KWELI ZA BIBLIA KUHUSU KUSANYIKO LA WATAKATIFU

 


KWELI ZA KIBIBLIA KUHUSU KANISA (LA WATAKATIFU) WALIONUNULIWA KWA DAMU YA YESU (BIBLICAL BLUEPRINT OF THE CHURCH)

DIBAJI

Biblia inasema, "wala msimpe Ibilisi nafasi" (Efe 4:27)! Kutofanya haya yafuatayo kwa wachungaji, waume, wake, wababa, wamama, watoto, mashemasi, wazee wa kanisa, washirika, na waaminio wote KUMEMPA IBILISI NAFASI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO! Kutoamini ambako ni dhambi kwa mujibu wa Warumi 14:23 (b) kumesababisha matendo haya ya imani kukosekana kwenye mwili wa Kristo  au pengine ni kukosa maarifa (Hosea 4:6) ambako kumesababisha maangamizi mengi!  Biblia inasema,"17Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu. 19Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. 20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 21Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. 25Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa." (Yakobo 2: 17-26) Kilichoelezwa hapa ni jinsi ya kulitenda Neno (Yak 1:22). Lengo la mwanzo huu wa somo hili ni kukusaidia kutubu na kurejea kwa Roho na Neno lake ili uache KUWAONA WENGINE WAMEKOSEA, AU WAO NDIO WANA MATATIZO, au ule uovu wa kulalamika kwamba kanisa hivi, kanisa vile, fulani hivi, fulani vile, mchungaji hivi, n.k. WAKATI WEWE MWENYEWE UNGETAKIWA KUWA SEHEMU YA SULUHISHO NA UTATUZI na wala haukuwajibika na umebaki kwenye kutazama vibanzi vya wengine na boriti lako mwenyewe hulioni!!! HUWEZI KUAMINI HALAFU UKAWA NA ROHO WA MUNGU USIWE NA MAJIBU (answers) na suluhisho (solution) la chochote unachokiita tatizo kwenye kanisa (mwili wa Kristo)! Milima ipo mingi leo kwa kuwa hamna wale wenye imani kiasi cha punje ya haradali wenye KUIAMBIA MILIMA NG'OKA HAPA UKATUPWE BAHARINI NAYO IKAWATII!!(Marko 11:23)[ Unbelieving generation!] Kama uling'oa mlima fulani na unaamini haupo, kwa nini unausemasema? kwa nini unauzungumzia zungumzia badala ya kumshukuru na kumtukuza Mungu kwamba MOUNTAIN IS GONE!! (Tatizo limekwisha!! tatizo halipo limeondoka kwenye ndoa, familia, kanisani, kazini, kwenye biashara, mwilini mwako au mwake, n.k)! Soma hii uanze kutengeneza hatima yako ya neno kuhusu huduma yako, kanisa, mumeo, mkeo, wanao, kazi ya mikono yako, biashara yako, mchungaji wako n.k Na ukiona uliharibu kwa sababu ya kutoamini kwako halafu ukamsingizia mwingine labda mkeo au mumeo kwamba ndiye mwenye shida ( kama Adamu alivyomwambia Mungu, na Hawa kumsingizia shetani,) tubu na ukayatengeneze mambo ya nyumba yako! VINGINEVYO KUJIDANGANYA KWAMBA UKO SAWA KUTAKUPELEKA MAHALI PABAYA KIROHO, KIAKILI, KIHISIA, NA KIMWILI!

UTANGULIZI

Biblia inasema,

“Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia” (Waebrania 4:2)

>>Neno linamfaa/linamletea faida/linampa manufaa/linaleta matokeo kwa yeye anayesikia IKIWA TU LITACHANGANYIKA NA IMANI “NDANI YAKE” ANAYELISIKIA.

[Faida na manufaa ya Neno = (Neno lenyewe + Imani ya Neno hilo) Ndani yake Aliyeliamini ]

Kweli hizi zimewekwa katika msingi huo wa IMANI YA NENO ndani yake anayeliamini! Imani ya Neno ndani ya mwamini ni uhalisia wa kilichonenwa na kilichoandikwa ndani ya roho, nafsi, na mwili wa mwamini. Imani hii huwa inaelezewa (expressed) hivi;

“Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Rum 10:10)

New King James Version
For with the heart one believes unto righteousness, and with the mouth confession is made unto salvation.” (Rom 10:10)

>> MTU HUWA ANALIAMINI NENO KWA MOYO WAKE NA KULIKIRI KWA KINYWA CHAKE!

>>KULE KULIKIRI NENO KWA IMANI NI UUMBAJI KWA MAANA NENO LA MUNGU LINA NGUVU YA UUMBAJI (CREATIVE POWER)!

>>BWANA WETU YESU ALIKUJA KWENYE MWILI ILI KUWAPA WOTE WAMWAMINIO ILE NGUVU YA UUMBAJI KUPITIA VINYWA VYAO, KWA NJIA YA KULIAMINI NA KULIKIRI NENO KWA ROHO WAKE MTAKATIFU

>>KABLA YA UUMBAJI HUWA KUNA “UKIWA NA UTUPU” KATIKA ULIMWENGU WA ROHO WA MWAMINI KILA AMBAPO HAMNA NENO NA IMANI KATIKA NENO HILO

GENESIS 1:2

New Living Translation
The earth was formless and empty, and darkness covered the deep waters. And the Spirit of God was hovering over the surface of the waters.

English Standard Version
The earth was without form and void, and darkness was over the face of the deep. And the Spirit of God was hovering over the face of the waters.

“Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.” (Mwa1:2)

>> Mungu alipoanza kuumba palikuwa na UKIWA (FORMLESSNESS) NA UTUPU (VOID/EMPTINESS)

>> KATIKA UKIWA NA UTUPU HUO GIZA LILIKUWA JUU YAKE

>> KISHA ROHO WA MUNGU AKATULIA JUU YA MAJI!!

>> ALIPOTULIA ROHO WA MUNGU JUU YA UKIWA, UTUPU, NA GIZA HILO, NDIPO MUNGU AKASEMA NENO LAKE!!!

“Roho ya BWANA ilinena ndani yangu,

Na neno lake likawa ulimini mwangu.” (2 Sam 23:2)

>>ROHO MTAKATIFU NDANI YA MWAMINI HUNENA NENO LA MUNGU KUPITIA KINYWA CHAKE.

 

Biblia inasema,

“Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.” (Zab 33:6)

>> MUNGU ALIUMBA VYOTE KWA NENO LA KINYWA CHAKE KUPITIA ROHO WAKE (PUMZI YA KINYWA CHAKE)

“ Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama” (Zab 33:9)

Na hapa asema,

“Roho ya Mungu imeniumba,

Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.” (Ayu 33:4)

>> ROHO MTAKATIFU NI ROHO WA UUMBAJI NA NDIYE CHANZO CHA UHAI WOTE (Yoh 6:63)

>> MUNGU ALIPOUMBA KWA NENO LAKE KWA NJIA YA ROHO WAKE ALIONDOA,

1) ULE UTUPU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KWA KUUJAZA KILA ALICHOKUSUDIA KWA NENO LAKE.

2) ULE UKIWA, AU HALI ILE YA KUKOSEKANA MAUMBILE HALISI YANAYOELEWEKA (FORMLESSNESS), NA KUJAZA YALE YOTE ALIYOYAKUSUDIA MUNGU KWA NENO LAKE.

>> YESU ALIKUJA KUTUPA NGUVU NA MAMLAKA YA UUMBAJI WA KILA ALICHOSEMA MUNGU KUPITIA NENO LAKE AMBACHO NI MAPENZI YAKE KWETU NA KWA JAMII ZA WANADAMU WOTE.

-          mapenzi yake kwa mtu mmoja mmoja, kwa  [mke, mume, na ndoa], kwa familia, kwa kanisa, kwa taifa, kwa nchi (land/earth), kwa huduma, kwa kazi, kwa biashara, kwa mahusiano, kwa mchungaji, kwa ofisi tano za Yesu [kwa mtume, kwa nabii, kwa mchungaji, kwa mwalimu, na kwa mwinjilisti], kwa Ufalme wa Mungu, kwa Injili, kwa utoaji, kwa maombi, kwa kujitoa, kwa utakaso, kwa maisha ya imani, kwa utakatifu, kwa upendo wake, kwa kufikiri na kuwaza  kwetu, kwa kutafakari kwetu, kwa fedha zetu (upatikanaji na matumizi)……..KWA KILA ENEO LA MAISHA YETU!

>>Kwa kuwa anguko liliharibu utaratibu wote wa ulimwengu wa roho kwa kumpa shetani mamlaka na nguvu zake za giza basi KWENYE UUMBAJI WOTE WA MUNGU KUKAWA NA UKIWA NA UTUPU KUTOKANA NA GIZA LILILOTAWALA kuanzia kwenye ulimwengu wa roho hadi ulimwengu wa mwili. Yesu alifanya mapinduzi katika ulimwengu wa roho na kuwapa waaminio ufalme, akiisha kuwaweka kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu hapa ulimwenguni (Ufu 5:9-10)!

>>Mamlaka hii ya kifalme (royal authority) inatimizwa na kutekelezwa kwa njia ya imani katika Neno la Kristo lililojaa mioyoni mwa wafalme, walio watoto wa Mungu ndani ya KRISTO YESU, na WANALOLINENA KWA MAMLAKA VINYWANI MWAO KWA IMANI kwa sababu Mungu amewapa roho ya imani.  

 “Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena”  (2 Kor 4:13)

Na kwa habari ya neno la Mungu hilo linaloumba imeandikwa,

“Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” (Isa 55:9-10)

>> NENO LA MUNGU LINABEBA MAPENZI YAKE

>>NENO LA MUNGU KAMWE HALIWEZI KUMRUDIA MUNGU BURE PALE LINAPOKUWA LIMETAMKWA KWA IMANI NA MAMLAKA

>>NENO HILO LA MUNGU SIKU ZOTE HUFANIKIWA KUTIMIZA MAPENZI YOTE YA MUNGU YALIYOTAMKWA

>>NENO LA MUNGU HILO SIKUZOTE HUFANIKIWA KATIKA MAMBO YALE ALIYOLITUMA NA KAMWE HALISHINDWI

>>HII NDIYO MAMLAKA YA KIFALME (ROYAL AUTHORITY) YA MWANA WA MUNGU YA KULITAMKA NENO LA MUNGU KWA IMANI NA MAMLAKA NA KUUMBA MAPENZI YA MUNGU POPOTE PALE PENYE UKIWA NA UTUPU MAISHANI MWAKO AMBAO UMEANZIA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

 

Biblia inasema,

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika” (Yoh 1:1-3)

>>VYOTE VILIFANYIKA KWA HUYO (NENO), NA KWA KUWA YESU KRISTO NI YEYE YULE JANA, LEO, NA HATA MILELE (EBR 13:8), VYOTE UNAVYOTAKA VIFANYIKE LEO HAVIWEZI KUFANYIKA PASIPO NENO LAKE! NA VYOTE VITAFANYIKA MILELE YOTE KWA NENO LAKE! CHOCHOTE KINACHOFANYIKA NJE YA NENO LAKE SIYO CHA MUNGU!! NA CHOCHOTE AMBACHO SIYO CHA MUNGU KIKO CHINI YA MAMLAKA NA NGUVU ZA GIZA ZA SHETANI KATIKA UFALME WAKE!

>>PASIPO KUZINGATIA KANUNI HII HUWEZI KAMWE KUSHINDA VITA VYA KIROHO NA WALA HUWEZI KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU, NA PIAKAMWE HUWEZI  KUMILIKI NA KUTAWALA KAMA MFALME NA KUHANI KWA MUNGU PAMOJA NA YESU KATIKA UFALME WA MUNGU(KWENYE ULIMWENGU WA ROHO); NA ZAIDI, NI KWAMBA UTAANZISHA MAMBO MENGI YATAKAYOKWAMA NA KUSHINDWA HATIMAYE KWA SABABU KABLA YA KUANZA HUKUUMBA MAPENZI YA MUNGU KWENYE NDOA YAKO, AU KWENYE BIASHARA YAKO, AU KWENYE HUDUMA YAKO, AMA KAZI YA MIKONO YAKO, AU KWENYE FEDHA ZAKO N.K NA HIVYO UMEMPA IBILISI NAFASI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO KUPITIA ULE UKIWA NA UTUPU (SPIRITUAL VOID AND FORMLESSNESS)

>>KAMA ULIUMBA BASI KILA UTAKAPOKUTANA NA UPINZANI UTASHINDA NA HATIMAYE KUPOKEA AHADI KWA IMANI NA UVUMILIVU (1 YOH 5:4 & EBR 6:12-15)

Sasa ni saa ya kuamka usingizini na kuumba mapenzi ya Mungu yote kwa njia ya imani ya Yesu kwa Roho Mtakatifu! MAMLAKA YA KIFALME YA MWAMINI NI MAMLAKA YA UUMBAJI! Na uumbaji huu NDIO UNAOONDOA UKIWA NA UTUPU na kumuwezesha mwamini kushirikiana na Roho wa Mungu kufanikisha mapenzi ya Mungu hapa duniani. Pasipo hili hauna mamlaka kama mfalme hata kama unafunga na kuomba kila siku! Ama hautaona matokeo au utaona matokeo kiduchu ambayo hayampi Mungu utukufu wote anaostahili kama alivyofanya Yesu na akasema wewe unayeamini unaweza kufanya kama yeye alivyofanya na zaidi ya alivyofanya (Yohana 14:12).

 

IMANI KUHUSU KUSANYIKO (KANISA) LA WATAKATIFU WALIONUNULIWA KWA DAMU YA YESU

 

1) WAEFESO 1:4

“kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo”

IMANI:

v  WATOTO ALIONIPA BWANA KUWALISHA, KUWACHUNGA, NA KUWALEA NI WATAKATIFU WASIO NA HATIA MBELE ZA MUNGU (NDANI YA KRISTO) KATIKA PENDO LAKE.

2) 1 PETRO 1:14-16

“Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu”

IMANI:

v  KUNDI ALILONIWEKA BWANA KULISIMAMIA NA KULIONGOZA NI WATOTO WA KUTII, AMBAO NI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WAO WOTE KAMA YEYE ALIYEWAITA ALIVYO MTAKATIFU KAMA ILIVYOANDIKWA MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.

3) WAKOLOSAI 3: 12-13

“Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi”

IMANI:

v  KANISA NINALOLICHUNGA NA KULIONGOZA NI LAWATEULE WA MUNGU WATAKATIFU WAPENDWAO, WALIOJIVIKA MOYO WA REHEMA, UTU WEMA, UNYENYEKEVU, UPOLE, UVUMILIVU, WANAOCHUKULIANA, NA KUSAMEHEANA MTU AKIWA NA SABABU YA KUMLAUMU MWENZAKE, KAMA BWANA ALIVYOWASAMEHE WAO.

4) WAGALATIA 5:16, 18, 22-23

Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.  Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”

IMANI:

v  WATAKATIFU WA KANISA HILI (UNALITAJA) WOTE WANAENENDA KWA ROHO NA WALA HAWAZITIMIZI KAMWE TAMAA ZA MWILI, WANAONGOZWA NA ROHO, HAWAPO CHINI YA SHERIA, NA WANAMZALIA MUNGU TUNDA LA ROHO NDANI YA KRISTO YESU BWANA WETU.

5) MATENDO 2:4, WARUMI 8:14

“Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

IMANI:

v  KANISA LA YESU NINALOLIHUDUMIA WOTE WAMEJAZWA NA WANAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU MAANA WAO NI WANA WA MUNGU.

 

6) 1 KOR 3:16, RUM 8:9

“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”

IMANI:

v  KANISA HILI KILA MMOJA NI MWANA WA MUNGU NAYE NI HEKALU LA MUNGU, ROHO MTAKATIFU ANAKAA NDANI YAKE, KAMWE HAUFUATI MWILI BALI ANAMFUATA ROHO; ANA ROHO WA KRISTO NDANI YAKE NA HIVYO NI MALI YA KRISTO.

7) ZECHARIA 4:6

“Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi”

IMANI:

v  KANISA HILI LILILONUNULIWA KWA DAMU YA YESU HAWAFANYI NENO LOLOTE KWA KUTEGEMEA UWEZO AU NGUVU ZAO BALI WANAMTEGEMEA MUNGU, NA WANATENDA YOTE KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAO.

8) WAKOLOSAI  3:16 & ZABURI 119:11

“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu; Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”

IMANI:

v  KANISA NINALOLISIMAMIA KILA MMOJA MOYONI MWAKE AMEJAA NENO LA KRISTO, NA WOTE WANAFUNDISHANA NA KUONYANA KWA ZABURI, NA NYIMBO, NA TENZI ZA ROHONI, HUKU WAKIMWIMBIA MUNGU KWA NEEMA MIOYONI MWAO, NA WALA HAKUNA ANAYEMTENDA DHAMBI MUNGU KWA KUWA AMEJAA NENO LAKE NDANI YAKE.

9) YAKOBO 1:22 & MATHAYO 7:24-25

“Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu; Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba

IMANI:

v  WATAKATIFU KWENYE KANISA HILI(………) NI WATENDAJI WA NENO SIKUZAO ZOTE, MANENO YOTE YA KRISTO WANAYOYASIKIA WANAYATENDA, NA HIVYO WAMEJENGWA JUU YA MWAMBA, HIVYO HATA MVUA ZIKINYESHA, MAFURIKO YAKIJA, PEPO ZIKIVUMA, NA KUIPIGA NYUMBA YAO YA KIROHO, HAWAANGUKI, NA WANASIMAMA IMARA NDANI YA YESU KWA KUWA MISINGI YAO IKO JUU YA MWAMBA.

10) YOHANA 8:31-32, 36

“Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru; Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli” (Yoh 8:31-32, 36)

 

IMANI:

 

v  WATAKATIFU WA KANISA HILI (…..) WALIOMWAMINI YESU WANAKAA SIKUZOTE KATIKA NENO LA KRISTO, NAO WAMEKUWA WANAFUNZI WA YESU KWELI KWELI; NAO WANAIFAHAMU KWELI AMBAYO IMEWAWEKA HURU; NAO WAKO HURU KWELI KWELI, MAANA KRISTO YESU BWANA WAO AMEWAWEKA HURU.

 

11) 2 KOR 13:8 & 1 KOR 16:13

“Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli; Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote”

 

IMANI:

v  KANISA HILI (………..) MAISHA YETU YOTE HATUWEZI KUTENDA NENO LOLOTE KINYUME CHA KWELI BALI KWA AJILI YA KWELI MAANA ROHO WA KWELI ALIYE NDANI YETU ANATUONGOZA SIKUZOTE NA KUTUTIA KWENYE KWELI YOTE HATUA KWA HATUA.

 

12) YOHANA 4:23-24 & WAEFESO 4:15

“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli; Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI (………) AMBAO TU HEKALU LA ROHO MTAKATIFU TUNAMWABUDU BABA YETU WA MBINGUNI KATIKA ROHO NA KWELI NDANI YA YESU, AMBAYO NDIYO IBADA HALISI (TRUE WORSHIP), NA TUMEISHIKA KWELI KATIKA UPENDO, NA TUNAKUA HATA KUMFIKIA KRISTO YESU KATIKA YOTE, YEYE ALIYE KICHWA.

 

13) RUM 6:22, RUM 6:11 & RUM 6:14

“Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele; Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI LA KRISTO (………) TUMEWEKWA HURU MBALI NA DHAMBI, TUNAENDELEA KUTAKASWA, TUNA UZIMA WA MILELE, TUMEIFIA DHAMBI NA TUNAMWISHIA MUNGU NDANI YA KRISTO YESU; NA DHAMBI HAIWEZI KUTUTAWALA KWA MAANA HATUKO CHINI YA SHERIA BALI CHINI YA NEEMA.

 

14) 1 YOHANA 3:4-6 & 1 YOHANA 3:9

“Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua; Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.”

IMANI:

v  BWANA WETU YESU AMEZIONDOA DHAMBI MIOYONI MWETU SISI KANISA LAKE (………), NASI TUNAKAA NDANI YAKE NA WALA HATUTENDI DHAMBI; TUMEZALIWA NA MUNGU NA HIVYO HATUTENDI DHAMBI, KWA KUWA UZAO WAKE UNAKAA NDANI YETU; WALA HATUWEZI KUTENDA DHAMBI KWA KUWA TUMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU.

 

15) WARUMI 12:1-2

“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI (……….) LA KRISTO KILA MMOJA AMEUTOA MWILI WAKE KUWA DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU, AMBAYO NDIYO IBADA YETU YENYE MAANA. WALA HATUIFUATISHI NAMNA YA DUNIA HII; BALI TUMEGEUZWA KWA KUFANYWA UPYA NIA ZETU, TUNAZIDI KUYAJUA HAKIKA MAPENZI YA MUNGU YALIYO MEMA, YA KUMPENDEZA, YA KUMPENDEZA, NA UKAMILIFU.

 

     16) 1 KOR 9:27, GAL 5:24, RUM 8:8-9

“bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake; Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”

IMANI:

v  KATIKA KANISA HILI LA KRISTO (………) KILA MWAMINI ANAUTESA MWILI WAKE NA KUUTUMIKISHA ISIWE AKIISHA KUWAHUDUMIA WENGINE YEYE MWENYEWE AJE KUWA MTU WA KUKATALIWA; KILA MTAKATIFU AMEUSULUBISHA MWILI WAKE PAMOJA NA MAWAZO YAKE MABAYA NA TAMAA ZAKE; KANISA LINAMPENDEZA MUNGU KWA KUWA HAKUNA ANAYEUFUATA MWILI, BALI KILA MMOJA ANAMFUATA ROHO MTAKATIFU AMBAYE ANAKAA NDANI YAKE.

 

17) 1 WATHESALONIKE 4:4-5

“kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.”

 

IMANI:

KILA MMOJA KATIKA KANISA HILI (……..) ANAJUA JINSI YA KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA, NA SI KATIKA HALI YA TAMAA MBAYA KAMA MATAIFA WASIOMCHA MUNGU.

 

18) 2 TIM 4:7, WAEFESO 6:11 & YUDA 1:3

“Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;  Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani;  Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”

IMANI:

v  WATAKATIFU KATIKA KANISA HILI (……….) WANAVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI VYA IMANI KATIKA MWENDO WAO WA WOKOVU, WAKIILINDA NA KUISHINDANIA SANA IMANI YAO MPAKA MWISHO;  IMANI  WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU; WAMEVAA SILAHA ZOTE ZA MUNGU NA HIVYO WANAZIPINGA HILA ZA SHETANI, HUKU WAKIZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA NA KATIKA UWEZA WA NGUVU ZAKE KILA IITWAPO LEO.

 

19) 2 WAKORINTHO 10:3-5

“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;”

IMANI:

v  INGAWA WATAKATIFU KATIKA KANISA HILI (…….) WANAENENDA KATIKA MWILI, HAWAFANYI VITA KWA JINSI YA MWILI; MAANA SILAHA ZA VITA VYAO SI ZA MWILI BALI ZINA UWEZO KATIKA MUNGU HATA KUANGUSHA NGOME; WANAANGUSHA MAWAZO NA KILA KITU KILICHOINUKA, KIJIINUACHO JUU YA ELIMU YA MUNGU; HUKU WAKITEKA NYARA KILA FIKIRA IPATE KUMTII KRISTO.

 

20) 1 YOH 5:4, YOHANA 14:30 & 1 YOH 4:4

“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

IMANI:

v  KANISA HILI LA KRISTO (………) WAMEZALIWA NA MUNGU, NAO  WAMEUSHINDA ULIMWENGU KUPITIA IMANI YAO KWA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU; NA KWA KUUSHINDA ULIMWENGU WAMEMSHINDA MKUU WA ULIMWENGU SHETANI AMBAYE HANA CHOCHOTE DHIDI YA MWILI HUU WA KRISTO, KWA MAANA ALIYE NDANI YA WATAKATIFU HAWA NI MKUU KULIKO YEYE SHETANI mungu WA DUNIA HII. NALO KANISA HILI LIMEJENGWA JUU YA MWAMBA WALA MALANGO YA KUZIMU HAYAWEZI KULISHINDA.

 

21) WAEFESO 5:25b-27

“…….kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.”

 

IMANI:

v   KANISA LA KRISTO NINALOLISIMAMIA NI TAKATIFU, TUKUFU, LISILO NA ILA WALA KUNYANZI, HALINA MAWAA; LIMETAKASWA NA KUSAFISHWA KWA MAJI KATIKA NENO NA BWANA WETU YESU KRISTO,  ALIYELIPENDA NA KUJITOA  KWA AJILI YAKE

 

 

 

22) YOHANA 13:34

“Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.” (Yohana 13:34)

 

IMANI:

v  KANISA NINALOLICHUNGA WATAKATIFU WOTE WANAPENDANA VILE VILE KAMA KRISTO YESU ALIVYOWAPENDA, NA WATU WOTE WANATAMBUA YA KUWA HAWA NI WANAFUNZI WA YESU KWELI KWELI KWA SABABU WANA UPENDO WA KRISTO WAO KWA WAO.

 

23) 1 YOH 3:16

“Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI (………) WAMELIFAHAMU PENDO LA KRISTO ALIYEUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YAO, NA HIVYO NA WAO KILA MMOJA AMEUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA NDUGU ZAKE.

 

24) WAFILIPI 1: 9-11

“Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.”

 

IMANI:

v  KANISA ALILONIWEKA BWANA KULISIMAMIA PENDO LAO LINAZIDI KUWA JINGI SANA KATIKA HEKIMA NA UFAHAMU WOTE; WANAYAKUBALI YALIYO MEMA ILI WAPATE KUWA NA MIOYO SAFI, BILA KOSA, MPAKA SIKU YA KRISTO HALI WAMEJAZWA MATUNDA YA HAKI KWA NJIA YA YESU KRISTO KWA UTUKUFU NA SIFA YA MUNGU

 

25) WAEFESO 3: 16-19

“awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.”

 

IMANI:

v  KUNDI LA BWANA YESU NINALOLIONGOZA MUNGU AMEWAJALIA, KWA KADIRI YA UTAJIRI WA UTUKUFU WAKE, KUFANYWA IMARA KWA NGUVU, KWA KAZI YA ROHO WAKE KATIKA UTU WA NDANI. KRISTO ANAKAA MIOYONI MWAO KWA IMANI WAKIWA NA SHINA NA MSINGI KATIKA UPENDO; NA WANAFAHAMU PAMOJA NA WATAKATIFU WOTE JINSI ULIVYO UPANA, UREFU, KIMO, NA KINA, NA KUUJUA UPENDO WAKE KRISTO  UPITAO UFAHAMU KWA JINSI ULIVYO MWINGI, NAO WANATIMILIKA KATIKA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU.

 

 

26) WAEFESO 1: 17-23

“Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”

 

IMANI:

v  MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO, BABA WA UTUKUFU, ANAWAPA KANISA NINALOLIONGOZA, ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO  KATIKA KUMJUA YEYE; MACHO YA MIOYO YAO YANATIWA NURU, HIVYO WANALIJUA TUMAINI LA WITO WAO JINSI LILIVYO; NA UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE KATIKA WATAKATIFU JINSI ULIVYO; NA UBORA WA UKUU WA UWEZA WAKE NDANI YETU TUAMINIO JINSI ULIVYO; KWA KADIRI YA UTENDAJI WA NGUVU ZA UWEZA WAKE; ALIOTENDA KATIKA KRISTO ALIPOMFUFUA KATIKA WAFU, AKAMWEKA MKONO WAKE WA KUUME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO; JUU SANA KULIKO UFALME WOTE, NA MAMLAKA, NA USULTANI, NA NGUVU, NA KILA JINA LITAJWALO WALA SI ULIMWENGUNI HUMU TU BALI KATIKA ULE UJAO PIA; AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, AKAMWEKA AWE KICHWA JUU YA VITU VYOTE KWA AJILI YAO KANISA; AMBAO NDIO UKAMILIFU WAKE YEYE ANAYEKAMILIKA KWA VYOTE KATIKA YOTE.

 

27) WAKOLOSAI  1: 9-11

“Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;”

 

IMANI:

v  KANISA HILI LA KRISTO TUNAJAZWA MAARIFA YA MAPENZI YAKE KRISTO KATIKA HEKIMA YOTE NA UFAHAMU WA ROHONI; NA TUNAENENDA KAMA ULIVYO WAJIBU WETU KWAKE BWANA, TUKIMPENDEZA KABISA; NA KUMZALIA MATUNDA KWA KILA KAZI NJEMA, NA KUZIDI KATIKA MAARIFA YA MUNGU; HUKU TUKIWEZESHWA KWA UWEZO WOTE, KWA KADIRI YA NGUVU YA UTUKUFU WAKE, TUPATE KUWA NA SABURI YA KILA NAMNA NA UVUMILIVU PAMOJA NA FURAHA

 

28) YOHANA 15:7

 

“Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI (….) TUNAKAA NDANI YA YESU, NA MANENO YAKE YANAKAA NDANI YETU, HIVYO TUNAPOOMBA LOLOTE TULITAKALO TUNATENDEWA

 

29) YOHANA 15:16

“Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”

IMANI:

v  BWANA WETU YESU AMETUCHAGUA SISI KWANZA NAYE AMETUWEKA KATIKA KANISA HILI (….) NA TUNAMZALIA MATUNDA; NA MATUNDA YETU YANAKAA, NA HIVYO LOLOTE TUMWOMBALO BABA KWA JINA LAKE YESU ANATUPATIA.

30) MARKO 11:24 & 1 YOH 5:14-15

“Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.”

 

IMANI:

v  KATIKA KANISA HILI (….) YOYOTE TUYAOMBAYO TUNAPOSALI TUNAAMINI YA KWAMBA TUNAYAPOKEA, NAYO YANAKUWA YETU SIKUZOTE; NASI TUNA UJASIRI WOTE KWAKE KWA KUWA SIKUZOTE HUWA TUNAOMBA KILA KITU SAWASAWA NA MAPENZI YAKE,  NAYE ANATUSIKIA, NA KWA KUWA TUNAJUA KWAMBA ANATUSIKIA TUNAPOOMBA CHOCHOTE, TUNAJUA KWAMBA SIKUZOTE TUNAZO ZILE HAJA TUMWOMBAZO; SISI NI KANISA TUNAOOMBA NA KUPOKEA MAJIBU PALE PALE WAKATI TUNAOMBA, NA TUNAONDOKA NA MAJIBU YETU TUNAPOMALIZA KUOMBA.

 

31) 1 YOHANA 3:18-22

 

“Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote. Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.”

 

IMANI:

v  KWENYE KANISA LETU HILI (….) TUNAPENDANA SI KWA NENO WALA KWA ULIMI TU, BALI KWA TENDO NA KWELI; NA KWA SABABU HIYO MIOYO YETU HAITUHUKUMU NA TUMEITULIZA MBELE ZA MUNGU ANAYEJUA MIOYO; NA TUNAFAHAMU KWAMBA UPENDO WETU NI WA KWELI, NA LOLOTE TUOMBALO, TWALIPOKEA KWAKE, KWA KUWA TWAZISHIKA AMRI ZAKE, NA KUYATENDA YAPENDEZAYO MACHONI PAKE.

 

32) WAKOLOSAI  3 : 23-24

“Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.”

 

IMANI:

v  KUNDI HILI LA BWANA NINALOLISIMAMIA LOLOTE TULIFANYALO TUNALIFANYA KWA MOYO KAMA KWA BWANA, NA WALA SI KWA MWANADAMU, TUKIJUA KWAMBA TUTAPOKEA KWA BWANA UJIRA WA URITHI, MAANA TUNAMTUMIKIA BWANA KRISTO; TUNA BIDII NYINGI YA UTUMISHI MBALIMBALI KAMA WA UTOAJI, MAOMBI, KUFADHILIANA, KUKIRIMU, N.K. NA HATULAZIMISHWI KUTENDA LOLOTE MAANA TUNAMTENDEA YESU NA SI MWANADAMU, NA PIA TUNAJUA KUNA UJIRA KWA YALE TUYATENDAYO YOTE.

 

33) MITHALI 8:13 & 16:6b

“ Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu,

Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.”

IMANI:

v  KANISA HILI (…….) TUNAMCHA BWANA MUNGU WETU, NA HIVYO TUNACHUKIA UOVU, KIBURI NA MAJIVUNO, NA NJIA MBOVU, NA KINYWA CHA UKAIDI PIA TUNAKICHUKIA; NA KWA KUMCHA BWANA HUKO TUNAJIEPUSHA NA MAOVU MAISHA YETU YOTE

 

34) MATHAYO 6:19-21

“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI (…….) SIKUZOTE TUNAJIWEKEA HAZINA ZETU MBINGUNI NA WALA SIYO HAPA DUNIANI AMBAPO ZINAWEZA KUHARIBIKA KWA NONDO NA KUTU, NA WEZI WANAWEZA KUVUNJA NA KUIBA; WAKATI HILI HALIWEZEKANI KWETU MBINGUNI; HAZINA ZETU ZIKO MBINGUNI ILIKO NA MIOYO YETU PIA.

 

35) MITHALI 19:17

“Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA;

Naye atamlipa kwa tendo lake jema.”

 

IMANI:

v  KATIKA KANISA HILI MAISHA YETU YOTE, KWA FEDHA NA MALI ZETU ZOTE, TUNAMKOPESHA BWANA MUNGU WETU KWA KUWASAIDIA MASKINI; NAYE ANATULIPA SIKUZOTE KWA MATENDO YETU MEMA

36) 1 NYA  29: 9 & 2 KOR  9:7

 

“Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea BWANA; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu; Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”

IMANI:

v  KANISA HILI (….) WATEULE WANAFURAHIA KUMTOLEA MUNGU KWA HIARI YAO WENYEWE, KWA SABABU  KWA UKAMILIFU WA MIOYO YAO, KWA HIARI YAO WENYEWE, WANAMTOLEA BWANA MUNGU WAO; KILA MMOJA ANATENDA KAMA ALIVYOKUSUDIA MOYONI MWAKE, SI KWA HUZUNI, WALA SI KWA LAZIMA, MAANA WANAJUA KWAMBA MUNGU ANAWAPENDA WALE WANAOMTOLEA KWA MOYO WA UKUNJUFU.

37) MATENDO 2:47b & MATENDO 9: 31

“………Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. 31Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI AMBALO BWANA AMELINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE, ANALIZIDISHA KILA SIKU KWA WALE WANAOOKOLEWA; NALO LINAJENGWA, LINAENDELEA, NA KUONGEZEKA KATIKA KICHO CHA BWANA YESU NA FARAJA YA ROHO MTAKATIFU.

38) MARKO 16:15-18, 20

“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.”

 

IMANI:

v  KANISA HILI LA WATAKATIFU WANAOMWAMINI YESU, WANALITII AGIZO LA YESSU KWA KUENENDA ULIMWENGUNI KOTE AMBAKO WANAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE; NA WATU WANAAMINI , WANABATIZWA, NA KUOKOKA; NA ISHARA HIZI ZINAFUATANA NA HAWA WANAOAMINI; KWA JINA LA YESU WANATOA PEPO; WANASEMA KWA LUGHA MPYA; WANASHIKA NYOKA; HATA WAKINYWA KITU CHA KUFISHA HAKIWADHURU; WANAWEKA MIKONO JUU YA WAGONJWA NAO WANAPATA AFYA; NA KOTEKOTE WANAKOHUBIRI BWANA YESU ANATENDA KAZI PAMOJA NAO, AKILITHIBITISHA LILE NENO KWA ISHARA ZINAZOFUATANA NALO.

39) RUM 15: 19 & EBR 2: 4

“kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu; Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.”

IMANI:

v  KANISA HILI LA KRISTO YESU BWANA WA KANISA TUNAHUBIRI INJILI KWA NGUVU ZA ISHARA NA MAAJABU, KATIKA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, TUNAHUBIRI KOTEKOTE KWA UTIMILIFU; MUNGU NAYE ANASHUHUDIA PAMOJA NASI KWA ISHARA NA AJABU NA NGUVU ZA NAMNA NYINGI, NA KWA MAGAWANYO YA ROHO MTAKATIFU KAMA APENDAVYO MWENYEWE.

40) 1THES 1:4-5 & 1 KOR 2:4

“ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu; Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.”

 

IMANI:

v  KATIKA KANISA HILI LILILONUNULIWA KWA DAMU YA YESU INJILI YETU TUNAYOIHUBIRI  HAIWAFIKII WATU KATIKA MANENO TU, BALI KATIKA ROHO MTAKATIFU, NA UTHIBITIFU MWINGI; NA NENO LETU NA KUHUBIRI KWETU SSI KWA MANENO YA HEKIMA YENYE KUSHAWISHI AKILI ZA WATU, BALI NI KWA DALILI ZA ROHO NA NGUVU; HIVYO IMANI YETU HAIWI KWENYE HEKIMA YA WANADAMU, BALI KATIKA NGUVU ZA MUNGU.

 

MUHIMU:

>>KANISA LA KWANZA NI WEWE (HEKALU LA ROHO MTAKATIFU).

>>HUWEZI KUMUOMBEA MWINGINE ILI MUNGU AMFANYE AWE VILE AMBAVYO WEWE MWENYEWE HAUJAMRUHUSU MUNGU AKUFANYE UWE HIVYO.

>> LAZIMA UMWAMINI MUNGU KWANZA KWA AJILI YAKO MWENYEWE NA KISHA NDIPO UMWAMINI MUNGU KWA AJILI YA MWINGINE/WENGINE.

>> MWAMINI MUNGU KWA AJILI YA MKEO/MUEO, WANAO, WAZAZI WAKO, MCHUNGAJI/WACHUNGAJI WAKO, WAZEE NA MASHEMASI WAKO, VIJANA, WAMAMA, NA WABABA; NA MWILI WA KRISTO KIUJUMLA.

 

Tunaposema UKIRI WA IMANI maana yake;

>>Umeliamini Neno

>>Umelishika Neno

>>Umeomba sawasawa na Neno uliloliamini

>>Umekemea na unakemea bado kila hali iliyo/kitu kilicho/mazingira yaliyo/wazo lililo, na kila fikira iliyo KINYUME NA NENO ULILOLIAMINI NA IMANI ULIYOYANO KWA NENO HILO!

>>Hii ndiyo mamlaka ya mwamini ambayo ina msingi kwenye lile neno “IMEKWISHA” (Yoh 19:30)

>>YESU ALIPOSEMA IMEKWISHA MAANA YAKE HAYA YOTE NA MENGINE KAMA HAYO TULIYOYAITA “IMANI” NDIYO YALE ALIYOYAKAMILISHA YESU MSALABANI, NA NDIYO MAPENZI YA MUNGU

>>PALE MSALABANI NENO LA MUNGU LOTE LILITIMIZWA KWENYE MAISHA YA MWAMINI

>>UTIMILIFU WAKE UNADHIHIRIKA KWENYE MWILI KUPITIA IMANI YA KANISA/WATAKATIFU WATEULE WA MUNGU KATIKA KRISTO YESU

>>UKIAMINI UTAONA MATATIZO YOTE, SHIDA ZOTE, UGUMU WOTE, UPINZANI WOTE, MAGONJWA YOTE, MARADHI YOTE, MIKWAMO YOTE, KUSHINDWA KOTE, UDHAIFU WOTE, UMASKINI WOTE, UBAHILI WOTE, KURUDI NYUMA KOTE, DHAMBI YOTE, GIZA LOTE, KUTOJUA KOTE, KUTOFAHAMU KOTE, KUTOELEWA KOTE, UHITAJI WOTE, UPUNGUFU WOTE, KUISHIWA KOTE, N.K. YAMEKWISHA/UMEKWISHA/ZIMEKWISHA/IMEKWISHA/KUMEKWISHA/IMEKWISHA/LIMEKWISHA/ N.K.

>>UKIWA NA UTUPU WOTE WA MWANZO 1:2 UMEKWISHA

>>UUMBAJI UMEKAMILIKA, LAKINI PIA UNAENDELEA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO MAANA,

 

“Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.” (Yoh 5:17)

>> BABA NA MWANA WAKO KAZINI HATA SASA

>>ROHO NA NENO LAKE WAKO KAZINI HATA SASA

>>UNAPOAMINI NDIPO UNASHIRIKIANA NA BABA NA MWANA

“hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.” (1 Yoh 1:3)

>>UNASHIRIKIANA NA ROHO NA NENO LAKE KUUMBA NENO JIPYA KILA PALIPO UKIWA NA UTUPU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ILI KULETA MABADILIKO KATIKA UTARATIBU WA ULIMWENGU WA ROHO (CREATING NEW ORDER IN THE HEAVENLIES); MABADILIKO AMBAYO YESU ALISHAYAKAMILISHA MSALABANI ALIPOSEMA IMEKWISHA!!!

>>HII NDIYO MAMLAKA YA KIFALME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO INAYOPELEKEA UUMBAJI HUO KUDHIHIRIKA KATIKA DAMU NA NYAMA ULIMWENGUNI

>>HII NDIYO NAMNA YA “KULIFANYA NENO LIFANYIKE MWILI” (HOW TO MAKE THE WORD BECOME FLESH)

 

>>TUMEWEKA MAENEO AROBAINI KAMA MFANO! SASA WEWE INGIA KWENYE NENO UKAONGEZE MAENEO AROBAINI MENGINE, KISHA UANZE “KAZI YA IMANI” ITAKAYOKUPELEKEA KWENYE “SABURI YA TUMAINI LAKO”, NA MWISSHO WAKE MAISHA YAKO YATAJIKITA KATIKA “TAABU YA UPENDO”

 

“3Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.”(1 THES 1:3)

>> LAZIMA UFANYE KAZI YA IMANI

>>LAZIMA UWE NA SABURI KATIKA TUMAINI LAKO

>>LAZIMA UDUMU KATIKA TAABU YA UPENDO

 

“Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.” ( Rum 8: 25)

 

IMANI: >>CHOCHOTE NINACHOKITARAJIAKUTOKA KWA BWANA NISICHOKIONA HUWA NINAKINGOJEA KWA SABURI SIKUZOTE!

“Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. (Yak 1:2-4)

IMANI:

MIMI NINAHESABU YA KUWA NI FURAHA TUPU ( na siyo huzuni tupu, hasira tupu, kukata tamaa kutupu, kuvunjika moyo kutupu, kurudi nyuma kutupu, lawama tupu, n.k.) , NINAPOANGUKIA KATIKA MAJARIBU YA NAMNA MBALIMBALI; MAANA NAJUA YA KUWA KUJARIBIWA KWA IMANI YANGU HULETA SABURI; NA KAZI YA SABURI HII NDANI YANGU NI KUNIFANYA KUWA MKAMILIFU NA MTIMILIFU NISIYEPUNGUKIWA NA KITU CHOCHOTE KIROHO, KIAKILI, KIHISIA, NA KIMWILI!!! (mature and perfect)

 

“ Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.” (Rum 5:1-5)

>>WEKA HAPA IMANI YAKO SASA

>>NA UENDELEE KUFANYA HIVYO KWA MAANDIKO 40 MENGINE! TUMIA HATA MWAKA MZIMA KUJENGA IMANI YAKO, NA KUVIPIGA VITA VYA KIROHO AMBAVYO NI VITA VYA IMANI;

>>KILA VILE ANAVYOTAKA MUNGU UWE NDANI YA KRISTO KUNAPATIKANA KWENYE MAANDIKO KWAKE YEYE AAMINIYE!

>>MUNGU AMEKUPA VYOTE NDANI YA KRISTO YESU AMBAVYO VYOTE VINAPATIKANA KWENYE MAANDIKO KWAKE YEYE AAMINIYE

 

“ Kwa kuwa uweza wake wa Uungu UMETUKIRIMIA VITU VYOTE VIPASAVYO UZIMA NA UTAUWA, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tama” (2 Pet 1:3-4)

 

UBARIKIWE SANA NA BWANA YESU

 

 

 

 

 

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post