AGANO LA URITHI WA KIROHO KWENYE UZAZI

 


AGANO LA URITHI WA KIROHO KWENYE UZAZI

Hili ni Agano la Mungu na wanandoa wote kwenye ndoa takatifu na ndoa za anguko! Ni agano ambalo ni sheria pia ya urithi wa kiroho inayotawala UZAZI WOTE TULIOUONGELEA MPAKA SASA!
1) UZAAJI MATUNDA YA HAKI, MATUNDA YA NURU, NA TUNDA LA ROHO (Flp 1:11, Ebr 12:11, Efe 5:9, Gal 5:22-23)
2) UZAZI KWA NJIA YA INJILI (1 Kor 4:15, )
3) UZAZI WA KIMWILI (Yohana 9:2, Luka 21:16, Waefeso 6:2)
4) KUMZALIA MUNGU MATUNDA
(Yohana 15:4-5, 8 & Marko 4:8)
>> KUMBUKA TULIONA MUNGU ALIIBARIKI NDOA TAKATIFU KWA BARAKA TANO, NA MOJA YA BARAKA HIZO NI BARAKA YA UZAZI!!!
Genesis 1:28
[28]And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every living thing that moveth upon the earth.
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

>> NDOA TAKATIFU INA BARAKA YA UZAZI NA WATOTO WANAOZALIWA HUMO "NI WATAKATIFU!" KWA MUJIBU WA MAANDIKO!
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; KAMA ISINGEKUWA HIVYO, WATOTO WENU WANGEKUWA SI SAFI; BALI SASA NI WATAKATIFU.
(1 Wakorintho 7:14)
>> WANAZALIWA NEEMA YA WOKOVU YA WAZAZI IKIWA JUU YAO TAYARI, HIVYO LAZIMA WATAOKOKA!! Biblia ina ahadi:

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
Matendo ya Mitume 16:30

31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Matendo ya Mitume 16:31

>> AHADI HII INATOA UHAKIKA WA WEWE KUOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO YOTE!
>>Kama wewe ni mtoto na wazazi wako na nduguzo hawajaokoka, UKIMWAMINI YESU, UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO!!
>> Kama wewe ni mmoja wa wanandoa ama mke au mume, UKIMWAMINI YESU, MKEO/MUMEO ATAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO YOTE!! Huu ni uhakika wa kuokoka mkeo, mumeo, wanao, ndugu zako, na jamaa zako, pamoja na ndugu na jamaa wa mumeo/mkeo pia!! Hii ndiyo "nyumba yako"! Inatakiwa wanaowaongoza sala ya toba watu "waongeze neno hili: NINAKUPOKEA BWANA YESU, INGIA MOYONI MWANGU SASA, NISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, MIMI NA NYUMBA YANGU YOTE, NINAKUPOKEA SASA, UWE BWANA NA MWOKOZI WANGU, PAMOJA NA NYUMBA YANGU!!" Yaani, hauokoki peke yako, bali unaokoka wewe na nyumba yako yote!! Kwa sababu andiko linasema:
1) mwamini Bwana Yesu!-wewe tayari umemwamini, siyo?
2) nawe utaokoka!-wewe si umeokoka, siyo?
3) pamoja na nyumba yako!! Yaani, UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO!! Je! unaamini wanao/kaka/dada/nduguzo/mkeo/mumeo WAMEOKOKA PAMOJA NAWE ingawa bado wanaonekana kimwili wakitenda dhambi? Uko tayari kusimama na neno mpaka litimie kwao wote mmoja mmoja??!! Uko tayari kusema asante Yesu kwa kuniokoa mimi pamoja na nyumba yangu huku kimwili wanaendelea na dhambi??!! Uko tayari kuamini kwa ajili yao??!! Uko tayari kukataa kuhukumu kwa kufuata unayoyaona na unayoyasikia kama maandiko yanenavyo?!!

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;
Isaya 11:2

3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;
Isaya 11:3

>> UKO TAYARI KUONA YASIYOONEKANA KWA KUTUMIA MACHO YALE SABA YA ROHO??!!
>> UKO TAYARI KUYATAJA YASIYOKUWAKO KANA KWAMBA YAMEKUWAKO KAMA ALIVYOFANYA IBRAHIMU BABA YETU WA IMANI?!

16 Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote;
Warumi 4:16

17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.
Warumi 4:17

18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Warumi 4:18

19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
Warumi 4:19

20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
Warumi 4:20

21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
Warumi 4:21

22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.
Warumi 4:22

23 Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake;
Warumi 4:23

24 bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;
Warumi 4:24

25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.
Warumi 4:25

>> Hayo yanayosumbua ndoa na familia yako, Bwana Yesu ameyatatua hivyo!! Lakini lazima uokoke, na kisha uishi na kuenenda kwa imani ya Yesu!! Kwa mujibu wa Waebrania 11:1 IMANI NI KUISHI NA KUENENDA UKIWA NA UHAKIKA WA YALE UNAYOYATARAJIA KUTOKA KWA BWANA, NA PIA NI USHAHIDI MOYONI (ROHONI) MWAKO WA KUYAMILIKI TAYARI YALE YASIYOONEKANA/YASIYOKUWEPO BADO! Unapoishi kwa imani ya Yesu UNA UHAKIKA KWAMBA wapendwa wako wanaoonekana walevi, makahaba, wezi, wavuta bangi, mashoga, mateja wa dawa za kulevya, waganga wa kienyeji, wasioamini, n.k. WAMEOKOKA!! UHAKIKA KWAMBA WATABADILIKA!! UHAKIKA KWAMBA HAWATAANGAMIA DHAMBINI!! UHAKIKA KWAMBA HAYO WANAYOYAFANYA WATAYAACHA NA KUMGEUKIA MUNGU KWA KUOKOKA!! Imani inakupa matumaini imara yanayokuvusha katika giza lolote nene la malezi, ndoa, ajira, masomo, n.k. 

18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
2 Wakorintho 4:18

>> USIANGALIE TAIFA LINALOYUMBA, UCHUMI UNAOZOROTA,
MAADILI YANAYOMOMONYOKA KWENYE TAIFA, KANISA LINALOPOA NA KURUDI NYUMA, MAASI YANAYOONGEZEKA, N.K. WEWE ITAZAME AHADI YA MUNGU NA NENO LAKE!!!
19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
(Warumi 4:19)

20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; (Warumi 4:20)

21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. (Warumi 4:21)

22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki. (Warumi 4:22)
>> TATIZO UNALO WEWE!! HUAMINI! HUMWAMINI YESU!! HUAMINI NENO LAKE!! Ndiyo maana unachanganyikiwa na mambo yanayojiri, umejaa hofu, unaona mambo yanaharibika kila upande, n.k. HABARI NJEMA NI KWAMBA UAMSHO WA AJABU KWENYE NDOA, KANISA (MWILI WAKE KRISTO), NA TAIFA UKO MLANGONI UNAKUJA!! TAIFA LINAPEWA NEEMA NA REHEMA ZA AJABU! UTUKUFU WA MUNGU UNASHUKA KWENYE TAIFA HILI KWA NAMNA AMBAYO HAIJAWAHI KUONEKANA POPOTE!! NURU KUU KUTOKA KWENYE UTUKUFU MKUU INAANGAZA KATIKA TAIFA LETU!! TAIFA LINAOSHWA KWA DAMU YA YESU!! TAIFA LINAJAZWA ROHO MTAKATIFU!!! Unaamini hayo?

9 lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
1 Wakorintho 2:9

10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
1 Wakorintho 2:10
 

BWANA WETU YESU AMELETA SULUHISHO LA KILA TATIZO!! AMELETA JIBU LA KILA SWALI!! MWAMINI YESU!! Ukiamini Roho Mtakatifu atakuonyesha majibu kwenye Neno lake!! Sasa Isaya anatuonyesha Agano la Urithi wa Kiroho ambalo ni sheria pia ya urithi wa kiroho KWA WAZAZI WOTE WANAOZAA KATIKA MAENEO TULIYOYAAINISHA HUKO JUU!! Biblia inasema,

Isaiah 59:21
[21]As for me, this is my covenant with them, saith the LORD; My spirit that is upon thee, and my words which I have put in thy mouth, shall not depart out of thy mouth, nor out of the mouth of thy seed, nor out of the mouth of thy seed's seed, saith the LORD, from henceforth and for ever.
Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.

 
>> HILI NI AGANO, SHERIA, NA KANUNI, KWA WANANDOA NA WAZAZI WOTE WA VIZAZI VYOTE!!
1) ROHO YA MUNGU ILIYO JUU YAKO- yaani lazima uwe umejazwa Roho Mtakatifu baada ya kumwamini Yesu (kuokoka!)
>> Kama haujaokoka lazima una roho nyingine ambayo si ya Mungu!! Nayo hiyo roho pia itatenda kazi kwa sheria hii hii isipokuwa ni kwa namna hasi iliyo kinyume na Kweli!!

Imeandikwa;
15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Yohana 14:15

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Yohana 14:16

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, MAANA ANAKAA KWENI, NAYE ATAKUWA NDANI YENU.
Yohana 14:17

>> WATAKATIFU WANA ROHO ATOKAYE KWA MUNGU AKAAYE NDANI YAO!! YEYE NDIYE ANAYEWASAIDIA KUITII KWELI NA KUYAFANYA MAPENZI YOTE YA MUNGU!!
2) NA MANENO YANGU NILIYOYATIA KINYWANI MWAKO!!! Roho wa Mungu akiwa ndani yako Yeye SIKUZOTE HUYANENA MANENO YA MUNGU!!
2 Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu.
2 Samweli 23:2
>> ROHO MTAKATIFU HUNENA NENO LA MUNGU! ROHO HUYU AKIWA NDANI YAKO HULIWEKA NENO LAKE KINYWANI MWAKO (ULIMINI MWAKO)
>> ROHO MTAKATIFU HUMNENA YESU KRISTO!! YEYE HUNENA NENO LA KRISTO!!
>> HIVYO MUNGU AMEAHIDI/AMEFANYA AGANO LAKE MILELE LA KUKUPA WEWE UNAYEMWAMINI YESU ROHO NA NENO LAKE!!
3) "hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele."
>> KWA WEWE ULIYEMPOKEA HUYU ROHO, NA UNAMTII NA KUMFUATA, ROHO HUYO NA NENO LAKE HATAONDOKA KWAKO WEWE (MOYONI NA KINYWANI MWAKO), WALA MIOYONI NA VINYWANI MWA WANAO, WALA MWA WAJUKUU WAKO TANGU UMEAMINI HATA MILELE!
>> ROHO MTAKATIFU NI ROHO WA AGANO JIPYA UNAPOOKOKA! Ni Roho anayekuwezesha KUZAA VITAKATIFU KWA NGUVU ZAKE!! Roho huyu atakaa ndani yako, ndani ya wanao, na ndani ya wajukuu wako pamoja na maneno yake ya uzima AMA WAKIWA NI WATOTO WA KIROHO KWA KWA NJIA YA INJILI AU WATOTO WA KIMWILI!! Petro alinena Neno hili kwa Roho Mtakatifu!!

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 2:38

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Matendo ya Mitume 2:39

Ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu!! Na watu wote watakaookoka!! Agano hili ni kwa ndoa yoyote itakayookoka!! Ndoa ya Anguko yaweza kuokoka na kujazwa Roho Mtakatifu!! Agano hili linamrithisha mwanao, na mjukuu wako Roho Mtakatifu na Maneno yake ya uzima!! Ukiamini ahadi hii! Ukilishika Agano hili! Ukiielewa sheria hii, na ukiwa unaenenda kwa Roho (Gal 5:16), HUWEZI TENA KUHANGAIKA/KUSUMBUKA/KUFADHAIKA/KUOGOPA/KUCHANGANYIKIWA NA LOLOTE KUHUSIANA NA "TABIA ZA SASA ZA WANAO" AU "HALI YA SASA YA KUHARIBIKA NA KUHARIBIWA KWA WATOTO" KWA KUWA UNA UHAKIKA KWAMBA MWANAO HATOKUWA MIONGONI MWAO WANAOONEWA NA SHETANI, KWA KUWA NI MTOTO ALIYE CHINI YA AGANO LILILOFANYWA IMARA KWA DAMU YA YESU!! YESUUU! (KWA NDOA IMARAAA!) YESUUUU! (KWA NDOA TAKATIFUUUU!) YESUUUU! (KWA WATOTO WATAKATIFUUU!) YESUUUU! (KWA WAJUKUU WATAKATIFUUUU!) YESUUUU! (KWA KANISA TAKATIFUUUU!)
Asante Yesu kwa Agano la Urithi wa Kiroho katika Roho Mtakatifu!! Agano la Kiroho!! Kama hauna huyu Roho wanao na wajukuu watarithi roho ya shetani ya dhambi uliyonayo, na maneno maovu kama uongo/majivuno/matusi/kujisifu/hila/jeuri/kiburi/ukaidi/ubishi/dharau/usengenyaji/uzushi/n.k.
>>MWAMINI YESU NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO!!
>> MWAMINI YESU NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NDOA YAKO!!
Ubarikiwe na Bwana Yesu! Tukijaliwa neema na kibali tutaendelea!!



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post