BARAKA ZA KIAKILI (MENTAL BLESSINGS)

 


BARAKA ZA KIAKILI (MENTAL BLESSINGS)

2. AMETUBARIKI KIAKILI ILI NA SISI TUWE BARAKA KWA WENGINE KIAKILI PIA (we are blessed mentally so that we can be a blessing to others mentally) [MENTAL BLESSINGS]

 Kwenye sehemu iliyopita ya baraka za kiroho tuliongelea kwa kina kuhusu muunganiko wa mwamini (believer) na Bwana wetu Yesu katika roho sawasawa na 1 Kor 6:17, na kwamba muunganiko huo unamfanya mwamini awe;

>> roho moja na Mungu

>> roho moja na (Mungu Aliye) Roho (Yoh 4:24)

>> roho moja na Neno maana Neno ni Mungu (Yoh 1:1)

Tukaona kuwa hii ndiyo baraka kuu kuliko zote, na ndiyo chanzo cha baraka zote za rohoni. Tukaona pia kwamba muunganiko huu unakufanya uwe;

>> mmoja na Neno (one with the word)

>> mmoja na Roho (one with the Holy Spirit)

>> mmoja na Mungu Baba wa mbinguni (one with the heavenly Father in glory)

Tukaona kwamba hii inakufanya uwe unapokea moja kwa moja roho ya kila andiko kwenye roho yako, na hivyo kujazwa roho yako na “roho ya kila neno/andiko” unaloliamini. Na hii inatokana na kweli hii kwamba “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” (Yoh 6:63) Tukaona kwamba neno au andiko lolote linakuwa roho pale unapoliamini na kulipokea kama neno la Mungu kweli, na kuliweka moyoni mwako. Tukasema neno linakaa moyoni mwako kama roho, na kwamba kadiri imani yako inavyozidi kuongezeka kwa neno la Mungu, ndivyo Yesu anavyozidi kuumbika ndani yako, na tunasema unazidi kujazwa Roho kwa namna endelevu (continued infilling of the Holy Spirit). Hii inaweza kuitwa “continued infilling of the Holy Word of God” (ujazo endelevu wa Neno la Mungu lililo takatifu sana). Tukaona kwamba huku ni kujazwa utakatifu wa Neno, au utakatifu wa Mungu, au usafi wa Neno (purity of the word); na kwamba huu ndio utakaso wa roho yako (sanctification of your spirit). Na hii inawezekana kadiri unavyoliamini neno na kuliweka moyoni mwako. Biblia inasema, “wala hakufanya tofauti kati ya sisi na wao, AKIWASAFISHA MIOYO YAO KWA IMANI.” (Mdo 15:9) Imani husafisha moyo (faith purifies). Tukaenda mbali zaidi kwa kusema, unapoamini na kupokea roho ya neno uliloliamini, unakuwa unabadilishwa na kuzidi kufanana na Yesu, kwa kuwa kila andiko ni roho unapokuwa umeliamini, na kila roho ni Yesu, na ni uzima, kwa kuwa Yesu, Adamu wa mwisho, ni Roho anayehuisha (life-giving Spirit) [1 Kor 15:45] Kila roho ya andiko inayokujaza roho yako inakujaza uzima, au uhai, au maisha ya neno. Biblia inasema, “ Maneno Ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.” (Zab 12:6) Neno linakutakasa unapoliamini, yaani, roho ya hilo andiko inakusafisha au kukutakasa roho yako. MUUNGANIKO NA NENO, MUUNGANIKO NA ROHO, MUUNGANIKO NA MUNGU, NDANI YA KRISTO YESU BWANA, NDIYO BARAKA KUU KULIKO ZOTE, NA MAMA WA BARAKA ZOTE ZA ROHONI. Kwa kuwa BARAKA ZA ROHONI NI BARAKA ZA NENO LOTE LA MUNGU. NA BARAKA ZOTE ZA ROHONI ZIMEKUSUDIWA KUKUFANYA UFANANE NA YESU KWA KILA KITU, NA UISHI KAMA YESU, MWANA WA MUNGU, ILI UMTUKUZE MUNGU NDANI YA YESU, NA UPATE KUWA SIFA YA UTUKUFU WAKE HAPA DUNIANI, NA MWISHOWE UPATE KUURITHI UTUKUFU WA MUNGU KATIKA UFALME WAKE WA MILELE.

“Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, AKILETA WANA WENGI WAUFIKILIE UTUKUFU, ……..” (Ebr 2:10)

HUU NDIO MWISHO ULIOLENGWA NA BARAKA ZA KIROHO 1) YESU KATIKA UTIMILIFU NA UKAMILIFU WAKE WOTE AONEKANE NDANI YAKO; ATENDE KAZI KWA ROHO NA NGUVU ZAKE ZOTE, NA KULETA MATOKEO YOTE ALIYOYASEMA KWENYE NENO LAKE ILI MUNGU ATUKUZWE NDANI YAKO, NA YESU PIA ATUKUZWE NDANI YAKO, NA DUNIA IUONE UTUKUFU WA MUNGU KUPITIA WEWE, KAMA ILIVYOUONA KWA YESU, NA MAELFU, NA MAMILIONI, NA MABILIONI, NA MATRILIONI, WAINGIE KWENYE UFALME WA MUNGU KUPITIA WEWE, N.K. 2) MWISHO WAKE WEWE MWENYEWE UINGIE MBINGUNI KAMA ANDIKO LILIVYOONYESHA HAPO JUU.

Baada ya mapitio haya sasa tunao msingi mzuri wa kuelezea baraka za kiakili kwa kuwa mambo yote huanzia rohoni, Tukisema akili tunaongelea eneo la “NAFSI (SOUL)” Tumeshasema huko nyuma kwenye somo hili kwamba mwanadamu ni roho, ana nafsi, na anaishi kwenye mwili. Kimsingi, mwili ni nyumba anayoishi mwanadamu akiwa hapa duniani. Biblia inasema kuna miili ya duniani, lakini pia kuna miili ya mbinguni (1 Kor 15:40); na pia kuna miili ya asili na miili ya roho (1 Kor 15: 44). Mwili hauwezi kuurithi ufalme wa Mungu (1 Kor 15:50), bali roho zetu katika miili ya roho au miili ya mbinguni isiyoharibika (1 Kor 15:51-54).

Sasa, Nafsi (Soul) = Akili/fikra/mawazo (Mind) + Mapenzi/nia/makusudi (Will) + Hisia (Emotions)

Nafsi ya mwanadamu ina sehemu hizi tatu;

1. Eneo la Akili, au mawazo, au fikra. (Mind)

>>Hili ni eneo la msingi sana, na ndilo eneo linalomtambulisha mwanadamu. Kwa kuwa maneno ya mwanadamu ni mawazo yake yaliyotamkwa kwa kinywa chake. Maneno kabla hayajatamkwa huwa yanaitwa mawazo. Kutafakari jambo au kulifikiria jambo mpaka ukalielewa ndiko kunakokupa akili. Akili ya mtu inatokana na vile alivyofikiri na kutafakari na kujua na kuelewa, na kisha kushawishika mawazoni mwake kwamba hivyo ndivyo ilivyo. Na huyu ndiye mtu mwenyewe halisi. Biblia inasema, “Aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo….” (Mith 23: 7) [NIV Proverbs 23:7; “For as he thinks within himself, so is he……”]

Hii inamaanisha kwamba MWANADAMU YUKO KAMA VILE FIKRA ZAKE ZILIVYO! Mwanadamu vile anavyotambulika ni zao la fikra zake. Maneno na matendo ya mwanadamu chanzo chake ni fikra na mawazo yake, au kufikiri kwake. Ukifikiri na kufikia hitimisho la hilo ulilolifikiria, hilo linakuwa ndiyo akili yako, ambayo imezaliwa na mawazo na fikra zako mwenyewe. Ili uweze kufikiri, kikawaida, lazima taarifa ziingie akilini au mawazoni mwako ama kutoka nje au kutoka ndani yako. Na taarifa hizi ndizo unazozifikiria na kuzitafakari akilini mwako mpaka kufikia hitimisho mawazoni mwako mwenyewe. Hitimisho hilo ndiyo akili yako, na utakapoongea au kutenda kwa akili hiyo ndipo ulimwengu utakupa mrejesho, kama ni akili njema au akili mbaya. Ukiwa mbinafsi siku zote utawaza kibinafsi, yaani, mawazo yako yatakuwa yanakupendelea wewe tu sikuzote (self-centered thinking). Ukiwa mwema utakuwa unafikiria mema na kuongea na kutenda mema sikuzote. Ukiwa mbahili sikuzote utafikiria kubana na kubana matumizi ya fedha na akili yako haiwezi kamwe kufikiria kutoa au kuwapa wengine kingi! bali kiduuuchu. Kuna akili za mwilini na akili za rohoni. Na kabla sijaenda mbali niseme hapa kwamba hakuna mawazo, kwa asili, ambayo hayatoki kwenye roho fulani ama ya Mungu au ya shetani.

Nimetoka kusema hapo juu kuwa aonavyo mtu nafsini mwake, afikirivyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo. Lakini tunajua kwamba nafsi ni ya roho! Huwezi kutenganisha roho iwe Tanzania, na nafsi ikawa China kama vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano kabisa. Hapana! roho ina nafsi na inakaa ndani ya mwili.

Tafsiri moja ya Biblia ya kiingereza na Kiswahili inasema;

3 “Put not your trust in princes, nor in the son of man, in whom there is no help.

Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wovu kwake.

4 His breath goes forth, he returneth to his earth; in that very day his thoughts perish.

Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.” (Zab 146:3-4)

Andiko hili linaonyesha kwamba siku mwanadamu anapofariki 1) Mwili hurudi mavumbini, 2) Roho yake hutoka, na 3) Mawazo yake hupotea.

>>Kwamba roho inapotoka kwenye mwili, hutoka na mawazo yake! (yaani, hutoka na nafsi yake)

Mungu alipomuumba mwanadamu ilikuwa hivi;

“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” (Mwa 2:7)

>> Mungu aliufanya kwanza mwili,

>> Kisha ule mwili akaupulizia puani pumzi ya uhai, ambayo ndiyo roho

>> Alipoweka roho ndani ya mwili, mwanadamu akawa nafsi hai.

Kibiblia mwanadamu anatambulishwa pia kama NAFSI HAI!  Na hii ndiyo maana tukasema hapo juu kwamba afikirivyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Tunaona hapa kwenye uumbaji kwamba nafsi hai iliingia pamoja na pumzi ya uhai ambayo ndiyo roho ya mwanadamu. Unaweza kuitafsiri roho kuwa ni pumzi ya uhai ya mwanadamu kutoka kwa Mungu. Na ndiyo maana imeandikwa mwili pasipo roho unakuwa umekufa (Yak 2:26). Kwenye Zaburi anasema, “Wewe wauficha uso wako, waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao.” (Zab 104:29)

Hapo juu nilisema yapo mawazo ya ndani yako na yapo mawazo ya nje yako, na mawazo haya yote ndiyo yanayokupa akili unapoyatafakari na kuyafikiria na kisha kushawishika mawazoni mwako kwamba ndivyo ilivyo na inavyopaswa kuwa. Adamu alipoumbwa alikuwa na ushirika na Mungu, na taarifa zote alizozipata zilitoka kwenye kile Mungu alichomwambia. Mawazo yake, fikra zake, na akili yake vilijaa Neno la Mungu, na ndiyo maana alitembea na Mungu na kuyafanya mapenzi ya Mungu, na kumpendeza sikuzote. Adamu ndiye aliyempa mkewe taarifa za kusudi na mpango wa Mungu kama alivyoupokea kutoka kwa Mungu, na pia alimpa utaratibu wa maisha yao bustanini. Kwamba walitakiwa kuishi kwa neno la Mungu. Nao walifanya vizuri mpaka pale nyoka alipokuja kumdanganya mwanamke. Mwanamke alipokea ushauri toka kwa shetani kwa kupitia nyoka, naye akaukubali, na akashawishika, yaani, akakubaliana nao mawazoni mwake; Biblia inasema, “ Mwanmke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala.” (Mwa 3:6) Mwanamke alipokea “wazo” la shetani na kukubaliana nalo, akaasi na kuanguka dhambini. Uasi unatokea pale unapoziamini taarifa za roho iliyoleta mawazo moja kwa moja mawazoni kwako, au kupitia vyanzo mbalimbali vya taarifa kama maneno ya watu, televisheni, redio, mitandao na intaneti, simu janja, vishikwambi, matangazo ya mabango, magazeti, majarida, vitabu, maandiko mbalimbali, n.k. Dunia imejaa taarifa mbalimbali ambazo zote zinatoka kwenye roho fulani ya ushawishi kwa mawazo yako. Biblia inasema, “Mwanamke ALIPOONA….” Kumbuka mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Wazo la roho ya shetani lilipoingia moyoni (rohoni) mwake lilimbadilisha afanane nayo, na hivyo kupoteza kule kufanana na Mungu. Aliliweka moyoni wazo lile baada ya kulitafakari na kushawishika mawazoni mwake. Alipoliweka moyoni mwake akawa ameipokea ile roho moyoni mwake na kumkataa Mungu. Maana alijua kabisa kwamba hakutakiwa kula matunda ya mti ule (Mwa 3:3). Alikubaliana na wazo la roho ya shetani lililokuwa kinyume na Neno la Mungu. Na kwa kuwa tunajua kwamba Mungu ni Neno, maana yake wazo alilolikubali lilikuwa kinyume na Mungu, na moyoni mwake akawa ameasi, na moyo wake ukawa umebadilika, akawa sasa ni muasi (rebel) mbele za Mungu. Hii ilimbadilisha kabisa kiroho kwa kujaza moyo wake (roho yake) na roho za shetani na kumpa akili ya uasi kutoka kwa roho ya uasi. Sikuzote roho ya uasi hukupa mawazo au akili ya kuasi, roho ya uadui hukupa mawazo au akili ya uadui, roho ya kusamehe hukupa mawazo au akili ya kusamehe, roho ya ulevi hukupa mawazo au akili ya kulewa, roho ya tamaa hukupa sikuzote mawazo ya kutaka zaidi na zaidi pasipo kutosheka, roho ya kiburi hukupa mawazo ya kujiinua na kujikweza juu ya wengine, kuwadharau wengine, na kutokubali kuwa chini yao kwa namna yoyote, n.k.

Leo hii mtu aliyeokoka kwa kuzaliwa mara ya pili, huwa anajaribiwa na mawazo ya shetani kutoka nje maana moyoni (rohoni) mwake amejaa Neno la Mungu. Akikubaliana na wazo la shetani ndipo anakuwa amechafua mavazi yake kwa kuruhusu wazo au mawazo machafu nafsini mwake. Akiamini uongo ule moyoni mwake roho ile itamwingia ndani yake, na kumfanya awe kinyume na Kweli katika ushawishi huo aliokubaliana nao na kuuweka moyoni mwake. Hii imeelezwa na Yakobo, “14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” (Yak 1:14-15)

>> Ni ile roho ya tamaa uliyonayo ndiyo inayojaribu kukushawishi kama hauna Neno la Mungu kinyume na tamaa hiyo!

>> Unavutwa na udanganyifu kwa njia ya mawazo yako mwenyewe!

>> Ukiruhusu mawazo maovu yakae akilini mwako hiyo inaitwa mimba ya dhambi! Unatafakari dhambi nafsini mwako!

>> Mimba huwa inaingia na kukaa moyoni na lazima izae dhambi! Hapa unakuwa umeshaamini uongo na dhambi imo moyoni mwako! (yaani, una roho ya dhambi!)

>> Ukiendelea kutenda dhambi bila kutubu, wala kusikiliza maonyo, wala kugeuka, wala kuhuzunika, wala kumsikiliza Roho Mtakatifu, hapo ndipo unakufa! Maana Roho Mtakatifu anakuacha ili, kama maandiko yasemavyo, “Ufuate akili zako zisizofaa, na uyafanye yasiyopasa kufanywa!” (Rum 1:28) Hapa ni wewe mwenyewe umeamua kung’ang’ania tamaa na sasa umeizalia mauti matunda! Ikabodi! (1 Sam 4:20-21) Katika hatua ya Ikabodi mwanadamu ameachwa na Mungu! Rushwa kwake ni kawaida, uzinzi kwake ni kawaida, wizi kazini kwake ni kawaida, udanganyifu kwenye biashara kwake ni kawaida, biashara haramu au za magendo kwake ni kawaida, magumashi kwake ni kawaida, uadui kwake ni kawaida, wizi wa sadaka kanisani kwake ni kawaida, pesa kwake ndiyo mungu, kutajirika kwa namna yoyote halali au si halali kwake ni kawaida, shughuli za dunia kwake ni muhimu kuliko mambo ya Mungu, n.k. Halafu unaweza kukuta mtu wa namna hii ndiye mtoaji maarufu au hata kiongozi wa kanisa, aliyewekwa na vipofu wanaoongoza vipofu ambao wote mwisho wao ni shimoni! (Mathayo 15:14)

Kwa mtenda dhambi asiyeokoka, jumla ya mawazo yake yote  hayako sawa, na sikuzote yuko kinyume na kweli. Moyoni mwake amejaza mawazo mabaya, na moyo wake unamilikiwa na kutawaliwa na roho za shetani. Kama wewe ni mtenda dhambi haijalishi wewe ni nani, una elimu gani ya dunia hii, KUFIKIRI KWAKO NI DHAMBI! (Your thinking is sinful!) Hata kama unasoma Biblia na kujaza maandiko kichwani mwako, na unaweza kuyatamka kwa kichwa, kuyafundisha, au kuyahubiri, bado mawazo yako si sawa mbele za Mungu. Kwa maana kule kufundisha kwako au kuhubiri kwako neno la Mungu ukiwa bado ni mwenye dhambi kunasaidia zaidi kukufanya uzidi kuwa na moyo mgumu, na kujihesabia haki, na kuzidi kujidanganya kwamba uko sawa mbele za Mungu, huku hujawahi kuokoka na kubadilika kwa kuwa na moyo mpya na roho mpya. Maana ni moyo mpya na roho mpya inayokupa mawazo mapya kutoka kwa Mungu kwa njia ya Roho wake Mtakatifu. Unaweza kusoma masomo ya Biblia kwa kiwango chochote, lakini pasipo kuokoka na kujazwa Roho Mtakatifu bado utazidi kujaa na kupotezwa na Kiburi cha moyo wako, ubishi, ukaidi, jeuri, dharau, majivuno, kujihesabia haki, kujiinua, kujikweza, chuki, uchungu, uadui, na ugomvi. Unaona hapa jinsi ambavyo unazidi kuzama dhambini maana unazidi kulitaja jina la Yesu pasipo kuacha dhambi kama 2 Tim 2:19 isemavyo, na hivyo kuzidi kufanyika mwana wa laana. Maana imeandikwa,  “Mtu yeyote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.” (1 Kor 16:21).

Ninapoongelea sasa baraka za kiakili elewa wewe mtenda dhambi ambaye hujaokoka kwamba jumla ya fikra zako ni dhambi, na ni fikra hizo hizo ndizo zimekufanya mpaka sasa uwe hujaokoka. Au uliokoka halafu ukarudi nyuma au kuanguka lakini unaahirisha kutubu na kumrudia Mungu. Jihadhari basi usijeahirisha kutubu mpaka ujikute unashuka kwenye shimo la giza nene ambapo utakuwa umepoteza nafasi adimu unayoichezea ya kurejea kwa sababu ya kiburi cha uzima ulichonacho, usitambue kwamba matumaini yako yote ni kama kutumainia nyuzi za buibui zikudake na kukuzuia kushuka jehanamu siku usiyoijua roho yako itakapoacha huo mwili wako!!! (Ayu 8:13-18)

BARAKA ZENYEWE ZA KIAKILI

Biblia inasema,

New International Version
for, “Who has known the mind of the Lord so as to instruct him?” But we have the mind of Christ.” ( 1 Cor 2:16)

“16Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.” ( 1 Kor 2:16)

>>THE MIND OF THE LORD IS THE GREATEST MENTAL BLESSING IN ALL CREATION!

>>MAWAZO AU AKILI YA BWANA NDIYO BARAKA KUU YA KIAKILI KULIKO ZOTE KATIKA UUMBAJI WA MUNGU!

Lile neno lililotafsiriwa “nia” ni neno “mind” linalomaanisha mawazo au fikra! Na tumeona huko nyuma kuwa akili ni zao za kufikiri na kutafakari kwako kwa habari ya taarifa zile ulizopata ama kutoka ndani au nje. Kuanzia sasa nitaongelea taarifa za kutoka ndani kwa mtoto wa Mungu uliyeokoka na kujazwa Roho Mtakatifu, na unayeenenda kwa imani iliyo hai kwa Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu. Tulisema roho ina nafsi na huyu ndiye mwanadamu halisi ambaye anaishi kwenye nyumba ya udongo (Ayu 4:19) hapa duniani inayoitwa mwili. Sasa kupitia Yesu Kristo (Neno la Mungu) Aliye Hai leo, tunapata mawazo yote ya Neno. Mawazo ya Neno ndiyo mawazo ya Roho Mtakatifu, nayo ni mawazo ya Bwana Yesu.

Mawazo ya Neno = Mawazo ya Bwana =Mawazo ya Roho

Biblia inasema, “13Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.” (Yoh 16:13-15)

>> Roho wa Kweli (Neno) akija atanena yale atakayoyasikia

>> Yeye hatanena maneno yake tu apendavyo (mawazo yake mwenyewe)

>> Huyo Roho atatwaa katika yaliyo ya Yesu na kuwapasha habari (habari kuhusu Yesu awazavyo na asemavyo)

>> Yote awazayo na asemayo Yesu ni yale yale ya Baba yetu wa mbinguni.

>> Hayo atakayoyasema Roho Mtakatifu wa Kweli ni kama alivyosikia kutoka kwa Yesu, naye ni kama alivyosikia kwa Baba wa mbinguni

NAFSI  = MAWAZO (MIND) + MAPENZI (WILL) + HISIA (EMOTIONS)

>>YALE YALIYOMO NAFSINI MWA BABA NDIYO YALE YALE YALIYOMO NAFSINI MWA NENO (YESU)

>> YALE YALIYOMO NAFSINI MWA YESU KRISTO NDIYO YALE YALE YALIYOMO NAFSINI  MWA ROHO MTAKATIFU

>>MUNGU MMOJA AMEJIFUNUA KATIKA OFISI HIZI TATU KWA KADIRI YA MAKUSUDI YAKE KATIKA UUMBAJI! AMEJIFUNUA KAMA 1) MUNGU MUUMBAJI (OFFICE OF CREATION), 2) MUNGU MKOMBOZI (OFFICE OF REDEMPTION), 3) MUNGU MFALME NDANI YA MOYO WA MWANADAMU (OFFICE OF GOD’S KINGDOM WITHIN MAN)

>>Ukisoma Biblia utakuta Mungu anaponena katika kila ofisi mojawapo anafunua KILE ANACHOFIKIRI NA ANACHOWAZA ambayo ndiyo yanaitwa mapenzi yake! Mawazo ya Mungu ndiyo mapenzi yake! Mawazo ya Mungu yamo kwenye neno lake! Mawazo ya Mungu ndiyo Kweli maana Neno lake ni Kweli. Mungu ndiye yuko sahihi sikuzote katika yote asemayo na ayawazayo. Mwanadamu wajibu wake ni kuamini, kukubali, kupokea, na kutii kila asemacho Mungu na ndipo ataweza kumpendeza Mungu. Mfano Mungu anaposema; “2(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)” (2 Kor 6:2)

>>Hapa maana yake Mungu anakutaka kwa Neno lake kwamba UOKOKE SASA HIVI! Kila kitu kiko upande wako wewe. Mungu haoni kwamba unatakiwa kuahirisha au kuchelewa kufanya uamuzi wa kuokoka maana kila kitu kiko tayari kwa ajili yako. Upatanisho umekwishafanyika kwa damu ya Yesu, wewe unasubiri nini? Hili ndilo wazo takatifu la Mungu Mtakatifu. Wewe usiyetaka kutii hili ina maana unapingana na akili ya Mungu, na hivyo unajiona una akili kuliko Mungu!! Ni uovu wa kiwango gani huu!! Wazo la Neno la Mungu ndilo linakupa akili sahihi na inayompendeza Mungu. Kama huna neno la Mungu nafsini mwako maana yake huna akili mbele za Mungu. Kama huna Neno la Mungu moyoni na akilini mwako  lazima utakuwa na akili mbovu, au akili ya uasi, au akili ya uovu, ambayo ni akili ya kutenda mabaya. Mungu aliuliza na hata sasa angali akiuliza; “9Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?” (Yer 8:9). UNAPOLIKATAA NENO LA MUNGU, UNAZIKATAA AKILI ZA MUNGU, AMBAZO NDIZO AKILI ZA ROHONI, ANAZOTOA ROHO MTAKATIFU KUPITIA NENO HILO!!! Kuna mwingine hauoni umuhimu wa kujazwa Roho Mtakatifu halafu umedanganywa kwamba si lazima kunena kwa lugha kwa kupotosha andiko hili; 30Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?” (1 Kor 12:28) Shetani anakuja kukudanganya na kukupotosha anapokwambia imeandikwa “siyo wote wanaonena kwa lugha!!!” Halafu unasema umejazwa Roho Mtakatifu pasipo ushahidi wa awali (initial biblical evidence) wa kunena kwa lugha! Hilo andiko linaongelea kwamba siyo wote wenye karama ya aina za lugha! Hapo zimekuwa zikiongelewa karama za Roho Mtakatifu. Na ndiyo maana kuna karama ya kutafsiri lugha hapo na karama za kuponya! Karama zinagawiwa kama apendavyo Roho Mtakatifu! Kama ingekuwa hivyo maandiko haya yangekuwa yanapingana na andiko hili!!! (Mdo 2:1-4, Mdo 10:44-48, Mk 16:17, Mdo 19:1-6 ) Anayejazwa Roho Mtakatifu lazima anene kwa lugha. Fikra za uongo zimezaa fundisho la uongo la shetani kwamba si wote wanaonena kwa lugha! Unaweza kuona kwamba watu wa namna hii hawana AKILI YA MUNGU, AU AKILI YA NENO, AU AKILI YA ROHO, AU AKILI YA YESU, AU AKILI YA MAANDIKO (they are not Scripture-minded, or Christ-minded, or Spirit-minded). KUBARIKIWA KIAKILI NI KUWA NA AKILI YA MUNGU INAYOPATIKANA KWENYE NENO LAKE, KWA NJIA YA IMANI ILIYO HAI KWA NENO ALIYE HAI, YAANI, YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU! Nje ya hapo huna akili! Akili mbele za Mungu ni ile aliyokupa Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu AKAAYE NDANI YAKO! Na kwa taarifa yako kunena kwa lugha muda mrefu kunafunua maandiko na kukuingizia akili ya Neno la Mungu; na hii ndiyo maana ukinena kwa lugha muda mrefu halafu ukasoma neno UNAPATA HOT BREAKING-NEWS FROM HEAVEN!!! (HABARI MPYA ZA MUDA HUO HUO MOJA KWA MOJA KUTOKA MBINGUNI) KWA NJIA YA UFUNUO!!! Alichofanya Yesu hapa kwa wanafunzi wake, leo hii anakifanya kutokea ndani yako kwa Roho Mtakatifu kama umeokoka na kujazwa Roho; “44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 45Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.” (Lk 24:44-45)

[ “New International Version
Then he opened their minds so they could understand the Scriptures.

New Living Translation
Then he opened their minds to understand the Scriptures.” (Lk 24:45)]

>>AKILI YAKO LAZIMA IFUNULIWE (IWE OPENED) ILI UPATE KUELEWA KILE MUNGU ANACHOSEMA KWENYE MAANDIKO! YAANI, UPATE KUELEWA MAWAZO YA MUNGU MTAKATIFU, ILI UWE NA AKILI ITOKAYO KWAKE!!! BARAKA YA KIAKILI YATOKA KWENYE NENO LA MUNGU!

UMEBARIKIWA KIAKILI UNAPOWAZA NA KUFIKIRI KAMA NENO LINAVYOWAZA NA KUFIKIRI. ROHO YA NENO IKIUNGANIKA NAWE NDIPO INAKUPA MAWAZO YAKE NAFSINI MWAKO. HAPO NDIPO UNAPOKUWA NA AKILI YA ANDIKO, AU YA NENO, AU YA BWANA, AU YA ROHO MTAKATIFU!!! HAPA NDIYO MBELE ZA MUNGU UNAKUWA UNA AKILI, NA TOFAUTI NA HIVI MBELE ZA MUNGU WEWE HUNA AKILI!!! BARAKA ZA KIAKILI ZINAHITAJI;

1) KUOKOKA, 2) KUJAZWA ROHO MTAKATIFU, 3) KUISHI KWA IMANI YA YESU (NENO), 4) KULITENDA NENO LA MUNGU SIKUZOTE, na 5) KUISHI KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU (Mt 4:4b)

Mwenye Akili Iliyobarikiwa Ni Yule Mwenye Kulitenda Neno La Mungu Kama Maandiko Yasemavyo;

“24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.” (Mt 7:24-27)

>>ANAYESIKIA NENO AU KULISOMA NENO NA KULIFANYA HUYO NDIYE MWENYE AKILI MBELE ZA MUNGU

>>ANAYESIKIA NENO LA MUNGU HALAFU ASIFANYE LISEMAVYO HUYO HANA AKILI, NA KIBIBLIA ANAITWA MPUMBAVU

Ndiyo maana Mungu anakushauri hivi;

“18 Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.” (1 Kor 3 :18)

[New International Version
Do not deceive yourselves. If any of you think you are wise by the standards of this age, you should become “fools” so that you may become wise.

New Living Translation
Stop deceiving yourselves. If you think you are wise by this world’s standards, you need to become a fool to be truly wise.] (1 Cor 3:18)

>> Kuna hekima au akili ya dunia hii na kuna hekima au akili ya Mungu! Hekima ya dunia hii (worldly learning) ina tabia ya kumkataa Mungu, kujivuna, kujiona bora, kujiinua, kupuuza mambo ya Mungu, kudharau wajumbe wa Mungu, kukataa neno, kujisifia, kupenda heshima za wanadamu, kutafuta sifa na utukufu wa wanadamu, kupenda na kutafuta kuonekana, kutumainia akili zako, kutegemea akili zako, kudhani na kufikiri unajua sana, umefuzu sana, elimu ya dunia hii inakutosha, na KUKATAA KUMWAMINI MUNGU!!! Hekima iliyojaa ubinafsi mtupu!

>>Ndiposa Mungu, ambaye ndiye peke yake mkamilifu wa maarifa, (perfect in knowledge) [Ayu 36:4] anakushauri kwamba ni bora uwe mpumbavu machoni pa dunia au wanadamu ili upate kuwa na hekima na akili ya kweli kwa kulikubali lile neno linaloonekana kama upuuzi mbele ya wenye hekima wa dunia hii. Kwa nini?

“20 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? 21Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.” (1 Kor 1:20-21)

>>Mungu ameifanya hekima ya dunia hii kuwa ni upumbavu

>>Lile neno lihubiriwalo laonekana upuuzi kwa wenye hekima wa dunia hii; lakini ndilo linalookoa wote waliaminilo!!

“19Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. 20Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.” (1 Kor 3:19-20)

>>Hiyo inayoitwa hekima au akili ya mtenda dhambi NI UPUUZI MBELE ZA MUNGU!

>>Bwana Yesu ANAYAFAHAMU MAWAZO YA WENYE HEKIMA WA DUNIA HII KUWA NI YA UBATILI

New International Version
and again, “The Lord knows that the thoughts of the wise are futile.”

New Living Translation
And again, “The LORD knows the thoughts of the wise; he knows they are worthless.” (1 Cor 3:20)

>>Inawezekana umejaa udanganyifu wa aina hii kichwani na moyoni mwako pia kwamba wewe ni mwenye akili hapa duniani na hekima pia kwa vigezo vyako mwenyewe; Iwapo hiyo unayoiita akili au hekima HAIMTAKI YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO; NA KAMA HAUONI UMUHIMU WA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU; NA KAMA HAUISHI KWA NENO LA MUNGU; NA KAMA WEWE UNAISHI DHAMBINI NA BADO UNAJITETEA; NA KAMA UMERUDI NYUMA, AU UMEANGUKA HALAFU HUTAKI KUTUBU; HIYO UNAYOIITA HEKIMA AU AKILI MBELE ZA MUNGU HAINA THAMANI YOYOTE NA HAIFAI KWA LOLOTE (worthless and futile!) HIYO AKILI NI AKILI YA UASI, NAYO NI AKILI MBOVU, INAYOTOKA KWENYE ROHO ZA UOVU; UMEDANGANYWA NA SHETANI, NA UNAJIVUNIA AKILI ZAKO MWENYEWE ZA KIMWILI NA AKILI ALIZOKUPA SHETANI.

Hata Adamu alipoasi alipokea akili kama za kwako pale alipokataa kutubu na kuanza kutoa utetezi na visingizio badala ya kutubu;

6Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.” (Mwa 3:6-7)

>>Walipopoteza utukufu wa Mungu na kujikuta wako uchi, BADALA YA KUTUBU WAO WAKAANZA KUJIPIGANIA NA KUJIPAMBANIA!! AKILI YAKO YA KUJIPIGANIA NA KUJIPAMBANIA NI AKILI YA UASI NA UBINAFSI AMBAYO HAIMTEGEMEI WALA KUMTUMAINIA MUNGU! HAPA NDIPO MWANZO WA MASUMBUFU YA MAISHA BAADA YA UASI KUINGIA. Biblia inasema,

“5 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. 7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.” (Mith 3:5-7)

>> AKILI ZAKO MWENYEWE HAZIFAI KITU KAMA VILE TU AMBAVYO AKILI ZA ADAMU NA HAWA HAZIKUFAA KITU!

“4 Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.” (Mith 23:4)

>> ACHA KUZITEGEMEA AKILI ZAKO MWENYEWE, MAANA HAZIFAI LOLOTE KWENYE UMILELE WAKO!!

>>UKIZITEGEMEA AKILI ZAKO MWENYEWE KAMWE HUWEZI KUWA NA AKILI ZAKE BWANA YESU NA KAMWE HAKUPI MAANA HAUMTEGEMEI ROHO MTAKATIFU. Marafiki wa Mungu kwenye Biblia walimtegemea Yeye sikuzote na walienenda kwa akili zake Aliye Juu.

Mfalme Selemani alikuwa na uhusiano na Mungu naye alipotakiwa aombe lolote alitakalo aliomba hivi; “7Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 8Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 9Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

10Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. 11Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 12basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. 13Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.” (1 Fal 3:7-13)

>> Mungu alimtokea Mfalme Sulemani kwenye ndoto usiku akamwambia omba lolote utakalo nami nitakutendea.

VITU AMBAVYO HAKUVIOMBA

1. Hakuomba kwamba Mungu awaue adui zake wa Ufalme wake!

2. Hakuomba kwamba Mungu ampe utajiri kwa ajili yake mwenyewe! Wewe unayefukuzana na fedha sikuzote hapa unadhani ungeomba nini?

3. Hakuomba kwamba Mungu ampe maisha marefu.

VITU ALIVYOVIOMBA

1. Aliomba apewe akili za kujua jinsi ya kuhukumu watu wa Mungu kama mtawala juu yao.

2. Aliomba apewe moyo wa kupambanua mema na mabaya ili aweze kutenda haki sawasawa na mapenzi ya Mungu.

>>Mungu alifurahishwa naye KWA KUWA HAKUOMBA KIUBINAFSI

>>Hakuomba lolote kwa ajili yake mwenyewe

MUNGU SIKUZOTE ANAFURAHISHWA NA KUPENDEZWA NA WALE WANAOOMBA KWAMBA MAPENZI YAKE MUNGU YATENDEKE HAPA CHINI YA JUA! MAPENZI YAKE KWA AJILI YA KANISA LAKE NA UFALME WAKE. YAANI, WALE WASIOOMBA KIBINAFSI! HUU NI MOYO WA MAOMBI UNAOTOKA KWAKE YESU.

VITU ALIVYOPEWA

1. ALIPEWA MOYO WA HEKIMA NA AKILI. ALIPEWA HEKIMA NA AKILI ZA MOYONI. ALIPEWA AKILI ZA ROHONI.

2. ALIPEWA AKILI NYINGI ZA MOYONI KIASI KWAMBA HAPAKUWA NA MTU KAMA YEYE KABLA YAKE NA BAADA YAKE!

Leo tuna Kitabu cha Mithali kwenye Biblia, Kitabu cha Mhubiri, na Kitabu cha Wimbo Ulio Bora kwenye Biblia alivyoviandika!

SIFA ZA SULEMANI

Alikuwa na hekima nyingi kupita watu wote (Solomon was a man of incredible and unprecedented renown because of his wisdom! He was blessed spiritually and mentally mpaka hapa tulipofikia kwenye somo letu!)

“29Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. 34Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.” (1 Fal 4:29-34)

>>Maelezo haya yanatosha  kuelezea ni jinsi gani Mfalme Sulemani alikuwa amebarikiwa!

SULEMANI ALIJIBIWA NA KUPEWA ZAIDI YA ALIVYOOMBA

 

“13Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.” (1 Fal 3:13)

>> NA MAMBO YALE USIYOYAOMBA NAYO NIMEKUPA

1. MALI.

2. FAHARI.

3. MALI NA FAHARI KULIKO MFALME YEYOTE BAADA YAKO.

New International Version
Moreover, I will give you what you have not asked for—both wealth and honor—so that in your lifetime you will have no equal among kings.

New Living Translation
And I will also give you what you did not ask for—riches and fame! No other king in all the world will be compared to you for the rest of your life!” (1 Kings 3:13)

1. WEALTH  & RICHES (UTAJIRI)

2. HONOUR (HESHIMA) AND FAME (UMAARUFU)

>> Do you get it now? It pleases God greatly when you seek his Kingdom first and his righteousness, because He has promised that all these other corruptibles and temporal or earthly things shall be added unto you bountifully. God wants you to set your heart completely on eternity and incorruption! The eternal destiny of humanity! This is the highest good you can do while you live, and this is the highest spirituality you can attain to in this life! [Mungu anakutaka uweke au uelekeze moyo wako wote kabisa kwenye mambo ya milele (umilele) na maisha ya kutoharibika! Weka moyo wako kwenye hatma ya milele ya wanadamu! Na kisha haya mambo yanayoharibika na ya muda mfupi ya hapa duniani utazidishiwa kwa wingi atakapoona moyo wako wote umeelekezwa huko kama apendavyo na atakavyo!!]

“20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;” (Efe 3:20)

“1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.” (Kol 3:1-4)

>>Nikupe siri ya utajiri na heshima wa kweli na udumuo: Kwa kiwango kile kile ambacho umeweka moyo wako na akili yako kutafuta, kuyawaza, kuyafikiri, kuyataka, kuyazingatia, kuyatamani, kuyahitaji, kuyaomba, na kuyatarajia mambo yasiyoharibika na ya milele, na hatma ya milele ya wanadamu; ndivyo utakavyopewa mambo ya thamani kwa ajili ya Ufalme wake, kwa utumishi uliotukuka, na haya mengine yenye kuharibika yatakukimbiza na kukufuata hata bila kuyaomba na kuyasumbukia bali Mungu mwenyewe atayaamuru yakufuate. Mungu wa Sulemani ndiye Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kamwe hakupungukiwa wala kuhitaji kwenye mazingira yeyote SIKUZOTE!! Yeye ndiye aliyepewa vitu vya thamani kutoka mbinguni ambavyo si vya kibinadamu hata kuiona shekeli iliyomo kwenye kinywa cha samaki wa kwanza kuvuliwa na Petro ili kulipa kodi ya hekalu; Huyu ndiye aliyezidisha mikate mitano na samaki wawili mpaka kulisha watu elfu tano; Huyu ndiye aliyegeuza maji kuwa divai; Huyu ndiye aliyetembea juu ya maji kwenda kwenye huduma; Huyu ndiye mapepo na majini walipomuona walimkimbilia na kusujudu miguuni pake wakimsihi asiwatese; Huyu ndiye aliyejua mawazo ya mwanadamu vile anavyofikiri kwa siri moyoni mwake; Huyu ndiye ambaye ALIJUA MAJIBU YA MASWALI YOTE; Huyu ndiye ambaye ALIKUWA NA SULUHISHO LA MATATIZO YOTE; Huyu ndiye ambaye ALIPONYA WOTE; Huyu ndiye ambaye aliona na kujua mambo yote ya duniani yaliyopita, yaliyopo, na yajayo mpaka mwisho wa dunia. Huyu ndiye alijua idadi ya nywele za kila mwanafunzi wake amwaminiye; Huyu ndiye ambaye amehesabu hatua zako zote utakazopiga ukiwa kwenye mwili huu wa damu na nyama; YESU MWANA WA MUNGU. Alisema kuhusu Mfalme Sulemani; “42Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.” (Mt 12:42)

>>Malkia wa kusini alitoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani, lakini akasema Yeye Mwana wa Mungu ni mkuu kuliko Sulemani!!! Glory! Haleluya! YESU NI MKUU KULIKO SULEMANI! HEKIMA YA SULEMANI ILITOKA KWAKE NENO! ALIYEKUJA KUVAA MWILI AKAITWA YESU! YESU ALINENA KUPITIA SULEMANI! YESU ALIMUUMBA SULEMANI MAANA WANADAMU WALIUMBWA KWA NENO! YESU NI NENO! (Kol 1:16) Maandiko yanasema kwamba Yesu amefanywa kwetu tuaminio kuwa hekima itokayo kwa Mungu (1 Kor 1:30). Biblia inasema, “23bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; 24bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.” (1 Kor 1:23-24)

YESU NDIYE HEKIMA YA ALIYEOKOKA! YESU NDIYE NGUVU ZA MUNGU ZA ALIYEOKOKA! YESU NDIYE HEKIMA YA MUNGU NDANI ZA ALIYEOKOKA! YESU NDIYE AKILI ZAKO WEWE ULIYEOKOKA! HUNA YESU, HUNA AKILI! MKATAE YESU, JUA UNAKATAA AKILI ZA MUNGU! KWA WEWE ULIYEOKOKA MAFUNDISHO HAYA YANAKUPA AKILI NA HEKIMA KUTOKA JUU, ILI UWAZE NA KUYATAFUTA YALE YA JUU YASIYOHARIBIKA NA YANAYODUMU! MBIO ZA KUFUKUZIA TU PEKE YAKE YALE YANAYOHARIBIKA NI MBIO ZA UPUMBAVU! YAANI, MBIO ZA KUKIMBILIA KWENYE SHIMO LA UHARIBIFU! NI MBIO ZA UBINAFSI NA UASI! UNAJIPIGANIA WEWE MWENYEWE NA MWISHO WAKO NI KUANGAMIA! MWAMINI NA UMTUMAINI YESU NAYE ATAKUPA AKILI  ZA MOYONI KATIKA MAMBO YOTE TIMOTHEO!!!

“7Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.” (2 Tim 2:7)

AKILI ZA KWELI, AKILI ZA MOYONI, AKILI ZA ROHONI, AKILI  ZA YESU, HUTOKA KWAKE MWENYEWE YESU, KWA ROHO WAKE YESU!!

>>HUKU NDIKO KUBARIKIWA KIAKILI; UNAKUWA NA AKILI KAMA YESU! UNA AKILI ZA YESU! UNA AKILI ZA NENO! UNA AKILI ZA ROHO MTAKATIFU! Haleluya!

“9Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo” (Ufu 17:9)

>>ALIYEBARIKIWA KIAKILI ANA AKILI ZENYE HEKIMA YA NENO!!!  Scripture-Minded! Word-Minded! Bible-Minded! Christ- Minded! Spirit-Minded! Glory to Jesus!

“33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! 34Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?” (Rum 11:33-34)

[33Oh, the depth of the riches of the wisdom and knowledge of God! How unsearchable his judgments, and his paths beyond tracing out! 34“Who has known the mind of the Lord? Or who has been his counselor?”]

NA TENA;

“16Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.” (1 Kor 2:16)

[16for, “Who has known the mind of the Lord so as to instruct him?” d  But we have the mind of Christ.]

>>WE HAVE THE MIND OF CHRIST! THIS IS HOW WE HAVE BEEN BLESSED MENTALLY! GLORY TO JRSUS, HALELLUJAH!

>> TUMEBARIKIWA KWA AKILI NA MAWAZO YA KRISTO! TUNA HEKIMA NA AKILI ZA KRISTO!

“2ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; 3ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.” (Kol 2:2-3)

>>HAZINA (TREASURES) ZOTE ZA HEKIMA NA MAARIFA ZIMO NDANI YAKE YESU, AMBAYE YUMO NDANI YAKO!!!

>>UNA UTAJIRI USIOPIMIKA WA HEKIMA NA MAARIFA! (YOU ARE RICHLY BLESSED MENTALLY)

KAMA DUNIA ISIPOKUJA KUTAFUTA NA KUULIZIA HEKIMA KWAKO ULIYEOKOKA, BADO UNA JUKUMU LA KUENDELEA KUYATAFUTA YALE YALIYO JUU MBINGUNI ALIKO KRISTO AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU; NA KUACHA KUYAKIMBIZA YALE YANAYOHARIBIKA NA YA MUDA MFUPI YA HAPA DUNIANI; BADILISHA VIPAUMBELE VYAKO VYA KUTAFUTA NA TAKASA MOYO WAKO UTAMANI NA KUTAFUTA NA KUTAKA SANA SIKUZOTE YALE YALIYO JUU NA YASIYOHARIBIKA, ILI UPEWE VITU VYA THAMANI KUTOKA KWENYE HAZINA ZA HEKIMA NA MAARIFA ZILIZOMO NDANI YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU. AMEN, UBARIKIWE.

 

Tukutane kwenye Baraka za Kihisia (Emotional Blessings)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post