HABARI MBAYA HUENEZWA NA WABAYA

 


HABARI MBAYA HUENEZWA NA WABAYA

JE! WEWE NI MBAYA AU MWEMA? SOMA HII!

 

“34 Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.” (Mathayo 12:34)

>> Watoto wa shetani huitwa "wazao wa nyoka" na huwa hawawezi kunena mema kwa kuwa wao ni wabaya!!! Mioyoni mwao wamejaza mabaya ambao huyanena kwa vinywa vyao kama ilivyoandikwa kwamba kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake!! Huwa unapenda kusema habari gani? Nzuri au mbaya? Ukiwa mbaya HUWEZI KUNENA MEMA NA WEWE NI MTOTO WA NYOKA!

35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya. (Mathayo 12:35)

>>Mtu mbaya katika akiba mbaya ya moyo wake hutoa mabaya!

>>Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoa mema!

Kama wewe ni mbaya utaona ni sawa tu au ni jambo la kawaida kusema habari mbaya kuhusu watu wengine, kuhusu serikali, kuhusu uchumi, kuhusu kanisa, kuhusu dhehebu, kuhusu watumishi wa Mungu, kuhusu marafiki zako, kuhusu maadui zako, kuhusu wafanyakazi wenzako, kuhusu wazazi wako, kuhusu mwajiri wako, kuhusu jirani yako, kuhusu ndugu zako, kuhusu mumeo/mkeo, kuhusu wanao, kuhusu hali mbalimbali za maisha, kuhusu VITU, WATU, HALI, MAZINGIRA, MIFUMO, MAHUSIANO, MATUKIO, TAASISI, IDARA, MIPANGO, UTENDAJI, IMANI ZA WENGINE, URATIBU, TARATIBU, HUDUMA, ELIMU, UONGOZI, UTAWALA NA WATAWALA, FAMILIA, KOO, MAKABILA, TAIFA, KAZI, BIASHARA, MAAMUZI, UTATUZI, YALIYOTENDWA, YALIYOPO, YATAKAYOKUWAKO, YALIYOKUWAKO, NA KILA KITU!!

>>>YOU ALWAYS DWELL ON THE BAD SIDE! YOU ALWAYS HAVE A BAD PERSPECTIVE, BAD ATTITUDE, BAD INTERPRETATION, BAD UNDERSTANDING, BAD MOTIVES, BAD REPORT, BAD TESTIMONY, BAD REACTION, BAD MOTIVATION, BAD INFLUENCE, BAD ASSOCIATIONS, BAD COMPANY, BAD ACTIONS, BAD EVERYTHING, AND BAD EVERYONE! You always dwell on the bad side!!

Unaharibu sifa za wengine, unachafua wengine, unawasema vibaya wengine, unawalaumu tu wengine, unawakosoa tu wengine, unawanyoshea vidole tu wengine, unawanung'unikia tu wengine, unawalalamikia tu wengine, unawahukumu tu wengine, UNA BUSARA, HEKIMA, NA AKILI YA KUTAFUTA MAKOSA YA WENGINE (EXPERT IN FAULT-FINDING)!!

Mazungumzo yako lazima yatahusisha ubaya wa jambo, ubaya wa mtu, ubaya wa tukio, ubaya fulani!

 Kwa nini uko hivi?

-EWE UZAO WA NYOKA UNAWEZAJE KUNENA MEMA UKIWA MBAYA!! YOU ARE INCAPABLE OF SPEAKING OR DOING GOOD THAT PLEASES GOD!!

44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. (Yohana 8:44)

1.      Baba yako ni Ibilisi (shetani)

2.      Moyoni mwako una roho ya shetani

3.      Ndiyo maana unapenda kuzitenda tamaa za dhambi za baba yako Ibilisi

4.      Una moyo mbaya uliojaa ubaya!

5.      Ndiyo maana unapenda ubaya, mabaya, na wabaya

Chuki ni uuaji kimaandiko! Unawachukia wema na wabaya! Yesu alisema wapende adui zako!! Wewe huwezi kwa kuwa ni mbaya MAANA UNA MOYO MBAYA ULIOJAA MABAYA!

>>Hauna Kweli ya Mungu moyoni mwako kama Ibilisi baba yako!! Neno la Mungu ndiyo Kweli (Yoh 17:17)

>> Kwa kuwa huna Neno la Mungu moyoni mwako unatenda dhambi!! Yesu ndiye Neno la Mungu Aliye Hai ambaye wewe humwamini, na ndiyo maana hujaokoka! Hata kama unadai umeokoka wewe ni mwongo maana mabaya na ubaya yaliyomo moyoni mwako uyanenayo kwa kinywa chako umeyatoa wapi??!!

“3Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.”(1 Yohana 2:3-4)

 Walio na Yesu mioyoni mwao (waliookoka) wana mioyo safi (Mathayo 5:8) na wamejaa Neno la Kristo mioyoni mwao waliloliamini. (Kol 3:16)

“11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”

(Zaburi 119:11)

“16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” (Wakolosai 3:16)

>> Unapotenda dhambi UNATENDA MABAYA UKIONGOZWA NA KUTAWALIWA NA SHETANI AMBAYE NI MBAYA NA ANAKUTUMIKISHA KWENYE UTUMWA WA DHAMBI

“34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.”  (Yohana 8:34)

>>UNAFURAHIA KUTENDA DHAMBI/UNAJISIFIA KUTENDA DHAMBI/UNAJIONA MWEREVU UNAPOTENDA DHAMBI/UNAJIITA MJANJA UNAPOTENDA DHAMBI

>>UNAWACHUKIA WANAOKUAMBIA UKWELI KWA SABABU WEWE NI MWOVU

“7Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.” (Mithali 9:7)

“8 Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.” (Mithali 9:8)

“9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;”  (Mithali 9:9)

>> HUPENDI KUKARIPIWA WALA KUKEMEWA KWA KUWA WEWE NI MBAYA!!! Ni mwenye kiburi, dharau, mbishi, mkaidi, mwenye jeuri, na majivuno! Unajiona huwezi kurekebishwa, unajua kila kitu, hupendi kujishusha, unajikweza, unapenda kuwa juu ya wengine n.k

“4 Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.” (Mithali 17:4)

>> MTENDA MABAYA UNAZIPENDA SANA NA UNAZICHANGAMKIA HABARI MBAYA KUTOKA KWENYE MIDOMO YA UOVU MAANA ZINAKUONGEZEA KWENYE HAZINA YAKO MBAYA YA MOYO WAKO ILI UKAZINENE KWINGINEKO MAANA KINYWA CHAKO SIKUZOTE KITANENA MABAYA YAUJAZAYO MOYO WAKO!

>> WEWE AMBAYE NI MWONGO UNAPENDA SANA KUTEGA SIKIO KUSIKILIZA ULIMI WA MADHARA!! YAANI, WALE WANAOONGEA YALE YANAYOENDA KUHARIBU SIFA ZA WENGINE, HESHIMA ZA WENGINE, MAHUSIANO YA WENGINE, KUWACHAFUA WENGINE N.K

>> ILI UOVU UENEE NA KUSAMBAA UNAHITAJI WABAYA NA WAOVU WAWILI WAKUTANE NA KUANZA KUZUNGUMZA! HAPO WATAJAZANA HABARI MBAYA KUTOKA KWENYE AKIBA MBAYA ZA MIOYO YAO! WATAJAZANA CHUKI MAANA YULE UNAYEMSEMA VIBAYA LAZIMA UMECHUKIA!!

“Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.” (Mithali 26:28)

>> CHUKI HUENEZWA NA WENYE CHUKI MOYONI

>> JIHADHARI NA WATU WANAOKUJA KWAKO WAKIONGEA MABAYA KUHUSU WENGINE NA KUHUSU KARIBU KILA KITU KWENYE JAMII! Siasa, uchumi, utafiti, huduma, kanisa, watumishi, n.k

“33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”  (1 Wakorintho 15:33)

“34 Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.”  (1 Wakorintho 15:34)

>>Mazungumzo mabaya yanaharibu tabia njema!! Maana mnajazana uovu! Na kisha mnakwenda kusambaza uovu huo!!!

>> Huwezi kushiriki kusengenya, kuteta, kusema wengine vibaya n.k ikiwa wewe si mbaya!! YOU HAVE TO BE EVIL TO TAKE PART IN EVIL CONVERSATIONS/LAZIMA UWE MWOVU ILI USHIRIKI MAZUNGUMZO MAOVU

“36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu”. (Mathayo 12:36)

“37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” (Mathayo 12:37)

>> UTATOA HESABU YA MANENO YAKO YOTE ULIYOYAONGEA UKIWA HAI MBELE ZA MUNGU SIKU YA HUKUMU

>>KWA MANENO YAKO UTAHESABIWA HAKI AMA KUHUKUMIWA

>> MALAIKA WA MUNGU WANAANDIKA NA PIA WANAREKODI MAONGEZI YAKO YOTE HADHARANI AU SIRINI

>>> KUOKOKA MAANA YAKE KUFUTIWA MASHITAKA YOTE KWENYE MAWAZO, MANENO, NA MATENDO KWA DAMU YA YESU UNAPOTUBU NA KUMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO, NA KUANZA MAISHA MAPYA YA UTAKATIFU NDANI YAKE KATIKA UFALME WA MUNGU!!

>> MUNGU ANATAKA AKUFIKISHE MAHALI AMBAPO UNAWEZA KUSEMA:

“Maneno yote ya kinywa changu yana haki; Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.”

(Mithali 8:8)

 

“Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.”

(Zaburi 49:3)

“Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki, Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.” (Ayubu 27:4)

“Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.” (Zaburi 35:28)

“Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.” (Zab 145:21)

TUBU NA UANZE KUJITAKASA MOYO NA KINYWA CHAKO KWA KUIAMINI NA KUITII KWELI!

“22Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo.” (1 Petro 1:22)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post