UTAKATIFU KAMA ULIVYOFUNDISHWA KWENYE WHATSAPP STATUSES
1) 7 kwa wote walioko Rumi, wapendwao na
Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo
kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. (Warumi 1:7)
>> KANISA LA RUMI (ROME) WALIITWA WAWE WATAKATIFU!! (called to be holy)
>>UTAKATIFU NI WITO WA MUNGU WA UTAKATIFU KWA WOTE WAMWAMINIO YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WAO, AMBAO YESU ANAKAA NDANI YAO KWA ROHO WAKE MTAKATIFU ANAYEWAWEZESHA KUISHI NA KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE MWENYEWE ALIVYOENENDA KATIKA HAKI, UTAKATIFU, NA KWELI, KATIKA SIKU ZA MWILI WAKE.
>> KANISA LA KRISTO NI TAKATIFU LOTE KWA KUWA ROHO MTAKATIFU
ANAKAA NDANI YAKE! "16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na
ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?" (1 Wakorintho 3:16) KUSANYIKO
LA WATENDA DHAMBI KAMWE SIYO KANISA!
Romans 1:7
"[7]To all that be in Rome, beloved of God, called to be saints: Grace
to you and peace from God our Father, and the Lord Jesus Christ.
kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu.
Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana
Yesu Kristo."
>> KAMA HUJAITWA KUWA MTAKATIFU WEWE SIYO KANISA, NA WALA HUJAWA MKRISTO BADO! UMEDANGANYWA! BIBLIA HAISEMI HIVYO!
2) 16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
(1 Wakorintho 3:16)
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
(1 Wakorintho 3:17)
>> ROHO WA MUNGU MTAKATIFU ANAKAA NDANI YA MKRISTO MTAKATIFU
>> MKRISTO NI HEKALU TAKATIFU LA ROHO MTAKATIFU, UKILIHARIBU KWA DHAMBI ZAKO ATAKUHARIBU!!
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
(1 Wakorintho 3:16)
>> MUNGU MTAKATIFU ANAKAA NDANI YA MKRISTO (HEKALU TAKATIFU)
>> WEWE UNAYEISHI DHAMBINI MUNGU HAYUMO NDANI YAKO, BALI SHETANI YUMO NDANI YAKO
>> KAMA UNAJIITA MKRISTO HUKU NI MTENDA DHAMBI UNAJIDANGANYA!! MKRISTO NI MTAKATIFU KWA MUJIBU WA BIBLIA!! 3) 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni
hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala
ninyi si mali yenu wenyewe;
(1 Wakorintho 6:19)
>> MWILI WA MKRISTO NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKE!!
>> HUYU ROHO MTAKATIFU UNAPEWA NA MUNGU UNAPOOKOKA KWA KUOSHWA DHAMBI ZAKO ZOTE NA KUPEWA UZIMA WA MILELE!!
>> MKRISTO NI MTAKATIFU ALIYEOKOKA AMBAYE ROHO MTAKATIFU ANAISHI NDANI YAKE!!
4) 2 kwa kanisa la Mungu lililoko
Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe
watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo
kila mahali, Bwana wao na wetu. (1 Wakorintho 1:2)
1) KANISA LA MUNGU NI WALE WALIOOSHWA DHAMBI ZAO KWA DAMU YA YESU
2) KANISA NI WALE WALIOITWA WAWE WATAKATIFU! KAMA SIYO WATAKATIFU HILO NI KUSANYIKO LA WATENDA DHAMBI NA PIA NI SINAGOGI LA SHETANI.
3) HAWA AMA WAMEDANGANYWA AU NI WAASI, NA WAKAIDI, WASIOMWAMINI YESU!
NAO WANANG'ANG'ANIA TU DHAMBI ZAO KWA MIAMVULI YA TAASISI ZAO, MADHEHEBU YAO, N.K. LAKINI HAWANA YESU INGAWA WANAMTAJA YESU!!
"19Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake.Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu." (2 Tim 2:19) Kama unalitaja Jina la Yesu huku ukiwa ni muovu, unajiletea hukumu iliyo kubwa zaidi!
5) 3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu
Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu
wa roho, ndani yake Kristo; (Waefeso 1:3)
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya
ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika
pendo. (Waefeso 1:4)
>> KANISA NI WALE WALIOCHAGULIWA TANGU KABLA ULIMWENGU HAUJAUMBWA,
ILI "WAWE WATAKATIFU, WATU WASIO NA HATIA MBELE ZA MUNGU KATIKA
PENDO!!"
>> KANISA NI WALE WALIOBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO!
>> MOJA YA BARAKA HIZO NI BARAKA YA UTAKATIFU AMBAYO INATOLEWA
KAMA NEEMA YA UTAKATIFU (ambayo ni roho ya utakatifu + Roho Mtakatifu na
nguvu zake!)-blessing of holiness!
6) 3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu
Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu
wa roho, ndani yake Kristo; (Waefeso 1:3)
>> KANISA NI WATAKATIFU WANAOISHI KWA IMANI YA YESU NDANI YA YESU!
>> WANAJUA WAMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE! HAWAHANGAIKI WALA KUKIMBIA KIMBIA HUKU NA KULE KUTAFUTA BARAKA!
>> HAWAWEZI KUTAFUTA BARAKA AMBAZO NI ZAO TAYARI WANAZIMILIKI, NAZO ZINADHIHIRIKA KWA WAKATI ULIOAMRIWA MAISHANI MWAO.
>> WATENDA DHAMBI WASIO NA YESU WAO HUTAFUTA TU VITU VYA KUHARIBIKA VYA DUNIA HII NAO HUVIITA "BARAKA" BARAKA NI ROHO NA LAZIMA IANZIE ROHONI KUPITIA NENO LA KRISTO AMBALO NI ROHO NA TENA NI UZIMA/MAISHA. (YOHANA 6:63)
7) KANISA NI WATAKATIFU WANAOMCHA BWANA MUNGU MWENYEZI
Proverbs 8:13
"[13]The fear of the LORD is to hate evil: pride, and arrogancy, and the evil way, and the froward mouth, do I hate.
Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia." Na tena;
"6 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; KWA KUMCHA BWANA WATU (WATAKATIFU) HUJIEPUSHA NA MAOVU." (Mithali 16:6)
BWANA YESU AMEWEKA ROHO YA KUMCHA BWANA NDANI YA WATOTO WAKE AMBAO NI KANISA, AMBALO NDILO MWILI WAKE, YEYE AKIWA NI KICHWA CHA KANISA (WAEFESO 1:22-23) KUMCHA BWANA HUKU NDIKO KUNAWAFANYA WACHUKIE UOVU NA KUJITENGA NAO NA KAMWE HAWARUDI NYUMA WALA KUMWACHA YESU; NA HII NDIYO INAKAMILISHA UTAKATIFU WAO KAMA MANDIKO YASEMAVYO; " 1 Basi,
wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na
uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha
Mungu." (2 Kor 7:1)
8) KANISA NI WATAKATIFU WALIOJAA HEKIMA
NA UFAHAMU WA ROHONI KWA KUWA WANAMCHA MUNGU NA KUJIEPUSHA NA UOVU!!
Job 28:28
[28]And unto man he said, Behold, the fear of the Lord, that is wisdom; and to depart from evil is understanding.
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
9) KANISA NI WATAKATIFU WENYE
AKILI MBELE ZA MUNGU KWA KUWA WANAMSIKILIZA NA KUMTII KWA KILA ASEMALO!
WAKO IMARA NDANI YA YESU!
24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
Mathayo 7:24
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile,
isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
Mathayo 7:25
HAWA SIYO KANISA>> 26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu
asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya
mchanga; (Mathayo 7:26)
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile,
ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. (Mathayo 7:27)
>> HAWA WANAJIITA WAKRISTO LAKINI MUNGU ANAWAITA WAPUMBAVU!
>> WAO HUWA WANASIKIA WEEEEE MANENO YA MUNGU NA MAFUNDISHO YAKE LAKINI HAWAYATENDI
WALA HAWAISHI SAWASAWA NA MANENO YA MUNGU!! HAWANA MUNGU BABA WALA MWANA
MIOYONI MWAO! WASIPOTUBU NA KUOKOKA NI WANA WA JEHANAMU TU HAWA! Je! wewe unamtii Mungu? Unaisi maisha ya kulitii neno lake?
10) Matthew 4:4
[4]But he answered and said, It is written, Man shall not live by bread
alone, but by every word that proceedeth out of the mouth of God.
Naye
akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila
neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
>> WAKRISTO NI WATAKATIFU WANAOISHI KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU
>> WAOVU WASIOAMINI WAO, DUNIANI HAPA, WANAHANGAIKIA "MKATE" TU PEKE YAKE!!
Imeandikwa,
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
(Mathayo 6:31)
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. (Mathayo 6:32)
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. (Mathayo 6:33)
NA TENA
27 Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho
hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo
ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. (Yohana 6:27)
>> ANACHOSEMA MUNGU HAPA NI KWAMBA MAISHA HAYAMO KWENYE VITU VINAVOHARIBIKA VYA MWILINI NA VYA HAPA DUNIANI; BALI MAISHA YAPO KWAKE! KWA ROHO WAKE NA KWENYE NENO LAKE!
11) New American Bible (Heb 12:14)
"Strive for peace with everyone, and for that holiness without which no-one
will see the Lord.[ 14 TAFUTENI KWA BIDII kuwa na amani na watu wote,
na HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao"]
>> MUNGU AMESEMA UTAKATIFU UNAPATIKANA HAPA DUNIANI UKIWA HAI, NA
SIYO BAADA YA KUFA; AMEKUAGIZA UUTAFUTE UTAKATIFU HUO, MAANA USIPOKUWA
NAO HUO MPAKA UNAKUFA KAMWE HUTAMWONA MUNGU!
>> IKIWA WEWE SIYO MTAKATIFU, BASI WEWE NI MTENDA DHAMBI
Na imeandikwa; "4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi."
(1 Yohana 3:4), na hapa tena;
"8 ATENDAYE DHAMBI NI WA IBILISI; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu
mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi
za Ibilisi." (1 Yohana 3:8)
>> KAMA WEWE SIYO MTAKATIFU SIYO WA YESU, BALI WEWE NI MALI YA
IBILISI, USIJIFICHE KWENYE KICHAKA CHA DINI YOYOTE AU DHEHEBU LOLOTE,
OKOKA!!
>> UTAIKWEPAJE HUKUMU YA KUTISHA YA MUNGU USIPOMWAMINI YESU, NA KUMPA MOYO WAKO NA MAISHA YAKO??!!
"17 Maana Mungu hakumtuma Mwana
ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye."
(Yohana 3:17)
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa
sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. (Yohana 3:18)
>> KAMA HUJAMWAMINI YESU BADO UMEKWISHA KUHUKUMIWA TAYARI!! " 36
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima,
BALI GHADHABU YA MUNGU INAMKALIA." (Yohana 3:36)
>> Ghadhabu ya Mungu ni kiwango cha juu kabisa cha Mungu kuchukizwa, kukasirishwa, kughadhabika, kutoa adhabu kali kuliko zote, kuangamiza, kutokomeza, kutowesha, kupondaponda, kusagasaga, kutesa, kuumiza, kuleta maumivu yasiyokoma, PASIPO HURUMA YOYOTE WALA KUGHAIRI AU KUGEUKA, NA KUTENGA MILELE NA USO WAKE AKIKUACHA KATIKA HALI HIZO ZA KUTISHA MILELE! Kwa nini? KWA SABABU ULIZIKATAA HURUMA ZAKE, UPENDO WAKE, NA MSAMAHA WAKE ULIPOMKATAA YESU! SASSA UKIFA KATIKA HALI HIYO HAYO YOTE YATAKUPATA KAMA MAANDIKO YANENAVYO:
"1 Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. 2Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. 3Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? 4Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? 5Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, 6atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; 7wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; 8na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; 9dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; 10bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; 11kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu." (Warumi 2:1-11)
ELIMU, FEDHA, MALI, VYEO, HESHIMA YA WANADAMU, SIFA ZA WANADAMU, DHEHEBU, AU DINI ULIYORITHI KWA WAZAZI, N.K. HAVIWEZI KUKUOKOA NA GHADHABU HII ISIPOKUWA YESU! UTUBU, UMWAMINI, NA UMPOKEE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO, UKIWA UMEMPA MOYO WAKO AKUONGOZE YEYE NA KUTAWALA MAISHA YAKO KWA ROHO WAKE MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!
12) 10 Na yule Ibilisi, mwenye
kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule
mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele
na milele. (Ufu 20:10)
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. (Ufu 20:15)
>> IBILISI ANAYEKUDANGANYA UAHIRISHE KUOKOKA ANATAKA UENDE NAYE KWENYE MATESO HAYO YA MILELE!
>> AMEKUDANGANYA USEME "NINA DHEHEBU LANGU!" AU "NINA DINI YANGU"
HUKU UNATENDA DHAMBI!! WEWE NA IBILISI MNASUBIRIWA NA GHADHABU HIYO YA
MUNGU YA MILELE.
UMEDANGANYWA NA IBILISI
KWAMBA HAKUNA KUOKOKA DUNIANI NA HAIWEZEKANI KUWA MTAKATIFU!! Biblia inasema, "3
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
(Zaburi 16:3) WATAKATIFU WALIOPO HAI DUNIANI HAO NDIO WANAOMPENDEZA MUNGU
MAISHA YAO, NA TAYARI WANA "TIKETI" YA "UTAKATIFU" MIOYONI MWAO,
ITAKAYOWAWEZESHA KUINGIA MBINGUNI!! Kama ilivyoandikwa, "bali kama yeye aliyewaita alivyo
mtakatifu, ninyi nanyi IWENI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WENU WOTE;" (1
Petro1:15)
>> USIDANGANYIKE, "4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi." (1 Yoh 3:4)
"5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake." (1 Yoh3:5)
6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. (1 Yoh 3:6)
>> NDANI YA YESU HAMNA DHAMBI BALI MNA UTAKATIFU TU!
>> UKIOKOKA UNAKAA NDANI YAKE NA HUWEZI KUTENDA DHAMBI; WEWE
UNAYETENDA DHAMBI HUJAWAHI KUMWONA YESU WALA KUMTAMBUA!! OKOKA UWE
SALAMA!
13) "9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu
hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi
kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu."
(1 Yohana 3:9)
>> UKIZALIWA MARA YA PILI/UKIOKOKA (YOH 3:3-7 & TITO 3:3-7) 1)
HUTENDI DHAMBI, NA 2) HUWEZI KUTENDA DHAMBI, KWA SABABU 1) MBEGU
TAKATIFU YA MUNGU IMO NDANI YAKO, 2) UMEZALIWA NA MUNGU MWENYEWE, NA
SASA WEWE NI MTAKATIFU, MWANA WA MUNGU!!
14) "16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu." (1 Petro 1:16)
>> MAPENZI YA MUNGU NI KWA WOTE WALIO WAKE WAWE WATAKATIFU, KWA KUWA YEYE NI MTAKATIFU
>> KUTOKUWA MTAKATIFU NI UASI, NI UBISHI, NI UKAIDI, NI KIBURI, NA
NI UOVU!! UNAPINGANA NA MUNGU KWA KUTENDA DHAMBI??!!! UTASTAHIMILI
GHADHABU YAKE??!!
"Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi
wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. (Rum1:18)
15) "3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili," (Warumi 1:3) NA TENA,
"4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya
utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;" (Warumi 1:4)
>> UKIMWAMINI YESU, ATAACHILIA UWEZA WAKE KWAKO, ULIOMFANYA YEYE
KUWA MWANA WA MUNGU, KWA JINSI YA ROHO YA UTAKATIFU, KWA KUFUFUKA KUTOKA
KWA WAFU
>> UWEZA HUO ULIOMFUFUA YESU, UTAKUPA WEWE roho mpya ya utakatifu KWA KUKUFUA TOKA MAUTINI KIROHO ILI UWE MTAKATIFU KAMA YEYE!
16) 1 Wakorintho 15:45 (NLT)
The Scriptures tell us, “The first man, Adam, became a living person.”
But the last Adam—that is, Christ—is a life-giving Spirit."["Mtu wa
kwanza, Adamu, akawa nafsi hai." Lakini Adamu wa mwisho-yaani, Kristo-ni
Roho anayehuisha/anayetia uzima/uhai/maisha]
>> UKITUBU DHAMBI ZAKO, UKAMWAMINI YESU, NA KUMPOKEA MOYONI MWAKO
AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO; YEYE ATAINGIA KAMA ROHO, ATAKAYEKUPA WEWE
ROHONI MWAKO MAISHA YAKE YA UTAKATIFU, KUPITIA NGUVU ZAKE ZILIZOMFUFUA
KUTOKA KWA WAFU!!
17) Utakatifu ni roho! MUNGU NI ROHO (Yoh
4:24), na pia MUNGU NI MTAKATIFU (Walawi 11:45 & 19:2)! Hivyo Mungu
ni ROHO MTAKATIFU!!! WEWE UMWAMINIPO YESU roho YAKO INAHUISHWA NA
KUFANYWA UPYA (RE-CREATED) NA ROHO MTAKATIFU ILI UFANYIKE MWANA, KWA
KUPEWA roho mpya ya utakatifu, UNAPOFUFULIWA KUTOKA MAUTI YA KIROHO KWA
KUSAMEHEWA NA KUONDOLEWA DHAMBI ZAKO! Unazaliwa mara ya pili ukiwa
mtakatifu, kwa uweza wa Roho Mtakatifu! Ndipo unaishi maisha ya
utakatifu, kwa nguvu za Mungu, ndani yake Yesu uliyemwamini!
18) Ukristo ni roho ya utakatifu ndani
yako baada ya kuzaliwa mara ya pili, iliyoungana na Roho wa Kristo
uliyemwamini na kumpokea moyoni mwako (1 Kor 6:17), na maisha ya
utakatifu ya Kristo akaaye ndani yako na kutenda kazi kwa Roho wake huyo
Mtakatifu na nguvu zake! UKRISTO NI MAISHA YA KULITENDA NENO LA MUNGU
(Yakobo 1:22), LAKINI SI KWA UWEZA WALA NGUVU ZAKO, BALI NI KWA ROHO
MTAKATIFU (ZACHARIA 4:6)! UKRISTO NI KUISHI NA KUENENDA KWA ROHO
MTAKATIFU (GAL 5:16, 25) UKRISTO NI UTAKATIFU, UPENDO, NA UTUKUFU WA
MUNGU NDANI YA MWAMINI!!
19) Mtu ni Mtakatifu kwa sababu ya roho ya
utakatifu iliyo ndani yake, inayomuongoza kuishi maisha matakatifu ya
Kristo yaliyomo kwenye Neno lake, kwa nguvu za Roho Mtakatifu wa Kristo,
aishiye ndani yake aliyempokea alipookoka na kubatizwa kwenye maji
mengi!!
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu
Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho
Mtakatifu.
(Matendo ya Mitume 2:38)
20) 2 akawauliza, JE! MLIPOKEA ROHO
MTAKATIFU MLIPOAMINI? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho
Mtakatifu hatukusikia.
Matendo ya Mitume 19:2
>> WEWE UNAYESEMA NI MKRISTO JE! ULIPOKEA ROHO MTAKATIFU ULIPOAMINI/ULIPOOKOKA??!!
>> ALIYEOKOKA YUMO KWENYE MPANGO WA MUNGU WA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU!!
>> HII NI KWA SABABU ROHO MTAKATIFU NDIYE ROHO WA UKRISTO!! MAANA
UKRISTO HAUPO BILA NGUVU ZA ROHO HUYU AMBAZO, PAMOJA NA MENGINE, NI
NGUVU ZA UTAKATIFU!