PENDO LA NAMNA GANI HILI!!!


PENDO LA NAMNA GANI HILI!!!

9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
1 Yohana 4:9

10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
1 Yohana 4:10
MUNGU,
Hakutukataa kwa kuwa tumetenda dhambi;
•  hakutuchukia;
•  hakututenga;
• hakutuacha tuangamie;
•  hakutususa;
• hakutupa kisogo;
• hakutusema vibaya;
•  hakutudhihaki;
•  hakusambaza ubaya wetu;
•  hakujitenga nasi;
•  hakutuacha taabuni;
•  hakutuacha kwenye maangamizo;
• hakutaka tupotee moja kwa moja na kuangamia;
•  hakutubeza;
• hakutulaumu;
• hakutukosoa;
•  hakutulalamikia;
•  hakutuacha hukumuni!! BALI ALIMTOA MWANAWE PEKEE YESU KRISTO AFE MSALABANI  NA KUFANYA UPATANISHO KWA AJILI YA DHAMBI ZETU KUPITIA DAMU YAKE; (2 KOR 5:18-19) AKATUSAMEHE, (Kol 1:13-14) AKATUOSHA, AKATUFANYA KUWA VIUMBE VIPYA (2 Kor 5:17) BAADA YA KUTUHUISHA NA KUTUFANYA UPYA ROHO ZETU KWA ROHO WAKE MTAKATIFU! (TITO 3:4-5)
>> YAANI, ALITUEPUSHA NA GHADHABU YAKE MWENYEWE! AKAINGIA GHARAMA YA KUTUNUNUA KWA DAMU YAKE (Efe 1:7) MWENYEWE ALIPOLIPA DENI LA DHAMBI ZETU!! ALIKUFA MSALABANI NA KUTUPATANISHA KWA MAUTI YAKE! (Rum 5:8,10) AKATUPA MAISHA MAPYA YASIYOHARIBIKA (2 Tim 1:10) ALIPOFUFUKA KUTOKA KWA WAFU!!
>> ALITUTAABIKIA NA KUTUHANGAIKIA SISI TULIOFARAKANA NAYE, SISI TULIOMUASI YEYE, SISI TULIOMKATAA YEYE, SISI TULIOKUWA HATUMTAKI YEYE, SISI TULIOKUWA ADUI ZAKE YEYE, SISI TULIOSTAHILI ADHABU YA MILELE KWENYE ZIWA LA MOTO USIOZIMIKA!! (Marko 9:43-48)

1. TULIKUWA TUMEASI
2. TULISTAHILI ADHABU YA MILELE
3. TULIKUWA HUKUMUNI TAYARI
4. ILIKUWA NI HAKI YETU KUANGAMIA KWA DHAMBI NA MAKOSA YETU
5. SISI NDIO TULIOKUWA TUMEHARIBU NA KUVURUNDA MBELE ZAKE
6. NA HIVYO TULIKUWA HATUNA HAKI MBELE ZAKE NA WALA HATUKUSTAHILI KUMKARIBIA AU KUPOKEA JEMA LOLOTE KWAKE
7. LAKINI YEYE AKATUSAMEHE, AKATUOSHA, AKATUTAKASA KWA DAMU YAKE MWENYEWE AKILIPA DENI LA DHAMBI ZETU MAANA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI (Rum6:23)
8. LAKINI YEYE HAKUTENDA DHAMBI BALI ALIFANYWA KUWA DHAMBI KWA AJILI YETU! (2 Kor 5:21) AKAIHUKUMU DHAMBI KWENYE MWILI (Rum 8:3) ALIPOIBEBA KWENYE MWILI WAKE PALE JUU MSALABANI!! (1Petro 2:24) ALIKUFA YEYE MAHALA PETU SISI ILI SISI TUISHI
MASWALI KWAKO
1. Unawatendeaje wanaokukosea, wanaokutenda mabaya, na wanaokutenda dhambi?
2. Unawatendeaje wanaokosea, wanaoharibu, wanaovurunda, wanaokupinga, wanaokubishia, na wanaofanya makosa na kutenda dhambi?
3. Je! umeweka moyoni mwako makosa ya wengine, dhambi za wengine, na mabaya ya wengine na wala hutaki kuachilia kiasi kwamba kila uyakumbukapo hayo unawaka hasira na unaona uchungu??!!
4. Je! umekataa kusamehe wengine kiasi kwamba bado una uchungu nao moyoni mwako na wala hutaki kuwa na ushirika nao mpaka sasa?
5. Unaona jinsi ambavyo chuki bado imo moyoni mwako mpaka sasa maana wengine hutaki hata kusalimiana nao au kukutana nao uso kwa uso kwa kuwa walikukosea au walikosea na hujawasamehe mpaka sasa??!!
6. Je! una tabia ya kuwasema vibaya watu mbalimbali waliokukosea, waliokosea wengine, walioharibu, waliovurunda, waliotenda mabaya, na waliotenda dhambi? Ukikaa na watu wako lazima uwaseme vibaya na kukumbushia makosa yao? Huoni Kuwa hiyo ni chuki na huo ni unafiki moyoni mwako??!! Na kwamba huna uzima wa milele ndani yako na bado umo gizani na mautini kwa mujibu wa maandiko??!!

8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa.
1 Yohana 2:8

9 Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.
1 Yohana 2:9

10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
1 Yohana 2:10

11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
1 Yohana 2:11

>>  NA TENA;
14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.
1 Yohana 3:14

15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
1 Yohana 3:15
● SASA UTAKUWAJE GIZANI? HALAFU NI MUUAJI MOYONI MWAKO, HUKU UNADAI UNA MUNGU?! AU UNA DINI YAKO, AU UNADAI UNA DHEHEBU FULANI ZURI? JE! HUONI UMEDANGANYIKA NA SHETANI AMEKUPOFUSHA ILI AKUPELEKE KUZIMU UKIFA NA KISHA JEHANAMU BAADA YA HUKUMU YA MWISHO?
HABARI NJEMA NI KUWA YESU ANAWEZA KUSAFISHA MOYO WAKO UKIMWAMINI! JAMBO AMBALO DINI YAKO NA DHEHEBU LAKO NA SALA ZAKO VIMESHINDWA NA KAMWE HAVITAWEZA!!!

8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Mathayo 5:8

14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebrania 12:14
>> WATAKATIFU NI WALE WALIOMWAMINI YESU WAKASAFISHWA MIOYO YAO DHAMBI ZAO ZOTE NA SASA WANAISHI MAISHA YA UTAKASO WASUBIRI KUMLAKI BWANA YESU MAWINGUNI ATAKAPOKUJA KUWACHUKUA WATAKATIFU WAKE!!!

1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
1 Yohana 3:1

2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
1 Yohana 3:2

3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
1 Yohana 3:3
>> WATU WAOVU NA WAASI HUWA WANAKAZANA SIKUZOTE KUYAKUZA MAKOSA NA DHAMBI ZA WENGINE, KUYATANGAZA, KULAUMU, KUKOSOA, KULALAMIKA NA KUNUNG'UNIKA, KUHUKUMU, KUCHAFUA WENGINE, KUSEMA WENGINE VIBAYA, KUSHIKIA BANGO MAKOSA NA MABAYA YA WENGINE N.K. HII INAITWA roho ya unafiki!!
1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
Mathayo 7:1

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
Mathayo 7:2

3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
Mathayo 7:3

4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
Mathayo 7:4

5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Mathayo 7:5

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post