BARAKA ZA NDOA TAKATIFU
Biblia inasema, " 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1:27
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni,
mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
Mwanzo 1:28
>> Baada ya kuumba ndoa takatifu MUNGU ALIWABARIKIA ( BLESSED
THEM)!! WANANDOA HAWA WALIKUWA TAYARI WAMEUMBWA KWA SURA NA MFANO WA
MUNGU!! NDIPO WAKABARIKIWA!! Leo hii baraka ya ndoa takatifu kama
tutakavyoitazama imekuwa adimu kwa sababu WANANDOA HAWAFANANI NA MUNGU!!
YAANI, HAWAFANANI NA NENO!! (KWA KUWA MUNGU NI NENO-YOHANA 1:1),
HAWAFANANI NA YESU!! ( MAANA YESU NI NENO ALIYEKUJA KWENYE MWILI, AKAFA
KWA AJILI YA DHAMBI ZETU, AKAFANYA UPATANISHO, AKAFUFUKA ILI TUHESABIWE
HAKI NA KUENENDA KATIKA MAISHA MAPYA NDANI YAKE YEYE ALIYE HAI MILELE!!)
>> KUFANANA NA YESU NI KUISHI NA KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE
ALIVYOENENDA!! "6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa
kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda."
(1 Yohana 2:6)
>> Yaani, kuenenda katika haki, utakatifu, nguvu za Mungu, upendo, unyenyekevu, utii, kicho, hekima, maarifa, ufahamu, mafunuo na maono ya
Baba yetu wa mbinguni, uweza na mamlaka, malengo, nia, na makusudi yake, utukufu wake, NA YOTE MENGI SANA MENGINEYO!! Haya ndiyo maisha ya Yesu
ambayo ni maisha yako UKIOKOKA, UKAJAZWA ROHO MTAKATIFU, UKAWA
UNAONGOZWA NA ROHO HUYO!! (Warumi 8:14) Maana YESU ANAINGIA MOYONI MWAKO
NA WEWE UNAKAA NDANI YAKE!! (2 KOR 5:17)!!
>> Maandiko yanasema, "63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo
niliyowaambia ni roho, tena ni uzima." (Yohana 6:63) KUFANANA NA YESU
MAANA YAKE MANENO YAKE NI UZIMA, NA ROHO NDANI YAKO, KWA KUWA
UMEYAAMINI NA YAKAKUBADILISHA KIROHO NA KUKUPA UZIMA AU MAISHA YAKE ROHONI MWAKO; MAANA UMEUNGANIKA NAYO KATIKA ROHO, NA SASA
WEWE NI ROHO MOJA NA BWANA YESU KAMA ILIVYOANDIKWA, "17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana
ni roho moja naye." (1 Wakorintho 6:17) KUHUSU KUFANANA HUKU NA YESU TUTALITAZAMA HILI KWENYE SOMO LINGINE.
>> BARAKA YA MUNGU YOYOTE SIKUZOTE LAZIMA IJE KUPITIA NENO!!
MUNGU ANAKUBARIKI KWA NENO LAKE, NA UKIPOKEA ILE BARAKA KWA IMANI, UNAKUWA
UMEPOKEA ROHO YA BARAKA!! Baraka haiwi baraka kabla haijawa roho kwanza!
Kwa sababu Neno la Mungu ni roho, na pia ni uzima! (Yohana 6:63) Mungu
ni Roho! ( Yohana 4:24) Hivyo uhusiano na mawasiliano ya mwanadamu na Mungu yote lazima
yawe ni kupitia roho yako!! Yaani, roho yako kwa Roho wake, ( unaposema
naye), na Roho wake kwa roho yako!! (anaposema nawe!) Huwezi kusema naye
kama ni wewe ni mtenda dhambi maana roho yako imekufa/haina uzima/haina uhai, na Mungu huwa hawasikii watenda dhambi! (Ezekiel 18:20, Isaya 59:1-2) Ni roho yako inayobarikiwa kwanza kwa
kupokea, au kujazwa, au kunenepeshwa, au kuunganishwa, na ile roho ya
Neno/Andiko la Baraka ulilolisoma au kulisikia, ukaliamini na kulipokea
moyoni (rohoni) mwako! Kisha baada ya kujaribiwa/kupimwa kwa majaribu ya
namna mbalimbali na kushinda, pamoja na kuvumilia kwingi, ndiposa LILE
NENO HUFANYIKA MWILI, YAANI, HUDHIHIRIKA KWENYE MWILI (MANIFESTATION
STAGE)!
"28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni,
mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
Mwanzo 1:28
>> Tukirudi mwanzo tunaona Mungu ALIWABARIKIA Adamu na Hawa
WALIOKUWA WAMEUMBWA KWA SURA NA MFANO WAKE!! Na Neno hili la Baraka lilikuwa na maeneo matano ya baraka
za ndoa takatifu ambazo Mungu alikusudia ziwe ni baraka za kila
mwanadamu, kila ndoa za wanadamu, na kila familia ulimwenguni ya
WATAKATIFU WANAOFANANA NAYE!! Mungu alichoumba hapa kwa utakatifu wake
ni MWANADAMU ASIYE NA DHAMBI, NA ASIYETENDA DHAMBI, KWENYE NDOA
TAKATIFU!! Shetani "nyoka" aliyemdanganya mwanamke pale bustanini ndiye
ALIYEUDANGANYA ULIMWENGU WOTE NA KUIBUA "DINI ZA, NA MADHEHEBU YA,
WATENDA DHAMBI, WANAOMWABUDU YEYE KWA MAJINA MBALIMBALI WAKIMWITA
"mungu" ingawa SI MUNGU MTAKATIFU ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI NA VYOTE
VIIJAZAVYO!! Huwezi kumwabudu Mungu Mtakatifu PASIPO KUWA MTAKATIFU!!
"Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;"
(1 Mambo ya Nyakati 16:29)
"Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu."
(Zaburi 29:2)
Psalms 96:9
[9]O worship the LORD in the beauty of holiness: fear before him, all the earth.
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
>> UZURI/UREMBO WA UTAKATIFU UMO NDANI YA YESU, NA NDIYO KAZI
AIFANYAYO ROHO MTAKATIFU YA KUMPAMBA BIBI HARUSI, MKE WA MWANA-KONDOO,
KWA AJILI YA HARUSI YAKE KATIKA UFALME WA MUNGU KWA NJIA YA UTAKASO!
(UFUNUO 19:7-9 & 22: 11, 14 &17)
MAENEO MATANO YA BARAKA YA NDOA TAKATIFU NI HAYA:
Genesis 1:28
[28]And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and
multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over
the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every
living thing that moveth upon the earth.
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi,
na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila
kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
1) BARAKA YA UZAZI ( BLESSING OF FRUITFULNESS)
Hii ni "roho ya uzazi"moyoni kwanza (rohoni) kabla haijaleta matokeo
yanayoonekana kwa macho ya damu na nyama!! Kuhusu "roho" yenyewe huwa
inafanya lile tendo lake wakati wote pasipo kupumzika!! Katika ulimwengu
wa roho hamna roho inayolala au kupumzika! Hivyo roho hii huwa inazaa
muda wote hata kama kwenye mwili hamna uzazi unaoonekana au kuendelea
kwa macho ya damu na nyama!! Ndiyo maana anayeamini anaweza kiusahihi
kusema ANAMZALIA MUNGU MATUNDA HATA KAMA HAMNA MATUNDA YANAYOONEKANA
KABISA ILI MRADI AMEAMINI NENO LA BARAKA YA UZAZI!!
>> Zaeni ( be fruitful!) Uzazi huu ni wa maeneo matatu! 1) Uzazi
wa kiroho-kuzaa watoto kwa njia ya Injili ya Yesu, 2) Uzazi wa watoto
kimwili, na 3) Uzaaji Matunda ndani ya Yesu kwa Aliyeokoka!
"15 Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa
mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa
kuvumilia." (Luka 8:15)
"20 Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao
lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja
sitini, na mmoja mia."
(Marko 4:20)
>> HII NI BARAKA YA UZAZI KWA WATAKATIFU WANAOMTII KRISTO YESU
BWANA WAO KWA KULITENDA NENO MAISHANI MWAO!! USIPOLITENDA NENO HUWEZI
KUZAA!!
>> Uzaaji huu ni muhimu sana kwenye mahusiano yote, na zaidi sana
kwenye ndoa!! Ndoa za anguko zinaizalia mauti matunda!! Ndoa takatifu
zinamzalia Mungu matunda!!
2) BARAKA YA ONGEZEKO KIIDADI (BLESSING OF MULTIPLICATION)
>> Hii ni baraka ambayo ni "roho ya ongezeko kwanza kiidadi" kabla idadi hiyo haijaongezeka kwa macho!!
>> Hili ni ongezeko la kiroho na kimwili! Ni baraka ya idadi ya
watu kuongezeka! Watoto kuongezeka kwenye familia na watu kuongezeka
katika taifa!! Baraka hii inaondoa utasa wote!! Ndoa takatifu huwa
inazaa na haina utasa! Yesu aliondoa na kukomesha utasa! Neno la Mungu
limekomesha utasa!
"9 Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha."
Zaburi 113:9
"1 Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa
kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake
aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana. "
(Isaya 54:1)
>> tasa anapoimba na kumshukuru Mungu kwa kumpa watoto wengi wa
kike na kiume ANAKUWA ANAZAA KATIKA ROHO INGAWA KATIKA MWILI ANAITWA
TASA! MWISHOWE HUJA KUZAA KIMWILI MAANA UTASA ULISHAONDOLEWA KATIKA ROHO
TANGU ALIPOAMINI!! HAKUNA TASA KWENYE NDOA TAKATIFU!!
>> Lakini pia hii ni baraka ya ongezeko kiidadi ya Kanisa la
Kristo!! Biblia imetuonyesha baraka hii ilivyodhihirika kwenye mwili:
47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Matendo ya Mitume 2:47
>> BWANA AKALIZIDISHA KANISA KILA SIKU KWA WALE WALIOKUWA
WAKIOKOLEWA!! Kanisa la Kristo linaongezeka kila siku kwa wale
wanaookolewa! Hii inaendelea pasipo kujali unaliona hilo kwa macho au
la!! Ili uone baraka hii lazima uamini kwamba BWANA ANALIZIDISHA KANISA
KILA SIKU KWA WALE WANAOOKOLEWA! Hii ni kweli na roho hii ya wokovu
inaokoa kila siku!! Sasa mtumishi aliyebarikiwa na mwenye huduma
iliyobarikiwa ANAJUA NA ANALIFAHAMU HILI: KWAMBA KANISA LINAONGEZEKA
KILA SIKU HATA KAMA IDADI INAONEKANA KUBAKI ILE ILE KWA MUDA MREFU!!
Hivi ndiyo namna ya kushinda na kuzaa!!
3) BARAKA YA KUIJAZA NCHI/ KUENEA ( BLESSING OF REPLENISHING THE EARTH)
>> Hii ni baraka ya kuenea pande zote, kaskazini, kusini,
mashariki, na magharibi! Kulia, kushoto, mbele, nyuma!! "2 Panua mahali
pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze;
ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.
Isaya 54:2
3 Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto;
na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa
kukaliwa na watu."
Isaya 54:3
>> Kwa upande wa Kanisa nalo tuliona hili: "6 na walipowakosa,
wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga
kelele, wakisema, WATU HAWA WALIOUPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA HUKU NAKO"
Matendo ya Mitume 17:6
>> WALISHANGAZWA NA AKINA PAULO KUFIKA "KULE NAKO!!"
>> HAKUNA MAHALI INJILI YA UFALME WA MUNGU HAITAFIKA!! NI BARAKA
YA KUIJAZA NCHI!! Bwana wetu Yesu aliagiza: "15 Akawaambia, Enendeni
ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe."
Marko 16:15
>> NI BARAKA INAYOTUFIKISHA FAMILIA YA KANISA (MWILI WA KRISTO)
ULIMWENGUNI KOTE! Baraka hii ni BARAKA YA NDOA TAKATIFU!! Ndipo tunasema
ndoa takatifu hupelekea kanisa takatifu !! Na pia taifa takatifu!!
4) BARAKA YA KUITIISHA NCHI (BLESSING OF SUBDUING)
>> Hii ni baraka ya udhibiti wa nchi na vyote vilivyomo! Ni baraka
inayofanya nchi itawalike na uumbaji wote wa Mungu uwe chini ya mamlaka
na udhibiti wa mwanadamu aliyebarikiwa kwenye ndoa takatifu!!
Katika hili Mungu amefunua maarifa mbalimbali kwa wanadamu ya asili na
pia yale yanayofundishwa katika ngazi mbalimbali za "elimu rasmi!!"
mashuleni na vyuoni pamoja na elimu isiyo rasmi pia!! Hii ndiyo maana
mwanadamu anaweza hata kufuga simba, mamba, nyoka, ndege, na wanyama
wote warukao na kutambaa!!
>> Lakini pia kanisa la Kristo limepewa mamlaka ya kumiliki na
kutawala kwa Neno na Roho Mtakatifu kupitia imani ya Yesu!! Maji, upepo,
miti, wanyama, ndege wa angani, na uumbaji wote unatii mamlaka ya
WATAKATIFU WANA WA MUNGU kwa JINA LA YESU!
5) BARAKA YA UTAWALA (BLESSING OF DOMINION)
>> Mkatawale ndege wa angani, samaki wa baharini, na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho juu ya nchi!! Adamu na mkewe walibarikiwa kutawala
uumbaji wote kupitia ndoa yao takatifu! Walipoasi wakapoteza utawala
kwa shetani! Lakini Mungu ashukuriwe aliyeturejeshea utawala katika
ulimwengu wa roho kupitia Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu!! Watakatifu
tuna Jina la Yesu! Ndoa takatifu zina Jina la Yesu! Kama wewe siyo
mtakatifu huna kibali wala uhalali wa kulitumia Jina la Yesu! Tubu
uiamini Injili!!
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Marko 1:15
30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.
Matendo ya Mitume 17:30
31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa
haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa
mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Matendo ya Mitume 17:31
>> JINA LA YESU NI JINA LIPITALO MAJINA YOTE!! LINA MAMLAKA NA NGUVU ZOTE ZA MUNGU!!
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
Wafilipi 2:5
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
Wafilipi 2:6
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Wafilipi 2:7
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Wafilipi 2:8
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Wafilipi 2:9
10 ILI KWA JINA LA YESU KILA GOTI LIPIGWE, LA VITU VYA MBINGUNI, NA VYA DUNIANI, NA VYA CHINI YA NCHI;
Wafilipi 2:10
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Wafilipi 2:11
>> Kwa Jina la Yesu tunatawala! Kwa Jina la Yesu
tunamiliki! Kwenye ndoa takatifu tunamiliki! Kwenye ndoa takatifu
tunatawala! KWA JINA LA YESU!!
Lile Neno Mungu akawabarikia
linaonyesha KUBARIKIWA KWA PAMOJA KWA MUME NA MKEWE! MUME NA MKE
WAMERITHISHWA BARAKA KWA PAMOJA!! HAKUBARIKIWA MUME PEKE YAKE NA MKE
PEKE YAKE!! WALIBARIKIWA KAMA MKE NA MUME ILI WARITHI BARAKA ZOTE KWA
PAMOJA! Hakuna baraka ya mke peke yake pasipo mumewe au mume peke yake
pasipo mkewe! Mume au mke hutenda kazi zote kila mmoja:
1) KWA AJILI YA MWENZI WAKE, NA
2) KWA NIABA YA MWENZI WAKE
3) NA WOTE NI KWA AJILI YA YESU!!
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa
ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka
kwa ajili yao.
2 Wakorintho 5:15
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
Wakolosai 3:23
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Wakolosai 3:24
>> BIASHARA/ KAZI/AJIRA YAKO MUME AU MKE NI 1) KWA
AJILI YA YESU, 2) KWA AJILI YA MKEO/MUMEO, NA 3) KWA NIABA YA MWENZI
WAKO!!
>> NDOA TAKATIFU NI MWILI MMOJA! Mwanamke ni ubavu uliotwaliwa
kutoka kwa mwanamume! MNAWEZAJE KUUTENGANISHA HUU MWILI??!! Kama hamuwezi
basi mjue HAMNA ANAYEMILIKI PESA, NYUMBA, GARI, SHAMBA, N.K. PASIPO
MWENZAKE!! VYOTE NI VYENU, NA NYIE WOTE NI WA YESU!! Shetani ndiye
amedanganya ndoa za anguko ili huyu aseme hiki changu, huyu hii yangu,
n.k. UBINAFSI, UCHOYO, UMIMI, TAMAA, MAGOMVI, MALALAMIKO, KUNYANYASANA,
KUDANGANYANA, KUFICHANA, N.K. VIKAINGIA KWENYE NDOA KWA KUTOTAMBUA
KWAMBA MUNGU HAKUMBARIKIA MUME AU MKE PEKE YAKE BALI ALIWABARIKIA!!
(GOD BLESSED THEM!!)
John (Yohana)16:13-14
[13]Howbeit when he, the Spirit of truth, is come, he will guide you
into all truth: for he shall not speak of himself; but whatsoever he
shall hear, that shall he speak: and he will shew you things to come.
LAKINI YEYE atakapokuja, HUYO ROHO WA KWELI, atawaongoza awatie kwenye
kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote
atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
[14]HE SHALL GLORIFY ME: for he shall receive of mine, and shall shew it unto you.
YEYE ATANITUKUZA MIMI, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
>> INJILI INAMTUKUZA NA KUMWINUA YESU, AMBAYE NI SULUHISHO LA MATATIZO YOTE!!
>> ROHO MTAKATIFU ANAMTUKUZA YESU, AMBAYE NI JIBU LA MASWALI YOTE!
>> JIBU LA MATATIZO YOTE KATIKA TAIFA HILI NI UAMSHO, NA UAMSHO UTAKAOANZIA KWENYE NDOA
NDOA TAKATIFU VS NDOA YA ANGUKO
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:24
>> WANANDOA KAMA WAKIAMBATANA KWENYE NDOA TAKATIFU, LAZIMA WAWE
MWILI MMOJA!! UPENDO WA ROHO LAZIMA UWEPO ILI KUAMBATANA KAMA TULIVYOONA
KUAMBATANA KUNACHUKUA MUDA NA KUNAENDA HATUA KWA HATUA! Kuambatana
kwenyewe kupo kwenye maeneo saba: 1) kiroho (spiritually), 2) kiakili
(mentally), 3) kihisia (emotionally), 4) kimwili, (physically), 5)
kifedha (financially), 6) Kimali na vitu (material possessions), na 7)
kijamii (socially). Haya ni maeneo saba ambayo ndoa huwa inakua,
inajengwa, inatengenezwa, inaimarishwa, inatiwa nguvu, inarekebishwa,
inafundishwa, na inalindwa! WALIMU, WAKUFUNZI, NA WANAFUNZI NI WANANDOA
WENYEWE!! WAKUFUNZI WA NDOA TAKATIFU LAZIMA WAWE WAMEISHI KATIKA NDOA
TAKATIFU KWA MIAKA MINGI, BADO WANAISHI HUMO, WAMEZAA WATOTO AMBAO
WAMELELEWA NA WANAENDELEA KATIKA UTAKATIFU, UNYENYEKEVU, UTAUWA, UTII,
HOFU YA MUNGU, UNYOOFU NA USAFI WA MOYO, MAONYO NA ADABU NJEMA KATIKA
BWANA, NA WANASHUHUDIWA HIVYO NA KANISA TAKATIFU, NA WATU WOTE!! NJE YA
HAPO HAWANA SIFA ZA KUFUNDISHA NDOA TAKATIFU MAANA WANAISHI KWENYE
NDOA ZA ANGUKO, AU NI WAONGO AMBAO WANATAFUTA UMAARUFU, SIFA NA UTUKUFU
WA WANADAMU, FAIDA BINAFSI, NA HAWANA UZOEFU WA KUISHI KATIKA NDOA
TAKATIFU PASIPO KUUACHA UTAKATIFU NA KUKUA NA KUKOMAA HIVYO! Hii ndiyo
maana Roho Mtakatifu aliponena kupitia Paulo kuhusu UONGOZI WA KIROHO
KWENYE KANISA LA KRISTO ALIZISEMA SIFA ZIFUATAZO:
2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke
mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye
kufundisha;
1 Timotheo 3:2
>> ASKOFU/MCHUNGAJI/MSIMAMIZI/
>> AWE MUME ASIYELAUMIKA (BLAMELESS TESTIMONY OF HIS PEERS)
>> AJUAYE KUFUNDISHA!! YAANI, MWENYE KUWEZA KUFUNDISHA KANISA LA
NDOA YAKE, NA KANISA LA FAMILIA YAKE NENO LA KWELI, LENYE UZIMA, LA
MUNGU
Kwa nini uongozi kanisani uhusishwe na ndoa??!! (mume wa mke mmoja??!!)
Ni kwa sababu NDOA TAKATIFU NDILO KANISA LA MSINGI LA KWANZA, AMBALO
LIKIONGEZEKA HUWA KANISA LA MSINGI LA PILI LA FAMILIA!! Kanisa la mahali
pamoja lina misingi hii miwili muhimu! Hivyo NDOA TAKATIFU, AMBAYO
MCHUNGAJI WAKE NI MUME, NDIYO HUTUPATIA KANISA IMARA TAKATIFU LA MAHALI
PAMOJA AMBALO NI MKUSANYIKO WA MAKANISA YA NYUMBANI MBALIMBALI AMBAYO
YANAUNDWA NA MAKANISA YA NDOA NA YA FAMILIA, NA MCHUNGAJI WA MAKANISA YA
MSINGI YA NYUMBANI NI "MUME WA MKE MMOJA"!! Shetani leo amefanya lile
lile alilolifanya bustanini la kupotosha Neno la Mungu, na kuigeuza
kweli kuwa uongo na kujaza wachungaji wanawake!! KIONGOZI WA KIROHO NI
MUME WA MKE MMOJA, NJE YA HAPO "NYOKA/SHETANI" ANATAWALA NA SI MUNGU
KAMWE!! Mwenye masikio na asikie neno hili asemalo Roho!!
4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
1 Timotheo 3:4
>> ASKOFU, MCHUNGAJI, MSIMAMIZI, AU KIONGOZI YEYOTE WA KIROHO,
LAZIMA AWE MUME WA MKE MMOJA, MWENYE WATOTO WATAKATIFU!! YAANI, LAZIMA
AWE AMETHIBITIKA, KWA USHAHIDI WA WATOTO WAKE KUSHUHUDIWA KUWA NA
MWENENDO MZURI WA HESHIMA, ADABU NJEMA, UTAUWA, UTAKATIFU, HOFU YA
MUNGU, N.K. LAZIMA WAWE WANAKUA KATIKA HEKIMA NA KIMO WAKIMPENDEZA MUNGU
NA WANADAMU KAMA YESU MWENYEWE ALIVYOKUA (LUKA 2:52)
>> KUNA WATU WAMETOKA KWENYE NDOA ZA ANGUKO AMBAZO HAZINA SIFA ZA
NDOA TAKATIFU, AMBAO WAMEPEWA UONGOZI WA KIROHO HUKU WAKIWA WAKO KINYUME
NA ROHO MWENYEWE MTAKATIFU, NA MATOKEO NI KUVAMIWA NA KUTUMIWA NA roho
za "nyoka" ALIYEMDANGANYA MWANAMKE NA KUWAANGUSHA DHAMBINI YEYE NA
MUMEWE ALIYERIDHIA UASI WA MKEWE! MAASKOFU NA WACHUNGAJI WALIOIACHA
KWELI HUWA WANAWEKA KUWA KIONGOZI MTU YEYOTE KAMA WANAVYOJISIKIA PASIPO KUMFUATA
ROHO MTAKATIFU NA NENO LAKE TAKATIFU!!
5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
1 Timotheo 3:5
>> IKO WAZI MPAKA HAPA KWAMBA KANISA LA NYUMBANI NDIO MSINGI IMARA
WA KANISA LA MAHALI PAMOJA! NA HII NDIYO BWANA WA KANISA ANAULIZA
KWAMBA MTU ASIYEJUA KUISIMAMIA NYUMBA YAKE VEMA ATALITUNZAJE KANISA LA
MUNGU? KAMA NDOA NA FAMILIA ZIMEKUSHINDA KUZILEA SAWASAWA NA NENO LA
MUNGU, MAANA YAKE UMESHINDWA KULITUNZA, KULILEA, KULILISHA, NA
KULISIMAMIA KANISA LA NYUMBANI, NA HUWEZI KULITUNZA KANISA LA MAHALI
PAMOJA KWA KUWA UMESHINDWA KWENYE KANISA LA MSINGI! NDOA YAKO SIYO
TAKATIFU MAANA INA HAWA ALIYEDANGANYWA NA ADAMU ALIYEASI KWA KURIDHIA
UASI WA MKEWE! NA WATOTO WENU WATAKUWA NI AKINA KAINI!! HUFAI KULIONGOZA
KANISA LA MUNGU ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE!!!
>> NYAKATI HIZI VIGEZO KAMA HIVI VYA MSINGI VYA KIMAANDIKO
HAVIFUATWI NA BADALA YAKE WASIO NA NDOA WANAPEWA KUSIMAMIA MAKANISA,
WALIOSHINDWA KUTUNZA NYUMBA ZAO NA KULEA WATOTO WAO KATIKA NJIA
ZIWAPASAZO AMBAZO HAWATAZIACHA HADI UZEENI, NAO WANAITWA WACHUNGAJI NA
HATA MAASKOFU, ILI MRADI WAMETOKA CHUO FULANI CHA BIBLIA!! HII NI roho
ya uasi ya Adamu ya kukubaliana na ukengeufu wa mkewe kinyume na Neno!!
Adamu akiwa askofu au mchungaji Hawa atafanya atakalo, na nyoka
atatawala!!
6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
1 Timotheo 3:6
>> MTU ALIYEOKOKA KARIBUNI BADO NI MTOTO MCHANGA KATIKA
KRISTO! HUYU HALIJUI VEMA NENO LA HAKI! BADO ANAHITAJI MAZIWA ILI KWA
HAYO APATE KUUKULIA WOKOVU (1 PETRO 2:2, 1 KOR 3:1-2, WAEBRANIA
5:12-14)! HUYU BADO HAWEZI MIKIMIKI YA VITA VYA KIROHO KWA KUWA
HAJAKOMAA KIROHO!! Lakini nyoka yule yule aliyemdanganya mwanamke
bustanini amewadanganya watumishi, wachungaji, maaskofu n.k. KUWARUHUSU
WATOTO WACHANGA KUHUDUMU MADHABAHUNI!! Utasikia mwimbaji maarufu wa
duniani kaokoka halafu siku mbili kaanza kuimba huko na huko, anatafuta
wadhamini maredioni, na kwenye TVs ili atoe albamu, mara amekuwa
mchungaji au mwinjilisti! Au mtu alikuwa mganga kaokoka, mara siku mbili
tatu kapelekwa chuo cha Biblia na akitoka huko anakuwa mchungaji mahali au
mwinjilisti!! CHUO CHA BIBLIA HAKIMFANYI MTU AKUE KIROHO BALI
KINAMUONGEZEA TU MTU MAARIFA KUHUSU MUNGU (KNOWLEDGE ABOUT GOD AND NOT
INTIMATE KNOWLEDGE OF GOD!!) WENGI WAMEPOTEZWA NA WANAENDELEA KUPOTEZWA na
WATUMISHI AKINA HAWA ALIYEDANGANYWA NA ADAMU ALIYEASI KUTOKA KWENYE NDOA
ZA ANGUKO!! Yaani, ile roho ya anguko inatenda kazi ndani yao! Dhambi!
Uasi wa Neno! Kulipuuza Neno! Kutolizingatia Neno!
7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
1 Timotheo 3:7
>> LAZIMA KIONGOZI WA KIROHO, HUYU MUME WA MKE MMOJA AWE NA
USHUHUDA WA MAISHA MATAKATIFU KWENYE JAMII INAYOMZUNGUKA ILI KUMFUMBA
KINYWA SHETANI, AKIANZIA KWENYE NDOA YAKE MWENYEWE!!
>> Ibilisi ndiye mshtaki wa watakatifu walio ndani ya Kristo!!
Anawashtaki mbele za Mungu mchana na usiku (Ufunuo 12:10), pia huleta
mashitaka ya uongo pia kupitia wale wenye roho za shetani za uzushi,
fitina, uongo, udanganyifu, usengenyaji, usingiziaji, n.k. alizoweka
ndani ya watenda dhambi anaowatumikisha dhambini!! Ndiyo maana Biblia
inasema;
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa. (1 Petro 2:12)
15 Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; (1 Petro 2:15)
20 Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu. (1 Petro 2:20)
21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. (1 Petro 2:21)
Na Paulo alisema,
3 Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;
2 Wakorintho 6:3
MWILI MMOJA
Maandiko yanasema, 24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba
yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:24
>> Mwili mmoja maana yake: Tunapendana, tunaheshimiana, tunajuana,
tunafahamiana, tunajuliana, tunapatiana, tunaendana, tunakubaliana,
tunashirikiana, tunasaidiana, tunafikiriana, tunaombeana,
tunachukuliana, tunasameheana, tunavumiliana, tunafurahishana, tunapeana
raha, tunahudumiana, tunafikiriana, tunawaziana, tunatangulizana,
tunafuatana, tunahurumiana, tunateteana, tunasitiriana, tunapiganiana,
tunalindana, tunaimarishana, tunajengana, tunafarijiana, tunatiana
moyo, tunainuana, tunaachiliana, tunatendeana mema, tunazawadiana,
tunasikilizana, tunapatana, tupo kila
mmoja alipo kwa ajili ya mwenza wake, kila mmoja anatafuta
faida/furaha/mema/na amani ya mwenza wake!!/tunawezeshana, tunatiana
nguvu, tunajuana hisia zetu, tunatafutiana, tunapumzishana,
tunarahisishiana, tunafundishana, tunaondoleana maumivu, tunashibishana,
tunashirikishana, tunajulishana, tunakumbukana, tunagawiana,
tunaambatana, tunajadiliana, tunakubaliana, hatuweki siri kati yetu,
(yaliyo moyoni mwangu yamo moyoni mwa mwenzangu), hatutengani,
hatuachani, hatufarakani, n.k. SISI NI MWILI MMOJA!! KILA NILIPO/ALIPO,
KILA NIENDAPO/ AENDAPO, NA KILA NILIFANYALO/ALIFANYALO
1) NI KWA FAIDA NA MANUFAA YA MWANANDOA MKE/MUME WANGU
2) NI KWA NIABA YA MKE AMA MUME WANGU!!
3) KIMSINGI MFUPA HAUWEZI KUTOKA KWENYE MWILI UKATEMBEA NA KUFANYA
SHUGHULI PEKE YAKE, HALI KADHALIKA NYAMA NAZO HAZIWEZI KUFANYA HIVYO
PIA! Biblia inasema,
21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
Mwanzo 2:21
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
Mwanzo 2:22
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu,
na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa
katika mwanamume.
Mwanzo 2:23
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:24
>> Popote alipo mume anamwakilisha mkewe na, yupo kwa ajili ya
mkewe! Kule kusema yuko kwa ajili ya mkewe kuna maanisha yuko kwa ajili
yake mwenyewe, KWA KUWA MKEWE NI MWILI WAKE! Hali kadhalika mke kokote
alipo, au lolote alifanyalo, NI KWA AJILI YA MUMEWE NA KWA NIABA YA
MUMEWE MAANA YEYE ALITWALIWA KUTOKA KWENYE MWILI WA MWANAMUME
NA HIVYO HAWEZI KUTENDA AMA KUENENDA NJE YA AU PASIPO MWILI ULE ALIKOTWALIWA!! Paulo alisema:
"33 BALI YEYE ALIYEOA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII, JINSI ATAKAVYOMPENDEZA MKEWE."
1 Wakorintho 7:33
"34 .............. Lakini YEYE ALIYEOLEWA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII, JINSI ATAKAVYOMPENDEZA MUMEWE."
1 Wakorintho 7:34
>> KATIKA MAMBO YOTE YA DUNIA HII UYAFANYAYO WEWE MUME MNUFAIKA WA KWANZA NI MKEO!!
>> NA KATIKA MAMBO YOTE YA DUNIA HII UYAFANYAYO WEWE MKE NI KWA AJILI YA MUMEO!!
>> HII INAITWA KANUNI YA MKE KWANZA-MUME KWANZA, WATOTO NA WENGINE
BAADAE!! Kutotumika kwa kanuni hii kuliangusha ndoa bustanini!!
Mwanamke alianza kwanza kula yeye na kushiba, kisha ndipo akamkumbuka
mumewe akiwa ameshaharibu!!! (ameshatenda dhambi!) Angechukua matunda
akayaleta kwa mumewe ili ampe wayale baada ya kumshirikisha "elimu
potofu" ya nyoka aliyopewa, pengine Adamu asingekubali na wangetubu na
kupona!! Kumbuka wewe "mwanamke unayejiona uko huru mbali na mamlaka ya
mumeo kwamba imeandikwa:
" 8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
1 Wakorintho 11:8
9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
1 Wakorintho 11:9
>>MWANAMKE ULIUMBWA KWA AJILI YA MWANAMUME!! Kanuni
ya ndoa takatifu (principle of submission to divinely-appointed
authority) ni hii: KWA AJILI YA YESU, KWA AJILI YA MKE WANGU!! (for
Jesus, for my wife!) na KWA AJILI YA YESU, KWA AJILI YA MUME WANGU! (for
Jesus, for my husband!)
Ubarikiwe na Bwana Yesu, haleluya!!