IWENI WATENDAJI WA NENO (BE YE DOERS OF THE WORD)

                            Word Of God Wallpapers - Wallpaper Cave

KULITENDA NENO LA MUNGU

Biblia inasema,

22Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24  Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake. (Yakobo 1:22-25)

Maisha ya Imani msingi wake wake mkuu ni KULITENDA NENO LA MUNGU! Hakuna mtu aliyeokoka kwelikweli ambaye halitendi Neno! Utii maana yake ni kulitenda Neno! Tabia zote za kiroho zinazaliwa na KULITENDA NENO! Ushindi wa msalaba ulipatikana kwa KULITENDA NENO! Kuyafanya mapenzi ya Mungu kunawezekana kwa KULITENDA NENO! Unapolitenda Neno ndipo Unayafanya mapenzi ya Mungu! Watakatifu hulitenda Neno! Watoto wa Mungu wanalitenda Neno! Kuongozwa na Roho Mtakatifu kunawezekana kwa KULITENDA NENO! Kwa sababu huyo Roho hutuongoza hatua zetu katika Neno la Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu!

133 Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki. (Zaburi 119:133)

Roho Mtakatifu anaonyesha kwa andiko hili kiu ya mtoto wa Mungu na njaa ya mtakatifu ya kuyafanya mapenzi ya Mungu KWA KULITENDA NENO LA MUNGU! Na ndiyo maana anaomba hatua zake zielekezwe katika Neno la Mungu lililo takatifu sana, ili aishi na kuenenda kwalo, ambayo ndiyo maisha ya utakatifu yaliyo mbali kabisa na uovu wa aina yoyote! Usafi wa moyo unaletwa na KULITENDA NENO na siyo kulisikiliza tu au kulisoma tu peke yake. Utukufu wa Mungu upo katika utendaji wa Neno na siyo vinginevyo! Maisha ya rohoni ni maisha ya KULITENDA NENO! Kulitenda Neno ndiyo hekima ya Mungu!

24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa(Mathayo 7:24-27)

-Wenye hekima na akili HULITENDA NENO

-Wapumbavu husikia halafu HAWATENDI WALICHOSIKIA

Mbinguni hamna upumbavu wala wapumbavu! Hawa sehemu yao ni kwenye ziwa liwakalo moto na kibiriti.

Kukua kwako kiroho, kukomaa kwako kiroho, kuishi kwako kiroho, kumzalia Mungu matunda yakaayo, kufanikiwa kwako, utakatifu wako, upendo wako, uchaji Mungu wako, kushinda kwako vita vya kiroho, kumpendeza Mungu kwako, kujibiwa kwako maombi, ushirika wako na Roho Mtakatifu, kiwango cha nguvu za Mungu zitendazo kazi maishani mwako, kiwango cha upako uliomo katika maisha na huduma yako, utukufu wa Mungu uliokufunika, mafunuo na uelewa wa Neno la Mungu ulionao, udhihirisho wa Roho Mtakatifu kwenye maisha na huduma yako, uzima wa milele, uponyaji wa mwili, ishara, maajabu na miujiza kwenye maisha na huduma yako, na mengi mengineyo, YOTE HUPATIKANA NA PIA HUONGEZEKA MAISHANI MWAKO KWA KULITENDA NENO LA MUNGU! NA PIA HUPUNGUA KWA KUTOLITENDA KWAKO NENO!

                     HATUA ZA KULITENDA NENO

1) HATUA YA ANDIKO:

Hii ni hatua muhimu ya kulisoma sana Neno kwa bidii yote, na pia kulisikiliza kwa umakini wote linapofundishwa au kuhubiriwa. Tabia ya mtendaji wa Neno ni hii hapa:

2Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. (Isaya 66:2)

-MTU ALIYE MNYONGE

-MWENYE ROHO ILIYOPONDEKA

-ATETEMEKAYE ASIKIAPO NENO LA MUNGU

Mtu wa namna hii hulipokea Neno kwa unyenyekevu wote na hofu na KULISHIKA!!!

23Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. (Yohana 14:23)

2) HATUA YA MAOMBI:

Hii ni hatua nyingine muhimu sana ya kuomba rehema na neema (Waebrania 4:16) ya Mungu ili kuwezeshwa kulitenda Neno kwa Roho Mtakatifu na Nguvu zake! (Zaburi 105:4 & Matendo 10:38).

Ni lazima kuomba mkono wa Mungu uwe juu yako kwa sababu Yesu alisema,

5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote (Yohana 15:5)

…… MAANA PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI NENO LOLOTE! MAPENZI YA MUNGU HUFANYWA KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU PEKEE!

Tuliokolewa kutoka katika NGUVU ZA GIZA kwa NGUVU ZA MUNGU!

13Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; (Wakolosai 1:13-14)

Ufalme wa Mungu una NGUVU ZA MUNGU ambazo ziliushinda ufalme wa giza na NGUVU ZAKE ZA GIZA! Leo hii tunaishi kwa NGUVU ZA MUNGU huku tukilindwa na NGUVU hizo!

5Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. (1 Petro 1:5)

Na Yesu ndiye Nguvu ya Mungu kwetu kama ilivyoandikwa;

“23bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; 24bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.” (1 Kor 1:23-24)

Katika ulimwengu wa roho kuna nguvu hizi mbili tu zinazotenda kazi! Hivyo wote walio katika ufalme wa Mungu huishi, kuenenda na kutenda kazi kwa NGUVU ZA MUNGU! Halikadhalika ufalme wa giza vivyo hivyo! Hivyo tunapoongelea Ufalme wa Mungu tunaongelea NGUVU ZA MUNGU kwa maana,

20Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. (1 Wakorintho 4:20)

Na hii ndiyo maana Mungu alitupa Roho Mtakatifu na NGUVU zake kama maandiko yasemavyo (Matendo 1:8). Hii ina maana KULITENDA NENO kunahitaji NGUVU ZA MUNGU KWA ROHO WAKE MTAKATIFU KUPITIA IMANI KATIKA NENO LA KRISTO! Sasa hatua hii ya pili ya kulitenda Neno ya maombi ni ya muhimu na ya lazima kama alivyosema Yesu PASIPO MIMI NINYI HAMUWEZI NENO LOLOTE! (Yohana 15:5c)! Anachosema Bwana hapa ni kwamba PASIPO NGUVU ZANGU MTASHINDWA NA NGUVU ZA GIZA! Hivyo ni lazima kuomba rehema na neema kama ulivyo  mwaliko alivyoutoa wa kuja kwenye kiti cha nehema wakati wowote ule! (24/7)

16Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. (Waebrania 4:16)

Tunahitaji rehema zake maana Mungu huwa hatutendei kwa kadiri ya makosa yetu, kushindwa kwetu, udhaifu wetu, mapungufu yetu na hata dhambi zetu! Kwa sababu ya wingi wa huruma zake kwetu sisi watoto wake! HIZI NI REHEMA ZAKE AMBAZO HUWA HAZIKOMI

22 Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. (Maombolezo 3:22)

TUNAHITAJI REHEMA ZA MUNGU KILA IITWAPO SASA!!!

Na nguvu za Mungu huja kwetu na kutenda kazi ndani yake kama NEEMA yake kwetu! Neema maana yake Roho Mtakatifu na Nguvu zake akitenda kazi ndani yako, na pia kupitia wewe kwa wengine! Imeandikwa si kwa uwezo wala kwa nguvu zako bali ni kwa Roho wake (Zecharia 4:6). Roho Mtakatifu ni Roho wa Neema, maana tumeokolewa kwa neema na wala si kwa matendo! (Waefeso 2:8-9) Ukifanya mambo ya Mungu pasipo Neema yake unakuwa unaikana Neema yake! Maisha na huduma vya Mkristo aliyeokoka ni kwa Neema ya Mungu na si vinginevyo!!!

11Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; (Tito 2:11-13)

TULIOKOLEWA KWA NEEMA, NA TUNAISHI KWA NEEMA HIYO HIYO!!! Tunaomba neema ya kulitendea kazi Neno ili tusifanye mambo ya Mungu kwa nguvu za kimwili! Hii inatufundisha unyenyekevu mbele za Mungu maana yeye huwapa neema wanyenyekevu tu!(1 Petro 5:5)

3) HATUA YA IMANI AU UKIRI:

Biblia inasema,

24Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, AMININI ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. (Marko 11:24)

Tunapoomba neema ya kulitenda Neno ni lazima tuamini kwamba tunapokea hiyo neema wakati huohuo tunapoendelea kuomba! Hii ina maana tunamaliza maombi tukiwa tumepokea neema! Ni muhimu kutamka kwamba “asante Baba ninapokea neema ya……” Hapa nitoe mifano kidogo!

 

 

1) Andiko:

21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? 22Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. (Mathayo 18:21-22)

2) Maombi:

Baba katika jina la Yesu, umeagiza nimsamehe ndugu mpaka saba mara sabini,na siyo mara saba tu kama Petro alivyokuuliza; najua huu ni msamaha usio na kikomo wala mwisho, na kwamba mimi peke yangu siwezi kamwe kusamehe namna hii; naomba unirehemu kwa kutosamehe namna hii huko nyuma; naomba sasa unikirimie neema yako ili niweze kuishi sawasawa na andiko hili nikisamehe watu wote, makosa yao yote, sikuzote, mahali pote pasipo kukoma, kughairi, kuchoka wala kuacha! naomba ee Bwana unijalie neema hii sawasawa na neno lako kwenye Waebrania 4:16 ambapo umenialika nije kwa ujasiri kwenye kiti chako cha neema! Bwana Yesu asante kwa neema yako hii ya ajabu; ninapokea sasa neema hii ya kusamehe sabini mara saba katika jina la Yesu! Roho Mtakatifu nisaidie kuliishi na kulitenda neno hili sikuzangu zote! Amina.

3) Imani na ukiri:

Kwa habari ya Imani na ukiri wa Imani Biblia inasema,

-Tunapoomba tuamini kwamba tunapokea yale tunayoyaomba nayo yatakuwa yetu (Marko 11:24)

-Tunapoomba sawasawa na mapenzi ya Mungu anatusikia, na tukijua anatusikia tunajua kwamba tunazo haja tulizomwomba (1Yohana 5:14-15)

Hii ina maana unapoomba unaondoka na jibu la maombi yako! Yaani, unakuwa umepokea haja zile ulizomwomba Mungu, na hivyo ni muhimu kumaliza maombi yako kwa kushukuru kwamba umepokea kile ulichokuwa unaomba! KUOMBA NAMNA HII NI LAZIMA KUWE SAWASAWA NA NENO LA MUNGU! Hakuna maombi ya Imani yasiyokuwa na msingi wake katika Neno! UKIOMBA KWA IMANI NI LAZIMA UONDOKE KWENYE MAOMBI UKIWA UNAZO ZILE HAJA ULIZOMWOMBA MUNGU! USIPOOMBA KWA IMANI HAUTAKUWA NA MSINGI WA KUOMBA KWAKO KATIKA NENO, NA KISHA UTAKUWA UNAMSUBIRI MUNGU AJIBU! BIBLIA INAFUNDISHA KWAMBA TUNAENENDA KWA IMANI SI KWA KUONA!!!(2 Wakorintho 5:7). Kama unasubiri uone kwa macho ya nyama ili useme Mungu amejibu WEWE HAUMWAMINI MUNGU NA USITEGEMEE KUPOKEA KITU KWAKE!!Kwa maana imeandikwa ukimwendea Mungu ni lazima UAMINI kwamba yupo naye HUWAPA thawabu wale wamtafutao! (Waebrania 11:6)

Sasa baada ya kupokea ndipo unapoendelea na ukiri wa Imani! Na kwa mfano wetu wa kusamehe saba mara sabini, baada ya maombi yetu sasa ninaamini kwamba mimi NINASAMEHE SABA MARA SABINI! Yaani, naamini kwamba sasa ninasamehe pasipo kikomo, bila kujali nimekosewa mara ngapi, au nimekosewa kosa gani, au na mtu yuleyule au na mwingine au wengine! Unaweza kuona haraka haraka kwamba msamaha wa kimwili una kikomo, una makosa usiyoweza kusamehe, na unaweza kutoweka ghafla na kubaki uchungu moyoni!

ASANTE YESU KWA KUNIPA NEEMA YA KUSAMEHE WATU WOTE, MAKOSA YOTE, MAHALI POTE, WAKATI WOTE, SIKU ZOTE MAISHANI MWANGU!

UNATAKIWA KUENDELEA KUKIRI HIVI HATA WAKATI HUJIONI HIVYO NA PIA KILA WAKATI UNAPOANZA KUUMIA KWAMBA KWA NINI FULANI AMEKUTENDEA HIVI AU VILE! KIRI MPAKA IUMBIKE HIVYO NDANI YAKO NA UTAJIKUTA UNAISHI HIVYO KWA NEEMA YA MUNGU! UNAPOKIRI HIVYO UNAMFANYA MUNGU AACHILIE NEEMA YAKE ULIYOIOMBA KWAKE! UTAJIKUTA UNASAMEHE, NA KUSAMEHE, NA KUSAMEHE KAMA BWANA WETU YESU KRISTO ALIVYOWASAMEHE! ”BABA UWASAMEHE MAANA HAWAJUI WALITENDALO”

Kwa kila andiko uliloliamini ni lazima utapitia hatua hizi, na huku ndiko kulitenda Neno hatua ya tatu! Hatua hii inakuhamisha mwilini maana sasa unaamini Neno na unajiona vile Neno linavyosema wewe uko, unajiona unatenda vile Neno lisemavyo, unajiona ndani ya Neno na Neno ndani yako! Wewe sasa unakuwa sehemu ya Neno na unaishi na kuenenda kwa Neno na si kwa kuangalia hali za macho zilizopo na zinazoonekana!

4) HATUA YA MAMLAKA YA MWAMINI:

Bwana wetu Yesu alisema,

19Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. (Luka 10:19)

NENO HILI AMRI KWENYE TAFSIRI NYINGI ZA LUGHA NYINGINE NI NGUVU (POWER) NA NYINGI ZAIDI NI MAMLAKA (AUTHORITY); HIVYO NIKIYACHUKUA HAYA PAMOJA NAWEZA KUSEMA;

NIMEWAPA [MAMLAKA YA NA NGUVU ZA] KUKANYAGA NYOKA NA NG’E, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, WALA HAKUNA KITU KITAKACHOWADHURU!!!

Watoto wa Mungu wana mamlaka juu ya ufalme wote wa giza na nguvu zake zote za giza! Bwana wetu Yesu alimshinda shetani pale juu msalabani kwa ajili yako wewe uliyeokoka! Ule ushindi wake dhidi ya shetani akakupa wewe! Wewe ni mshindi ndani yake Yesu; Yesu amekuweka juu sana ya shetani kimamlaka na nguvu katika ulimwengu wa roho. Paulo alieleza nguvu na uweza wa ajabu aliotukirimia Yesu ambao tunapaswa kuujua na kuuelewa:

17Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; 18macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 19na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; 20aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote. (Waefeso 1:17-23)

MST 19-21:

Roho Mtakatifu anatuombea hapa ili tujue

-UBORA WA UKUU WA UWEZA WAKE/NGUVU ZAKE NDANI YETU TUAMINIO JINSI ULIVYO

-KWAMBA NGUVU/UWEZA WAKE HUO NDIO ULIOMFUFUA KRISTO KATIKA WAFU

 -UWEZA HUO UMEMWEKA KRISTO MKONO WA KUUME WA MUNGU BABA MWENYEZI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, JUU SANA KULIKO UFALME WOTE, MAMLAKA, USULTANI, NGUVU, NA KILA JINA (AU CHEO) LITAJWALO KATIKA ULIMWENGU HUU NA ULE UJAO PIA. (WEWE UNAYEAMINI UKO JUU SANA KULIKO UFALME WA GIZA WOTE NA NGUVU ZOTE ZA GIZA MAANA UKO NDANI YA YESU)

Waefeso 2:6 inasema tulifufuliwa pamoja naye na kuketishwa pamoja naye mkono wa kuume wa Baba katika ulimwengu wa roho.

MST 22-23:

-MUNGU AMEVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YA KRISTO KWA AJILI YA KANISA ILI KRISTO AWE KICHWA JUU YA VYOTE. HII NI MAMLAKA JUU YA UUMBAJI WOTE NA SI JUU YA MASHETANI TU PEKE YAKE. HAKIKA KRISTO AMEREJEZA UTAWALA NA UMILIKI ALIOPOTEZA ADAMU BUSTANINI EDENI KWA KANISA (HEKALU LA ROHO MTAKATIFU)

Kuelewa mamlaka hii kimaandiko, katika Roho Mtakatifu, ni muhimu na lazima ili kuweza kutembea katika mamlaka hiyo na kuyafanya mapenzi ya Mungu katika Ufalme wa Mungu. Ufalme wa Mungu maana yake NGUVU ZA MUNGU ZINATAWALA! (1 Wakorintho 4:20). Pasipo NGUVU ZA MUNGU basi nguvu za giza zinatawala! Pia KWA KIWANGO KILE NGUVU ZA MUNGU ZIMEPUNGUA BASI NGUVU ZA GIZA ZINATAWALA! NGUVU ZA MUNGU NDIZO ZINAZOSABABISHA NURU YA UTUKUFU WA MUNGU ING’AE NA WANADAMU WAUONE UTUKUFU WA MUNGU! (2 Wakorintho 4:4,6). Msingi wa NGUVU ZA MUNGU ni Imani Iliyo Hai katika Neno la Mungu!!! Kwa maana Biblia inasema kwa habari ya Neno kwamba,

12Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. (Waebrania 4:12-13)

-NENO LA MUNGU LI HAI

-NENO LA MUNGU LINA NGUVU

-NENO LA MUNGU NI UPANGA WA ROHO UKATAO KUWILI

-NENO LA MUNGU LINACHOMA MOTO DHAMIRI MBAYA NA MIOYO YENYE DHAMBI

-NENO LA MUNGU LINAYATAMBUA MAWAZO NA MAKUSUDI YA MIOYO YOTE

-VIUMBE VYOTE VIKO WAZI MBELE ZA NENO LA MUNGU

-VIUMBE VYOTE VIKO UCHI NA VIMEFUNULIWA MBELE YA NENO LA MUNGU

-BWANA WETU YESU KRISTO NI NENO ALIYE HAI LEO AMBAYE ALIFANYIKA MWILI (YOHANA 1:14)

-UKIMWAMINI ANATENDA KWA NGUVU ZAKE KUPITIA KWA ROHO WAKE!!!

Yesu amemaliza yote kuhusu shetani! Ameshamshinda! Ameshamnyang’anya funguo za kuzimu na mauti, JUKUMU LIMEBAKI KWAKO UNAYEAMINI KULITENDA NENO NA KUENENDA KATIKA USHINDI WA MSALABA!

 

 

Biblia inasema,

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu (Ufunuo 1:17-18)

Yesu amekupa pia funguo za Ufalme wa Mungu ili uweze kufunga na kufungua kama mbinguni wanavyofunga na kufungua!!

18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. (Mathayo 16:18-19)

Na tena,

18Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. (Mathayo 18:18)

Hiyo Mathayo 16:18 inasema wazi KANISA HALIWEZI KUSHINDWA NA MILANGO YA KUZIMU! KUZIMU NA MAUTI HAVINA NGUVU TENA KWA MKRISTO ANAYEAMINI! Kuelewa haya ni muhimu ili uweze kutembea katika mamlaka kamili juu ya ufalme wote wa giza! Imeandikwa watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa! (Hosea 4:6) Hivyo kukosa maarifa maarifa sahihi kunapelekea kushindwa vita vya kiroho dhidi ya ufalme wa giza! Mamlaka ya mwamini ipo ili kulinda ushindi wetu wa msalaba tuliopewa na Kristo Yesu Bwana wetu; maana Yesu ALIMALIZA YOTE! Biblia inasema,

15 Na baada ya kuvunja nguvu na mamlaka ya shetani, Mungu alimfedhehesha hadharani kwa kuonyesha ushindi wa msalaba juu yake. (Wakolosai 2:15)

15 And having disarmed the powers and authorities, he made a public spectacle of them, triumphing over them by the cross. (Colossians 2:15 NIV)

-YESU AMEVUNJA NGUVU NA MAMLAKA YA SHETANI JUU YA WANADAMU NA UUMBAJI WOTE!!!(JE! UNAAMINI HILI? UNALIPOKEAJE?)

-YESU AMEMNYANG’ANYA SHETANI NA MAJESHI YAKE SILAHA ZAO ZOTE PALE MSALABANI!!!(TAFSIRI YA NIV)

-SHETANI NA MAJESHI YAKE WAMEFEDHEHESHWA NA KUAIBISHWA PALE JUU MSALABANI NA BWANA WETU YESU KRISTO!!!

-HIVYO WEWE MTOTO WA MUNGU UNA ADUI AMBAYE HANA NGUVU WALA MAMLAKA JUU YAKO TENA; NA NI ADUI AMBAYE SILAHA ZAKE AMENYANG’ANYWA TAYARI, HIVYO UKO SALAMA DHIDI YAKE MAANA HANA SILAHA YA KUTUMIA DHIDI YAKO ISIPOKUWA “UDANGANYIFU” ILI AKUIBIE NENO, AHARIBU UPENDO WAKO NA KUUA IMANI YAKO (YOHANA 10:10 a).

-UNAPOISHI NA KUENENDA KATIKA KWELI SHETANI NA MAJESHI YAKE HAWAWEZI KITU DHIDI YAKO (POWERLESS AGAINST YOU)

Kwa hiyo siri ya mamlaka ya mwamini kutenda kazi ni UTII WAKO NA UAMINIFU WAKO KWA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU!

Biblia inasema,

19Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. 20Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. (Warumi 16:20)

-NI LAZIMA UWE MTII WA NENO LA MUNGU LOTE

-UKIWA MTII NAMNA HIYO UTAKUWA MWENYE HEKIMA KATIKA MAMBO MEMA

-NA UTAKUWA MJINGA KATIKA MAMBO MABAYA

-NDIPO MUNGU ATAMSETA SHETANI SHETANI UPESI CHINI YA MIGUU YAKO MWANA WA MUNGU

Hii haimaanishi kwamba Mungu hajamseta shetani bado, bali anamaanisha ili wewe mwamini uone mamlaka ya Kristo inatenda kazi ndani yako kiukamilifu unahitaji kuwa MTIIFU sawasawa na maandiko yasemavyo! Kule kumseta shetani chini ya miguu yako kulikamilika msalabani kama tulivyosoma katika WAEFESO

22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo (Waefeso 1:22)

-UTII WAKO KWA KRISTO UNALETA KUSETWA HUKU (KUTIWA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKO) NDANI YA MAISHA NA HUDUMA YAKO WEWE BINAFSI NA WATU WOTE KUONA KWA MACHO UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA MUNGU WAZIWAZI!!!

MUHIMU:

-HAPA IELEWEKE WAZI KWAMBA MAMLAKA YA MWAMINI HAIKO KWENYE KUKEMEA KWA SAUTI KUBWA NA KWA NGUVU SANA NA BIDII, BALI KATIKA UTII, UNYENYEKEVU NA KICHO MBELE ZA MUNGU

- ANAYEAMINI NI MNYENYEKEVU

- ANAYEAMINI ANA HOFU YA MUNGU/ANAMCHA MUNGU

- ANAYEAMINI NI MTIIFU SIKUZOTE

HUYU ANA NEEMA YA MUNGU MAISHANI MWAKE YENYE KUMWEZESHA, KAMA MAANDIKO YASEMAVYO,

“10angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.” (Yeremia 1:10)

-KUNG’OA UFALME WA GIZA KILA MAHALI ULIPO

-KUBOMOA UFALME WA GIZA KILA MAHALI ULIPO

-KUHARIBU KAZI ZA SHETANI KILA MAHALI

-KUANGAMIZA MIPANGO, HILA, MAFICHO, KAMBI, KAZI NA MAKUSUDIO YA UFALME WA GIZA KILA MAHALI

-KUJENGA NA KUPANDA UFALME WA MUNGU DUNIANI KOTE

Na hivyo kuwa, kama andiko linenavyo, RUNGU LA BWANA

“20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; 21na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; 22na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; 23na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.” (Yeremia 51:20-23)

-MAMLAKA YAKO MWAMINI NI KUFANYA KAZI HIZI HAPA KWENYE ANDIKO KWA KADIRI YA NEEMA YA MUNGU ULIYOJALIWA!

Kumbuka tunaongelea hatua za kulitenda Neno katika kipengele cha mamlaka ya mwamini. Hii mamlaka ni ya lazima maana shetani yupo kupinga ingawa ameshindwa! Tunachofanya ni KULINDA NA KUSIMIKA USHINDI WETU WA MSALABA KATIKA MAENEO YA MILKI YETU HAPA DUNIANI KAMA WAFALME NA MAKUHANI KWA MUNGU WETU AMBAO TUNATAWALA PAMOJA NA KRISTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, 10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. (Ufunuo 5:9-10)

Na tena,

9Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; (Waefeso 5:8)

-KWA MAMLAKA TULIYONAYO NDANI YA YESU SISI NI WATAWALA JUU YA NCHI!!! TUMEWEKWA ILI KUSABABISHA MAPENZI YA MUNGU YAFANYIKE HAPA DUNIANI KAMA MBINGUNI!

-TUMEWEKWA HAPA ILI TUUENEZE NA KUUSAMBAZA UFALME WA MUNGU DUNIANI KOTE

-UFALME WA MUNGU NI WA ROHONI, NA KUTOKEA ROHONI TUNAMILIKI NA KUTAWALA MPAKA MWILINI

-TUKO JUU SANA YA MAMLAKA ZOTE ZA GIZA, NA ZA WANADAMU, NA TUNA NGUVU NA UWEZO WA KUAMURU CHOCHOTE NA KUBADILISHA MFUMO WOWOTE ILI ULETE FAIDA KWA KANISA NA UFALME WA MUNGU HAPA DUNIANI

-TUNAFANYA HAYA YOTE KATIKA USHIRIKA NA BABA NA MWANA NA MSINGI WAKE NI UTII WETU WA KWELI; HII NDIYO MAMLAKA YAKO:

21Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake (Yohana 14:23)

-MAMLAKA YA KRISTO IKITENDA KAZI NDANI YAKO NI LAZIMA UTUKUFU WA MUNGU UONEKANE KWA KUPITIA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA MUNGU KWENYE KUYAFANYA KWAKO MAPENZI YAKE NA PIA KWENYE KUHARIBU KAZI ZA SHETANI!!!

5) HATUA YA KUNGOJEA:

Matumizi ya mamlaka ya mwamini katika kipengele kilichopita ni ya sikuzote na wakati wote! Kwa maana adui yupo sikuzote kujaribu kupinga ama kuzuia, na hata kuchelewesha mapenzi ya Mungu kutimizwa katika maisha ya mwamini! Hivyo kwa kujua mamlaka yako juu yake na urithi wako ndani ya Kristo ni lazima kumfukuza, kumng’oa, kumwondoa, kumtoa, kumkemea, kumharibu n.k kwa jina la Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu. Sasa baada ya kutumia mamlaka hiyo katika eneo husika ni lazima ujue kwamba Mungu analiangalia Neno lake na kulitimiza, na hivyo yupo kazini AKIFANYA VILE ULIVYOAMURU/ULIVYOKEMEA/ULIVYOTAMKA/ULIVYOKIRI N.K

Ni muhimu sana kujua pia kwamba Mungu awapo kazini huwa hatazami mambo kama wewe kwa macho yako ya damu na nyama! Na mara zote itaonekana hamna kilichobadilika au kilichotokea!!! Na mara nyingi utakuta mambo yanazidi ama kuharibika ama kuwa magumu zaidi!!! Na wakati mwingine utasubiri sana mambo huku hali zikiwa kinyume nawe, na Mungu haonekani kabisa kufanya lolote! Unaweza kushambuliwa na ugonjwa, au kupata hasara, au kufukuzwa kazi, au kufilisika, au kudharauliwa, au kunyanyaswa, au kupuuzwa, au kudhulumiwa, au kushindwa, au kufeli, au kusingiziwa, au kuteswa, au kutendwa mabaya, au kuaibishwa, au kuachwa, au kuishiwa, au kukosa ulichotamani, au kutopata ulichotaka, au kutengwa n.k WAKATI WEWE UNAJUA HAYO SIYO MAPENZI YA MUNGU KWAKO KWA MUJIBU WA MAANDIKO!!! Na tena haya yanaweza kuendelea kwa muda mrefu kiasi cha wewe kuchoshwa na kuona sasa imezidi kiasi! Lakini kama umefuata hatua hizi tulizoeleza kwa uaminifu na bado unayafanya hayo basi jua ya kwamba Mungu ni mwaminifu na kamwe hajakuacha! Na lazima atakutokezea na kukupatia haja ya moyo wako ila  pengine ni kwa namna tofauti na ulivyofikiri! Muhimu ujue tu kwamba:

a) 19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? (Hesabu 23:19)

-MUNGU KAMWE HASEMI UONGO

-ALICHOKISEMA ATAKITENDA

-ALICHONENA ATAKITIMIZA

b) 14Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. 15Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. (Isaya 49:14-15)

-MUNGU HAJAKUSAHAU NA HAWEZI KAMWE KUKUSAHAU

-MUNGU HAWEZI KAMWE KUKUACHA

c) 5Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. (Waebrania 13:5)

-MUNGU HAWEZI KAMWE KUKUACHA WALA KUKUPUNGUKIA

d) 6Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; (Wafilipi 1:6)

-MUNGU AMEANZA KAZI MOYONI MWAKO AMBAYO LAZIMA ATAIMALIZA ILI HATIMAYE UFANANE NA YESU MWENYEWE!! USIJIHUKUMU WALA USIJIANGALIE ULIVYO LEO! JIANGALIE NENO LINAVYOKUONA!

e) 31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha. (Maombolezo 3:31-33)

-MUNGU KAMWE HAWEZI KUMTUPA MTU WAKE (MWANAWE) MILELE

-ATAMPITISHA KWENYE VIPINDI VYA HUZUNI LAKINI ATAMREHEMU KWA KADIRI YA WINGI WA REHEMA ZAKE

-MOYONI MWAKE MUNGU HAPENDI (ANACHUKIA)KURUHUSU UPITE KWENYE MATESO WALA HUZUNI!

-ILA USITESWE KWA SABABU YA KUTENDA MABAYA!!!

15Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 16Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo (1 Petro 4:15-16)

f) 25 BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu. (Maombolezo 3:25-26)

-NI MAPENZI YA MUNGU WEWE KUNGOJEA UTULIVU UTIMILIFU WA AHADI ZAKE NA NENO LAKE

-WAKATI WA KUNGOJEA NI VEMA KUMTAFUTA MUNGU KATIKA MAENEO USIYOELEWA VIZURI AU UNA MASHAKA NAYO ILI AKUFAFANULIE

-UKIMNGOJEA BWANA UTAUONA WEMA WAKE WOTE

-NI VEMA BASI KATIKA KUNGOJEA UKAWA UKITARAJIA KUPOKEA TOKA KWAKE SAWASAWA NA ULIVYOAMINI NA KULITENDEA KAZI NENO ULILOLIAMINI

-NI VEMA KUMNGOJEA MUNGU KWA UTULIVU BADALA YA KUHANGAIKA HUKU NA KULE, AU KUJIHANGAIKIA WEWE MWENYEWE KWA NJIA ZA KIBINADAMU AMBAZO ZOTE HUMLETA “ISHMAELI BADALA YA ISAKA”!!!

24Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? 25Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi. (Warumi 8:24-25)

-TARAJIA! MNGOJEE BWANA KWA SABURI!

13 Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, 14akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. 15Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. (Waebrania 6:13-15)

-IBRAHIMU, KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI!

10Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. 11Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho; 12ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu. (Waebrania 6:10-12)

-AHADI ZOTE ZA MUNGU ZINARITHIWA KWA IMANI NA UVUMILIVU, NA SI IMANI PEKE YAKE!

-HIVYO HATUA YA MWISHO YA KULITENDA NENO NI KUNGOJEA KWA UVUMILIVU! KUNGOJEA KWA SABURI!

IMANI + UVUMILIVU = KURITHI AHADI

NENO HILI ULIKUMBUKE SIKUZOTE, KWAMBA PALE UNAPOONA HAMNA KINACHOENDELEA, MAMBO YAMEHARIBIKA AU YANAHARIBIKA, NA MUNGU HAONEKANI KUSHUGHULIKA, UJUE MUNGU YUKO KAZIN AKISHUGHULIKIA YALE ULIYOYAAMINI. TANGU MWANZO MUNGU HAJAWAHI KUPUMZIKA BALI ANASHUGHULIKIA UTIMILIFU WA AHADI ZAKE NA NENO LAKE KATIKA DUNIA YOTE KWA VIZAZI VYOTE!

“17Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.” (Yohana 5:17)

Baba na Mwana yuko kazini! Roho na Neno lake yuko kazini kwa nguvu zake kushughulikia yote uliyoyaamini, uliyoyapokea, unayoyamiliki rohoni mwako, uliyo na uhakika nayo,  na unayoyayatarajia! Maana imani ni kuwa na uhakika na mambo uyatarajiayo, bayana ya mambo yasiyoonekana. (Waebrania 11:1)

>>YOUR STEADFAST FAITH KEEPS THE LORD OF HOSTS BUSY IN THE HEAVENLIES! HE IS WORKING NON-STOP AND ROUND-THE-CLOCK FOR YOU!

“16Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; 17(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. 18Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 19Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. 20Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; 21huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. 22Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki. 23Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; 24bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; 25ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.” (Warumi 4:16-25)

Ubarikiwe na Bwana Yesu        

 Word Of God Wallpapers - Wallpaper Cave

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post