UKIRI KUHUSU USEMI WA KINYWA CHANGU

                                 Free download Psalm 1914 Let the words of my mouth and the meditation of my  heart [960x960] for your Desktop, Mobile & Tablet | Explore 50+ Psalms 19  14 Wallpaper | F

UKIRI KUHUSU USEMI WA KINYWA CHANGU

 (MANENO YATOKAYO KINYWANI MWANGU)

Biblia  inasema Mungu aliumba ulimwengu na vyote viujazavyo kwa Neno la Kinywa chake!

“Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru ikasimama” (Zab 33:9)

-Mungu alisema Neno, ikawa kama alivyosema! Aliamuru iwe, ikawa kama alivyoamuru kwa kinywa chake!!! MUNGU NI MUUMBAJI, na pale Biblia inaposema sisi tuliumbwa kwa sura na mfano wake inamaanisha alitupa pia UWEZO, MAMLAKA NA NGUVU HII YA UUMBAJI KUPITIA VINYWA VYETU! MANENO YETU! Tukiwa upande wa Mungu tunaitumia mamlaka hii kwa mapenzi mema ya Mungu; na tukiwa watenda dhambi tunaitumia mamlaka hii kwa uharibifu, wizi na mauti!! Sasa kwa sisi tuliookoka eneo mojawapo tunalohitaji kulizingazatia pengine kuliko yote ni NINI TUNATAMKA KWA VINYWA VYETU KUHUSU MAISHA YETU NA JAMII YETU!!! Mungu alituumba katika Kristo Yesu ili tuishi na kuenenda kwa Imani!!! Ndiyo maana Paulo alisema,

“Lakini kwa kuwa tuna roho ileile ya Imani;kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini na kwa sababu hiyo twanena” (2 Kor 4:13)

-MUNGU AMETUPA ROHO YA IMANI NDANI YETU NA HIVYO; TUNANENA KILE TUNACHOAMINI NA TUNAPATA MATOKEO YAKE HAYO HAYO; HII HAIJALISHI TUNAJUA AU HATUJUI, MAISHA YETU NI SAWA SAWA NA VILE TULIVYOYATAMKA KWA KUWA VINYWA VYETU VINAUMBA MEMA AU MABAYA! ; TUNAPOTAMKA NENO LA MUNGU KWENYE HALI MBALIMBALI ZA MAISHA YETU TUNATENGENEZA HATMA YA MAISHA YETU WENYEWE SAWASAWA NA NENO LISEMAVYO: HAPA NIMEWEKA BAADHI TU KATI YA MAANDIKO MENGI MNO YA KWENYE BIBLIA TAKATIFU AMBAYO:

1) UKIYAAMINI, 2) UKAYAPOKEA, 3) UKAANZA KUYATENDEA KAZI, IKIWEMO KUYAKIRI, KUYATUMIA KWENYE MAOMBI, KUYATUMIA KWENYE KUKEMEA, KUYATUMIA KWENYE MATAMKO YA KIROHO YENYE MAMLAKA, KUYAIMBA, KUYATAFAKARI, NA KUTENDA SAWASAWA NA YASEMAVYO N.K LAZIMA WEWE MWENYEWE UTABADILIKA, WAPENDWA WAKO WATABADILIKA, MAISHA YAKO YATABADILIKA, NA KIUJUMLA MAISHA YAKO YATAKUWA NDANI YA MAMLAKA YAKO MWENYEWE SAWASAWA NA NENO LILIVYOSEMA!!! LAZIMA UKIRI MFULULIZO BILA KUKATA TAMAA AU KUWA MVIVU KWA WIKI, MIEZI NA HATA MIAKA MPAKA UONE MAMBO YAMEBADILIKA! HUU NI MOJA YA UFUNGUO WA UFALME WA MBINGUNI AMBAO WATOTO WA MUNGU WAMEPEWA NA BWANA YESU!!! TAFUTA MAANDIKO MENGINE KUHUSU NDOA YAKO, MKEO/MUMEO, KAZI YAKO, BIASHARA YAKO, KILIMO CHAKO, KAZI YA MIKONO YAKO, MASOMO YAKO, WAZAZI WAKO, WANAO, WALIMU WAKO, NDUGU ZAKO, MCHUNGAJI WAKO, KIROHO CHAKO, FEDHA ZAKO, MAHUSIANO YAKO, HUDUMA YAKO, WIZARA YAKO, VIONGOZI WA SERIKALI YAKO NGAZI ZOTE, TAIFA LAKO, NCHI YAKO, N.K MAJIBU YOTE YA MASWALI YAKO NA UTATUZI WOTE WA MATATIZO YAKO, NA YA WENGINE PIA,YAMO MOYONI MWAKO NA KINYWANI MWAKO!!!

“Lakini yanenaje? Lile Neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, lile neno la Imani tulihubirilo” (Rum 10:8)

Maandiko haya unayokwenda kuyasoma ndivyo Yesu alivyonena kwa uchache wake siku za mwili wake! Kwa kuwa andiko moja tu laweza kubadili maisha yako kabisa ukiliamini na kulitendea kazi kama ilivyoandikwa:

2 Tim 3:16 SUV

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki”

Utakapokuwa umeyashika maandiko haya, umeyakiri mwaka mzima, miaka miwili, mitatu n.k utakuwa moyo wako na kinywa chako VIMEJAA KRISTO YESU BWANA WETU katika nguvu na uweza wake wote!maana maandiko haya hukaa moyoni mwako kwa Imani KAMA roho! HIVYO UKIYAJAZA UTAKUWA UMEJAA ROHO!!!Kama Paulo alivyosema (Efeso 5:18)

  MANENO YA KINYWA CHANGU                           

.1)“………… .. nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili” (Efeso 6:18-19)

>>ASANTE BWANA YESU KWA KUNIJALIA USEMI NA KUNIFUMBUA KINYWA CHANGU, NA SASA NINAIHUBIRI KWA UJASIRI ILE SIRI YA INJILI

2) “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu,

Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.” (Zab 19:14)

>>ASANTE EE MUNGU BABA, KATIKA JINA LA YESU, KWA KUWA MANENO YOTE YA KINYWA CHANGU NA MAWAZO YOTE YA MOYO WANGU YAMEPATA KIBALI MBELE ZAKO EE BWANA.

3)ZABURI 141:3 SUV

Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.”

>>ASANTE BABA KATIKA JINA LA YESU KWA KUNIJALIA MLINZI KATIKA KINYWA CHANGU, NA MNGOJEZI MLANGONI PA MIDOMO YANGU SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU:HIVYO MANENO YA KINYWA CHANGU NI YALE YAKUPENDEZAYO WEWE SIKUZOTE.

4)MITHALI  8:8 SUV

Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.”

>>MANENO YOTE YA KINYWA CHANGU YANA HAKI; HAPANA HATA NENO MOJA LILILOPOTOKA AU LA UKAIDI SIKU ZOTE ZA KUISHI KWANGU.

5) “Mit 8:7 SUV

Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.

>>KINYWA CHANGU KINASEMA KWELI SIKUZOTE, NA UOVU NI CHUKIZO KWA MIDOMO YANGU MAISHA YANGU YOTE

6) “Roho ya BWANA ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu. (2 Sam 23:2)

   “Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu” (Math 10:20)

>>ROHO MTAKATIFU NDIYE ANENAYE NDANI YANGU SIKUZOTE, NA HII NDIYO MAANA NENO LA KRISTO LIKO KINYWANI MWANGU SIKUZOTE, WAKATI WOTE, NA KILA MAHALI.

7) “kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.”  (Luka 21:15)

>>BWANA YESU AMENIPA KINYWA NA HEKIMA AMBAYO WATESI WANGU WOTE HAWAWEZI KUSHINDANA NAYO WALA KUIPINGA!!!

8) “Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. 30Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” (Efeso 4:29-30)

>>NENO LOLOTE LILILO OVU HALITOKI KINYWANI MWANGU KAMWE

>> KILA NENO LINALOTOKA KINYWANI MWANGU NI JEMA NA LENYE KUMFAA MWENYE KUHITAJI

>>KILA NENO LA KINYWA CHANGU LINAWAPA NEEMA WANAOSIKIA

>>WALA SIMHUZUNISHI ROHO MTAKATIFU KWA MANENO YA KINYWA CHANGU

9) “ Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima;

Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,” (Mith 10:11a)

>>KINYWA CHANGU MIMI MWENYE HAKI WAKE NI CHEMCHEMI YA UZIMA (FOUMTAIN OF LIFE)KWA WOTE WANISIKIAO

10) “ Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu;

Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.” (Mith 10:13a)

>>HEKIMA YA MUNGU INAPATIKANA MIDOMONI MWANGU KWA KUWA MIMI NI MWENYE UFAHAMU

11) “Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi;

Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.” (Mith 10:21a)

>>MIDOMO YANGU INALISHA WATU WENGI KWA KUWA MIMI NI MWENYE HAKI WA MUNGU NDANI YA YESU KRISTO

12) “Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa;

Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.” (Mith 10:32a)

>>MIDOMO YANGU INAJUA YATAKAYOKUBALIWA KABLA YA KUYASEMA POPOTE, SIROPOKI! MAANA MIMI NI MWENYE HAKI MBELE ZA MUNGU…..!

13) “Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki;

Bali shahidi wa uongo hutamka hila.” (Mith 12:17)

>>NINAFUNUA HAKI SIKUZOTE KWA KUTAMKA MANENO YA KWELI KILA MAHALI

14) “Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga;

Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.” (Mith 12:18)

>>ULIMI WANGU NI AFYA KWA WAGONJWA, NA WOTE WENYE MARADHI MBALIMBALI KIHISIA, KIAKILI NA KIMWILI

15) “ Mdomo wa kweli utathibitishwa milele;

Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.” (Mith 12:19)

>>YOTE NIYANENAYO SIKU ZOTE HUWA YANATHIBITIKA MILELE MAANA NI YA KWELI, TOFAUTI NA WANAOSEMA UONGO AMBAO UNADHIHIRIKA BAADA YA MUDA KITAMBO TU!

16) “ Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha;

Bali neno jema huufurahisha. (Mith 12:25)

>>KINYWA CHANGU SIKUZOTE HUTAMKA MANENO MEMA YENYE KUFURAHISHA NA KUONDOA UZITO KATIKA MIOYO YAO WANISIKIAO KILA MAHALI.

17) “Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake;

Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri” (Mith 13:2)

>>NINAKULA MEMA SIKUZOTE AMBAYO NI MATUNDA YA KINYWA CHANGU

18) “3 Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;

Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.” (Mith 13:3)

>>NINAILINDA NAFSI YANGU NA NINAJILINDA MWENYEWE KWA KUKILINDA KINYWA CHANGU MWENYEWE!!! USALAMA WANGU SIKUZOTE UNATOKANA NA KUKILINDA KINYWA CHANGU KWA YALE NIYATAMKAYO!

19) “ Mwenye haki huchukia kusema uongo;

Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu. (Mith 13:5)

>>MIMI NACHUKIA KUSEMA UONGO SIKUZOTE MAANA NI MWENYE HAKI…..!

20) “ Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi,

Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. (Mith 14:3)

>>MIMI NI MWENYE HEKIMA NA MIDOMO YANGU INANIHIFADHI NA KUNIWEKA SALAMA DHIDI UOVU WA WAOVU WA DUNIA HII

21) “Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri;

Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. (Mith 15:2)

>>ULIMI WANGU NI ULIMI WA MWENYE HEKIMA NA NDIYO MAANA HUWA NATAMKA MAARIFA VIZURI SIKUZOTE

22) “Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo (Mith 15:4)

>> ULIMI WANGU SAFI NI MTI WA UZIMA UNAOWAPA UZIMA WOTE WASIKIAO MANENO YA UZIMA KUTOKA KINYWANI MMWANGU KILA NIENDAKO SIKUZOTE.

23) “Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa;

Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.” (Mith 15:7a)

-MIMI NI MWENYE HAKI NA NDIYO MAANA MIDOMO YANGU SIKUZOTE INAENEZA MAARIFA YA MUNGU YAALIYOMO KWENYE NENO LAKE.

24) “Mng’ao wa macho huufurahisha moyo;

Habari njema huinenepesha mifupa.” (Mith 15:30)

-KINYWA CHANGU SIKUZOTE KINALETA HABARI NJEMA ZENYE KUNENEPESHA MIFUPA YA WANAOZISIKIA NA KUZIPOKEA!!!

>> NINA MACHO YANGU ANGAVU YENYE KUUFURAHISHA MOYO SIKUZOTE!

25) “ Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake;

Huzidisha elimu ya midomo yake. (Mith 16:23)

>>MOYO WANGU WENYE HEKIMA NDIO WENYE KUFUNDISHA KINYWA CHANGU JINSI YA KUNENA; NA PIA HUZIDISHA ELIMU NA USHAWISHI WA MIDOMO YANGU

26) “Maneno yapendezayo ni kama sega la asali;

Ni tamu nafsini, na afya mifupani. (Mith 16:24)

>>MANENO YOTE YA KINYWA CHANGU YANAPENDEZA NAYO NI KAMA SEGA LA ASALI; NI MATAMU KWA WAYASIKIAYO NA AFYA MIFUPANI MWAO!!!

27) “ Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi;

Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.” (Mith 18:4)

>>MANENO YA KINYWA CHANGU NI KAMA MAJI YA KILINDI (KINA); NI KIJITO KIBUBUJIKACHO; CHEMCHEMI YA HEKIMA

28) “Yeye ajibuye kabla hajasikia

Ni upumbavu na aibu kwake.” (Mith 18:13) &

“Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini si mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika” (Yak 1:19)

>>MIMI NI MWEPESI WA KUSIKIA NA KUSIKILIZA, LAKINI SI MWEPESI WA KUSEMA, KUJIBU, WALA KUKASIRIKA!!!NINASIKILIZA KWA UMAKINI SANA KABLA SIJASEMA WALA KUJIBU.

 

29) “ Moyo wa mwenye busara hupata maarifa;

Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.” (Mith 18:15)

>>MOYO WANGU UNAPATA MAARIFA SIKUZOTE, NA SIKIO LANGU SIKUZOTE HUTAFUTA MAARIFA. NINA NJAA NA KIU YA MAARIFA ISIYOKOMA SIKU ZOTE!

30) “ Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;

Na wao waupendao watakula matunda yake.” (Mith 18:21)

>>NINAISHI NA KUENENDA KATIKA MAISHA HAYA NIKIWA NIMEJAA NGUVU YA UZIMA/MAISHA YA NENO KWA ROHO WA UZIMA KUPITIA KINYWA CHANGU; AMBAPO MAUTI IMEKIMBIA KABISA MBALI NA MAISHA YANGU NDANI YA YESU, NA MAISHA YA WOTE NINAOWATAMKIA UZIMA!NINAKULA MATUNDA MEMA KUPITIA KINYWA CHANGU KINENACHO NENO LA KWELI SIKUZOTE.

31) “Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,

Atajilinda nafsi yake na taabu.” (Mith 31:23)

>>MIMI NINAZUIA KINYWA CHANGU NA ULIMI WANGU, NA NDVYO NINAVYOJILINDA NAFSI YANGU NA TAABU ZOTE SIKUZOTE!

32) “Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe;

Mtu mgeni wala si midomo yako wewe.” (Mith27:2)

>>KAMWE SIJISIFU KWA KINYWA CHANGU MWENYEWE WALA MIDOMO YANGU; BALI WATU WENGINE NA WAGENI NDIO HUFANYA HIVYO

33) “28 Wanawe huondoka na kumwita heri;

Mumewe naye humsifu, na kusema, 29 Binti za watu wengi wamefanya mema,

Lakini wewe umewapita wote.” (Mith 31:28-29)

>>WATOTO WETU HUMWITA MKE WANGU “HERI” (WEWE NI MAMA ULIYEBARIKIWA); NA MIMI HUWA NAMSIFU  SIKUZOTE NA KUSEMA BINTI ZA WENGI WAMETENDA MEMA LAKINI WEWE MKE WANGU UMEWAPITA NA UMEWAZIDI WOTE

34) “Zab 49:3 SUV

Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.”

>>KINYWA CHANGU SIKUZOTE HUNENA HEKIMA, NA FIKRA ZA MOYO WANGU NI ZA BUSARA MILELE

35) “ Zab 71:15 (SUV)

Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.”

>>KINYWA CHANGU SIKUZOTE KINASIMULIA HAKI NA WOKOVU WA BWANA VISIVYOWEZA KUHESABIKA; NINA SHUHUDA ZISIZO NA IDADI.ZA WOKOVU NA HAKI YAKE YESU KRISTO BWANA.

36) “Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.” (Yak 3:2)

>>KWA NEEMA YA MUNGU SIJIKWAI KATIKA KUNENA, NA HIVYO MIMI NI MKAMILIFU, NA NINAWEZA PIA KUUZUIA NA MWILI WANGU WOTE KAMA KWA LIJAMU

>>YAANI, NINAUZUIA NA KUUDHIBITI MWILI WANGU WOTE KWA KUWA NAWEZA KUKIZUIA KINYWA CHANGU NA KUUZUIA ULIMI WANGU

37) “BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako?

Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu?

2 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,

3 Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,

Wala hakumsengenya jirani yake.” (Zab 15:1-3)

>>NINAKAA/ISHI SIKUZOTE HEMANI/HEKALUNI MWA BWANA; MASKANI YANGU NI KATIKA KILIMA CHA MUNGU KITAKATIFU, KWA KUWA;

>>a) NINAENENDA KWA UKAMILIFU NA KUTENDA HAKI, b) NINASEMA KWELI KWA MOYO WANGU, NA c) WALA SISINGIZII KWA ULIMI WANGU, d) SIMTENDI MWENZANGU MABAYA, e) NA WALA SIMSENGENYI JIRANI YANGU.

38) “Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. (Math 5:37)

>>SINA KIGEUGEU WALA KUSITASITA WALA KAULI MBILI MBILI KATIKA MANENO NA MISIMAMO YANGU; NIKISEMA NDIYO INABAKI NDIYO YA MILELE, NA NIKISEMA HAPANA INABAKI HAPANA MILELE KWA KUWA MIMI NI MTUMISHI WA MUNGU ALIYE HAI!!!

39) “13Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; (2 Kor 4:13)

-BWANA YESU AMENIPA ROHO YA IMANI NA HIVYO KINYWA CHANGU KINAONGEA NA KINASEMA IMANI; SIKUZOTE NINANENA YALE NIYAAMINIYO KUTOKA KATIKA NENO LA KRISTO

40) “MANENO YOTE YA KINYWA CHANGU NI FARAJA, AMANI, FURAHA, BARAKA, USHINDI, TUMAINI, DAWA, UPONYAJI, NEEMA, REHEMA, UZIMA, HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU, KICHO, USHAURI, UWEZA, NGUVU, UFUNUO, SULUHISHO, UTATUZI, YAJENGAYO, HUIMARISHA, UTAKASO, ULINZI, HUTIA MOYO, WOKOVU, UAMSHO, UFUFUO, NA MENGI ZAIDI SANA SANA KWA WOTE WAYASIKIAYO SIKU ZANGU ZOTE!!!”

USIISHIE HAPA TAFUTA MAANDIKO MENGINE ILI UWEZE KUUTUNZA NA KUUDHIBITI ULIMI WAKO UWE MTU MKAMILIFU (Yakobo 3)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post