LEO YANGU NDANI YA YESU

 Today Show Logo - Today Show Australia Logo, HD Png Download -  3508x2480(#3457810) - PngFind

KILA IITWAPO LEO!! (SIKU ZANGU, MAISHA YANGU NDANI YA YESU)

>> HAYA NI MAISHA YAKO KATIKA ROHO MTAKATIFU NA NENO LAKE! (Wagalatia 5:16,25)
>> HAYA UYAFANYE PIA KUWA NDIYO MALENGO YAKO YA KILA SIKU, MAPENZI YA MOYO WAKO YA KILA SIKU, MATAKWA YA MOYO WAKO YA KILA SIKU, UNAVYOAMINI MOYONI MWAKO KILA SIKU MAANA UNAISHI NA KUENENDA KWA NENO LA MUNGU KILA SIKU, KATIKA ROHO MTAKATIFU!
>> UNATAMKA KWA IMANI, UNAOMBA KWA IMANI, UNATABIRI KWA IMANI, UNAKIRI KWA IMANI, UNAUMBA KWA NENO, UNAUMBA ULIMWENGU WAKO WA ROHO KWA NENO KILA SIKU
Biblia inasema, “2 Roho ya BWANA ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu” (2 Sam 23:2)
>>
Roho Mtakatifu akinena ndani yako Neno lake huwa liko ulimini mwako!! Neno la Mungu unalolitamka kwa imani, huwa linatoka kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Maandiko yananena, “4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai” (Ayu 33:4)
>> Roho ya Mungu iliyokuumba wewe, bado inaumba mapenzi ya Mungu yaliyomo kwenye Neno lake, kupitia kinywa chako wewe mwenyewe, pale unaponena Neno la Mungu kwa imani! Pale unaposema yale uliyoyaamini (2 Kor 4:13)

>> SEMA, KIRI, TAMKA, AMURU, TANGAZA, ILI IWE!!! BADILISHA MAISHA YAKO KWA NENO, PAMOJA NA NENO, KWA NJIA YA NENO! ENDELEA KUSEMA NA KUTAMKA MPAKA IWE BILA KUTAZAMA HALI MBAYA ZA MACHO, AU HALI MBAYA UNAZOAMBIWA, AU TAARIFA MBAYA ZOZOTE KINYUME NA ULIVYOKUSUDIA NA KUAZIMIA! haya yanaitwa malengo, makusudio, na maazimio katika Roho Mtakatifu ndani yake Yesu Kristo Mwana wa Mungu! Lazima uwe umeokoka ili ukiri huu uwe na faida kwako, na Bwana atakupa ufahamu katika mambo yote!


1. Je! leo nitakuwaje baraka kwa mke/mume/baba/mama/rafiki/adui/na watu wote? Nimebarikiwa ili niwe baraka kwa wengine (Mwa 12:1-3 & Efe 1:3)
2. Leo ni siku nyingine ya kuenenda katika upendo wa Mungu kwa watu wote, hususani adui zangu! Ni siku ya kutenda mambo yote kwa upendo wa Roho. ( Lk 6:27:35 & 1 Kor 16:14)
3. Leo ni siku nyingine ya kuyatenda mapenzi ya Mungu yote kila nitakapokwenda au nitakapokuwepo na kamwe kutoifuatisha namna ya dunia hii. (Rum 12:2 & Efe 5:17)
4. Leo ni siku nyingine ya kulitenda neno la Mungu kila nitakapokwenda, na kwa namna hiyo kuyatenda yale yampendezayo yeye wakati wote na mahali pote pale nitakapokuwepo. (Yak 1:22-25)
5. Leo ni siku nyingine ya kupokea kila nitakaloliomba mbele za Mungu, kwa kuwa sikuzote ninalishika Neno lake, Amri zake, na Kuyatenda yale yapendezayo machoni pake. (1 Yoh 3:22)
6.Leo ni siku nyingine ya kuongeza bidii na juhudi katika kutenda mema kwa watu wote, maadui, marafiki, ndugu, wanaonipenda, wasionipenda, wema, wabaya, n.k. maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu Baba yetu wa mbinguni. (Tit 2:14, Gal 6:9, 2 Thes 3:13, & Efe 2:10)
7. Leo ni siku nyingine ya kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza na haki yake kila niendako na katika kila nitakalolifanya kila mahali. (Mt 6:33)
8. Leo ni siku nyingine ya kuyawaza, kuyatafakari, kuyafikiri, na kuyatafuta yale yote yaliyo ya juu mbinguni, ya milele, yasiyoharibika, yaliyoko kule alikoketi Kristo mkono wa kuume wa Baba. (Kol 3:1-4)
9. Leo ni siku nyingine ya kumwona Mungu akitenda yale yote nimwombayo kwa maana ninakaa ndani yake, na maneno yake yanakaa ndani yangu sikuzote. (Yoh 15:7)
10. Leo ni siku nyingine ya kumtukuza Baba wa mbinguni kwa kumzalia sana matunda nikiwa ndani ya Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu. (Yoh 15:8 & Yoh 15:5)
11. Leo ni siku nyingine ya kumzalia Mungu matunda yanayokaa, na hivyo kupokea kutoka kwa Baba yetu wa mbinguni lolote nimwombalo ( Yoh 15:16)
12. Leo ni siku nyingine ya kuenenda kwa Roho Mtakatifu na kutozitimiza kamwe tamaa za mwili. (Gal 5:16) Maana ninaishi kwa Roho na kuenenda kwa Roho (Gal 5:25) na sikuzote ninaongozwa na Roho huyo (Rum 8:14).
13. Leo ni siku nyingine ya kujikana, kujitwika msalaba wangu, na kumfuata Yesu (Mt 16:24-25)
14. Leo ni siku nyingine ya kumpenda jirani yangu kama nafsi yangu (Mt 22:39)
15. Leo ni siku nyingine ya kuangaza mbele za wanadamu wote kwa nuru ya utukufu wa Mungu aliye ndani yangu, kwa watu kuyaona matendo yangu mema, na kumtukuza Mungu kwa ajili ya neema yake aliyonikirimia ya kuyatenda hayo yote na kunifanya kuwa nuru ya ulimwengu na chumvi ya dunia. (Mt 5:14-16)
16. Leo ni siku nyingine ya kuenenda katika pendo halisi la Mungu kwa kuutoa uhai wangu kwa ajili ya ndugu zangu, kama Kristo naye alivyoutoa uhai wake kwa ajili yangu, maana imenipasa kufanya hivyo kama agizo lake lilivyo. (1 Yoh 3:16)
17. Leo ni siku nyingine ya kuidhihirisha kila mahali harufu ya kumjua Yesu Kristo Bwana Mwenyezi kwa kazi zangu; maana mimi ni manukato ya Kristo mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; kwa hao wa kwanza mimi ni harufu ya uzima iletayo uzima, na katika hao wa pili mimi ni harufu ya mauti iletayo mauti. (2 Kor 2:14-16)
18. Leo ni siku nyingine ya kunena, siyo kama wale wanaolighoshi neno la Mungu, bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, na mbele za Mungu, ninanena katika Kristo. (2 Kor 2:17)
19. Leo ni siku nyingine ya kukataa mambo ya aibu yaliyositirika, kutoenenda kwa hila, na kutolichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli najionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikinishuhudia mbele za Mungu. (2 Kor 4:2)
20. Leo ni siku nyingine ya mimi kujisifia ushuhuda wa dhamiri yangu, kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; ninaenenda katika dunia hii, kila mahali niendako sikuzote. (2 Kor 1:12)
21. Leo ni siku nyingine ya kuitumia karama niliyopokea kwa Bwana Yesu kwa ajili ya kuuhudumia mwili wa Kristo kama wakili mwema wa neema ya Mungu niliyopewa; Ninasema kama mausia ya Mungu; Ninahudumu kwa nguvu nilizojaliwa na Mungu; Na Mungu anatukuzwa katika mambo yote kwa Yesu Kristo, utukufu na uweza una yeye hata milele. (1 Pet 4:10-11)
22. Leo ni siku nyingine ya kuweka hazina mbinguni, na siyo hapa duniani, maana huko wevi hawawezi kuvunja wala kuiba, nako hakuharibiki kitu kwa nondo wala kutu, tofauti na ilivyo hapa duniani. Moyo wangu uko kwa Baba juu mbinguni ambako ndiko nyumbani ninakowekeza hazina yangu yote. (Mt 6:19-21)
23. Leo ni siku nyingine ya kuenenda kama mgeni, msafiri, na mpitaji hapa duniani tofauti na wale wanaonia na kuyatafuta mambo ya hapa duniani tu. Maana uraia na uenyeji wangu uko mbinguni ambako kutoka huko namtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo. (Flp 3:18-21 & 1 Pet 2:11)
24. Leo ni siku nyingine ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli kwa maana hii ndiyo ibada halisi na ya kweli anayoitaka Baba yetu wa mbinguni. (Yoh 4:23-24)
25. Leo ni siku nyingine ya kuutoa mwili wangu uwe dhabihu iliyo hai, takatifu, na ya kumpendeza Mungu, maana hivi ndivyo ninavyomwabudu Mungu kwa ibada impendezayo na yenye maana. Nimeyatoa macho yangu na masikio yangu, nimeitoa midomo yangu, nimeitoa ngozi yangu, nimezitoa nywele na kucha zangu, nimeitoa mikono na miguu yangu, na mwili wangu wote dhabihu kwa Mungu, kumpendeza na kumwabudu sikuzote za mwili huu na si kwa ajili ya uchafu na uasi wa namna yoyote. (Rum 6:12-14, 19 & Rum 12:1)
26. Leo ni siku nyingine ya kukaa na mke wangu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisichokuwa na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwangu kusizuiwe. (1 Pet 3:7)
27. Leo ni siku nyingine ya kumtii mume wangu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa changu, kama Kristo naye alivyo kichwa cha Kanisa; naye ni Mwokozi wa mwili. Hivyo leo ni siku nyingine ya kumtii mume wangu katika mambo yote vile vile kama Kanisa linavyomtii Kristo katika mambo yote. (Efe 5:22-24)
28. Leo ni siku nyingine ya kumpenda mke wangu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Kadhalika na mimi leo ni siku ya kumpenda mke wangu kama mwili wangu mwenyewe; ni siku nyingine ya kumlisha na kumtunza mke wangu. (Efe 5: 25-29)
29. Leo ni siku nyingine ya kumtii na kunyenyekea kwa mume wangu kwa mwenendo safi na wa hofu, uliojaa kicho, upole, utulivu, huku nikizidi kuongezeka katika urembo huo wa moyoni, katika matendo mema, adabu nzuri, moyo wa kiasi, heshima kwake na uchaji Mungu, kama walivyojipamba wanawake wa zamani waliowatii waume zao na kumtumaini Mungu. (1 Pet 3:1-6 & 1 Tim 2:9-10)
30. Leo ni siku nyingine tena ya kuwalea watoto wangu katika njia iwapasayo ambayo hawataiacha hata watakapokuwa wazee. (Mith 22:6)
31. Leo ni siku nyingine tena ya kumcha Bwana Mungu wetu Mwenyezi kwa kuzidi kuuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. (Mith 8:13)
32. Leo ni siku nyingine tena ya kuenenda katika hekima na ufahamu wa Mungu; kwa maana Kumcha Bwana NDIYO HEKIMA, na kujitenga na uovu NDIYO UFAHAMU. Leo ni siku nyingine ya kumcha Mungu na kujitenga na uovu. (Ayu 28:28)
33. Leo ni siku nyingine ya kutenda haki, kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wangu ndani yake Kristo Yesu Bwana. (Mik 6:8)
34. Leo ni siku nyingine ya kulijaza neno la Mungu moyoni mwangu ili nisije nikamtenda Mungu dhambi. (Zab 119:11 & Kol 3:16)
35. Leo ni siku nyingine ya kuimarisha na kudumisha urafiki wangu na Yesu kwa kuyatenda yote anayoniamuru. (Yoh 15:14-15)
36. Leo ni siku nyingine ya kuendelea kuomba pasipo kukoma wala kukata tamaa na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. ( Lk 18:1-8 & 1 Thes 5:17-18)
37. Leo ni siku nyingine ya kukataa kulipa baya kwa baya; na badala yake kulipa jema au mema kwa mabaya yote niliyotendewa na nitakayotendewa na hivyo kuushinda ubaya kwa wema. (1 Thes 5: 15, Mith 17:13 & Rum 12:19-21)
38. Leo ni siku nyingine ya kujitakasa na kujiepusha na uasherati kwa kuudhibiti na kuutawala mwili wangu katika hali ya utakatifu na heshima; na wala si katika hali ya tamaa mbaya kama mataifa wasiomjua Mungu. (1 Thes 4:4-5)
39. Leo ni siku nyingine ya kujitakasa kwa kuitii Kweli hata kufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki; basi leo ni siku ya kujitahidi kuwapenda ndugu kwa moyo wangu wote. (1 Pet 1:22)
40. Leo ni siku nyingine ya kuwa barua kwa wote wanionao kila nitakapokwenda; barua ya Kristo kwao iliyoandikwa moyoni mwangu na Roho Mtakatifu; ambayo inajulikana na kusomwa na watu wote kila mahali kupitia maneno na matendo yangu maishani mwangu. (2 Kor 3:2-3)
41. Leo ni siku nyingine ya kuzidi kumpendeza Mungu kwa kuenenda kwa imani, na wala si kwa kuona, maana najua hakika kwamba Mungu yupo naye huwapa thawabu wale wamwendeao. (Ebr 11:6 & 2 Kor 5:7)
42. Leo ni siku nyingine ya kuzidi kutulia na kutenda shughuli zangu, na kufanya kazi, kwa mikono yangu mwenyewe kama neno lilivyoagiza; ili nienende kwa adabu mbele yao walio nje kwa kutokuwa na haja ya kitu chochote. (kutokuwa mhitaji) {1 Thes 4:11-12)
43. Leo ni siku nyingine ya kufanya juhudi, na kutenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yangu mwenyewe, ili nipate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji (kutoa) {Efe 4:28}
44. Leo ni siku nyingine ya kuwa mwepesi wa kusikia, lakini si mwepesi wa kusema wala kukasirika. (Yak 1:19)
45. Leo ni siku nyingine ya kuutesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. (1 Kor 9:27)
46. Leo ni siku nyingine ya kuvipiga vita vilivyo vizuri vya imani, katika mwendo wangu wa wokovu, nikiishindania sana na kuilinda imani hii tuliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. (2 Tim 4:7 & Yud 1: 3)
47. Leo ni siku nyingine ya kuzidi kuwa hodari katika Bwana na uweza wa nguvu zake; na ya kuzivaa silaha zote za Mungu, ili nipate kuweza kuzipinga hila za shetani. (Efe 6:10-11)
48. Leo ni siku nyingine ya kumtii Mungu kwenye mambo yote na kwa namna hiyo kumpinga shetani, na kumfanya anikimbie. (Yak 4:7)
49. Leo ni siku nyingine ya kuenenda katika mamlaka niliyopewa ya kukanyaga nyoka na ng’e, na nguvu zote za yule adui, na wala hakuna kinachowez kunidhuru. (Lk 10:19)
50. Leo ni siku nyingine ya kutafuta kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hakuna atakayemwona Bwana asipokuwa nao. (Ebr 12:14)
51. Leo ni siku nyingine tena ya kujilinda na yule mwovu kutonigusa kwa namna yoyote, maana nimezaliwa na Mungu na wala sitendi dhambi. (1 Yoh 5:18)
52. Leo ni siku nyingine ya wewe...........................!
53 Leo ni siku nyingine ya wewe..............................!

100. Leo ni siku nyingine tena ya kutotenda neno lolote au jambo lolote kinyume na kweli bali kwa ajili ya kweli; maana siwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli. (2 Kor 13:8)



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post