UTAKATIFU NI MAISHA YAKE YEYE ALIYEMWAMINI YESU KRISTO NA KUMPOKEA MOYONI MWAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI,
AKIWA AMEOSHWA DHAMBI ZAKE ZOTE, MOYO WAKE UMESAFISHWA KABISA, ANA MOYO
SAFI, ANAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KULITENDA NENO LA MUNGU NA KUFANYA
YOTE ASEMAYO BWANA YESU, AKIFANYA YOTE HAYO KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
AKAAYE NDANI YAKE, ALIYEMPOKEA MARA BAADA YA KUOKOKA NA KUBATIZWA KWENYE
MAJI MENGI, AKICHUKIA UOVU, HATENDI DHAMBI, NA WALA HAWEZI KUTENDA
DHAMBI MAANA AMEZALIWA MARA YA PILI NA MUNGU MWENYEWE KWA MBEGU TAKATIFU
ISIYOHARIBIKA ILIYOMO NDANI YAKE YA NENO LA UZIMA LIDUMULO HATA
MILELE!! Biblia inasema, "4 kama vile alivyotuchagua katika yeye
kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio
na hatia mbele zake katika pendo." (Waefeso 1:4)
>> UTAKATIFU NI MAISHA YA UTII NA UAMINIFU ANAYOISHI MTOTO WA
MUNGU ALIYE NDANI YA KRISTO YESU, AMBAPO HANA HATIA WALA KOSA LOLOTE
MBELE ZA MUNGU KATIKA PENDO; YAANI, KATIKA KUMPENDA KWAKE MUNGU HANA
UPUNGUFU WALA LAWAMA YOYOTE MACHONI PA MUNGU MTAKATIFU!! MUNGU
AKIMTAZAMA ANAFURAHISHWA NA KUPENDEZWA NAYE MAANA ANAENENDA KATIKA PENDO
LILE LILE LILILOKUWEMO NDANI YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU!!
Mtume Yohana aliandika; "5 Lakini yeye alishikaye neno lake,
katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua
ya kuwa tumo ndani yake."
1 Yohana 2:5
>> MTAKATIFU ANALISHIKA NENO LA KRISTO NA KULIISHI! MAISHA YA MTAKATIFU NI
SAWASAWA NA NENO LISEMAVYO!! MTAKATIFU ANAISHI MAISHA YA NENO AMBAYO
NDIYO MAISHA YA YESU KRISTO ALIYEMWAMINI, MAANA YESU KRISTO NI NENO LA
MUNGU ALIYE HAI NDANI YA MOYO WA MTAKATIFU MWANA WA MUNGU
UPENDO WA MUNGU UMEKAMILIKA KWELI KWELI NDANI YA MTAKATIFU! MOYO WAKE UMEJAA PENDO LA MUNGU!!
Maandiko yanasema, "6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani
yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda."
1 Yohana 2:6
UTAKATIFU NI MAISHA YA YESU ALIYOISHI KWENYE MWILI! MAISHA YA YESU NI
MAISHA YA MUNGU KWENYE MWILI! MTAKATIFU AMEZALIWA MARA YA PILI KWA ROHO
MTAKATIFU NA NENO, NA HIVYO NI MWANA WA MUNGU ANAYEISHI NA KUENENDA VILE
VILE KAMA YESU ALIVYOENENDA!
UTAKATIFU NI MAISHA KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU, KWA NGUVU ZA ROHO WA MUNGU ALIYEMO NDANI YA MTOTO WA MUNGU ALIYEOKOKA KWA KUMWAMINI YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE! Imeandikwa pia,
"6 Kila akaaye ndani yake hatendi
dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua." (1 Yohana
3:6)
9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake
wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa
kutokana na Mungu.
(1 Yohana 3:9)
UTAKATIFU NI MAISHA YA KUTOTENDA DHAMBI UKIWA NDANI YA YESU! UTAKATIFU
NI MAISHA YA KUCHUKIA DHAMBI NA KUTOWEZA KUTENDA DHAMBI UKIWA NDANI YA
YESU! UNAKUWA NDANI YA YESU UNAPOOKOKA AMA UNAPOZALIWA MARA YA PILI!!
Yesu alisema, 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na
kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (Yohana 10:10) Na pia imenenwa,
Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.
1 Yohana 2:25
>> UTAKATIFU NI UZIMA TELE WA MILELE NDANI YAKE YEYE AMWAMINIYE YESU KRISTO BWANA WETU
>> UTAKATIFU NI MAISHA TELE YA MILELE NDANI YAKE KILA AMWAMINIYE YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU
Biblia inasema, "11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; (Tito 2:11)
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi
kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;" (Tito 2:12)
>> UTAKATIFU NI NEEMA YA MUNGU NDANI YAKE AMWAMINIYE YESU,
INAYOMFUNDISHA NA KUMWEZESHA KUKATAA UBAYA NA TAMAA ZOTE ZA KIDUNIA; ILI
KUISHI MAISHA YA KIASI, HAKI, NA UTAUWA KATIKA ULIMWENGU HUU WA SASA!! Paulo aliandika, 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa
katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki,
na utakatifu, na ukombozi;
1 Wakorintho 1:30
>> UKIOKOKA YESU ANAKUWA NDANI YAKO NA WEWE NDANI YAKE, NAYE
ANAKUWA AMEFANYIKA 1) HAKI YAKO, 2) UKOMBOZI WAKO, 3) HEKIMA YAKO, NA 4)
UTAKATIFU WAKO!!
>> UTAKATIFU NI YESU NDANI YAKO UNAPOMPA MOYO WAKO NA KUMPOKEA AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO MILELE! UTAKATIFU HAURITHIWI KAMA ULIVYORITHI
DINI FULANI AU DHEHEBU KWA WAZAZI WAKO! UTAKATIFU UNAUPOKEA UNAPOAMUA
KUTUBU DHAMBI ZAKO NA KUZIACHA MOJA KWA MOJA, KWA KUMPA MOYO NA MAISHA
YAKO YESU KRISTO ALIYEKUFIA MSALABANI ILI AKUOSHE DHAMBI ZOTE KWA DAMU
YAKE, NA KUKUPA MOYO MPYA WA NYAMA NA ROHO MPYA YA UTAKATIFU PALE
UNAPOMKARIBISHA AINGIE MOYONI MWAKO! YESU ANAKUFANYA WEWE UWE MTAKATIFU
NA YEYE ANAKUWA NDIYE UTAKATIFU WAKO, KWA ROHO WAKE MTAKATIFU, NA NGUVU
ZAKE ZA UTAKATIFU!!
MUNGU ALIISHI KWENYE MWILI KWA MIAKA
MITATU NA NUSU (1 TIMOTHEO 3:16) JINA LAKE LILIKUWA NI 'YESU'!! MAISHA
ALIYOYAISHI NDIYO UTAKATIFU NA NDIYO UPENDO! UKIMWAMINI YESU UKAOKOKA
YESU ATAINGIA NDANI YAKO NA KUKUWEZESHA KWA NGUVU ZA ROHO WAKE KUISHI
MAISHA YALE YALE YA UTAKATIFU WAKE YEYE MWENYEWE MAANA NA WEWE SASA UMEKUWA
MWANA WA MUNGU KAMA YESU! HAUTUMII NGUVU ZAKO KUUTAFUTA UTAKATIFU KWA
KUFUNGA, KUOMBA, KUTOA, N.K. MWAMINI YESU, ISHI KWA IMANI, NEEMA YAKE
ITAKUWEZESHA KUISHI MAISHA MATAKATIFU!!
Mwandishi wa Waebrania anaandika, 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na
watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao;
Waebrania 12:14
>> BIDII YA KUUTAFUTA UTAKATIFU NI BIDII YA KUSOMA NENO,
KULIAMINI, KULISHIKA, KULITUNZA MOYONI MWAKO, KULITENDA, KUFANYA KAMA
LISEMAVYO, KULIZINGATIA, KULIHESHIMU, KULIKUMBUKA, KULITAFAKARI,
KULITUMAINIA, KULISEMA NA KULIKIRI, KUOMBA SAWASAWA NA NENO HILO,
KULITHAMINI KULIKO VYOTE, KULIPENDA KULIKO WOTE NA KULIKO YOTE, NA
KULIJAZA KWA WINGI MOYONI MWAKO ILI KULIISHI KWA KADIRI YA NEEMA YAKE!! NDIPO UTAKATIFU WA BWANA
UTAONEKANA KWAKO! Imenenwa, 8 Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.
2 Wakorintho 13:8
>> UTAKATIFU NI KWELI UNAYOIISHI, KWELI ULIYONAYO NDANI YAKO,
KWELI INAYOKUTAKASA, KWELI UNAYOIPENDA, KWELI UNAYOITHAMINI, KWELI
UNAYOIZINGATIA, KWELI USIYOWEZA KABISA KUIACHA WALA KUTENDA NENO LOLOTE
KINYUME CHAKE, KWELI UNAYOISHUHUDIA NA KUITETEA, KWELI UNAYOSIMAMA NAYO
HATA IKIBIDI KUFA KWA AJILI YAKE!! NENO LA MUNGU NI KWELI! YESU NI
KWELI! ROHO NI KWELI! Ubarikiwe na Bwana!