BARAKA ZA MUNGU KWA NEEMA YAKE
Biblia inasema,
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo (Waefeso 1:3)
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo AMEKWISHA KUTUBARIKI SISI TUMWAMINIO YESU KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo!! Haikuandikwa “atatubariki” bali “ametubariki”!! Suala la kubarikiwa limekamilika tayari na Mungu HATATUBARIKI KWA MAANA AMESHATUBARIKI TAYARI!! Sasa kama wewe bado unasubiri baraka kamwe hutaziona! Lile neno “Imekwisha” pale msalabani maana yake mpango wa Mungu wa kuubariki ulimwengu umekamilika tayari! Ulimwengu uliopotea dhambini umebarikiwa “ndani ya Yesu”.
BARAKA
Neno Baraka lina maana ya Mungu kuachilia kwako WEMA WAKE WOTE, UPENDO WAKE WOTE, REHEMA ZAKE ZOTE, HURUMA ZAKE ZOTE, AMANI YAKE YOTE, FURAHA YAKE YOTE, UVUMILIVU WAKE WOTE, FADHILI ZAKE ZOTE, KIBALI CHAKE CHOTE, FURAHA YAKE YOTE, AMANI YAKE YOTE, UTU WEMA WAKE WOTE, KIASI CHAKE CHOTE, ISHARA ZAKE ZOTE, MAAJABU YAKE YOTE, MIUJIZA YAKE YOTE, NEEMA YAKE YOTE, UTAKATIFU WAKE WOTE, UNYENYEKEVU WAKE WOTE, UUNGU WAKE WOTE KWA JINSI YA MWILI, MAPENZI YAKE YOTE, UAMINIFU WAKE WOTE, HEKIMA YAKE YOTE, MAARIFA YAKE YOTE, UFAHAMU WAKE WOTE, KICHO CHAKE CHOTE, NGUVU ZAKE ZOTE, UTUKUFU WAKE WOTE KWA JINSI YA MWILI, USHAURI WAKE WOTE, UFUNUO WAKE WOTE, ULINZI WAKE WOTE, UONGOZI WAKE WOTE, UTAJIRI WAKE WOTE, HESHIMA YAKE YOTE, UTETEZI WAKE WOTE, UPOLE WAKE WOTE, MSAMAHA WAKE WOTE, UCHUKULIANAJI WAKE WOTE (FORBEARANCE), HAKI YAKE YOTE, MAMLAKA YAKE YOTE KWA JINSI YA MWILI, MEMA YAKE YOTE, SIRI ZAKE ZOTE, MSAADA WAKE WOTE, UZURI WAKE WOTE, AKILI YAKE YOTE KWA JINSI YA MWILI, MAFUNDISHO YAKE YOTE, MAWAZO YAKE YOTE, MAPENZI YAKE YOTE,MAKUSUDI YAKE YOTE, NA MENGI SANA MENGINEYO! Alipomuumba mwanadamu alimbariki hivi,
28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. (Mwanzo 1:28)
-AKAWABARIKIA AKAWAAMBIA……Mwanadamu amebarikiwa KWA NENO LA MUNGU
-MWANADAMU AMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE HAPA
-MWANADAMU ALIPEWA KUZAA, KUONGEZEKA, KUIJAZA NCHI, KUTIISHA, KUMILIKI NA KUTAWALA! Hivyo Mungu alimuweka mwanadamu awe mtawala juu ya uumbaji wake wote!
Haya yote mwanadamu aliyapoteza kwa shetani alipoasi kwa kulikataa Neno la Mungu, na badala yake kuliamini na kulitendea kazi neno la shetani! (Mwanzo 3:1-7) Neno la Mungu linakaa ndani ya moyo wa mwanadamu kama roho! Maneno yote ya mwanadamu yanatoka kwa roho fulani ama ya Mungu au ya shetani! Mungu ni Roho (Yohana 4:24), na maneno yake nayo ni roho! (Yohana 6:63)
Biblia inasema,
4Je! Umetamka maneno kwa nani?
Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako? (Ayubu 26:4)
Unapotamka maneno kuna roho inayoongea ndani yako, na hiyo roho hutoka kwako kwenda kwa wanaokusikia kwa njia ya maneno yako! Wakiyapokea hayo maneno yako basi inakuwa wamepokea hiyo roho iliyotoka kwako!!! Sasa Mungu aliubariki ulimwengu kwa Neno lake lakini mwanadamu akaliasi lile Neno la Mungu! Alichokifanya shetani ni kuligeuza, kulipindua na kulipotosha lile Neno la Mungu!
16BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. (Mwanzo 2:16-17)
>>………SIKU UKILA MATUNDA HAYO UTAKUFA HAKIKA!!!
4Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa (Mwanzo 3:4)
>>........WEWE KULA TU, HAKIKA HAUTAKUFA!!!
MWANADAMU AKALA AKAFA KIROHO NA CHA KIMWILI, YAANI MAUTI YA MWILI IKAINGIA ULIMWENGUNI!!! Mauti ni,
-Kupoteza uhai wa kiroho (spiritual death)
-Kupoteza uzima wa Mungu, au maisha ya Mungu (God’s life)
-Kupoteza uhusiano wa moja kwa moja na Mungu (no relationship with God))
-Kupoteza mawasiliano na Mungu (lost communication with God)
-Kupoteza sauti ya Mungu maishani mwako (lost voice of God)
-Kupoteza ushirika na Mungu maishani mwako (lost fellowship with God)
-Kupoteza uwepo wa Mungu na nguvu zake maishani mwako (lost presence and power of God)
-Kupoteza uongozi wa Mungu maishani mwako, na hivyo kuendelea kuishi katika dhambi na uasi KINYUME KABISA NA MUNGU! Una roho ya shetani na sauti yake moyoni mwako pale ambapo hauna Neno la Mungu na sauti ya Roho wake Mtakatifu. Na hii ndiyo maana Daudi alisema,
11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:11)
Neno la Mungu halikai moyoni kwa kulisoma na kulikariri tu! Kukaa kwa Neno la Mungu moyoni mwako ni PALE UNAPOTUBU NA KUIAMINI INJILI, KWA KUMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO KWANZA, NA KISHA KUENDELEA KULIJAZA NENO HILO MOYONI MWAKO ILI LIKUONGOZE, LIKUTAWALE, LIKUHEKIMISHE, LIKUONYE, LIKUELEKEZE, LIKUSAFISHE/LIKUTAKASE, LIKUFAHAMISHE, LIKUSHAURI, LIKUTIE NGUVU, LIKUPE MAWAZO NA AKILI YA MUNGU, LIKUFUMBUE MACHO, MDOMO NA MASIKIO, LIKUPONYE, LIKULINDE, LIKUTAHADHARISHE, LIKUJULISHE, LIKUFUNULIE, LIKUTATULIE, LIKUFUMBULIE, LIKUJIBU NA MENGI SANA MENGINEYO! MUDA NA NAFASI HAVITOSHI KWA SASA!
Sasa Yesu ni Neno aliyefanyika mwili (Yohana 1:14)
14Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Kumwamini Yesu ni kuokoka na ndio mwanzo wa Neno kukaa moyoni mwako! Yesu anakaa moyoni mwako kwa Imani unapolijaza Neno lake! Biblia inasema,
63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima (Yohana 6:63)
-MANENO YA YESU NI ROHO
-MANENO YA YESU NI UZIMA/LIFE
-MANENO YA YESU NI KUTOKA KWA ROHO WA UZIMA!! (SPIRIT OF LIFE) UZIMA NI MAISHA! HUYU NI ROHO WA MAISHA YA KRISTO YALIYOMO KWENYE NENO LAKE AMBAYE NDIYE MWENYE KUKUWEZESHA KUYAISHI MAISHA HAYO! HAYO NI MAISHA YASIYOHARIBIKA YALIYO YA MILELE! HUO NDIO UZIMA WA MILELE.
Yesu anakaa moyoni mwako kama Roho!
45Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. (1 Wakorintho 15:45)
-ADAMU WA MWISHO NI YESU AMBAYE NI ROHO MWENYE KUHUISHA (LIFE GIVING SPIRIT or SPIRIT OF LIFE)
17Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; (Waefeso 3:17)
-KUWA NA YESU MOYONI NI KUWA NA NENO LAKE KAMA ROHO!
-YESU NI NENO LILILO HAI NDANI YA MWAMINI
-UHAI WA NENO NI ROHO WA HILO NENO MAANA TUMESOMA ROHO NDIYE ATIAYE UZIMA (WHO GIVES LIFE)- [YOHANA 6:63]
Mpaka hapa tumeona kwamba Mungu alimtuma Neno lake ulimwenguni(Yohana 1:14), na ndiposa tunasema;
- MUNGU ALIUBARIKI ULIMWENGU KWA NENO LAKE!!!
-AKAJA SHETANI AKAMDANGANYA MWANADAMU AKALIKATAA NA KULIASI NENO
-BADALA YA BARAKA SASA IKAJA LAANA MAANA UKILIASI NENO UNAKUWA CHINI YA LAANA YA UASI (CURSE OF DISOBEDIENCE)
-ULIMWENGU WOTE UKAWA UMEASI
-IKABIDI MUNGU ALITUME NENO LAKE TENA ULIMWENGUNI KATIKA NAMNA AMBAYO KILA ATAKAYELIPOKEA NA KULIAMINI AWE SALAMA, NA PIA AWE NA NGUVU ZA KUKATAA NA KUSHINDA UASI!
-NDIPO AKAZALIWA YESU (NENO KATIKA MWILI) ILI AVAE MWILI DHAIFU WA KIBINADAMU NA KUISHINDA DHAMBI NA HATIMAYE KUIONDOA PALE JUU MSALABANI
Yesu alizaliwa, akakua, akajazwa Roho Mtakatifu alipobatizwa kwenye maji mengi ya mto Yordani na Yohana Mbatizaji!
13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. 16Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; 17na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. (Mathayo 3:13-17)
Baada ya Roho wa Neno kushuka juu yake ndiposa ndani ya Yesu kukawa na Neno kama kitabu cha Waebrania kinavyoeleza,
12Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. (Waebrania 4:12-13)
Bwana wetu Yesu alitembea ulimwenguni humu akiwa ni Neno,
-Lililo hai
-Lenye nguvu za Mungu
-Lenye ukali kuliko upanga wowote ukatao kuwili
-Lenye kuchoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake
-Lililo jepesi/quick kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo wa mwanadamu
-Ambalo viumbe vyote viko wazi mbele zake
-Ambalo vitu vyote viko utupu/naked na kufunuliwa/open mbele zake
-BARAKA ZOTE ZIKO KWENYE NENO LA MUNGU
-CHOCHOTE KISICHOTOKANA NA NENO LA MUNGU SIYO BARAKA BALI NI LAANA NA DHAMBI
-CHOCHOTE KISICHOTOKANA NA NENO LA MUNGU HAKIKUTOKANA NA MUNGU
-CHOCHOTE KISICHOANZIA KWENYE NENO LA MUNGU HAKIKUANZIA KWA MUNGU
-BARAKA YA KWELI YA MUNGU HAIPO KWA YEYOTE ASIYEMWAMINI YESU/YEYOTE ASIYEZALIWA MARA YA PILI/YEYOTE ASIYEOKOKA MAANA IMO ROHO YA DHAMBI NDANI YAKE INAYOMPELEKEA KUMTUMIKIA SHETANI NA KUYAFANYA MAPENZI YA SHETANI KWA MAWAZO, MANENO NA MATENDO YAKE!!
-MWENYE DHAMBI NI MBINAFSI NA AMEJAA UMIMI NA LOLOTE ALIFANYALO, HATA KAMA NI JEMA, LINA NIA/MAKUSUDI/MALENGO YA KIBINAFSI AMBAYO NI MALENGO NA MAKUSUDI YA DHAMBI
-MWENYE DHAMBI HUJIVUNIA MAFANIKIO ANAYOYAITA “YAKE” KWA SABABU ANATEGEMEA AKILI ZAKE, NGUVU ZAKE, JUHUDI ZAKE, BIDII ZAKE, FEDHA ZAKE, ELIMU YAKE, CHEO CHAKE, MALI ZAKE, HISTORIA YAKE, MAHUSIANO YAKE, N.K
-MWENYE DHAMBI KAMWE HAMPI MUNGU UTUKUFU NA WALA HANA ULE UFAHAMU WA KUWA NA MUNGU HATUA KWA HATUA MAISHANI MWAKE
-MWENYE DHAMBI ANAKIRI MUNGU YUPO NA ANAWEZA YOTE ILA HAMTEGEMEI MUNGU NA WALA HATAKI KUACHA DHAMBI
-MWENYE DHAMBI ANAMFANYA MUNGU KUWA NI MTUMWA WAKE WA KUMFANYIA TU YALE ANAYOYATAKA YEYE LAKINI HANA HAJA NA MUNGU WALA NENO LAKE
-MWENYE DHAMBI HAJAWAHI KUMKIRI YESU YA KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WAKE NA KUPATANISHWA NA MUNGU KWA NJIA YA DAMU YAKE
-MWENYE DHAMBI ANAJUA YA KWAMBA ANAISHI DHAMBINI ILA HATAKI KUOKOKA NA WALA HANA HAJA YA NENO LA MUNGU
-MWENYE DHAMBI ANAABUDU SANAMU ZA PESA, MALI, VYEO, UMAARUFU, HESHIMA YA WANADAMU, HOFU YA WANADAMU, MIUNGU ISIYONENA WALA KUWA NA UHAI, MIUNGU ISYOWEZA KUOKOA WALA KUKEMEA DHAMBI ZAKE
-MWENYE DHAMBI AMEJITENGENEZEA DINI YAKE NA MADHEHEBU YAKE AMBAPO ANADAI ANAMWABUDU MUNGU, LAKINI ANAINGIA NA DHAMBI ZAKE NA KUTOKA NAZO WIKI BAADA YA WIKI, MWEZI BAADA YA MWEZI, MWAKA BAADA YA MWAKA NA MPAKA SASA BADO AMEJIDANGANYA NA KUDANGANYWA!!!
MWENYE DHAMBI HUNA YESU, HUNA NENO! HUNA NENO, HUNA UZIMA! HUNA UZIMA YOTE UYAFANYAYO NI KWA AJILI YA KUSHIBISHA MATAKWA NA MALENGO YAKO YA KIBINAFSI NA HAYAMPI MUNGU SIFA, HESHIMA, SHUKRANI WALA UTUKUFU!
MUNGU AMEUBARIKI ULIMWENGU WA LEO KWA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI (GOD HATH BLESSED THE WORLD WITH JESUS). YESU NI BARAKA YA MUNGU KWA ULIMWENGU WOTE ULIO DHAMBINI! LAKINI NI LAZIMA UMWAMINI, UTUBU, NA UMPOKEE ILI UWEZE KURITHI BARAKA!!! KUMPOKEA YESU NI KUPOKEA BARAKA ZOTE ZA NENO ZILIZOMO KWENYE NENO LA UZIMA! YESU NDIYE BARAKA NA CHANZO CHA BARAKA MNA KIINI CHA BARAKA ZOTE ZA KIBIBLIA!
14Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. (Warumi 8:14-17)
OKOKA, MPOKEE YESU, NJOO KWA YESU ILI UWE MWANA WA MUNGU AMBAYE NENO LINAKAA NDANI YAKE KWA ROHO WA KRISTO, NDIPO UTAKUWA MRITHI WA KWELI WA MUNGU UNAYERITHI PAMOJA NA KRISTO BARAKA ZOOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KAMA MAANDIKO YANENAVYO!!!
BARAKA ZA ROHONI
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; (Waefeso 1:3)
Zinaitwa baraka za rohoni kwa sababu zinaanzia kwa Mungu aliye Roho (Yohana 4:24)
MUNGU NI ROHO………………. (1)
63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. (Yohana 6:63)
NENO NI ROHO…………………. (2)
NENO NI UZIMA………………… (3)
-Mungu ni Roho ambaye alilituma Neno lake ulimwenguni kuja kuukomboa ulimwengu kutoka dhambini, naye Neno Akavaa mwili na kuitwa Mwana wa Mungu Yesu Kristo! Neno ni Roho na ndiyo kusema Roho Mtakatifu alikuja ulimwenguni kwa Neno lake na kuvaa mwili! Ndani ya mwili wa Yesu alikuwemo Roho na Neno lake katika roho ya mwanadamu Yesu! [(Roho Mtakatifu + roho ya mwanadamu Yesu) + Nguvu za Roho Mtakatifu wa Kristo] Roho na Neno lake ni mmoja! (The Spirit and his Word are one!)
New King James Version
For there are three that bear witness in heaven: the Father, the Word, and the
Holy Spirit; and these three are one. (1 John 5:8)
8Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni mmoja. (1 Yohana 5:8)
BABA,NENO NA ROHO MTAKATIFU NI MMOJA! HUWEZI KUMTENGANISHA MUNGU NA NENO LAKE KAMA VILE MTU ASIVYOWEZA KUKUTENGANISHA WEWE NA NENO LAKO!!! NA NENO LA MUNGU NI ROHO! [Yohana 6:63) NA TUNAJUA MUNGU NI ROHO! [Yohana 4:24]
Sasa basi kila anachokifanya Mungu ni kwa Neno lake! Neno lake limebeba mapenzi yake, matakwa yake, makusudi yake na nia yake!! Hivyo hivyo kila anachokifanya Mungu kwa mwanadamu ni lazima kwanza Neno lake litangulie!! Neno lake ni baraka kwa ulimwengu!! Neno lake likitangulia ndipo Roho hutekeleza kile kilichonenwa!
Neno la Mungu liliumba!
6 Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. (Zaburi 33:6)
Roho wa Mungu aliumba!
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. (Ayubu 33:4)
MUNGU AMBAYE NI ROHO ALIUMBA KWA NENO LAKE, ANAUMBA KWA NENO LAKE, NA ATAZIDI KUUMBA KWA NENO LAKE! TUMEBARIKIWA NDANI YA YESU KWA BARAKA YA UUMBAJI! MAANDIKO YANASEMA YESU KRISTO NI YEYE YULE JANA, LEO NA HATA MILELE (Waebrania 13:8)! HIVYO BADO ANAWEZA KUUMBA NENO JIPYA KATIKA MAISHA YAKO HATA SASA!
Msingi wa uumbaji wa Yesu leo hii katika maisha ya mwamini ni Yohana 10:10!
10Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele (Yohana 10:10)
Mungu amemtuma Yesu ulimwenguni kuja,
-kurejeza kila alichoiba shetani
-kufufua kila alichoua shetani
-kutengeneza kila alichoharibu shetani, katika maisha ya mwamini! (believer)
Kisha baada ya hapo kumjaza Uzima tele kwa njia ya Neno lake; ndiyo maana Paulo anaandika,
16Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu (Wakolosai 3:16)
Neno kwa wingi moyoni ni uzima tele moyoni maana Neno ni roho, na tena ni uzima!(Yohana 6:63)
-HAPA NI LAZIMA IELEWEKE KWAMBA NENO LA MUNGU HALIKAI KATIKA MOYO WA MTENDA DHAMBI
-KWA MTENDA DHAMBI NENO LINAKAA KICHWANI TU (HEAD KNOWLEDGE)
-MOYONI NENO LINAKAA KWA IMANI YA YESU ILIYO TAKATIFU SANA
-NENO HILO LINAKAA KWA ROHO WA YESU ALIYE MTAKATIFU
-KWA MTAKATIFU ASIYE NA NENO MOYONI KWA WINGI NI LAZIMA;
1) ATARUDI NYUMA,
2) ATAPOA BADALA YA KUWA MOTO,
3) ATASHINDWA VITA YA KIROHO AMBAYO NI VITA YA IMANI
4) HATAWEZA KUZAA MATUNDA YAPASAYO TOBA WALA KUMZALIA MUNGU MATUNDA
5) HATAWEZA KUKUA KIROHO,
6) HATAWEZA KUMPENDEZA MUNGU MAANA HATAWEZA KUISHI KWA IMANI!
7) HATAWEZA KURITHI BARAKA ZAKE
Hii ni kwa sababu baraka zote huja kwa njia ya Roho na neno lake!
MTIRIRIKO WA BARAKA
1) Yote huanzia kwenye Neno
2) Ukiliamini Neno unapokea roho ya hilo Neno uliloliamini
-Kwa njia ya hiyo roho ya hilo neno/andiko utaweza kuomba/kusali, kuombea, na kuendelea kuvipiga vita vya Imani dhidi ya kila upinzani na mashambulizi ya kuzimu na mauti, na mashetani yote yanayolenga KUKUIBIA LILE NENO ILI KUUA IMANI YAKO NA KUHARIBU UHUSIANO WAKO NA MUNGU; ILI HATIMAYE KUKUFANYA USIPOKEE BARAKA YA LILE NENO!
-Hakuna baraka inayokuja pasipo mashindano na adui katika ulimwengu wa roho. Ndiyo maana Paulo akaandika,
12Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. (Waefeso 6:12)
-TUNASHINDANA NA UFALME WA GIZA ILI KUZISHIKILIA BARAKA ZETU TULIZONAZO KATIKA KRISTO
-TUMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE YESU KRISTO TAYARI
-SHETANI ANAJARIBU KUZIIBA HIZO BARAKA AU KUZICHELEWESHA ILI ZISITUFIKIE
-SISI TUNAOAMINI TUNASHINDANA NAYE TUKIWA TUMEZING’ANG’ANIA BARAKA ZETU
-UNAZING’ANG’ANIA BARAKA KWA KULING’ANG’ANIA NENO LA KRISTO LA HIZO BARAKA HUSUSANI PALE AMBAPO KILA KITU KIKO KINYUME NAWE, MAMBO YANAHARIBIKA, AU YAMEHARIBIKA, MAMBO YAMEKWAMA, MAMBO HAYAENDI UNAVYOTAKA AU ULIVYOTARAJIA, MAMBO YAMEKUWA MAGUMU N.K
23Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. (Yohana 14:23)
-INAJULIKANA KWAMBA UMELISHIKA NENO NYAKATI ZA KUJARIBIWA AMA NYAKATI ZA VITA
-KULISHIKA NENO NI KULITUMIA KAMA UPANGA WA ROHO DHIDI YA KILA KILICHO KINYUME NA NENO
-NA NDIPO UTAUONA UTUKUFU WA MUNGU MAANA UMEAMINI! UTAONA NGUVU ZAKE, MOTO WAKE, UAMINIFU WAKE, UKUU WAKE, WIVU WAKE N.K
-NDIYO MAANA TUNAHITAJI KILA IITWAPO SASA REHEMA ZAKE NA NEEMA YAKE KAMA MAANDIKO YASEMAVYO,
16Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. (Waebrania 4:16).
Hii ndiyo neema ya Mungu!
6Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi. 7Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie. (Hosea 4:6)
>> SI KWA UWEZA WALA SI KWA NGUVU, BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!!!
UBARIKIWE KWA JINSI UTAKAVYOFANYA MILIMA MIKUBWA KUWA TAMBARARE KWA ROHO MTAKATIFU KUPITIA IMANI YAKO ILIYO HAI KWA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WAKO.
AMEN, UBARIKIWE