JINSI YA KUPOKEA BARAKA YA NENO

                        Ephesians 1:3 WEB - Blessed be the God and Father of our Lord Jesus                      

JINSI YA KUPOKEA BARAKA YA NENO

Awali ya yote ieleweke kwamba Yesu ni Neno Aliye Hai ndani yake yeye amwaminiye (aliyeokoka)!!!

23Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele (1 Petro 1:23)

Kuzaliwa mara ya pili ni;

>> kuokoka kutoka kwenye utumwa wa dhambi zote,

>> kuokoka kutoka kwenye kutawaliwa, kuonewa, kukandamizwa, kutumikishwa, na kufungwa na nguvu za giza zote,

>>kuokoka kutoka kwenye utawala, mamlaka na ufalme wa shetani na majeshi yake yote,

>> kuokoka kutoka kwenye ukengeufu na upotovu wa roho zidanganyazo na mafundisho ya shetani,

>> kuokoka kutoka kwenye kuonewa na kuteswa na magonjwa, maradhi, na udhaifu wote,

>>kuokoka kutoka kwenye upofu, uziwi, ulemavu, na ububu wa kiroho, na wa kimwili pia, na kuponywa kabisa,

>> kuokoka kutoka kwenye umaskini, uhitaji, kupungukiwa, na kuishiwa kwa aina zote,

>>kuokoka kutoka kwenye kushindwa, kutengwa, kukataliwa, kukwama, kukosa msaada, upweke, huzuni, masikitiko, uchungu, uadui, ugomvi, kukata tamaa, kuvunjika moyo, kukosa tumaini, kuibiwa, na kila aina ya ubaya UNAOWAPATA WALE WATENDA DHAMBI WASIO NA TUMAINI WALA MSAADA WA MUNGU MAANA WAMEFARAKANA NAYE KWA DHAMBI ZAO!

>>kuokoka kutoka kwenye kifungo cha maisha yanayoharibika na tamaa zake zenye kudanganya,  na kupewa na kuwezeshwa kuyaishi maisha yasiyoharibika, au uzima wa milele

>> kuokoka kutoka kwenye giza la kiroho na kutiwa nuru ya uzima, na kuendelea kuishi kwenye nuru hiyo ya utukufu wa Mungu ndani yake Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wa dunia yote.

>> kuokoka kutoka kwenye kuufuata mwili na tamaa zake mbaya zenye kudanganya na zenye kupelekea uharibifu, pamoja na mawazo yake mabaya; na kuishi maisha mapya ya utakatifu ya Kristo Yesu kupitia imani iliyo hai kwa Neno lake la kweli, kwa kuwezeshwa na nguvu za Roho wake Kristo Aliye Mtakatifu.

>> kuokoka kutoka kwa shetani, na uovu wake wote, vitisho vyake vyote, hila zake zote, ubaya wake wote, ubinafsi wake wote, uongo wake wote, ukengeufu wake wote, upotovu wake wote, kiburi chake chote, ubishi wake wote, ukaidi wake wote, jeuri yake yote, dharau yake yote, majivuno yake yote, hasira zake zote, ghadhabu zake zote, uchungu wake wote, uadui wake wote, mauti yake yote, kujihesabia haki kwake kote, kujikweza kwake kote, kujiinua kwake kote, kujipendelea kwqke kote, uchoyo wake wote, ubahili wake wote, n.k. NA KUANZA KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU ALIYOYAISHI YESU KRISTO! UNAWEZA KUISHI MAISHA HAYO KWA IMANI ILIYO HAI NA TAKATIFU YA YESU KRISTO, KUPITIA NENO LAKE LA KWELI! NA KUMZALIA MUNGU MATUNDA YA HAKI, TUNDA LA NURU, NA TUNDA LA ROHO KWA NJIA YA YESU KRISTO.

HUKU NDIKO KUOKOKA! NI LAZIMA KUOKOKA ILI KUURITHI UZIMA WA MILELE NA KUINGIA MBINGUNI BAADA YA MAISHA HAYA KWENYE MWILI. YESU PEKEE NDIYE MWOKOZI!

12Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. (Yohana 1:12-13)

-Watoto wa Mungu ni wale waliompokea Yesu mioyoni mwao kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao

-Hawa ni wale waliaminilo jina lake

-Hawakuzaliwa kwa damu hawa!

-Wala hawakuzaliwa kwa mapenzi ya mwili (hakuna mimba iliyotungwa kwa mbegu ya mume tumboni mwa mwanamke!))

-Wala mwanadamu hakuhusika kwenye uzazi huu

-BALI WALIZALIWA NA BADO WANAZALIWA NA MUNGU KWA NENO LAKE [1 PETRO 1:23]

6Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. (Yohana 3:6)

>> roho yako mwanadamu ndiyo yenye kuzaliwa mara ya pili!

Mwanadamu = ( roho + nafsi ) + mwili, yaani ,mwanadamu ni roho  mwenye nafsi na anaishi kwenye mwili!

-roho yako inazaliwa mara ya pili, ndipo tunasema wewe umeokoka! Umezaliwa mara ya pili kwa Imani katika Neno aliye hai, Yesu!

14Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. (Yohana 1:14)

-Neno la Mungu lilivaa mwili wa mwanadamu!!! Kivipi?! Kwa kuwa Neno ni roho!!!

63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. (Yohana 6:63)

-Maneno ya Mungu ni roho, na tena ni uzima (life)

Hii ni muhimu kuelewa ili kujua jinsi ya kupokea Baraka ya Neno, maana kila baraka itokayo kwa Mungu ni roho! Haianzii kwenye mwili bali katika roho!! Ukisoma maandiko ya Yohana 1:1 na Yohana 4:24 utaona kwamba Mungu ni Neno, na pia ni Roho!

 

For there are three that bear record in heaven, the Father, the Word, and the Holy Ghost: and these three are one. (1 John 5:7 KJV)

“Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni mmoja.” (1 Yohana 5:7)

-HAWA WATATU NI MMOJA!!! Baba + Neno + Roho Mtakatifu = 1

-MUNGU BABA HULITUMA NENO LAKE KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU

-MUNGU BABA YETU HUZITENDA KAZI ZAKE KUPITIA NENO LAKE KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU

-Mungu wa mbinguni hufanya kazi zote kwa Neno lake, kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu! Roho Mtakatifu hudhihirisha kwenye mwili lile Neno lililotendwa na Baba wa mbinguni.

Huwezi kumtenganisha Mungu na neno lake! Neno la Mungu ni Mungu! Nalo linafanya afanyacho Mungu, linafanya mapenzi yake, linafunua mapenzi yake, lina nguvu zote za Mungu, lina uhai wote wa Mungu, lina moto wote wa Mungu, lina utukufu wote wa Mungu, lina makusudi yote ya Mungu kwa wanadamu, lina mamlaka yote ya Mungu, lina uzima wote wa Mungu, lina uponyaji wote wa Mungu, lina wokovu wote wa Mungu, lina miujiza yote ya Mungu, lina maajabu yote ya Mungu, lina ishara zote za Mungu, linaumba vile vile aumbavyo Mungu, lina tabia zote za Mungu, lina macho yote ya Mungu, lina hekima yote ya Mungu, lina ufahamu wote wa Mungu, lina maarifa yote ya Mungu, lina kicho chote cha Mungu, lina ukamilifu wote wa Mungu, lina  ushauri wote wa Mungu, lina uweza wote wa Mungu, lina ufunuo wote wa Mungu, lina unyenyekevu wote wa Mungu, lina upendo wote wa Mungu, lina furaha yote ya Mungu, lina amani yote ya Mungu, lina uvumilivu wote wa Mungu, lina utu wema wote wa Mungu, lina fadhili zote za Mungu, lina uaminifu wote wa Mungu, lina upole wote wa Mungu, lina kiasi chote cha Mungu, lina siri zote za Mungu, lina maonyo yote ya Mungu, lina maelekezo yote ya Mungu……”HAPO MWANZO PALIKUWAPO NENO, HUYO NENO ALIKUWAPO KWA MUNGU, HUYO NENO ALIKUWA MUNGU.” (Yohana 1:1) MUNGU HABADILIKI!!! MUNGU NI NENO!!!

Yote haya niliyoyanena kuhusu Neno/Mungu yanafanyika kwa Roho Mtakatifu! Yanawezekana kwa Roho Mtakatifu! Yanawezekana katika roho!!! Na yanatendeka katika roho!!! Mambo ya Mungu yote yanatendeka katika roho!!! Yanapoonekana kwa macho ya damu na nyama tayari yalishatendeka katika roho kwanza!!! Kwa hiyo hapo ni kwamba YANADHIHIRIKA tu katika mwili!!! Yaani, Neno linafanyika mwili!!! (the Word becomes flesh!!)

>> YESU ALIKUJA ULIMWENGUNI ILI NENO LA MUNGU LIFANYIKE MWILI (YAANI, LITIMIE) KWA WOTE WAMWAMINIO YEYE, KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAO! Sasa tukirudi katika andiko la Yohana 6:63 tunasoma,

“63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

HUWEZI KURITHI BARAKA ZA NENO PASIPO KUELEWA KWAMBA NENO NI ROHO!!! Roho Mtakatifu ni Roho wa Uzima (life-giving Spirit/Spirit of life) kwa maana Uzima (life) unatoka kwake!!! Maisha yanatoka kwake!!! Lakini haiwi PASIPO NENO ULILOLIAMINI!!! Baraka ya Mungu ni uzima!!! Baraka ya Mungu ni maisha!!!

“10……………… mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10)

HAPA YESU ANAONGEA KWAMBA KUSUDI  LA YEYE KUJA ULIMWENGUNI NI KUTUPA SISI TUAMINIO UZIMA TELE (ABUNDANT LIFE)!!! HIVYO HAPA KUNA BARAKA YA UZIMA TELE KUTOKA KWA NENO (Yohana10:10 b);

- HAPO KWENYE YOHANA 6:63a INASEMA, “Roho ndiye atiaye uzima!

- HAPA KWENYE YOHANA 1:4 “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu,” NDANI YAKE NENO NDIMO ULIMO UZIMA!

-NI DHAHIRI KWAMBA HUU UZIMA UMO NDANI YA ROHO WA NENO HUSIKA AMBAYE NI ROHO WA UZIMA!

Mfano namba 1:

“1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.” (Luka 18:1)

-ANDIKO HILI LINA ROHO YA KUMWOMBA MUNGU SIKUZOTE PASIPO KUKATA TAMAA!!

-UKILIAMINI NA KULIPOKEA NENO HILI MUNGU ANACHILIA NEEMA NDANI YAKO YA KUOMBA SIKUZOTE PASIPO KUKATA TAMAA!!!(YOU DO NOT TAKE NO FOR AN ANSWER IN THIS KIND OF PRAYING)

-KUONYESHA KWAMBA UMELIAMINI NENO HILI UTAOMBA; Ee Mungu Baba katika jina la Yesu,naomba unirehemu kwa kukata tamaa kwangu mara nyingi pale nilipoona mambo hayawi au hayatokei au yamekawia. Naomba unijalie neema yako ili niweze kuomba sikuzote pasipo kukata tamaa licha ya mazingira yoyote ya kukatisha tamaa ambayo nitakutana nayo; maana umesema si kwa uweza wangu wala kwa nguvu zangu, bali ni kwa Roho wako Mtakatifu; Hivyo ninaweza kuomba hivyo Baba yangu ukinitia nguvu kwa Roho wako maana imeandikwa nayaweza mambo yote katika wewe unitiaye nguvu; ni katika jina la Yesu nimeomba.

-Sasa kwa mujibu wa Marko 11:24, “Yoyote myaombayo mkisali aminini kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu.” Hii ina maana utakuwa sasa umepokea neema hiyo ya kumwomba Mungu sikuzote pasipo kukata tamaa!!!

A) TULIANZA NA NENO LA MAOMBI YASIYOKOMA WALA KUKATA TAMAA

B) TUKALIAMINI NA KULIPOKEA LILE NENO, NA TUKAOMBA REHEMA KWA KUTOLITII HUKO NYUMA

C) TUKAOMBA NEEMA YA KULIISHI HILO NENO/ANDIKO

D) KWA KUWA NI MAPENZI YAKE, MUNGU AKAACHILIA HIYO NEEMA YAKE KWETU

E) SASA YANAFUATA MAISHA YA MAOMBI SAWASAWA NA HILO NENO

Watu wa pembeni watakuwa wanaona wewe unamwomba Mungu sikuzote pasipo kukata tamaa haijalishi kuna upinzani gani au vita! Hawajui hiyo ni neema ya Mungu iliyotokana na Imani yako. Hapo tayari una baraka ya Mungu maishani mwako! Na maisha hayo ni yale yale ya Yesu!

Mfano namba 2;

3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu (Yuda mst 3)

-ANDIKO HILI LINA ROHO YA KUISHINDANIA IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU

-NI LAZIMA KULIAMINI NA KULIPOKEA HILI ANDIKO MOYONI MWAKO

-KUMBUKA IMEANDIKWA HERI WENYE NJAA NA KIU YA HAKI MAANA HAO WATASHIBISHWA

-KUSHIBISHWA KWAKO INATEGEMEA UNALITAKA NA KULIHITAJI KWA KIASI GANI LILE TAKWA LA ANDIKO AMBALO NDILO MAPENZI YA MUNGU

-UTAOMBA KAMA TULIVYOOMBA HUKO JUU, LAKINI NI KATIKA MUKTADHA WA ANDIKO HILI

-MUNGU ATAKAPOKUWA AMEACHILIA NEEMA YAKE KWAKO UTAKUWA NA ROHO YA KUISHINDANIA IMANI UKIJUA KWAMBA UMEKABIDHIWA HIYO MARA MOJA TU!

HAPA UNAWEZA KUOMBA “MOYO WA” AU “ROHO YA” MAANA YOTE NI SAWA!!

>> MUHIMU KULIKO YOTE KATIKA MAOMBI HAYA NI LAZIMA UJIFUNGE UNYENYEKEVU UNAPOKWENDA MBELE ZAKE! AINA YOYOTE YA KIBURI KISICHOTUBIWA ITAKUZUILIA BARAKA ZA NENO ZILIZO TAKATIFU SANA!!! KUMBUKA NENO HILI LIMESAFISHWA MARA SABA KATIKA TANURI LA MUNGU LA UTAKATIFU (ZABURI 12:6)

MFANO NAMBA 3:

7Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe. (1Petro 3:7)

Hili mume unajiombea mwenyewe na mke unamuombea mumeo wa sasa au mtarajiwa!

-ANDIKO HILI LINA BARAKA YA “AKILI/HEKIMA YA KUKAA NA MKE VILE APENDAVYO MUNGU”

-HUU NI MOYO WA AU ROHO YA KUKAA NA MKE KWA AKILI, NA TAFSIRI ZINGINE ZINASEMA MOYO WA KUKAA NA MKE KWA HEKIMA. HII NI HEKIMA YA MUME AU AKILI ZA MUME KUTOKA KWA BWANA YESU!

-TWAWEZA SEMA KWAMBA HUU NI MOYO WA KUKAA NA MKE KWA HEKIMA NA AKILI ZITOKAZO KWA MUNGU!!

-PIA PANA MOYO WA KUMPA MKE HESHIMA KAMA CHOMBO KISICHOKUWA NA NGUVU, (YAANI, HESHIMA YA MUME KWA MKE KUTOKA KWA YESU) NA KAMA WARITHI PAMOJA WA NEEMA YA UZIMA

ILI KUOMBA KWENU KUSIZUILIWE!!!! KAMA HAMUELEWANI NA MKEO AU MUMEO USIJISUMBUE KUOMBA WALA KUHUDUMU!!! UNAJIDANGANYA NA KUWADANGANYA UNAOWAHUDUMIA!!! MUNGU HAKUSIKII!!! KUOMBA KWAKO KUMEZUILIWA!!

USISOME TU ANDIKO, KUNA BARAKA GANI KATIKA ANDIKO HILO AMBAYO NI MAPENZI YA MUNGU? (roho gani au roho ipi ya andiko ipo?)

-INAANZA NA NENO

-INAFUATA IMANI KATIKA NENO

-YANAFUATA MAOMBI YA IMANI

-NDIPO MUNGU AKIONA UNAAMINI HUACHILIA ROHONI MWAKO NEEMA YA KULITENDA NENO/KULIISHI HILO ANDIKO

-UNAISHI SASA MAISHA YA NENO/LIFE OF GOD/LIFE OF THE WORD/LIFE OF THE SPIRIT

 

NENO LINA››››››ROHO›››››››NAYO INA UZIMA (LIFE)— (Yohana 6:63)

NENO LINA ROHO WA UZIMA!!!

New International Version
All Scripture is God-breathed and is useful for teaching, rebuking, correcting and training in righteousness, (2Tim 3:16)

New Living Translation
All Scripture is inspired by God and is useful to teach us what is true and to make us realize what is wrong in our lives. It corrects us when we are wrong and teaches us to do what is right. (2 Tim 3:16)

>> MAANDIKO YOTE YANA PUMZI(ROHO) YA MUNGU!!!

-KABLA MUNGU HAJAKUPATIA HAJA YA MOYO WAKO LAZIMA AKUPE KWANZA ‘UZIMA” AU “MAISHA” AU “UHAI WA KIROHO” ULIO WA MILELE (USIOHARIBIKA!!) HAYA NI MAISHA YA KRISTO ROHONI MWAKO YALIYO YA MILELE! MUNGU AKIKUPA CHOCHOTE KINACHOHARIBIKA KABLA YA KUKUPA VILE VISIVYOHARIBIKA ATAKUWA HAJAKUSAIDIA NA WALA HATAKUWA MUNGU TENA BALI MWANADAMU ASIYEWEZA KUKUPA CHOCHOTE KISICHOHARIBIKA! YESU ALIFUNUA UZIMA/MAISHA NA KUTOHARIBIKA KWA NJIA YA INJILI (2 TIMOTHEO 1:10) NA MAISHA HAYA NDIYO MAISHA KWENYE UFALME WA MUNGU! MAISHA KWENYE UFALME WA MUNGU NI MAISHA YASIYOHARIBIKA! HAPA NDIPO KANISA LILIPOKOSEA KWA KUDHANI MAISHA NI KUWA NA VITU TELE VYA DUNIA HII VINAVYOHARIBIKA!!! Biblia inasema,

>> “15Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.” (Luka 12:15)

>> “36Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?” (Marko 8:36)

>> “25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

31Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” (Mathayo 6:25-33)

>> “27Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.” (Yohana 6:27)

MFANO NAMBA NNE:

“1Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.

2Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele.” (Zaburi 112:1-3)

-HILI NI MOJA YA MAANDIKO NINAYOYAPENDA NA AMBALO NIMELIOMBA KWA MUDA MREFU SANA! SIKILIZA SASA NINAVYOAMINI, NA VILE NILIVYO HAKIKA;

a) MIMI NINAMCHA BWANA, MUNGU WANGU

b) MIMI NINAPENDEZWA SANA NA MAAGIZO YA BWANA

c) WAZAO WANGU (WA KIROHO NA KIMWILI) NI HODARI SANA DUNIANI KATIKA MAMBO YOTE

d) KIZAZI CHANGU NI KIZAZI CHA ADILI NA KIMEBARIKIWA

e) NYUMBANI MWANGU MNA MALI NA UTAJIRI

>> a & b ni baraka za rohoni

>> c & d inahusu wazao wangu wa kiroho na kimwili

>> e ni baraka yangu mwilini ya mali na utajiri (mimi ni tajiri sana wa mali na pesa)

Sasa jambo moja muhimu sana ni kujua kwamba  unapojenga Imani katika andiko, ukaamini na kupokea, ukaanza kungojea, mpaka kuja kupokea mwilini ni lazima  UJARIBIWE SANA! AMBAPO SHETANI HAKUBALI NA HAAMINI KWAMBA WEWE UNAISHI KWA IMANI! NA BWANA YESU ANATAKA KUITHIBITISHA IMANI YAKO! IWAPO UMEJENGWA JUU YA MWAMBA AU MCHANGA!!! (Mathayo 7:24-27)

Lazima ujue kwamba muda mrefu au mfupi utapita, utapambana sana kuing’ang’ania Imani yako dhidi ya adui, utapitia magumu mengi na dhiki nyingi pia. Lakini Yakobo anasema,

“2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” (Yakobo 1:2-4)

1) Hesabu kuwa ni furaha tupu unapoangukia katika majaribu ya namna mbalimbali

2) Kujaribiwa kwa Imani yako huleta SABURI

3) Saburi ina kazi KAMILIFU ya kukufanya wewe uwe MKAMILIFU NA MTIMILIFU USIYEPUNGUKIWA NA KITU!!!(perfect and entire wanting or lacking nothing!!)

Andiko linaposema Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu, lina maana WEWE HAUATHIRIWI KIROHO, KIAKILI, KIHISIA WALA KIMWILI NA KUWEPO AMA KUTOKUWEPO CHOCHOTE KILE KINACHOONEKANA, KUSHIKIKA, AU KUHARIBKA.

-Kwa hiyo wewe ni HUNA UNAVYO na UNAVYO HUNA!!!! Yaani ,

>> KWAKO KUWA NAVYO=KUTOKUWA NAVYO, NA

>> KUWA NAYE=KUTOKUWA NAYE,

>> KUPATA =KUTOPATA,

>> UTELE=UCHACHE, N.K

~ ~ FURAHA NA AMANI YAKO, HAIANZII WALA HAITEGEMEI WATU AU VITU VYA DUNIA HII!!! UTOSHELEVU WAKO, KURIDHIKA KWAKO, KUTOSHEKA KWAKO, , KUSHIBA KWAKO, NA USALAMA WAKO, HAUTEGEMEI FEDHA, MALI, WATU, AU VITU  AMBAVYO VYOTE HUHARIBIKA. HUU NI UKAMILIFU NA UTIMILIFU WA YESU NDANI YAKO, ANAOZUNGUMZIA YAKOBO, AMBAO UNAZALIWA NA SABURI!!

                   [ SABURI NI MAMA WA TABIA ZOTE ZA UUNGU]

Mungu anasababisha uzingojee ahadi zake, na ulingojee Neno lake kutimia hali akiwa kazini kuumba vitu vya kiroho kama uvumilivu, utu wema, upole, ukarimu, unyenyekevu, utii, uchaji Mungu n.k NDANI YAKO!

>> LITENDEE KAZI NENO URITHI BARAKA ZA KWELI ZA MUNGU!!!

-33Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. (Mathayo 6:33)

-20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; 21wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. (Luka 17:20-21)

-UFALME WA MUNGU UMO NDANI YENU

-Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme (Luka 12:32)

-BABA YAKO WA MBINGUNI AMEONA VEMA KUKUPA ULE UFALME

 JE! UNAZO BARAKA ZOTE ZA UFALME WA MUNGU?! UNAISHI KAMA MFALME LEO?!

>> BARAKA ZOTE ZA UFALME WA MUNGU NI BARAKA ZA NENO! BARAKA ZA MUNGU KWAKO WEWE MTOTO WAKE UNAYEMWAMINI YESU ZIKO KWENYE NENO LAKE! BARAKA ZAKE ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO AMEKUKIRIMIA WEWE NDANI YAKE KRISTO YESU! YESU NDIYE BARAKA YA MUNGU KWA ULIMWENGU! KUPITIA IMANI YAKO KWA YESU ROHO MTAKATIFU HUDHIHIRISHA ILE BARAKA ULIYOIPOKEA KATIKA ROHO NA KUINGOJEA HUKU UKIVUMILIA NA KUSTAHIMILI MAJARIBU YA NAMNA MBALIMBALI YA IMANI YAKO!

“3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; 4tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. 5Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. 6Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 8Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, 9katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. 10Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 11Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.”

>> VUMILIA, NGOJEA, UKIWA UMEJAA MATUMAINI NA MATARAJIO, UKIWA NA UHAKIKA KWAMBA IMEKWISHA! UNAZO HAJA ULIZOMWOMBA MUNGU! UNAZO AHADI ULIZOZIAMINI KWENYE NENO LAKE! MAANA YEYE ANALIANGALIA NENO LAKE NA KULITIMIZA! UKIAMINI YEYE ANAKUWA AMEKWISHATENDA! AMEKWISHAFANYA! IMEKWISHAKUWA! IMEKWISHATOKEA! IMEKWISHAFANYIKA! UMEKWISHAPONA! UMEKWISHAINULIWA! AMEKWISHAKUTENDEA! UMEAMINI NINI? UNAAMINI? AAMINIYE HAHITAJI KITU! AAMINIYE ANAZO HAJA ZA MOYO WAKE! AMEKWISHAPOKEA! HAZIONEKANI KWA MACHO YA DAMU NA NYAMA BADO LAKINI UNA UHAKIKA NAZO KWA KUWA UMEAMINI! HAZIJAJA BADO KWENYE MWILI LAKINI WEWE UNAZIMILIKI TAYARI MOYONI MWAKO, KINYWANI MWAKO, AKILINI MWAKO, MAWAZONI MWAKO! UNAVYO VISIVYOKUWEPO! UNAMILIKI VISIVYOONEKANA! HIVI NDIVYO NAMNA YA KUPOKEA BARAKA ZILIZO KUU ZA KIROHO! NI KWA KUAMINI NA KUVUMILIA! NI KWA KUNGOJEA KWA UTULIVU NA MATUMAINI! HAUHANGAIKI TENA WALA HAUSUMBUKI TENA! UNA AMANI YA BWANA YESU IPITAYO AKILI ZOTE! UNAJUA HAKIKA KWAMBA HATA SASA BABA NA MWANA YUKO KAZINI AKISHUGHULIKIA MAMBO YAKO! UNA UHAKIKA! HAUBAHATISHI! HAUFADHAIKI TENA! HAUKASIRIKI KABISA! NA FURAHA YA BWANA IMO NDANI YAKO! UMEJAA ROHO MTAKATIFU NA IMANI! UNATENDA MAMBO YASIYOWEZEKANA KWA KUWA UNAZO BARAKA ZAKE BWANA WA MABWANA, NA MUNGU WA MIUNGU!!! UFALME WA MUNGU UMO NDANI YAKO! MFALME MKUU YUMO NDANI YAKO! ALIYE NDANI YAKO NI MKUU KULIKO ALIYE WA DUNIA HII! UMEUSHINDA ULIMWENGU HUU NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA WETU! MKUU WA ULIMWENGU HUU HANA KITU KWAKO! HANA MASHITAKA KWAKO! MUNGU AMEMSETA CHINI YA MIGUU YAKO UPESI! UNAKULA MEMA YA NCHI MAANA UMEKUBALI NA KUTII! HALELUYA! UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO ALIYEFUFUKA KATIKA WAFU!! SHINA LA YESE, NA MZAO WA DAUDI!! UTUKUFU WA MUNGU UMEKUFUNIKA NA UNAONEKANA KWAKO! HAKIKA MUNGU AMEMTUKUZA MWANAWE PEKEE NDANI YAKO ILI NA YEYE ATUKUZWE KATIKA KRISTO YESU BWANA, KATIKA KANISA, NA KATIKA VIZAZI VYOTE HATA MILELE! NI KATIKA JINA LA YESU, HALELUYA!

 

   Ephesians 1:3 WEB - Blessed be the God and Father of our Lord Jesus

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post