UPENDO WA MUNGU (MFULULIZO WA SEHEMU SITA FUPIFUPI)
UPENDO SEHEMU YA KWANZA
1 John 5:1-2
[1]Whosoever believeth that Jesus is the Christ is born of God: and every one that loveth him that begat loveth him also that is begotten of him.
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
[2]By this we know that we love the children of God, when we love God, and keep his commandments.
Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
>>Kumpenda Mungu ni kuzishika amri zake
>> Kumpenda Mungu maana yake ni kuwapenda watoto wa Mungu!
>> ANAYEMPENDA MUNGU NI YULE ANAYEWAPENDA WATOTO WA MUNGU!!
“Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.”
1 Yohana 3:14
>> Asiyewapenda ndugu zake waliookoka bado yuko mautini! Yaani, hajaokoka!! kwa maana aliyeokoka ana uzima wa milele ndani yake ambayo ndiyo maisha ya milele ya Neno/Mungu/Upendo!
>> Aliyeokoka anawapenda ndugu zake kivitendo na si kwa maneno matupu!!
Biblia inasema,
17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?
1 Yohana 3:17
18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
1 Yohana 3:18
>> Maisha ya aliyeokoka ni maisha ya kuwapenda kivitendo kila siku ndugu zako waliookoka, na wanadamu wengine!!
>> KUOKOKA KUNAONEKANA KILA SIKU KIMATENDO!! UNAPENDAJE? YAANI, UNAFANYA AU UNATENDA NINI KWA NDUGUZO KILA IITWAPO LEO KUTHIBITISHA NA KUONYESHA UPENDO WAKO WA KWELI MAISHANI?
>> TWAWEZA KUSEMA KUOKOKA NI KUISHI MAISHA YA KUMPENDA MUNGU NA MWANADAMU KILA IITWAPO LEO
Lakini Biblia inasema,
“Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.”
1 Yohana 4:20
>> HUWEZI KUMPENDA MUNGU USIYEMWONA HUKU UNAMCHUKIA NDUGU YAKO UNAYEMWONA!!
>> UKISEMA UNAMPENDA MUNGU, HUKU UNAMCHUKIA NDUGUYO WEWE NI MUONGO!! HUJAOKOKA!!! BADO UMO GIZANI!!
>> UPENDO WA MUNGU NDIYO NURU YA KWELI!! TUKIPENDANA NDIPO MUNGU HUKAA NDANI YETU
“Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.”
1 Yohana 4:12
>> Tusipopendana "shetani" NDIYE HUKAA MIOYONI MWETU!! Na chuki yake ndiyo IMEJAA NA INATAWALA MIOYO YETU!
“Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.”
1 Yohana 4:8
>> WEWE USIYEPENDA (MWENYE CHUKI) HUJAWAHI KUMJUA MUNGU!!
>> Yaani, haijalishi mambo mangapi ya kidini umeyafanya (religious endevours/activities), au unajidhania wewe ni mtu wa kidini namna gani (religious), au unaonekana religious namna gani, HUJAWAHI KUMJUA MUNGU, HUNA MUNGU, NA HUJAOKOKA, MAANA MUNGU NI UPENDO!!
UPENDO KIVITENDO-2
“17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.”
1 Yohana 3:17-18
1 John 3:17 (New International Version)
If anyone has material possessions and sees a brother or sister in need but has no pity on
them, how can the love of God be in that person?
Tafsiri hii inasema;
1) IKIWA UNA VITU VYA MWILINI UNAVYOVIMILIKI, mfano nguo, viatu, simu, fedha, laptop, nyumba, gari, kiwanja, furniture, chakula, redio, televisheni, godoro, baiskeli, pikipiki, bajaj, kanga, kitenge, suti, mtungi wa gesi, friji, kitanda, kabati, chumba/vyumba, sahani, vyombo, n.k.(hizi na zinginezo ni material possessions, siyo?!)
2) HALAFU UNAONA KWAMBA NDUGUYO WA KIKE AU WA KIUME ANA UHITAJI WA KILE ULICHONACHO NA UNA UWEZO WA KUMSAIDIA;
3) LAKINI HAUMHURUMII WALA KUMSAIDIA!! YAANI, UNAMNYIMA!! UNAMBANIA!! UNAMZUILIA HURUMA YAKO; YAANI, UNAMPOTEZEA; HAUFANYI KITU KWAKE CHOCHOTE: "UNAUCHUNA"; "UNAMCHUNIA" YAANI, NI KAMA VILE UNASEMA MOYONI MWAKO "SHAURI YAKE/ATAJIJU/KILA MTU ABEBE MZIGO WAKE/ AKATAFUTE VYAKE/KWANI YEYE ALIKUWA ANANITEGEMEA MIMI?/YAANI MIMI NIPATE TAABU YEYE NIMPE TU KIULAIIINII/ANAJUA MIMI NIMEVIPATAJE?/YEYE SIYO JUKUMU LANGU (HE/SHE IS NOT MY RESPONSIBILITY) N.K. (shetani ndivyo anavyoongea mioyoni na akilini mwa wabinafsi na wenye chuki-watenda dhambi)
>> NDUGU YAKO NI WAJIBU WAKO, NA HIYO NI AMRI NA AGIZO LA BWANA YESU KWAMBA LAZIMA UUTOE UHAI WAKO KWA AJILI YAKE NDUGU YAKO HUYO!(1 Yohana 3:16) UPENDO (KAMA UMO NDANI YAKO) UTAKUELEKEZA KWAKE HUYO, KUMHUDUMIA, KUMSAIDIA, KUMPATIA MAHITAJI YAKE, KUONDOA SHIDA ZAKE, KUONDOA MATESO YAKE, KUBEBA MIZIGO YAKE, KUMHURUMIA, N.K. KWA AJILI YA YESU ULIYEMWAMINI, ALIYEUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YAKO MSALABANI, NA WEWE SASA UNAFANYA KAMA YEYE ALIVYOFANYA, KWA UPENDO ULE ULE ULIOKUWA NDANI YAKE AMBAO UMEMIMINWA MOYONI MWAKO SASA! NA HUO NDIO UTII WA UPENDO WA KIBIBLIA/KIKRISTO!
1 John 3:16
[16]Hereby perceive we the love of God, because he laid down his life for us: and we ought to lay down our lives for the brethren. { Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.}
>> KAMA KWELE UMELIELEWA PENDO LA MUNGU KWAKO, IMEKUPASA KUYATOA NA WEWE MAISHA YAKO KWA AJILI YA NDUGU ZAKO KATIKA MWILI WA KRISTO!! NDUGU ZAKO NI JUKUMU NA WAJIBU WAKO!! KAMA WEWE NI MTENDA DHAMBI USIYE NA YESU INA MAANA HAUMO KATIKA MWILI WA KRISTO! HAPO SAWA, ENDELEA KUISHI KIBINAFSI NA KWA CHUKI; LAKINI UJUE KUNA SIKU UTASIMAMA MBELE ZAKE YEYE ALIYEKUFIA MSALABANI HALAFU UKAMKATAA NA KUUKATAA UPENDO WAKE!
>> KUYATOA MAISHA YAKO NI KUJITOA WEWE MWENYEWE VYOTE VILE ULIVYO (ALL THAT YOU ARE), NA VYOTE ULIVYONAVYO (ALL THAT YOU HAVE) KWAO NA KWA AJILI YAO!!
>> YAANI, KUYATOA MAISHA YAKO NA VYOTE ULIVYONAVYO "SADAKA KWA MUNGU" KWA AJILI YA NDUGU ZAKO!!
>> HILI NDILO PENDO! HUKU NDIKO KUMPENDA YESU!! HUU NDIO UPENDO WA ROHO KIMATENDO!!
“17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?”
1 Yohana 4:17
4) NDIPO YESU, NDIPO ROHO MTAKATIFU, NDIPO MUNGU (UPENDO MWENYEWE) ANAULIZA "UPENDO WA MUNGU UNAWEZAJE KUKAA NDANI YAKO?!" YAANI, HUNA MOYO ANAOWEZA KUKAA MUNGU MAANA UMEJAA SHETANI (CHUKI NA UBINAFSI)!! KUMBUKA, MUNGU NI UPENDO (1 YOH 4:8)
>> ANDIKO LINASEMA, “UKIONA NDUGUYO NI MHITAJI........!” UPENDO UNA MACHO YA KUONA UHITAJI WA NDUGUYO!! WEWE UNAJUA UHITAJI WA NDUGUZO WENGI, NA HUJAWAHI KUTATUA CHOCHOTE ZAIDI YA KUWADHARAU NA KUJIONA UNA AKILI NA MJANJA ZAIDI YAO, KUJIONA WA KIROHO ZAIDI YAO, UMEBARIKIWA ZAIDI YAO, (WENGINE) UMEKOMBOLEWA ZAIDI YAO (KWA HIYO WAO ETI WANA LAANA BADO!!!)
>> ANDIKO LINAONYESHA WAZI KWAMBA NDUGUYO SIYO MPAKA AJE AKUOMBE!! BALI LINASEMA UKIONA KWAMBA YEYE NI MHITAJI, UNA WAJIBU WA KUMSAIDIA KWA KUMTOA KWENYE HUO UHITAJI!! KAMA HAUFANYI HIVYO NDIPO ANDIKO LINASEMA "UPENDO WA MUNGU UNAWEZAJE KUKAA NDANI YAKO???!!" YAANI, UPENDO HUO HAUJAWAHI KUWEMO NDANI YAKO! NA KWA KUWA MUNGU NI UPENDO, INA MAANA, MUNGU HAJAWAHI KUWEMO MOYONI MWAKO KWA KUWA HUJAWAHI KUWA NA MOYO NAOWEZA KUKAA YEYE AMBAYE NI UPENDO!! NA MOYO WA MWANADAMU LAZIMA AMA UWE UNA MUNGU AU SHETANI!! USIPOKUWA NA MUNGU, LAZIMA UWE NA SHETANI!
>> UNAWEZA KUJIDANGANYA NA DHEHEBU AU DINI YAKO NZURI, LAKINI MOYO WAKO HAUNA MUNGU! YAANI, HAUNA YESU!! HUJAOKOKA!! MAANA, UPENDO HAUONEKANI MAISHANI MWAKO!! UNAWEZA KUFANYA MENGI KWA JINA LA MUNGU LAKINI UNAPOTEZA MUDA KWA KUWA MUNGU ANA HAJA NA MOYO WAKO AMBAKO NDIKO ILIKO roho yako! MUNGU HANA SHIDA YA CHOCHOTE UNACHOMPA NA WALA HAJAWAHI KUKUOMBA UMFANYIE HAYO UNAYOYAFANYA KWA JINA LA DINI HUKU HAUJAMPA NAFASI MOYONI MWAKO AUTAWALE!!
New Living Translation (1 John/Yohana 3:17)
If someone has enough money to live well and sees a brother or sister in need but shows no compassion—how can God’s love be in that person?
TAFSIRI HII INASEMA:
1) IKIWA UNA FEDHA ZA KUKUTOSHA KUISHI MAISHA MAZURI
2) HALAFU UNAMUONA NDUGU YAKO WA KIKE AU WA KIUME AKIWA NI MHITAJI
3) HALAFU HUONYESHI HURUMA YOYOTE KWAKE! YAANI, HUMHURUMII KABISA NA KUMSAIDIA
4) UPENDO WA MUNGU UNAWEZAJE KUWA NDANI YAKO?
>> TUNARUDI PALE PALE KWAMBA HUNA UPENDO NDANI YAKO, NA HIVYO HUNA YESU, NA HII INA MAANA HUJAOKOKA BADO!! UKIFA SASA HUTAMWONA MUNGU MILELE!!
English Standard Version (1 John/Yohana 3:17)
“But if anyone has the world’s goods and sees his brother in need, yet closes his heart
against him, how does God’s love abide in him?”
TAFSIRI HII INASEMA:
1) IKIWA UMEJALIWA KUMILIKI VITU VYA DUNIA HII
2) HALAFU UNAMUONA NDUGU YAKO NI MHITAJI
3) KISHA UNAMFUNGIA MOYO WAKO/HAUMFUNGULII MOYO WAKO
4) UPENDO WA MUNGU UNAKAAJE NDANI YAKO?
>> HAKUNA NAMNA UPENDO WA MUNGU UNAWEZA KUKAA NDANI YAKO!!!
>> HII INAMAANISHA LAZIMA UTUBU, UOKOKE, UBADILISHWE MOYO, UUPOKEE UPENDO WA MUNGU KWA KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO, NA KUANZA KUISHI MAISHA HALISI YA UPENDO WA KRISTO KIVITENDO!!!
Berean Standard Bible (1 John/Yohana 3:17)
“If anyone with earthly possessions sees his brother in need, but withholds his compassion
from him, how can the love of God abide in him?”
TAFSIRI YAKE INASEMA;
1) IKIWA MTU YEYOTE ANAMILIKI VITU VYA DUNIA HII (VINAVYOHARIBIKA)
2) HALAFU UNAMUONA NDUGU YAKO NI MHITAJI
3) KISHA UKAMZUILIA HURUMA YAKO
4) UPENDO WA MUNGU UNAWEZAJE KUKAA NDANI YAKO??!!
>> KAMA HUNA UPENDO MAANA YAKE HUNA MUNGU! HATA KAMA UNAJISEMA UNA DINI IPI AU DHEHEBU LIPI, UNAJIDANGANYA! HUNA UPENDO, HUNA MUNGU! WEWE UNA UPENDO WA VITU NA SIYO UPENDO WA MUNGU! UNAABUDU SANAMU PESA, MALI, NA UTAJIRI! HUNA MUNGU MAANA HAJAWAHI KUWEMO MOYONI MWAKO, INGAWA UNAJISEMA WEWE NI MTU WA DINI SANA, AU DHEHEBU FULANI, AMA VYOVYOTE VILE! TUBU UOKOKE, VINGINEVYO UTAANGAMIA! NI MBAYA SANA KUJIDANGANYA HALAFU SIKU YA MWISHO UKAJIKUTA UMEPOTEA NA KUINGIA KWENYE ADHABU YA MILELE!
UPENDO SEHEMU YA TATU
Tumetoka kuona jinsi ambavyo UPENDO WA MUNGU UKIWEMO NDANI YAKO UTAISHI MAISHA YA KUSAIDIA, NA KUSAIDIA, NA KUSAIDIA, KWA UPENDO; NA KWAMBA KAMWE HUWEZI KUMUONA NDUGUYO NI MHITAJI, AU KUJUA UHITAJI WA NDUGUYO, NA UNA UWEZO WA KUSAIDIA, HALAFU "UKAKAUSHA!!!" HIYO NI ISHARA KUU KWAMBA HUNA MUNGU (UPENDO)!!
>> USIPOTUBU NA KUMZALIA MUNGU MATUNDA YAPASAYO TOBA KUONYESHA KWAMBA UMEBADILIKA MOYO WAKO....!
“8 Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.”
Luka 3:8
“9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”
Luka 3:9
>> LAZIMA UKATWE KUTOKA MAISHA HAYA HAPA DUNIANI; NA LAZIMA UKATWE PIA NA KUTOKA KATIKA MWILI WA KRISTO/KANISA; LAZIMA UKATWE NA KUONDOLEWA KWENYE HUDUMA, NA KISHA KUTUPWA MOTONI KAMA HAWA HAPA SIKU YA MWISHO!!
“31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;”
Mathayo 25:31
“32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;”
Mathayo 25:32
“33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.”
Mathayo 25:33
“34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;”
Mathayo 25:34
“35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;”
Mathayo 25:35
“36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.”
Mathayo 25:36
“37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?”
Mathayo 25:37
“38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?”
Mathayo 25:38
“39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?”
Mathayo 25:39
“40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”
Mathayo 25:40
“41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;”
Mathayo 25:41
“42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;”
Mathayo 25:42
“43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.”
Mathayo 25:43
“44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?”
Mathayo 25:44
“45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.”
Mathayo 25:45
“46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”
Mathayo 25:46
>> UPENDO NDIYO AMRI MPYA YA YESU, KWA AGANO JIPYA LA DAMU YA YAKE!
>> UPENDO NDIYO "DINI" YA AGANO JIPYA!!
“34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Yohana 13:34
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”
Yohana 13:35
>> ALIYEOKOKA ANATAMBULIKA NA KUTOFAUTISHWA NA DUNIA KWA UPENDO WAKE KIVITENDO KILA MAHALI ALIPO
>> KANISA NALO LINATAMBULIKA KWA UPENDANO WA NDUGU WALIOOKOKA WANAVYOISHI NA KUSHUHUDIWA NA DUNIA INAYOWAZUNGUKA KWA UPENDO WAO
>> UPENDO KIVITENDO UNAKUTAMBULISHA KWAMBA YESU YUKO NDANI YAKO HAKIKA
>> JE! UNASHUHUDIWA KWA UPENDO KAZINI? CHUONI? NYUMBANI? SHULENI? NA KILA ULIPO?
"Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi."(mst 35)
>> WATU WOTE WATATAMBUA KWELI MMEOKOKA!!
>> UPENDO KILA WAKATI, UPENDO KILA MAHALI NDIO USHUHUDA WA MKRISTO!!(LOVE EVERYWHERE, LOVE EVERY TIME)
Agizo la Upendo ni hili:
“31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
Luka 6:31
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”
Luka 6:38
Na tena,
“24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Marko 4:24
25 Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.”
Marko 4:25
UPENDO SEHEMU YA NNE
Wale wa kwenye Mathayo 25:46 watakwenda kuingia JEHANAMU kwa sababu WALIISHI KINAFIKI WAKIJIDANGANYA NA KUDANGANYA WENGI huku Upendo wa Mungu HAUMO NDANI YAO (MIOYONI MWAO)!!
“lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.”
2 Timotheo 3:13
“Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.”
Yakobo 1:22
>>Walikuwa hawalitendi NENO! Walikuwa hawaitendi KWELI! Hawakuwa na Upendo wa Kweli wa Mungu mioyoni mwao!
-Walionekana ni watu wa kushika dini sana (they seemed to be very religious)
-Walitenda mema hapa na pale WALIPOPATAKA NA KUPACHAGUA WAO, KWA WATU WAO WALIOWAPENDA NA KUWACHAGUA, HUKU WAKIWABAGUA NA KUJITENGA NA WENGINE WALIOWAONA MIZIGO (LIABILITIES), NA KWAMBA HAWANA KITU CHA KUWAONGEZEA, ZAIDI ZAIDI WATAWAPUNGUZIA!! WALIWAFIKIRIA HIVYO NDUGU ZAO AMBAO YESU ALIWAFIA MSALABANI!!! HAKIKA WALIKUWA WANA WA JEHANAMU SIKU ZAO ZOTE!! Yesu alikataa unafiki wa jinsi hii:
“27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,” (Luka 6:27)
>> MPENDE ADUI YAKO, NA SIYO KUMCHUKIA!! HUO NDIO UPENDO WA MUNGU!! KUWAPENDA MAADUI ZAKO KIVITENDO!
“20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.”
Warumi 12:20
“21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.”
Warumi 12:21
-UPENDO WA MUNGU SIKUZOTE HUUSHINDA UBAYA KWA WEMA!
>> YAANI, WATENDEE MEMA WOTE WANAOKUCHUKIA KILA UPATAPO NAFASI! NA PIA UITAFUTE HIYO NAFASI!!
“28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.”
Luka 6:28
>> WABARIKI WALE WOTE WANAOKULAANI!!
>> WAOMBEE WANAOKUONEA/WANAOKUDHULUMU/WANAOKUTENDA MABAYA, N.K.
>> UPENDO HAURUDISHI LAANA KWA LAANA!
“29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.”
Luka 6:29
>> USIGOMBANE/USIPIGANE KIMWILI/USIJITETEE KIMWILI/USIJILIPIZE KISASI/KUBALI KUONEWA, KUPIGWA AU KUNYANG’ANYW!, WEWE NYENYEKEA TU! UWE TAYARI HATA KUTENDWA MABAYA ZAIDI; HIVI NDIVYO ALIVYOISHI YESU, NA NDIYO MAISHA YAKE YESU LEO NDANI YAKO KAMA UNAO UPENDO WAKE!
“7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.”
Isaya 53:7
>> YESU ALIONEWA LAKINI ALINYENYEKEA NA WALA HAKUJITETEA!
>>MTU AKIKUNYANG'ANYA KITU CHAKO CHOCHOTE, UWE TAYARI KUMUACHIA NA KINGINE CHAKO CHOCHOTE! MWACHE ACHUKUE!! BAKI NA YESU!! ATAKUPA VYOTE!!! HUU NI UTAYARI WA KUNYANG'ANYWA MALI ZAKO!
“34 Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.”
Waebrania 10:34
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
Luka 6:30
>> MPE KILA AKUOMBAYE! USIMNYIME MTU ANAYEKUOMBA! MWENYE UPENDO HANYIMI WATU VITU WANAVYOMWOMBA!! (USITENDE DHAMBI KWA KUTOA KWAKO KWA KIGEZO CHA UPENDO!!)
>> akunyang'anyaye vitu vyako usitake akurudishie!!
Imeandikwa
"15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."
Luka 12:15
>> UNAPOGOMBANA/KUVUTANA/KUPIGANA N.K. KWA SABABU YA KUNYANG'ANYWA VITU VINAVYOHARIBIKA, WEWE BADO MOYO WAKO UKO KWENYE VITU, NA UNATUMAINIA VITU, UNA TAMAA BADO!! TUMAINI LAKO HALIKO KWA MUNGU!! KWANI ALIKUAMBIA NANI KWAMBA MUNGU HAWEZI KUKURUDISHIA ZAIDI YA HIVYO ULIVYONYANG'ANYWA? USIABUDU SANAMU VITU, MWABUDU YAHWEH!!
“31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.”
Luka 6:31
>>USICHOTAKA WEWE KUTENDEWA, USIMTENDEE MWINGINE!
>> UNACHOTAKA WEWE KUTENDEWA ANZA WEWE KUWATENDEA WENGINE!!
>> ISHI MAISHA YA KUWATENDEA WENGINE VILE UNAVYOTAKA WEWE KUTENDEWA ILI KUTHIBITISHA KWAMBA MOYO WAKO HAUNA UBINAFSI NA CHUKI! (SELFISHNESS AND HATRED)
“32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.”
Luka 6:32
>> USIWAPENDE WALE TU WANAOKUPENDA WEWE!! HUO NI UBINAFSI TU WA WAOVU!! SIYO UPENDO HUO!
>> LAZIMA IWEPO TOFAUTI KATI YA WATENDA DHAMBI NA WEWE MTOTO WA MUNGU ULIYEJAA UPENDO WA MUNGU
“33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.”
Luka 6:33
>> USIWATENDEE MEMA WALE TU WANAOKUTENDEAGA MEMA, HUO NI UMIMI/UCHOYO/UBINAFSI, NA SIYO UPENDO!
>> LAZIMA IWEPO TOFAUTI KATI YA WATENDA DHAMBI NA WEWE MTOTO WA MUNGU ULIYEJAA UPENDO WA MUNGU
“34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.”
Luka 6:34
>> UKIKOPESHA USITARAJIE KULIPWA!! MAANA HIYO NI IBADA YA SANAMU NA NI KUTUMAINIA FEDHA BADALA YA MUNGU!!
>> LAZIMA IWEPO TOFAUTI KATI YA WATENDA DHAMBI NA WEWE MTOTO WA MUNGU ULIYEJAA UPENDO WA MUNGU
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
Luka 6:35
>> HAYA MATATU NDIO UPENDO NA NDIKO KUOKOKA KULIVYO
1) KUWAPENDA MAADUI ZAKO, 2) KUTENDA MEMA BILA UBAGUZI WALA UPENDELEO, PASIPO KUKOMA! 3) KUKOPESHA NA USITUMAINI KULIPWA, NA MUNGU ATAKULIPA YEYE MWENYEWE!! HIVYO NDIVYO MTOTO WA MUNGU ANAVYOISHI KWA UPENDO WA MUNGU
“36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.”
Luka 6:36
>> MSINGI WA HAYO YOTE NI HURUMA YA UPENDO (MUNGU) NDANI YAKE YESU KRISTO!
“38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”
Luka 6:38
>> KATIKA MAISHA YAKO WEWE DUMU KATIKA KUWAPA WATU VITU, NAWE UTAPEWA KIPIMO TELE CHA KUJAA, KUSHINDILIWA, KUFURIKA HATA KUMWAGIKA!!!
>> UPENDO UNATOA, UNATOA, KISHA UNATOA, NA KUTOA; HALAFU UNAENDELEA KUTOA, KUTOA, KUTOA, NA KUZIDI KUTOA KILA SIKU, KILA MAHALI, KILA ALIPO MHITAJI, NA ADUI, NA MASKINI, NA WATU WOTE PASIPO HASIRA, GHADHABU, KUZIRA, KUSUSA, KUGHAIRI, KUACHA, KURUDI NYUMA, KUYUMBA, KUBAGUA, KUKATA TAMAA, WALA KUVUNJIKA MOYO! UPENDO NI TAJIRI WA MATENDO MEMA!
16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
1 Yohana 3:16
17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?
1 Yohana 3:17
18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
1 Yohana 3:18
19 Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,
1 Yohana 3:19
22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. (1 Yohana 3:22)
23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.
1 Yohana 3:23
24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
1 Yohana 3:24
>> LAZIMA IWEPO TOFAUTI KATI YA WATENDA DHAMBI NA WEWE MTOTO WA MUNGU ULIYEJAA UPENDO WA MUNGU
>> KUNA UTOAJI WA MAENEO SABA
1) UTOAJI KIROHO (SPIRITUAL GIVING)
2) UTOAJI KIAKILI (MENTAL GIVING)
3) UTOAJI KIHISIA (EMOTIONAL GIVING)
4) UTOAJI MWILI WAKO (PHYSICAL PRESENCE AND HELP)
5) UTOAJI FEDHA (FINANCIAL GIVING)
6) UTOAJI MALI NA VITU (MATERIAL GIVING)
7) UTOAJI KIJAMII (SOCIAL GIVING)
>> JAMII INAFAIDIKA VIPI NA UPENDO WA MUNGU ULIO NDANI YAKO?
UPENDO SEHEMU YA TANO
“10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.”
Warumi 13:10
>> PENDO LA MUNGU HALIMFANYII JIRANI UBAYA WA NAMNA YOYOTE
>> UBAYA WOWOTE UNAOMFANYIA MTU AWAYE YOTE, NI USHAHIDI KWAMBA HUNA UPENDO WA MUNGU NDANI YAKO!! HII MAANA YAKE HUNA MUNGU KWA MAANA MUNGU NI UPENDO (1 YOH 4:8)
>> ALIYE NA MUNGU (UPENDO) NDANI YAKE HATENDI MABAYA KAMWE, NA WALA HAMTENDEI MABAYA JIRANI YAKE (MTU YEYOTE), BALI SIKUZOTE HUTENDA MEMA (EFE 2:10) NA TENA ANA BIDII KATIKA KUTENDA MEMA (TIT 2:13-14)
>>DUNIA INAYOMTAZAMA NA JAMII INAYOMZUNGUKA MTOTO WA MUNGU, INASHUHUDIA UPENDO ULIOMO NDANI YAKE KWA WATU WOTE KIVITENDO, NA INAMTUKUZA MUNGU KWA AJILI YAKE!!
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
Mathayo 5:14
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Mathayo 5:15
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Mathayo 5:16
>> MATENDO MEMA YALIYOJAA NA KUFURIKA KWA MTOTO WA MUNGU NI "TAA YA UPENDO" ING'ARAYO NA INAYOWAANGAZA WOTE WANAOMZUNGUKA!!!
>> KUTENDA MEMA KWA HURUMA NA UPENDO NDIKO KUANGAZA KWA ULIMWENGU!! "ndani yake Neno ndimo ulimokuwa uzima, NAO ULE UZIMA ULIKUWA NURU YA WATU" (Yoh 1:4)
NENO MOYONI NI UZIMA, NAO HUO UZIMA NI NURU YA WATU!!
>> HII MAANA YAKE UPENDO HAUJIFICHI!! UPENDO UNATENDA!! UPENDO UNAWATENDEA WENGINE MEMA!! PENDO HALIMFANYII JIRANI NENO BAYA! PENDO HUTENDA MEMA TU NA KAMWE SI MABAYA!
IKIWA AU IWAPO WEWE UNAMTENDEA JIRANI YAKO NENO BAYA;
Unamsema vibaya, unamuwazia vibaya, unamtakia mabaya, unamsengenya, unamnyima na kumzuilia mema yaliyo katika uwezo wako, unamficha taarifa au habari njema, unamficha fursa za kufanikiwa, unamuonea wivu, unapingana naye, hautaki kutambua na kukubali neema aliyopewa na Mungu, unaona kuwa hawezi kukuambia kitu maana umemshusha na kujikweza juu yake, unapenda kujilinganisha na kujipima naye ili ujione bora zaidi yake, unamdhulumu, unamdharau, unamnyanyasa, unamchukia, unamwonea uchungu, unamringia, unamchafua, unamsingizia, unamwibia, unamtapeli, unamdanganya, unampotosha, unambagua, unamsaliti, unamkwaza, unamlalamikia, haumfundishi, haumwombei, haumtakii mema, haumpi wala kumsababishia nafuu, unambebesha mizigo isivyo sawa, hauwazi kumpunguzia wala kumuondolea mizigo, unamchonganisha, unaeneza habari zake mbaya, hauna moyo wa shukrani kwake wala moyo wa kulipa fadhila, unamuelemea, haumsaidii, haumpumzishi, haumridhishi, haumtoshelezi, haujali utu wake, haumheshimu, unamnyoshea vidole, unamkosoa, unamnunia, unamhukumu, unajivuna kwake, unafurahia mabaya yanayompata na kusema amezidi!! haumsaidii katika shida na uhitaji wake, unashindana naye, unamburuza, unamkandamiza, unamtegea, unamuumiza, unamdhuru, unamchongea, unamwaibisha, unamdhalilisha, unamuonea, unamzushia, unamharibia, unamtesa, unamsumbua, unampunja, unampuuza, haumjali, unamsaliti, unamzira, unamsusa, unamtenga, unamtumia tu kwa faida yako, unamgeuka kwa kubadili kauli na ahadi zako kwake, unamtelekeza, unamtenda kwa hila au hiana, unamuasi, haumthamini, haumlindi, unamuudhi/unamkasirisha/unamchukiza kwa makusudi, unamharibia, unamvurugia, unamnyima haki yake, hautimizi wajibu wako kwake, haumtakii mema, sikuzote unaishi kwa kuona makosa, mapungufu, na udhaifu wa wengine na KUYAKUZA, sikuzote unatazama kushindwa, kujikwaa, au kuteleza kwake, NA KUYAKUZA HAYO ZAIDI, NA KUYAZUNGUMZA HAYO ZAIDI, NA KUYAKUMBUKA HAYO ZAIDI!!! UNAMTENDEA MABAYA YOYOTE KWA MAWAZO, MANENO, NA MATENDO; WEWE HUNA YESU/HUJAOKOKA/HUNA MUNGU (UPENDO), kwa maana;
10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
Warumi 13:10
>> UKIPENDA UNAKUWA UMEZITIMIZA AMRI KUMI ZOTE, PAMOJA NA TORATI/SHERIA YOTE YA MUSA!!
>> KAMA UNATENDA MABAYA KAMA HAYO HAPO JUU, HUNA UPENDO MAANA PENDO HALIMFANYII JIRANI NENO BAYA!!
8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
Mathayo 15:8
9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Mathayo 15:9
16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Tito 1:16
>> DINI YA YESU NI UPENDO! DINI TAKATIFU NI UPENDO AU YESU MOYONI MWAKO!
11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo wa Yohana 22:11
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Ufunuo wa Yohana 22:14
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Ufunuo wa Yohana 3:19
Namna nyingine ya kuwatendea mabaya wengine ambayo hufanywa na WAOVU WENYE CHUKI ni kuishi maisha ya kuangalia na kutazama MABAYA PEKE YAKE (always dwelling on the bad side of others!) NA KUYAKUZA MNO HAYO, NA KUYAZUNGUMZIA SIKU ZOTE KANA KWAMBA HANA MEMA HUYO MTU, AU HAO WATU!! Unakataa kabisa kuchukua mema yake na/au kutarajia mema kwake bali kwa makusudi kabisa umeamua kuyakuza mabaya yake KWA SABABU MOYO WAKO NI MBAYA NA PIA UMEJAZA MABAYA HUMO! HUNA UPENDO! HUNA MUNGU! Imeandikwa;
8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
1 Petro 4:8
>> UPENDO HUSITIRI WINGI WA DHAMBI!! UNAYEMCHUKIA NDIYE UTAKUWA MWEPESI KUELEZEA NA KUFUNUA UBAYA WAKE, DHAMBI ZAKE, NA MAKOSA YAKE!!! HUU NI MOYO WA KUSITIRI WENGINE!!! Mwenye UPENDO anapenda kusema mema ya wengine, sifa njema za wengine, habari njema za wengine, mambo mema ya wengine, NA LOLOTE LILILO JEMA LA WENGINE!! Maana Pendo Halimfanyii Neno Baya Jirani Yake!!
Upendo SIKUZOTE hujenga, hufariji, hutia moyo, hufadhili, huhurumia, huvumilia, hutetea, hufundisha, huheshimu, hunyenyekea, hujishusha, hujidhili, hujikana, hujizuia, husaidia, huombea, hubebea mizigo, husamehe, huachilia, hupatanisha, huimarisha, hulinda, huhudumia, hutumikia, hutendea mema, husitiri, hutunza siri, hutii, hurehemu, hujitoa, husema kweli, hutenda haki, huwatanguliza wengine kwa heshima, hutafuta amani, hutafuta faida, manufaa, na mafanikio ya wengine, huwapa wengine zawadi njema zilizo bora, huwafikiria wengine, huthamini wengine, husikiliza wengine, huponya wengine, huinua wengine, hufaidisha wengine, huokoa wengine, hubariki wengine, huwa msaada kwa wengine, hujali wengine, hutafuta amani na wengine, hupatanisha, huwawazia wengine mema, huamini kwa ajili ya wengine, huwapa wengine na wala hanyimi, huwezesha wengine, huwakumbuka wengine kwa mema, hutoa mashauri mema, huunganisha na kuleta umoja, hunena mema, ya kupendeza, na ya kufaa kwa wengine, hukirimu wengine, hauweki kumbukumbu ya mabaya ya wengine, hutafuta mema ya wengine, huzingatia, hujali na kulinda maslahi na faida ya wengine, huheshimu matakwa ya wengine, hutatua shida, adha, na uhitaji wa wengine, hutoa wengine kwenye mateso, haufurahii mabaya kuwapata wengine, hulipa mema kwa mabaya, haulipi baya kwa baya, huwaombea wanaokuonea, huwatendea mema wanaokuchukia, huwapenda adui zake kwa kuwatakia, kuwaombea, na kuwatendea mema, haulipi kisasi, huvumilia mabaya yote, hustahimili yote, hauna majivuno, hauna kiburi, unaridhika na kutosheka na ulichonacho, hauna maringo, hauna jeuri, hauna ukaidi, hauna dharau, si mwepesi wa hasira, mpole, ni wenye kujizuia, una amani, una furaha, ni mwaminifu, umejaa wema na matunda mema, hautafuti sifa, umaarufu, au kuonekana, haujikwezi wala kujiinua, hauna tamaa, hauna mashindano wala majibizano, haubishani, hauenezi ubaya, unaishi kwa imani, unalitenda neno, unampendeza Mungu na wanadamu, unachukia na kujitenga na uovu, unaishi maisha ya utakaso, unatafuta faida ya Kanisa na Ufalme wa Mungu, unawaleta waliopotea kwa Yesu, unawarejeza waliopotea mbali na Kweli, hautafuti maslahi binafsi, hautangulizi matakwa yake bali sikuzote hutanguliza na kutafuta matakwa na maslahi ya Yesu na wengine, na yote kama hayo, SIKUZOTE, MAHALI POTE, NA WAKATI WOTE KWA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA MUNGU!! Pendo HALIMFANYII JIRANI NENO BAYA!!!
Upendo wa Mungu UNAFANYA YOTE HAYA NA ZAIDI UKIWEMO NDANI YAKO katika Kulishika Neno la Kristo (Yoh 14:23) na Kulitenda (Yak 1:22) kwa NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU!! (Zech 4:6) NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU
SIFA/TABIA ZA UPENDO-1
HII NI LOVE THERMOMETER (KIPIMA JOTO CHA UPENDO) AMBAPO UNAWEZA KUJIPIMA PASIPO KUJIDANGANYA KAMA UNA UPENDO KWELI AU HAPANA! MAANA,UPENDO, UKIWEMO NDANI YAKO UNA SIFA/TABIA ZIFUATAZO:
1 Corinthians 13:4-8
[4]Charity suffereth long, and is kind; charity envieth not; charity vaunteth not itself, is not puffed up,
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
[5]Doth not behave itself unseemly, seeketh not her own, is not easily provoked, thinketh no evil;
haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
[6]Rejoiceth not in iniquity, but rejoiceth in the truth;
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
[7]Beareth all things, believeth all things, hopeth all things, endureth all things. huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
[8]Charity never faileth: but whether there be prophecies, they shall fail; whether there be tongues, they shall cease; whether there be knowledge, it shall vanish away.
Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
1) MST 4: Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
a) Upendo huvumilia! Unayempenda utamvumilia, usiyempenda hauwezi kumvumilia! Upendo wako kwake au kwao ndio unaoamua UTAWAVUMILIA KWA KIASI GANI!! Ubinafsi na chuki HAVINA UVUMILIVU!!
b) Upendo hufadhili! Upendo unabidiisha kusaidia! Upendo unasukuma kutoa msaada mkubwa na/au mdogo! Upendo ndo mfadhili mwenyewe! Upendo unamfadhili mwingine!! Unayempenda utamfadhili, unayemchukia hauwezi kumfadhili japo uwezo wa kumfadhili unao! Kwa kuwa umejaa ubinafsi na chuki!! Upendo unafadhili pasipo upendeleo wowote au ubaguzi!!
c) Upendo hauhusudu! Upendo hauonei mwingine wivu! Unayempenda hauwezi kumuonea wivu! Aina ya wivu ambao si wivu wa Bwana ni ule uovu unaotamani alichonacho mwingine kingekuwa chako na unaumia kwa kuwa anacho yeye na wewe huna!! Wivu uovu unatamani nafasi aliyonayo ingekuwa yako, na unaumia kwa sababu anayo yeye na wewe huna! Wivu ambao ni uovu unatamani sifa, heshima, shukrani, na kibali apatazo au alizonazo mwingine, ambazo wewe huna au hupati, na unaumia moyo kwa sababu hiyo! Huu ni ubinafsi na chuki! Unayempenda hauwezi kumuonea husuda au kijicho namna hii!! Upendo hauhusudu!
d) Upendo hautakabari! (love does not brag) Kutakabari ni kujisifia au "kujimwambafai!" Unayempenda hauwezi kuanza kujisifia na kujimwambafai mbele yake na dhidi yake! Huu ni ubinafsi na chuki vyenye lengo la kumuumiza hisia zake, au moyo wake, na kumshusha chini na kujiweka juu!! Upendo hautakabari!!
e) Upendo haujivuni (love is not arrogant); Upendo HAUJIVUNI
Majivuno yote hutoka kwenye mioyo iliyojaa ubinafsi na chuki! Hapa kuna roho ya kupenda kuwa juu ya wengine na kusifiwa kuliko wao! Anayejivuna hawezi kumpa Mungu utukufu maana anautaka yeye huo utukufu wa Mungu, na sifa, na heshima, na shukrani zote!! Majivuno yana kiu ya shetani ya kuabudiwa, kuenziwa, kustaajabiwa, n.k. Lakini Upendo humpa Mungu utukufu kwa Kristo Yesu Bwana wetu! Upendo haujivuni! Upendo unawatanguliza, unawaheshimu, na unawathamini wengine sikuzote, na ndiyo maana HAUJIVUNI
1 Corinthians (Wakorintho) 13:5 KJV
[5]Doth not behave itself unseemly, seeketh not her own, is not easily provoked, thinketh no evil;
haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
Berean Standard Bible (1 Corinthians 13:5)
It is not rude, it is not self-seeking, it is not easily angered, it keeps no account of wrongs.
Hauna jeuri, hautafuti mambo yake, haukasiriki kirahisi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.
1) MST 5a: Upendo haukosi kuwa na adabu!!(Love is not rude) Upendo hauna moyo au roho ya jeuri!! Jeuri hujibu kwa mkato bila heshima, au hutoa majibu au kauli za kuvunjia heshima wengine, jeuri haijali inaongea na nani na yenyewe haizingatii adabu njema wala heshima na staha kwa wengine! Ubinafsi na chuki hauzingatii lile neno: "heshima, kwa wanaostahili heshima"!! Jeuri hujibu kwa hasira na dharau! Upendo haukosi kuwa na adabu!!!: Upendo hauvunjii wengine heshima kwa wazo, neno, au tendo!!
2) MST 5 b: Upendo hautafuti mambo yake!!(Love is not self-seeking) Hii ni kusema upendo hauna ubinafsi!! Yaani, upendo unatanguliza na kutafuta maslahi, matakwa, faida, manufaa, raha, amani, utoshelevu, mafanikio, ushindi, mema, usalama, afya njema, uponyaji, wokovu, kibali, elimu, maarifa, nafuu, utajiri, kufaidika, NA KILA JEMA LA WENGINE!! Msukumo wa Upendo kwenye maisha ni KUMFAIDIA UNAYEMPENDA! KUMNUFAISHA UNAYEMPENDA! Upendo HAUTAFUTI FAIDA BINAFSI AU MANUFAA BINAFSI! Upendo hauna ubinafsi HATA CHEMBE na unaishi kwa AJILI YA KUWAPA NA KUWATENDEA MEMA WENGINE KATIKA KRISTO YESU!! Na hivi ndivyo upendo unavyoweka hazina mbinguni!! LOVE ALWAYS SPENDS AND IS SPENT FOR THE BENEFIT OF THOSE YOU LOVE!!! Upendo sikuzote unatafuta faida ya mkeo/mumeo/bosi wako/mwajiriwa wako/mfanyakazi mwenzako/mwanachuo mwenzako/mwanafunzi mwenzako/jirani yako/mteja wako/anayekuuzia/unayemuuzia/anayekuhudumia/unayemhudumia, n.k. Upendo hautafuti mambo yake!
24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.
1 Wakorintho 10:24
3) MST 5c Upendo hauoni uchungu!(Love is not easily angered): Upendo hauna hasira za haraka!! Upendo hauhifadhi hasira moyoni kama uchungu maana hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu kama uchungu ( Mhu 7:9) Upendo mwenyewe (Mungu) SI MWEPESI WA HASIRA!! (Kut 34:6, Zab 145:8), na ameagiza TUWE WEPESI WA KUSIKIA, LAKINI SI WEPESI WA KUSEMA WALA KUKASIRIKA (Yak 1:19)! Uchungu ni kichocheo cha ugomvi na faraka! Upendo hujenga, na kulinda, na kuimarisha mahusiano! Upendo hauoni uchungu! Uchungu ni chuki! Uchungu ni uadui! Uchungu ni mauti! Uchungu ni uovu! Upendo hauoni uchungu BALI UMEJAA HURUMA, REHEMA, NA MATENDO MEMA!!
31 Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Waefeso 4:31
32 tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Waefeso 4:32
4) MST 5d Upendo hauhesabu mabaya (Love keeps no record of wrongs): Upendo hauweki moyoni na akilini kumbukumbu ya mabaya uliyotendewa!! Upendo husamehe maovu/dhambi/uasi/makosa/na udhalimu WOTE, na kisha huyaachilia yatoke moyoni na akilini, na mwishowe kumbukumbu zote kufutika kabisa! Hii ni kwa sababu Upendo (Mungu) mwenyewe ndiye mwanzilishi wa kufanya hivyo KWETU TULIOLIAMINI NA KULIPOKEA PENDO LAKE!
“16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo,”
Waebrania 10:16
“17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.” (Waebrania 10:17)
>> UPENDO MWENYEWE ANASEMA DHAMBI ZETU NA UASI WETU HAUKUMBUKI TENA KABISA
>> HILI NI AGANO LA UPENDO!!! KUSAMEHE, KUACHILIA, NA KUSAHAU!!
>> KAMA UNA UPENDO WA KRISTO MOYONI MWAKO HAUWEZI KUWEKA KUMBUKUMBU YA MABAYA YOYOTE UNAYOTENDEWA MOYONI MWAKO
>> KUTOSAMEHE NDIKO KUNAKUFANYA UKUMBUKE "ALINIFANYIA HILI, AKANIFANYIA LILE, AKARUDIA HILI TENA, ANAFANYA MAKUSUDI HUYU, SIKUZOTE NDIYO TABIA YAKE HII!!"
>> WENGI WAMEBEBA CHUKI MIOYONI MWAO KWA SABABU WAMEJAZA KUMBUKUMBU ZA MABAYA WALIYOFANYIWA! CHUKI IMEATHIRI MAHUSIANO YAO NA WATU WENGINE KWA KIASI KIKUBWA! ZILE KUMBUKUMBU MBAYA ZA MABAYA ZIMEATHIRI MITIZAMO YAO, MISIMAMO YAO, MAONGEZI YAO, MATARAJIO YAO, N.K. WAMESHAWAHUKUMU WATU WALE WANAODHANI AU KUAMINI KUWA WALIWATENDEA MABAYA! WAMEWALAUMU, WAMEWAKOSOA, WAMEWALAUMU, NA WAMEWANYOOSHEA VIDOLE!! HAWAWEZI KUWA NA UPENDO HAWA, MAANA MIOYO YAO IMEJAA UCHUNGU NA KUTOSAMEHE! HII SIYO TU IMEATHIRI UHUSIANO NA HAO, BALI PIA INAENDELEA KUATHIRI MAHUSIANO YAO MENGINE YA SASA! WAMEFUNGWA NA JANA YAO (PRISONERS OF PAINFUL PAST)!!! LAKINI UPENDO HAUHESABU MABAYA!
>> Kutosamehe ni kuhifadhi uchungu moyoni na kumbukumbu ya mabaya! Kuhesabu mabaya ni kuhuisha maumivu na uchungu ulionao moyoni dhidi ya huyo unayemchukia!! Upendo hauhesabu mabaya!! Kama unahesabu mabaya uliyotendewa HUNA UPENDO, HUNA YESU, HUNA MUNGU, NA HUJAOKOKA, BADO UKO GIZANI!!! TUBU USAMEHEWE NA KUSAFISHWA MOYO WAKO KWA DAMU YA YESU NA KUTAKASWA KWA NENO LAKE!
>> HAKUNA MWENYE UCHUNGU ANAYEHESABU MABAYA ATAKAYEINGIA MBINGUNI AU ATAKAYEMWONA MUNGU!!!
TABIA/SIFA ZA UPENDO-2
1 Corinthians (Wakorintho) 13:6
“[6]Rejoiceth not in iniquity, but rejoiceth in the truth;
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;”
>> UPENDO HAUFURAHII UDHALIMU BALI HUFURAHI PAMOJA NA KWELI
Hii ni kwa sababu asili ya Upendo ni UTAKATIFU! ( love is holy and pure!!) Upendo uko mbali kabisa na uovu! Upendo hauridhii uovu!! Upendo hauruhusu uovu! Upendo hauhalalishi uovu! Upendo haufumbii macho uovu! Upendo haujiepushi kukemea uovu! Ukiwa na Upendo wa Kristo ndani yako UTAISHI MAISHA MATAKATIFU! Hakuna aliye na Upendo wa Mungu ndani ya moyo wake HALAFU AKAWA NI MTENDA DHAMBI!! Upendo unaishi sawasawa na Kweli! Upendo unaitenda Kweli! Upendo hauwezi kutenda lolote kinyume na Kweli!!
“8 Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.”
2 Wakorintho 13:8
[ LOVE IS ALWAYS FOR THE TRUTH!! UPENDO SIKUZOTE UPO UPANDE WA KWELI!!]
Upendo wa Mungu unaanzia hapa:
John (Yohana) 14:23-24
[23] Jesus answered and said unto him, If a man love me, he will keep my words: and my Father will love him, and we will come unto him, and make our abode with him.
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
[24] He that loveth me not keepeth not my sayings: and the word which ye hear is not mine, but the Father's which sent me.
Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.
>> UKIMPENDA YESU UTALISHIKA, UTALITENDA, NA KULIISHI NENO LAKE!!
>> UKIMCHUKIA YESU HUWEZI KULISHIKA, KULITENDA, NA KULIISHI NENO LAKE!!!
>> NENO LAKE NDIYO KWELI!!
>>WANAOMCHUKIA MUNGU, HAWALIPENDI NENO LAKE!! HAWALIFURAHII NENO LAKE!! HAWALISTAHIMILI NENO LAKE!! HAWALITAKI NENO LAKE! NENO LAKE LINAWAKERA!! HAWALIHESHIMU NENO LAKE! WANACHUKIA NENO LAKE LINAPOWAKEMEA NA KUFUNUA UOVU WAO!! HAWA NI WABINAFSI WENYE KIBURI, UBISHI, UKAIDI, JEURI, DHARAU, MAJIVUNO, HASIRA NA GHADHABU, UCHUNGU, UGOMVI, UADUI, NA NI WATU WASIOPENDA WALA WASIOTAKA KUKEMEWA AU KUAMBIWA KWELI!! HAWAMPENDI MUNGU WALA WANADAMU!! NI WAOVU WASIOMCHA MUNGU! HAWANA UPENDO! HAWANA MUNGU! HAWANA YESU! UHUSIANO WA MWENYE UPENDO, NA NENO (KWELI), NI KAMA TAWI NA MTI, AU JICHO NA MBONI! MWENYE UPENDO NI MMOJA NA KWELI (ONE WITH THE TRUTH)! Upendo haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na Kweli!!
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
1 Wakorintho 13:7
1) MST 7a Upendo huvumilia yote!! UKIWA NA UPENDO MOYONI MWAKO, UTAVUMILIA YOTE!! Biblia haikusema, huvumilia BAADHI ya mambo, BALI HUVUMILIA YOTE!! Hivyo unapokuwa umechoka au umeshindwa kumvumilia yeyote au kuvumilia lolote maana yake UPENDO WAKO UMEKOMA!! MUNGU NI UPENDO (1 Yoh 4:8) Kuwa na Upendo moyoni mwako ni kuwa na Mungu!! Uvumilivu wa Upendo ndani yako HAUWEZI KUSHINDWA KUVUMILIA CHOCHOTE AU LOLOTE!! Isitoshe Uvumilivu unatiwa nguvu na tumaini!! Imeandikwa "tumaini halitahayarishi kwa maana pendo la Mungu limekwishamiminwa mioyoni mwetu na huyo Roho tuliyepewa" (Rum 5:5) Upendo unavumilia yote kwa sababu ya tumaini imara lililopo!
11 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho;
Waebrania 6:11
12 ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.
Waebrania 6:12
>> UKIWA NA UTIMILIFU WA MATUMAINI UTAVUMILIA MPAKA MWISHO!!! Upendo huvumilia yote!!!
2) MST 7b Upendo huamini yote! Imani hutenda kazi kwa Upendo (Gal 5:6)! Upendo ndio nguvu ya Imani! Pasipo Upendo Imani haitendi kazi!! Upendo huamini yote! Upendo ukiwemo ndani yako utaamini yote, sikuzote! Imani yako itakwenda pamoja na uvumilivu wa Upendo huku ukiwa na utimilifu wa matumaini hadi mwisho! IMANI YA NAMNA HII HAIWEZI KUSHINDWA!! Maana nguvu yake ni Upendo, na hivyo Upendo HUAMINI YOTE!
3) MST 7c UPENDO HUTUMAINI YOTE, NA PIA 4) MST 7d UPENDO HUSTAHIMILI YOTE
>> Matumaini ya Upendo na Ustahimilivu wa Upendo HAYAKOMI KAMWE SIKU ZOTE!
>> Yaani, UPENDO HUSTAHIMILI YOTE NA HUTUMAINI YOTE!
>> Kupoteza matumaini kwa aina yoyote ni kumchukia Mungu na mwanadamu!
>>Kushindwa kustahimili kokote ni kumchukia Mungu na wanadamu!
>> Unayempenda utamstahimili!! Unayempenda utakuwa na matumaini naye sikuzote!
>> Nguvu ya kustahimili na kutumaini ni UPENDO!(Mungu)
>> Mwenye Upendo ANA MATUMAINI YOTE na USTAHIMILIVU WOTE, SIKUZOTE!!
SIFA/TABIA ZA UPENDO-MWISHO
1 Corinthians 13:8
[8]Charity never faileth: but whether there be prophecies, they shall fail; whether there be tongues, they shall cease; whether there be knowledge, it shall vanish away.
Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
>> UPENDO HAUSHINDWI KAMWE! UPENDO HAUPUNGUKIWI NENO KAMWE! UPENDO UNAWEZA YOTE! UPENDO HAUPUNGUI NENO KAMWE!
>> VIPAWA, KARAMA, NA UJUZI MWINGINE WOTE VYAWEZA KUKOMA! LAKINI UPENDO UNADUMU MILELE NA LAZIMA UWE NA HAYO YOTE: LAKINI HAYO HUWA YANAKOMA, NA PIA YANAWEZA YASIWE NA UPENDO!
>> maarifa yanaweza yasiwe na upendo, na si ya milele; LAKINI UPENDO NI WA MILELE!
>> KARAMA ZA AINA ZA LUGHA NA TAFSIRI ZA LUGHA, AU UNABII, ZINA KIKOMO, NA PIA ZAWEZA KUTENDA KAZI PASIPO UPENDO, LAKINI UPENDO UNA YOTE!! UPENDO UNA VYOTE!! UPENDO UNADUMU SIKU ZOTE!! UPENDO UNA HEKIMA YOTE, MAARIFA YOTE, UFAHAMU WOTE, KICHO CHOTE, USHAURI WOTE, NGUVU ZOTE, MAFUNUO YOTE, AMANI YOTE, FURAHA YOTE, UVUMILIVU WOTE, UTU WEMA WOTE, FADHILI ZOTE, UAMINIFU WOTE, UPOLE WOTE, KIASI CHOTE, UNYENYEKEVU WOTE, UTUKUFU WOTE, BARAKA ZOTE, HESHIMA YOTE, UWEZA WOTE, UTAJIRI WOTE, NEEMA YOTE, KWELI YOTE, WEMA WOTE, UKARIMU WOTE, HURUMA ZOTE, REHEMA ZOTE, KIBALI CHOTE, ISHARA ZOTE, MIUJIZA YOTE, MAAJABU YOTE, NA MEMA YOTE!!!
>> UPENDO UKIWEMO NDANI YAKO HUWEZI KAMWE KUSHINDWA KWENYE MAHUSIANO, KWENYE KUTATUA, KUEPUSHA, KUOKOA, KUJENGA, KULINDA, KUSHAURI, KUPONYA, KUTIA MOYO, KUFARIJI, KUJENGA, KUIMARISHA, KUJALI, KUTUNZA, KUZINGATIA, KUTHAMINI, KUHUDUMIA, KUTUMIKIA, KUNYENYEKEA, KUJISHUSHA, KUJIDHILI, KUJIKANA, KUSAMEHE, KUVUMILIA, KUFUATILIA, KUFUNDISHA, KUCHUKULIANA, KUSTAHIMILI, KUTUMAINI, KUNGOJEA, KUJITOA, KUTOA, KUTENDA MEMA, KUHESHIMU, KUONGOZA, KUELEKEZA, KUTOSHELEZA, KUSHIBISHA, KUTII, KUNYAMAZA KIMYA, KUJIZUIA, KIASI, KUSHUKURU, KUSIFU, KURIDHIKA, KUTOSHEKA, KUTOJITETEA, KUJIHADHARI, KUOMBA, KUOMBEA, KUTAFAKARI MEMA, NA KILA TENDO AU NENO JEMA UNALOLIWAZA AU UNALOLIJUA AU UNALOLIFIKIRI!!
Upendo haushindwi kamwe! Talaka zinatokana na KUKOSA UPENDO WA MUNGU MOYONI!! YAANI, KUTOKUWA NA MUNGU MOYONI!! TALAKA NI ZAO LA CHUKI NA UBINAFSI!! UPENDO HAUSHINDWI NENO KAMWE!!
12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
(Wakolosai 3: 12-14)
>> UPENDO NDIO KIFUNGO CHA UKAMILIFU
MAOMBI NA BARAKA ZA UPENDO
1) “9 Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; 10 mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; 11 hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.” (Wafilipi 1:9-11)
2) “14 Kwa hiyo nampigia Baba magoti,15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, 16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; 18 ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.” (Waefeso 3:14-19)
3) “12 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; 13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.” (1 Wathesalonike 3:12-13)