KORNELIO ALIKUWA HAJAOKOKA

12,698 Calvary Stock Photos - Free & Royalty-Free Stock Photos from  Dreamstime

 HABARI HII YA KORNELIO NAYO ILISAMBAZWA KUPITIA STATUS ZA WHATSAPP NA HAPA IMEWEKWA KAMA ILIVYOKUWA MWANZO BILA KUFANYIWA MAREKEBISHO

[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Matendo ya Mitume 10:1

>> FUATANA NAMI KATIKA STORY YA KIBIBLIA YA KORNELIO KWENYE KITABU CHA MATENDO YA MITUME SURA YA KUMI UJIFUNZE HAKI YA MUNGU!!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: "2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima."
Matendo ya Mitume 10:2
KORNELIO ALIKUWA NA SIFA NNE ZA KIDINI: ALIKUWA 1) Mtauwa (godly), 2) Mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, 3) Akiwapa watu sadaka nyingi (generous giver), na 4) Akimwomba Mungu daima (mtu wa dua, sala na maombi sikuzote! Sifa hizi nne za Kornelio pengine wewe na nyumba yako yote hamna! Alikuwa ni mtu wa kushika dini kikwelikweli (devout man)!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Ingelikuwa leo hii watu wote wangesema Kornelio ni mtakatifu, anamwamini Yesu, na ameokoka! Lakini hakuwa ameokoka ingawa alikuja kuokoka baadae! Ila alikuwa ni mtu ambaye moyo wake, akili yake, mawazo yake, nguvu zake, maombi yake, mali na fedha zake zote ALIZIWEKA WAKFU KWA MUNGU ili azitumie kutenda mema maisha yake yote! Alimtanguliza, alimheshimu, alimcha, alimtaka, alimtumikia, na alitafuta kumpendeza Mungu katika maisha yake yote! Je! wewe na dini yako, na dhehebu lako leo, umemkaribia Kornelio angalau kwa mbaaaaali hata kiduuuchuu?
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! (Matendo ya Mitume 10:3)
4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
(Matendo ya Mitume 10:4)
5 Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro.
(Matendo ya Mitume 10:5)
>> MUNGU ALIONA MOYO WA KORNELIO AKAMPELEKEA MTUME PETRO
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10:4
>> MUNGU ALIONA MOYO WAKE NA MATENDO YAKE MEMA, AKAYARIDHIA, AKAWEKA KUMBUKUMBU YAKE!
>> MUNGU AKAAMUA KUFANYA KILE ASICHOWEZA KORNELIO WALA MWANADAMU AWAYE YOTE KUKIPATA KWA MATENDO YAKE MEMA NA YA HAKI, AU KWA UCHAJI MUNGU WAKE, AU KWA SADAKA ZAKE NYINGI!!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Matendo ya Mitume 10:5-33 inaeleza habari nzima jinsi malaika alivyomtokea Kornelio, ujumbe aliompa kuhusu sadaka zake na maombi yake kufika kwa Mungu na kuwekwa kumbukumbu; na kwamba atume watu kwa Petro Yafa ili aje kusema naye Maneno ya Uzima: Na jinsi pia Petro alivyoonyeshwa maono kuhusu kupeleka Injili kwa Kornelio, mtu wa mataifa, na watu aliokuwa nao, na jinsi Petro alivyowapokea wajumbe wa Kornelio na kufuatana nao kwenda kwa Kornelio baada ya kupelekwa na Roho Mtakatifu!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Hivi ndivyo Petro alivyoanza kuhubiri habari njema (Injili) za Yesu Kristo;
"34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
(Matendo ya Mitume 10:34)
35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
(Matendo ya Mitume 10:35)
36 Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),"(Matendo ya Mitume 10:36)
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. (Matendo ya Mitume 10:38)
39 Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. (Matendo ya Mitume 10:39)
>> PETRO ANAENDELEA KUHUBIRI NA KUSHUHUDIA HABARI ZA YESU NYUMBANI KWA KORNELIO!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu.
(Matendo ya Mitume 10:42)
43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. (Matendo ya Mitume 10:43)
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
(Matendo ya Mitume 10:44)
>> WAKASIKIA NENO, WAKAAMINI, WAKAOSHWA, NA KUJAZWA ROHO
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, 47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? 48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.
(Matendo ya Mitume 10: 45-48)
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Kornelio na watu wa nyumbani mwake WALISIKIA INJILI YA YESU, WAKAAMINI, WAKAHESABIWA HAKI ILE YA IMANI NA SIYO HAKI YA MATENDO ILE YA KIFARISAYO, WAKAOSHWA DHAMBI ZAO KWA DAMU YA YESU, WAKAWA WAMEOKOLEWA KWA NEEMA YA KRISTO, WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU SAWASAWA NA KUSUDI NA MPANGO WA MUNGU KWENYE AGANO JIPYA! WALIOKOKA!! LICHA YA SIFA ZILE NNE ZA MATENDO 10:2 KORNELIO NA WATU WAKE WALIKUWA HAWAJAIPOKEA NEEMA YA MUNGU!!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: 24 Siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, hali amekusanya jamaa zake na rafiki zake. (Matendo ya Mitume 10:24)
KORNELIO, ALIPOSIKIA HABARI NJEMA, HAKUBISHA NA KUSEMA MIMI NA NYUMBA YANGU YOTE TUNAMCHA MUNGU/ MIMI NAWAPA WATU SADAKA NYINGI/MIMI NAOMBA NA KUSALI SANA/MIMI NAISHI MAISHA YA UTAUWA!! ALIAMINI MOYONI MWAKE AKAHESABIWA HAKI (AKAOKOKA!)
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Warumi 10:10
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Kornelio na watu wa nyumbani mwake walitimiza andiko hili:
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 2:38
1) mioyoni mwao walitubu na kuiamini Injili, 2) wakahesabiwa haki (wakaokoka), 3) wakatangulia kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, 4) kisha wakabatizwa kwa maji mengi ili kuitimiza haki yote (Mt 3:15)
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Hujafikia pengine hata sifa moja kati ya zile nne za Kornelio! Unaingia kwenye jengo fulani kuabudu! Unatoa sadaka na michango hapo! Unawapa watu sadaka pia pengine! Lakini hujafikia wala kukaribia alipofika Kornelio! Hata ungemfikia Kornelio BADO UNGETAKIWA KUOKOKA ILI USIPOTEE NA KUANGAMIA MILELE BAADA YA MAISHA HAYA!! Sasa bado utajivunia dhehebu huku ukimkataa Yesu??!! Utajivunia kutoa na kusaidia watu??! Utajivunia kusali na kuomba??! KORNELIO ALIFANYA HAYO NA KUKUZIDI! Je! Utajivunia kumcha Mungu kwa matendo ya sheria??! KORNELIO ALIFANYA HAYO NA ANAKUZIDI SANA! Utasema unaishi maisha ya utauwa??! KORNELIO NI ZAIDI YAKO!! Hata kama UNAFANANA NA KORNELIO AU UMEMZIDI BADO LAZIMA UOKOKE!
[18:20, 3/10/2023] Jesus Is Lord: Roho Mtakatifu amemuweka Kornelio ili kukutoa wewe kwenye UDANGANYIFU WA KIDINI (RELIGIOUS DECEPTION) na UDANGANYIFU WA KIMADHEHEBU (DENOMINATIONAL DECEPTION!) KORNELIO ASINGEOKOKA ASINGEINGIA MBINGUNI LICHA YA SIFA ZILE NNE ALIZOKUWA NAZO!! WEWE UNA SIFA ZIPI? SIFA ZAKO ZA KIDINI HAZIKUSAIDII KUHESABIWA HAKI MBELE ZA MUNGU!!!
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; (Waefeso 2:8)
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. (Waefeso 2:9)


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post