MAAGIZO NANE KWA MATAJIRI WALIOOKOKA


MAAGIZO KAMA YALIVYOFUNDISHWA KUPITIA WHATSAPP STATUSES

 "17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. (1 Timotheo 6:17)
18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; (1 Tim 6:18)
19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli."
(1 Timotheo 6:19)

MAAGIZO NANE (8) KWA MATAJIRI WALIO NDANI YA YESU! WANAOMWAMINI YESU, YAANI WALIOOKOKA!! (tufuatane)


AGIZO LA KWANZA: 

"17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha."
1 Timotheo 6:17

1) WASIJIVUNE!! roho ya majivuno ni ya shetani! Unapojivuna unakuwa unajilinganisha na wengine, unajikweza, una kiburi, unadhani umejipatia utajiri kwa nguvu zako kinyume na Kweli (Kumb 8:18), unajiinua, unaikana neema ya Mungu iliyokupatia vyote unavyovimiliki KWA NIABA YA YESU na KWA AJILI YA YESU, unakuwa umeukana umiliki wa Yesu wa vyote ulivyonavyo pamoja na wewe mwenyewe (Rum 14:17 & Kol 1:15-16)
>> KUJIVUNA NI KUTOKA KATIKA NEEMA YA MUNGU! " Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.(Habakuki 2:4)
KUJIVUNA NI KUACHA KUMWAMINI NA KUMTUMAINIA MUNGU NA BADALA YAKE KUTUMAINIA NGUVU ZAKO, MALI NA VITU ULIVYONAVYO! YAANI, UMEIACHA IMANI, NA HUNA UNYENYEKEVU MBELE ZA MUNGU! HUWEZI KUMWONA MUNGU USIPOTUBU NA KUREJEA KWA YESU!

AGIZO LA PILI: 

1 Timothy 6:17

"[17]Charge them that are rich in this world, that they be not highminded, nor trust in uncertain riches............"

Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini.........."
2) WASIUTUMAINIE UTAJIRI USIO WA HAKIKA
-Imeandikwa "mbingu na nchi zitapita lakini Neno halitapita!(Mt 24:35) Mungu ni Neno, Yesu ni Neno (Yoh 1:1,14)! Mali haziokoi (Mith11:4,28) KUTUMAINIA MALI NI SAWA NA KUTUMAINIA NYUZI ZA BUIBUI ZIKUSHIKE USIDONDOKE KUTOKA JUU YA DARI (Ayubu 8:14)

AGIZO LA TATU: 

"17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha."  (1 Timotheo 6:17)
3) BALI WAMTUMAINI MUNGU ATUPAYE VITU VYOTE ILI TUVITUMIE KWA FURAHA!
>> Mtumaini Mungu asiyebadilika na asiye na mwisho, aliyeko, aliyekuwako, na atakayekuja! Mali zitapita! (Mith 23:5), ulimwengu unapita (1 Yoh 2:17), lakini Yesu Kristo ni Yeye yule, jana, leo, na hata milele! Weka tumaini kwa Yeye atakayekuwako baada ya mali na utajiri kukoma/kutoweka/kuharibika! Vinginevyo, unakuwa mwabudu sanamu!
>> UKIWEKA TUMAINI LAKO KWA MUNGU UNAUPENDEZA MOYO WAKE! UKIWEKA TUMAINI KWENYE VITU AU WATU HUWEZI KUMPENDEZA MAANA HAUMWAMIMI (EBR 11:6) NA MOYO WAKO UNA miungu migeni AMBAYO NI MACHUKIZO KWAKE! WENGI WANAMWABUDU "mungu pesa" na "mungu mali" NA MAISHA YAO YOTE WANAITUMIKIA miungu YAO HII KWA BIDII ZOTE!! HUWEZI KUMTUMIKIA MUNGU NA MALI (Mt 6:24) " 1 Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. (Zaburi 125:1)
2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. (Zaburi 125:2)


AGIZO LA NNE:

"18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;" (1 Timotheo 6:18)

4) WATENDE MEMA-Mungu alimwambia Ibrahimu "NITAKUBARIKI ILI WEWE NAWE UWE BARAKA KWA WENGINE" (Mwa 12:1-3) Ndani ya Kristo Mungu ametubariki KWA BARAKA ZOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (Efe 1:3) ILI NASI TUWE BARAKA KWA KANISA NA ULIMWENGU KWA NAMNA ZOTE SIKUZOTE! Mungu anakutajirisha NDANI YAKE YESU ILI UWE BARAKA KWA KUTENDA MEMA SIKUZOTE KWA KANISA NA WATU WOTE (Efe 2:10), NA HIVYO KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI (Mt 6:19-21)! LENGO LA KUTAJIRISHWA NI ILI UTENDE MEMA NA SI KULIMBIKIZA UTAJIRI HUO DUNIANI!

AGIZO LA TANO:

"18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;" (1 Timotheo 6:18)

5) WAWE MATAJIRI KWA KUTENDA MEMA-Mungu alikusudia matajiri waliookoka WASIWE TU MATAJIRI WAKAISHIA HAPO! WASINGEKUWA TOFAUTI NA MATAJIRI WATENDA DHAMBI! Bwana ameagiza MATAJIRI WALIOMWAMINI YESU WAWE MATAJIRI KWA KUTENDA MEMA ILI DUNIA IJIFUNZE NA KUUJUA UPENDO WA MUNGU KUPITIA WAO WASIOUTEGEMEA UTAJIRI UNAOHARIBIKA, AMBAO WANAUTUMIA KUJIPATIA UTAJIRI USIOHARIBIKA, WENYE THAWABU, UNAODUMU, ULIOWEKWA TAYARI MBINGUNI NYUMBANI KWAO!

AGIZO LA SITA:

"8 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;" (1 Timotheo 6:18)

6) WAWE TAYARI KUTOA MALI ZAO-Matajiri watenda dhambi ni wachoyo na si watoaji! Utoaji wao Kanisani Yesu aliukataa kwenye Marko 12:41-44! Wanatoa kiduuchu wanabakiza kiiingii kwenye hazina zao wanazozitegemea! Wengine wanatoa kwa masharti, na pia wanatoa ili wafaidike kwa namna mbalimbali! Huu si utoaji! Hawa ni wachoyo, wabahili, wenye tamaa, na waabudu sanamu!
MATAJIRI WALIOOKOKA HUWA NA MIOYO ILIYOJAA UPENDO NA HURUMA YA UTOAJI NA UTAYARI WA KUTOA MARA WANAPOTAKIWA KUFANYA HIVYO AU KILA WANAPOONA UHITAJI! 

>> WAWE TAYARI KUTOA MALI ZAO-Matajiri waliokoka hawasubiri kuombwa ili watoe au kutenda mema! Mioyo yao iliyojaa pendo la Mungu ina huruma kwa maskini na wahitaji! Ni wakarimu na Mungu huwapa macho ya kuona wahitaji na maskini, na masikio ya kusikia vilio vyao! WAO HUJITWIKA NA HUBEBA MAJUKUMU YA KUSAIDIA MAANA HAYO NDIYO MAISHA, HUDUMA, NA UTUMISHI KWAO! Hawajivuni, na hawafanyi kwa kutaka sifa au kuonekana na watu! Wanapotenda mema hawatafuti faida binafsi! Siyo wachoyo wala wanyimivu! WAKO TAYARI KUTOA MALI ZAO!!

AGIZO LA SABA:

"18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;" (1 Timotheo 6:18)

7) WASHIRIKIANE NA WENGINE KWA MOYO-Kuna watenda dhambi wanapojiona wamepata mali hujikweza, hujiinua, na kujiona wao ni bora kuliko wanadamu wengine WASIOKUWA NA VILE WALIVYONAVYO WAO! Wao hujipa daraja la juu kuliko "maskini" WAOVU HAWA MPAKA MAKANISANI WAPO! Wana wa jehanamu kama hawa HAWAPENDI WALA HAWATAKI KUCHANGAMANA, KUSHIRIKIANA, WALA KUWASILIANA NA WALE "binadamu duni wa hali ya chini!!" Wasipotubu na kubadilika wajiandae kwa moto usiozimika milele!
>> WASHIRIKIANE NA WENGINE KWA MOYO!!-Kwa Yesu hakuna aliye bora kuliko mwingine! WOTE WAMENUNULIWA KWA DAMU YA THAMANI YA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU! Mungu ANAWAPENDA WOTE SAWA, ANAWATHAMINI WOTE SAWA, ANAWAJALI WOTE SAWA! ANA MIPANGO BORA YA MEMA KWA WOTE SAWA! ANATOA YAKE KWA WOTE SAWA ILI WAYAFANYE MAPENZI YAKE! HANA UPENDELEO KWA YEYOTE BALI KILA MMOJA ANA NAFASI SAWA YA KUFANIKIWA, NA KUTIMIZA MAKUSUDI YAKE KWA KADIRI ANAVYOAMINI NA KULITII NENO LAKE! MUNGU HAHITAJI ELIMU, CHEO, RANGI, SURA, AU KABILA BALI MOYO ULIOPONDEKA, ULIOTUBU, NA KUNYENYEKEA KWAKE!!

AGIZO LA NANE:

"19huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli." (1 Timotheo 6:19)
8) HUKU WAKIJIWEKEA AKIBA IWE MSINGI MZURI KWA WAKATI UJAO-Waliookoka, na matajiri waliookoka WANATAKIWA KUISHI MAISHA YA KUJIWEKEA AKIBA MBINGUNI KWA AJILI YA MAISHA YA MILELE KATIKA UFALME WA MBINGUNI! Kutenda mema ndani ya Yesu ni kujiwekea akiba mbinguni! Kusaidia maskini na wahitaji ni kuweka hazina mbinguni! Kutoa sana na kutawanya ni kujiwekea hazina mbinguni! Kumtumikia Mungu kwa fedha na mali zako ni kujiwekea hazina mbinguni! FEDHA, MALI, NA UTAJIRI NI KWA KUSUDI LA KUTENDEA MEMA KATIKA UFALME WA MUNGU, NA KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI!
>> HII NDIYO MAANA YESU ALISEMA NI VIGUMU KABISA KWA TAJIRI KUINGIA KWENYE UFALME WA MUNGU
23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! (Marko 10:23)
24 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! (Marko 10:24)
25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. (Marko 10:25)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post