NDOA TAKATIFU






SEHEMU YA KWANZA

Neno la Mungu linasema,

"Psalms 12:6
[6]The words of the LORD are pure words: as silver tried in a furnace of earth, purified seven times.
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba."
 

Na tena, 

"Psalms 105:42
[42]For he remembered his holy promise, and Abraham his servant.
Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake."

 
NENO LA MUNGU NI SAFI NA TAKATIFU! (holy and pure!) YAANI, HALINA WAA WALA KUNYANZI!! LIMEJARIBIWA NA KUSAFISHWA "MARA SABA" KWENYE TANURU LA MOTO ULAO! NI NENO LA KWELI NA LA HAKIKA! NALO LINAFUNUA HAKI YAKE ( HIS RIGHTEOUSNESS)! Mungu ni Mtakatifu (1 Petro 1:16), na kwa kuwa YEYE NI NENO PIA ( Yoh 1:1), NENO HILO NI TAKATIFU SANA! UTAKATIFU WOTE WA MUNGU UMO KWENYE NENO LAKE TAKATIFU!! Mungu anaponena Neno lake hunena kwa utakatifu wake!! Kila anachokinena huwa ni kitakatifu! Kila alifanyalo huwa ni takatifu! Mawazo, maneno, na matendo yake yote ni SAFI NA MATAKATIFU! Anatenda kwa utakatifu wake! Malengo, mipango, nia, makusudi, na mapenzi yake yote ni SAFI NA MATAKATIFU!! Aliumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo kwa utakatifu wake! Na alipotaka kuumba mwanadamu alisema;
"26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:26

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1:27

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
Mwanzo 1:28

>> NENO HILI LA MWANZO 1:26-28 NI TAKATIFU SANA, NALO NDILO LILILOANZISHA NDOA TAKATIFU ULIMWENGUNI!!!
>> NENO HILI LINAFUNUA KWAMBA MPANGO NA MAKUSUDI YA MUNGU ULIMWENGUNI YAMEFUNGWA KUPITIA NDOA TAKATIFU!!
Ndoa takatifu lazima IANZIE KWA MUNGU MTAKATIFU na lazima IUMBWE KWA NENO LAKE TAKATIFU! NDOA TAKATIFU INAUNDWA NA WANANDOA WATAKATIFU NA SIYO VINGINEVYO!

SIFA ZA NDOA TAKATIFU
1) LAZIMA WANANDOA WAWE WATAKATIFU
>> Watakatifu huishi maisha ya utii kwa Mungu Mtakatifu siku zao zote! Watakatifu wanaishi kwa kulitenda Neno la Mungu! Watakatifu wanaongozwa na Neno takatifu la Mungu wanaloliamini: [ walilolikubali, walilolipokea mioyoni mwao, wanaloliheshimu, wanalolizingatia katika kila hatua ya maisha yao, linaloongoza na kutawala maisha yao yote, wanalolitumainia, walilolishika na kulitunza mioyoni, mawazoni, akilini, na midomoni mwao ] WANAISHI KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU! (Mt 4:4) Watakatifu, kama Samuel nabii, HAWALIACHI KAMWE NENO LOLOTE LA MUNGU LIANGUKE CHINI! (1 Sam 3:19)
Watakatifu katika siku zetu ni lazima wawe 1) WALIOKOKA, 2) WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU BAADA YA, AU WAKATI WA, AMA BAADA YA KUBATIZWA KWENYE MAJI MENGI KAMA YESU ALIVYOBATIZWA! (Matendo ya Mitume 2:38 & Mathayo 3:13-17), 4) WANAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU MAISHA YAO YOTE (WARUMI 8:14), NA 5) WANAMZALIA MUNGU MATUNDA YA NURU (WAEFESO 5:8-9), MATUNDA YA HAKI (ISAYA 32:17, WAFILIPI 1:11, WAEBRANIA 12:11), NA TUNDA LA ROHO ( WAGALATIA 5:22-23)! Kumzalia Mungu matunda ni ushahidi kwamba unaenenda kwa Roho (Gal 5:16), unakua katika neema na katika kumjua Kristo Yesu Bwana na Mwokozi (2 Petro 3:18)! Na kwamba maisha yako si tu yanampendeza Mungu unayemwamini (Waebrania 11:6), bali pia unamtukuza Mungu katika maisha yako yote na kwamba wewe ni mwanafunzi wa Yesu kweli kweli!! (Yoh 15:8) Na hii ndiyo BARAKA YA UZAZI WA KIROHO NA WA KIMWILI TANGU MWANZO!!
"Genesis 1:28
[28]And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every living thing that moveth upon the earth.
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

>> NDOA TAKATIFU YA WATAKATIFU INAMZALIA MUNGU MATUNDA (IT IS FRUITFUL) NA INAMZALIA MUNGU WATOTO WA KIROHO NA WA KIMWILI!
>> Ndoa takatifu INA MUME ALIYEOKOKA, ALIYEJAZWA ROHO (Mdo 2:1-4), ANAYEENENDA KWA ROHO, (Gal 5:16), NA ANA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU (2 Kor 13:14)!! MUME HUYU ANAMSIKIA MUNGU SAUTI YAKE (Yohana 10:27), NA ANAMTII SIKU ZOTE! (Yakobo 4:7) MUME HUYU AMEBEBA MAONO (VISION) ALIYOYAPOKEA KUTOKA KWA MUNGU ( Luka 1:8-25)NA ANAISHI KWA KUYATII, KUYATEKELEZA, NA KUYATENDA MAONO HAYO YA KIHUDUMA, KIUTUMISHI, KIBIASHARA, KIFAMILIA, NA KIJAMII AKISHIRIKIANA NA ROHO MTAKATIFU, HUKU AKISAIDIWA NA MKEWE!
 

NDOA TAKATIFU-SEHEMU YA PILI

MWANZO 2:15-20

15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 2:15

>> MUME KATIKA NDOA TAKATIFU AMEWEKWA NA MUNGU ILI AYAFANYE MAJUKUMU YA KIKAZI KAMA ALIVYOKUSUDIA MUNGU! HAFANYI TU KAZI YOYOTE!! MUNGU HUWA ANAKUWA NAYE KATIKA YALE AYAFANYAYO MAANA NI MAPENZI YAKE!!
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
Mwanzo 2:16

>> MUME KATIKA NDOA TAKATIFU ANALO NENO LA MUNGU LINALOONGOZA NA KUTAWALA MAISHA YAKE YOTE KWENYE NDOA YAKE NA FAMILIA!! MUME HUYU YUKO CHINI YA MAMLAKA YA MUNGU NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA WETU KAMA MAANDIKO YASEMAVYO: " 

"(1 Corinthians 11:3)
[3]But I would have you know, that the head of every man is Christ; and the head of the woman is the man; and the head of Christ is God.
Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu."

>>KUWA KICHWA NI KUWA KIONGOZI NA MCHUNGAJI! MUME YUKO CHINI YA KRISTO, NA MKE YUKO CHINI YA MUME!! KRISTO YUKO CHINI YA MUNGU!! HUU NI UTARATIBU WA MAMLAKA NA UTAWALA, NA MADARAKA YA KILA MMOJA KWENYE NDOA TAKATIFU! NDOA TAKATIFU LAZIMA IWE NA;

1) MUNGU BABA ANAYEONGOZA NDOA HIYO KUPITIA,

2) KRISTO YESU BWANA WETU ANAYEONGOZA NDOA HIYO KUPITIA

3) MUME ANAYESAIDIWA NA MKEWE!! MKE SIYO KIONGOZI BALI NI MSAIDIZI!! (MWANZO 2:18) KAMA HAIKO HIVI HIYO SIYO NDOA TAKATIFU BALI NI NDOA YA ANGUKO YA WATENDA DHAMBI! NA MAPENZI YA MUNGU HAYAWEZI KUFANIKIWA KWENYE NDOA HII MPAKA WATAKAPOOKOKA  NA KUKUA NA KUKOMAA KIROHO! MUME ALIYE KICHWA ANA UHUSIANO, MAWASILIANO, USHIRIKIANO, MAELEWANO, MAPATANO, MASIKILIZANO, NA MAKUBALIANO NA YESU ALIYE KICHWA KWNAAKE! LAZIMA MUME KATIKA NDOA TAKATIFU AWE NA USHIRIKA NA KRISTO WA "WAKATI WOTE" KILA MAHALI SIKUZOTE! ISIPOKUWA HIVYO HAIWEZI KUWA NDOA TAKATIFU MAANA UTAKATIFU WA YESU HAUPO!
>>MAPENZI YA MUNGU BABA, NDIYO MAPENZI YA YESU KRISTO, NAYO NDIYO MAPENZI YA MUME, AMBAYO NDIYO MAPENZI YA MKE, NAYO NDIYO MAPENZI YA WATOTO NA WOTE WALIOMO NYUMBANI KUPITIA ROHO MTAKATIFU NA NENO LAKE TAKATIFU!! HII NDIYO NDOA TAKATIFU NA FAMILIA TAKATIFU! NJE YA HAPO SHETANI LAZIMA ATAWALE NA HIVYO DHAMBI ITATAWALA!!

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 2:17

>> HILI NDILO NENO LA MUNGU MTAKATIFU LILILO TAKATIFU SANA NA SAFI AMBALO MWANAMUME ALIAMBIWA KABLA HATA HAJALETEWA MSAIDIZI ( MKEWE HAWA!)
>> IKIWA, MUME HAJAWA NA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU KIASI CHA 1)  KUZUNGUMZA NAYE YESU, 2) KUSEMEZANA NAYE, 3) KUPOKEA MAELEKEZO NA USHAURI WAKE, 4) KUONYWA NAYE, 5) KUFUNDISHWA NAYE, 6) KUMSIKILIZA NA KUMTII, 7) KUSHIRIKISHWA NA KUFUNULIWA NAYE SIRI ZA UFALME WA MUNGU, 8) NA KUPOKEA KWA USAHIHI KUTOKA KWAKE YESU HUDUMA, KAZI, NA UTUMISHI WOTE ALIOKUSUDIWA KUUFANYA TANGU KABLA HAJAUMBWA TUMBONI MWA MAMA YAKE, NI DHAHIRI KUWA HAWEZI KUPATA MSAIDIZI SAHIHI (UWEZEKANO WA KUKOSEA AU SHETANI KUMLETEA ASIYEKUSUDIWA KUMUOA NI ASLIMIA 99%) KWA KUWA HANA YESU/HANA NENO LA BWANA MOYONI MWAKE!! NENO LA BWANA LISIPOKUWEPO LAZIMA KUTAKUWEPO NENO LA "NYOKA" (SHETANI) KAMA ILIVYOKUWA BUSTANINI EDENI KWA MWANAMKE: ( Mwanzo 3:1-6) MWANAMKE ALIDANGANYWA AKALIACHA NENO LA MUNGU, AKAMTII "NYOKA", NA MUMEWE NAYE AKAMSIKILIZA MKEWE, AKALA YALE MATUNDA, WAKAANGUKA DHAMBINI WOTE!! (NDOA TAKATIFU IKAPOTEA MAANA DHAMBI (UASI) IMEINGIA!!
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Warumi 5:12

>>Tangu hapa wanadamu wote wakawa wameanguka dhambini! Wote tulikuwa viunoni mwa Adamu alipotenda dhambi kwa kuliasi Neno la Mungu maana dhambi ni uasi (1Yoh 3:4) Ndoa zote zilizofuata baada ya hapa zilikuwa ni "NDOA ZA ANGUKO!!" na siyo "NDOA TAKATIFU TENA!!"
 

NDOA TAKATIFU-SEHEMU YA 3

18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2:18

>> MUNGU NI ROHO (YOHANA 4:24), NAYE HUTENDA MAMBO YOTE KWA ROHO WAKE, KWA NJIA YA NENO LAKE!! LOLOTE ANALOLIFANYA MUNGU (ALIYE NENO-YOHANA 1:1) HUWA NI ROHO KWANZA HALAFU NENO HILO HUFANYIKA MWILI NA NDIPO LIKAONEKANA!! Anaposema SI VEMA HUYO MTU AWE PEKE YAKE HAPA ANAFUNUA roho ya upweke ALIYOKUWA NAYO ADAMU! AKAONA, KATIKA MPANGO NA MAKUSUDI YAKE, AMUONDOLEE UPWEKE HUO!! Msaidizi anayeongelewa hapa ni roho mwenye nafsi, ambaye ANAUMBWA KWA NENO KWANZA, HALAFU BAADAE ATAWEKWA KWENYE MWILI (Mwanzo 2: 21-23) Tunajua mwanadamu ni roho mwenye nafsi anayeishi kwenye mwili!! [ man= {spirit+soul} + flesh/body] HIVYO MWANAMKE NI roho msaidizi ALIYEUMBWA KUMSAIDIA MWANAMUME ALIYE roho kiongozi! NDOA TAKATIFU INA:
1) roho kiongozi (leader spirit), na
2) roho msaidizi (helper spirit)
>> Huu ndio uumbaji wa Mungu (God's design of man and woman) Hii ndiyo Paulo, kwa Roho Mtakatifu, aliiita "MWANAMUME NI KICHWA CHA MWANAMKE!! ( 1 Kor 11:3) MUNGU AMEMPA MWANAMUME UONGOZI WA KIROHO NA SIYO MWANAMKE NA NDIYO MAANA PAULO ALIANDIKA:
1 Timothy 2:12-13
[12]But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in silence.
Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

>> NENO LA MUNGU LILILO TAKATIFU SANA HALIKUMPA MWANAMKE RUHUSA YA KUFUNDISHA WALA KUMTAWALA MWANAMUME!!
[13]For Adam was first formed, then Eve.
Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye."

>> ADAMU ( MWANAMUME NDIYE ALIYEANZA KUUMBWA, NA NDIYE ALIYEANZA KUFANYA KAZI NA MUNGU, NA NDIYE ALIYEKABIDHIWA SERIKALI YA MUNGU (THE GOVERNMENT OF GOD) ULIMWENGUNI!! KAMA NDOA ZOTE ZINGEKUWA TAKATIFU MUNGU ANGETAWALA MOJA KWA MOJA ULIMWENGU KWA NENO LAKE KUPITIA "NDOA"!! NDOA TAKATIFU NI ZAIDI YA TAASISI, MAANA NI KANISA (KANISA LA NDOA) AMBAPO MUME ALIYE MTAKATIFU NDIYE MCHUNGAJI, NA PIA FAMILIA NI KANISA (KANISA LA FAMILIA) AMBAPO BABA (SIYO MUME) NI MCHUNGAJI, NA MAMA (SIYO MKE) NI MAMA MCHUNGAJI! HIVYO,
[KANISA LA NYUMBANI = KANISA LA NDOA + KANISA LA FAMILIA]
>> KANISA LA MAHALI PAMOJA LINA MISINGI MIWILI AMBAYO NI KANISA LA NDOA NA KANISA LA FAMILIA AMBAKO KUNA BABA, MAMA, WATOTO ( NA PIA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA HATA MAJIRANI WANAKARIBISHWA). IBADA ZILIZO HAI NA ZENYE NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU LAZIMA ZIANZIE KWENYE "MISINGI HII MIWILI!!" KISHA ZIENDELEE "PALE MNAPOKUSANYIKA PAMOJA KANISA LA PAMOJA (LOCAL CHURCH)!!"
>> Taifa la wacha Mungu linazaliwa na NDOA TAKATIFU NA FAMILIA TAKATIFU ambako WATOTO WANALELEWA KATIKA UTAKATIFU, HAKI, NA KWELI YOTE, NA WANAKUA KATIKA MAONYO NA MAUSIA YA BWANA. NJIA HII NDIYO INAYOWAPASA NA AMBAYO HAWATAIACHA HATA WATAKAPOKUWA WAZEE (MITHALI 22:6)
>> NDOA TAKATIFU HUZAA KANISA PIA TAKATIFU NA TAIFA TAKATIFU!!
>> KANISA LA LEO HALIZINGATII KINACHOENDELEA KWENYE MAKANISA YA MSINGI (NDOA NA FAMILIA) NA HIVYO INAKUWA RAHISI UTUKUFU WA MUNGU KUPOTEA (IKABODI) KUANZIA KWENYE MSINGI WA KWANZA "NDOA" NA WA PILI "FAMILIA"!
>>HII NDIYO MAANA BWANA WETU YESU ALILETA KWELI INAYOOKOA NDOA NA FAMILIA YOTE, AKILENGA KUUREJEZA UTUKUFU WA MUNGU KWENYE NDOA NA FAMILIA.

MTUNZA JELA
30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
Matendo ya Mitume 16:30

31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Matendo ya Mitume 16:31

32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.
Matendo ya Mitume 16:32

33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.
Matendo ya Mitume 16:33

34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.
Matendo ya Mitume 16:34

>> UKIMWAMINI BWANA YESU, UTAOKOKA, (SI WEWE PEKE YAKO TU), BALI PAMOJA NA NYUMBA YAKO YOTE!! (mkeo/mumeo, wanao, nduguzo, na jamaa zako wote pia!)

KORNELIO
24 Siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, hali amekusanya jamaa zake na rafiki zake.
Matendo ya Mitume 10:24

44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
Matendo ya Mitume 10:44

45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 10:45

46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,
Matendo ya Mitume 10:46

47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
Matendo ya Mitume 10:47

48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.
Matendo ya Mitume 10:48

>> Kornelio na nyumba yake, na jamaa zake, na rafiki zake, WALIMWAMINI YESU, WAKAOKOKA, WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU, NA WAKABATIZWA WOTE!! Neema ya wokovu si kwa ajili yako peke yako BALI NI KWA AJILI YAKO NYUMBA YAKO YOTE!! Hii inatatua matatizo ya ndoa na familia maana SIMBA WA KABILA LA YUDA AMEINGIA KANISANI, GIZA LOTE LAZIMA LIKIMBIE MAANA NURU HUNG'AA GIZANI! (Yohana 1:5)

RAHABU KAHABA
17 Na mji huu utakuwa wakfu kwa Bwana, mji wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma.
Yoshua 6:17

23 Basi wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli.
Yoshua 6:23

>> RAHABU KAHABA ALIOKOKA YEYE, BABA YAKE, MAMA YAKE, NDUGU ZAKE, NA VYOTE WALIVYOKUWA NAVYO VIKAJA CHINI YA DAMU YA YESU "ATAKAYEFUNULIWA!!", BILA KUWASAHAU JAMAA ZAKE WOTE!!
>> HIVI NDIVYO MUNGU ANAVYOTENDA KWA WINGI WA REHEMA, NEEMA, HURUMA, NA UPENDO WAKE!! OKOA NYUMBA YAKO YA SASA (uliyeoa/kuolewa) NA YA BAADAE (utakayeoa/olewa) KWA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO SASA!
 

NDOA TAKATIFU -SEHEMU YA NNE

Tunaendelea kuitazama ndoa takatifu kama ilivyofunuliwa kwenye maandiko matakatifu! Biblia inasema,
MATHAYO 19:3-6
>> "3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?"
Mathayo 19:3

>> KUNA UHALALI MBELE ZA MUNGU MTU KUMWACHA MKEWE KWA "KILA SABABU??!!" (Is it lawful? Is it sriptural?)
>> "4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,"
Mathayo 19:4

>> JIBU LA YESU (NENO LA MUNGU) LILIKUWA "JE! HAMKUSOMA....?!" KAMA UNATAFUTA MAJIBU YA MASWALI YA NDOA "SOMA BIBLIA KWA ROHO MTAKATIFU!!" UTAYAPATA YOTE KUTOKA KWAKE YESU!! AKASEMA, HAPO MWANZO WA KUUMBA KWAKE MUNGU ALIUMBA 1) MTU MUME, NA SIYO MTU MUME ANAYEJIGEUZA, AU ANAYEJIFANYA, AU MWENYE TABIA ZA, AU ANAYEFANYWA, AU ANAYETENDA KAMA MTU MKE!! ULAWITI NI roho ya shetani ya kugeuza KWELI KUWA UONGO NA UONGO KUWA KWELI!!, 2) MTU MKE, NA SIYO MTU MKE ANAYEJIFANYA/ANAYEJIGEUZA/AU MWENYE TABIA ZA/AU ANAYETENDA KAMA MTU MUME!! Tabia na mazoea ya kugeuza Neno la Mungu nyuma mbele na mbele nyuma ni roho ya ulawiti!! Hii roho inaanza kwenye UASI WA KWELI na kisha inakuwa ovu zaidi inapofikia sasa UONGO NDIO KWELI NA KWELI NDIO UONGO!! Usihangaike kutafuta ushoga na usagaji ulianzia wapi!! ULIANZIA KWENYE NDOA ILIYOASI NENO HALAFU IKAGEUZA KWELI KUWA UONGO NA UONGO KUWA KWELI!! WATOTO WATAKAOZALIWA KWENYE NDOA HII WATAZALIWA NA roho hii IKIWA NDANI YAO!!
>> Sasa hapo mwanzo Mungu aliumba MTU MUME NA MTU MKE!! YAANI, NDOA NI YA MTU MUME (MMOJA) NA MTU MKE (MMOJA), lakini shetani ataleta roho chafu itakayosema wanawake zaidi ya mmoja kwa mtu mume mmoja au wanaume zaidi ya mmoja kwa mtu mke mmoja!! Huu ni zaidi ya uzinzi bali ni ulawiti kiroho!! (yaani, kugeuza kweli kuwa uongo na uongo kuwa ndiyo kweli!!) Jamii imefanya hayo, kanisa limefanya hayo, familia imefanya hayo, NDOA IMEZAA HAYO!! DHAMBI ILIINGIA KWENYE NDOA NA KWA KUPITIA KWENYE NDOA ILIINGIA KWA KAINI, HALAFU IKAINGIA ULIMWENGUNI!!! NDOA YA ANGUKO ILIZAA HAYO! NDOA ZA ANGUKO LEO ZINAZAA HAYO!! YESU ANAHITAJIKA KWENYE NDOA ZA ANGUKO ILI WANANDOA WAKIOKOKA NDOA ZITAKASWE ILI ZIWE TAKATIFU!!

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Mathayo 19:5

A: KUAMBATANA(Mathayo 19:5b)
>> KWENYE NDOA TAKATIFU WANANDOA HUWA WANAAMBATANA!! NDOA ZA ANGUKO HAZINA KUAMBATANA!!
Kuambatana ni roho ya kuwa pamoja, kwenda pamoja, kupanga pamoja, kujadiliana pamoja, kutenda pamoja, kuishi pamoja, kuabudu pamoja, kufuatana pamoja, kumtumikia Mungu pamoja, kupanga mipango pamoja, kutekeleza pamoja, kukubaliana na kupatana pamoja, kuendana pamoja, kusaidiana pamoja, kufanana pamoja, n.k. Biblia inasemaje kuhusu hili?


RUTHU NA NAOMI (RUTHU 1:14-17)
14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye.
Ruthu 1:14

>> Baada ya kufiwa na wanawe wawili wa kiume walioacha wajane wawili Orpa na Ruthu, Naomi akaamua kurejea kwao nchi ya Yuda kutoka nchi ya Moabu! Akawasihi wale wakweze wawili Ruthu na Orpa waende kwao wakaolewe maana yeye anarudi kwao na sasa amezeeka! Orpa akalia akaagana naye, lakini RUTHU AKAAMBATANA NAYE!! 

roho ya kuambatana 

"15 Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako." (Ruthu 1:15)
>> Hii ndiyo roho ya kuambatana hapa chini ikinena ndani ya Ruthu na kujifunua jinsi ilivyo katika maeneo au tabia saba;
"16 Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; (Ruthu 1:16)
17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami."

(Ruthu 1:17)
1) roho hii ya kuambatana haitaki na haikubali hata lile wazo au ule ushauri wa kutokwenda pamoja kwenye uhamisho, huduma, n.k. (usinisihi, nikuache nirejee, nisifuatane nawe) Hii ni roho ya kufuatana au kwenda pamoja mguu kwa mguu!!
2) "maana wewe unakokwenda kokote nami nitakwenda" Ruthu anamwambia mkwewe unakokwenda kokote nami nitakwenda! Kwenye Ndoa takatifu ANAKOKWENDA MUME KOKOTE KIMAISHA MAKE ANAKWENDA NAYE/ANAFUATANA NAYE!! Ndoa nyingi za anguko mume yuko kaskazini anaishi na kufanya kazi, na mke yuko kusini anaishi na kufanya kazi!! KUAMBATANA HAKUPO NA NDOA HII IMEPOTEZA SIFA MUHIMU YA NDOA TAKATIFU-KUAMBATANA!! Kuambatana kupo pia kwenye zile huduma za watumishi! Unapokwenda kwenye semina, mikutano, warsha, makongamano, mikutano ya injili, kwenye uamsho, n.k. AMBATANA NA MKEO/MUMEO!!
3) "wewe ukaapo nami nitakaa" Hii inamaanisha utakapoishi mume wangu hapo ndipo nitakapoishi!!! Kwenye ndoa takatifu mume na mke huwa wanaishi pamoja na kamwe siyo mbalimbali kwa sababu yoyote! Kama ni ndoa takatifu basi inaongozwa na kuendeshwa na Neno la Mungu!! Mume na mke LAZIMA WAISHI PAMOJA MJI MMOJA, KITONGOJI KIMOJA, NYUMBA MOJA, NA KULALA CHUMBA KIMOJA, KWENYE KITANDA KIMOJA KWA SABABU NDIYO MAPENZI YA MUNGU KAMA MAANDIKO YASEMAVYO:
3A) "18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye." (Mwanzo 2:18)
>> BAADA YA KUKABIDHIWA SERIKALI YA MUNGU (LEO NI KAZI NA HUDUMA KATIKA UFALME WA MUNGU) MUNGU ALIONA, KWA UTAKATIFU, NA HEKIMA ,NA UFAHAMU, NA MAARIFA YAKE, KWAMBA SI VEMA "MTU HUYO MUME" AWE PEKE YAKE!! Kumbuka Adamu aliwekwa bustanini Edeni ili "AILIME NA KUITUNZA" (Mwanzo 2:15) Haya ni majukumu ya kazi za mikono!! Ili mtu mume amtumikie Mungu katika kazi na huduma huku akitenda kwa utukufu wa Mungu, sawasawa na makusudi na malengo ya uumbaji wa Mungu kiroho, kiakili, kihisia, kimwili, na kijamii LAZIMA AWE NA MSAIDIZI, MKEWE KUTOKA KWA BWANA! Pasipo msaidizi mtu mume ni dhaifu, amepungukiwa, na lazima kuna vita atashindwa, na kuna majukumu hatayatimiza ipasavyo, na hataweza kumpendeza Mungu, na mwishowe ataanguka!! Anahitaji SI TU MSAIDIZI BALI MSAIDIZI WA KUFANANA NAYE ILI WAWE NA USHIRIKA, WAPATANE, WASAIDIANE, WAENDANE, WAKUBALIANE, WAJADILIANE, WABADILISHANE MAWAZO, WAJENGANE, WATIANE MOYO, WASHAURIANE, WAFARIJIANE, WAHIMIZANE, WAOMBEANE, WATIANE NGUVU, WAHUDUMIANE, N.K. SIKU ZAO ZOTE! LAZIMA WALALE NA WAAMKE KWENYE KITANDA KIMOJA!!
3B) " 9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao."
Mhubiri 4:9

>> WAWILI KWENYE NDOA TAKATIFU HUPATA IJARA NZURI KWA KAZI YAO (A GOOD REWARD FOR THEIR LABOUR!) Iko thawabu njema zaidi na matokeo bora zaidi wayapatayo wanandoa walio pamoja na wanaotenda kwa pamoja katika umoja wao!! Baraka yake na thawabu yake ni kubwa maana ina kibali cha Mungu na hayo ndiyo mapenzi yake!!
"10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!"
Mhubiri 4:10

>> Kwenye ndoa takatifu kuna nguvu ya ushindi ya wanandoa katika umoja wao!! Hakuna maanguko katika umoja wao maana mmoja akianguka mwenzake humwinua! Maanguko hutokea kwa kutolitendea kazi na kulitii neno!!
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
Mathayo 7:26

27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; NALO ANGUKO LAKE LIKAWA KUBWA.
Mathayo 7:27

>> KWA KUWA WANANDOA KWENYE NDOA TAKATIFU WANAISHI KWA NENO LA MUNGU, MMOJA AKIANGUKA MWINGINE HUMWINUA KWA KUMKUMBUSHA NENO, KUMREJESHA KWENYE NENO, KUMWONYA KWA NENO, KUMSHAURI KWA NENO, KUMWOMBEA KWA NENO, N.K.
>> Kuna maeneo mume ni dhaifu na mkewe humsaidia, hali kadhalika kuna maeneo mke ni dhaifu mumuwe humsaidia! WANAINUANA, WANASAIDIANA, NA KUTIANA NGUVU!! Ole wako wewe unayeishi peke yako mbali na mumeo/mkeo utakapoanguka HUNA MSAADA WA MUNGU KUPITIA HUYO MWENZA WAKO ALIYEPAKWA MAFUTA KUKUSAIDIA NA KUKUINUA KWENYE SAA YA KUJILIWA KWAKO!! Na hakuna "mbadala" wa mumeo/mkeo! Uzinzi haukusaidii na unazidi kujikita kwa shetani aliyefanikiwa kukutenganisha na mkeo/mumeo mkae mbali mbali ILI AKUANGUSHE NA KUKUPELEKA JEHANAMU USIPOTUBU NA KUOKOKA!
>> Kwa kukosa msaada hivyo nguvu za giza zinapata nafasi ya kuingiza uovu, ubaya, na uharibifu kwenye ndoa!! NDOA TAKATIFU HAINA HAYA MAANA WANANDOA WANALITENDA NENO NA WANAISHI KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
Mhubiri 4:11

>> HAPA KUNA TATIZO LA "BARIDI" NA MUNGU AMELITATUA KWENYE NDOA TAKATIFU KWA MUME NA MKE KULALA KITANDA KIMOJA SIKUZOTE!
>> KAMA MUME NA MKE HAWALALI KITANDA KIMOJA KWA KUWA HAWAISHI PAMOJA NA WAKO MBALIMBALI, HALI NDOA HAIJAVUNJIKA, SHETANI HUPATA NAFASI YA KUWATESA KILA MMOJA KULE ALIPO NA TATIZO LA "BARIDI", NA HATIMAYE KUTOA SULUHISHO LA UONGO LA UZINZI!! KWA HIYO UZINZI AU BARIDI NI MATOKEO YA KUTOITII KWELI!! HAMNA SABABU INAYOKUBALIKA YA KUSABABISHA BARIDI AU UZINZI NJE YA NDOA, MAANA SABABU HIYO LAZIMA IWE KINYUME NA NENO LA MUNGU!! MENGINE KUHUSU HILI HAPA SI MAHALI PAKE!!

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi."
Mhubiri 4:12

>> MUNGU AMEWEKA KWENYE NDOA TAKATIFU ROHO NA NGUVU ZA KUMSHINDA SHETANI KWENYE VITA VYA KIROHO AMBAVYO NI VITA VYA IMANI!!
>> HAKUNA PEPO/JINI/MCHAWI/KUZIMU/MAUTI/SHETANI AU KIUMBE CHOCHOTE KINACHOWEZA KUWASHINDA MTU MUME MTAKATIFU NA MTU MKE MTAKATIFU KWENYE NDOA TAKATIFU IKIWA WANAENDELEA KWENYE UTII, UNYENYEKEVU, KICHO, UTAUWA, NA KWELI YOTE KATIKA UMOJA WAO!! WANANDOA WENYEWE NDIO WANAOMPA IBILISI NAFASI KWA KUTOTII KWAO.
(A HOLY COUPLE IN A HOLY MARRIAGE ARE SIMPLY INVINCIBLE!!) HAWA WANANDOA NI KANISA TAKATIFU LILILOJENGWA JUU YA MWAMBA AMBALO MILANGO YA KUZIMU HAIWEZI KAMWE KULISHINDA (Mt 16:18)
>> NDOA IKISHINDA FAMILIA IMESHINDA, NA KANISA LA NYUMBANI LIMESHINDA! WATAKATIFU WALIO "KANISA LA/ MWILI WA KRISTO" WANAPOKUSANYIKA KWENYE IBADA ZAO PANAKUWEPO MKUSANYIKO WA MAKANISA YA NYUMBANI YALIYOMSHINDA, NA YASIYOWEZA KUSHINDWA NA SHETANI NA NGUVU ZAKE ZOTE!!
16 Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; (Ruthu 1:16)
4) "watu wako watakuwa watu wangu!" Roho Mtakatifu hapa anafunua tabia au sifa nyingine ya kuambatana!! WATU WAKO MUME WANGU WATAKUWA WATU WANGU, NA WATU WAKO MKE WANGU WATAKUWA WATU WANGU! Kwenye ndoa takatifu wanandoa huambatana kiasi cha KUPANUA NA KUUNGANISHA FAMILIA NA KUTENGENEZA UNDUGU WA KIUMENI NA KIKENI KWA KUWALETA PAMOJA KUWA FAMILIA TAKATIFU!! KWA KUWA WAMEOKOKA, WANANDOA HAWA HUWA NI SABABU YA KUOKOKA NDUGU ZAO WOTE WALIOKUSUDIWA WOKOVU KAMA MAANDIKO YASEMAVYO!! "Mwamini Bwana Yesu nawe UTAOKOKA, PAMOJA NA NYUMBA YAKO YOTE" (Matendo ya Mitume 16:30-34)
>> Andiko hili ni sawa na KUWAINGIZA KWENYE SAFINA YA WOKOVU KAMA ZAMANI ZA NUHU NDUGU NA JAMAA WOTE WA WANANDOA WALIOMO KWENYE NDOA TAKATIFU!!
>> Neema ya wokovu imefunuliwa KWA WANANDOA WOTE KWENYE NDOA TAKATIFU, NA FAMILIA ZAO, NA NYUMBA ZAO/ JAMAA ZAO!! Unapomwamini Bwana Yesu nuru ya uzima inakuwa imeangaza kwenye familia yako yote na ndugu na jamaa zako wote! Hatimaye inatengenezwa familia moja kubwa iliyoangazwa kwa nuru ya Injili ya Utukufu wake Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu! Kitakachofuata ni kuokoka mmoja baada ya mwingine pande zote mbili za mke na mume KUPITIA IMANI NA UTII WA WANANDOA WATAKATIFU HAWA WALIOMO KWENYE NDOA TAKATIFU!! Ndoa za anguko zinaweka mipaka isiyoweza kuvukwa ili kulinda "undugu au familia zao" ambapo mke au mume HAKUBALIKI MOJA KWA MOJA UPANDE MWINGINE KWA KUWA AMETOKA "KABILA JINGINE!" NA KWA WALE WANA NDOA AMBAO MKE AU MUME AMETANGULIA KUOKOKA, MAANA WALIKUWA WOTE HAWAJAOKOKA, IKITOKEA HUYU LABDA DINI HII AU DHEHEBU HILI NA MWINGINE DINI NA/AU DHEHEBU LINGINE, HUWA HAKUBALIKI KABISA UPANDE WA PILI!! HAPA PANA MIPAKA YA KIDINI NA KIMADHEHEBU!! UKIMALIZA KUISOMA HABARI YOTE YA RUTHU NA NAOMI MKWEWE UTAKUTA RUTHU ALIAMBATANA NA NAOMI MPAKA NCHI YA YUDA, AKAOLEWA HUKO NA BOAZ, WAKAMZAA OBEDI, ALIYEMZAA YESE, BABA YAKE DAUDI!! (Mathayo 1:5-6)!! Leo tunasoma Zaburi za Daudi ambaye ni uzao wa hao walioenenda kwa roho ya kuambatana!! Kuna siri na mpango wa Mungu kwenye kuambatana! Ruthu alikuwa Mmoabi lakini ALIWAKUBALI YUDA KAMA WATU WAKE MWENYEWE! NAO WAKAMPOKEA KAMA MMOJA WAO!! Ndoa za Anguko haziko hivyo maana HAZINA YESU MOYONI NA NDUGU ZAO PIA HAWANA YESU! Hawa ndio wanaoingilia mambo ya familia kutaka mali, au humfukuza, au kumdhulumu mke, mumewe akifa, hawamkubali kama mmoja wao maana HAWANA YESU, na hawana roho ya kuambatana!! Hawana upendo wa Mungu mioyoni mwao!!
5) "Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu!!" Ruthu anamwambia Naomi maamuzi ya moyo wake ya kumwabudu Mungu wa Israeli! Hii ina maana Mmoabu Ruthu ALIAMUA KUACHANA NA miungu ya Wamoabu NA KUMWAMINI, KUMWABUDU, NA KUMTUMIKIA Mungu wa Naomi!! RUTHU KIMSINGI ALIAMUA KUOKOKA!! ( KWA LUGHA YA AGANO JIPYA!) Siyo tu Ruthu aliambatana na Naomi kimwili, bali alikwishaambatana naye moyoni mwake! Kuna
1) kuambatana kiroho, ( spiritual cleaving)
2) kuambatana kiakili, (mental cleaving)
3) kuambatana kihisia, (emotional cleaving)
4) kuambatana kimwili (physical cleaving)
5) kuambatana kwenye mambo ya kijamii (social cleaving)
>> NI LAZIMA KUAMBATANA KIROHO KWANZA ILI KUWEZA KUAMBATANA KWENYE MAENEO MENGINE!!! KAMA WANANDOA HAWAMWABUDU MUNGU MMOJA HAWAJAAMBATANA KIROHO NA HAWAWEZI KUAMBATANA KWENYE MAENEO YOTE MENGINE!! Maana ile roho ya kuambatana haipo na badala yake inakuwepo roho ya ubinafsi na faraka ambapo kila mmoja anaabudu "mungu" au "Mungu" wake!! Wakiwa hawajaokoka wote wanamwabudu shetani NA HAWAJAAMBATANA HATA KIDOGO! Ndoa kwao inabaki ni "uhusiano wa kimwili tu!!" (it only remains a physical relationship!) ambao hauna mizizi rohoni mwao, na ni rahisi kabisa kwa shetani KUVURUGA UHUSIANO HUU!! Kuambatana ni barabara ya kuelekea kuwa MWILI MMOJA! WANANDOA KWENYE NDOA TAKATIFU WANAMWABUDU MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO KATIKA ROHO NA KWELI (Yohana 4:23-24) Kwa hiyo:

4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
Waefeso 4:4

5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
Waefeso 4:5

6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
Waefeso 4:6
>> WANANDOA KATIKA NDOA TAKATIFU WAMEOKOKA NA HIVYO WANAYE 1) MUNGU MMOJA MUUMBA WA MBINGU NA NCHI, NDIYE BABA YAO ALIYEWAZAA MARA YA PILI KWA NENO LAKE LA UZIMA (1 PETRO 1:23), 2) BWANA MMOJA YESU KRISTO, ALIYEWAOKOA, 3) WANA IMANI MOJA TAKATIFU YA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYEWANUNUA KWA DAMU YAKE, 4) WANA UBATIZO MMOJA WA MAJI MENGI NA WA ROHO MTAKATIFU,[ UBATIZO WA ALIYEOKOKA= UBATIZO WA MAJI MENGI + UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU], 5) WAO NI VIUNGO WA MWILI MMOJA WA KRISTO AMBAO NI KANISA LAKE, 6) WANAYE ROHO MMOJA MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAO, MAANA WAO NI KANISA (HEKALU LA ROHO MTAKATIFU), 7) WANALO TUMAINI MOJA LA KUURITHI UTUKUFU WA MILELE KWA NJIA YA YESU KRISTO!!
17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
Ruthu 1:17

6) "pale utakapokufa na mimi nitakufa na kuzikwa hapo hapo" Ruthu aliambatana na Naomi mpaka kwenye mauti! Sikuachi, sitengani nawe kamwe, nitakaa nawe mpaka utakapokufa, na hapo ndipo nitakapozikwa!! WANANDOA WALIOAMBATANA WANAZIKWA PAMOJA, MAANA NI NDUGU, NI JAMAA MOJA, WANA IMANI MOJA, WANA MUNGU MMOJA, HAMNA KIKWAZO CHOCHOTE! Hamna ule uovu wa kumfukuza mke mume akifa! Mume akifa mke hubakia pale mpaka kifo kitakapomchukua maana yeye ni jamaa moja na wale jamaa wa mumewe! Aondoke aende wapi? Mke anabaki pale mpaka kifo, na akifa anazikwa pale alipozikwa mumewe! Ruthu amefundisha hili kivitendo na siku ya hukumu atasimama kuwahukumu hatia watu waovu waliokuwa wanatenda kinyume na kweli hii ya kuambatana! Vikwazo na matengano, migogoro, na faraka vyote vya leo ni VYA NDOA ZA ANGUKO ZISIZO NA UTUKUFU WA MUNGU NA ZISIZO NA KUAMBATANA!!
7) " Bwana na anitende hivyo na kuzidi ila KIFO TU KITATUTENGA WEWE NA MIMI!! CHOCHOTE KILE TOFAUTI NA KIFO KINACHOWATENGANISHA WANANDOA WAWE MBALIMBALI KIMETOKA "KUZIMU" NA NI "DHAMBI" NA "MAUTI"!!! HAMNA UHALALI WA KUKAA MBALIMBALI KWA VIGEZO DHAIFU VYA KIDUNIA KAMA AJIRA/ELIMU/BIASHARA/MASOMO N.K. Soma umalize kusoma halafu uingie kwenye MAJUKUMU MAZITO YA NDOA TAKATIFU! Hakuna kilicho bora tofauti na kumtumikia Mungu Aliye Hai KATIKA MPANGO NA MAKUSUDI YAKE ULIMWENGUNI KATIKA UFALME WAKE, NDANI YA YESU KRISTO! NDOA TAKATIFU NI HUDUMA!  NDOA TAKATIFU NI UTUMISHI! NDOA TAKATIFU NI WITO!! USIKIMBILIE KAMA HAUJAITWA AU HAUNA VIGEZO! DHAMBI NDIYO INAWAHARAKISHA WATU KUWAHI KUINGIA NA MATOKEO YAKE WANAKWENDA KUYAFANYA MAPENZI YA SHETANI NA SIYO MUNGU KWENYE NDOA YA ANGUKO!! NIMEELEZA ZAIDI KUAMBATANA MAANA NDIKO KUNAPELEKEA " MWILI MMOJA!" AMBAO TUTAUTAZAMA KADIRI TUNAVYOENDELEA!! MUNGU AWABARIKI WAPENDWA WOTE KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYEFUFUKA KUTOKA KWA WAFU! AMEN!
Somo linalofuata tutaangalia NDOA YA ANGUKO!!


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post