Ephesians 4:13 (Amplified Bible)
"until we all reach oneness in the faith and in the knowledge of the Son of God, [growing spiritually] to become a mature believer, reaching to the measure of the fullness of Christ [manifesting His spiritual completeness and exercising our spiritual gifts in unity]."
Waefeso 4:13
" mpaka sisi sote tutakapofikia kuwa 'mmoja' katika imani, na katika kumjua Mwana wa Mungu, [kukua kiroho] hata kuwa mwamini aliyekomaa, na kufikilia kipimo cha ukamilifu na utimilifu wa Kristo [ tukidhihirisha/tukionyesha ukamilifu na utimilifu wake kiroho, huku tukizitenda kazi zake kwa karama za kiroho kama mmoja]"
>> KAZI ZAKE KRISTO (Yohana 14:12) ZINATENDWA KWA NGUVU ZA ROHO WAKE MTAKATIFU, KATIKA UDHIHIRISHO WA ROHO MTAKATIFU NA KARAMA ZAKE ZOTE!
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Yohana 17:21[ New Living Translation-John 17:21
"I pray that they will all be one, just as you and I are one—as you are in me, Father, and I am in you. And may they be in us so that the world will believe you sent me."]
"23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi."
Yohana 17:23 [ New Living Translation-John 17:23
"I am in them and you are in me. May they experience such perfect unity that the world will know that you sent me and that you love them as much as you love me."]
1) MWANA NDANI YA BABA,
2) BABA NDANI YA MWANA,
3) KANISA NDANI YA BABA NA MWANA
>> BABA, MWANA, NA KANISA LAZIMA WAWE "MMOJA"!! KUNA TOFAUTI YA KUWA NA UMOJA, NA KUWA MMOJA!
>> MNAWEZA KUWA NA UMOJA KATIKA MAENEO KADHA WA KADHA, LAKINI BADO KILA MMOJA AKAWA NA YAKE YASIYOKUWEMO KATIKA ULE UMOJA!!
>> MNAPOKUWA "MMOJA" HAKUNA MWENYE LAKE PEKE YAKE TOFAUTI NA WENGINE, BALI KILA ALILONALO HUYU NDILO ALILONALO HUYU! ALIVYO HUYU NDIVYO ALIVYO HUYU, ANALOTENDA HUYU NDILO ANALOTENDA HUYU!! MKIWA NA UMOJA WA ROHO MNAKUWA MMOJA!! MNATENDA KWA PAMOJA, MNAMILIKI KWA PAMOJA! MNAFANANA KWA KILA KITU!
>> NGUVU ZA BABA NDIZO NGUVU ZA MWANA, NA NDIZO NGUVU ZA ROHO NDANI YA KANISA!!
>> PENDO LA BABA NDILO PENDO LA MWANA, NA NDILO PENDO LA ROHO MTAKATIFU NDANI YA KANISA!
>> UTAKATIFU WA BABA NDIO UTAKATIFU WA MWANA, AMBAO NDIO UTAKATIFU WA ROHO MTAKATIFU NDANI YA KANISA!
>> UTUKUFU WA BABA NDIO UTUKUFU WA MWANA, NA NDIO UTUKUFU WA ROHO WA UTUKUFU NDANI YA KANISA!
>> MAMLAKA, UWEZA, HEKIMA, UTAJIRI, MAARIFA, HESHIMA, UFAHAMU, USHAURI, KICHO, UFUNUO, UNYENYEKEVU, NGUVU, N.K. VYA BABA, AMEMPA MWANA, AMBAYE AMELIPA KANISA KWA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKE!! YAANI, NDANI YA MWILI WA KRISTO!!
>> KATIKA KUWA MMOJA (IN BEING ONE!) KILA KITU NI CHETU SOTE, TUNAFANYA KAMA MMOJA MAANA TU MMOJA, TUNAMILIKI KAMA MMOJA MAANA VYOTE NI VYETU SOTE, N.K. HATUNA UMOJA MAANA TU MMOJA!!
>> MWILI WA KRISTO NI MMOJA! MGUU UNAOVAA KIATU HAUMILIKI KILE KIATU PEKE YAKE, BALI KIATU NI CHA MWILI! SAA UNAYOVAA MKONO SI YA MKONO BALI NI YA MWILI!! NYWELE SI MALI YA KICHWA, BALI NI ZA MWILI! MDOMO UNAOTAFUNA CHAKULA UNATAFUNA KWA AJILI YA MWILI SI KWA AJILI YAKE!! HAKUNA KIUNGO KINACHOFANYA KAZI KWA AJILI YAKE, BALI NI KWA AJILI YA MWILI!
>> MWILI NDIO UNAMILIKI NA SIYO KIUNGO
>> VIUNGO VYOTE VINATENDA KAZI KWA USHIRIKIANO KUFANIKISHA LENGO LA MWILI NA SIYO LENGO LA KIUNGO!!
>> BABA MMOJA, BWANA MMOJA, IMANI MOJA, ROHO MMOJA, UBATIZO MMOJA (WAEFESO 4:3-6) NA MUNGU MMOJA!!
Ndiyo maana Roho wa Utukufu anaagiza;
" 24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake." (1 Wakorintho 10:24)
Hii ni kwa sababu HAKUNA KIUNGO CHA MWILI KINACHOFANYA LOLOTE KWA FAIDA YAKE, BALI KWA FAIDA YA MWILI!! Hata mkono unaposhika mswaki kusafisha meno na meno yakiwa safi mwili uko safi! Meno hayawezi kujisifia kwa kung'aa maana yameng'arishwa! Na kung'aa kwake ni kung'aa kwa mwili!! HIVI NDIVYO KANISA LA KRISTO LILIVYO, NA LINAVYOTAKIWA KUWA! KAMA KANISA HALIKO HIVI NI KWA SABABU HALINA MUUNGANIKO NA BABA NA MWANA!! HIVYO HAKUNA UMOJA WA ROHO KATIKA KIFUNGO CHA AMANI!!
Kanisa lisilo na utukufu halina "oneness" (roho ya kuwa mmoja-spirit of oneness!) na matokeo yake ubinafsi (selfishness) umetawala kama ulivyotawala kwa wasiomjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo!! Siyo na haikuwa mpango wa Mungu kuwe na migawanyiko iliyopo leo!! Ingekuwa leo ndiyo zamani za akina Paulo, basi Paulo na Sila wangeanzisha dhehebu lao, na Barnaba na Marko wangeanzisha dhehebu lao!! Lakini kwa kuwa wote walikuwa wakitafuta kumtukuza Kristo Yesu Bwana wetu hawakufanya hivyo!! Hakujawahi kuwa na kugombea madaraka kwenye kanisa la kwanza la mfano! Haiwezi kutokea mguu na mkono wakagombea kuvaa suruali! Mikono inavalisha mwili suruali ikishirikiana na miguu, na macho pia! Macho yanaona kwa ajili ya mwili usijikwae na kuumia, au usijigonge, au usitumbukie shimoni, n.k. Masikio yanasikia kwa faida na manufaa ya mwili! Nywele zipo mwilini kwa faida ya mwili! Kila kiungo Mungu amekiweka kwenye mwili kwa faida na manufaa ya mwili!! Mwili wa Kristo ni mmoja lakini viungo ni vingi! Na Yesu atakuja kuunyakua mwili Kama kuna kiungo kinajiona siyo sehemu ya mwili na kuenenda hivyo, utukufu wa Mungu haupo pamoja nacho!! Na kama utukufu wa Mungu haupo pamoja nawe huwezi kuuingia utukufu wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu! Jipime maisha yako unavyoenenda!!!
>> Je! Unafanya kazi au biashara KWA FAIDA na MANUFAA YA MWILI WA KRISTO?
>> Je! Ni malengo na makusudi ya moyo wako kufanya kazi zote uzifanyazo na yote uyafanyayo KWA FAIDA NA MANUFAA YA MWILI WA KRISTO?
>> Je! Unaishi maisha ya utumishi na huduma kwa mwili wa Kristo siku zako zote katika mambo yote KAMA KWA BWANA NA SIYO MWANADAMU KAMA MAANDIKO YASEMAVYO??!!
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
Wakolosai 3:23
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Wakolosai 3:24
1) LOLOTE ULIFANYALO
2) LIFANYE KWA MOYO WAKO WOTE
3) LIFANYE KWA MOYO KAMA KWA BWANA
4) USIMFANYIE AU KUMTENDEA MWANADAMU MTENDEE YESU!!
5) BWANA MWENYEWE ATAKULIPA MSHAHARA! (UJIRA WA URITHI)
6) UNAMTUMIKIA KRISTO YESU BWANA UFANYAPO HIVYO/HAYO
7) Unapomfanyia mwanadamu badala ya Yesu unakuwa HAUFANYI UTUMISHI HUU WA KILA SIKU KWA BWANA WAKO YESU, NA KANISA LAKE, NA UFALME WAKE! NA KWA NAMNA HIYO HUWEZI KAMWE KUMZALIA MUNGU MATUNDA, KWA KUWA BADO NI MBINAFSI! HIVYO HUWEZI KUMTUKUZA MUNGU MAANA HUMZALII MATUNDA NA HIVYO HUWI MWANAFUNZI WA YESU!!
John 15:1-2,4-8
[1]I am the true vine, and my Father is the husbandman.
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
[2]Every branch in me that beareth not fruit he taketh away: and every branch that beareth fruit, he purgeth it, that it may bring forth more fruit.
Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
[4]Abide in me, and I in you. As the branch cannot bear fruit of itself, except it abide in the vine; no more can ye, except ye abide in me.
Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
[5]I am the vine, ye are the branches: He that abideth in me, and I in him, the same bringeth forth much fruit: for without me ye can do nothing.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
[6]If a man abide not in me, he is cast forth as a branch, and is withered; and men gather them, and cast them into the fire, and they are burned.
Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
[7]If ye abide in me, and my words abide in you, ye shall ask what ye will, and it shall be done unto you.
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
[8]Herein is my Father glorified, that ye bear much fruit; so shall ye be my disciples.
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
>> A DICSIPLE OF CHRIST IS ALWAYS FRUITFUL!! MWANAFUNZI WA KRISTO YESU SIKUZOTE HUMZALIA YESU MATUNDA!!