MIMI (YAWEZA KUWA WEWE PIA NA ZAIDI UKIAMINI)
1) NI MTENDAJI WA NENO SIKUZOTE (DOER OF THE WORD)-[Yakobo 1:22-25]
2) NI MTAKATIFU KATIKA MWENENDO WANGU WOTE KAMA YEYE ALIYENIITA ALIVYO MTAKATIFU (1 Petro 1:15)
3) NI MTAKATIFU NISIYE NA HATIA MBELE ZA MUNGU KATIKA PENDO (Efeso 1:3)
4) NINAISHI NA KUENENDA KWA ROHO SIKUZOTE NA WALA SIZITIMIZI KAMWE TAMAA ZA MWILI ( Wagalatia 5:16)
5) NINAISHI NA KUENENDA, NIKIONGOZWA NA ROHO (Wagalatia 5:25, Warumi 8:14)
6) MAISHA YANGU YOTE NI KWA AJILI YA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU (Mathayo 7:21)
7) MUNGU ALIYENITUMA HANIACHI PEKE YANGU MAANA SIKUZOTE NAYAFANYA YALE YAMPENDEZAYO YEYE (Yohana 8:29) SIKUZOTE NINAISHI NA KUENENDA KATIKA UWEPO WAKE NA NGUVU ZAKE NDANI YA YESU KRISTO BWANA WETU.
8) MUNGU AMENITIA MAFUTA KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU NAMI NINAZUNGUKA HUKU NA HUKO NIKITENDA KAZI NJEMA NA KUPONYA WOTE WALIOONEWA NA IBILISI, MAANA MUNGU YU PAMOJA NAMI (Matendo 10:34)
9) ISHARA HIZI ZINAAMBATANA NAMI KWA KUWA NAAMINI: KWA JINA LA YESU NINATOA PEPO, NINASEMA KWA LUGHA MPYA, NINASHIKA NYOKA, HATA NIKINYWA KITU CHA KUFISHA HAKINIDHURU, NA NINAWEKA MIKONO YANGU JUU YA WAGONJWA NAO WANAPATA AFYA (Marko16:17-18)
10) NAMI SIKUZOTE NINATOKA NA KUHUBIRI KOTEKOTE, BWANA AKITENDA KAZI PAMOJA NAMI, NA KULITHIBITISHA LILE NENO KWA ISHARA ZINAZOFUATANA NALO (Marko 16:20)
11) NA NENO LANGU NA KUHUBIRI KWANGU SI KWA MANENO YA HEKIMA YENYE KUSHAWISHI AKILI ZA WATU, BALI NI KWA DALILI ZA ROHO NA NGUVU, HIVYO IMANI ZA WATU HAZIWI KATIKA HEKIMA YA BINADAMU BALI KATIKA NGUVU ZA MUNGU (1 Wakorintho 2:4-5)
12) INJILI YANGU HAIWAFIKII WATU KWA MANENO TU BALI KATIKA ROHO MTAKATIFU, NA NGUVU, NA UTHIBITIFU MWINGI (1 Wathesalonike 1:5)
13) NINAHUBIRI INJILI KOTEKOTE KWA NGUVU ZA ISHARA NA MAAJABU, KATIKA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, NA WOTE KILA MAHALI WANATII KWA NENO NA TENDO; NIKIHUBIRI ZAIDI KULE AMBAKO JINA LA YESU HALIJATAJWA KIKAMILIFU. (Warumi 15:19-20)
14) SIWEZI KUFANYA NENO LOLOTE KINYUME CHA KWELI BALI KWA AJILI YA KWELI MAISHA YANGU YOTE ( 2 Wakorintho 13:8)
15) NIMESULUBIWA PAMOJA NA KRISTO LAKINI NI HAI, WALA SI MIMI TENA NINAYEISHI, BALI KRISTO YU HAI NDANI YANGU; NA UHAI NILIO NAO KATIKA MWILI NINAISHI KWA IMANI YA MWANA WA MUNGU AMBAYE ALINIPENDA AKAJITOA NAFSI YAKE KWA AJILI YANGU (Wagalatia 2:20)
16) KATIKA MAISHA YANGU YOTE NINAYAWAZA YALIYO JUU WALA SI YALIYO KATIKA NCHI; NINAYATAFUTA YALIYO JUU, KRISTO ALIKO AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU, KWA MAANA NILIKUFA NA UHAI WANGU UMEFICHWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA MUNGU, KRISTO ALIYE UHAI WANGU ATAKAPOFUNULIWA NDIPO NA MIMI NITAKAPOFUNULIWA PAMOJA NAYE (Wakolosai 3:1-4)
17) MIMI NI NURU YA ULIMWENGU NA CHUMVI YA DUNIA (Mathayo 5:13-14)
18) MIMI NINAISHI KWA AJILI YA YESU TU PEKE YAKE, MAANA ALIKUFA KWA AJILI YANGU ILI NIISHI MAISHA YANGU KWA AJILI YAKE TU (2 Kor 5:15)
19)MIMI NINAISHI NIKIWA NI MALI YAKE YESU, NA NIKIFA PIA NI MALI YAKE, NDIYO MAANA NINAISHI KWA AJILI YAKE (Rumi 14:7-9)
20) MIMI NIMEUNGWA NA BWANA NA NI ROHO MOJA NAYE (1 Kor 6:17), YAANI MIMI NI MMOJA NA YESU (Yohana 15:1-6)
21) MIMI NINAKAA NDANI YA YESU, NA MANENO YAKE YESU YANAKAA NDANI YANGU, HIVYO LOLOTE NINALOLIOMBA NINATENDEWA (Yohana 15:7)
22) NINAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU (Flp 4:13) MAANA YOTE NIYAFANYAYO KATIKA MAISHA YANGU YOTE SI KWA UWEZO WANGU WALA NGUVU ZANGU BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU (Zech 4:6)
23) NINAMCHA BWANA KWA HIYO NINACHUKIA UOVU, KIBURI, MAJIVUNO NA NJIA ZOTE MBOVU; NA KINYWA CHA UKAIDI PIA NAKICHUKIA (MITHALI 8:13)
24) KWA KUPIGWA KWAKE YESU MIMI NIMEPONA, NI MZIMA, SIUMWI (Isa 53:5, 1 Pet 2:24)
25) BWANA YESU ALIUCHUKUA UDHAIFU WANGU, AKAYACHUKUA MAGONJWA YANGU NA KUYABEBA MAUMIVU YANGU (Math 8:14-17) HIVYO SIUMWI NA SINA MPANGO WA KUUMWA WALA KUUGUA.
26) YESU ANAISHI NDANI YANGU NA NDANI YA FAMILIA YANGU, NA SISI NDANI YAKE! SISI NI SAYUNI, NYUMBANI KWA MUNGU ALIYE HAI, AMBAKO HAKUNA ASEMAYE MIMI MGONJWA AU MIMI NINAUMWA, KWA KUWA TUMESAMEHEWA MAOVU YETU (Isa 33:24 & Zab 103:3)
27) MIMI NI KICHWA NA SIYO MKIA, NIKO JUU TU WALA SIYO CHINI KWA KUWA NINAMSIKILIZA BWANA MUNGU WANGU NA KUYATII MAAGIZO YAKE YOTE (Kumb 28:13)
28)NIMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO YESU (Efeso 1:3)
29) KWA KUWA BARAKA YA BWANA HUTAJIRISHA NA WALA HACHANGANYI HUZUNI/MATATIZO PAMOJA NAYO (MITHALI 10:22), NDIPOSA MUNGU WANGU AMENITAJIRISHA KWA UTAJIRI WOTE WA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE YESU KRISTO (Efe 1:3 + Mith 10:22)
30) NINA UTAJIRI USIOPIMIKA WA YESU KRISTO ( Efe 3:8)
31) KWA KUWA NINAMCHA BWANA MUNGU WANGU, NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE SIKUZOTE,
-wazao wangu wa kiroho na kimwili ni hodari duniani
-wazao wangu ni wenye adili na wamebarikiwa
-NYUMBANI MWANGU MNA MALI NA UTAJIRI (Zab 112:1-3)
32) KWA KUWA NINAMCHA MUNGU KUHITAJI KOTE KUMEISHA MAISHANI MWANGU, YAANI, SIHITAJI CHOCHOTE (Zab 34:9-10)
33)PENDO LA MUNGU BABA, NEEMA YA BWANA YESU KRISTO NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU VIKO NAMI NA NYUMBA YANGU SIKUZOTE! (2 Kor 13:14)
34) PENDO LAKE MUNGU BABA LINAZIDI KUWA JINGI SANA NDANI YANGU KATIKA HEKIMA NA UFAHAMU WOTE, NIMEYAKUBALI YALIYO MEMA, NINAZIDI KUWA NA MOYO SAFI PASIPO LAWAMA MPAKA SIKU YA KRISTO, HALI NIMEJAZWA MATUNDA YA HAKI KWA NJIA YA YESU KRISTO (Flp 1:9-11)
35) MUNGU AMENIPA ROHO YA HEKIMA, NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE; MACHO YA MOYO WANGU YANAZIDI KUTIWA NURU ILI NIPATE KUJUA TUMAINI LA WITO WAKE JINSI LILIVYO; NA UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE KATIKA WATAKATIFU JINSI ULIVYO; NA UBORA WA UKUU WA UWEZA WAKE NDANI YETU TUAMINIO JINSI ULIVYO; KWA KADIRI YA UTENDAJI WA NGUVU ZA UWEZA WAKE, ALIOTENDA KATIKA KRISTO ALIPOMFUFUA KATIKA WAFU, NA KUMWEKA MKONO WAKE WA KUUME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, JUU SANA KULIKO UFALME WOTE, MAMLAKA, USULTANI NA NGUVU NA KILA JINA LITAJWALO, WALA SI KATIKA ULIMWENGU HUU TU BALI NA KATIKA ULE UJAO PIA; AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, AKAMWEKA AWE KICHWA JUU YA VITU VYOTE, KWA AJILI YA KANISA, AMBALO NDILO MWILI WAKE, UKAMILIFU WAKE YEYE ANAYEKAMILIKA KWA VYOTE KATIKA VYOTE. (Waefeso 1:17-23)
36)MAMBO YOTE YA FAMILIA YETU NA KANISA LETU YANATENDEKA KATIKA UPENDO; MAMBO YANGU YOTE NINAYATENDA KWA UPENDO (1 KOR 16:14)
37)MUNGU WANGU AMENIJALIA, KWA KADIRI YA UTAJIRI WA UTUKUFU WAKE, KUFANYWA IMARA KWA NGUVU KWA KAZI YA ROHO WAKE KATIKA UTU WA NDANI; KRISTO ANAKAA MOYONI MWANGU KWA IMANI, NIKIWA NA SHINA NA MSINGI KATIKA UPENDO; NA NINAZIDI KUFAHAMU PAMOJA NA WATAKATIFU WOTE JINSI ULIVYO UPANA, NA UREFU, NA KIMO, NA KINA, NA KUUJUA UPENDO WAKE MUNGU, UPITAO UFAHAMU KWA JINSI ULIVYO MWINGI (Efe 3:16-19)
38) ALIYE NDANI YANGU NI MKUU KULIKO ALIYE KATIKA DUNIA HII (1 Yoh 4:4)
39) MIMI NIMEOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YANGU (MDO 16:31-33), NA TUNAMZALIA MUNGU MATUNDA YAPASAYO TOBA (Luka 3:8-9)
40) MUNGU AMENIINUA JUU KUTOKA MAVUMBINI KWENYE UNYONGE, NA KUNIPANDISHA KUTOKA JALALANI KWENYE UHITAJI, NAYE AMENIKETISHA JUU PAMOJA NA WAKUU (1 SAM 2:8)
.
.
.
.
.
100)MIMI NI BIKIRA SAFI WA KRISTO (2 KOR 11:2), NA MKEWE MWANAKONDOO, NIMEJIWEKA TAYARI KWA AJILI YA KARAMU YA HARUSI YA MWANAKONDOO (UFU 19:7-9) [TAYARI KWA UNYAKUO]
HEBU JAZA 41-99 ILI UJIONE, UJIJUE, UJIFAHAMU, UJIELEWE NA UJITAMBUE VILE MUNGU:
-ANAVYOKUONA
-ANAVYOKUTAZAMA
-ALIVYOKUKIRIMIA
-ALIVYOKUFANYIA
-ALIVYOKUFANYA/ALIVYOKUTENGENEZA
-ALIVYOKUUMBA
-ALIVYOKUKUSUDIA
-ANAVYOKUTARAJIA
-ANAVYOKULINDA, ANAVYOKUONGOZA, ANAVYOKUPIGANIA, ANAVYOKUTETEA, ANAVYOKUWEZESHA, ANAVYOKUTENDEA MEMA, ANAVYOKUJALI, ANAVYOKUPENDA,
- MIUJIZA, ISHARA NA MAAJABU ALIYOKUTENDEA NA ANAYOKUSUDIA KUITENDA KUPITIA WEWE
-MALENGO YAKE, MAKUSUDI YAKE, MIPANGO YAKE, NIA YAKE NA MAPENZI YAKE KWAKO! TUSHIRIKI BARAKA HIZI ZA AJABU AMBAZO ZINAPATIKANA KWA YESU PALE UNAPOMWAMINI NA KUDUMU KATIKA IMANI HIYI; NA HAKI YA MUNGU IKIZIDI KUDHIHIRIKA NDANI YAKO TOKA IMANI HATA IMANI (RUM 1:16) KADIRI YA NGUVU ZA MUNGU!
UBARIKIWE NA BWANA