KIBURI & COMPANY
UTANGULIZI
Kiburi huwa hakipo peke yake kamwe! Moyo wa mwenye kiburi ni moyo mgumu wa mtenda dhambi ambaye kiti cha enzi cha moyo huo amekaa shetani aliye kiini cha roho ya kiburi. Kiburi hukaa mahali pasipo na unyenyekevu! Leo nitaleta utangulizi tu wa marafiki (companions) watano wa kiburi ambao kila umwonapo mmoja akijidhihirisha ujue wote wamo!!
1) KIBURI ( PRIDE)
>> hii ndiyo roho ya shetani iliyomsababishia anguko lake! Ni roho ambayo ilimfanya shetani aasi mamlaka ya Mungu Aliyemuumba kwa kuazimia na kutaka kujiinua na hata kuwa sawa na Mungu!
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
Ezekieli 28:14
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
Ezekieli 28:15
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza,Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
Ezekieli 28:16
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Ezekieli 28:17
>> KIBURI HUJIINUA JUU YA MAMLAKA ZOTE ZILIZOPO KUTOKA KWA MUNGU
>> KIBURI KINA "umungumtu" NDANI YAKE, YAANI KUJIINUA KWA NAMNA YA KUTAKA KUABUDIWA KAMA mungu KWA SABABU YA UZURI WAKO, KIROHO CHAKO, ELIMU YAKO, FEDHA ZAKO, MALI ZAKO, UREMBO WAKO, SIFA ZAKO, CHEO CHAKO, MAFANIKIO YAKO, HUDUMA YAKO, NAFASI YAKO, KABILA LAKO, DINI YAKO, DHEHEBU LAKO, HADHI YAKO, N.K.
>> SHETANI ALIPOTAKA KUWA MUNGU ALIISHIA KUSHUSHWA CHINI MPAKA KUZIMU! JEHANAMU YA MOTO AMEWEKEWA YEYE ALIYE KIINI NA CHANZO CHA roho hii ya kiburi!
>> KIBURI NDIYO KIINI NA CHANZO CHA UBINAFSI WA DHAMBI WA MWANADAMU. KWA KIBURI CHAKE SHETANI ALIANGUKA;
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
Isaya 14:12
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
Isaya 14:13
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
Isaya 14:14
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Isaya 14:15
>> UKISOMA VIZURI MISTARI YA 13 NA 14 UTAZIONA " NITA" SITA, INGAWA MOJA HAIJATAJWA MOJA KWAMOJA( Nitaketi pande za mwisho za kaskazini)
>> HAYA NI MAKAMIO YA KUTOMTUMAIA MUNGU, NA BADALA YAKE KUJITUMAINIA UWEZO NA NGUVU ZAKO ZA KIBINADAMU (USIPOMTUMAINIA MUNGU BIDII NA JUHUDI ZAKO ZOTE KATIKA MAMBO YOTE NI BIDII ZA KUASI ILI KUWA KAMA MUNGU KWA KUJITUMAINIA WEWE MWENYEWE ULIVYO NA ULIVYONAVYO!
>> KIBURI CHAKO KINATAKA NAFASI YA MUNGU PALE UNAPOTAWALA NA KUONGOZA, ILI UABUDIWE/ UHESHIMIWE/USIKILIZWE WEWE TU/ UTETEMEKEWE/ UOGOPWE/UNYENYEKEWE N.K. NA ISIPOKUWA HIVYO UNAWAKA HASIRA YA SHETANI ILE ILE (DEMONIC ANGER)
>> NDIYO MAANA ".......KWA NGUVU NA UKALI UNAWATAWALA." (EZE 34:4 f)
>> LAKINI MAANDIKO YANASEMA SI KWA UWEZO WAKO WALA NGUVU ZAKO (ZECHARIA 4:6)
>> UKIWA NA roho hii ya Kiburi SIFA NA SHUKRANI ZOTE NI ZAKO WEWE NA SIYO MUNGU; HESHIMA YOTE NA UTUKUFU WOTE NI VYAKO NA WALA SIYO MUNGU!! UKO HAPO KWA FAIDA NA MANUFAA YAKO NA SIYO MUNGU!!
Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.
Mithali 13:10
Wenye kiburi wamenidharau mno, Sikujiepusha na sheria zako.
Zaburi 119:51
>> MWENYE KIBURI HANA NA HAWEZI KUWA NA UNYENYEKEVU WA KRISTO NA NDIYO MAANA YESU ALITOA MWALIKO WA WENYE DHAMBI KUJA KWAKE:
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:28
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:29
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Mathayo 11:30
>> JITIENI NIRA YANGU NA KUJIFUNZA KWANGU KWA KUWA MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU WA MOYO!!
2) UBISHI (STUBBORNNESS) NA,
3) UKAIDI (OBSTINACY)
>> spirit of stubbornness and spirit of obstinacy- roho za ubishi na ukaidi ni roho zenye kukaidi, kukataa, kubisha, kupinga, kuasi, na kushindana na kila shauri jema la kutoka kwa Mungu na wanadamu!! Nazo hufanya hivyo kwa kiburi kwa sababu ya kutimiza matakwa ya ubinafsi wake! Mwenye kiburi hubisha na kukaidi hata kama ni jambo la msingi kwa sababu kwake yeye jambo la maana na la msingi LAZIMA LITOKE KWAKE NA WENGINE WALIKUBALI NA KULIPOKEA!!!
Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
1 Samweli 15:23
Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa Bwana, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
Mithali 3:32
Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
Mithali 4:24
Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Mithali 8:13
Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha Bwana; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
Mithali 14:2
Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.
Mithali 17:20
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Mithali 21:24
wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.
Waefeso 5:4
Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.
Mithali 13:10
>> MWENYE KIBURI YEYOTE NI MBISHI NA MKAIDI NAYE HUPENDA MASHINDANO ILI AIBUKE MSHINDI NA KUTIMIZA KIBURI CHAKE
4) JEURI (roho ya jeuri/spirit of rudeness)
[What is the meaning of Jeuri in English?
rude
Adjective. -jeuri (declinable) rude (bad-mannered, insolent, tough) ]
>> mwenye jeuri hana spirit of politeness/roho ya kuheshimu, kuthamini, na kuwajali wengine
● mwenye kiburi hana adabu, heshima, na wala hathamini na kujali wengine; hana pia roho ya utu na ubinadamu (spirit of humanity), na ndiyo maana anaweza kukuumiza kwa maneno na wala asijali hata kidogo! Wengine wenye roho hii hujiita " wainjilisti "!! KWAO WAO HUDHANI KUVUNJIA WATU HESHIMA NA KUTOJALI HADHI NA UTU WAO NDIO UINJILISTI NA HIVYO HUROPOKA CHOCHOTE WAKIJIFANYA NI WATUMISHI!!
[noun (politeness)
• behaviour that is respectful and considerate of other people.
"he always treated me with the utmost politeness"]
12 Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo;
Isaya 30:12
13 basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, palipo tayari kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafula kwa mara moja.
Isaya 30:13
12 Maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi, na maovu yetu tumeyajua;
Isaya 59:12
13 katika kukosa na kumkana Bwana, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena jeuri na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.
Isaya 59:13
5) DHARAU ( CONTEMPT)
[What is the meaning of Dharau?
to despise or disdain
-dharau (infinitive kudharau) to despise or disdain (to regard with contempt or scorn) to slight or insult someone.]
● Mwenye kiburi ana dharau pia moyoni mwake! Kiburi na dharau vinatenda kazi pamoja! Kiburi hupelekea kudharau wengine kwa sababu eti una cheo kuliko wao, una umri mkubwa kuliko wao, umesoma kuliko wao, una huduma kubwa kuliko wao, Mungu anakutumia kuliko wao, una upako kuliko wao, ni wa kiroho kuliko wao, ulitangulia kabla yao, ulianzisha wewe, una pesa na mali kuliko wao, umewazidi wao kwa namna yoyote mawazoni mwako! n.k.
● MWENYE KIBURI HANA UNYENYEKEVU (has no spirit of humility)
Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote; Ana uweza katika nguvu za fahamu.
Ayubu 36:5
Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.
Mithali 3:34
Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
Mithali 11:12
Wenye kiburi wamenidharau mno, Sikujiepusha na sheria zako.
Zaburi 119:51
6) MAJIVUNO (ARROGANCE/CONCEIT)
[Arrogant is an adjective for describing people who are too proud and look down on others,]
● Mwenye Kiburi huwa na majivuno pia! ( whomever has the spirit of pride also has this spirit of arrogance too)
>> yeye huwa ni mwenye kujisifia, kujivuna, kuwashusha wengine na kujistahilisha kuwa juu zaidi yao; ni mwenye kuringa na kupenda kuwaumizia na kuwatesa wengine kwa kile anachojivunia kwamba amewazidi au kuwapita ama kuwashinda au anacho na wao hawana!!!
● mwenye majivuno hana unyenyekevu na pia hana roho ya kujishusha na kujidhili! Bali yeye hupenda kujisifu na kusifiwa, hupenda kuonekana, hutafuta sana kujulikana na kuwa maarufu kwa sababu ya vile alivyo, alivyovifanya, na vile alivyonavyo! Huyu hupenda kujiweka daraja la juu zaidi kupita wanadamu wenzake na hupenda wote wamtazame hapo juu na kumstaajabia!!
3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
1 Samweli 2:3
Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.
Zaburi 31:18
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Mithali 21:24
Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Isaya 2:17
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
Isaya 13:11
Tumesikia habari za kiburi cha Moabu, ya kwamba ni mwenye kiburi kingi; habari za majivuno yake, na kiburi chake, na ghadhabu yake; majivuno yake si kitu.
Isaya 16:6
Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi alivyotakabari moyoni mwake.
Yeremia 48:29
Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
Yakobo 3:5
Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.
Yakobo 4:16
HUU NDIO MOYO WAKO MBINAFSI:
Ubinafsi= Kiburi+Ubishi+Ukaidi+Jeuri+Dharau+Majivuno
TUTAENDELEA TUKIJALIWA, UBARIKIWE