YESU NI MUNGU
Biblia inasema,
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1)
“Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.” (Yohana 1:3)
Maandiko hapa yako wazi kwamba;
1) LINI? MWANZO! KWAMBA NENO ALIKUWAKO TANGU MWANZO
2) WAPI? NENO HUYO ALIKUWAKO KWA MUNGU (WAS WITH GOD)
3) ALIKUWA NANI? NAYE HUYO NENO ALIKUWA NDIYE MUNGU!
>>KAMA NENO ALIKUWA MUNGU, HATA LEO BADO NENO NI MUNGU, NA HUYU NENO ATABAKI KUWA MUNGU MILELE! (HE IS GOD FROM EVERLASTING TO EVERLASTING!)
Mpaka hapa hakuna shaka yoyote kwamba NENO = MUNGU, ambayo maana yake ni kwamba;
- Uungu wa Neno ndio uungu wa Mungu
- Mamlaka ya Neno ndiyo mamlaka ya Mungu
- Utukufu wa Neno ndio utukufu wa Mungu
- Nguvu za Neno ndizo nguvu za Mungu
- Mungu alipokuwako, Neno naye alikuwako,
- Mungu anachotenda ndicho Neno anachotenda,
-Mungu asemacho ndicho asemacho Neno! Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe! n.k. Neno na Mungu ni mmoja (God and the Word are one!) Neno ni la Mungu! Na pale anaposema “naye Neno alikuwako kwa Mungu”anamaanisha huyu Neno alikuwako kifuani mwa Mungu! Hii maana yake pasipo Neno hakuna Mungu, na pasipo Mungu hakuna Neno lake!
Uumbaji wa Neno
“6 Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake” (Zaburi 33:6)
“Vyote vilifanyika kwa huyo(Neno); wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika” (Yohana 1:3)
>> BWANA MUNGU MWENYEZI ALIUMBA VYOTE NA ANAFANYA YOTE KWA NENO LAKE!
“9 Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama.” (Zaburi 33:9)
Uumbaji wa Mungu
“1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” (Mwanzo 1:1)
“3Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.” (Mwanzo 1:3)
>> MUNGU ALIUMBA MBINGU NA NCHI NA VYOTE VILIVYOMO KWA NENO LAKE
Mpaka hapa tumeona jinsi Mungu alivyojifunua kwetu na utendaji wake: MUNGU NA NENO LAKE!
Biblia inasema;
“Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yoh 1:14)
1) Neno ambaye tumeona kwamba ni Mungu aliamua kufanyika mwili
2) Alipofanyika mwili akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake
3) Utukufu wake tuliouona ni utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba
4) Huyu Mwana pekee atokaye kwa Baba alikuja akiwa amejaa Neema na Kweli.
Hapa tumeona Neno anafanyika mwili, anakaa kwetu, nasi tunampokea kama Mwana pekee wa Mungu atokaye kwa Baba. Hapa sasa tuna Baba na Mwana! Mungu amekuwa Baba, na Neno amekuwa Mwana!
“26Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. 28Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? 30Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. 32Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.”(Luka 1:26-32)
1) Mungu anamtuma malaika Gabrieli kwa Bikira Mariamu, na kumjulisha kwamba amepata neema kwa Mungu
2) Kwamba atachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume ambaye atamwita jina lake, Yesu.
3) Huyu Yesu ataitwa Mwana wa Aliye juu, yaani Mwana wa Mungu!
Mariamu aliyekuwa bikira akahoji itawezekanaje yeye kuzaa mwana huku hajui mwanamume? Malaika Gabrieli akamwambia;
“34Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? 35Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (Luka 1:34-35)
1) Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;
2) kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Kwamba mimba ya Yesu ilitungwa kwa;
1) Neno la Mungu la Luka 1:31-35, na 2) Roho Mtakatifu na Nguvu zake
[MIMBA TAKATIFU YA YESU = NENO + ROHO MTAKATIFU + NGUVU ZAKE]
>>NENO AMBAYE NI MUNGU ANAVAA MWILI (INCARNATION) KWA KUZALIWA NA BIKIRA KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU [mimba ya Mariamu ilikuwa ni mimba ya Neno(Mungu) kwa Roho Mtakatifu]
KANUNI:UZAZI WOTE LEO WA KIROHO AU WA KIMWILI, KAMA UNA LENGO LA KUZAA “VITAKATIFU” LAZIMA UWE NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KUPITIA IMANI ILIYO HAI KWA YESU, NENO LA MUNGU!
>> MARIAMU ANAAMBIWA KWA SABABU HIYO HICHO KITAKACHOZALIWA KITAITWA “KITAKATIFU MWANA WA MUNGU” HIVYO NI DHAHIRI KUWA YESU ALIZALIWA NA MWANAMKE KWA MBEGU TAKATIFU YA NENO, NA MIMBA IKATUNGISHWA TUMBONI MWA MARIAMU KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE, PASIPO MBEGU YA MUME AU MWANADAMU KUHUSIKA! MIMBA ILIKUWA NI TAKATIFU! NENO LA UJAUZITO LILILOUMBA MWANA TUMBONI MWA MARIAMU LILIKUWA NALO TAKATIFU! ALIYEZALIWA NAYE NI MTAKATIFU MWANA WA MUNGU ALIYE JUU! (HOLY CONCEPTION VIA A HOLY WORD, HOLY PREGNANCY, AND A HOLY CHILD BY THE POWER OF THE HOLY SPIRIT)
Mpaka hapa tumeongeza Roho Mtakatifu! Biblia inasema, Mungu ni Roho (Yohana 4:24) na pia Mungu ni Mtakatifu (1 Petro 1:16) Kwa hiyo Mungu ni Roho Aliye Mtakatifu! Ile asili yake kama Roho inamwezesha kuwa na sifa ya kuwa mahali pote kwa wakati mmoja. (Omni presence) Hivyo tunapoongelea Mungu ambaye sasa amekuwa Baba wa Mwana pekee, tunaongelea Roho Aliye Mtakatifu sana! Bila shaka ndiyo maana maandiko yanasema;
“1 John 5:7-8
King James Version
7 For there are three that bear record in heaven, the Father, the Word, and the Holy Ghost: and these three are one.”
TAFSIRI YAKE
1 Yohana 5:7-8
“ Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni mmoja.”
KUNA BABA, NENO, NA SASA ROHO MTAKATIFU, NA HAWA WATATU NI MMOJA! Yohana 1:1 tunaweza kuisoma hivi sasa; “Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu (Aliye Roho), naye Neno huyo alikuwa Mungu (Roho)”
NENO = MUNGU = ROHO, WATATU HAWA NI MMOJA (yaani, 1+1+1=1)
Tunahitimisha hapa kwamba MUNGU NI ROHO ALIYE MTAKATIFU, NAYE SIKUZOTE HUTENDA KAZI ZAKE ZOTE KWA NENO LAKE, KWA NGUVU ZAKE MWENYEWE ROHO MTAKATIFU, MAANA YEYE NI MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU! KWA KUWA BABA, NENO, NA ROHO MTAKATIFU NI MMOJA!
NENO KUFANYIKA MWILI
Yesu, Mwana wa Mungu, alikuja kwenye mwili, kwa Neno kufanyika mwili kama tulivyoona kwenye Luka 1:31-35 & Luka 2:1-7 Kuanzia alipozaliwa Yesu na mwanamke na pia jinsi alivyozaliwa;
1) WANADAMU WOTE WATAKAOMWAMINI YESU WATAZALIWA MARA YA PILI, ROHO ZAO, HIVYO KWA NENO (YESU) WALIYEMUAMINI, ROHO MTAKATIFU, NA NGUVU ZAKE.
2) WOTE WAAMINIO NAO WATAPOKEA AHADI ZOTE ZA MUNGU ZILIZOMO KATIKA KRISTO YESU KWENYE MWILI,( 2 KOR 1:20) PALE NENO LAKE WALIAMINILO LITAKAPOFANYIKA MWILI KAMA VILE LILIVYOFANYIKA MWILI AKAZALIWA YEYE YESU KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE.
3) KANUNI ILIYOPO YA IMANI NI NENO KUFANYIKA MWILI KWA JINA LA YESU KUPITIA IMANI ILIYO HAI KWAKE, KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU. NA NDIPO UNAPOKEA AHADI ZAKE NA NENO LAKE KUTIMIA KWAKO, NA HIVYO KUTIMIZA MAKUSUDI NA MAPENZI YAKE KWAKO, NDANI YAKE YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU.
4) MWANA WA MUNGU YESU NI MUNGU KATIKA MWILI KWA MAANA NENO NI MUNGU! HIVYO NI DHAHIRI MUNGU ALIAMUA KUJA KWENYE MWILI, NA HILI LINATHIBITISHWA NA MAANDIKO;
“16Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.
Mungu alidhihirishwa katika mwili,
Akajulika kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na malaika,
Akahubiriwa katika mataifa,
Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.” (1 Timotheo 3:16)
>> MUNGU ALIYE NENO ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI KWA KUZALIWA NA MWANAMKE AKAITWA MWANA WA MUNGU
>> ILI AWE MWANA ILIBIDI AUWEKE PEMBENI UTUKUFU ULE ALIOKUWA NAO NA BABA YAKE MBINGUNI TANGU KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU; NA ALIPOKUWA AKIMALIZA MWENDO ALIMUOMBA BABA YAKE AMRUDISHIE ULE UTUKUFU WAKE ALIOUWEKA PEMBENI PALE , UTUKUFU ALIOKUWA NAO SAWA NA BABA YAKE KABLA HAJAJA KWENYE MWILI, ALIKOZALIWA NA MWANAMKE AWE MWANADAMU.
“5Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.” (Yohana 17:5)
>> Hivyo kuna utukufu wa Yesu, Neno la Mungu, kabla hajafanyika mwili. Yaani, utukufu wake pasipo mwili,
>> Na pia kuna utukufu ule aliopewa na Baba yake ili awe nao kwenye mwili, utukufu ambao tuliuona kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa Neema na Kweli.(Yohana 1:14)
>> Ndiposa twasema utukufu wa Mungu Baba yetu pasipo mwili huu ni mbali na utukufu wa Mungu wetu kwenye mwili.
>> Utukufu aliokuwa nao Bwana wetu Yesu ni utukufu uliokuwa umekusudiwa kwetu sisi tuliomwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wetu, utukufu ambao Bwana wetu Yesu ametupa sisi kama maandiko yanenavyo;
“22Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.” (Yohana 17:22)
>> HILI NENO ‘UMOJA’ LILILOTUMIKA HAPA NI NENO ‘MMOJA (ONE)’ NA ANDIKO LINASOMEKA KIUSAHIHI KAMA “.....ili wawe mmoja kama sisi tulivyo mmoja” KWA HIVYO MUNGU AMETUPA SISI UTUKUFU ULE ALIOMPA MWANAWE PEKEE YESU, ILI WOTE TUAMINIO TUWE MMOJA KAMA BABA, MWANA, NA ROHO MTAKATIFU WALIVYO NI MMOJA!
Kwenye maombi yake kwa Baba yake, Bwana wetu Yesu alisema,
“6JINA LAKO nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na NENO LAKO wamelishika.”(Yohana 17:6)
“12Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa JINA LAKO ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.”(Yohana 17:12)
“26Nami naliwajulisha JINA LAKO, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”(Yohana 17:26)
>> “YESU” NI JINA LA BABA YAKE YESU ALILOMPA MWANAWE PEKEE YESU! YAANI, YESU NI JINA LA MUNGU BABA KWENYE MWILI.
>> MUNGU AMETUPA SISI TUNAOMWAMINI JINA LAKE, NENO LAKE, ROHO WAKE, IMANI YAKE, NGUVU ZAKE, NA PENDO LAKE ILI YEYE ATUKUZWE NDANI YETU NA PIA KUPITIA SISI; YAANI, UTUKUFU WAKE ALIOTUPA UONEKANE KWETU NA SISI TUPATE KUWA SIFA YA UTUKUFU WAKE! UTUKUFU WAKE NI NGUVU YA UUNGU WAKE NDANI YETU TUMWAMINIO YESU!
Mwana wa Mungu Yesu ni Mungu kwenye mwili! Utimilifu wote na ukamilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya mwili ulikaa ndani yake yake YESU!
>> YAANI, YESU NI MUNGU ALIYEKAMILIKA KWA JINSI YA MWILI
Kwa kuwa Mungu hajawahi kabla ya Yesu kuja kwenye mwili, na hatakuja tena kufanya ukombozi wa mwanadamu maana amekwishaikamilisha kazi hiyo mara moja tu pale msalabani! (Ebr 10:14)
YESU NI JINA LA MUNGU KWENYE MWILI!! Mungu alikuja kukaa ndani ya mwili wa mwanadamu akaitwa Yesu!!
Paulo anaandika,
“Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol 2:9)
New International Version
For in Christ all the fullness of the Deity lives in bodily form,
New Living Translation
For in Christ lives all the fullness of God in a human body.
>>MAANA KATIKA KRISTO UTIMILIFU NA UKAMILIFU ‘WOTE’ WA MUNGU [KWA JINSI YA MWILI] UNAISHI/UNAKAA!
>>Yesu ni Mungu katika mwili………....(1)
>> Yesu pia ni Mwana wa Mungu………(2)
Tukiunganisha (1) na (2) tunaona kuwa,
>> MUNGU KATIKA MWILI NI MWANA WA MUNGU YESU
>> KULE KUVAA MWILI KUNAMAANISHA KUNA UTUKUFU WAKE ALIOKUWA NAO MBINGUNI ALIUWEKA PEMBENI ILI AWEZE KUONEKANA NA MFANO WA MWILI WA MWANADAMU
“Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako”(Yoh 17:5)
>> KUNA UTUKUFU AMBAO BABA ALIMRUDISHIA NENO BAADA YA KURUDI MBINGUNI ALIPOIMALIZA KAZI!
Kuna utukufu wa Mungu kama Roho (Yoh 4:24) mbinguni, na kuna utukufu wa Mungu katika mwili (Yesu) ambao huo ametupa sisi na ni lazima tufikie kuishi, kuenenda, na kutenda kazi na huduma zote katika utukufu huo!
“Nami UTUKUFU ULE ULIONIPA NIMEWAPA WAO; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.” (Yoh 17:22-23)
>>YESU NDANI YETU, NA BABA (ROHO) NDANI YA YESU
>>HIVYO BABA NA MWANA NDANI YETU, NA SISI NDANI YA BABA NA MWANA [HUU NDIO UTUKUFU TULIOPEWA UNAOTUPELEKEA SISI KUWA miungu KAMA MAANDIKO YANENAVYO]
“ Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu (Zab 82:6-7)
“Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka)” (Yoh 10:33-35)
>>KAMA VILE MWANA WA MUNGU YESU ALIVYOKUWA NI MUNGU KWENYE MWILI (GOD IN THE FLESH),
>>NDIVYO TULIVYO WANA WA MUNGU KWAMBA NI miungu KWENYE MWILI
Huu ndio utukufu alioukusudia Mungu kwa ajili yetu tangu kabla haijawekwa misingi ya ulimwengu kwamba tuje kuwa miungu ndani ya miili yetu; na Yesu ndiye aliyeanzisha mwendo huo na kila ambaye,
>> Ataendelea kukua kiimani pasipo kudumaa na kuanza kwenda kwa kuona,
>> Ataendelea kujitakasa na kuongezeka utakatifu wake bila kukoma wala kuridhika au kujivuna,
>> Ataendelea kuongezeka upendo wake bila kukoma wala kuridhika,
>> Atajaa wivu wa Bwana na kuendelea kujaa wivu huo bila kukoma ili Yesu aonekane ndani yake katika utimilifu wake wote,
>> Ataendelea kuzidi kuwa mnyenyekevu, na kuzidi kujishusha, na kuzidi kuwa mtumishi wa wengine pasipo kukoma na kujiona sasa anastahili kutumikiwa,
>> Ataendelea kumtaka Bwana na nguvu zake zaidi, na zaidi, na zaidi pasipo kukoma,
>> Atazidi kuongezeka njaa na kiu yake ya haki pasipo kukoma,
>> Atakuwa akiongezeka na kuzidi sana kutafuta kuyajua, kuyafanya, kuyaelewa, kuyaishi, na kuyatenda mapenzi yote ya Mungu ndani ya Kristo Yesu pasipo kukoma,
>> Atazidi kujiona kwamba hajafika bado, hajakamilika bado, na sikuzote kuuchuchumilia ukamilifu na utimilifu wa Kristo Yesu katika mambo yote pasipo kukoma, akijua kuwa hayo ni mapenzi ya Mungu maishani mwake sikuzote,
>> Atazidi kutafuta kwamba Ufalme wa Mungu na haki yake uwe kipaumbele chake namba moja katika yote ayafanyayo, na maisha yake yote, akijua kwamba yeye ni mfalme na kuhani wa Mungu ndani ya Yesu hapa ulimwenguni; akawa akiishi kwa ajili ya lengo hilo kuu kuliko yote la kuutafuta ufalme wa Mungu uje kwenye kila moyo wa kila mwanadamu wa kila lugha, jamaa, taifa, na kabila ulimwenguni, na kudhihirika katika jamaa na jamii zote za wanadamu pasipo kukoma maisha yake yote,
>> Hataridhika na mafanikio yake ya kimwili ya vitu vinavyoharibika kama pesa, mali, na utajiri, na akawa anatafuta neno moja tu: UTUKUFU WA BABA NA MWANA NDANI YAKE MWENYEWE KWANZA, KATIKA KANISA, NA KATIKA VIZAZI VYOTE HATA MILELE, N.K
>> MTU WA NAMNA HIYO, ROHO WA KRISTO ATAMPELEKA KWENYE VIWANGO VYA UTUKUFU WOTE WA MUNGU KWA JINSI YA MWILI KAMA ALIVYOKUSUDIA MUNGU, KISHA AKATUPA UTUKUFU HUO NDANI YA KRISTO YESU!!! HUYO ATATEMBEA KATIKA DUNIA HII KAMA mwana wa Mungu ambaye ni “mungu” (a god) katika mwili!!!
YESU NA FILIPO
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.” (Yoh 14:6-7)
>>KAMA MNGENIJUA MIMI (YESU) MNGEMJUA BABA (MUNGU)
“Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha” (Yoh 14:8)
>>FILIPO ANAMWAMBIA YESU AWAONYESHE BABA YAKE!!!
“Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?” (Yoh 14:9)
Yesu anamjibu Filipo aliyemtaka awaonyesshe Baba hivi;
>>MIMI NIMEKUWAPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE HIZI WEWE USINIJUE, FILIPO?
-Yesu (Baba kwenye mwili) anamshangaa Filipo kwa kuuliza lile swali.
-Lakini pia anamshangaa kwamba amekuwa na Baba siku nyingi lakini bado hamjui??!!
Ndipo Yesu akamfunulia waziwazi:
>>ALIYENIONA MIMI AMEMUONA BABA!!!
>>BASI WEWE WASEMAJE TUONYESHE BABA??!!
Filipo na wanafunzi wote wa Yesu walikuwa wanaishi, wanakula na kunywa, na wanatembea na Baba lakini bado hawakumjua !!!
Baba ni Roho (Yoh 4:24), Baba ni Neno ( Yoh 1:1), na Baba amemzaa Neno kwenye mwili wa Bikira Mariamu (Luka 1:35, Yoh 1:14)
Roho Mtakatifu aliponena ndani ya Yesu ni Baba alikuwa akinena!!
“Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (Lk 1:34-35)
>>NITAZAAJE NA MIMI SIJUI MUME?!
>>UTAPOKEA MIMBA KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU
-[Mimba ya Yesu = (Roho Mtakatifu + Nguvu zake) + Neno lake] juu ya Mariamu kama kivuli
-Kitakachozaliwa ni Kitakatifu, Mwana wa Mungu
>> VITAKATIFU VINAZALIWA MAISHANI MWETU KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KUPITIA IMANI KATIKA NENO LAKE
>> WANA WA MUNGU TUNAMZALIA MUNGU MATUNDA KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KWA KUPITIA IMANI KATIKA NENO LAKE
>>UUNGU WA YESU NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KUPITIA IMANI ILIYO HAI KWA YESU
>>NA UUNGU WETU WANA WA MUNGU AMBAO NI miungu KWENYE MWILI NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KUPITIA IMANI ILIYO HAI KWA NENO LA KRISTO
“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet 1:3-4)
Sisi wana wa Mungu ni washirika wa tabia ya uungu kupitia uweza wake wa uungu na pia ahadi zake (kwenye neno lake) kubwa mno na za thamani kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
>> Baba wa Yesu ni Roho! Yesu ni Neno (Mungu) kwenye mwili!!!
>> Akiwa kwenye mwili Neno ni Mwana kwa kuwa alizaliwa!!
>> Baba na Mwana ni Roho na Neno lake!!! Baba na Neno ndani yetu ni Roho na Neno lake ndani yetu!! Huu ndio upendo wa Mungu ndani yetu!!!
“Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” (Yoh 14:23)
>>…….NASI (Roho na Neno)TUTAKUJA KWAKE NA KUFANYA MAKAO KWAKE!! Haleluya!!
>>Mimi ni “mungu” katika mwili! Mimi ni mwana wa Mungu niliyezaliwa kwa Neno la Mungu, na ninaishi na kutembea katika utukufu wa wana wa Mungu vilevile kama Yesu Mwana wa Mungu ambaye ni Mungu katika mwili alivyotembea hapa ulimwenguni; na sasa anatembea ndani yangu!!
“6Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” (1 Yoh 2:6)
>>Baba na Mwana (Roho na Neno lake) anakaa ndani yangu!
>>Mimi na Yesu ni mmoja! Mimi na Baba ni mmoja!
Biblia inasema,
“Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili,
Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika,
Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.” (1 Tim 3:16)
>>MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI!!! MUNGU ALIONEKANA KWA MACHO YA DAMU NA NYAMA
>> MUNGU LAZIMA ADHIHIRISHWE NDANI YA MWILI WAKO TENA ILI YOHANA 14:12 ITIMIZWE KUPITIA WEWE!!!
Tunaposema Mungu kwa jinsi ya mwili ni muhimu kujua kwamba kuna Mungu kwa jinsi ya roho!! Kwa kuwa kiasili Mungu, ambaye ni Roho, ni OMNIPRESENT, OMNISCENT, NA OMNIPOTENT! Na neno lake ambaye aliitwa Yesu alipokuwa kwenye mwili ATATIISHWA CHINI YA YEYE ALIYEMTIISHIA VYOTE (ALIYEMPA MAMLAKA YOTE) BAADA YA MAMBO YOTE KUKAMILIKA!!
“Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.”
(1 Kor 15:28)
>> Hii ndiyo maana Yesu alisema,
“Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.” (Yoh 14:28)
>>KULE KUSEMA BABA NI MKUU KULIKO MIMI HAKUONDOI UKWELI KWAMBA MWANA WA MUNGU YESU NI MUNGU KWENYE MWILI
>>BABA AMBAYE NI ROHO NI MKUU KULIKO NENO LAKE, LAKINI BADO YEYE NA NENO LAKE NI MMOJA (Yoh 10:30)
>>KAMA VILE AMBAVYO WEWE NA NENO LAKO NI MMOJA LAKINI WEWE NI MKUU KULIKO NENO LAKO!!
>>KILA ALIPO MWANA, BABA YUPO PIA, KWA MAANA HAWA WAWILI NI MMOJA!
Hivyo Yesu ni Mwana wa Mungu ambaye ni Mungu kwenye mwili, na alipopaa maana yake Neno alirudi kwake yeye aliyemtuma KUJA KUUOKOA NA KUUPONYA ULIMWENGU!
“Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.” (Zab 107:20)
>>MUNGU ALIMTUMA NENO ULIMWENGUNI, SI KUPITIA VINYWA VYA MANABII, BALI KUPITIA MWILI WA MWANADAMU!!
>> MUNGU ALIONA VEMA KUJA KWENYE MWILI ILI ATIMIZE MPANGO WAKE WA UKOMBOZI WA MWANADAMU KAMA ALIVYOKUSUDIA TANGU KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU
>> “yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.” (2 Kor 5:19)
>>MUNGU NDANI YA KRISTO!! BABA NDANI YA YESU!! ROHO NDANI YA NENO!!! BABA NA MWANA!!!
“20NASI TWAJUA KWAMBA MWANA WA MUNGU AMEKWISHA KUJA, NAYE AMETUPA AKILI KWAMBA TUMJUE YEYE ALIYE WA KWELI, NASI TUMO NDANI YAKE YEYE ALIYE WA KWELI, YAANI, NDANI YA MWANA WAKE YESU KRISTO. HUYU NDIYE MUNGU WA KWELI, NA UZIMA WA MILELE.” (1 YOHANA 5:20)