KUOKOKA NI UUMBAJI MPYA NDANI YAKO
SEHEMU YA KWANZA-UTANGULIZI
Biblia inasema kuhusu Yesu kwamba,
“Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” (Lk 19:10)
>> Bwana wetuYesu alikuja KUTAFUTA NA KUOKOA kile kilichopotea!
Wanadamu wote walianguka dhambini katika Adamu,
“Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi…………….” (Rum 5:19)
Maandiko yanasema mshahara wa dhambi ni mauti (Rum 6:23) na hivyo katika Adamu wote tulitenda dhambi na kufa kiroho na kisha kimwili pia baadae! (1 Kor 15: 21-22). Isaya naye anasema,
“Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe……”
(Isa 53:6)
>>Wote tulipotelea kila mmoja kwenye njia yake mwenyewe! Huyu amepotelea kwenye dhehebu hili, huyu dhehebu lile, yule dini ile, na hawa dini hii, n.k. Kila mmoja anajaribu kumtafuta Mungu kwa kupitia njia yake mwenyewe ingawa hawezi kamwe kumpata maana dhambi imemfarakanisha mwanadamu na Mungu na wala hataki kusikia maombi ya mwenye dhambi!
“Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia” (Isa 59:1-2)
Mungu aliamua kumtuma Mwanawe pekee ulimwenguni ili aje kuwaokoa wanadamu waliopotea dhambini hapa duniani, ambao katika hao hapana mmoja wao awezaye kuwaokoa! Akaleta neno lake ambalo ukiliamini unaokolewa kutoka dhambini.
“Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.” (Yoh 5:34)
Yesu ni Neno la Mungu Aliye Hai Kutoka mbinguni kwa Baba (Yoh 1:1, 14) na kila amwaminiye ANAOKOKA kutoka dhambini kwa neema yake.
-Yesu ndiye kuhani wa milele aliyefanya upatanisho wa dhambi za wanadamu wote kwa mauti na damu yake aliyoimwaga msalabani kwa ajili ya watenda dhambi wote ( Ebr 7:21-26, 2 Kor 5:18-20)
“Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.” (Rum 5:6-11)
>>Yesu alikamilisha ukombozi wa mwanadamu kwa kuutoa uhai wake msalabani ili watu wale waliokuwa wafu kwa sababu ya dhambi wawe hai kwa sababu ya haki kupitia imani yao katika damu yake!
“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.” (1 Pet 2:24-25)
>>Ukombozi wa mwanadamu kutoka dhambini umekamilika msalabani nao unapokelewa kwa imani tu na si kwa matendo!!!
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” (Efe 2:8-9)
>>>NEEMA YA MUNGU NDIYO INAYOOKOA KWA NJIA YA IMANI KWA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU
“Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata WOKOVU.” (Rum 10:8-10)
>>HAKUNA JINA JINGINE CHINI YA MBINGU LINALOWEZA KUOKOA ISIPOKUWA “YESU” NA WALA HAKUNA MWINGINE AWEZAYE KUOKOA
“jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama hali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. WALA HAKUNA WOKOVU KATIKA MWINGINE AWAYE YOTE, KWA MAANA HAPANA JINA JINGINE CHINI YA MBINGU WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO.”
(Matendo 4:10-12)
>>>KUOKOKA NI KWA NJIA YA KUMWAMINI YESU KRISTO PEKE YAKE, KWA KUMPOKEA MOYONI MWAKO KAMA BWANA NA MWOKOZI, NA KUISHI UKILIITIA JINA LAKE KATIKA UTAKATIFU, HAKI, NA KWELI.
“kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka” (Rum 10:13)
SEHEMU YA PILI: UUMBAJI MPYA
Biblia inasema,
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya” (2 Kor 5:17)
>>MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA!
>>YA KALE YAMEPITA TAZAMA! YAMEKUWA MAPYA!
New
King James Version
“Therefore, if anyone is in
Christ, he is a new creation;
old things have passed away; behold, all things have become new.” (2 Cor 5:17)
New American Standard Bible
“Therefore if anyone is in Christ, this
person is a new creation; the old things passed away; behold, new things
have come.” (2 Cor 5:17)
>>MTU YEYOTE AKIWA NDANI YA KRISTO, AMEKUWA UUMBAJI MPYA; MAMBO YA KALE YAMEPITA; TAZAMA, MAMBO YOTE YAMEKUWA MAPYA
Hii maana yake mtu huyu ameumbwa upya!!! Kumbuka mtu ni roho, ana nafsi, na anaishi ndani ya mwili. Nabii Ezekiel alitabiri kuhusu huu uumbaji mpya namna hii:
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” (Eze 36:25-27)
>> UUMBAJI MPYA HUU UNATOKEA KWA KUSAFISHWA MOYO WAKO PALE UNAPOMWAMINI YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO
“wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.” (Mdo 15:9)
>> KULE KUSAFISHWA MOYO KWA IMANI NDIKO KUZALIWA MARA YA PILI KWA MAJI NA NA KWA ROHO (Yoh 3:5)
>> MAJI YANAYOSEMWA HAPA NI MAJI YA NENO LA MUNGU
“kama Kristo naye ALIVYOLIPENDA KANISA, AKAJITOA KWA AJILI YAKE; ILI MAKUSUDI ALITAKASE NA KULISAFISHA KWA MAJI KATIKA NENO; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” (Efe 5:25-27)
>> Uumbaji mpya huu unasafisha moyo na kuutakasa ili uwe safi, usio na mawaa, ila, kunyanzi, uovu, ubaya, dhambi, au lolote kama hayo!! Mtu huyu anafanywa upya kuwa mtakatifu mwana wa Mungu aliyezaliwa upya! (born again)
>> Ezekiel anasema “nitawatakaseni na uchafu wenu wote na vinyago vyenu vyote (sanamu zenu zote)!”
>>Kinachofanyika siyo tu usafi wa moyo uliochafuka bali Ezekieli anasema, “nami nitawapa ninyi moyo mpya!” Yaani, Mungu anaweka ndani yake aliyemwamini Yesu MOYO MPYA! Kabla ya kutia moyo mpya kwanza anautoa ‘moyo wa jiwe’ uliomo ndani ya huyu asiyeamini! Na kisha moyo mpya anaoutia ndani yake ni ‘moyo wa nyama.’
1) Moyo wa jiwe haumwamini Mungu wakati moyo wa nyama unamwamini Mungu.
2) Moyo wa jiwe haumtaki Mungu kabisa wakati moyo wa nyama unamtaka sana Mungu.
3) Moyo wa jiwe hauna toba ndani yake wakati moyo wa nyama una toba ndani yake.
4) Moyo wa jiwe haumtegemei Mungu kamwe wakati moyo wa nyama unamtegemea Mungu kabisa sikuzote.
5) Moyo wa jiwe umejaa uchafu na vinyago wakati moyo wa nyama umejaa utakatifu wa Mungu.
6) Moyo wa jiwe hauna Mungu ndani yake wakati moyo wa jiwe una Mungu ndani yake.
7) Moyo wa jiwe hauna neno la Mungu wakati moyo wa nyama umejaa neno la Mungu ndani yake.
8) Moyo wa jiwe umejaa chuki na visasi wakati moyo wakati moyo wa nyama umejaa upendo na kusamehe.
9) Moyo wa jiwe hauna hofu ya Mungu wakati moyo wa nyama umejaa hofu ya Mungu.
10) Moyo wa jiwe hauwezi kumpendeza Mungu wakati moyo wa nyama unampendeza Mungu sikuzote.
11) Moyo wa jiwe hauwezi kumtii Mungu wakati moyo wa nyama unampenda na unamtii Mungu sikuzote..
Ezekieli anasema kuhusu uumbaji mpya kuwa,
“nami nitatia roho mpya ndani yenu.” …………………(1)
“ nami nitatia roho yangu ndani yenu…………………...(2)
>> roho mpya hapa ni roho ya mwamini iliyofanywa upya!!
“Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, ALITUOKOA; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.” (Tito 3:4-7)
English
Standard Version(Tit
3:5)
he saved us, not because of works done by us in righteousness, but according to
his own mercy, by the washing of regeneration and renewal of the Holy Spirit,
Berean Study Bible (Tit 3:5)
He saved us, not by the righteous deeds we had done, but according to His
mercy, through the washing of new birth and renewal by the Holy Spirit.
Berean Literal Bible (Tit 3:5)
He saved us, not by works in righteousness that we did, but according to His
mercy, through the washing of
regeneration and renewing of the
Holy Spirit,
>>Mungu alituokoa kwa kuoshwa KWA KUZALIWA MARA YA PILI na KUFANYWA UPYA NA ROHO MTAKATIFU.
>>Uumbaji mpya ni kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu pale tunapookoka! Sisi ambao ni roho wenye nafsi ndani ya mwili “ tunaumbwa au kufanywa upya na kuhuishwa roho zetu”!! Hivyo kwanza tunapewa roho mpya iliyofanywa upya na kuhuishwa!
>>Kisha Mungu anatupa Roho wake ( “nitatia roho yangu ndani yenu”) kwenye ubatizo wa Roho Mtakatifu ambapo TUNAUNGWA NA BWANA YESU na kuwa roho moja naye (one spirit with the Lord Jesus) [1 Kor 6:17] Yaani,
>>roho mpya ya mwamini + Roho wa Kristo Yesu = Kiumbe Mpya Ndani ya Kristo (2 Kor 5:17)
>>ALIYEOKOKA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI KIUMBE MPYA KABISA AMBAYE HAKUWAHI KUWEPO ULIMWENGUNI!!! Kumbuka mtu ni roho ana nafsi na anaishi kwenye mwili wa nyama. Amezaliwa mara ya pili kwa neno la Mungu (1Pet 1:23)
“Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.” (1Pet 1:23)
>>KUOKOKA NI KUZALIWA MARA YA PILI KWA MBEGU ISIYO YA KIBINADAMU, BALI MBEGU YA MUNGU ISIYOHARIBIKA, AMBAYO NI NENO LA MUNGU!
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yoh 1:12-13)
>> WALIOOKOKA WAMEZALIWA MARA YA PILI NA MUNGU MWENYEWE!! WAMEZALIWA KWA MBEGU YA NENO LAKE!!! MBEGU ISIYOHARIBIKA INAYODUMU HATA MILELE!
Hili ni la muhimu sana kulielewa maana wengi hupotosha ukweli muhimu huu kuhusu UZAO MPYA WA ALIYEOKOKA! Hakuna uhusiano wowote katika roho kati ya aliyeokoka na familia yake ya kimwili na ukoo wake wa kimwili!! Uhalali wa shetani kumtawala mwanadamu na kumtumikisha kwenye dhambi unakufa na kupoteza nguvu kwa kuwa huyu ni mtu mpya mwenye asili mpya kutoka mbinguni! Biblia inasema,
“Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha” (1 Kor 15:45)
>>ADAMU AKAWA NAFSI HAI LAKINI YESU NI ROHO YENYE KUHUISHA (Life-giving Spirit or Spirit of Life)
>>Tumezaliwa mara ya pili kiroho kwa kufufuliwa kutoka mautini kiroho na kupewa uzima wa milele! Hakuna uhusiano wa zamani na sasa katika roho! Aliyeokoka ni uumbaji mpya! Hawezi kuhusishwa katika roho na familia yake na ukoo wake wa kimwili! Anayesema aliyeokoka anaweza kuwa na roho za laana au roho sijui za mababu ni shetani peke yake aliyepondwa kichwa na Yesu!! Huyu haelewi kabisa mambo ya roho yanavyotenda kazi! Biblia iko wazi,
“Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni” (1 Kor 15:48)
>>WASIOOKOKA WANA SURA YA ADAMU NA WANAWEZA KUWA NA LAANA ZOTE ZA UKOO NA MABABU KWA KUWA MUNGU ALISEMA ANAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO HADI KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WAMCHUKIAO ( Kut 20:5)
>>WALIOOKOKA WANA SURA YA YESU NA HAWAWEZI KAMWE KUWA NA LAANA YOYOTE BALI WANA BARAKA ZOTE ZA ROHONI NDANI YA KRISTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (Efe 1:3)
>>KUMTANGAZIA ALIYEOKOKA LAANA NI INJILI YA NAMNA NYINGINE NA AMELAANIWA YEYOTE ANAYEHUBIRI AU KUFUNDISHA HIVYO KWA MUJIBU WA MAANDIKO
“Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.” (Gal 1:8-9)
Biblia inasema,
“Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.” (1Kor 15:49)
>>TULIKUWA NA SURA (IMAGE)YA YULE WA UDONGO AMBAYO NDIYO SURA INAYOWEZA KUWA CHINI YA LAANA
>>LAKINI SASA, BAADA YA KUOKOKA, TUNA SURA (IMAGE) YA YULE WA MBINGUNI AMBAYO NI YA BARAKA, REHEMA, NA NEEMA YA MUNGU
Ukoo wetu na familia yetu asili yake na chanzo chake ni mbinguni sasa. Asili yetu ni mpya ya mbinguni. Biblia inasema,
“Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.” (Efe 2:19-22)
>>SISI SASA NI WA FAMILIA NA UKOO WA WATAKATIFU WALIOBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU
>>FAMILIA NA UKOO WETU VIMEJENGWA JUU YA MSINGI WA MITUME NA MANABII, NA YESU KRISTO NDIYE JIWE KUU LA PEMBENI
>>KATIKA KRISTO YESU SISI KANISA LOTE TUNAUNGAMANISHWA NA KUKUA HATA TUWE HEKALU TAKATIFU KATIKA BWANA
>>KATIKA KRISTO SISI SOTE TUNAJENGWA PAMOJA KUWA MASKANI YA MUNGU KATIKA ROHO
>>MUNGU HAWEZI KULAANI MAKAZI YAKE MWENYEWE KATIKA ROHO
>>SISI TUMEUNGANIKA NA MUNGU KATIKA ROHO KWA NJIA YA YESU NA LAANA HAIPO BALI BARAKA TELE
Kwenye Waebrania imeandikwa,
“Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili” (Ebr 12:22-24)
>> SISI NI RAIA WA SAYUNI, MJI WA MUNGU ALIYE HAI (NDIKO TUNAKOISHI KATIKA ROHO)
>>KWETU NI YERUSALEMU WA MBINGUNI, YAANI, HUKU NDIKO ASILI NA CHIMBUKO LETU KIROHO
>>KWETU TUNAISHI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO PAMOJA NA MAJESHI YA MALAIKA YASIYOHESABIKA AMBAO WOTE HAO NI ROHO WATUMIKAO KUTUHUDUMIA KWA NENO, KATIKA NENO, NA KWA AJILI YA NENO (Ebr 1:14 & Zab 103:20)
>> FAMILIA YETU KUNA MKUTANO MKUBWA SANA NA KANISA LA WAZALIWA WA KWANZA WALIOANDIKWA MBINGUNI (WALIOTANGULIA KWANZA MBINGUNI)
>>TUNAISHI NDANI YA NA PAMOJA NA MUNGU MWAMUZI (JUDGE) WA WATU WOTE
>>PAMOJA NA ROHO ZA WENYE HAKI WAKAMILIFU WALIOANDIKWA MBINGUNI
>>TUKO NA YESU MJUMBE WA AGANO JIPYA AMBAYE NI KAKA YETUMZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU
>>TUKO NA DAMU YA YESU AMBAYO HATA SASA INANEMA MEMA KWA AJILI YETU TULIOOKOKA NA NDIYO ILIYOTUUNGANISHA NA UKOO MZIMA NA FAMILIA NZIMA YA WATAKATIFU WALIOPO HAPA NA KULE JUU!! FAMILIA NA UKOO WETU HAUJAWAHI KUWA NA LAANA MAANA ASILI YETU NI BARAKA, CHANZO CHETU NI BARAKA, KUISHI KWETU NI BARAKA, KUENENDA KWETU NI BARAKA, KUTENDA KWETU NI BARAKA, NA HATA MAUTI YA MWILI WETU NI BARAKA!! TUNAISHI KATIKA UTUKUFU NA UUNGU WA MUNGU WA UTUKUFU KWA ROHO WA UTUKUFU AKAAYE NDANI YETU
HII NDIYO FAMILIA YETU MPYA NA HUU NDIO UKOO WETU MPYA SISI TULIOUMBWA UPYA NDANI YA YESU, AMBAO HATUNA UHUSIANO WOWOTE NA FAMILIA NA KOO ZA KIDUNIA KATIKA ROHO!
>>TUKO HURU MBALI NA LAANA NA DHAMBI ZOTE NA MAGONJWA NA UOVU NA UBAYA WOTE!!!
>>SISI TUMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE NA TUNA UTAJIRI WOTE!!!
>>TUNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU KWA NJIA YA IMANI YETU KWA YESU!!! (1 Petro 1:5)
>>SISI NI WATU AMBAO TUMEZALIWA MARA YA PILI!!!
Hii maana yake kule kuzaliwa kwa jinsi ya mwili kulikotokana na Baba na mama zetu hakuna tena nguvu wala uhusiano na HUKU KUZALIWA MARA YA PILI NA BABA YETU WA MBINGUNI! Wazazi wetu kwa jinsi ya mwili walituzaa kutoka chini (born from below), na Baba yetu wa mbinguni ametuzaa kutoka juu (we are born from above)
Kama vile Yesu asivyokuwa na Baba wa kimwili mwanadamu na sisi tuliookoka hatuna baba mwanadamu! Baba yetu ni Roho (Yoh 4:24) na hivyo ukisema laana unamaanisha Mungu ambaye ni Roho ameturithisha laana katika roho badala ya Baraka! Je! Huko siyo kumtukana Mungu? Je! Hili fundisho siyo la kuzimu na linaloukana msalaba wa Yesu, na kuikana kazi iliyokamilika ya msalaba ya Yesu? Je! Hili fundisho halikukusudia kuikana imani na kulipotosha neno la Mungu? Hili ni fundisho la nyoka wa zamani aliyemdanganya Hawa bustanini Edeni!!!
ATUKUZWE MUNGU BABA WA BWANA WETU YESU KRISTO ALIYETUBARIKI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI NDANI YAKE KRISTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (Efe 1:3)
>> Baraka ya utakatifu, baraka ya uungu, baraka ya nguvu za Mungu, baraka ya utukufu wa Mungu, baraka ya usafi wa moyo, baraka ya moyo unaoamini, baraka ya uzima tele, baraka ya uzima wa milele, baraka ya nguvu za Mungu ndani yetu, kwa ajili yetu, na kupitia sisi kwa ulimwengu, baraka ya neema tele, baraka ya ulinzi wa Mungu kwa nguvu zake, baraka ya kufundishwa na Roho Mtakatifu, baraka ya Roho Mtakatifu, baraka ya utauwa, baraka ya utii wa kweli, baraka ya unyenyekevu, baraka ya hofu ya Mungu, baraka ya ufahamu wa rohoni, baraka ya maarifa ya rohoni, baraka ya hekima ya Mungu, baraka ya ufunuo wa rohoni, baraka ya ukuaji kiroho, baraka ya uongozi wa Roho Mtakatifu, baraka ya kufanywa wana, baraka ya rehema za Mungu, baraka ya utoaji, baraka ya kuushinda ulimwengu, baraka ya kumiliki katika roho, baraka ya kutawala katika roho, baraka ya uzazi kiroho na kimwili, baraka ya kutiisha nchi, baraka ya ongezeko la kiroho, baraka ya ushirika na Mungu………BARAKA ZOTE!!
>>Mtu anayeishi kwa imani huwezi kumhukumu kwa hukumu ya macho wakati wowote kwa maana hujui amemwamini Mungu vipi na kwa mambo yapi na anamgojea Mungu kwenye mambo yapi, na anamtarajia Mungu kwenye mambo na maeneo yapi, na Mungu ana makusudi gani kwake, na anampeleka wapi, na sasa amefikia wapi kwenye kutembea kwake na Mungu n.k
>> Mtu wa rohoni hauwezi kumhukumu kwa macho au masikio! Anapitia umaskini lakini yeye ni tajiri sana, ni kana kwamba hana lakini ana vyote, ni kana kwamba hawezi lakini anaweza yote, ni kana kwamba hajui lakini anajua yote, ni kana kwamba mnyonge kumbe ana nguvu zote, n.k.
>>Mungu hahukumu kwa kumuangalia mtu kwa nje vile alivyo na anavyoonekana kwa macho sasa!!!
“Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake, kwa maana mimi nimemkataa.BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA HUUTAZAMA MOYO.” (1 Sam 16:7)
>>BIBLIA INAPOSEMA MOYO INAMAANISHA roho ya mwanadamu NA SIYOMOYO KIUNGO KINACHOSUKUMA DAMU KUZUNGUKA MWILINI.
>>NDANI YA MOYO KUNA ROHO AMBAYO INAMTAMBULISHA MTU!!!
Mkristo aliyeokoka moyo wake una Roho wa Mungu aliyeuumba upya na pia kujaa ndani yake kwenye ubatizo wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha kila “roho ya andiko” ambayo ndiyo inayohuisha (inayotia uzima/which gives life)
“Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2 Kor 3:6)
>>Uzima/maisha hayako kwenye neno la msamaha bali roho ya msamaha, siyo kwenye neno la utoaji bali roho ya utoaji, siyo kwenye neno la maombi bali roho ya maombi, siyo kwenye neno la uimbaji bali roho ya uimbaji, siyo kwenye neno la sifa bali roho ya sifa, siyo kwenye neno la utakaso bali roho ya utakaso, siyo kwenye neno la ukarimu bali roho ya ukarimu, siyo kwenye neno la kufundisha bali roho ya ufundishaji, siyo kwenye neno la imani bali roho ya imani………UZIMA HAUKO KWENYE ANDIKO BALI KWENYE ROHO YA ANDIKO!
>> Roho Mtakatifu ni Roho wa Andiko ama Roho wa Neno, na unapojazwa Roho lengo la Mungu ni kukupa uzima/uhai/maisha yaliyomo kwenye kila andiko!
“Ndani yake (Neno) ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.” (Yoh 1:4)
>>Neno uliloliamini huwa linakaa moyoni kama roho, na hiyo roho ndiyo inayohuisha au kutia uzima (Yoh 6:63)
Pasipo Roho Mtakatifu yote uyafanyayo kwa jina la Mungu ni “dead works” (matendo mafu)! Hivyo kuna wanaoomba lakini hawaombi (mbele za Mungu), kuna wanaotoa lakini hawatoi (mbele za Mungu), kuna wanaofundisha lakini hawafundishi (mbele za Mungu), kuna wanaohubiri lakini hawahubiri (mbele za Mungu), kuna wanaotabiri lakini hawatabiri mbele za Mungu, n.k KWA NINI? Kwa sababu hawakufanya hayo yote kwa Roho Mtakatifu. Hizi ndizo kazi zitakazoteketea siku ile. (1 Kor 3:11-15)
>>Mungu akiweka Roho wake ndani ya mwamini ni kwa lengo la kulipa neno lake uhai ndani ya mwamini na hivyo kumjaza mwamini uzima wa hilo neno (to fill the believer with the life of the word)
>>PROGRAMU YA MUNGU KWA MWANAWE ALIYEOKOKA KWA KUMWAMINI YESU NI KUMWONGOZA MWANAWE KWA ROHO WAKE NA KUMTIA KWENYE KWELI YOTE (Yoh 16:13)
>>HII INAMAANISHA MWAMINI AMEKUSUDIWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU NA KUTIWA KWENYE UZIMA WOTE WA NENO AMBAO NDIO UZIMA TELE (Yoh 10:10b) WA YESU KRISTO
[A born-again child of God in Christ is divinely programmed for abundant life through the guidance of the Spirit of life of Christ through his/her living faith in the living word of God! Divine programmes never fail! Divine programmess are always fulfilled and accomplished in due time. Once you are born-again the programme begins in you by the Holy Spirit of Christ and it continues until it is fully accomplished! Don’t ever judge the born-again children of God by the way you see them now! See them through the eyes of truth! Eyes of the word! Eyes of the Holy Spirit! Eyes of God! You will never point a finger at born again children of God! God is at work in them right now and he will never stop working until he is done with them in every grace of their lives in Christ!They are blessed in everything and in every way though the blessings may not be visible for a little while, THEY SHALL DEFINITELY BE MANIFEST IN AND THROUGH THEM]
Funga kinywa chako kuhusu watoto wa Mungu maana Mhubiri anasema:
“Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.” (Mhu 11:5)
Na tena hapa anasema,
“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.” (Flp 1:6)
“Amplified
Bible
I am convinced and confident of
this very thing, that He who has begun a good work in you will [continue to]
perfect and complete it until
the day of Christ Jesus [the time of His return].” (Phillipians 1:6)
ALIYEOKOKA ANA UHAKIKA WA KUFANANA NA YESU NA KUISHI MAISHA YA KILA BARAKA ILIYOMO KWENYE NENO LA MUNGU! BABA NA MWANA HATA SASA ANASHUGHULIKIA HILO KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU. (YOHANA 5:17) JAMBO LOLOTE ANALOLISHUGHLIKIA MUNGU KWETU TUAMINIO LIMEKAMILIKA MAANA MUNGU HANA KIGEUGEU, NA WALA HABADILIKI, NA WALA HAKUNA NENO GUMU LOLOTE LA KUMSHINDA!HIVYO MTOTO WA MUNGU ANAISHI AKIWA NA UHAKIKA WA MAMBO AYATARAJIAYO, NA HUKU AKIWA NA USHAHIDI MOYONI MWAKE WA KUYAMILIKI TAYARI YOTE AYANGOJEAYO INGAWA HAYAPO, AU HAYAONEKANI SASA KWA MACHO YA NYAMA! AMEOMBA SSAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU YALIYOMO KWENYE NENO, AMEAMINI, MUNGU AMEMSIKIA, NAYE ANAJUA KWAMBA MUNGU AMEMSIKIA, NA HIVYO ANAZO TAYARI ZILE HAJA ALIZOMWOMBA MUNGU! (1 YOHANA 5:14-15) MWANA WA MUNGU NDANI YA KRISTO YESU NI MWANADAMU ASIYE NA UHITAJI WOWOTE MAANA ANAZO HAJA ZOTE ALIZOMWOBA BABA YAKE WA MBINGUNI KWA JINA LA YESU KRISTO MWOKOZI!