MAISHA HALISI (REAL LIFE)


*MAISHA HALISI (REAL LIFE)* 

Mathayo 6:24-25

[24]Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. 

No man can serve two masters: for either he will hate the one, and love the other; or else he will hold to the one, and despise the other. Ye cannot serve God and mammon.

[25]Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 

Therefore I say unto you, Take no thought for your life, what ye shall eat, or what ye shall drink; nor yet for your body, what ye shall put on. Is not the life more than meat, and the body than raiment?

● Bwana ni yule anayeutawala na kuuongoza moyo wako ama kuitawala na kuingoza roho yako, nafsi yako, na mwili wako!! Bwana lazima awe ni "roho" ama ya shetani au Roho wa Mungu! Huyu roho ndiye anayeunganika na roho yako na kuongoza maisha yako yote na wewe ukimpendeza yeye, ukimtumikia yeye, ukiyafanya mapenzi yake yeye, ukimtii na kumfuata yeye, ukimsikiliza na kumheshimu yeye, ukimjali na kumtukuza yeye, ukiyasikiliza mashauri yake yeye na kuyafuata, ukiyazingatia, kuyatimiza, na kuyatekeleza matakwa yake yeye sikuzote! 

● Bwana ni ama Mungu au "mungu" unayemuabudu, unayemtumikia, unayemtegemea, unayemkimbilia, ambaye umeweka tumaini lako lote kwako!! Ndiyo maana hawawezi kuwepo mabwana wawili kwa moyo mmoja!! Sikuzote ni moyo mmoja na Bwana mmoja!! 

● Bwana ni yule unayempenda kupita wengine wote!! Na huyu ndiye ambaye maisha yako yote upo kwa ajili yake! Yaani, yeye ndiye MNUFAIKA MKUU NA WA KWANZA WA MAISHA YAKO KATIKA roho, nafsi, na mwili!! Bwana ndiye MFAIDIKA MKUU WA MAISHA YAKO YOTE AU UTUMISHI ULE UNAOMTUMIKIA UKIWA KWENYE MWILI WA DAMU NA NYAMA!

● Bwana wako ndiye anayekupa akili mbaya au nzuri ya maisha kwa kuwekeza kwenye mawazo ya moyo wako (roho yako) ambayo ndiyo huja kuwa mawazo ya nafsini mwako ambapo hutawala akili yako (your mind), nia/makusudio/mapenzi ya moyo wako, na hisia za nafsi yako!! ( soul= mind+will+emotion)

● Sikuzote lazima utafanana kiroho na nafsi yako na Bwana wako maana unaishi kama yeye apendavyo na kuyafanya mapenzi yake maana unamsikiliza na kumtii; na hivyo yeye hukuwezesha kwa nguvu zake (ama nguvu za Mungu au nguvu za giza) Bwana ni huyo "roho" anayekutawala na kuongoza maisha yako!!

● kama Bwana wako ameweka tamaa ya fedha au mali moyoni mwako wewe unakuwa mpenda fedha au mali kiasi cha fedha kuwa kama " mungu" kwako kwa hiyo unakuwa unaabudu sanamu inayoitwa "mungu pesa" au " mungu mali"!! Ndipo ukizipata kwa wingi unajiona kana kwamba umekuwa "mungu" hivi kwa sababu kiburi cha pesa kimekudanganya kama maandiko yanenavyo;

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? 

Obadia 1:3

>> MTENDA DHAMBI UNAMWABUDU SHETANI KAMA SANAMU ZA AINA MBALIMBALI UNAZOJIVUNIA (zikiwemo pesa, mali, utajiri, elimu, cheo n.k.), DINI POTOFU, NA IMANI POTOFU. Huwezi kumwabudu wala kumtumikia Mungu wa kweli mpaka aridhie toba yako ya dhati itakayopelekea kusamehewa na kuoshwa dhambi zako na damu ya Yesu, kuokoka, na kupewa uzima(maisha ya) wa milele!!

>> WATAKATIFU WALIOOSHWA KWA DAMU YA YESU NDIO PEKEE WANAO MWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI MAANA WAMEZALIWA MARA YA PILI roho ZAO KATIKA UFALME WA MUNGU NA YESU ANAKAA MIOYONI MWAO KAMA BWANA NA MWOKOZI!!

>> Wewe Bwana wako ni nani? Umeokoka? Kama bado hujaokoka lazima kuna sanamu unaabudu!!! Kama umeokoka, je! unamwabudu Mungu katika Roho na Kweli? Au pengine kuna sanamu hizi unaziabudu?

Marko 4:18-19

[18]Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, 

And these are they which are sown among thorns; such as hear the word,

[19]na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. 

And the cares of this world, and the deceitfulness of riches, and the lusts of other things entering in, choke the word, and it becometh unfruitful.

NA HAPA TENA;

Luka 21:34

[34]Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 

And take heed to yourselves, lest at any time your hearts be overcharged with surfeiting, and drunkenness, and cares of this life, and so that day come upon you unawares.


 *MAISHA KWAKO NI YAPI?* 

>> Kwa mujibu wa maandiko maisha kwenye ufalme wa Mungu siyo kula, kunywa, kulala, kuvaa, kumiliki mali n.k.

>> Kama uko "bize" unakimbizana na vitu vinavyoharibika vya dunia hii wewe umepotea njia!!! YESU NDIYE NJIA!!! (YOHANA 14:6) Naye alisema;

1) Luka 12:15

[15]Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. 

And he said unto them, Take heed, and beware of covetousness: for a man's life consisteth not in the abundance of the things which he possesseth.

>> KUWA NA MALI NYINGI SIYO KWAMBA NDIO UMEYAPATIA MAISHA!! KAMA ULICHONACHO NI FEDHA NA MALI NYINGI NA DINI FULANI POTOFU AU IMANI FULANI POTOFU AMBAZO ZOTE HAZINA UZIMA WA MILELE, AU HAZIOKOI UMEPOTEA!! UNAABUDU UKIWA NA DHAMBI ZAKO!! MAISHA HALISI HAYAMO KWENYE WINGI WA VITU ULIVYONAVYO!!!

2) Mathayo 6:25

[25]Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 

Therefore I say unto you, Take no thought for your life, what ye shall eat, or what ye shall drink; nor yet for your body, what ye shall put on. Is not the life more than meat, and the body than raiment?

>> KWA WEWE UNAYESUMBUKIA MAISHA YAKO KWA VITU VINAVYOHARIBIKA PEKE YAKE, SIKILIZA!

● MAISHA ALIYOLETA YESU NI ZAIDI YA CHAKULA! Wewe si unakula ili uishi? Sasa Yesu amesema hapa kuwa MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA!! Paulo naye anaeleza kuwa huku kwenye ufalme wa Mungu,

Warumi 14:17-18

[17]Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 

For the kingdom of God is not meat and drink; but righteousness, and peace, and joy in the Holy Ghost.

[18]Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. 

For he that in these things serveth Christ is acceptable to God, and approved of men.

NA TENA;

1 Wakorintho 8:8

[8]Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu. 

But meat commendeth us not to God: for neither, if we eat, are we the better; neither, if we eat not, are we the worse.

●Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

1 Wakorintho 6:13

>> VYAKULA UNAVYOVIHANGAIKIA NI KWA TUMBO NA TUMBO NI KWA VYAKULA LAKINI VYOTE VIWILI MUNGU ATAVITOWESHA!! MBINGUNI HATUINGII NA TUMBO LINALOSHIBA BIRIANI!!!

>> KUNA MAISHA AMBAYO HAYAHITAJI CHAKULA KINACHOHARIBIKA AMBAYO YESU AMEYALETA!!

● YESU ALISEMA PIA KWAMBA MWILI NI ZAIDI YA MAVAZI

>> YESU ANATOA MWILI USIOHARIBIKA AMBAO HAUHITAJI MAVAZI YANAYOHARIBIKA BALI UNAVIKWA UTUKUFU WA MUNGU!! HUU NI MWILI USIOKUFA!! 

● INJILI YA YESU IMEYAFUNUA MAISHA HAYA YASIYOHARIBIKA NA YASIYO NA MWISHO!!

2 Timotheo 1:10

[10]na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; 

But is now made manifest by the appearing of our Saviour Jesus Christ, who hath abolished death, and hath brought life and immortality to light through the gospel:

>> YESU ALIIUA MAUTI KWA MAUTI YAKE!! KIFO CHAKE KILIUA KIFO CHA MTENDA DHAMBI NA NDIYO MAANA UKIOKOKA HUFI BALI UNAONDOKA KWENYE HUU MWILI, UNABEBWA NA MALAIKA, UNAPELEKWA KWA YESU  PARADISE UKIWA NA MWILI WA ROHO USIOHARIBIKA 

>> KUFA NI KUTENGWA NA MUNGU MILELE KWA SABABU YA DHAMBI ZAKO!! KUFA NI KUTENGWA NA UZIMA WAKE, NI KUTENGWA NA MAISHA YAKE YESU!!!

Waefeso 2:1-2

[1]Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; 

And you hath he quickened, who were dead in trespasses and sins;

[2]ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; 

Wherein in time past ye walked according to the course of this world, according to the prince of the power of the air, the spirit that now worketh in the children of disobedience:

>> UMEKUFA KIROHO MTENDA DHAMBI!! HUNA MAISHA HALISI YASIYOHARIBIKA AMBAYO NDIYO HUITWA UZIMA WA MILELE!!

>> NA KADIRI UNAVYOZIDI KUYASUMBUKIA MAISHA HAYO ULE NINI, UNYWE NINI, UVAE NINI NA KUTOTAFUTA UFALME WA MUNGU KWANZA NA HAKI YAKE ILI UWE NA UZIMA AU MAISHA HALISI YA KWELI, NDIVYO UNAVYOZIDI KWENDA MBALI UPOTEVUNI!!

>> YESU ALISEMA MIMI NDIMI NJIA, KWELI, NA UZIMA!! (YOH 14:6)

>> YESU NDIYO MAISHA!! MAISHA NI YESU!! NDANI YA YESU KUNA HUYO ROHO WA HAYO MAISHA AITWAYE ROHO WA UZIMA AMA ROHO WA NENO!! BIBLIA INASEMA,

Yohana 1:1,3-4

[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 

In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.

[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 

All things were made by him; and without him was not any thing made that was made.

[4] Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

In him was life; and the life was the light of men.

● LIFE IS IN THE WORD (MAISHA YAMO KWENYE NENO)

>> YESU NI NENO LA LENYE UZIMA/MAISHA LIDUMULO HATA MILELE

1 Petro 1:23

[23]Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 

Being born again, not of corruptible seed, but of incorruptible, by the word of God, which liveth and abideth for ever.

>> KUZALIWA KWETU MARA YA PILI NI KWA MBEGU TAKATIFU ISIYOHARIBIKA, NENO LA MUNGU!!!

>> HATUKUZALIWA KWA MBEGU ZA BABA ZETU ZINAZOHARIBIKA BALI KWA MBEGU YA MUNGU TAKATIFU ISIYOHARIBIKA KWENYE roho ZETU!

>> HII NDIYO MAANA TULIPOKEA MAISHA YASIYOHARIBIKA!!!

● MUDA USINGETOSHA HAPA KUELEZA KAZI INAYOENDELEA NDANI YA MTOTO WA MUNGU ALIYEOKOKA YA KUMUUMBA YESU!!

19 Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu; 

Wagalatia 4:19

● ITOSHE TU KUSEMA HUYU ROHO WA KRISTO TULIYEMPOKEA NDIYE CHANZO NA KIINI CHA MAISHA YETU MAPYA TULIYOYAPOKEA KUTOKA KWA YESU KUPITIA NENO LAKE

Yohana 6:63

[63]Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. 

It is the spirit that quickeneth; the flesh profiteth nothing: the words that I speak unto you, they are spirit, and they are life.

John 6:63

[63]It is the Spirit who gives life; the flesh profits nothing. The words that I speak to you are spirit, and they are life.

●● KWA HIYO

31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 

Mathayo 6:31

32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 

Mathayo 6:32

33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 

Mathayo 6:33

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post