NDOA YA ANGUKO
Ndoa ya Anguko ni ndoa iliyomuasi Mungu! Ni ndoa iliyolikataa Neno la Mungu!
Ni ndoa isiyomtaka Mungu! Ni ndoa isiyomtegemea Mungu! Ni ndoa inayotegemea
nguvu zake, juhudi zake, akili zake, mipango yake, utatuzi wake, suluhisho
lake, mipango yake, elimu yake, fedha zake, mali zake, mbinu zake, utajiri
wake, miungu yake, PASIPO MUNGU!! Ni ndoa inayoendeshwa kwa akili, uweza,
maarifa, na matakwa ya mwanadamu! Ni ndoa isiyo na Yesu moyoni!! Ni ndoa isiyo
na Neno la Mungu moyoni! Ni ndoa yenye neno la "nyoka moyoni" badala
ya Neno la Mungu!! Ni ndoa isiyompendeza Mungu maana inayafanya mapenzi ya
nyoka!! Ni ndoa yenye uadui na Mungu aliyeiumba kama maandiko yanenavyo:
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani
waweza kula,
Mwanzo 2:16
>> Adamu aliambiwa na Mungu kwamba anaweza kula matunda ya kila mti wa
bustani!
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku
utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 2:17
>> Alikatazwa kula matunda ya mti mmoja tu: MTI WA UJUZI WA MEMA NA
MABAYA!
Baada ya mwanamume kupewa Neno hili la Mungu akafanyiwa na kuletewa msaidizi wa
kufanana naye!! KWENYE NDOA TAKATIFU WANANDOA LAZIMA WAFANANE MAANA WOTE WAWILI
WALIUMBWA WAKIFANANA NA MUNGU! (Mwanzo 1:26). Mungu ni Roho na hivyo kufanana
huku na Mungu ni katika roho uliyonayo kutoka kwake, roho ambayo ndiyo inakupa
akili na mawazo kutoka kwake!! Kwa hiyo una roho itokayo kwa Mungu, na pia una
mawazo kama yake, fikra kama zake, akili kama zake maana UMELIKUBALI,
UMELIPOKEA, UMELISHIKA, UNALITAFAKARI, UNALITENDA, UNALIFANYA, NA UNALIISHI
NENO LAKE!! Maisha yako unaishi kama Mungu maana Yeye ni Neno Lililo Hai!!
Mwanadamu ambaye ni roho, ana nafsi, na anaishi kwenye mwili anafanana na
Muumba wake rohoni na nafsini kama anaishi kwa kila neno litokalo katika kinywa
cha Mungu (Mathayo 4:4)
>> Mwanamume aliambiwa kwamba siku atakayokula matunda ya mti wa ujuzi wa
mema na mabaya ATAKUFA HAKIKA!! Mwanamke aliambiwa Neno hili na mumewe maana
hakuwa ameumbwa Mungu alipomwambia mwanamume hili Neno!! Tafakari: ADAMU
ALIKUWA NA UMRI MKUBWA KULIKO HAWA MAANA ALITANGULIA KUUMBWA, NA MKEWE AKAUMBWA BAADAE!!
KWENYE NDOA TAKATIFU MWANAMUME ANA UMRI UNAOMZIDI MKE WAKE!! Kama mwanamume amezidiwa
umri na mkewe, Je! ni nani alitangulia kuumbwa katika tumbo la mama yake?
Unaweza kuona hapa uwezekano wa kuwa huyo hakuwa mke wake sahihi!! (Tafakari
halafu ujijibu mwenyewe!!)Tazama: MASWALI MUHIMU KUHUSU NDOA
>> Nyoka alipokuja kwa mwanamke alianza kwa kupotosha Neno la Mungu:
"1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya
Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile
matunda ya miti yote ya bustani?"
Mwanzo 3:1
>> ATI HIVI NDIVYO ALIVYOSEMA MUNGU, MSILE MATUNDA YA MITI YOTE YA
BUSTANI??!! Linganisha maneno haya na mstari huu: [" 16 Bwana Mungu
akamwagiza huyo mtu, akisema, MATUNDA YA KILA MTI WA BUSTANI WAWEZA KULA,
Mwanzo 2:16]
>> shetani ndivyo anavyokuletea mawazo yaliyo kinyume na Neno la Mungu!!
Analeta mashaka kwa neno!! Kwamba hivi kweli Mungu kasema hivi au vile? roho ya
shetani ni roho inayopotosha na kugeuza Neno!!
>> Kosa la kwanza la mwanamke ni kukubali kujibizana na ile roho
iliyorusha wazo ovu lililo kinyume na Neno! Alitakiwa aikemee ile roho na
kulikataa lile wazo, na kumkemea shetani aondoke pale alipo!! Alipomjibu kwenye
Mwanzo 3: 2-3 shetani akarusha mshale wake wa moto kwenye mst wa 4!
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
Mwanzo 3:2
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala
msiyaguse, msije mkafa.
Mwanzo 3:3
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3:4
>> HAPA NAPO NYOKA ANAIGEUZA KWELI KUWA UONGO!! Linganisha na mstari huu:
[ 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana SIKU
UTAKAPOKULA MATUNDA YA MTI HUO UTAKUFA HAKIKA.
Mwanzo 2:17]
>> Hapa pana UTAKUFA HAKIKA VS HAKIKA HAMTAKUFA
Hii ndiyo dhambi!! Huyu ndiye shetani! Huu ndio uasi!Ä€ Huu ndio
ukengeufu! Huu ndio upotovu! Yaani;
- KULIKATAA NENO LA MUNGU,
- KULIASI NENO LA MUNGU,
- KULIPUUZA NENO,
- KULIDHARAU NENO,
- KUTOKUWA NA HAJA NA NENO,
- KUAMINI KINGINE KILICHO KINYUME NA NENO,
- KUTOLIZINGATIA NENO,
- KURIDHIKA NA UFANYAJI MAAMUZI PASIPO KUZINGATIA NENO,
- KUISHI PASIPO KUONGOZWA NA NENO,
- KUBISHANA NA NENO,
- KUFANYA, KUTENDA, NA KUENENDA PASIPO KULIFUATA WALA KUONGOZWA NA NENO,
- KULIONEA MASHAKA NENO,
- KULIGHADHIBIKIA NENO,
- KULIKANUSHA NENO KABISA KUWA SIYO LA KWELI,
- KULIGEUZA NENO KUWA LIMESEMA UONGO,
- KUIGEUZA KWELI KUWA UONGO!! Hivi ndivyo shetani alivyomdanganya/alivyompotosha/alivyomkengeusha/na kumpoteza mwanamke AMBAYE ALIIKANA KWELI KWA MATENDO YAKE, AKAFANYA MAAMUZI YAKE YEYE MWENYEWE KIVYAKE PASIPO KUMSHIRIKISHA MUMEWE: AKATWAA KATIKA YALE MATUNDA, NA KISHA AKAYALA!! AKAMPA MUMEWE, NAYE AKAYALA!! Sasa tumeona kwenye masomo yaliyotangulia kwamba mwanamume ni kichwa cha mkewe, kwa maana ya kuwa kiongozi wa mkewe na mchungaji wa kanisa la ndoa KWENYE NDOA TAKATIFU!! Hapa mwanamke, kwa kushawishiwa na nyoka, anafanya maamuzi kinyume na Kweli!! Alichofanya mwanamke hapa:
1) NI KULIASI NENO LA MUNGU MOJA KWA MOJA
2) NI KULIACHA NENO LA KWELI NA KUAMINI UONGO
3) NI KUASI MAMLAKA KWA KUCHUKUA UONGOZI TOKA KWA MWANAMUME KWA KUFANYA MAAMUZI
MAKUBWA YA NDOA PASIPO HATA KUMSHIRIKISHA MUMEWE! ALIASI MAMLAKA YA MUMEWE, NA
KUMUASI MUNGU ALIYEMWEKA KUWA MSAIDIZI NA SIYO KIONGOZI!
4) MWANAMKE AKICHUKUA UONGOZI WA KIROHO TOKA KWA MWANAMUME LAZIMA ADANGANYIKE
KIRAHISI NA KUASI MAANA HAKUUMBWA KUONGOZA BALI KUSAIDIA!! HANA MAFUTA YA
UONGOZI WA KIROHO!!
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye. (Mwanzo 2:18)
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe
katika utulivu. (1 Timotheo 2:12)
13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. (1 Timotheo 2:13)
14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika
hali ya kukosa.
(1 Timotheo 2:14)
>> Uongozi uliwekwa kwa mwanamume na siyo mwanamke! Hii ndiyo maana
mwanamume aliumbwa kwanza, akaanza kumjua Mungu kwanza, kuwa na ushirika
na Mungu kwanza, kufanya kazi na Mungu kwanza, baada ya kukabidhiwa UONGOZI NA UTAWALA JUU
YA UUMBAJI WOTE PALE BUSTANINI, akapewa pia majukumu ya kazi za mikono
bustanini kuilima na kuitunza (Mwanzo 2:15), akaambiwa Neno la Mungu la kuishi
nalo bustanini, akapewa chakula na sehemu ya kuishi, NA KISHA NDIPO AKALETEWA
MSAIDIZI!!
5) MWANAMKE ALITENDA KWA KIBURI PALE ALIPOCHUKUA MAAMUZI YA KIUONGOZI WAKATI
YEYE SIO KIONGOZI!! ALIPINGANA NA MUNGU ALIYEWEKA UTARATIBU HUO YEYE MWENYEWE,
KWA HEKIMA YAKE NA UTAKATIFU WAKE! LAKINI PIA ALIMDHARAU NA KUMUASI MUMEWE MAANA
HAKUTHAMINI WALA KUTAMBUA NA KUHESHIMU NAFASI YA MWANAMUME ALIYOPEWA NA MUNGU
KATIKA KUUMBA KWAKE!! HIKI NI KIBURI KILE KILE KILICHOMUANGUSHA SHETANI PALE
ALIPOTAKA KUWA MUNGU!! (Ezekiel 28:12-19 & ISAYA 14: 4-17) Dunia leo
ikiongozwa na shetani yule yule aliyemdanganya Hawa inamdanganya na
imemdanganya mwanamke KUCHUKUA UONGOZI WA KIROHO KUTOKA KWA MWANAMUME!! LENGO
NI KUMPANDIKIZA KIBURI KILE KILE KILICHOHARIBU NDOA ILE TAKATIFU YA ADAMU NA
HAWA HATA IKAWA NDOA YA ANGUKO ILIPOINGIA DHAMBI!!
6) MWANAMKE ALIKUBALI USHAWISHI KUTOKA "NJE" YA NDOA NA KUUTENDEA
KAZI " NDANI" YA NDOA!! HIVI NDIVYO NDOA ZA ANGUKO ZILIVYO LEO! DUNIA
INA USHAWISHI MWINGI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI, UTANDAWAZI, NA HARAKATI NYINGI
ZINAZOMLENGA MWANAMKE AMBAZO ZOTE UKIZICHUNGUZA ZINALENGA KUMPOTOSHA MWANAMKE
NA KWENDA KUVURUGA UTARATIBU WA MUNGU KWENYE NDOA YAKE ILI AYAFANYE MAPENZI YA
SHETANI! MWANAMKE UNATAKIWA UMBEBE YESU SIKUZOTE NA UPOKEE USHAWISHI WA NENO
LAKE NA SIYO USHAWISHI WA DUNIA!!
7) KITENDO CHA KUTWAA MATUNDA YA ULE MTI, AKALA KWANZA, NA KISHA AKAMLETEA
MUMEWE ALE KINAMAANISHA MWANAMKE ALIKUWA SASA ANATOA AMRI KWA MUMEWE!! YAANI,
NENO LA MWANAMKE SASA LINA NGUVU KULIKO NENO LA MUNGU ALILONALO MUMEWE!!
UTARATIBU MZIMA SASA UMEBADILIKA NA MWANAMUME ANASIKILIZA AMRI ZA MKEWE!! ADAMU
MUME WANGU, MATUNDA HAYA MATAMU HEBU KULA NAWEEE! ADAMU AKALA!!
MWANAMUME
>> MWANAMUME YEYE ALIMSIKILIZA MKEWE AKALA! HII INAMAANISHA ALIRIDHIA
YOTE ALIYOYAFANYA MKEWE NA YEYE MWENYEWE AKAASI!
[NDOA YA ANGUKO = HAWA ALIYEDANGANYWA + ADAMU ALIYEASI]
>> ADAMU ALIPOASI SHETANI "NYOKA" AKAWA NDIYE MTAWALA NA mungu
JUU YA UUMBAJI WOTE BADALA YA ADAMU ALIYEASI!!
>> MWANAMKE ALIPOPORA MAMLAKA (URSUP AUTHORITY) SHETANI AKAWA ANATAWALA!!
ADAMU AKARUHUSU (SANCTION) HILO LITOKEE!! KUMBUKA SERIKALI YA MUNGU ALIKABIDHIWA
MWANAMUME! YEYE AKAIACHIA MAMLAKA HIYO KWA NYOKA KUPITIA MKEWE!! Ndoa za Anguko ziko hivyo:
HAWA (MKE) KIVYAKE KIMAAMUZI NA KIMIPANGO na ADAMU (MUME) ANARIDHIA!! Hii
imepoteza na kuharibu wengi makanisani na kwenye jamii zetu!!
NDOA YA ANGUKO-SEHEMU YA PILI
>> HIVI NDIVYO DHAMBI ILIVYOINGIA KWENYE NDOA NA KUINGIA ULIMWENGUNI
KOTE!! WATOTO WOTE TUMEZALIWA KWENYE NDOA HIZO ULIMWENGUNI!! DAUDI ALIANDIKA:
Psalms 51:5
[5]Behold, I was shapen in iniquity; and in sin did my mother conceive me.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba
hatiani.
>> WANADAMU WOTE WALIUMBWA MATUMBONI MWA MAMA ZAO KATIKA HALI YA UOVU, NA
WAKAZALIWA HIVYO KWENYE DINI NA MADHEHEBU YAO!!
>> MIMBA ZA WANADAMU WOTE ZILITUNGWA HATIANI (DHAMBINI)
>> Anachosema Daudi ni kwamba KUNA MIMBA ZINATUNGWA KATIKA UTAKATIFU
(KWENYE NDOA TAKATIFU) na KUNA MIMBA ZINATUNGWA KWENYE DHAMBI! (KWENYE NDOA ZA
ANGUKO) WALE WANAOZALIWA KWENYE NDOA TAKATIFU HUWA WANAZALIWA NA AHADI KWA
WAZAZI WAO KUHUSU KUOKOKA KWAO NA HIVYO KUNA NEEMA YA MUNGU JUU YAO TAYARI
KUPITIA WAZAZI!! NI LAZIMA WATAOKOKA KWA SABABU NI MPANGO NA KUSUDI LA MUNGU!!
NA PIA WAKO SALAMA KWA KUWA WAZAZI WAO WAMEOKOKA! WALE WANAOZALIWA KWENYE NDOA ZA ANGUKO HAWANA NEEMA HIYO, NA WANAZALIWA WAKIWA
CHINI YA UFALME, MAMLAKA, NA NGUVU ZA GIZA!! WANAOKOKA WANAPOISIKIA INJILI NA
KUIAMINI, NA KUTUBU, NA KUMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAO!!
>> Kwa mujibu wa andiko hili: " Psalms 51:5
[5]Behold, I was shapen in iniquity; and in sin did my mother conceive me.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba
hatiani." KILA DINI NA KILA DHEHEBU DUNIANI HUPOKEA WAABUDUO "WATENDA
DHAMBI" KUTOKA KWENYE "NDOA ZA ANGUKO"!!! NA HII NDIYO MAANA
YESU ALISEMA NI LAZIMA KUZALIWA MARA YA PILI KIROHO KWENYE UFALME WA MUNGU!!
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya
pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Yohana 3:3
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia
tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
Yohana 3:4
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho,
hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Yohana 3:5
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
Yohana 3:6
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Yohana 3:7
>> Na tena:
4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu,
ulipofunuliwa, alituokoa;
Tito 3:4
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,
kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Tito 3:5
6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
Tito 3:6
7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa
milele, kama lilivyo tumaini letu.
Tito 3:7
>> Na hapa tena,
23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile
isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
1 Petro 1:23
WOKOVU (KUZALIWA MARA YA PILI) NDIO UNAOONDOA DHAMBI ZOTE NA KUONDOA
MATOKEO YOTE HASI YA DHAMBI KWENYE ROHO, NAFSI, MWILI, NA MAISHA YA MWANADAMU
KADIRI ANAVYOISHI NA KUENENDA KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU,
NA KUKUA KATIKA NEEMA YA MUNGU NA KATIKA KUMJUA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI
WETU!!
>> KWA WANANDOA AMBAO MMOJA AMETANGULIA KUOKOKA NENO LA AHADI NI HILI:
30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate
kuokoka?
Matendo ya Mitume 16:30
31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Matendo ya Mitume 16:31
NA TENA:
37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume
wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Matendo ya Mitume 2:37
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo,
mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 2:38
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu
wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Matendo ya Mitume 2:39
>> Kisha maagizo ya Bwana Yesu ni haya:
12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu
mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
1 Wakorintho 7:12
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa
naye, asimwache mumewe.
1 Wakorintho 7:13
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke
asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu
wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
1 Wakorintho 7:14
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au
ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
1 Wakorintho 7:15
16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe
mwanamume, kama utamwokoa mkeo?
1 Wakorintho 7:16
>> HIVI NDIVYO NDOA YA ANGUKO INAVYOWEZA KUGEUKA KUWA NDOA TAKATIFU KUPITIA NEEMA YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WA DUNIA YOTE!
3Maana
hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi,
tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi
katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 4Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5si
kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake,
kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. (Tito 3:3-7)