MUME ADAMU AMESHINDWA UCHUNGAJI

 


MUME ADAMU AMESHINDWA UCHUNGAJI

Tumekuwa tukisisitiza kuwa Mume kwenye Ndoa Takatifu ni Mchungaji wa Kanisa la ndoa!! Uchungaji anaoufanya ni kwa mkewe na pia kwenye Kanisa la Familia ambalo lina watoto walioko "viunoni mwake!" Yeye ni mume, ni baba, ni kiongozi, na pia ni msimamizi!! Kama mchungaji Mume kwenye ndoa takatifu lazima afanye kile Yesu, Mchungaji Mwema, alichomwagiza Petro:

John 21:15-17
[15]So when they had dined, Jesus saith to Simon Peter, Simon, son of Jonas, lovest thou me more than these? He saith unto him, Yea, Lord; thou knowest that I love thee. He saith unto him, Feed my lambs.
Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
[16]He saith to him again the second time, Simon, son of Jonas, lovest thou me? He saith unto him, Yea, Lord; thou knowest that I love thee. He saith unto him, Feed my sheep.
Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, CHUNGA KONDOO ZANGU.
[17]He saith unto him the third time, Simon, son of Jonas, lovest thou me? Peter was grieved because he said unto him the third time, Lovest thou me? And he said unto him, Lord, thou knowest all things; thou knowest that I love thee. Jesus saith unto him, Feed my sheep.
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, LISHA KONDOO ZANGU.

>> MUME LAZIMA UMPENDE YESU KULIKO MKEO, NA WANAO, NA WATU WOTE!! Upendo wako LAZIMA UWE MKUBWA SANA KWA YESU KULIKO KWA MWANADAMU YEYOTE MWINGINE, AMA KITU CHOCHOTE KINGINE!! Yesu awe ndiye PENDO KUU LA MOYO WAKO!! HII ndiyo sifa ambayo itakufanya ufae na ustahili KUWA MCHUNGAJI WA KANISA LA NYUMBANI LENYE MAKANISA YA MSINGI MAWILI, AMBAYO NI KANISA LA NDOA NA KANISA LA FAMILIA!! Pendo lako kwa Yesu lisipozidi pendo lako kwa mkeo, wanao, nduguzo, n.k. HUWEZI KUMPENDEZA MUNGU NA HUFAI KUCHUNGA WATU WAKE MAANA ZILE NYAKATI ZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UOVU HUTAFANYA HIVYO, HUTAKUWA MCHA MUNGU MAANA ZIKO NYAKATI UTAFUMBIA MACHO UOVU! LAKINI PIA ZIKO NYAKATI UTACHAGUA KUWAPENDEZA WANADAMU KULIKO YESU, NA PIA ZIKO NYAKATI UTATAFUTA UTUKUFU WA WANADAMU KULIKO UTUKUFU WA KRISTO YESU BWANA MAANA UPENDO WAKO KWA YESU HAUJAKAMILIKA!! YAANI, MOYO WAKO HAUJAKAMILIKA KATIKA PENDO MBELE ZAKE MAANA MOYONI UMEWAWEKA WANADAMU MAHALA PA YESU!! "Petro unanipenda kuliko hawa wote??!!"

23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. (Yohana 14:23)
>> UKIWAPENDA WATU AU CHOCHOTE KINGINE KULIKO YESU, MFANO, FEDHA, HUWEZI KULISHIKA NENO LAKE!! LAZIMA KUNA NYAKATI UTAMWACHA YESU KWA KULIACHA NENO LAKE!!
12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho.
1 Samweli 3:12
13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.
1 Samweli 3:13

>> Kuhani Eli aliwapenda na kuwaheshimu wanawe kuliko Bwana Mungu Mwenyezi!! Akajiletea maangamizo ya Yeye na wanawe hao hasira ya Bwana ilipowaka dhidi yao (1 Samueli 2: 12-17, 22-36)
>> Sauli naye alimwacha Yesu kwa kuliacha Neno!!
 

22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
1 Samweli 15:22

23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; KWA KUWA  UMELIKATAA NENO LA BWANA, YEYE NAYE AMEKUKATAA WEWE USIWE MFALME.
1 Samweli 15:23

>> Sauli, ukisoma habari hii, alikiuka maagizo ya Bwana, akafanya vile alivyoona yeye mwenyewe kuwa ni vema kinyume na Neno la Bwana! Dhambi ni uasi (1 Yohana 3:4), na hapa Mungu anasema KUASI NI KAMA DHAMBI YA UCHAWI!! UNAPOASI NENO LA MUNGU HAUNA TOFAUTI YEYOTE NA MCHAWI!! Sauli na mwanawe Yonathani walikufa vitani KWA SABABU YA KULIASI NENO LA BWANA! Kuhani Eli na wanawe wawili walikufa kwa siku moja! Wanawe walikufa vitani, na yeye alianguka na kuvunjika shingo alipopata habari mbaya za kutekwa sanduku la Bwana na kufa kwa wanawe!!
24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. (Yohana 14:24)
>> >> UPENDO WA YESU UNAPIMWA KWA JINSI GANI UNALISHIKA NENO KWENYE MAISHA NA HUDUMA YAKO!!! Yaani, SIYO KWA KUSOMA MAANDIKO TU! SIYO KWA KUKARIRI MAANDIKO TU! SIYO KWA KUSOMA BIBLIA TU! BALI NI KWA KULITENDA NENO!! Yesu aliuliza, "46 Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?"(Luka 6:46)
>> KAMA UNAMPENDA YESU UTATENDA YOTE ASEMAYO!! KAMA UNAMCHUKIA YESU HAUTAYATENDA YALE YESU ASEMAYO!
>> Maisha ya Upendo wa Mungu ni maisha ya kulitenda Neno!!! Ni maisha ya kufanya yote asemayo Yesu! Biblia inasema Mungu ni Upendo (1 Yohana 4:8) na hivyo kumtii Mungu ni kumtii Upendo! Mungu ni Neno (Yohana 1:1) na hivyo kulishika Neno ni kumshika Upendo, na ndiko kuushika upendo moyoni na kinywani mwako, na kuenenda kwa huo!

15 Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
Yohana 21:15

>> MCHUNGAJI KAMA UNAMPENDA YESU UTALISHA WANA-KONDOO WAKE!! Chakula anatoa Yesu!! Yeye alisema, 27 Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho MWANA WA ADAMU ATAWAPA, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. (Yohana 6:27)
>> BWANA WETU YESU NDIYE ANAYETOA CHAKULA CHA UZIMA CHENYE KUWAFAA 1) WANA-KONDOO, NA 2) KONDOO, KUPITIA MCHUNGAJI MWEMA WA KONDOO

>> Sasa tukirudi kwa mchungaji Adamu, tunamuona akipokea Neno la Mungu kuhusu "maisha bustanini"!!

15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 2:15

16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
Mwanzo 2:16

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 2:17

>> HILI NI NENO LA BWANA KWA KIONGOZI NA MTUMISHI WAKE ALIYEMWEKA BUSTANINI "KUILIMA NA KUITUNZA!" (Mwanzo 2:15) Adamu amepewa majukumu ya kufanya kwa Neno la Mungu, na kisha akaambiwa Neno la Mungu kuhusu jinsi gani ataishi bustanini!! Ndipo mstari wa 18 Mungu anaanza kumuumba mwanamke kwa Neno lake pia! Katika Neno aliloambiwa Adamu msisitizo ulikuwa wazi!!
1) MATUNDA YA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA 'USILE'
2) KWA MAANA SIKU UTAKAPOKULA MATUNDA YA MTI HUO, "UTAKUFA HAKIKA!!!"
Baada ya hapo mkewe akaumbwa na kuletwa kwake! (Mwanzo 2: 18, 21-25)! Ni dhahiri Adamu ndiye aliyemwambia Neno la Bwana mkewe maana sura ya tatu inaanza na habari za nyoka jinsi alivyokuwa mwerevu na alivyomdanganya mwanamke! Isitoshe, Mungu alishasema MWANAMKE NI MSAIDIZI ANAYEFANANA NA MWANAMUME!! Mungu ALIUMBA MSAIDIZI MWANAMKE!! Ulimwengu wote ulitokana na ndoa!! Kanisa limeanzia kwenye ndoa! Taifa limezaliwa na ndoa!! KATIKA YOTE HAYA MUNGU ALIKUSUDIA NA AMESEMA MWANAMKE NI MSAIDIZI WA MWANAMUME!! Dunia imegeuza hili Neno kwa ushawishi wa shetani (nyoka-Mwanzo 3) na kumpa mwanamke uongozi!!! Kuasi Neno ni kama dhambi ya uchawi (1 Samuel 15:23)
>> ADAMU, ALIKUWA AKIKUMBUKA VEMA NENO LA MUNGU!! NA NDIYO MAANA ALIMWAMBIA MKEWE NENO HILO, NA MWANAMKE ALIPOJIBIZANA NA NYOKA, ALIONYESHA KUWA ANALIJUA NENO HILO, INGAWA ALIAMUA KULIACHA, KULIPUUZA, NA KULIASI!!

6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi ALITWAA KATIKA MATUNDA YAKE AKALA, AKAMPA NA MUMEWE, NAYE AKALA.
Mwanzo 3:6

>> Hapa mwanamke ameshadanganywa akadanganyika na kulitendea kazi neno la nyoka!! Usipolitendea kazi neno la Mungu lazima utalitendea kazi neno la "nyoka" maishani mwako, maana uliumbwa kwa Neno, na ukapangiliwa (programmed) kutenda kazi kwa Neno! Hivyo roho yako inahitaji kupokea kutoka ama kwa Mungu Aliye Roho, au shetani (roho ya uasi!) Mabaya yote duniani yalizaliwa na uasi wa Kweli maana Mungu aliona kuwa kila kitu alichokiumba, tazama, NI CHEMA SANA!! (Mwanzo 1:31)
  Hapa kwenye Mwanzo 3:6 tunaona:

>> MWANAMKE ALITWAA KATIKA YALE MATUNDA, AKALA
>> KISHA AKAMPA NA MUMEWE, NAYE AKALA!!
1) Adamu, hali akijua matunda yale wamekatazwa kuyala, AKAYAPOKEA KUTOKA KWA MKEWE, NA KISHA KUYALA!!
2) Adamu anakubaliana na uasi wa mkewe!
3) Adamu anaridhia uasi wa mkewe!
4) Adamu anashindwa kukemea na kukaripia uasi wa mkewe!
5) Adamu anayaonea haya maneno ya Mungu kwa sababu ya mkewe
6) Adamu analiacha Neno la Mungu (anashindwa kulishika!) lianguke chini!!
7) Adamu anawaheshimu wanadamu kuliko Mungu na Neno lake
8) Adamu anapoteza "kicho" chake cha Bwana, anaacha kumcha Mungu kwa kuufumbia macho uovu wa mkewe!!
9) Adamu anamuasi Mungu na kumkaribisha nyoka moyoni na maishani mwake!
10) Adamu anajitia chini ya utawala na mamlaka ya shetani kwa kulikataa Neno la Mungu, na kulitii Neno la nyoka (shetani)
11) Adamu anapoteza nafasi yake kama mchungaji, kiongozi, na kichwa cha mkewe na wanawe (ulimwengu) waliomo viunoni mwake, maana ANAFARAKANA NA MUNGU ALIYE ROHO, NA KUJIUNGAMANISHA NA roho ya shetani ya mpinga Kristo/roho ya uasi/roho ya ukengeufu/roho idanganyayo/roho ya upotevu/roho ya dhambi!!
12) Adamu anapoteza kule kufanana na Mungu, na sasa anafanana na shetani aliyempokea moyoni mwake na anayemtii! Kwa kuwa roho ya shetani imeungana na roho yake Adamu, na kuchukua sura na mfano wake!
>> Ndiyo maana alipoteza utukufu wa Mungu na kubaki "uchi!!"

7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Mwanzo 3:7

>> WAKAFUMBULIWA MACHO YA MWILINI YASIYO NA UTUKUFU WA MUNGU!! Yaani, ndoa ikapoteza lile vazi la utukufu!! Yule Roho wa Utukufu akaondoka, nao wakabaki watu tu wa mwilini!
>> Yale macho ya utukufu yaliyokuwa yakimwona Mungu yakafumbwa!! Jicho la hekima, na la maarifa, na la ufahamu, na la shauri, na la kicho, na la uweza/nguvu, na la ufunuo YAKATIWA GIZA!! Giza la shetani likaingia!!
>> Hawamuoni Mungu na hivyo wanaanza maisha ya kujitegemea/kujitumainia, kujitetea, kujisumbukia wenyewe, kujihangaikia, na kujipigania WAO WENYEWE PASIPO MSAADA WA MUNGU! ("... wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo." )

Nisiingie huko sana maana hilo ni somo lingine, bali sasa tumrudie mchungaji Adamu bustanini: maandiko yanasema kwa habari ya mchungaji mwema;
11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. (Yohana 10:11)

12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.
(Yohana 10:12)

13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. (Yohana 10:13)
>> Adamu alikuwa kipofu na hakuweza kumuona shetani tangu mbali kwamba atakuja kushambulia "ndoa" yake!!
>> Kama umeutoa uhai wako kwa ajili ya mkeo maana yake UKO TAYARI KUUWAWA KWA AJILI YAKE!! Huu ndio Upendo wa Mungu:
16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. (1 Yohana 3:16)
>> KAMA UMELIFAHAMU PENDO KWAMBA YESU ALIUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YAKO, UTAJUA KWAMBA NI LAZIMA NA WEWE UUTOE UHAI WAKO KWA AJILI YA UWAPENDAO!! NAWE UTAFANYA HIVYO KWA FURAHA!!
>> Mungu akiona moyo wako umejaa pendo lake ATAKUFUMBUA MACHO SABA YA UPENDO UPATE KUONA JINSI YA KUWAHUDUMIA/KUWALINDA/KUWAPIGANIA/KUWATETEA/KUWAOKOA/KUWATENDEA MEMA UWAPENDAO, N.K.
>> HUWEZI KUUTOA UHAI WAKO KWA AJILI YA MWINGINE PASIPO YESU KUWA NDANI YAKO!!
>> YESU AKIWA NDANI YAKO UTAONA KWA MACHO YA UPENDO KAMA MCHUNGAJI MWEMA WA KANISA LA NYUMBANI MWAKO, NA KANISA LA MAHALI PAMOJA!!
>> Macho haya ni macho ya moyoni ambapo wewe na mkeo mlio mwili mmoja mnapewa kuona kwa upendo! Mume hakuna hatari au baya kwa mkewe ambalo hataliona tangia mbali!! Na mke naye, halikadhalika, hakuna baya au hatari, ambayo hataiona kuhusu mumewe tangu ikiwa mbali!!
22 Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? KWA MAANA BWANA AMEUMBA JAMBO JIPYA DUNIANI; MWANAMKE ATAMLINDA MWANAMUME. (Yeremia 31:22)
>> ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAYEFUNUA MAMBO YA SIRI YOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KWA WOTE WAMPENDAO BWANA WETU YESU!!
10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
1 Wakorintho 2:10

12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
1 Wakorintho 2:12

>> ADAMU HAKUSIMAMA KATIKA ZAMU YAKE YA ULINZI KAMA ALIVYOFANYA HABAKUKI:

1 Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.
Habakuki 2:1

2 Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
Habakuki 2:2

>> "1 Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu."
Habakuki 2:1
1) Nitasimama katika zamu yangu
2) Nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia nione atakaloniambia
3) Na jinsi nitakavyojibu katika hali ya kulalamika kwangu!!

"2 Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji."
Habakuki 2:2
>> BWANA AKANIJIBU AKASEMA...
>> IANDIKE NJOZI KWENYE VIBAO ISOMEKE WAZI WAZI...
Habakuki alisimama katika zamu yake mbele za Bwana Mungu Mwenyezi! Na Mungu akasema naye na kumfunulia mpango na makusudi yake kwa siku zijazo katika maono na njozi!! Biblia inasema, kwa habari ya zama hizi tulizonazo, kwamba;
 "13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake."
Yohana 16:13

>> UKIISHI NA KUENENDA KWA ROHO, YEYE ATAKUPASHA HABARI ZA MAMBO YAJAYO!!
>> MUME MCHUNGAJI LAZIMA UWE NA TAARIFA ZA MKE NA WANAO, KUTOKA KWA BWANA, ZA SIKU ZIJAZO!!!
>> Mchungaji Adamu hakuwa katika zamu yake kiroho na hivyo alishindwa jukumu lake la uchungaji katika roho; na ndipo ikaja roho ya shetani (nyoka) ikamdanganya mkewe!
>> Mchungaji Adamu alishindwa zaidi kwenye jukumu lake pale alipoona kwenye mwili (maana hakuona katika roho) kwamba mama mchungaji Hawa amechuma na kula matunda waliyokatazwa kwa Neno la Bwana, na hivyo kumuasi Mungu, lakini bado akashindwa kufanya huduma ya upatanishi
1) Kukataa kuyapokea matunda yale, na kumweleza mkewe kwamba ametenda dhambi na lazima atubu!
2) Kisha kwa kumuombea rehema mkewe mbele za Mungu
3) Kisha kuomba neema ya Mungu awasaidie kuishi kwa unyenyekevu, utii, na hofu ya Mungu bustanini!!
>> Hapo mchungaji Adamu angekuwa ameiponya familia yake yote! Yaani, mkewe Hawa, wanawe aliokuwa amewabeba viunoni mwake ambao ni ulimwengu wote! (sisi sote wanadamu)
>> Hivi hivi ndivyo shetani anavyoingia makanisani kupitia ndoa pale akina mchungaji na askofu "Adamu" na wake zao akina "Hawa" wanapoasi na kuondokewa na utukufu wa Mungu, na kujikuta wako uchi!! Makundi wanayoyachunga yanaingia matatizoni kupitia "watumishi" walioiacha Kweli!!
6 Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, WACHUNGAJI WAO WAMEWAPOTEZA; WAMEWAPOTOSHA MILIMANI; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Yeremia 50:6

>> Mchungaji Adamu alimpoteza mkewe kwa kushindwa kusimama kwenye zamu yake na pengine angemwokoa!!
>> Mbaya zaidi mchungaji Adamu hakuwa na moyo wa kujutia makosa na dhambi zake na hivyo hakutubu!! Mungu alimuuliza swali ambalo lililenga kumpa nafasi ya kutubu, lakini hakufanya hivyo akaanza kujitetea na kujihesabia haki kuliko hata Mungu!!
9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
Mwanzo 3:9

10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Mwanzo 3:10

11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Mwanzo 3:11

12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
Mwanzo 3:12

>> MST 10 hofu ya adhabu imewaingia/wametoka kwenye uwepo wa Mungu/hawatamani tena kuingia uweponi mwake/wanaona bora wasikutane na wakae mbali na Mungu Mtakatifu/hivyo wamejificha, ingawa Mungu anawaona!/dhambi imewakimbiza toka uweponi mwa Mungu!
>> MST 12. (1) ADAMU ANAMTIA MUNGU HATIANI, KWAMBA AMEMLETEA MWANAMKE ALIYESABABISHA YEYE ATENDE DHAMBI (2) MWANAMKE NDIYE ALIYEANZISHA NA NDIYE ALIYEMPA MATUNDA YALE AYALE!! (3) AKASHINDWA KUTUBIA UOVU WAKE!!
>> Anguko likakamilika kwa adhabu kutolewa palipokosekana toba ya mchungaji Adamu!!
>> Ndoa za Anguko zimejaa kujihesabia haki na kumuona "mwenzi wako" kuwa ndiye mwenye tatizo/matatizo, lakini kamwe hugusi wala huzungumzii matatizo yako mwenyewe!!
>> Wachungaji walioasi kama Adamu sikuzote wanawalalamikia washirika kuwa ndio wenye matatizo!! Wanasahau imeandikwa:
Hosea 4:9
[9]And there shall be, like people, like priest: and I will punish them for their ways, and reward them their doings.
Hata itakuwa, kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani; nami nitawaadhibu kwa ajili ya njia zao, na kuwalipa kwa matendo yao.

>> roho ya kuhani ndiyo roho iliyo ndani ya watu wake anaowaongoza kiroho
>> kiongozi wa kiroho anaongoza na kuchunga roho za watu!
>> ndiyo maana analisha roho zao kwa chakula cha kiroho alichopewa na mwajiri wake Yesu! Au shetani kama amemuacha Yesu!! Hii ni sheria ya urithi wa kiroho TAZ SOMO HILI ambalo ni agano pia! Watoto wako uliowazaa kiroho na unaowalisha kiroho watakuwa na roho iliyo ndani yako!
-mchungaji shoga atakuwa na washirika wengi mashoga!!
-mchungaji mpenda fedha atakuwa na washirika wapenda fedha
-mchungaji anayeipenda dunia atakuwa na washirika wanaoipenda dunia
-mchungaji mpenda anasa atakuwa na washirika wapenda anasa
-mchungaji mwenye ndoa ya anguko atakuwa na washirika wengi wenye matatizo ya ndoa, n.k. Yesu alisema mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, bali yamtosha kuwa kama mwalimu wake (Mathayo 10:25)
>> KAMA AMBAVYO ADAMU HAKUWA SAHIHI KUMLAUMU MKEWE NA KUMSINGIZIA KUWA YEYE NDIYE MWENYE TATIZO NA ALIYEANZISHA TATIZO, VIVYO HIVYO NDIVYO SIYO SAHIHI KWA MCHUNGAJI YEYOTE KULAUMU NA KUSINGIZIA WASHIRIKA KUWA NDIO WENYE MATATIZO!! HUO NI USHAHIDI KWAMBA AMESHINDWA NA AMEANGUKA KUTOKA KWENYE UCHUNGAJI/UONGOZI WA KIROHO!!
>> Paulo aliwazaa Wakorintho kiroho! Walipotenda dhambi aliwakemea kwa ukali kwenye waraka wa Wakorintho wa kwanza!! Na barua yake ilileta matokeo mazuri ya toba!!
8 Kwa sababu, ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule, sijuti; hata ikiwa nalijuta, naona ya kwamba waraka ule uliwahuzunisha, ingawa ni kwa kitambo tu.
2 Wakorintho 7:8

9 Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.
2 Wakorintho 7:9

10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
2 Wakorintho 7:10

11 Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.  2  Wakorintho 7:11
>> Yesu alisema WALIO WA MUNGU HUYASIKIA MANENO YA MUNGU, NA KUYAAMINI, NA KUYAPOKEA, NA KUYASHIKA, NA KUYATENDA!!

43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu.
Yohana 8:43

47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
Yohana 8:47

Kwa leo tuishie hapa! Ubarikiwe sana, tutaendelea tukijaliwa na kupata kibali kwa Bwana!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post