASIPO LILE NENO
-WAKIUTAZAMA MWENENDO WENU SAFI (PURE CONDUCT) NA WA HOFU (HOLY REVERENCE)
MKE MCHA MUNGU ANATAKIWA AWEZE KUMVUTA NA KUUTEKA MOYO WA MUMEWE KWA MWENENDO WAKE SAFI NA WA HOFU PASIPO KULIHUBIRI LILE NENO! YAANI, UNATAKIWA KUHUBIRI KWA MWENENDO WAKO BILA MANENO!
Biblia inasema,
1) “Wives, submit yourselves unto your own husbands, as unto the Lord.
Enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana” (Waefeso 5:22)
>> WAKE WAMETAKIWA KIMAANDIKO KUWATII WAUME ZAO KANA KWAMBA NI KUMTII BWANA YESU MWENYEWE
>> YAANI, UTII WA MKE KWA BWANA YESU HAUPO KAMA HAMTII MUME WAKE! KAMA MKE ANAMTII MUMEWE LAZIMA ATAKUWA ANAMTII MUMEWE KWANZA!
>> KICHO CHA MKE KWA BWANA YESU HAKIPO KAMA HANA KICHO KWA MUMEWE!
>> MKE ANAMCHA MUNGU KWA KIWANGO KILE ANACHOMCHA MUMEWE! MKE ANAMCHA BWANA YESU ALIYEMUOKOA KWA KUMCHA MUMEWE!
>> HIKI KINAITWA KICHO CHA MKE KWA MUME
2) “For the husband is the head of the wife, even as Christ is the head of the church:
Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa naye ni mwokozi wa mwili.” (Waefeso 5:23)
>> KWA NINI MKE AMCHE MUME WAKE HIVI KATIKA BWANA?
>> JIBU LIMETOLEWA HAPA KWENYE MSTARI HUU KWAMBA NI KWA SABABU MUME NI KICHWA CHA MKEWE, VILE VILE KAMA KRISTO NAYE ALIVYO NI KICHWA CHA KANISA NAYE NI MWOKOZI WA MWILI! MUME NAYE ANA NAFASI YA KIPEKEE YA WOKOVU WA MKEWE DHIDI YA UFALME WOTE NA NGUVU ZA GIZA ZOTE, KUPITIA USHIRIKA WAKE ALIONAO NAO NA BABA NA MWANA, YAANI, ROHO NA NENO LAKE NA NGUVU ZAKE!
3) “Therefore as the church is subject unto Christ, so let the wives be to their own husbands in everything.
Kwa hiyo kama vile Kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” (Waefeso 5:24)
>> UTII WA MKE KWA MUMEWE UNATAKIWA KUWA SAWASAWA NA VILE KANISA LINAVYOMTII KRISTO!!! YAANI, UTII WA KANISA KWA KRISTO =UTII WA MKE KWA MUMEWE
>> KAMA VILE KANISA LINAVYOMTII KRISTO, NDIVYO AMBAVYO IMEMPASA MKE KUMTII MUMEWE KATIKA MAMBO YOTE!!!
>> KAMA MUME HAFANANI NA KRISTO AU NI MUOVU, UTII HUU WA MKE KWAKE UNA NGUVU ISIYOZUILIKA YA KUMBADILISHA MUMEWE (1 PETRO 3:1)
>> HAYA NDIYO MAPENZI YA MUNGU KWA YEYOTE AITWAYE MKE KWA YEYOTE AITWAYE MUMEWE PASIPO KUJALI TABIA ZOZOTE ALIZONAZO HUYU MUME!!MUME ASIYEAMINI HUWA ANATAKASWA KUPITIA MKEWE ALIYE SAFI, MTAKATIFU, MCHA MUNGU, NA MCHA MUME!!! (1 Wakorintho 7:13-14, 16)
MWENENDO WAKE
Mcha Mungu, mpole, mnyenyekevu, mtiifu, mkimya, mtulivu, asiyebishana, asiyejibizana, asiye na jeuri, mwaminifu, msikivu, mwenye kumuheshimu mumewe, asiyeweza/asiyetaka/na asiyependa kumuudhi, wala kumkosea, wala kumkasirisha mumewe! Aliyejitia kabisa na kiukamilifu chini ya mamlaka ya mumewe, aliyejitoa kuishi na kumhudumia mumewe maisha yake yote, anayependa na kufurahia wajibu na majukumu yake kwa mumewe, anayependa kumtii na kuyafanya yale yote ayapendayo na anayoyafurahia mumewe, anayewaza na kutafuta sikuzote nini afanye ili amfurahishe na kumpendeza mumewe, asiyeweza kufanya lolote kivyake pasipo kushauriana na mumewe ama kupata kibali chake, anayetambua kwamba aliumbwa kwa ajili ya mumewe kama maandiko yanenavyo;
“Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.” (1 Kor 11:9)
Mke huyu mcha Mungu anajua, anafahamu, anaelewa na anatambua kwamba HAWEZI KUDAI ANAMCHA MUNGU PASIPO KUMCHA MUME WAKE!!! Biblia inasema,
“Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.” (1Kor 11:3)
-KICHWA CHA MWANAMKE NI MWANAMUME
-KICHWA CHA MWANAMUME NI KRISTO
-KICHWA CHA KRISTO NI MUNGU
MUNGU NI KICHWA CHA
▼
KRISTO, ALIYE KICHWA CHA
▼
MWANAMUME, AMBAYE NI KICHWA CHA
▼
MWANAMKE.
KUNA VITU VYA KIROHO VITAKUJA KWA MKE KUPITIA MUMEWE TU, NA HAPA NDIPO PENYE KICHO CHA MKE KWA MUMEWE!
Mke mcha Mungu anajua thamani ya mumewe aliyonayo mbele za Mungu, na kwamba yeye ni kiongozi wa kiroho wa mkewe na familia, na kwamba kusudi la Mungu kwa familia linatimizwa kwa uongozi wa mumewe; mke mwema huyu anathamini, anaheshimu na kuyatii maamuzi ya Mungu ya kumpa mume wa namna hii, na yeye kupewa nafasi maalumu ya usaidizi kwa mumewe!
NDOA YA NAMNA HII INADUMU NA INA BARAKA TELE KWA SABABU TU YA MKE MCHA MUNGU ANAYEENENDA KAMA ULIVYO WAJIBU WAKE KWA BWANA. ANDIKO LIFUATALO TUTAMWANGALIA MUME MCHA MUNGU!
MUNGU AKUBARIKI SANA