UAMSHO WA NDOA
JIBU MASWALI HAYA YAFUATAYO KIMAANDIKO, NA KIMAOMBI MBELE ZA MUNGU ILI
NURU YA UZIMA IANGAZIE NDOA ZA JANA, LEO, NA KESHO ILI KUZIFUFUA NA
KULETA UAMSHO WA NDOA NA FAMILIA!!
1) JE! MIGOGORO YA NDOA INASABABISHWA NA NINI?
2) KWA NINI HAKUNAGA SULUHISHO MPAKA WANANDOA WANAFIKIA KUTALIKIANA?
3) NINI KIFANYIKE KUZUIA MIGOGORO YA NDOA NA KUVUNJIKA KWA NDOA?
4) KWA NINI WANANDOA HUFIKIA KUCHOKANA?
5) NI JINSI GANI MKE NA MUME KILA MMOJA HUCHANGIA KUZOROTA NA HATIMAYE KUVUNJIKA NDOA YAO?
6) JE! INAWEZEKANA MKE AU MUME PEKE YAKE AKAWA SABABU YA KUZOROTA MPAKA KUVUNJIKA NDOA?
7) KWA NINI WANANDOA HUCHEPUKA?
8) NINI KIFANYIKE KUKOMESHA MICHEPUKO?
9) NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI WANA SEHEMU GANI KATIKA KUZOROTESHA NA HATA KUVUNJA NDOA?
10) FEDHA INA MCHANGO UPI KATIKA KUZOROTESHA NA HATA KUVUNJA NDOA?
11) ELIMU YA MKE AU MUME INA MCHANGO GANI KWENYE KUDHOOFISHA AU HATA KUVUNJA NDOA?
12) NDOA ZA MAPEMA KWENYE UMRI MDOGO ZINADUMU AU HAZIDUMU? KWA NINI?
13) KWA NINI KUNA ONGEZEKO LA WADADA KUZALISHWA NA KUKIMBIWA KABLA YA NDOA?
14) NDOA BORA NA IMARA NI IPI?
15) UDANGANYIFU KWENYE FEDHA WA MKE AU MUME HUSABABISHWA NA NINI? NA SULUHISHO LAKE NI LIPI?
16) TABIA YA KUPENDA FEDHA MKE AU MUME INAATHIRI VIPI NDOA?
17) KWA NINI MKE AMDHARAU MUME? AU MUME AMDHARAU MKE? HII INAATHIRI VIPI NDOA? NA SULUHISHO LAKE NI LIPI?
18) UTANDAWAZI UNA MCHANGO UPI KWENYE KUZOROTESHA, KUHARIBU, AU HATA KUVUNJA NDOA?
19) DHAMBI AU UTAKATIFU VINA ATHARI ZIPI KWENYE NDOA?
20) JE? TALAKA NI SULUHISHO LA MATATIZO YA NDOA?
21) MALEZI NA MAKUZI YA WAZAZI NA WALEZI YANA ATHARI ZIPI KWENYE KUANDAA TALAKA ZA NDOA ZA KESHO ZA WATOTO WAO?
22) JE! NGUVU ZA GIZA ZINA SEHEMU GANI KWENYE KUVUNJA NDOA? NINI KIFANYIKE KUZISHINDA NGUVU HIZO ZA SHETANI?
23) NI SAHIHI MZEE KUOA BINTI MDOGO ANAYEFANANA NA MWANAWE? NA JE! NI
SAHIHI MAMA MTU MZIMA KUOLEWA NA KIJANA ANAYELINGANA NA MWANAWE? KWA
NINI? ATHARI ZAKE NI ZIPI KWENYE NDOA ZA AINA HII?
24) JE! NI SAHIHI MWANAMUME AMUOE MWANAMKE ALIYEMZIDI KIPATO? KUNA
ATHARI ZIPI KWENYE NDOA IKIWA MUME HANA AU AMEZIDIWA KIPATO NA MKEWE?
25) KUNA ATHARI ZIPI KWENYE NDOA IKIWA MUME AMEZIDIWA SANA KIELIMU NA MKEWE?
26) JE! WAZAZI WA MKE AU MUME WANA MCHANGO UPI KWENYE KUDHOOFISHA AU HATA KUVUNJA NDOA?
30) JE! WATOTO WANAOZALIWA KWENYE NDOA WANAWEZA KUWA NA MCHANGO KWENYE KUDHOOFISHA AU KUVUNJA NDOA?
31) JE! AJIRA AU BIASHARA ZINAWEZA KUCHANGIA KUDHOOFISHA NA HATA KUVUNJA NDOA?
32) JE! IMANI POTOFU ZINACHANGIAJE KUDHOOFISHA AU HATA KUVUNJA NDOA?
33) UCHOYO NA UBINAFSI VINACHANGIAJE KUDHOOFISHA NA HATA KUVUNJA NDOA?
34) NINI MAANA YA KUAMBATANA? NINI PIA MAANA YA MWILI MMOJA?
35) JE! NDOA INAWEZAJE KUSABABISHA WANANDOA WAENDE AMA MBINGUNI AU JEHANAMU BAADA YA MAISHA HAYA?
36) 4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
Mathayo 19:4
>> UNADHANI NI KWA NINI MUNGU ALIANZA KUWAUMBA MTU MUME NA MTU MKE (NDOA) HAPO MWANZO KABISA?
>> JE! UNADHANI ALIYEGEUZA HII IKAWA "MTU MUME-MKE, NA MTU MKE-MUME NI NANI?
37) DHAMBI ILIINGIA ULIMWENGUNI KUPITIA NDOA, UNADHANI DHAMBI ITAONDOKAJE ULIMWENGUNI KUPITIA NDOA HIYO HIYO?
38) JE! UDANGANYIFU WA MWANAMKE BUSTANINI EDENI UNA MCHANGO GANI KWENYE KUVUNJIKA NDOA LEO HII?
14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
1 Timotheo 2:14
39) 17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala
matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa
kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
Mwanzo 3:17
>> KITENDO CHA MWANAMUME WA KWANZA KUISIKILIZA SAUTI YA MKEWE HAWA
NA KURIDHIA UASI WAKE, NA YEYE KULA MATUNDA, KUMEATHIRI VIPI NDOA, NA
KUNACHANGIA VIPI NDOA, NA HUDUMA KUDHOOFIKA NA KUVUNJIKA?