MAENEO SABA YA BARAKA ZA UPENDO (MUNGU)

 Ephesians 1:3 Inspirational Image

MAENEO SABA YA BARAKA ZA UPENDO (MUNGU)-SEVEN-FOLD BLESSINGS OF LOVE(GOD)

Mungu ametubariki katika maeneo haya saba ili na sisi tuwe baraka kwa wengine katika maeneo hayo hayo kwa wengine;

 1. AMETUBARIKI KIROHO ILI SISI NASI TUWE BARAKA KIROHO KWA WENGINE (we are blessed spiritually so that we can be a blessing unto others spiritually) [SPIRITUAL BLESSINGS]

2. AMETUBARIKI KIAKILI ILI NA SISI TUWE BARAKA KWA WENGINE KIAKILI PIA (we are blessed mentally so that we can be a blessing to others mentally) [MENTAL BLESSINGS]

3. AMETUBARIKI KIHISIA ILI NA SISI TUWE BARAKA KWA WENGINE KIHISIA (we are blessed emotionally so that we, too, can be a blessing unto others emotionally) [EMOTIONAL BLESSINGS]

4. AMETUBARIKI KIMWILI ILI NA SISI TUWE BARAKA KWA WENGINE KIMWILI (we are blessed physically so that we, too, may be a blessing unto others physically) [PHYSICAL BLESSINGS]

5. AMETUBARIKI KIFEDHA ILI NA SISI TUWE BARAKA KWA WENGINE KIFEDHA (we are blessed financially so that we, also, may become a blessing unto others financially) [FINANCIAL BLESSINGS]

6. AMETUBARIKI KWA VITU NA MALI ILI NA SISI TUPATE KUWA BARAKA KWA WENGINE KWA MALI NA VITU (we are blessed materially so that we, too, can be a blessing unto others materially) [MATERIAL BLESSINGS]

7. AMETUBARIKI KIJAMII ILI NA SISI TUWE BARAKA KWA WENGINE KATIKA JAMII (we are blessed socially so that we, also, may be a blessing unto others socially) [SOCIAL BLESSINGS]

 

1. BARAKA ZA KIROHO (SPIRITUAL BLESSINGS)

“3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;” (Efe 1:3)

>>Kwa wewe uliyeokoka, unayeishi kwa imani iliyo hai ya Yesu Kristo, imani itendayo kazi kwa upendo, uliye ndani ya Yesu, andiko linasema UMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YA KRISTO YESU BWANA WETU.

Yesu ni Neno la Mungu aliyefanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli! ((Yoh 1:14) Biblia inasema,

“1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.”

(Yoh 1:1-2)

NENO NI MUNGU!  YESU NI NENO LA MUNGU KATIKA MWILI! Hii inamaanisha Mungu aliamua kuja kwenye mwili kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu wote!

Baraka ya Mungu kwa ulimwengu wote ni Yesu!! Neno la Mungu Aliye Hai leo! Biblia inasema,

MUNGU NI ROHO (Yoh 4:24). Yaani, asili yake ni Roho! Umbile lake ni Roho! Yeye hana mwili kama wa mwanadamu, wala haonekani kwa milango mitano ya fahamu ya mwanadamu. Ila Mungu aliye Roho anaweza kuvaa mwili kama alivyofanya alipokuja duniani akaitwa Yesu. (1 Tim 3:16) Hivyo tunasema Mungu ameubariki ulimwengu kwa Neno lake! Na kwa kuwa Mungu ni Roho tunaweza kusema Roho ameubariki ulimwengu kwa Neno la Kristo! Hivyo tunapoongelea baraka za Mungu lazima tuanzie kwenye Roho wa Mungu na Neno lake lenye Uzima! Ndiposa twasema,

[BARAKA ZA MUNGU KWA ULIMWENGU = ROHO WAKE + NENO LAKE]

Biblia inasema, “63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” (Yoh 6:63) [New King James Version (John 6:63)
It is the Spirit who gives life; the flesh profits nothing. The words that I speak to you are spirit, and they are life.]

Roho (Mungu) ndiye chanzo cha maisha (uhai wote)! Biblia ya Kiswahili imetafsiri neno “life” kuwa ni “uzima” ambao ni “uhai” ama “maisha.”

Neno la Kristo ni roho! Neno la Kristo pia ni uzima/uhai/maisha! Hivyo uzima au uhai au maisha yamo kwenye “roho.” Lakini hii ni roho ya neno au kama Biblia isemavyo roho ya andiko!!

“6Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.” (2 Kor 3:6)

Andiko halisaidii kitu peke yake mpaka pale andiko hili litakapokuwa “roho” ndani ya mwanadamu. Inajulikana kwamba mwanadamu mtenda dhambi hana uhusiano na Mungu aliye Roho. Hii ndiyo maana ni lazima kuzaliwa mara ya pili “roho” yako kama maandiko yasemavyo;

“5Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” (Yoh 3:5-6)

>>Kuzaliwa mara ya pili roho yako ni kuokoka!! Yaani, kuhuishwa na kufanywa upya na Roho Mtakatifu!  “4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, ALITUOKOA; 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;” (Tit 3:4-5)

>> roho za waaminio (believers) zimezaliwa upya kwa Roho Mtakatifu kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho huyo.

>>Huku kufanywa upya roho yako ni kule kupewa moyo mpya na roho mpya kunakoelezwa katika maandiko

“25Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. 26Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.” (Eze 36:25-26)

>>Unapoamua kumpokea Yesu moyoni (rohoni) mwako awe Bwana na Mwokozi wako unaoshwa kwa kunyunyiziwa maji safi ya Neno lake na kuoshwa uchafu wako wote, sanamu na vinyago vyako vyote, na kisha roho yako kuhuishwa na kufanywa upya (regenerated and renewed) na hivyo wewe kuwa na roho mpya au moyo mpya. Ule moyo mgumu wa jiwe usiomwamini Mungu wala kumkubali, moyo ule usio na toba na uliojaa kiburi, ubishi, ukaidi, jeuri, dharau, majivuno, hasira, ghadhabu, uchungu, chuki, uadui, ugomvi, na kila tendo baya unakuwa umeondolewa ndani yako! Sasa hivi unakuwa umeumbiwa moyo safi wa nyama, kwa maana ya moyo wenye unyenyekevu, kicho, na upole; na wenye kumwamini na kumtumaini Mungu. BADILIKO LA MOYO LIMETOKEA LENYE KUKUPA MOYO MPYA NA ROHO MPYA NA KUKUFANYA WEWE UWE KIUMBE KIPYA NDANI YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WA DUNIA YOTE (2 KOR 5:17)

KIUMBE KIPYA = MOYO MPYA + ROHO MPYA

Baada ya hapa kinachofuata ni hiki anenacho nabii;

“27Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda” (Eze 36:27)

>>Mungu anaposema nitatia “roho yangu” ndani yenu anaongelea Roho wake Mtakatifu! Huu ni ujazo wa Roho Mtakatifu ambapo linatimia andiko la 1 Kor 6:17, “17Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.”

>>Hii maana yake umeunganishwa na Bwana Yesu katika roho. Yaani, roho yako imeunganishwa na Roho Mtakatifu na wewe sasa umekuwa roho moja na Bwana Yesu. Kuwa roho moja na Bwana maana yake ni kuwa mmoja naye! Wewe sasa ni mmoja na Bwana! (one with the Lord)

>>HII NDIYO BARAKA KUU KULIKO ZOTE ANAZOWEZA MWANADAMU KUZIPATA

Kwa sababu roho moja na Bwana au kuwa mmoja na Bwana maana yake:

▪ roho yako sasa imeunganika na Roho wa Kristo, ambaye ndiye Roho wa Mungu

▪ wewe sasa umeunganika na Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo na kuwa mmoja naye (roho moja naye)

▪ wewe sasa umeunganika na Kristo Yesu na kuwa mmoja naye (one with the Lord Jesus!)

▪ wewe sasa umeunganika na Neno la Mungu na kuwa mmoja nalo (one with the Word)

▪ wewe sasa umeunganika na Roho wa Neno na kuwa mmoja na Neno, na pia na Roho huyo!

Biblia inasema, “4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.” (Yoh 1:4), Kwa hiyo,

▪ wewe sasa umeunganika na Uzima wa Neno kwa kuunganika na Roho wa Neno ambaye ndiye atiaye Uzima kama tulivyosoma kwenye Yohana 6:63 kwamba, “63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

Hii ina maana wewe sasa unafaidika na andiko kwa maana linakuwa “roho” kwako na kukupa uzima wa andiko, uhai wa andiko, au maisha ya andiko moja kwa moja kwenye roho yako.

Hii maana yake ni hii;

1. roho yako inapokea roho ya andiko lolote uliloliamini baada ya kulisikia au kulisoma.Nabii Ezekieli alisema hivi; “2Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami.” (Eze 2:2) Yaani, unaposikia Neno lililonenwa kwa Roho Mtakatifu au ulisomapo kwa Roho Mtakatifu, na kuliamini, na kulipokea kama Neno la Mungu “roho” ya hilo neno inakuingia rohoni mwako! Hivyo roho yako inakuwa imejazwa roho ya andiko/neno uliloliamini! Neno huwa linakaa moyoni kama “roho” unapoliamini!

[UJAZO ENDELEVU WA ROHO MTAKATIFU = (ROHO YAKO + ROHO YA ANDIKO ULILOLIAMINI) MOYONI MWAKO ]

>>Hii ina maana roho yako inazidi kushiba chakula cha uzima ambacho ni mwili wa Yesu. Yaani, unazidi kuula mwili wa Yesu! Yesu ambauye ni Roho anayehuisha (Life-giving Spirit) [1 Kor 15:45] anazidi kukujaza “roho” kwenye roho yako kwa Roho Mtakatifu.

Roho anakujaza roho yako kwa roho ya neno/andiko kwa kuwa umeliamini na kulipokea neno moyoni (rohoni) mwako kama andiko linavyoagiza;

“21Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.” (Yak 1:21)

>>Lile neno linakuwa limepandwa ndani ya roho yako! Biblia inaposema moyo wako huwa inamaanisha roho yako! Na hivi ndivyo linavyotimia lile andiko la Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu......! (Kol 3:16). Neno linakaa kama roho na wewe kuwa na uzima, uhai, au maisha ya hiyo roho na hilo andiko/neno lake.

>>Neno hilo ndilo linalokusafisha na kukuondolea uchafu wote na ubaya wa roho yako. Huu ndio utakaso wa roho yako! Unaitakasa roho yako kwa kuamini na kulipokea rohoni mwako lile neno ambalo umeliamini, umelikubali, unajua kwamba ni neno la Mungu, na kisha umeliweka moyoni mwako. Daudi alisema, “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.” (Zab 119:11). Na Paulo ndani akikumbuka andiko hili anaandika kwa Roho Mtakatifu;

“16Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” (Kol 3:16)

>>Neno la Kristo linapokaa kwa wingi ndani yako yako kwanza linakufanya ufanane na Neno hilo rohoni mwako! Kumbuka Yesu ni Neno Aliye Hai ndani yako! Kila roho ya andiko ni Yesu! Kila Neno lenye uzima ni Yesu! Kila andiko lina pumzi ya Mungu ambayo ni ya Yesu kwa maana Yeye ndiye Roho atiaye uzima, au Roho wa Uzima ndani yako. Kujaa Neno rohoni mwako ni kujaa Yesu!! Na hivyo Yesu kuzidi kuumbika ndani yako!! Kadiri Yesu anavyozidi kuumbika ndani yako ndivyo unavyozidi kujaa Yesu. Mfano;

>>unapojaa Neno la msamaha huko ni kujaa roho ya msamaha; na kadiri unavyojaa roho ya msamaha maana yake unajaa msamaha kama Yesu alivyojaa msamaha. Hivyo na wewe utakuwa unasamehe kama Yesu kwa nguvu za roho hiyo ya msamaha.

>>Ukijaa Neno la utoaji maana yake unajaa roho ya utoaji ambayo itakuwezesha na kukuongoza kutoa kama anavyotoa Yesu kwa nguvu za roho hiyo ya utoaji n.k.

Kumbuka wewe mwanadamu ni roho na una nafsi , na unakaa ndani ya mwili. Hivyo kadiri unavyojaa roho ya Neno maana yake unazidi kubadilika na kufanana na Yesu kutoka utukufu hadi utukufu, na haki ya Mungu inazidi kudhihirishwa ndani yako toka imani hadi imani. (Rum 1:17 & 2 Kor 3:18). Na pia ndivyo unavyozidi kuendelea toka nguvu hadi nguvu (Zab 84:7). Unapobadilika maana yake badiliko hilo ni la kiroho! (your spirituality or spiritual constitution changes and you attain to Christ-likeness more and more).

Biblia inasema kwamba , “12Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” (Ebr 4:12)

• Unapozidi kujaa Neno unazidi kujaa Uzima wa Neno ama Uhai wa Neno au Maisha yaliyomo kwenye hilo neno uliloliamini.

Nisisitize hapa kwamba Neno lililojaa kichwani halafu halimo moyoni maana yake haujaliamini na halina uzima wowote, na linakaa kama andiko tu. Kwa hiyo bado unakaa mautini tu kwa maana ya kukosa kuwa na roho ya neno na uzima wa neno. Kwa maana Roho ndiye atiaye Uzima na Neno la Kristo ni roho na tena ni uzima. (Yoh 6:63) Unaweza kusoma Biblia kila siku kwa miaka 1000 lakini kama hukuokoka kwa kuzaliwa mara ya pili kwa Roho Mtakatifu Neno la Mungu halina manufaa yoyote kwako! Na badala yake litakujaza kiburi cha kujua tu maandiko yaliyo kichwani mwako kama “letter” yaani, maandishi tu ya Biblia yamejaa kichwani mwako kwa kuyakariri. Yesu aliwaambia Wayahudi,

“38Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye. 39Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. 40Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. 41Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. 42Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.” (Yoh 5:39-42)

>>Hawakuwa na Neno lake ndani yao kwa kuwa hawakumwamini Yeye! Huwezi kuwa na Neno moyoni (rohoni) mwako mpaka umwamini Yesu na kuokoka! Maana hapo sasa utakuwa na roho inayoamini na inayoweza kulipokea neno la Kristo ambalo ni takatifu sana ndani yako.

>>Walikuwa wanajitaabisha bure kuyachunguza maandiko ambayo yalikuwa yote yanamshuhudia Yesu, lakini hawakuwa na mioyo ya kuelewa kilichoandikwa maana walikuwa bado hawamwamini na hawataki kuokoka na walikuwa wameng’ang’ania dini yao ya Uyahudi. Dini yoyote isiyoleta wokovu, na utakatifu, na badiliko la moyo, na hivyo badiliko la maisha kabisa, na kumfanya mwanadamu kuachana kabisa na dhambi, na dunia hii, na kumgeukia Mungu, na kumwabudu katika roho na kweli, na kumtumikia, HIYO NI DINI YA SHETANI! Yesu alileta dini ya wokovu, utakatifu, hofu ya Mungu, maisha ya utakaso, kumtumikia Mungu, kujazwa, kuongozwa, na kutawaliwa na Roho Mtakatifu, na kuyafanya mapenzi ya Mungu sikuzote sawasawa na Neno lake, pamoja na kuishi kwa ajili yake Yesu na Ufalme wake wa milele. Nje ya hapo kuna kujiunga na kikundi cha shetani na raia wa jehanamu wanaoyafanya mapenzi ya Baba yao ibilisi, shetani, au yule nyoka wa zamani. (Yoh 8:44) Haijalishi kama wanalijaza Neno vichwani mwao na kulifundisha na kulihubiri. Yote hii inaitwa huduma na/au utumishi wa mauti!!! Nini??!! Unalitaja jina la Yesu halafu unaishi na kuenenda kwenye dhambi? Hukusoma? Kuwa kila alitajaye jina la Yesu na auache uovu??!! (2 Tim 2:19)

• Kadiri unavyozidi kujaa neno rohoni mwako Neno hilo linazidi kukuongeza nguvu za kiroho. Maana Neno li hai, na tena LINA NGUVU!

Mara kadhaa mitume walisemwa kuwa wamejaa Imani na Roho Mtakatifu! (Mdo 6:5 & Mdo 11:24) au Roho Mtakatifu tu ( Mdo 4:8, 7:55, 13:9, n.k.). Hii inamaanisha walikuwa wamejaa Neno waliloliamini mioyoni mwao!

Ukijaa Neno uliloliamini unakuwa umejaa Roho ya hilo Neno na nguvu zake. (Mdo 1:8)

Kujaa Imani = Kujaa Roho ya Neno Uliloliamini

Kujaa Roho wa Neno = Kujaa nguvu za huyo Roho

Hivyo; Kujaa Imani =Kujaa [Roho wa Neno + Nguvu zake]

[UDHIHIRISHO WA ROHO = UJAZO WA ROHO + UJAZO WA NENO ULILOLIAMINI + UJAZO WA NGUVU ZA HILO NENO]

UDHIRISHO WA ROHO= [ROHO +IMANI +NGUVU] ZA NENO!!

[IMANI ={ roho yako +Roho Mtakatifu} + roho ya neno ndani yako]

Tukipanga haya vizuri tunapata,

[IMANI = (Roho Mtakatifu + roho yako) + roho ya neno uliloliamini moyoni mwako]

Hivyo tukiipanga vema hesabu hii ya kimaandiko tunapata;

Udhihirisho wa Roho = [(Roho Mtakatifu + roho yako) + roho ya andiko + nguvu za hilo andiko/Neno] ndani yako

>>Wewe uliyeungwa na Bwana na kuwa roho moja naye ={ Roho + roho}, hivyo;

[UDHIRISHO WA ROHO = WEWE + ROHO YA ANDIKO ULILOLIAMINI + NGUVU ZA HILO ANDIKO] NDANI YAKO

Hiki ndicho kinachotokea unapoamini Neno la Mungu na kulitenda! Utukufu wa Mungu unadhihirika pale,

1. Unapoamini Neno

2. Ukalitendea kazi (kulisema, kulihubiri, kulifundisha, kuomba kwa hilo neno, kuhudumia mhitaji kwa hilo neno, kufanya lisemavyo n.k)

3. Roho Mtakatifu akakujalia au kukuwezesha kufanya kama Neno lisemavyo na kudhihirisha matokeo yaliyosemwa kwenye hilo Neno. Kama ni kuweka mikono juu ya mgonjwa kwa jina la Yesu, basi Roho humpa afya huyo mgonjwa kwa nguvu zake ambazo ndizo nguvu za Neno. Kama ni kutoa pepo, kwa mfano, wewe unaamuru kwa jina la Yesu, na Roho analifanya hilo kwa nguvu zake (Mt 12:28). Sikuzote lazima pawepo haya matano ili utukufu wa Mungu uonekane;

1) Roho Mtakatifu

2) roho yako iliyoungwa naye na kuwa roho moja naye (Bwana Yesu)

3) Neno la Mungu uliloliamini ambalo,

4) Limekuwa roho na uzima ndani yako wewe

5) Na hivyo nguvu za Mungu, aliye Roho, zinatenda kazi kulidhihirisha lile uliloliamini, ambayo ndiyo maisha ya hilo neno/andiko

Kwenye hiyo Waebrania 4:12 nimeongelea mambo mawili tu; a) Neno li Hai, na b) Neno lina Nguvu. Hayo mengine yatafakari wewe mwenyewe ili uone matokeo ya kuamini kwako Neno na kuliweka moyoni mwako kwa wingi. Nayo ni haya;

c) Lina ukali kuliko upanga wowote ukatao kuwili (huu utakuwa kinywani mwako ukiamini)

d) Tena li jepesi hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake (huyu ni wewe uliyejaa imani)

e) Tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya mioyo (neno linafunua siri za mioyo)

f) Wala hakuna kiumbe chochote kisichokuwa wazi mbele zake (neno linajua siri zote, na mambo yote, na vitu vyote)  [Ebr 4:13]

g) Lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.(vitu vyote viko wazi/utupu mbele za neno) (Ebr 4:13)

>>Haya ni matokeo saba ya Neno Kujaa kwa wingi ndani yako!!! Neno lililochanganyika na imani ndani yako wewe uliyelisikia. (Ebr 4:2)

>>Yaani, huyu ndiye wewe uliyejaa Roho Mtakatifu na Imani; na haya ndiyo madhihirisho saba (sevenfold manifestations) ya Roho Mtakatifu ndani yako wewe na pia kupitia wewe! Amini! Tendea kazi Neno! Ishi kwenye Neno! Tembea kwenye Neno! Fikiri Neno! Kiri Neno! Tafakari Neno! Tamka Neno! Amuru kwa Neno! Kemea kwa Neno! Shauri kwa Neno! Fundisha Neno lisiloghoshiwa! Hubiri Kweli yote! Fanya yoye ukiwa na shina na msingi kwenye Neno! Anzia kwenye Neno na maliza kwenye Neno! Neno ndiyo mamlaka yako ya juu kuliko zote chini ya jua! Ukiacha Neno huwezi kuuona utukufu wa Mungu! Ukiacha Neno huwezi kamwe kumuona Mungu! BARAKA ZOTE ZA MUNGU NDANI YA KRISTO YESU NI BARAKA ZA NENO KUANZIA MWA 1:1 HADI UFU 22:21. Baraka za Neno ni Baraka za Roho wa Neno!!! Lazima uanze na roho ya Neno uliloliamini kabla ya kuja kuona udhihirisho wa Neno na Ahadi za Mungu maishani mwako!

Maisha yako halisi ni yale unayoyaishi kwa Neno la Mungu! Maana Yesu alisema, “4Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” (Mt 4:4)

>>Mwanadamu hakuumbwa ili aishi kwa MKATE TU! Bali aliumbwa ili,

>>AISHI KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU!!

Biblia inasema, “13Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula……” (1Kor 6:13) Na huu ndio mwisho wa maisha ya mkate! Mungu atalitowesha tumbo na vyakula, vyote viwili! Kama unaishi kwa mkate tu jiandae kutoweshwa pamoja na mwili wa udongo na vyakula vyote vinavyorudi kwenye udongo! Unaishi maisha yenye kuharibika! Kama unachohangaikia ni maisha yanayoharibika tu basi jiandae na wewe mwenyewe kuharibika na kutengwa na Mungu milele yote! Maana tunajua kwamba Yesu aliufunua Uzima na kutoharibika kwa ile injili!!! “10na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; ALIYEBATILI MAUTI, NA KUUFUNUA UZIMA NA KUTOKUHARIBIKA, KWA ILE INJILI;” (2 Tim 1:10) [New King James Version 2 Tim 1:10:
“but has now been revealed by the appearing of our Savior Jesus Christ, WHO HAS ABOLISHED DEATH AND BROUGHT LIFE AND IMMORTALITY TO LIGHT THROUGH THE GOSPEL,”]

>>BWANA WETU YESU AMEBATILISHA MAUTI/AMEIHARIBU MAUTI; KISHA AKAUFUNUA UZIMA (LIFE) NA KUTOHARIBIKA (IMMORTALITY)

>>DEAR BRETHREN, THERE IS A HIGHER REALM OF LIVING! A REALM OF INCORRUPTION! A REALM OF ETERNITY WITH GOD IN ALL HIS GLORY!

>>NDUGU YANGU, CHOCHOTE KINACHOKUWEKA BUSY KWENYE MAISHA HAYA, KINACHOHARIBIKA, HATA UKASAHAU HATIMA YAKO YA MILELE ISIYO NA UHARIBIFU, NI UOVU UTAKAOKUPELEKA MAHALI PABAYA MILELE!

>>NI VEMA UKAMKIMBILIA YESU, AKUPE UZIMA NA KUTOHARIBIKA! MWILI WA UDONGO UNATAKA MKATE TU AMBAO UNAHARIBIKA! KAMA UNAISHI KWA AJILI YA MKATE TU, KAMA UNAHANGAIKIA MKATE TU, KAMA UNASUMBUKA KWA AJILI YA MKATE TU, KAMA UNATAABIKA KWA AJILI YA MKATE TU, WEWE UNAHANGAIKIA HATIMA MBOVU SANA YENYE UHARIBIFU NA MAUTI MILELE!!! DHIKI, SHIDA, TAABU, NA MATESO MILELE MBALI NA MUNGU ALIYE HAI!

>>MUNGU HAKUKUUMBA KWA AJILI YA KUHANGAIKIA NA KUSUMBUKIA MKATE TU!! AMESEMA MWANADAMU ATAISHI KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU!! HUU NDIO UZIMA! HAYA NDIYO MAISHA! HUU NDIO UHAI WA MILELE NDANI YA YESU! MAISHA YASIYO NA MWISHO MILELE! RAHA YA MILELE! UTUKUFU WA MILELE! AMANI MILELE! BARAKA MILELE!

>>MBIO ZOZOTE ZA KUFUKUZIA BARAKA ZINAZOITWA BARAKA ZENYE KUHARIBIKA NI MBIO ZA JEHANAMU MILELE!

>>FANYA KAZI KWA BIDII ZOTE KWA AJILI YA KUMTUMIKIA MUNGU KWA,

 1) VYOTE VILE ULIVYO SIKUZOTE,

2) VYOTE ULIVYONAVYO UNAVYOVIMILIKI,

3) MUDA WOTE ULIOPEWA CHINI YA JUA,

4) NGUVU ZOTE ULIZONAZO CHINI YA JUA,

5) FEDHA ZOTE UNAZOZIPATA CHINI YA JUA,

6) AKILI ZOTE ULIZOJALIWA KUWA NAZO CHINI YA JUA,

7) HISIA ZOTE ULIZOJALIWA CHINI YA JUA,

8) UZOEFU WOTE ULIOUPATA CHINI YA JUA,

9) MALI ZOTE ULIZONAZO CHINI YA JUA,

10) MAHUSIANO YOTE ULIYONAYO CHINI YA JUA,

11) MWILI WAKO WOTE KUTOKA UTOSINI MPAKA CHINI YA NYAYO ZA MIGUU YAKO, 12) UWEZO WOTE ULIONAO CHINI YA JUA!!

13) ELIMU YOTE ULIYONAYO CHINI YA JUA,  N.K.

Unatafuta baraka kwa ajili yako, siyo? Biblia inasema,

1) WEWE SI MALI YAKO WEWE MWENYEWE AMA UKIWA HAI AU UMEKUFA

“7Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. 8Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. 9Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.” (Rum 14:7-9)

>> KAMA KWELI UMEOKOKA , SI TU VITU, PESA, AU CHOCHOTE KINGINE SI MALI YAKO, BALI HATA WEWE MWENYEWE SI MALI YAKO MWENYEWE

>> HIVYO HAURUHUSIWI KUISHI KAMA UTAKAVYO AU UPENDAVYO WEWE MWENYEWE HAPA DUNIANI, BALI KAMA ATAKAVYO NA APENDAVYO NENO (YESU)

>>RAIA WA JEHANAMU HUWA WANAISHI KWA AJILI YAO WENYEWE TU, NAO HUFANYA LOLOTE WALITAKALO BILA KUMFIKIRIA MUNGU HATA KIDOGO!! HUU NI UOVU SIKUZOTE

HAKUNA ALIYE WA YESU, HAKUNA MKRISTO ALIYEOKOKA,  HAKUNA MTOTO WA MUNGU, ANAYERUHUSIWA KUISHI KWA AJILI YAKE MWENYEWE BALI KWA AJILI YA YESU (EXCLUSIVELY FOR JESUS!!!)

2) YESU ALIKUFA AKAFUFUKA ILI WALIO HAI WASIISHI TENA KWA AJILI YAO WENYEWE BALI KWA AJILI YAKE YEYE TU.

“15tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.” (2 Kor 5:15)

>> KAMA KWELI WEWE UMEPOKEA UZIMA NA KUTOHARIBIKA LAZIMA UTAKUWA NA MALENGO YA JUU ZAIDI KULIKO MALENGO YA MAISHA YALE YANAYOHARIBIKA! CHOCHOTE KINACHOHARIBIKA LAZIMA KITUMIKE KWA AJILI YA KUFIKIA LENGO KUU LA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WAKO: KUTENDA MEMA KWA WANADAMU KWA AJILI YA 1) JINA LAKE YESU, 2) NDANI YAKE YESU, 3) PAMOJA NAYE YESU, 4) KWA AJILI YAKE YESU, 5) KWA NJIA YAKE YESU, 6) KWA SIFA ZAKE YESU, 7) KWA SHUKRANI ZAKE YESU, 8) KWA HESHIMA YAKE YESU, NA 9) KWA UTUKUFU WAKE YESU.

Imeandikwa kwamba si wewe unayeishi bali Yesu ndiye anayeishi ndani yako, siyo?

Kama kweli unaamini (if you are a true believer) basi hii ni kweli kwako; kwamba “umesulubiwa pamoja na Kristo; lakini u hai;wala si wewe tena, bali Kristo yu hai ndani yako; na uhai ulio nao sassa kwenye mwili, unao kwa imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alikupenda , akajitoa nafsi yake kwa ajili yako.” (Gal 2:20)

Andiko hili LINAONDOA UBINAFSI WOTE NDANI YAKO! Na linamweka Yesu akiwa ndiye anayeishi ndani yako maana wewe halisi utafunuliwa baadae atakapofunuliwa Yesu!! Kwa sasa maandiko yanasema, (kama kweli umeokoka na unaishi kwa imani ya Yesu) “wewe ulikufa (uliposulubiwa pamoja naye) na uhai wako (maisha yako halisi) umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu; Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wako, ndipo na wewe utakapofunuliwa pamoja naye katika utukufu.” (Kol 3:3-4) Kristo Yesu aliposulubiwa, wote wamwaminio walisulubiwa pamoja naye! Yaani, ule utu wa kale au utu wa dhambi au utu wa zamani au wewe wa zamani, ulisulubiwa na kufa! Ukiamini hili, nguvu ya msalaba inaleta kule kufa ndani yako na kumuumba Yesu ndani yako kupitia Neno la kweli ya Injili katika Roho Mtakatifu ulilolipokea. Wewe wa zamani ulikuwa mbinafsi na mtenda dhambi usiyemtaka wala kumjali Mungu wala wanadamu wengine! Lakini kama sasa umemwamini Mwokozi Yesu na kumpokea kama Bwana na Mwokozi wako HAUISHI TENA KWA AJILI YAKO MWENYEWE! Bali kwa ajili ya Yesu na Ufalme wake! Biblia inasema Yesu alipofufuliwa na wewe ulifufuliwa pamoja naye!!! Na baada ya kufufuliwa pamoja naye kuna maisha mapya ambayo unatakiwa kuyaishi na Mungu amekupa Roho Mtakatifu ili akusaidie na kukuwezesha kuishi hivyo sawasawa na mapenzi yake na kusudi lake!

“1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi” (Kol 3:1)

>>HAYA NDIYO MAISHA YA JUU ALIYOKUSUDIA MUNGU UYAISHI NDANI YA YESU VILE VILE KAMA YESU ALIVYOISHI; Hakuna yeyote asiyeishi kama Yesu ambaye ataingia kwenye ufalme wa Mungu! Maana maandiko yanasema,

“6Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” (1 Yoh 2:6)

>>YEYE ASEMAYE KUWA ANAKAA NDANI YAKE IMEMPASA KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE MWENYEWE YESU ALIVYOENENDA!!

>>Unapoenenda vile vile kama Yesu alivyoenenda ndiposa 1) UTAYATAFUTA YALIYO JUU KRISTO ALIKO, AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU (Kol 3:1), 2) UTAYAFIKIRI YALIYO JUU, SIYO YALIYO KATIKA NCHI.(Kol 3:2)

Na haya yote ni mambo yale yasiyoharibika! Hakuna hata moja hapa la duniani, linaloharibika, au la hapa chini.

>>Neno hili lina maana ikiwa kweli umefufuliwa pamoja na Kristo, baada ya kuusulubisha utu wa kale (ubinadamu wako uliojaa ubinafsi) na kufa, basi UTAWEKA MOYO NA MAWAZO KWENYE MAMBO YALE YA JUU MBINGUNI KRISTO ALIKO AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU! NA MAMBO HAYO ni baraka zako zote za rohoni katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo Yesu (Waefeso 1:3)

>>Isitoshe siyo tu kwamba Kristo amekaa huko mkono wa kuume wa Baba yetu peke yake, bali sisi nasi tuliketishwa pamoja naye mkono wa kuume wa Mungu Baba yetu katika ulimwengu wa roho kwa mujibu wa maandiko;

“6Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;” (Efe 2:6)

>>KUKETISHWA MKONO WA KUUME WA MUNGU MAANA YAKE SISI TU WATENDA KAZI PAMOJA NA MUNGU NDANI YA KRISTO!!

>>MUNGU NDIYE ANAYETENDA KAZI NDANI YETU,  KUTAKA KWETU NA KUTENDA KWETU, KWA KULITIMIZA KUSUDI LAKE JEMA. (Flp 2:13)

Hii mana yake tunaishi kwa kusudi au lengo la Mungu na si kusudi la mwanadamu!! Tunaishi, tunaenenda, na kutenda kazi katika ulimwengu wa roho maana maisha yetu mapya ni ya kiroho ndani yake Yesu! hivyo tunayawaza, na kuyafikiri, na kuyatafuta, na kuyataka, mambo ya kiroho yasiyoharibika na ya milele!

>>ILI HAYA YAWEZEKANE LAZIMA TUUNGANIKE NA YESU NA KUWA MMOJA NA YESU KATIKA ROHO, AMBAYO MAANA YAKE NI HII;

1. Anayetuona sisi anamuona Yesu.

2. Anayetusikia sisi anamsikia Yesu.

3. Anayetutendea sisi anamtendea Yesu.

4. Anayetupokea sisi anampokea Yesu.

5. Anayetukataa sisi anamkataa Yesu.

6. Anayetupinga sisi anampinga Yesu

7. Anayetuamini sisi anamuamini Yesu.

8) Anayetukaribisha sisi, anamkaribisha Yesu,

9) Anayetupuuza sisi anampuuza Yesu,

10) Anayetudharau sisi, anamdharau Yesu,

11) Anayetuheshimu sisi anamheshimu Yesu,

12) Anayetufadhili sisi anamfadhili Yesu,  n.k.

“……..na ye yote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma……” (Lk 9:48)

“ 16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.” (Lk 10:16)

“ 40 Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.” (Mt 10:40)

>>HII ILIWEZEKANA KWA KUWA SI WAO WALIOKUWA WAKIISHI, BALI YESU NDANI YAO!!! (Gal 2:20)

>>HII INAWEZEKANA UNAPOKUWA WEWE NI MMOJA NA YESU (ONE WITH THE LORD JESUS) KATIKA ROHO (1 Kor 6:17)

>>MWENDO HUU UNAANZA PALE UNAPOISHI KWELI KWELI KWA IMANI ITENDAYO KAZI KWA UPENDO (Gal 5:6)

NA JAMBO LA MUHIMU ZAIDI NI HILI:

>>JE! UNATAFUTA NINI NDANI YA YESU KATIKA MAISHA UNAYOYAISHI KWENYE MWILI?

>> JE! LENGO KUU LA MAISHA YAKO NI LIPI? UNA MALENGO YA KIDUNIA, AU YA KIMBINGU?

>>JE! KWA NINI UNAFANYA KAZI KWA BIDII MNO MAISHANI MWAKO?

>>JE! KWENYE MAOMBI YAKO UNAOMBEA ZAIDI NINI? NI KIPI KILIO KIKUU CHA MAISHA YAKO MBELE ZA MUNGU?

>>JE! LENGO LAKO KUU LA KUINGIA KWENYE HUDUMA NI LIPI? YESU? AU FAIDA YAKO KIFEDHA KWA AJILI YA FAMILIA YAKO?

>>JE! FEDHA YAKO ILIYO NYINGI ZAIDI UNAITUMIA KWENYE NINI? MAMBO YA YESU, KANISA, NA UFALME WAKE, AU MAMBO YAKO BINAFSI NA FAMILIA YAKO?

>>JE! UNATAFUTA KWA NAMNA YOYOTE KUONEKANA, KUJULIKANA, KUPATA UMAARUFU, SIFA, HESHIMA, MALI, UTUKUFU WAKO, AU CHOCHOTE CHA KWAKO WEWE NA SI CHA YESU?

>>JE! MATENDO YA MUNGU YAKITENDEKA KWA MKONO WAKO UNAJIONA KWAMBA WEWE NI WA KIROHO ZAIDI AU UNAMCHA MUNGU ZAIDI KULIKO WENGINE?

>>JE! UNAJIONA KWAMBA UNASTAHILI KUITWA MTUMISHI WA MOJAWAPO YA OFISI TANO ZA YESU KWA SABABU TU UMESOMA CHUO FULANI CHA BIBLIA?

>>JE! UNAONA KWAMBA DHEHEBU ULILOMO AU KANISA UNALOLISIMAMIA KWAMBA NDILO BORA ZAIDI KIROHO KULIKO MENGINE?

>>JE! UKO TAYARI KUPIGANIA DHEHEBU ZAIDI KULIKO YESU?

>>JE! BADO UNAWEKA MIPAKA YA KIDHEHEBU NA BADO UNAJITAMBULISHA KWA MISINGI YA KIMADHEHEBU NA SIYO KUJITAMBULISHA KAMA MTAKATIFU ULIYE NDANI YA YESU, MCHA MUNGU UNAYEMTUMIKIA YESU, NA KUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI?

>>JE! UKO TAYARI KUFUMBIA MACHO UOVU UNAOTENDEKA KWENYE DHEHEBU LAKO KWA KUWA TU UMEJIUNGA HUKO, AU NI KIONGOZI HUKO, AU UNATUMIKA HUKO, AU UNAPATA MKATE HUKO? BADALA YA KUSIMAMA NA YESU KUKEMEA NA KUKATAA UOVU HATA IKIBIDI UFUKUZWA?

>> JE! WEWE NDIYE MMOJA WA WALE WANAODHANI KWAMBA MUNGU ANASTAHAILI ASILIMIA KUMI TU PEKE YAKE NA ASILIMIA TISINI YA FEDHA AU MAPATO YAO NI YA KWAO WENYEWE? JE! WEWE NDIYE UNAYEMPENDA MUNGU KWA ASILIMIA KUMI YA FEDHA ZAKO? NA KUMKATAA KWA ASILIMIA 90 YA FEDHA ZAKO?

UNAWEZA KUONA HAPA WATU AMBAO HAWAFANANI NA YESU KABISA NA WALA HAWAENENDI KAMA YESU ALIVYOENENDA KABISAAA! JE! YESU HAKUSEMA TAFUTENI UFALME WA MUNGU KWANZA NA HAKI YAKE, NA HAYO MENGINE (YANAYOHARIBIKA) MTAZIDISHIWA? (MATTHEW 6:33)

SASA KWA NINI WEWE UNATAFUTA YALE AMBAYO MUNGU AMESEMA UTAZIDISHIWA NA KUYAPA KIPAUMBELE ZAIDI KWA KUYAONA NI MUHIMU ZAIDI, NA KUACHA YALE MAKUU AMBAYO NDIYO UNATAKIWA NA UMEAGIZWA KUWEKA MOYO WAKO HUKO?

>>JE! UTAENENDA HIVYO NA KUDAI KWAMBA WEWE NI ROHO MOJA NA YESU NA KWAMBA UNATAFUTA UFALME WA MUNGU KWANZA NA HAKI YAKE SIKU ZOTE, HUKU UKIJUA HAKIKA KWAMBA HAYO MENGINE UTAZIDISHIWA?

>>JE! UTABADILISHA VIPAUMBELE VYA MUNGU HALAFU UKASEMA UMEOKOKA NA UNATARAJIA KUINGIA MBINGUNI? HAPANA! KAMWE!

>>BARAKA KUU YA KIROHO NI KUWA KAMA YESU ALIVYOKUWA (TO BE COMPLETELY CHRIST-LIKE)!! (RUM 8:29) LAZIMA,

1) KUISHI KWA MALENGO YALE YALE YA YESU!!!

2) KUISHI KWA MAKUSUDI YALE YALE YA YESU!!

3) KUFURAHIA YALE YALE ANAYOFURAHIA YESU!!!

4) KUCHUKIA YALE YALE ANAYOYACHUKIA YESU!!!

5) KUTAFUTA YALE YALE ANAYOYATAFUTA YESU!!!

6) KUJIKANA VILE VILE KAMA ALIVYOJIKANA YESU!!!

7) KUMTEGEMEA BABA WA MBINGUNI VILE VILE KAMA YESU ALIVYOMTEGEMEA BABA YETU WA MBINGUNI!!!

8) KUWA MTAKATIFU VILE VILE KAMA YESU ALIVYOKUWA MTAKATIFU!!

9) KUENENDA KWA ROHO YULE YULE NA VILE VILE KAMA YESU ALIVYOENENDA KWA ROHO MTAKATIFU!!!

10) KUFURAHIA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU VILE VILE KAMA YESU ALIVYOFANYA!!!

11) KUKATAA YOTE ALIYOYAKATAA YESU!!!

12) KUISHI KWA IMANI VILE VILE KAMA YESU ALIVYOFANYA!

13) KUDHIHIRISHA NGUVU ZILE ZILE KAMA YESU ALIVYODHIHIRISHA!!

14) KUSIMAMA KWENYE KWELI VILE VILE KAMA YESU ALIVYOFANYA!!!

15) KUPATA MATOKEO NA MAFANIKIO KIHUDUMA VILE VILE KAMA YESU ALIVYOAGIZA!!!

16) KUISHI SAWASAWA NA AMRI MPYA YA AGANO JIPYA VILE VILE KAMA ALIVYOAGIZA YESU

17) KUKUA KIIMANI NA KUFIKIA CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WAKE KRISTO!!!

18) KUKUA KATIKA MAMBO YOTE HATA KUMFIKIA YESU ALIYE KICHWA CHA ENZI YOTE NA MAMLAKA KATIKA YOTE!!!

>>KUFANYA KAZI ZILE ZILE KAMA ALIZOZIFANYA YESU, NA KUBWA KULIKO HIZO!!!

>>HUKU NDIKO KUBARIKIWA KIROHO NA SIYO VINGINEVYO! KAMA HAUNA MALENGO HAYA HIYO INAONYESHA JINSI UNAVYOABUDU SANAMU NA KUITUMIKIA MIUNGU YAKO MWENYEWE NA KAMWE SIYO MUNGU ALIYE HAI!!!

>>BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YA KRISTO YESU ZIMEKUSUDIA KUKUFIKISHA MAHALI PA WEWE KUWA, NA KUENENDA VILE VILE KAMA YESU, NA MAANDIKO MENGI YANATHIBITISHA HILI! MWABUDU SANAMU ANATAFUTA MAGARI, MAJUMBA, PESA, UMAARUFU, MKATE, MAVAZI, VYEO,  MALI, MAJENGO, VITU, N.K. WAKATI MAANDIKO YAKO WAZI KWAMBA MUNGU ANAJUA KWAMBA UNAYAHITAJI HAYA YOTE, NA AMEAGIZA UUTAFUTE UFALME WA MUNGU KWANZA NA HAKI YAKE NA MENGINE YOTE HAYO UTAZIDISHIWA!!!

 23Amani na iwe kwa ndugu, na pendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo. 24Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika. (Efe 6:23_24)

 

Tukutane katika sehemu inayofuata ya Baraka za Kiakili (Mental Blessings)!



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post