UTOAJI WA UPENDO (THE GIVING OF LOVE)

 John 13:34-35

UTOAJI WA UPENDO (THE GIVING OF LOVE)

SEHEMU YA KWANZA (UTANGULIZI)

Tunasoma kwenye Yohana 3:16;

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

>> Mungu aliupenda ulimwengu kiasi kwamba upendo wake ukampelekea KUTOA!!!

>> Upendo wako wa kweli lazima utakusukuma KUTOA!!!

ALITOAJE?

>>Mungu ALIMTOA MWANAWE PEKEE!!!

Kumbuka Biblia inafunua kwamba MUNGU NI UPENDO (1 Yoh 4:8), na hivyo UPENDO ALIMTOA MWANAWE PEKEE! Upendo wako, ili uwe ni wa kweli, lazima utoke kwake! Ujumbe wa Biblia ni ujumbe wa Upendo (Mungu). Roho Mtakatifu ni Roho wa Upendo!!! Waliooshwa kwa damu ya Yesu wanapopokea upendo wa Mungu (YESU MWANA WA MUNGU) mioyoni mwao, huwa wanapewa zawadi ya Upendo ambayo ni Roho Mtakatifu kutoka kwa Upendo Mwenyewe (Mungu).

“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” (Mdo 2:38)

“…….kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.” (Rum 5:5)

>>KUMWAMINI YESU NI KUAMINI PENDO LA MUNGU KWAKO NA KWA WANADAMU WOTE

>>KUMPOKEA YESU NI KULIPOKEA PENDO LA MUNGU ROHONI, NAFSINI, NA MWILINI MWAKO, NA HIVYO KWENYE MAISHA YAKO YOTE!

>>Utoaji wa Upendo UNA MALENGO NA MAKUSUDI YA UPENDO!!! Upendo lazima uelekezwe kwa mtu au watu maalumu! UPENDO NI MAALUMU (EXCLUSIVE FOR) KWA WANADAMU WALIOUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU

>>UPENDO WA VITU NI CHUKIZO KWA MUNGU MAANA NI IBADA YA SANAMU!

“Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.” (1 Tim 6:10)

>>UKIPENDA FEDHA HUWEZI KUMPENDA MUNGU NA PIA HUWEZI KUMWAMINI MUNGU, KWA MAANA IMANI YA YESU INATENDA KAZI KWA UPENDO (Gal 5:6)

>>UKIPENDA FEDHA HUWEZI KUTOA KWA UPENDO KAMA MUNGU ALIVYOTOA MAANA PENDO LAKE HALIMO NDANI YAKO

“5Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.” (Ebr 11:5)

>>UKIPENDA FEDHA HUWEZI KAMWE KURIDHIKA NAYO WALA KUTOSHEKA NAYO! NA HUWEZI PIA KURIDHIKA NA VITU ULIVYONAVYO KAMWE KWA SABABU MOYONI MWAKO MNA TAMAA ISIYOSHIBA YA MALI NA UTAJIRI

“Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza. Hayo pia ni ubatili” (Mhu 5:10)

>>UKIPENDA FEDHA HATA UPATE FEDHA NYINGI KIASI GANI HUWEZI KURIDHIKA WALA KUTOSHEKA; BALI UTATAKA ZAIDI NA ZAIDI!!

>>UKIPENDA WINGI KAMWE HAUTASHIBA NYONGEZA!! YAANI, HATA MALI NA VITU VIONGEZEKE VIPI KAMWE HAUSHIBI/HAUTOSHEKI/NA HAURIDHIKI

>>TAMAA YOYOTE (LUST OR GREED) HUWA HAISHIBI MPAKA ITAKAPOKUMEZA WEWE MWENYEWE KWENDA KUZIMU

“Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi.” (Mith 27:20)

>> Kutosheka ni roho, kutotosheka nako ni roho; (contentment vs discontentment)

>> kuridhika ni roho, halikadhalika kutoridhika nako ni roho; (satisfaction vs dissatisfaction)

 >> kushiba ni roho, na kutoshiba nako ni roho! (having enough vs never having enough)

>> ILE roho YA KWANZA INAKUVUTA JUU KWA MUNGU; HALI ILE roho YA PILI INAKUVUTA CHINI KUZIMU

>> Kule kutotosheka, kutoridhika, na kutoshiba ni ishara kuu ya moyo na akili vinavyotawaliwa na shetani; wakati kule kutosheka, kuridhika, na kushiba ni ishara ya moyo unaotawaliwa na Roho wa Mungu. Kumbuka TAMAA YOYOTE HAISHIBI KAMWE!

>> Mwenye tamaa yeyote hawezi kumpenda wala kumtumaini Mungu kamwe, bali huweka tumaini lake kwenye VITU!

>> Vilevile ukipenda mali na vitu HUWEZI KUMPENDA MUNGU, NA HIVYO HUWEZI KUMWAMINI MUNGU MAANA IMANI YA YESU INATENDA KAZI KWA UPENDO!

>> Tumaini lako haliwezi kuwa kwa Mungu kama wewe ni mwenye tamaa ya mali, pesa, utajiri, na umaarufu! (GREED AND LUST FOR MONEY, RICHES, AND FAME)

>> Unapopokea pendo la Mungu TAMAA ZOTE HUWA ZINAONDOLEWA MOYONI MWAKO, NA KUFIKIRI KWAKO KUHUSU MALI, FEDHA, NA UTAJIRI huwa kunabadilishwa hatua kwa hatua kadiri unavyoliamini Neno la Mungu na kulitii! Na hivyo ndivyo unavyokua katika neema ya Mungu na pia katika kumjua Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu.

>> Ukiendelea kubadilishwa kufikiri kwako ndipo mitazamo yako kuhusu fedha, mali, na utajiri hubadilishwa na Neno la Mungu! Kufikiri kwako kuhusu sifa za na utukufu wa wanadamu hubadilishwa nazo! Na ndipo malengo yako kuhusu fedha, mali, na utajiri hubadilika nayo. Malengo yako kuhusu KUTOA hubadilika vilevile!

Sasa tumeona mwanzo wa ujumbe huu wa upendo kwamba Mungu ALIUPENDA ULIMWENGU HATA KUMTOA MWANAWE PEKEE (Yoh 3:16)

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa umepotea dhambini

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa umepotea gizani

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa chini ya nguvu za giza

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa chini ya hukumu yake kwa sababu ya dhambi zake

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa unaishi kwa ubinafsi (selfishness) na chuki (hatred)

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa umemkataa yeye, haumtaki, na unamchukia

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa unategemea nguvu na uwezo wa mwanadamu (mkono wa mwili)

Ø  Aliupenda ulimwengu uliokuwa unategemea mawazo na akili ya mwanadamu, mali, fedha, elimu ya kidunia peke yake, njia za kibinadamu, ufumbuzi wa kibinadamu, utatuzi wa kibinadamu, majibu ya kibinadamu, mafundisho ya wanadamu, imani za wanadamu, juhudi na bidii za kibinadamu, mipango ya kibinadamu, malengo ya kibinadamu, taratibu na sheria za kibinadamu n.k. AMBAVYO VYOTE HAVIWEZI KABISA KUMUOKOA NA KUMKOMBOA KUTOKA CHINI YA VIFUNGO VYA SHETANI, NGUVU ZA SHETANI, roho ZA SHETANI, UVUVIO WA SHETANI, USHAWISHI WA SHETANI,UOVU WA SHETANI, DHAMBI ZA SHETANI, TAMAA ZA SHETANI, UBINAFSI WA SHETANI, UASI WA SHETANI, KIBURI CHA SHETANI, UBISHI WA SHETANI, UKAIDI WA SHETANI, JEURI YA SHETANI, DHARAU YA SHETANI, MAJIVUNO YA SHETANI, CHUKI NA KISASI VYA SHETANI, UADUI WA SHETANI, MAGOMVI YA SHETANI, DHULUMA ZA SHETANI, UONGO WA SHETANI, UDANGANYIFU WA SHETANI, FITINA ZA SHETANI, MIGAWANYIKO YA SHETANI, MAGONJWA NA MARADHI YA SHETANI, UZINZI WA SHETANI, UCHOYO WA SHETANI, UBAHILI WA SHETANI, UKANDAMIZAJI WA SHETANI, UNYONYAJI WA SHETANI, HILA ZA SHETANI, UBAGUZI WA SHETANI, UUAJI WA NA MAUTI YA SHETANI, UDHAIFU WA SHETANI, HOFU YA SHETANI, UHARIBIFU WA SHETANI, WIZI WA SHETANI, ULEVI WA SHETANI, ANASA ZA SHETANI, UKATILI WA SHETANI, UMASKINI WA SHETANI, UBAYA WOTE WA SHETANI NA MAMLAKA YA SHETANI!!!

Mwanadamu amezaliwa na kujikuta akiishi katika haya yote na mengineyo mengi yasiyoandikwa hapa, naye akaona kwamba haya ndiyo maisha ya kawaida ya mwanadamu kwa kuwa wote anaoishi nao, anaokua nao, anaowasikia na kuwaona, anaofanya nao kazi n.k WAKO HIVYO! Lakini maisha hayo hapo juu ni maisha chini ya ufalme wa giza wa shetani na hizo zote ni roho za shetani zilizomo ndani ya mioyo ya wanadamu, ambazo zote

>> zinamchukia Mungu, zimemwasi Mungu, hazimtaki Mungu na zimemkataa Mungu NDANI YA WATENDA DHAMBI

>> ziko kinyume na Mungu pamoja na watu wake wanaomcha na kumtii; ziko kinyume na malengo yao, mipango yao, na makusudi yao NDANI YA WATENDA DHAMBI WASIOAMINI

>> ziko kinyume na utendaji wao na kila wanalolifanya NDANI YA WAOVU WOTE

>> ziko kinyume na maisha yao yote, wao na watoto wao, na kila walichonacho, na wanachokifanya NDANI YA WANAOTUMIKISHWA KWENYE DHAMBI

Kwa kuwa Mungu ni upendo ALIMPENDA HUYU MWANADAMU ALIYE MATATIZONI NAMNA HII HATA AKAMTOA MWANAWE PEKEE ILI KILA MWANADAMU AMWAMINIYE ASIPOTEE MILELE!!! Maana baada ya kufa ni hukumu inafuata (Ebr 9:27); Maana hapa duniani anaishi akiwa amepotea na hajui anakokwenda! Anahangaikia mambo ya muda mfupi yanayoharibika ya hapa duniani na kamwe hawezi kuhangaikia yale ya milele na yasiyoharibika!

Bwana Yesu alikuja kubadili maisha ya mwanadamu na kumpa maisha mapya ndani yake mwenyewe!!! Haya yote yana uhusiano gani na lengo la kutoa? 

 

LENGO LA KUTOA-SEHEMU YA PILI

Kwenye sehemu ya kwanza tuliona jinsi Mungu alivyoupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele (Yoh 3:16)

>>Tatizo la msingi lilikuwa ni KUPOTEA KWA MWANADAMU, na bado hata sasa Mungu analishughulikia hilo kupitia KANISA!!

>> Upendo wa Mungu ulifunuliwa kwenye mwili (in the likeness of human flesh) KWA LENGO LA KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KILICHOPOTEA!!

“Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” (Lk 19:10)

>> UPENDO WA MUNGU SIKUZOTE UNA LENGO KUU LA KUTAFUTA NA KUOKOA KUTOKA UPOTEVUNI

Upotevuni:

1) ni mbali na Kweli ya Mungu (bali ni kwenye uongo na udanganyifu wa shetani)                              

2) ni mbali na Neno la Mungu (bali ni kwenye neno la nyoka-shetani)                                

3) ni mbali na Makusudi na Mipango ya Mungu (bali ni kwenye mipango na makusudi ya mwanadamu na shetani)   

4) ni mbali na Utakatifu wa Mungu (bali ni kwenye dhambi za shetani)                       

5) ni mbali na Amani ya Mungu (bali ni kwenye uchungu, hofu, mashaka, kuvunjika moyo, hasira, wasiwasi, kufadhaika, huzuni, n.k. kutoka kwa shetani)

6) ni mbali na Kibali cha Mungu (bali ni kwenye kutengwa/kusalitiwa/kukataliwa/kuachwa/kupuuzwa n.k.)

7) ni mbali na Afya ya Kimungu (bali ni kwenye udhaifu, maradhi, na magonjwa ya shetani)

8) ni mbali na Neema ya Mungu (bali ni kwenye jitihada, juhudi na bidii za kibinadamu zisizoweza kumshinda shetani)

9) ni mbali na Roho wa Mungu (bali ni kwenye kumilikiwa na kutawaliwa na roho za shetani)

10) ni mbali na Utii kwa Mungu (bali ni kwenye uasi wa shetani)

11) ni mbali na Unyenyekevu wa Mungu (bali ni kwenye kiburi cha shetani)

12) ni mbali na Kicho cha Mungu (bali ni kwenye ushupavu na kujikinai toka kwa shetani)

13) ni mbali na Ufahamu wa Mungu (bali ni kwenye uongo wa shetani)

14) ni mbali na Maarifa ya Mungu (bali ni kwenye maarifa ya uasi ya shetani)

15) ni mbali na Umoja wa Roho (bali ni kwenye migawanyiko na matengano ya shetani)

16) ni mbali na Utukufu wa Mungu (bali ni kwenye uvuvio na uwepo wa shetani)

17) ni mbali na Nguvu za Mungu (bali ni kwenye nguvu za majini na mapepo ya shetani)

18) ni mbali na Sauti ya Mungu (bali ni kwenye kusikiliza roho zidanganyazo za shetani)

19) ni mbali na Rehema za Mungu (bali ni kwenye kuwa chini ya ghadhabu na hasira ya Mungu)

20) ni mbali na Fadhili za Mungu (bali ni kwenye kufadhiliwa na shetani na watumishi wake)

21) ni mbali na Huruma za Mungu (bali ni kwenye ukatili wa shetani)

22) ni mbali na Uaminifu wa Mungu (bali ni kwenye kukosekana uaminifu kabisa kwa shetani)

23) ni mbali na Wema wa Mungu (bali ni kwenye ubaya wa shetani)

24) ni mbali na Furaha ya Mungu (bali kwenye hasira, ghadhabu, chuki, wivu, uchungu n.k. vya shetani)

25) ni mbali na Upendo wa Mungu (bali ni kwenye chuki ya shetani)

26) ni mbali na Uvumilivu wa Mungu (bali ni kwenye kukosa uvumilivu kwa shetani-impatience)

27) ni mbali na Utu Wema wa Mungu (bali ni kwenye kutojali na ubaya na uovu na ubinafsi wa shetani)

28) ni mbali na Upole wa Mungu (bali ni kwenye ukali wa shetani)

29) ni mbali na Kiasi (self-control) cha Mungu (bali ni kwenye tamaa, kutojizuia, kutojidhibiti, n.k. vya shetani)

30) ni mbali na Haki ya Mungu (bali ni kwenye kutomwamini wala kumtegemea Mungu, wala kumpendeza Mungu anakosababisha shetani)

31) ni mbali na Utajiri na Utele wa Mungu (bali ni kwenye umaskini, uhitaji, kupungukiwa, na kuishiwa vya shetani)

32) ni mbali na Uongozi wa Mungu (bali ni kwenye kuongozwa na tamaa na uovu wa mioyo toka kwa shetani)

33) ni mbali na Uzima wa Milele (bali ni kwenye mauti ya milele sasa na baadae kwenye ziwa liwakalo moto na kiberiti-mauti ya pili)

34) ni mbali na Uponyaji wa Kiungu (bali ni kwenye kuugua na magonjwa ya shetani, na matibabu ya kibinadamu yasiyoweza kabisa kuondoa roho za magonjwa, bali yanashughulika tu na dalili na uharibifu wa hizo roho mwilini)

35) ni mbali na Baraka za Kiungu (bali ni kwenye laana za aina zote kwa sababu ya kumuasi na kumkataa Mungu)

36) ni mbali na Hekima ya Mungu (bali ni kwenye upumbavu-folly kutoka kwa shetani)

37) ni mbali na Ushauri wa Kimungu (bali ni kwenye ushauri wa wanadamu tu na wa shetani pia)

38) ni mbali na Mapenzi ya Mungu (bali ni kwenye mapenzi ya wanadamu na shetani)

39) ni mbali na Uwepo wa Mungu kwenye Utukufu na Uhuru wake (bali ni kwenye uwepo wa mapepo, majini, na wachawi kutoka kwa shetani;  na kwenye kuonewa nao, kuteswa nao, kukandamizwa nao, kuibiwa nao, na kuharibiwa nao )

40) ni mbali na Ufalme wa Mungu (bali ni kwenye ufalme wa giza wa shetani) n.k.

>>BWANA WETU YESU KRISTO NI UPENDO WA MUNGU KWA WANADAMU WOTE WALIOPOTEA DHAMBINI KWENYE UTUMWA WA GIZA KAMA TULIVYOONYESHA HAPA JUU

Mungu ambaye ni Upendo:

1) ALIUTUMA UPENDO WAKE NDANI YA MWILI WA MWANADAMU, UPENDO UKAZALIWA NDANI YA MWANAMKE (Lk 2: 5-7)

2) UPENDO WAKE ULIKUJA KWA NJIA YA NENO LAKE LA UPENDO (Yoh 1:1,14 & Lk 1:35)

3) (UPENDO) HUO ULIOKUJA KWA NJIA YA (NENO LAKE UPENDO), ULIKUWA NDANI YA (ROHO WAKE UPENDO) ALIYE MTAKATIFU (Yoh 14:9-10)

Hapa tunamtaja Mungu kama Upendo kwa kuwa Mungu ni Upendo (1 Yoh 4:8)

4) UPENDO HUO ULIKUJA KUOKOA ROHO, KUPONYA MIILI, KUPONYA NAFSI, KUBADILISHA MIOYO, KUHUISHA (KUTIA UZIMA MPYA/MAISHA MAPYA), KUKOMBOA KUTOKA KWENYE NGUVU ZA GIZA, KUWEZESHA, KUINUA, KUOSHA NA KUTAKASA, KUREJEZA, KUFUFUA, KUHEKIMISHA, KULETA MEMA, KUSHINDA UBAYA, KUFARIJI, KUJENGA, KUTIA MOYO, KUTIA NGUVU, KULETA MAWAZO NA FIKIRA MPYA ZA UPENDO, N.K. KUPITIA IMANI KWA PENDO LA MUNGU YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WA DUNIA YOTE

“3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 4Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;” (Tit 3:3-4)

“18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,” (Lk 4:18)

>>UPENDO KIVITENDO LAZIMA UOKOE KUTOKA NA KUTOA KABISA TAABUNI!!

>>UPENDO KIVITENDO LAZIMA UOKOE NA KUTOA KABISA KUTOKA KWENYE TAABU/SHIDA/DHIKI/MAANGAMIZI/MAUTI/UBAYA/UOVU N.K.

>>UTOAJI WA UPENDO UKIWA NDANI YAKO WEWE ULIYEUAMINI UPENDO WA MUNGU, NA KUUPOKEA, LAZIMA UWE NA MALENGO NA MAKUSUDI YA KUBADILISHA KABISA MAISHA YA WENGINE NA KUWATOA KWENYE GIZA LOLOTE, AU NGUVU ZOZOTE ZA GIZA, AU VIFUNGO VYOVYOTE VYA GIZA, AU UTUMWA WOWOTE WA SHETANI, AMA UONEVU WOTE WA SHETANI KAMA TULIVYOONYESHA “UPOTEVUNI NI WAPI HAPO JUU!

>>KUWA NA MALENGO YA NAMNA HII KWA DHATI YA MOYO WAKO, AU KWA MAISHA YAKO YOTE, KUNASABABISHA MUNGU AKUPE NEEMA YA KUTIMIZA MALENGO HAYO YA UPENDO!

>>PENYE UPENDO PANA MATENDO TELE YA UPENDO YANAYOTENDWA KWA MOYO WA UPENDO NA KWA NGUVU ZA UPENDO (MUNGU)!!!

Sasa ili kuelewa vizuri zaidi malengo ya kutoa ni vema tukaangalia mambo mawili;

1) MTOAJI HALISI (REAL GIVER) NI YUPI? NA

2) LENGO HALISI LA KUTOA NI LIPI?

1) MTOAJI HALISI (REAL GIVER)

Ili Upendo utimize makusudi na malengo yake ni lazima KUUTOA UHAI WAKO KWA AJILI YA UWAPENDAO vinginevyo HAUWEZI KUWA NA UPENDO KUTOKA JUU!!

>>Mungu ambaye ni Upendo ALIMTOA MWANAWE PEKEE kwa ajili yetu sisi ambao hatukustahili kabisa

>>KWA HIVYO UPENDO HUU UKIWA NDANI YAKO LAZIMA UUTOE UHAI WAKO KWA AJILI YA WASIOSTAHILI, AMBAO UNAWAPENDA KWA UPENDO WA KRISTO ULIOMO NDANI YAKO

>> MTOAJI HALISI NI YULE AMBAYE KWANZA AMEUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA NDUGU ZAKE, NA WANADAMU WOTE PIA.

“16Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.” (1 Yoh 3:16)

>>KWA KUWA YESU ALIUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YETU SISI;

>> “IMETUPASA…..”!!!

Contemporary English Version(1 John 3:16)
We know what love is because Jesus gave his life for us. THIS IS WHY WE MUST GIVE OUR LIVES for each other.”

>>YAANI, HAPA HAMNA NAMNA NYINGINE YOYOTE ISIPOKUWA NI LAZIMA KUUTOA UHAI WAKO KWA AJILI YA WENGINE, UKIANZIA KWENYE MWILI WA KRISTO (KANISA), KISHA KWA WENGINE WOTE!

>> TAFSIRI (DEFINITION) YA UPENDO NI KUUTOA UHAI WAKO KWA AJILI YA WENGINE KAMA ALIVYOFANYA YESU, (UPENDO WA MUNGU), AMBAYE ANAKUWEZESHA WEWE UNAYEMPENDA, NA HIVYO KUMTII, KUTIMIZA MALENGO NA MAKUSUDI YALE YALE YA UPENDO ULIOMIMINWA MOYONI MWAKO (Rum 5:5) KWA ROHO WA UPENDO ULIYEPEWA, ULIPOMPOKEA YESU (UPENDO WA MUNGU) KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO!

-Ulikuwepo Upendo mbinguni

-Upendo huo ukafunuliwa ulimwenguni kwenye mwili wa damu na nyama

-Ukauamini na kuupokea Upendo huo toka kwa Mungu (Upendo)

-Upendo huo sasa umo ndani yako kukuwezesha, kwa nguvu zake, kupitia Roho wa Upendo, kuyatimiza malengo na makusudi yote ya Upendo!!!

-Umeokolewa na Upendo, unaishi kwa Upendo, Unatenda yote kwa Upendo, Unasambaza Upendo, unajenga/unapanua/unaimarisha Ufalme wa Upendo (Mungu) duniani kwenye mioyo ya na maisha ya wanadamu.

-Ufalme wa Upendo umo ndani yako ili kuvunja na kuharibu ufalme wa ubinafsi na chuki wa shetani ulimwenguni!

>>Kwa habari ya Upendo wa Mungu Biblia inasema,  “18Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.” (1Yoh3:18)

>>UPENDO HALISI NI WA VITENDO!! KUPENDA HALISI KIBIBLIA NI KWA MATENDO! NA KWA KUWA MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU HATA KUMTOA……..! NDIPOSA NA WEWE LAZIMA UJITOE NA KUTOA KWA WALE UWAPENDAO!

KATIKA MUKTADHA WA SOMO HILI TUTAKAPOSEMA UPENDO AU KUPENDA TUTAKUWA TUKIMAANISHA UTOAJI WA UPENDO!!! HUWEZI KUPENDA PASIPO KUTOA! NA TUMEANZA KUONA KWAMBA WATOAJI HALISI KWANZA WAMEJITOA ROHO, NAFSI, NA MWILI KWA MUNGU NDANI YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU! NA KISHA WAKAUTOA UHAI WAO KWA NDUGU KATIKA MWILI WA KRISTO NA WANADAMU WOTE PIA!!!

UNAUTOAJE UHAI WAKO?

Kuutoa uhai wako ni kuyatoa maisha yako yote! Hatua hii ya kuyatoa maisha yako yote lazima ianze kwa kuyatoa maisha yako yote kwa Yesu kama Bwana na Mwokozi wako.

Kisha ni lazima, kama andiko lisemavyo, kuishi maisha yako kwa ajili ya Yesu (Upendo) pekee muda uwapo hapa ulimwenguni. Biblia inasema,

“15tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao” (2 Kor 5:15)

>> Yesu alikufa akafufuka ili WALIO HAI NDANI YAKE, WASIWE HAI TENA KWA AJILI YA NAFSI ZAO WENYEWE,

>> BALI WAWE HAI KWA AJILI YAKE YEYE ALIYEKUFA AKAFUFUKA KWA AJILI YAO.

>> ILI KUTIMIZA MALENGO NA MAKUSUDI YA UPENDO NI LAZIMA UISHI KWA AJILI YAKE YESU (UPENDO) PEKEE!

>> roho yako ni mali yake Yesu (Upendo), nafsi yako ni mali yake Yesu (Upendo), mwili wako ni mali yake Yesu (Upendo) na hivyo WEWE NI MALI YAKE UPENDO!

“7Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. 8Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. 9Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.” (Rum 14:7-9)

>>KUTOTAMBUA, KUTOELEWA, NA KUTOJUA KWA DHATI KWAMBA WEWE NI MALI YA UPENDO, NA KWAMBA KUISHI KWAKO DUNIANI NI KWA AJILI YAKE UPENDO, NI KIKWAZO KIKUU CHA KUYAJUA, KUYAELEWA, KUYAKUBALI, NA KUYATEKELEZA/TIMIZA MALENGO NA MAKUSUDI YA UPENDO!

>>NA KWA KUWA UPENDO UNA TABIA KUU YA KUTOA LAZIMA UTASHINDWA KUTOA KAMA UPENDO WA MUNGU UNAVYOTAKA, NA ULIVYOKUSUDIA TANGU MWANZO

Uhai wa mwili uko kwenye roho! Maisha ya Upendo wa Mungu yamo kwenye roho yako kadiri unavyojazwa na Roho wa Upendo.

“63Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” (Yoh 6:63)

>> Kujazwa Roho Mtakatifu ni kujazwa Upendo!!!  Uzima tele wa Yesu (Yoh 10:10 b) ni uzima wa Roho/ambao ni uzima wa Mungu (Upendo) maana Mungu ni Roho!!!

>> Uzima wa Upendo ni Uhai wa Upendo, nao ni Maisha ya Upendo; Uzima tele maana yake Upendo tele!!! Uzima wa milele ni Upendo wa milele!!! Roho Mtakatifu ni Roho wa Upendo tele wa milele!!!

Biblia inasema ndani yake Neno/Mungu/Upendo ndimo ulimokuwa uzima (Yoh 1:4)

Daudi anasema “…………..Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.” (Zab 23:5b)

>>KIKOMBE KINACHOFURIKA HAPA NI KIKOMBE CHA UPENDO

>>MAFUTA YA ROHO NI MAFUTA YA UPENDO

>>KUFURIKA UPENDO KUNAPELEKEA KUMWAGIKA (OVERFLOW) HUO UPENDO!!

>>HUDUMA YAKO, KWA ROHO MTAKATIFU, NI MMWAGIKO WA UPENDO KWA WENGINE (OVERFLOW OF LOVE UNTO OTHERS) KUTOKA KWENYE MOYO ULIOJAA NA KUFURIKA UPENDO!

>>KIKOMBE HAKIWEZI KUFURIKA PASIPO MAISHA YALIYOKABIDHIWA KWA “MJAZAJI” MWENYEWE (THERE CAN NEVER BE AN OVERFLOW OF LOVE UNTO OTHERS WITHOUT A SUBMITTED LIFE!) {SUBMITTED HEART, MIND, AND BODY}

>>MAISHA YALIYOKABIDHIWA KWA MJAZAJI ROHO (UPENDO) YESU, ILI AYATUMIE KWA MAKUSUDI NA MALENGO YA UPENDO, NDIYO YANAYOWEZA KUTIMIZA MALENGO, MAKUSUDI, NA MIPANGO YAKE MUNGU WA UPENDO NDANI YAKE YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU!!

>>MOYO ULIOKABIDHIWA KWA YESU HUWA UNAJAZWA UPENDO KWA WALIOPOTEA!! (Kumbuka tulivyoonyesha upotevuni ni wapi kule juu)

Kwa kujazwa Upendo wa Mungu mpaka kufurika ndipo unaweza kutoa upendo huo kwa wengine kupitia maisha na huduma yako maana moyo wako umejaa huruma ya Upendo, na hao unaowahudumia unafanya hivyo kwa moyo wako wote kama Upendo alivyoagiza kwenye Neno lake la Upendo:

“23Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, 24mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. (Kol 3:23-24)

>> Lolote ulifanyalo LIFANYE KWA MOYO!! Lolote lile mfano kusoma, kula, kupika, kuuza, kununua, kuoga, kushauri, kuvaa, kwenda, kurudi, kulala, kuamka, KUTOA, kuimba, kualika, kusimamia, kufariji, kujenga, kukirimu, kutia moyo,  n.k.

>> LIFANYE KWA MOYO KAMA KWA BWANA NA SI KWA MWANADAMU!! soma kwa ajili ya Yesu, kula kwa ajili ya Yesu, mpikie Yesu, uza kwa ajili ya Yesu, nunua kwa ajili ya Yesu, oga kwa ajili ya Yesu, mvalie Yesu, nenda kwa ajili ya Yesu, rudi kwa ajili ya Yesu, lala kwa ajili ya Yesu, amka kwa ajili ya Yesu, toa umpe Yesu, mwimbie Yesu, mwalike Yesu, mtendee mema Yesu, FANYA KWA AJILI YA YESU, NA MFANYIE YESU! Kwa kufanya hivyo Roho wa Upendo atakuongoza kwenye njia ya Upendo Kivitendo kwa ajili ya Yesu!! Na unachomfanyia Yesu au unachompa Yesu kwa kupitia wanadamu HAKIWEZI KUWA DUNI WALA HAKIWEZI KUWA NA UBINAFSI NDANI YAKE!

>> UKIJUA KWAMBA UTAPOKEA KWA BWANA UJIRA WA URITHI! Yaani, kuna mshahara!!!!

>> KWA SABABU KWA KUFANYA HIVYO UNAMTUMIKIA BWANA WA UPENDO KRISTO!!!

>> KUMTUMIKIA KRISTO NI KWA UPENDO! WATUMISHI WA MUNGU NI WATUMISHI WA UPENDO! PASIPO UPENDO UTUMISHI WAKO HAUKUBALIKI NA WALA HAUNA THAWABU YOYOTE, NA WALA HAUWEZI KUTIMIZA MALENGO NA MAKUSUDI YA UPENDO

“1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.” (1 Kor 13:1-3)

>> UPENDO NDIYE BWANA NA MWOKOZI WAKO! HIVYO LAZIMA UTENDE MAMBO YOTE {KWA AJILI YA UPENDO/PAMOJA NA UPENDO/NDANI YA UPENDO/KWA NJIA YAKE UPENDO}, NA KWA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA UPENDO!!

>> UTUKUFU WA UPENDO WA MUNGU NDIO UTAKATIFU WAKE!!!

Mpaka hapa tumesema;

1) Jitoe kila vile ulivyo kwa Upendo (give all that you are to Love). Hii ni dispossession of your “self” (au deliverance from self) ili wewe usiwe mali yako mwenyewe tena bali unakuwa wake! Unaunganishwa naye katika roho (1Kor 6:17) na kuwa roho moja naye.

“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu” (Gal 2:20)

-SI WEWE TENA UNAYEISHI BALI YESU ANAISHI NDANI YAKO!

2) UKIJITOA KWAKE UPENDO (MUNGU) VYOTE VILE ULIVYO, NDIPO UTAWEZA KUTOA VYOTE ULIVYONAVYO KWAKE!! (giving unto Jesus everything you have and possess). YAANI, UNAMKABIDHI VILIVYO VYAKE ILI YEYE AWE NDIYE MMILIKI HALISI, NA WEWE UNABAKI KAMA WAKILI/MSIMAMIZI MWAMINIFU (STEWARD) WA NEEMA ZAKE MBALIMBALI ALIZOKUKIRIMIA NA ANAZOENDELEA KUKUKIRIMIA KADIRI UNAVYOZIDI KUONGEZEKA KIIMANI ILI KUTIMIZA MALENGO NA MAKUSUDI YAKE YA UPENDO!! Huku ni kuziondoa mali, pesa, na utajiri moyoni mwako na akilini mwako ili akujaze Upendo (Roho)!!

3) Hivyo unakuwa umejitoa kwake kabisa, na kisha umetoa vyote ulivyonavyo kwake, na NDIPO UTAWEZA KUTOA KWA UPENDO kwa sababu tayari wewe ni mali ya upendo roho, nafsi, na mwili, na unaongozwa na kutawaliwa na upendo.

Kwa hatua hizi tatu, ambazo ni mchakato katika maisha yako ndani ya Yesu, unakuwa umebadilishwa roho yako na kuwa kiumbe kipya mwenye roho mpya (2 Kor 5:17), ambaye mawazo na akili yake vimebadilishwa na vinaendelea kubadilishwa ili kuwaza na kufikiri kama Neno la Upendo lisemavyo! Na mwili wako unakuwa ukitumika kutimiza na kutekeleza mipango, malengo, na makusudi ya Upendo.

Hakuna upendo wa maneno matupu! Na upendo unatakiwa uwe unaongezeka mpaka kufikia ukamilifu wa Mungu (Upendo) mwenyewe kwa jinsi ya mwili (Kol 2:9).

“Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; 10mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; 11hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.” (Flp 1:9-11)

>> PENDO LAKO LIZIDI KUWA JINGI SANA KATIKA HEKIMA NA UFAHAMU WOTE

>> UPATE KUYAKUBALI YALIYO MEMA

>> ILI UPATE KUWA NA MOYO SAFI, BILA KOSA, MPAKA SIKU YA KRISTO

>> HALI UMEJAZWA MATUNDA YA HAKI KWA NJIA YA YESU KRISTO,

>> YOTE HAYA NI KWA SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU (UPENDO)

Upendo uliofunuliwa kwenye Agano Jipya ni Upendo kwa waasi, watenda dhambi, waovu, wabaya, wanaomchukia Mungu (Upendo), wasio na shukrani, waongo, wadhalimu, wauaji; na uovu na ubaya wote wa kila namna; hivyo ndivyo wote tulivyokuwa wakati upendo uliotuokoa ulipofunuliwa! Lakini Mungu alitupenda sisi maadui zake!

>> SIFA KUU YA UPENDO WA MUNGU NI KUWAPENDA MAADUI!!! KUWAPENDA WASIOPENDEKA!! KUWAOMBEA! KUWATENDEA MEMA! KUWATAKIA MEMA! N.K.

>> HUKU NDIKO KUTOA UPENDO!

a) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda chuki!

b) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda uchoyo!

c) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda tamaa!

d) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda uadui!

e) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda hasira na ghadhabu!

f) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda uchungu!

g) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda tamaa ya mali!

h) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda kupenda fedha!

i) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda uonevu!

j) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda dhuluma!

k) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda umaskini!

l) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda uhitaji!

m) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda kupungukiwa!

n) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda kuishiwa!

o) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda magonjwa!

p) upendo unahitajika ndani yako ili kuvunja vifungo vya giza!

q) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda roho zidanganyazo!

r) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda mafundisho potofu!

s) upendo unahitajika ndani yako kushinda ulemavu!

t) upendo unahitajika ndani yako kushinda upofu!

u) upendo unahitajika ndani yako kushinda uziwi!

v) upendo unahitajika ndani yako kushinda ububu!

w) upendo unahitajika ndani yako kushinda utasa!

x) upendo unahitajika ndani yako kushinda ubahili!

y) upendo unahitajika ndani yako kushinda huzuni!

z) upendo unahitajika ndani yako kushinda ukandamizaji!

a1) upendo unahitajika ndani yako ili kushinda ubinafsi!

b1) upendo unahitajika ndani yako kushinda mauti!

b2) upendo unahitajika ndani yako uasi na dhambi zote!!

Huduma (ministry) ya Upendo na maisha ya Upendo LAZIMA YAANZE NDANI YAKO KWANZA, na kisha mafuriko (overflow) ya Upendo yaelekee kwa wengine; ndiyo lengo la Upendo na ndiyo Lengo la Utoaji wa Upendo!!! Biblia inasema, UPENDO HAUSHINDWI NENO KAMWE!!

1 COR 13:8

Berean Literal Bible
LOVE NEVER FAILS; but if there are prophesies, they will be done away; if there are tongues, they will be ceased; if there is knowledge it will pass away.

King James Bible
CHARITY NEVER FAILETH: but whether there be prophecies, they shall fail; whether there be tongues, they shall cease; whether there be knowledge, it shall vanish away.

New King James Version
LOVE NEVER FAILS. But whether there are prophecies, they will fail; whether there are tongues, they will cease; whether there is knowledge, it will vanish away.

>>UMEONA HITAJI LA UPENDO LILIVYO KUBWA LEO? INUA MACHO YAKO TAZAMA NDUGU ZAKO, RAFIKI ZAKO, WASHIRIKA WENZAKO, WAKRISTO WENZAKO WALIOOKOKA, WOTE WASIOOKOKA, WAFANYAKAZI WENZAKO, WANACHUO WENZAKO, WAFANYABIASHARA WENZAKO, WANAFUNZI WENZAKO, TAIFA LAKO, KANISA LAKO, WAAJIRIWA WAKO, WAAJIRI WAKO, N.K. UNAONA NINI? JE! UNAONA HITAJI LA UPENDO? UNAFANYA NINI KWA AJILI YAO? JE? UNAO UPENDO WA KWELI WA KUTOA?

>>Hivi unajua upendo ni

1) wewe mwenyewe ndani ya Yesu KWA AJILI YAO?!

2) vyote vile ulivyo ndani ya Yesu KWA AJILI YAO?

3) vyote ulivyo navyo ndani ya Yesu KWA AJILI YAO?

4) vyote unavyomiliki ndani ya Yesu KWA AJILI YAO?

5) pesa za Yesu zote ulizoaminiwa uwakili juu yake KWA AJILI YAO?!

6) mali za Yesu zote ulizoaminiwa uwakili juu yake KWA AJILI YAO?

7) utajiri wa Yesu wote ulioaminiwa uwakili juu yake KWA AJILI YAO?!

8) elimu aliyokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

9) cheo alichokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

10) nguvu alizokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

11) uzoefu aliokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

12) exposure (kwenda huko na huko na kuona na kujua mengi) alikokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

13) mtandao (network) wa watu ulionao wote maishani aliokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

14) maarifa yote aliyokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

15) ufahamu wote aliokujalia Yesu KWA AJILI YAO?!

16) YOTE ALIYOKUJALIA YESU KWA AJILI YAO?!

17) VYOTE ALIVYOKUJALIA YESU KWA AJILI YAO?! n.k. n.k.

‘KWA AJILI YAO’ kwa kuwa imeandikwa,

“24Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake” (1 Kor 10:24)

>>UPENDO AMEAGIZA MTU ASITAFUTE FAIDA YAKE MWENYEWE BALI YA MWENZAKE

>>WATOAJI HALISI WA UPENDO (real givers) HAWATAFUTI FAIDA NA MANUFAA YAO BINAFSI

“Kila mmoja miongoni mwetu na ampendeze jirani yake,  apate wema, akajengwe. Kwa maana KRISTO MWENYEWE HAKUJIPENDEZA MWENYEWE;……….” (R UM 15:2-3a)

>>UTOAJI WA UPENDO HAUKO KWENYE FEDHA TU KAMA WENGI WANAVYOFIKIRI BALI UKO KWENYE KUUTOA UHAI WAKO WOTE (MAISHA YAKO YOTE) KWA AJILI YA WENGINE!!!

“12Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.14Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.” (Yoh 15:12-14)

>>TOA UHAI WAKO KWA AJILI YA WENGINE ILI UWE RAFIKI WA UPENDO (YESU); NDIPO UTAKUWA NI MTOAJI HALISI (REAL GIVER)

Biblia inafundisha kwamba Kujitoa wewe mwenyewe maisha yako kwa Yesu, na kwa wengine NI IBADA NJEMA YENYE KIBALI KWA MUNGU (Rum 12:1); Biblia inasema Mungu Baba (Upendo) anatafuta WAABUDUO HALISI (real worshippers) ILI WAMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI (Yoh 4:23-24); NA KWAMBA KIPINDI HIKI CHA NEEMA (dispensation of grace) WAABUDUO HALISI NI WALE WATOAJI HALISI WA UPENDO (real love givers);

>>WATOAJI HALISI WA UPENDO WA MUNGU NDIO WANAOMWABUDU MUNGU KIUHALISIA KATIKA “TENDO NA KWELI” (1 Yoh 3:18)

>> HATA SASA BABA (UPENDO) ANATAFUTA WATOAJI HALISI ILI AWAJAZE UPENDO KWA KIWANGO CHA KIKOMBE KUFURIKA, NA YALE MAFURIKO YA UPENDO HUO YAWAFIKIE WENGINE KATIKA roho, nafsi, na miili yao!

>> Watoaji halisi wanahudumia roho za wanadamu kwa upendo!!

>>Lakini pia wanahudumia miili na nafsi za wanadamu kwa upendo!!

Nafsi (soul) = Mawazo/akili (mind) + Mapenzi/Makusudi/Nia (will) + Hisia (emotions)

Hivyo watoaji halisi WANATOA UPENDO (minister love), KWA ROHO MTAKATIFU, kwenye akili, mawazo, nia, mapenzi, makusudi, na hisia za wanadamu NA KULETA BADILIKO, FAIDA, NA MANUFAA YALIYOKUSUDIWA NA UPENDO YA KUTOA UPOTEVUNI,

-lost/deceived/corrupted/ depraved/carnal/unspiritual MINDS (akili na mawazo potofu)

-man’s captured will obeying the flesh (man’s will) and satan’s will (mapenzi ya mwanadamu nay a shetani)

-Lakini pia watoaji halisi (real givers) hutoa upotevuni BODIES SERVING SIN’S INTERESTS IN LUST, GREED, and SENSUALITY; Bodies also in sickness, disease, and infirmity!![miili inayotumikishwa kwenye tamaa za dhambi, maradhi, magonjwa, na udhaifu]

>>KUTOA KABLA YA KUJITOA NI DHAMBI MAANA LAZIMA KUTAKUWA NA MALENGO NA NIA NA MAKUSUDI YA KIBINAFSI ! Dharau, kujiinua, kutaka kuabudiwa, kutaka kutetemekewa, kutaka kutumikiwa, kutaka kusifiwa, kutaka kitu baada ya kutoa (seeking something in return), kutafuta kuonekana, kutafuta umaarufu, n.k

>>Watoaji wasio halisi wote wako kama baba yao ibilisi alivyofanya hapa;

“8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. 10Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” (Mt 4:8-10)

>>SHETANI ALIPOKWENDA KUMJARIBU YESU ALIMWAMBIA “angempa milki zote za ulimwengu, na fahari zake, KAMA TU ANGEMSUJUDIA!

>>WATOAJI WOTE WASIO HALISI (WASIOSUKUMWA NA UPENDO BALI UBINAFSI NA CHUKI) HUTOA KWA MASHARTI AMA YA MOJA KWA MOJA YA KUTAMKWA AU YA KUANDIKWA (KIMKATABA), AU MASHARTI YASIYOTAMKWA MIOYONI MWAO YENYE SURA YA MATARAJIO FULANI KUTOKA KWA WANAOPOKEA VITU VYAO!!! NA WASIPOTIMIZA MATARAJIO YAO CHUKI YOTE HUDHIHIRISHWA KWA KUDHALILISHWA /KUSEMWA VIBAYA/ KUZIRWA /KUSUSWA/ N.K.

>>WATOAJI HALISI HUWA HAWANA MASHARTI; WALA HAWAJIVUNI; WALA HAWAJIONI KWAMBA WAO NDIO WAMETOA BALI HUMPA MUNGU UTUKUFU WOTE; WAO HUMPA YESU NA SIYO MWANADAMU; HUWA WANAWEKA HAZINA MBINGUNI;NA MWISHO HUWA WANAMKOPESHA BWANA MUNGU WAO NA KAMWE SIYO MWANADAMU;

“17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.” (Mith 19:17)

Watoaji halisi (real givers) HUWA WANAWAPENDA JIRANI ZAO KAMA NAFSI ZAO!!! Hii ni sifa muhimu sana katika kizazi hiki cha ubinafsi, umimi, na uchoyo, ubahili, na chuki! Biblia inasema,

“31Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi” (Mk 12:31)

Hii ndiyo Amri ya pili kwa ukubwa na ukuu katika Amri zote 613 za Torati! (zikiwemo Amri Kumi zilizotolewa kama utangulizi)! Hii ni amri inayoondoa kabisa ubinafsi wa dhambi ambapo, kwa mtoaji halisi, [ Jirani yake = Nafsi yake ] kwenye mambo yote!! Huu ndio mtazamo wake; hii ndiyo akili yake; hizi ndizo fikra zake; huku ndiko kufikiri kwake; hii ndiyo imani yake; hivi ndivyo anavyoenenda sikuzote, maisha yake yote! Yaani,

1) Chochote ambacho ANGEJINUNULIA YEYE MWENYEWE, anapenda/anataka/anatamani/na anafurahia KUMNUNULIA JIRANI YAKE PIA anayempenda! (jirani yake = nafsi yake)

2) Chochote ambacho ANGEJIFANYIA YEYE MWENYEWE, anapenda/anataka/anatamani/na anafurahia KUMFANYIA JIRANI YAKE PIA anayempenda (jirani yake = nafsi yake)

3) Chochote ambacho ANGEPENDA KUWA NACHO YEYE MWENYEWE, anapenda/anataka/anatamani/na anafurahia KUMPA JIRANI YAKE AWE NACHO PIA anayempenda (jirani yake = nafsi yake)

4) Chochote ambacho ANGEJIWEKEA AKIBA NAFSI YAKE YEYE MWENYEWE anapenda/anataka/anatamani/na anafurahia KUMWEKEA AKIBA JIRANI PIA anayempenda (jirani yake = nafsi yake)

5) Chochote ambacho ANGEPENDA AU ANGETAKA KUKIPATA YEYE MWENYEWE anapenda/anataka/anatamani/na anafurahia JIRANI YAKE NAYE AKIPATE KILE KILE, yule anayempenda (jirani yake = nafsi yake)

6) Chochote ambacho ANGEPENDA AU KUTAKA KUTENDEWA YEYE MWENYEWE huwa anapenda/anataka/anatamani/na anafurahia KUMTENDEA JIRANI YAKE PIA anayempenda (jirani yake = nafsi yake)!

7) Chochote ambacho ASINGETAKA YEYE MWENYEWE KUTENDEWA huwa hapendi/hataki/hatamani/na hafurahii KUMTENDEA JIRANI YAKE PIA ANAYEMPENDA (jirani yake = nafsi yake)!

>>Mtoaji halisi (real giver) ana huruma ya Yesu (Upendo) moyoni mwake na hivyo ANAJALI, ANAGUSWA, NA ANATHAMINI SANA HALI ZA WENGINE NA MAISHA YAO KIUJUMLA WAKE!

“4Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 5Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;” (Flp 2:4-5)[ New American Standard Bible
do not merely look out for your own personal interests, but also for the interests of others.

English Standard Version
Have this mind among yourselves, which is yours in Christ Jesus,

Berean Study Bible
Let this mind be in you which was also in ChrisJesus]

>>UPENDO UNAFIKIRIA WENGINE KWANZA! NA MTOAJI HALISI NI MTOAJI WA UPENDO AMBAYE ANAWAFIKIRIA WENGINE KWANZA!

>>UPENDO MWENYEWE (YESU) NDIVYO ALIVYOFANYA, NA ANAVYOTAKA KUFANYA LEO NDANI YAKO UKIMRUHUSU KWA IMANI NA UTII WAKO WA KWELI, PAMOJA NA UNYENYEKEVU NA KICHO!!!

>>Mtoaji halisi (real giver) HACHOKI KATIKA KUTENDA MEMA MAANA NDIYO MAISHA YAKE!! KILA APATAPO NAFASI ANAWATENDEA WATU WOTE MEMA NA WALA HACHAGUI WALA HABAGUI!!!

“9Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.(Gal 6:9-10)

Mpaka hapa tuko tayari kutazama malengo halisi ya KUTOA maana tumeshaona kwamba KUTOA TUNAKOZUNGUMZIA NI KUTOA UPENDO, KWA ROHO NA NGUVU ZA UPENDO, KWA AJILI YA UPENDO, PAMOJA NA UPENDO, KWA JINA LA UPENDO (YESU), KWA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA UPENDO (MUNGU)

 >>TWENDE SASA TUKAANGALIE “LENGO HALISI LA KUTOA”

2) LENGO HALISI LA KUTOA (MWISHO)

Tumekuwa tukiangalia UTOAJI WA UPENDO na jinsi ambavyo UPENDO HUU UKIWA NDANI YAKO utakavyokupelekea na wewe KUTOA KAMA MUNGU MWENYEWE (UPENDO MWENYEWE) alivyotoa. Tukaangalia,

>> UTOAJI WA MUNGU MWENYEWE AMBAYE NDIYE UPENDO (Yohana 3:16)

>> UTOAJI WAKO WEWE ULIYEJAZWA UPENDO HUO (1Yohana 3:16)

Tukaona pia kwamba UPENDO UNAJITOA VYOTE VILE ULIVYO na VYOTE ULIVYONAVYO ili kutimiza makusudi na malengo ya Upendo. Mungu (Upendo) alikusudia kwamba mioyo ya wanadamu ijazwe na Yeye mwenyewe (Upendo) ili WOTE WAISHI NA KUENENDA KATIKA PENDO LAKE! Kwa kuwa mwanadamu alimkataa Upendo na Upendo wake na kuanguka dhambini kwenye Ubinafsi na Chuki, ilimbidi Upendo ajitoe kwa ajili ya wanadamu walioasi na KUPOTEA dhambini! Yesu (Upendo wa Mungu) ALIKUJA KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KILICHOPOTEA! YAANI,

- mioyo iliyopotea kwa kujazwa ubinafsi na chuki ambavyo ni dhambi,[roho zilizopotea na zilizokufa]

-akili na mawazo yaliyopotoka + nia ovu na makusudi maovu + hisia ovu pia, [ambayo hii ni nafsi iliyopotea,]

-na miili inayomilikiwa, kutawaliwa, na kutumikishwa katika utumwa wa dhambi, tamaa mbaya, pamoja na ubaya wa kila namna; miili inayougua na yenye maradhi ya aina zote na udhaifu wa kila namna.Yote haya sivyo alivyokusudia Upendo (Mungu) iwe tangu mwanzo.

Sasa Upendo umekuja katika nguvu zake, ili kutimiza mipango, makusudi, na malengo ya Upendo NDANI YA MWAMINI ALIYEJAZWA UPENDO HUO KWA ROHO MTAKATIFU! Tukaona pia kwamba KUMPENDA MUNGU NI KULISHIKA NENO LA UPENDO WAKE (YESU); na hii hupelekea Mungu (Upendo) na Neno lake (Yesu) KUJA KUFANYA MAKAZI NDANI YAKO (Yohana 14:23). Hii inapelekea wewe umwaminiye Yesu KUISHI NA KUENENDA KATIKA UPENDO WA MUNGU NDANI YA KRISTO YESU sikuzote za maisha yako.

Sasa ni Upendo huu ndio unaokupelekea kutimiza makusudi na malengo ya Upendo maishani mwako kwa nguvu zake mwenyewe kupitia imani yako kwa Yesu (Upendo wa Mungu) kama ilivyondikwa;

“13Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” (Flp 2:13)

>> NI MUNGU (UPENDO) ATENDAYE KAZI NDANI YAKO

>> UPENDO NDIYE ANAYEKUPA KUTAKA (TO WILL) [i.e. He gives you the desire to do his will]

>> UPENDO NDIYE AKUPAYE NEEMA (NGUVU ZA UPENDO KWA ROHO MTAKATIFU WA UPENDO) YA KUYATENDA MALENGO YA UPENDO.

Utoaji halisi wa kimungu unahitaji Roho Mtakatifu na Nguvu zake za Upendo!!! Watoaji halisi lazima wawe wamejaa Roho! yaani, wamejaa Upendo! Upendo huu ni uzima tele ndani yao!! Hawa ndio wakinena, mito ya Upendo (rivers of love) hutoka ndani yao (Yoh 7:37-39). Haya ni mafuriko ya Upendo! Yaani, kikombe cha Upendo kinafurika (overflow of love from the heart) na kuwahudumia wahitaji wa Upendo ulimwenguni kote!

LENGO KUU LA KUTOA LILIFUNULIWA KWENYE BARAKA HII YA IBRAHIMU,

 

“15Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni 16akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 17katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; 18na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.” (Mwa 22:15-18)

MSTARI WA 15:

>>UPENDO MWENYEWE ANAMWITA IBRAHIMU KUTOKA MBINGUNI!!! UNAWEZA PIA NAWE UKAITWA KUTOKA MBINGUNI!!

MSTARI WA 16:

>> Mungu anamsifu Ibrahimu kwa IMANI, UPENDO, NA UTII WAKE KWAKE YEYE (UPENDO)

>> IBRAHIMU ALITENDA JAMBO KWA IMANI NA UPENDO KWA MUNGU, LILILOMGUSA MUNGU MNOOOO MOYO WAKE WA UPENDO

>>BAADA YA KUSUBIRI KWA MUDA WA MIAKA 25 KUMPATA MWANA WA AHADI (ISAKA), ALIPOJARIBIWA UNYOOFU WA UPENDO WAKE, ALIMTOA MWANAWE PEKEE ILI AWE SADAKA YA KUTEKETEZWA KWA MUNGU (UPENDO)!! Biblia inasema. “wala hukunizuilia mwanao, mwanao pekee,”

>> Mungu alikuwa anatambulisha lengo kuu la Upendo wake ulimwenguni! Alikuwa anahubiri Upendo utakaofunuliwa kwenye mwili “baadae”!! Alikuwa anaonyesha Upendo huo ulivyo na utakavyokuwa unatenda kazi ulimwenguni kupitia wanadamu waaminifu na watiifu kama Ibrahimu, WATAKAOMWAMINI, NA KUMTUMAINI, NA KUMTII MUNGU HATA KAMA HAWAELEWI MUNGU KWA NINI AMESEMA AU KUAGIZA HIVYO!!!

>> Ibrahimu alihubiri Upendo na Imani kwa Mungu miaka mingi kabla UPENDO HAJAVAA MWILI kuja duniani KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KILICHOPOTEA!

>> Ibrahimu atavihukumu vizazi vyote baada yake KUWA NI VIOVU siku ya hukumu, ikiwa watashindwa kumwamini, kumpenda, na kumtii Mungu kama vile atakavyo na apendavyo; maana ameeleza kwenye Neno lake la Upendo.

>>Vizazi vyote baada ya Yesu vitakosa cha kusema mbele ya Ibrahimu aliyetenda TENDO LILE LA IMANI, UPENDO, NA UTII PASIPO HATA KUWA NA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKE; (without even having the indwelling Holy Spirit in him) MAANA ROHO ALIKUWA BADO HAJAJA KUKAA NDANI YA WOTE WENYE MWILI WAAMINIO, KAMA NABII YOELI ALIVYOKUJA KUTABIRI BAADAE. (Yoeli 2:28-29)

>> NDIYO MAANA IBRAHIMU ALIPEWA CHEO CHA BABA WA IMANI, NA YESU NDIYE MWANZILISHI WA IMANI ILIYOFUNULIWA NAYE!!

>>UPENDO HAUMZUILII MUNGU CHOCHOTE KILE!!! IBRAHIMU ALIKUWA NA MTOTO MMOJA TU WA AHADI, LAKINI ALIPOJARIBIWA AMCHINJE KAMA SADAKA KWA MUNGU, ALIKUBALI!!! Biblia inasema Ibrahimu alishamchinja mwanawe pekee moyoni mwake, na aliamini kwamba kwa kuwa Mungu alishamwambia mataifa yote watabarikiwa kupitia yeye basi angeweza hata kumfufua Isaka kutoka kwa wafu! naye akampata tena kutoka huko kwa mfano!! Haleluya!

“17 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, 19akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano” (Ebr 11:17-19)

>> HUU NDIO UTOAJI WA UPENDO ULIOMGUSA MUNGU KIASI CHA KUMWAPIA IBRAHIMU KWAMBA LAZIMA ITAKUWA KAMA ALIVYOSEMA, ALIVYOMWAMBIA, NA ALIVYOKUSUDIA MAISHANI MWAKE, NA PIA KUPITIA YEYE, KWA UZAO WAKE BAADA YAKE!! [Ahadi ya Mungu na Kiapo cha Mungu juu yake!!! how sacred!!! how how awe-inspiring!!! how ‘sure’ and ‘certain’ the promise is! IT REALLY MUST BE EXACTLY AS IT WAS SAID!!)

>>Lakini kilichomsukuma Mungu kuahidi na kuongeza kiapo juu yake NI UTOAJI WA UPENDO WA IBRAHIMU ALIYEMWAMINI MUNGU!!

>>WEWE UNATOAJE SADAKA NA MATOLEO YAKO SIKUZOTE??!! JE! UNATOA KAMA WALE MATAJIRI WENGI WALIOTOA MAPESA MENGI SADAKA (HALAFU WAKABAKIZA NYINGI ZAIDI SANA SANA KWENYE AKIBA ZAO), LAKINI WAKAZIDIWA NA MWANAMKE MJANE MASKINI ALIYETIA SENTI MBILI ILIYOKUWA NDIYO AKIBA YAKE YOTE? [Marko 12: 41-44] (rejea sehemu ya kwanza ya somo hili) Mwanamke mjane alikuwa mtoaji halisi (real giver); na wale matajiri wengi hawakuwa watoaji halisi (they were not real givers) mbele za Mungu! Kama wewe siyo mtoaji halisi UTOAJI WAKO WOTE HAUNA THAWABU MBELE ZA MUNGU!!! MAANA HAUKUTOA KWA UPENDO!!!

“3Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, KAMA SINA UPENDO, HAINIFAIDII KITU.” (1 Kor 13:3)

1 Cor 13:3

NASB 1977
And if I give all my possessions to feed the poor, and if I deliver my body to be burned, but DO NOT HAVE LOVE, IT PROFITS ME NOTHING.

Amplified Bible
If I give all my possessions to feed the poor, and if I surrender my body to be burned, BUT DO NOT HAVE LOVE, IT DOES ME NO GOOD AT ALL”

>>DUNIA IMEJAA WENGI MASKINI KWA MATAJIRI WANAOTOA KUANZIA KWENYE NGAZI YA MTU MMOJA MMOJA, TAASISI, NA HATA TAIFA; LAKINI MBELE ZA MUNGU HAWA SIYO WATOAJI HALISI, NA UTOAJI WAO MUNGU HAUKUBALI NA HAUWALETEI WAO FAIDA AU MANUFAA YOYOTE KWA KUWA “HAWANA UPENDO WA MUNGU MIOYONI MWAO; NA HIVYO HAWAWEZI KAMWE KUTOA KWA MALENGO NA MAKUSUDI YA UPENDO!!!

>>UTOAJI WAO NI WA KIBINAFSI NA WENYE MALENGO YA KIBINAFSI!!!

MSTARI WA 17:

“17katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;”

>>KWENYE MSTARI HUU KUNA BARAKA ZA AJABU ZA KUTOA KWA UPENDO! SITAINGIA HUKO SANA ILA NITAJE TU MAENEO MATATU HAPA YA BARAKA HII YA IBRAHIMU;

1) UHAKIKA WA BARAKA TELE (ABUNDANT BLESSINGS), 2) UHAKIKA WA BARAKA ZA ONGEZEKO (BLESSING OF MULTIPLICATION), NA 3) UHAKIKA WA UZAO WAKE KUMILIKI MLANGO WA ADUI ZAO (BLESSING OF SPIRITUAL DOMINION OF HIS SEED).

 

MSTARI WA 18:

“18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.”

>>MUNGU ALIMUAHIDI IBRAHIMU BARAKA, NA KUMWAPIA KWAMBA HAKIKA YAKE LAZIMA ANGEMBARIKI KAMA ALIVYOAHIDI!

>>LENGO LA MUNGU HALIKUWA BARAKA ZILE ZIISHIE KWA IBRAHIMU TU PEKE YAKE.

>>IBRAHIMU ALIKUWA AMEKUSUDIWA NA UPENDO (MUNGU) AJE KUWA BARAKA KWA MATAIFA YOTE YA DUNIA!!

>> MUNGU ANAKUJAZA UPENDO NA ZAWADI ZA UPENDO ILI UWE BARAKA KWA MATAIFA YOTE YA DUNIA NDANI YA YESU (UPENDO KATIKA MWILI).

>>LENGO HILI LA UPENDO (MUNGU) LILITIMIA KWA KUPITIA YESU KRISTO BWANA WETU; NA LINAENDELEA KUTIMIA SASA KUPITIA KANISA (HEKALU LA ROHO WA MTAKATIFU WA UPENDO) LILILOJAZWA UPENDO WA ROHO NDANI YAKE.

“7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. 8Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.” (Gal 3:7-9) Na tena,

“13Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.” (Gal 3:13-14)

>>BARAKA YA IBRAHIMU IMEWAFIKIA MATAIFA YOTE KWA NJIA YA YESU KRISTO!!

>>UPENDO UNA MAKUSUDI NA MALENGO YANAYOKWENDA MBALI ZAIDI KUPITA WEWE MWENYEWE NA FAMILIA YAKO TU!!!

[This is to say LOVE IS INCREDIBLY FAR-SIGHTED!! LOVE GOES FAR-BEYOND YOU AND YOUR FAMILY]

>>MAKUSUDI YA UPENDO NI KUKUJAZA WEWE KWA KIWANGO CHA KUFURIKA NA KUMWAGIKA, AU KAMA ANDIKO LISEMAVYO, KUKUJAZA MPAKA KUSHINDILIWA, KUSUKWA-SUKWA, HATA KUMWAGIKA , KWA LENGO LA WEWE KUWA BARAKA KWA KIZAZI CHAKO, NA VIZAZI VYAKO VYOTE VITAKAVYOFUATA BAADA YAKO MPAKA UNYAKUO!

>>UPENDO ANAKUPA ILI UWAPE!!! NA KWA KADIRI UNAVYOWAPA NDIVYO ANAVYOKUZIDISHIA “CHA KUWAPA” IWAPO TU UMEJAA MAKUSUDI, MIPANGO, NA MALENGO YA UPENDO; AMBAYO NI KUWAPA NA KUZIDI KUWAPA SIKUZOTE!

Kwenye MST WA 16 tuliona hili Neno ambalo Mungu alimwambia Ibrahimu; “wala hukunizuilia mwanao, mwanao pekee,” ILI UWEZE KWENDA NA UPENDO; ILI UWEZE KWENDA KATIKA UPENDO; ILI UWEZE KUTIMIZA MAKUSUDI, MIPANGO, NA MALENGO YA UPENDO NI LAZIMA UISHI MAISHA YA:

[“KUTOMZUILIA MUNGU CHOCHOTE HUSUSANI VILE VYA THAMANI KUBWA KABISA UNAVYOVITHAMINI SANA (NA KWA WENGINE UNAVYOVITUMAINIA SANA- i.e. Your prized possession), NA VILE VYOTE VILIVYOMO KWENYE HAZINA YAKO YOTE TEULE ULIYOJIWEKEA HAPA DUNIANI; UKAJIWEKEE HAZINA MBINGUNI KWA KUVITOA KWA UPENDO-(GIVE AWAY IN LOVE!!)]

>>Kama hii inaonekana ni upuuzi kwako (if this appears foolish to you) basi moyo wako bado una upendo wa vitu badala ya Mungu na watu wake!! Ina maana Ibrahimu alikuwa mpuuzi kiasi cha kuitwa na Mungu ‘baba’ wa imani!!! Basi ni bora uwe mpuuzi kwenye kutoa kwako kama Ibrahimu alivyomtoa mwanawe pekee, ili utimize malengo, mipango, na makusudi ya Upendo!! Hapa ndipo WEWE NA WENGI WALIPOKWAMIA, MAANA HAWAWEZI KUPENDA KWA KIWANGO HIKI CHA IBRAHIMU, NA CHA MUNGU WETU ALIYEMTOA YESU BWANA NA MWOKOZI WETU, AMBAYE ALIUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YETU!!!

>>Nguvu ya Upendo iko kwenye SUCH SACRIFICIAL GIVING!!!  (KWENYE UTOAJI DHABIHU WA GHARAMA KUBWA NAMNA HIYO!)  Kwa maana Mungu (Upendo anataka aone moyo wako uko wapi kihalisia??!! JE! MOYO UMEJAA VITU VYA DUNIA HII VINAVYOHARIBIKA AU UMEJAA MUNGU (UPENDO)??!! Hii ndiyo inaamua sikuzote unatoaje, na unatoa nini, na kwa kiwango au kiasi gani!!!

>>Lengo la Baraka za Mungu siyo ZIJAE NA KUFURIKA KWAKO bali ZIENDE KWA WAHITAJI WA UPENDO WALIOJAA KWENYE DUNIA HII MBOVU INAYOPITA!! NI UPENDO WA NAMNA HII AMBAO TWAWEZA KUUITA ‘UPENDO WA GHARAMA KUBWA’ NDIO WENYE KUBADILISHA KWANZA MIOYO, NA MAISHA YA WENGINE!!! NA ZAIDI SANA HUFAA UNAPOELEKEZWA KWA MAADUI ZAKO!!

>>UPENDO KWA MAADUI UNA NGUVU KUBWA MNO YA KUMALIZA UADUI KABISA NA KUBADILISHA MIOYO!!

>>UPENDO WA KWELI UNATENDA ISHARA, MAAJABU, NA MIUJIZA KIROHO, KIAKILI, KIHISIA, KIMWILI, KIFEDHA, NA KIMALI NA VITU, KWA JINA LA YESU!!

[TOA KWA LENGO LA KUBADILISHA KABISA MAISHA YA MWINGINE/WENGINE KUTOKA ‘UPOTEVUNI KWAO’ KAMA TULIVYOONA KWENYE SEHEMU YA PILI YA UJUMBE HUU WA UPENDO]

>> UPENDO UNABEBA JUKUMU!! (TAKE RESPONSIBILITY) LA KUBADILISHA MAISHA.

-spiritual responsibility (jukumu la kuhudumia mahitaji ya kiroho kwa waliookoka na kwa wasiookoka).

-mental responsibility (jukumu la kuhudumia mahitaji ya kiakili kwa watoto wa Mungu na ya wengine wote).

-emotional responsibility (jukumu la kubariki hisia za waliookoka na za wengine wote).

-physical responsibility (jukumu la la kuhudumia mahitaji ya kimwili kwa Wakristo na wasio Wakristo-  yaani,ustawi wa kimwili, uponyaji na afya njema kwa wote).

-financial responsibility (jukumu la kuhudumia mahitaji ya kifedha kwa kanisa la Kristo na kwa watu wengine wote).

-material responsibility (jukumu la kuhudumia mahitaji ya mali na vitu kwa mwili wa Kristo na kwa wengine wote).

-social responsibility (jukumu la kuhudumia wengine kwa mahitaji mbalimbali kwenye jamii zote)

HAYA NI MAENEO SABA YA KUTOA UPENDO (GIVING LOVE SACRIFICIALLY) KWA WOTE, UKIANZIA NA JAMII YA WAAMINIO! LENGO KUU NI;

-kufikisha upendo huo mioyoni mwao ili na wao WAPENDE KAMA UNAVYOPENDA kwa mioyo yao (huduma kwa roho zao).

-kusababisha upendo huo ubadilishe kufikiri kwao ili nao WAWE NA MAWAZO NA AKILI YA KUPENDA KUTOKA KATIKA NENO LA MUNGU (UPENDO) [huduma kwa akili zao-mind)

-kusababisha WAONGEE MANENO YA UPENDO uliojaa ndani ya mioyo yao, maana imeandikwa kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake! (huduma kwa mioyo na vinywa vyao vinenavyo yaliyojaa mioyoni mwao).

-kusababisha nao wawe watoaji halisi WANAOPENDA KIVITENDO NA SIYO KWA MANENO MATUPU! (maisha mapya yaliyojaa Upendo wa Kristo).

 

MTIRIRIKO WA UPENDO:

 

UPENDO ULIKUWEPO MBINGUNI (Yoh 1:1)

UPENDO UKASHUKA KWENYE MWILI (YESU)-[Yoh 1:14]

UPENDO UNAKAA NDANI YA KANISA (HEKALU LA ROHO WA UPENDO)-[ 1 Kor 3:16 & 1 Kor 6:19]

KANISA LINAHUBIRI UPENDO KWA MAISHA YAKE, (MANENO NA MATENDO YAKE, AMBAO NI USHUHUDA WA UPENDO ULIMWENGUNI)[2 Kor 3:2-3 & Yoh 13:34]

UPENDO UNAAMINIWA, UNAKUBALIKA, NA UNAPOKEWA MIOYONI DUNIANI (Yoh 17:18-23 & Mdo 2:41-42,47)

>>AGIZO KUU LA BWANA WETU YESU NI AGIZO LA UPENDO, NA LIMETUTAKA KUHUBIRI UPENDO ULIMWENGUNI KOTE, KWA MAISHA YETU KAMA BARUA, KWA MAHUBIRI YETU YA UPENDO WAKE NDANI YA KRISTO YESU, NA KWA MATENDO YETU MEMA YA UPENDO KWA WATU WOTE!!!

NIMALIZIE KWA KUANGALIA PAULO ANASEMA NINI KUHUSU UTOAJI HALISI;

2 WAKORINTHO 9:6-13

“6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. 7Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. 8Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; 9kama ilivyoandikwa,

Ametapanya, amewapa maskini,

Haki yake yakaa milele.

10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; 11mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. 12Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; 13kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.”

MSTARI WA 6:

>>UKIPANDA UPENDO HABA UTAVUNA UPENDO HABA!! (Weymouth New Testament
But do not forget that he who sows with a stingy hand will also reap a stingy crop, and that he who sows bountifully will also reap bountifully.)

>>Hilo neno “stingy” ni ubahili! Ukipanda kwa roho ya ubahili maana yake unamzuilia Mungu kupanda Upendo kwa watu aliowakusudia kupitia wewe maana unang’ang’ania vitu vile ulivyoaminiwa uwakili na Mungu; na unakataa kutoa upendo; lazima utavuna hivyo hivyo pia!!!

“24Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.”

>>Unapozuia isivyo haki (kwa kutoamini na kwa kutoitii kweli) Mungu (Upendo) naye LAZIMA ATAZUKUZUILIA VITU VYAKE VYA THAMANI na kupelekea wewe KUWA MHITAJI WA UPENDO (MUNGU)

>>Uhitaji wako utajionyesha kwenye maeneo ya kiroho, kiakili, kihisia, kimwili, kifedha, kimali na vitu, au kijamii! KUNA VITU HUTAVIONA AU KUVIPATA KUTOKA KWA MUNGU! Kuna maeneo katika hayo saba hutamwona Mungu kama ambavyo ungemuona kama USINGEMZUILIA CHOCHOTE KWA KUTOKUTOA!!!

>>TAWANYA MBEGU ZA UPENDO ILI UZIDISHIWE MBEGU ZA KUPANDA!!!

>>Mungu amekumiminia pendo lake lote kwa Roho wake moyoni mwako (Rum 5:5)

>>Jukumu lako ni kutoa pendo hilo lote kwa Kanisa, na kwa watu wote wengine!

>>Mungu (Upendo) amekukirimia pia zawadi mbalimbali za Upendo kwa neema yake, ambazo zote ni mbegu za Upendo za Kupanda.

>>Jukumu lako ni kupanda mbegu hizo zote za Upendo kwenye maisha na mioyo ya wengine!

>>Kupanda Upendo kunakupelekea kuvuna Upendo zaidi toka kwa Mungu, na wanadamu pia!

>>Mungu anakuzidishia mbegu ili uzipande kwenye shamba lake kubwa zaidi! Ukubwa wa shamba lako unategemea na jinsi gani unakuwa mwaminifu kwenye zile mbegu chache anazokupa Mungu, unazipandaje? Je! unazipanda zote au unazuia mbegu na kuacha shamba lililokusudiwa kupandwa mbegu hizo likiwa NA UHITAJI WA PENDO ALIOUWEKA MUNGU NDANI YAKO NA ZAWADI ZA UPENDO ALIZOKUAMINI MUNGU UWAKILI KWA AJILI YAKE MWENYEWE!!

>>UHITAJI WOTE DUNIANI KIROHO, KIAKILI, KIHISIA, KIMWILI, KIFEDHA, KIMALI NA VITU, NA KIJAMII UNASABABISHWA NA “WACHOYO NA WABAHILI WASIO NA UPENDO WA MUNGU, AU AMBAO WAMEPEWA MBEGU ZA UPENDO WAKAZIZUIA KWA KUTOAMINI KWAO; NA SASA UHITAJI NI MWINGI AMA KIROHO, KIAKILI, KIHISIA, KIMWILI, KIFEDHA, KIMALI NA KIVITU, NA KIJAMII!!

>>Kanuni ni kupanda kwa UKARIMU NA KWA MOYO WA UKUNJUFU, KWA HIARI PASIPO KULAZIMISHWA, NA KWA WATU WOTE WAHITAJI WA UPENDO, PASIPO KUBAGUA! NA ZAIDI SANA KWA MAADUI WA MSALABA WA KRISTO, MAADUI WAKO, NA WALE WOTE WASIOPENDEKA NA WANAOCHUKIWA NA WOTE (mst wa 6 & wa 7)

>>UPENDO KAMWE HAULAZIMISHWI WALA KUTISHWA ILI  KUTOA! YEYOTE ANAYELAZIMISHWA AU KUTISHIWA LAANA YEYOTE HALAFU NDIO AKATOA HUYO HAKUTOA MBELE ZA MUNGU!! MUNGU HAKULAZIMISHWA KUMTOA YESU!! ANAPENDEZWA NA BIDII YA UPENDO KWA HIARI NA KWA MOYO WA UKUNJUFU SIKUZOTE.

 

MSTARI WA 8:

“8Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;”

Kwa kule kupanda kwa ukarimu, kwa moyo wa ukunjufu, kwa hiari pasipo kulazimishwa, unasababisha Mungu (Upendo)

>>AKUJAZE KILA NEEMA KWA WINGI,

>>ILI UWE NA RIZIKI ZA KILA NAMNA SIKUZOTE,

>>ILI UPATE KUZIDI KATIKA KILA TENDO JEMA.

-UNACHOTOA KWA UPENDO NI MBEGU ZA UPENDO UNAZIPANDA!

-UNAPANDA ILI UVUNE MBEGU ZAIDI ZA UPENDO!

-ILI MBEGU HIZO UZIPANDE ZOTE KATIKA SHAMBA LA MUNGU (ULIMWENGU ULIOPOTEA DHAMBINI), NA NYUMBA YA MUNGU (KANISA)!

-UAMINIFU WAKO KATIKA KUPANDA MBEGU ZOTE ANAZOKUPA MUNGU NDIO UNAOSABABISHA AKUJAZE MBEGU ZA KILA NAMNA; ILI UKIWA NA MBEGU HIZO ZA KILA NAMNA SIKUZOTE; UPATE KUZIDI (ABOUND) KATIKA KILA TENDO JEMA.

-HAMNA MBEGU UNAYORUHUSIWA KUIZUIA!! MAANA MUNGU HAKUKUZUILIA MWANAWE PEKEE BALI ALIMTOA KWA AJILI YAKO, NA KWA AJILI YA ULIMWENGU WOTE!

-KAMA HAULIAMINI PENDO LA MUNGU HUWEZI KAMWE KUPANDA MBEGU ZOTE!!! HII NDIYO MAANA YA KUUZA VYOTE ULIVYONAVYO MAANA MUNGU MWENYEWE (UPENDO MWENYEWE) ATAKUJAZA UPENDO TELE KWA KIWANGO CHA KUFURIKA NA KUMWAGIKA KWA ULIMWENGU WOTE, IKIWA TU MOYO WAKO HAUNA SANAMU VITU, PESA, AU MALI ZA DUNIA HII!!

>>Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE ZA UPENDO za kiroho KWA AJILI YA KANISA LAKE na KWA ULIMWENGU WOTE PIA (spiritual riches for the church and the whole world).

>>Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE ZA UPENDO za kiakili KWA AJILI YA KANISA LAKE na KWA ULIMWENGU WOTE PIA (mental wealth for the church and the whole world).

>> Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE ZA UPENDO za kihisia KWA AJILI YA MWILI WAKE na KWA ULIMWENGU WOTE PIA (emotional wealth).

>> Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE ZA UPENDO za kimwili KWA AJILI YA KANISA LAKE, na KWA AJILI YA ULIMWENGU WOTE PIA (physical wealth).

>> Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE ZA UPENDO za kifedha KWA AJILI YA KANISA LAKE, na KWA AJILI YA ULIMWENGU WOTE PIA (financial wealth).

>>Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE ZA UPENDO za mali na vitu KWA AJILI YA KANISA NA ULIMWENGU WOTE PIA (material wealth).

>>Mungu ATAKUJAZA MBEGU TELE za kijamii KWA AJILI YA KANISA LAKE NA KWA ULIMWENGU WOTE PIA [social wealth, i.e. divine connections, divine networks, rich relationships with a divine origin, God-given (love-given) social status, recognition, acceptance,  honour, respect etc for your life]

Hapa ni lazima ieleweke kwamba hakuna kujazwa kabla ya kuuza vyote ulivyonavyo!!! NI LAZIMA UTOE VYOTE KWA KRISTO KWANZA; NA KISHA KWA KANISA LAKE; NA KISHA KWA ULIMWENGU WOTE!!

Mungu kamwe hakujazi ili ubaki navyo wewe, na kisha ujivune unapojilinganisha na wengine na kujiona wewe umebarikiwa kuliko wao; na hivyo unamjua Mungu kuliko wao, au ni bora kiroho kuliko wao!! HAYA NI MAWAZO YA WAOVU WASIO NA UPENDO WA MUNGU MIOYONI MWAO MAANA UPENDO WA MUNGU HAUJIVUNI (I KOR 13:4e)! Wote wanaowaza hivi SIYO WATOAJI HALISI (REAL GIVERS)! NA WAJAPOTOA LAKINI MBELE ZAKE UPENDO HAWAJATOA, NA WANATENDA DHAMBI KWA KUTOA KWAO KIUBINAFSI!!!

>>LENGO LA KUTOA NI ILI UTOE TENA; NA KISHA UTOE TENA NA TENA! UNATOA ILI UZIDI KUTOA! UNATOA ILI UZIDI KUONGEZEWA NEEMA YA KUTOA, NA HIVYO KUONGEZEKA KATIKA KUTOA; KILA KUTOA KUNAPELEKEA KUTOA ZAIDI KWA KADIRI YA NEEMA YA KUTOA UNAYOKIRIMIWA!!

>>WALE WASIO WATOAJI HALISI HUHESABU VITU, MALI, NA PESA WALIVYOTOA (MAANA UTOAJI WAO UPO KWENYE MAENEO HAYO MATATU TU PEKE YAKE!!!), NA KISHA HUJIVUNA NA KUJISIFU!!! HUU NI UOVU!!

>>WATOAJI HALISI HUWA WANA AKILI HII;UFAHAMU HUU;MAWAZO HAYA;

“13Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (Flp3:13-14)

>>WATOAJI HALISI HUWA WANATOA NA KUTOA NA KUTOA NA KUTOA, NA KILA WANAVYOTOA WANASAHAU WALIVYOTOA HUKO NYUMA NA WANACHUCHUMILIA UTOAJI MKUBWA ZAIDI ULIOPO MBELE YAO KWA NEEMA WALIYOPEWA; HAWAJIHESABII KWAMBA SASA WAMETOA VYA KUTOSHA NA KUACHA KUTOA! WANA BIDII YA KUTOA KILA WAPATAPO NAFASI, WANATAFUTA SANA KUTOA; WANAJISHUGHULISHA NA KUTOA; WANAPOKEA KWA MUNGU ILI WATOE! WANATOA ILI WAZIDI KUTOA!! WANACHUCHUMILIA THAWABU YA UTOAJI ILIYO MBELE YAO; WANAJUA SIKUZOTE KUNA WAHITAJI ZAIDI WA UPENDO WA MUNGU!! WAHITAJI WAPO NYUMBANI KWAKO, KWENYE FAMILIA YAKO, JIRANI ZAKO, NDUGU ZAKO, KANISANI KWAKO, KIJIJINI KWAKO, TARAFANI KWAKO, KITONGOJINI KWAKO, KATANI KWAKO, WILAYANI KWAKO, MKOANI KWAKO, KWENYE MIKOA/WILAYA/TARAFA/KATA/VITONGOJI/VIJIJI VYA MIKOA MINGINE; KWENYE TAIFA LAKO; KWENYE MATAIFA MENGINE YOTE DUNIANI!!! WAHITAJI WA UPENDO WA MUNGU HAWAWEZI KWISHA MPAKA UTAKAPOONDOKA KWENYE MWILI HUU KWENDA NYUMBANI KWA BABA!!! UTOAJI WA UPENDO HAUKOMI WALA KWISHA! MUNGU AMETUWEKEA HUO ILI TUJIWEKEE HAZINA MBINGUNI KWETU, KWA MAANA ANDIKO LINASEMA TULIZALIWA UCHI NA TUTAONDOKA UCHI (Ayubu 1:21); LAKINI TUNAWEZA KUHAMISHA MFANO WA VITU VYA DUNIA HII NA KUVIWEKA KWENYE AKAUNTI ZETU JUU MBINGUNI KWENYE UTUKUFU MKUU (we transfer the spiritual equivalent of earthly possessions and materials into our spiritual bank accounts in the highest glory above! glory to Him who sitteth on the Throne of Majesty and Glory for ever and ever, amen). TUNAHAMISHA KWA UPENDO TUNAOUTOA KIVITENDO SIKUZOTE!!!

>>KAMWE HAUTOI ILI UPOKEE NA KULUNDIKA HAPA DUNIANI; BALI UNATOA ILI UWEKE HAZINA MBINGUNI: NA MUNGU ANAKUONGEZEA MBEGU ZA KUPANDA ILI UZIDI KUPANDA UPENDO!!

>>PANDA→VUNA→PANDA ZAIDI→VUNA ZAIDI→PANDA ZAIDI SANA→VUNA ZAIDI SANA→PANDA ZAIDI SANA SANA→VUNA ZAIDI SANA SANA→PANDA………..VUNA…….PANDA….VUNA, NA ZAIDI, NA ZAIDI, NA ZAIDI!!!

MSTARI WA 10

>> “10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;”

>>MUNGU ANAYEKUPA MBEGU ZA KUPANDA, NA MKATE UWE CHAKULA

>>ATAKUPA MBEGU ZA KUPANDA NAKUZIZIDISHA SANA (MBEGU TELE NI MAISHA YA UTELE-ABUNDANCE, KATIKA MAENEO SABA HAYO HAPO JUU)

>> LENGO LA KUTOA NI KUJA KUTOA ZAIDI!!!UNATOA ILI UTOE TENA! UNATOA TENA, ILI UTOE TENA NA TENA, NA HIVYO HIVYO SIKUZOTE!!!

Imeandikwa,

“35Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.” (Mdo 20:35)

>>Bwana wetu Yesu alisema, NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA!!

>>KUTOA KWA UPENDO KUNA LENGO LA KUTOA TENA NA TENA!!

>>UNATOA KWA LENGO LA KUTOA TENA NA TENA ILI KUONDOA UHITAJI WOTE KATIKA MAENEO YOTE SABA 1) KIROHO, 2) KIAKILI, 3) KIHISIA, 4)KIMWILI, 5) KIFEDHA, 6) KIMALI NA VITU, 7)KIJAMII, KWENYE KANISA LA KRISTO, NA KISHA ULIMWENGUNI KOTE!!

>> TOA ILI UTOE TENA MAANA UMEBARIKIWA KWA BARAKA YA UTOAJI NDANI YA KRISTO AMBAYO NDIYO NEEMA YA KUTOA!! KUA KATIKA NEEMA HII KWA KUTOA, NA KUTOA, NA KUTOA TENA, NA TENA, NA TENA, NA TENA SIKUZOTE, MAHALI POTE, KWA WATU WOTE, KWA NJIA ZOTE, KWA NAMNA ZOTE, MAISHA YAKO YOTE ILI UJITAJIRISHE KWA MUNGU, KWA KUNENEPESHA HAZINA YAKO MBINGUNI

 

“19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; 20bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” (Mt 6:19-21)

>>UKIWEKA HAZINA YAKO MBINGUNI MOYO WAKO UTAKUWA MBINGUNI KWA MUNGU WAKO, NYUMBANI KWAKO!!! HAPA SIYO KWAKO! WAPENDWA MUDA UBAKIO SI MWINGI!! YESU ANARUDI KULICHUKUA KANISA LILILOJAA UPENDO!! JE! UTAONDOKA HAPA UKIWA MASKINI MBINGUNI NA TAJIRI DUNIANI AMBAKO MOYO WAKO USIO NA UPENDO WA MUNGU UKO??!!  NA MOYO HUO UMEJAA VITU VINAVYOHARIBIKA VYA DUNIA HII INAYOPITA?!

>>SIKIA NDUGU YANGU; KULE ULIKOWEKA HAZINA YAKO NA AMBAKO BADO UNAWEKA LEO NDIKO MOYO WAKO ULIKO!! HUKO NDIKO KWAKO!! UKIWEKA HAZINA HAPA KWENYE DUNIA INAYOHARIBIKA NA INAYOPITA INA MAANA KWAKO NI KWENYE UHARIBIFU MILELE!! WALE WALIOJAA UPENDO NA WATOAJI HALISI WANAWEKA MBINGUNI HAZINA ZAO MAANA WANA UZIMA WA MILELE NDANI YA KRISTO, NA WANA UZIMA NA KUTOHARIBIKA ( LIFE AND IMMORTALITY) NDANI YAO!!!

>> KUTOA KWA UPENDO NDIKO KUNAKOTAKASA MOYO MAANA UNATOA VYOTE ULIVYONAVYO NA KUJAA MUNGU (UPENDO)!!!

>>UNATOA KWA KUTAPANYA!! AU KUTAWANYA!! TAWANYA ILI UKUSANYIWE KWA BABA YAKO!!! TAWANYA ILI UONGEZEWE VYA KUTAWANYA!!

“kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.” (MST WA 9)

Biblia inasema,

“11mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu” (2 Kor 9:11)

>>NIMESHASEMA KUHUSU UTAJIRI (UTELE)

>>NA SASA NASEMA TOA ILI MUNGU APEWE SIFA ZOTE, SHUKRANI ZOTE, HESHIMA YOTE, NA UTUKUFU WOTE!!

>>TOA ILI KUMTUKUZA MUNGU!! TOA ILI MUNGU AHESHIMIWE SIYO WEWE; TOA ILI MUNGU ASHUKURIWE NA SIYO WEWE; TOA ILI MUNGU ASIFIWE NA SIYO WEWE!! DHAMBI NDIYO INAPENDA KUCHUKUA SIFA ZA MUNGU, HESHIMA YA MUNGU, SHUKRANI ZA MUNGU, NA UTUKUFU WA MUNGU NDANI YAO WASIO NA UPENDO WA MUNGU; NA WANAOTOA KIBINAFSI!!!

 

MSTARI WA 12:

“12Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;

>>Utumishi huu wa HUDUMA YA UTOAJI WA UPENDO kwanza unawatimizia watakatifu riziki walizopungukiwa!!

>>Lakini zaidi sana faida yake kuu ni SHUKRANI NYINGI APEWAZO MUNGU!!

>>TOA ILI MUNGU APEWE SHUKRANI NA SIYO WEWE ULIYEPEWA NEEMA TU YA UTOAJI HUO!!

>>WATOAJI HALISI MAISHA YAO YOTE WANASABABISHA SHUKRANI NYINGI ZIMWENDEE MUNGU KUTOKA KWA WATAKATIFU WANAOHUDUMIWA NAO, LAKINI PIA NA WATU WOTE WENGINE!!

“Atoaye dhabihu za kushukuru Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.” (Zab 50:23)

>>WATOAJI HALISI WANASABABISHA MUNGU (UPENDO) ATUKUZWE SIKUZOTE NA WATAKATIFU WANAOTOA DHABIHU ZA KUSHUKURU KUPITIA UTOAJI WAO WA UPENDO!!! HII HUSABABISHA MUNGU (UPENDO) AWAZIDISHIE MBEGU ZA UPENDO ZAIDI ILI WAZIDI SANA KATIKA MATENDO MEMA!!!

MSTARI WA 13:

“13kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.”

>>TOA KWA UPENDO KWELI KWELI ILI WATAKATIFU NA WATU WOTE WAMTUKUZE MUNGU ALIYEKUJAZA UPENDO NAMNA HIYO!

>>TOA UPENDO HUO ILI WATU WAMTUKUZE MUNGU KWA KUPITIA UTII WAKO WA INJILI YA UPENDO (YESU KRISTO BWANA WETU)

>>TOA ILI WATU WAUJUE UPENDO, UKARIMU, WEMA, UTAKATIFU, NA UTUKUFU WA MUNGU NDANI YA YESU KRISTO BWANA WA UPENDO!!!

 

BADO NINGALI NINAYO MENGI YA KUSEMA, LAKINI HAYA YANATOSHA KWA HABARI YA LENGO HALISI LA KUTOA! MUNGU WA UPENDO AKUBARIKI MOYO WAKO, NAFSI YAKO, MWILI WAKO, NA MAISHA YAKO YOTE, KATIKA JINA LA YESU KRISTO BWANA NA MFALME ALIYE HAI MILELE! AMINA.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post