MUNGU SIYO MUNGU WA WAFU
Matthew/Mathayo 22:32
[32]I am the God of Abraham, and the God of Isaac, and the God of Jacob? God is not the God of the dead, but of the living.
Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.
>> MUNGU AMESEMA HAPA KWAMBA YEYE SI MUNGU WA WAFU, BALI NI MUNGU WA WALIO HAI
>> MUNGU YUKO HAI KWA AJILI YA WALIO HAI, NA SI KWA AJILI YA WAFU
>> KAMA MUNGU AMEKATAA KUWA MUNGU WA WAFU, UNAWEZAJE KWENDA
KUMWOMBA MUNGU KWA AJILI YA WAFU??!! ATAKUSIKILIZAJE??!! ATAKUBALIJE
IBADA YAKO KWA AJILI YA WAFU??!!
>> WAFU HUWAKILISHA "MAUTI" AMBAYO NI roho ya shetani!! Na ndiyo
maana Yesu alimharibu shetani aliyekuwa na nguvu na mamlaka ya
mauti/kifo KWA NJIA YA MAUTI YAKE!! Kwa kufa kwake mwili alifanya
upatanisho kati ya Mungu na wanadamu kwa kulipa deni la dhambi za
wanadamu!! Maana mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23), lakini Yeye
YESU hakutenda dhambi (1 Petro 2:22), na hivyo KIFO CHAKE KILIKUWA NI
KUPOKEA HUKUMU ADHABU YA DHAMBI ZETU SISI WANADAMU! YAANI, ALIUWAWA
BADALA YETU SISI! ALIUWAWA MAHALI PETU SISI!! GHADHABU YA MUNGU IKAWA
JUU YAKE YEYE ILI ISITUPATE SISI!! ALIUWAWA NA MUNGU AKAMFUFUA KUTOKA
MAUTINI KWA MAANA HAIKUWEZEKANA UCHUNGU WA MAUTI UMSHIKE!! "ambaye
Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana
ashikwe nao." (Matendo ya Mitume 2:24) HAIKUWEZEKANA PIA AUONE UHARIBIFU
WALA NAFSI YAKE IBAKIE KUZIMU!!
Psalms/Zaburi 16:10
"[10]For thou wilt not leave my soul in hell; neither wilt thou suffer thine Holy One to see corruption.
Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu."
NA HAPA TENA;
"Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu."
(Matendo ya Mitume 2:27)
>> MAUTI ILISHINDWA KUMSHIKA!! KIFO KILISHINDWA KUMKAMATA!! KUZIMU
HAKUKUWEZA KUMSHIKA!! KUZIMU NA MAUTI VILISHINDWA KUMSHINDA WALA
KUMSHIKA!! AKAFUFUKA KUTOKA KWA WAFU SIKU YA TATU AKIWA AMEVUNJA NA
KUHARIBU MAMLAKA, UTAWALA, NA NGUVU ZA DHAMBI, KUZIMU, NA MAUTI!!! ANAZO
FUNGUO SASA ZA KUZIMU NA MAUTI!!!
" 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa.
Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa
kwanza na wa mwisho,
(Ufunuo wa Yohana 1:17)
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu."
(Ufunuo wa Yohana 1:18)
>> KULE KUSEMA ANAZO FUNGUO ZA KUZIMU NA MAUTI MAANA YAKE ANAYO MAMLAKA NA NGUVU JUU YA KUZIMU NA MAUTI!!
14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye
naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu
yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, (Waebrania 2:14)
>> KWA NJIA YA MAUTI YAKE YESU ALIMHARIBU SHETANI ALIYEKUWA NA
MAMLAKA NA NGUVU ZA MAUTI, NA ALIYEKUWA AMEWAFUNGA WANADAMU KWENYE
UTUMWA WA HOFU YA MAUTI; AKAWAFUNGUA NA KUWAWEKA HURU!!
15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. (Waebrania 2:15)
>> YESU AMEIHARIBU MAUTI KWA MAUTI YAKE! AMEKIUA KIFO KWA KUFA
KWAKE! ALIPOFUFUKA TUKAPATA USHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MAUTI, NA
TUKAPOKEA MAISHA MAPYA YALE YALE YALIYOMLETA TENA YEYE KUTOKA KWA WAFU!!
>> IBADA ZA WAFU NI IBADA ZA WATENDA DHAMBI WASIOAMINI AMBAO BADO WAKO
KWENYE UTUMWA ULE WA HOFU YA MAUTI!!! WANADHANI KUNA MAWASILIANO YA
KIIBADA KATI YA WALIO HAI NA WALIOKUFA! HAPANA! NA KAMA YAPO HAYATOKI
KWA MUNGU BALI KWA roho za mauti na kuzimu ZA SHETANI!!! Ibada ya wafu
ni kuabudu mauti na kuzimu roho zinazomtawala mtenda dhambi asiyeokoka
bado!! Yesu ameleta uhuru lakini yeye bado ANAKAA MAUTINI!!
24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye
aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita
kutoka mautini kuingia uzimani. (Yohana 5:24)
>> TOKA MAUTINI UINGIE UZIMANI KWA KUMWAMINI YESU!! Kama bado umo
mautini kiroho kwa sababu ya dhambi zako, basi utakuwa na mawazo na
ndoto za mauti, na utapenda IBADA ALIZOZIKATAA MUNGU ZA WAFU MAANA
AMESEMA YEYE SI MUNGU WA WAFU BALI NI MUNGU WA WALIO HAI!! NA WALIO HAI
NI WALE WALIOFUFULIWA PAMOJA NA YESU NA KUPEWA UZIMA WA MILELE ROHONI NA
NAFSINI MWAO NDANI YAKE YESU!!
1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
Waefeso 2:1
2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya
ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule
atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
Waefeso 2:2
3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika
tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa
kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Waefeso 2:3
4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
Waefeso 2:4
5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
Waefeso 2:5
6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
Waefeso 2:6
HAPA KWENYE WARUMI PAULO ANAELEZA VEMA KWAMBA SISI TULIOMWAMINI YESU/TULIOOKOKA, tulisulubiwa pamoja naye, tukafa na kuzikwa pamoja naye, na kisha tukafufuliwa pamoja naye MAANA TULIKUWA KIFUANI (ROHONI) MWAKE, NAYE ALIKUWA AMEKUSUDIA KUTUPA UZIMA WA MILELE TANGU KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU!!
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika
mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya
utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Warumi 6:4
5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
Warumi 6:5
>> HATUHITAJI KWENDA KWA WAFU KWA AJILI YA WALIO HAI!!
32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.
Mathayo 22:32
TENA,
27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.
Marko 12:27
LUKA NAYE ANASEMA;
38 Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.
Luka 20:38
>> MUNGU AMEKATAA KWAMBA YEYE SI MUNGU WA WAFU!! UNAPOWAOMBEA WAFU UNAWAOMBEA KWA MUNGU YUPI??!
>> KAMA MAUTI NA KUZIMU NI roho ZA SHETANI MAANA YAKE UNAMFANYIA
IBADA SHETANI UNAPOWAOMBEA AU KUWAOMBA WAFU!!! SISI TULIOAMINI
TUNAMWABUDU MUNGU ALIYE HAI!! MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO!!
>> YESU HAYUPO MAKABURINI!!! USIENDE MAKABURINI KUMTAFUTA YESU!! AMEFUFUKA!!
1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Luka 24:1
2 Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,
Luka 24:2
3 Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.
Luka 24:3
4 Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;
Luka 24:4
5 nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, KWA NINI MNAMTAFUTA ALIYE HAI KATIKA WAFU?
Luka 24:5
6 Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya,
Luka 24:6
HUWEZI KAMWE KUMPATA MUNGU ALIYE HAI MAKABURINI! HUWEZI KAMWE KUMPATA YESU ALIYE HAI MAKABURINI!! IBADA ZOTE ZA WAFU HAZINA BABA WALA MWANA! ROHO MTAKATIFU HAYUMO KWENYE IBADA HIZO!
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu
aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope,
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
Ufunuo wa Yohana 1:17
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Ufunuo wa Yohana 1:18