DIVAI MPYA KWENYE KIRIBA KIPYA*



 *DIVAI MPYA KWENYE KIRIBA KIPYA* 

37 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama akitia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe itamwagika, na viriba vitaharibika. 

Luka 5:37

>> BIBLIA INASEMA HAKUNA MTU MCHA MUNGU ANAYEMTII MUNGU NA KUIAMINI BIBLIA AMBAYE ANAWEZA KUTIA DIVAI MPYA KWENYE KIRIBA KIKUUKUU!! SABABU NI KUWA ILE DIVAI MPYA ITAKIHARIBU KILE KIRIBA KIKUUKUU NA KISHA ITAMWAGIKA! DIVAI MPYA INATAKA KIRIBA KIPYA!!! ( Luka 5:38). HIVI NDIVYO MAMBO YA MUNGU YANAVYOKWENDA! Biblia inasema pia,

39 Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema. 

Luka 5:39

>> NA YEYE ANYWAYE DIVAI YA KALE HAWEZI KUTAMANI DIVAI MPYA MAANA HUSEMA ILE YA KALE NDIYO ILIYO NJEMA!!

>> TUKIELEKEA MWAKA MPYA LAZIMA UFANYE MABADILIKO YA LAZIMA NA YA MSINGI YATAKAYOKUWA SABABU YA KULETA MAISHA MAPYA YATAKAYODUMU NA YENYE TIJA NA MANUFAA!

>> YESU ALILETA BADILIKO LA MSINGI, LA KWELI, NA LA MILELE LA "MOYO"!! NA NDIYO MAANA IMEANDIKWA,

17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 

2 Wakorintho 5:17

>> KRISTO YESU NDIYE AKUPAYE MOYO MPYA UKIMWAMINI NA KUMPOKEA MOYONI MWAKO KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO BINAFSI! NABII EZEKIELI ALITABIRI KUHUSU BADILIKO LA MOYO;

25 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. 

Ezekieli 36:25

26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 

Ezekieli 36:26

MST 25: YESU ATAKUOSHA DHAMBI ZAKO ZOTE MOYONI MWAKO KWA DAMU YAKE UKIZIUNGAMA KWA NIA YA KUZIACHA!

MST 26: UNAPOMWAMINI YESU ANAKUPA MOYO MPYA ULIOOSHWA DHAMBI ZOTE! HII INAMAANISHA YESU ANAUFANYA UPYA MOYO WAKO NA KUIHUISHA roho YAKO ILIYOKUWA IMEKUFA KWA SABABU YA DHAMBI ZAKO (WAEFESO 2:1)! YAANI. ANAKUPA roho mpya iliyozaliwa mara ya pili! (Yohana 3:3-7)

3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 

Tito 3:3

4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 

Tito 3:4

5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 

Tito 3:5

6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 

Tito 3:6

7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. 

Tito 3:7

● Tukirudi kwenye Ezekieli tunasoma;

27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 

Ezekieli 36:27

●  BAADA YA KUPEWA MOYO MPYA (roho mpya iliyozaliwa mara ya pili), Yesu anakupa Roho wake kwenye ubatizo wa Roho Mtakatifu, ambapo unaunganika naye na kuwa roho moja naye!!

27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 

Ezekieli 36:27

Na sasa,

>> KIUMBE KIPYA = ROHO MPYA + ROHO WA KRISTO = MOYO MPYA

>> Hii inamaanisha sasa wewe uliyeokoka una kiriba kipya ambacho ni moyo wako mpya, ambao ni roho yako iliyozaliwa mara ya pili! Kupitia moyo huu mpya sasa DIVAI MPYA KUTOKA MBINGUNI KWA BABA HAITAKOMA! DIVAI MPYA KAMA hekima, maarifa, ufahamu, kicho, shauri, nguvu, mafunuo, mafuta, neema, rehema, n.k. HAVIWEZI KUKOMA KWAKO!!

>> HUWEZI KUPOKEA CHOCHOTE KUTOKA KWA MUNGU UKIWA NI MTENDA DHAMBI ULIYEJIFICHA KWENYE DINI, DHEHEBU, N.K. MWENYE MOYO USIOBADILIKA!!

Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli?

Ezekieli 18:31

Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?

Ezekieli 33:11

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post