HIZI NI STATUS ZA WHATSAPP KAMA ZILIVYOCHUKULIWA KWENYE SIMU YA MKONONI PASIPO KUREKEBISHWA (UNEDITED) KUHUSU MTAKATIFU
[06:10,
3/12/2023] Jesus Is Lord: 3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu
Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa
roho, ndani yake Kristo; (Waefeso 1:3)
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya
ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika
pendo. (Waefeso 1:4)
>> MKRISTO NI YULE ALIYECHAGULIWA NDANI YA KRISTO YESU TANGU KABLA
YA KUUMBWA ULIMWENGU ILI "AWE MTAKATIFU ASIYE NA HATIA MBELE ZAKE MUNGU
KATIKA PENDO!!"
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 4 kama vile alivyotuchagua katika yeye
kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio
na hatia mbele zake katika pendo. (Waefeso 1:4)
>> MUNGU ALIKUSUDIA KUUMBA MWANADAMU MTAKATIFU ASIYE, NA ASIYEWEZA, KUTENDA DHAMBI!
>> MWANADAMU AKAANGUKA DHAMBINI ALIPOMUASI MUNGU PALE ALIPODANGANYWA NAME SHETANI
>> SULUHISHO LIKAWA NI KUMTUMA YESU (NENO LAKE) ULIMWENGUNI, ILI
KILA ATAKAYEMWAMINI, AKAE NDANI YAKE AKIWA MTAKATIFU ASIYE NA HATIA
YOYOTE MBELE ZA MUNGU!!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye (YESU)
alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
(1 Yohana 3:5)
>> YESU ALIKUJA ULIMWENGUNI KAMA "SADAKA YA DHAMBI" ILI KWA DHABIHU YA NAFSI YAKE AFANYE UPATANISHO WA DHAMBI!
>> YESU NDIYE ALIYEICHUKUA DHAMBI YA ULIMWENGU KATIKA MWILI WAKE PALE JUU MSALABANI
29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
(Yohana 1:29)
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye (YESU)
alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
(1 Yohana 3:5)
1) YESU HAKUTENDA DHAMBI, 2) YESU ALIISHINDA DHAMBI, 3) YESU ALIIBEBA
DHAMBI YA ULIMWENGU PALE JUU MSALABANI, 4) YESU ALIISTAHIMILI HUKUMU YA
DHAMBI ZETU PALE MSALABANI ILI KUTUEPUSHA SISI NA GHADHABU YA MUNGU
ITAKAYOKUJA! 5) YESU ALIFANYA UPATANISHO WA DHAMBI ZA ULIMWENGU KWA DAMU
YAKE MWENYEWE! 6) ALIUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YETU, AKICHUKUA MAHALI
PETU SISI! 7) GHADHABU YA MUNGU IKAWA IMETIMIZWA KWAKE YEYE BADALA YETU
SISI!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 6 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna
nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.
(Warumi 5:6)
8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa
Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
(Warumi 5:8)
10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya
Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima
wake. (Warumi 5:10)
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
(1 Petro 2:22)
24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti,
tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa
kupigwa kwake mliponywa. (1 Petro 2:24)
>> YEYE YESU HAKUTENDA DHAMBI NA HIVYO HAKUSTAHILI KUFA MAANA IMEANDIKWA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI (RUM 6:23)
>> ALIZICHUKUA DHAMBI ZETU AKAZIGONGOMELEA MSALABANI MAANA YEYE MWENYEWE ALIFANYWA KUWA DHAMBI YA ULIMWENGU (2 KOR 5:21)
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 18 Lakini vyote pia vyatokana na
Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa
huduma ya upatanisho; (2 Kor 5:18)
>> Mungu Aliye Roho (Yoh 4:24) alitupatanisha watenda dhambi wote
kupitia damu yake mwenyewe aliyoimwaga kwa njia ya Kristo Yesu Mwokozi
wetu!
>> Sisi tunapokea huo upatanisho kwa NJIA YA KUMWAMINI TU YESU
AMBAYE AMELIPA DENI LA DHAMBI ZETU LOTE!! TUNAAMINI KAZI YA MSALABA
ILIYOKAMILIKA NA TUNAPOKEA MSAMAHA WA DHAMBI ZETU BURE TUNAPOMWAMINI
YESU!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: Hatuokoki au kuhesabiwa haki kwa kuwa
TUNAFUNGA, TUNASALI, TUNAHUDHURIA IBADA, TUNATOA SADAKA, TUNATOA
MICHANGO, TUNATOA ZAKA, TUNASAIDIA MASKINI NA WAHITAJI, N.K. BALI
TUNAOKOKA KWA NEEMA KWA NJIA YA IMANI!! " 8 Kwa maana mmeokolewa kwa
neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni
kipawa cha Mungu;
(Waefeso 2:8)
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. (Waefeso 2:9)
>> WOKOVU AU KUHESABIWA HAKI HAKUPATIKANI KWA MATENDO MEMA AU MATENDO YA HAKI, "BALI KWA KUMWAMINI TU YESU!!"
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa
hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na
anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na
kuchukiana. (Tito 3:3)
4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
(Tito 3:4)
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema
yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho
Mtakatifu; (Tito 3:5)
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
(Tito 3:4)
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema
yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho
Mtakatifu; (Tito 3:5)
>> TUNAOKOLEWA KWA SABABU TU YA HURUMA, UPENDO, NA WEMA WAKE MUNGU NA KAMWE HATUKUSTAHILI!!
>> HUWEZI KUTENDA WEMA WOWOTE AU MEMA YOYOTE ILI UOKOKE, BALI
IMANI YAKO KWA YESU HUPELEKEA WEWE KUPOKEA NEEMA YA WOKOVU BURE!!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; (Tito2:11)
><UNAPOMWAMINI YESU NA KUMPOKEA AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO, MUNGU
ANAKUPA NEEMA YAKE BURE YA MSAMAHA WA DHAMBI ZAKO ZOTE, KUHESABIWA HAKI,
NA KUPOKEA UZIMA WA MILELE!!
>> WOKOVU NI ZAWADI YA MUNGU KWA WATU WOTE WATAKAOMWAMINI YESU NA
KUMPA MAISHA YAO AYATAWALE NA KUYAONGOZA KWA ROHO WAKE MTAKATIFU! WOKOVU
HAUTENDEWI KAZI (IS NOT EARNED) KWA JUHUDI ZA KIBINADAMU BALI
UNAPOKELEWA KWA KUMWAMINI YESU TU!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye
ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi;
ampokea yeye aliyenipeleka. (Yohana 13:20)
>> KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO KWA IMANI NDIKO KUPOKEA UTAKATIFU, AU WOKOVU NA YOTE YATOKANANAO!
>> UTAKATIFU NI NEEMA YA MUNGU KWA NJIA KRISTO YESU!
>> UKIAMINI, UNAPOKEA NEEMA YA UTAKATIFU, NA NEEMA YA UTAKASO KWA
NJIA YA KWELI KWENYE MAISHA YAKO YA KILA SIKU! BAADA YA KUOKOKA MAISHA
YOTE UNAISHI KWA NEEMA YAKE KRISTO!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; (Tito2:11)
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi
kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; (Tito 2:12)
>> WATAKATIFU TUMEPEWA NEEMA NA TUNAISHI KWA NEEMA HIYO! NEEMA YA
MUNGU INATUWEZESHA KUISHI MAISHA MATAKATIFU SIKU ZOTE PASIPO KUWA NA
LAWAMA YOYOTE MBELE ZAKE!! " 4 kama vile alivyotuchagua katika yeye
kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio
na hatia mbele zake katika pendo."(Waefeso 1:4)
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na
watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao; (Waebrania 12:14)
>> UTAKATIFU HAUTAFUTWI KWA MATENDO YA HAKI AU MATENDO MEMA YOYOTE!!
>> UTAKATIFU UNAPATIKANA KWA NEEMA KWA NJIA YA IMANI YA YESU!
KADIRI UNAVYOMWAMINI YESU UNAPOKEA NEEMA YAKE YA KUYATENDA MAPENZI YAKE
YOTE KAMA YALIVYOFUNULIWA KWENYE NENO LAKE!
>> MTAKATIFU ANAWEZESHWA KWA UWEZO WOTE KUISHI SAWA NA NENO LA KRISTO!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: 1) MTAKATIFU KWANZA AMEHESABIWA HAKI
BURE KWA NEEMA KWA KUMWAMINI YESU! MTAKATIFU ANAMWAMINI YESU SIKUZOTE!
2) KULE KUMWAMINI MAANA YAKE ANAMTEGEMEA NA KUMTUMAINI KABISA KWA MAMBO
YOTE, ANAMPENDA, ANAMHESHIMU, ANA USHIRIKA NAYE KILA WAKATI, ANAZUNGUMZA
NAYE KILA WAKATI, ANAMSIKILIZA YESU WAKATI WOTE NA KUYAFANYA YOTE
AYASEMAYO, MTAKATIFU ANAISHI KWA UNYENYEKEVU, UTII, NA KICHO VYA KRISTO
YESU ALIYE NDANI YAKE KWA ROHO WAKE MTAKATIFU!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: >> MTAKATIFU ANAWEZESHWA NA ROHO MTAKATIFU KUITII KWELI YOTE AMBAYO NI NENO LA MUNGU
>> MTAKATIFU HAIPENDI DUNIA HII MBOVU ILIYOHARIBIKA KWA DHAMBI,
TAMAA, UBAYA, NA UOVU KATIKA MIFUMO YAKE YOTE YA SIASA, SERIKALI NA
UONGOZI, DINI POTOFU, UCHUMI, BIASHARA, UTAMADUNI,SANAA, NDOA NA
FAMILIA, IMANI POTOFU, N.K. NAYE HUJITENGA NA KUJIEPUSHA NA roho
zinazowatawala na kuwatumikisha dhambini watenda dhambi wa dunia hii
wanaompendeza shetani, kumwabudu, na kumtumikia!! MTAKATIFU KWAKE NI
MBINGUNI
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: >> MTAKATIFU HATENDI DHAMBI,
ANACHUKIA DHAMBI, ANAJITENGA NA DHAMBI, HASHIRIKI KWENYE DHAMBI,
HASHAWISHIKI KWA DHAMBI KWA NAMNA YOYOTE!
>> MTAKATIFU NI RAFIKI WA ROHO MTAKATIFU! AMEJAA ROHO MTAKATIFU NA
IMANI! ANAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU, ANAMSIKILIZA NA KUMTII ROHO
MTAKATIFU, ANAISHI SAWASAWA NA NENO LA MUNGU KWA KUWEZESHWA NA ROHO
MTAKATIFU! MTAKATIFU ANAPOKEA NEEMA JUU YA NEEMA YA KRISTO KUTOKA KWA
HUYU ROHO WA NEEMA! MTAKATIFU ANAENENDA KWA ROHO SIKUZOTE!
[06:10, 3/12/2023] Jesus Is Lord: Anza maisha ya utakatifu kwa kusema
sala hii ukimaanisha kubadilika toka moyoni mwako uanze maisha mapya ya
kumpendeza Mungu: Sema;
"Ee Yesu, mimi ni mwenye dhambi! Siwezi kuziondoa dhambi zangu kwa
matendo yangu mwenyewe mema na ya haki! Nisamehe dhambi zangu Yesu!
Nioshe moyo wangu sasa Yesu! Nifanye kuwa kiumbe kipya Yesu! Niwezeshe
kuishi maisha ya utakatifu yanayokupendeza Yesu! Karibu moyoni mwangu
sasa Yesu! Mimi ni mwanao sasa Baba wa mbinguni! Asante kwa kuniokoa
Yesu! Tawala na ongoza maisha yangu yote Yesu! Amina"