DHAMBI HAIWEZI KUSHAMIRI.......!
Dhambi haiwezi kushamiri kwa siri au waziwazi mahali ambapo yupo Mungu!! Kama unadhani inawezekana nenda ukamuulize;
1. Sauli kama alifanikiwa kuficha dhambi nyakati za nabii Samuel! (1 Samuel 15:1-35)
2. Daudi kama alifanikiwa kuficha dhambi nyakati za nabii Nathani! (2 Samuel sura za 11 & 12)
3. Gehazi kama alifanikiwa kuficha uovu huku akiwa chini ya huduma ya nabii Elisha! (2 Wafalme 5:1-27)
4. Anania na mkewe Safira kama walifanikiwa kuficha dhambi huku wakiwa kanisani wakiongozwa na Petro, Yakobo, na Yohana!! (Matendo ya Mitume 5:1-11)
5. Akani kama alifanikiwa kuficha dhambi akiwa chini ya Joshua (Yoshua sura yote ya saba)
>> Biblia iko wazi kuwa nuru hung'aa gizani na kwamba gizani haliiwezi nuru ( Yohana 1:5)! Nuru ikiwepo giza haliwezi kuwepo! Giza huikimbia nuru!! Watu wa Mungu waliotakaswa na kuoshwa kwa damu ya Yesu na Neno lake huwa wana macho ya Mungu ndani yao (roho saba za Mungu)! Lile neno limeyatia nuru macho ya mioyo yao ( Zab 19:8 & Efe 1:17-18) nao giza haliwafichi kitu tena!!
Zaburi 139:12
[12]Giza nalo halikufichi kitu,
Bali usiku huangaza kama mchana;
Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
Yea, the darkness hideth not from thee; but the night shineth as the day: the darkness and the light are both alike to thee.
>> UFALME WA GIZA UNAFANIKIWA KUFICHA MAOVU YAKE KWA VIPOFU KIROHO!!
>> USAFI WA MOYO (MT 5:8) NI USAFI WA MACHO YA MOYONI (MACHO YA KIROHO)
>> KUJAA ROHO KUNA MAANA PIA YA KUJAA NURU YA UTUKUFU WA MUNGU
Yohana 8:12
[12]Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Then spake Jesus again unto them, saying, I am the light of the world: he that followeth me shall not walk in darkness, but shall have the light of life.
>> UKITAZAMA KWA UMAKINI ULE UOVU WALIOSHINDWA KUUFICHA KWA SABABU YA NURU ILIYOKUWEPO UTAKUTA KUNA:
• Dhambi za mfalme (Sauli na Daudi)
• Dhambi za mshirika kanisani (Akani)
• Dhambi za mhudumu/mtumishi kanisani (Gehazi)
• Dhambi za wanandoa kanisani (Anania na Safira)
>> HIVYO USIAANZE KUNYOOSHA KIDOLE KWA MCHUNGAJI AU MSHIRIKA, WEWE NDIWE KIPOFU UNAYEONGEA SANA NA KUPONDA WENGINE, KUWADHARAU, KUSENGENYA, KUJIONA BORA, KUJIONA NI TAJIRI KUMBE NI MASKINI, KUJIONA UNAONA KUMBE NI KIPOFU, KUJIONA NI KITU KUMBE SI LOLOTE MBELE ZA MUNGU MAANA UNAISHI DHAMBINI HALAFU KWA SABABU HUJAGUNDULIKA, UNADHANI MUNGU NAYE NI KAMA VIPOFU WANAOKUZUNGUKA; NA PIA NI KAMA AKINA ELI WANAOFUMBIA MACHO UOVU WAKO!! USIPOTUBU UTAJUTA SANA SANA SANA MILELE!!
>> WEWE NDIWE UMETAKIWA KUWA NURU YA NDOA YAKO, FAMILIA YAKO, UKOO WAKO, KAZINI KWAKO, KWENYE BIASHARA YAKO, KILIMO CHAKO NA KAZI YA MIKONO YAKO KWA KUTOIFUATISHA NAMNA YA DUNIA HII!!! LAKINI UNAPIGA MBIO ZILE ZILE, NA VILE VILE WAPIGAVYO MATAIFA, BADALA YA KUPIGA MBIO KUTAFUTA WALICHOKUWA NACHO MANABII NA MITUME!!
>> ZAMANI ZA AKINA ELIYA, ELISHA, NATHANI, YEREMIA, EZEKIEL, YONA, NA WENGINEO DHAMBI HAIKUWEZA KUSHAMIRI WALA KUNYAMAZIWA BILA KUJALI AMEITENDA MFALME AU YEYOTE!!
>> KUNA NABII LEO? KUNA MTUME LEO?!!! NIONYESHE NABII AU MTUME NIKUONYESHE MAELFU KWA MALAKI WANAOTUBU NA KUOKOKA! NIKUONYESHE ISHARA ZA MITUME NA MANABII AMBAPO YESU PEKEE ANAINULIWA NA KUTUKUZWA!! NIONYESHE HAO NIKUONYESHE UAMSHO NA HOFU YA MUNGU KWENYE KANISA NA TAIFA!! NADHANI NI WAKATI WA KUTUBU!! NA KUANZA KULIITIA JINA LAKE KWA UTUKUFU WA JINA HILI KUU KUPITA MAJINA YOTE: JINA LA YESU!!
>> DHAMBI INASHAMIRI PALIPOJAA VIPOFU!!
>> ALIPO YESU DHAMBI HAIWEZI KUSHAMIRI
3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
Yohana 8:3
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
Yohana 8:4
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
Yohana 8:5
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Yohana 8:6
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Yohana 8:7
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Yohana 8:8
9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
Yohana 8:9
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
Yohana 8:10
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
Yohana 8:11
>> UWEPO WA YESU KWA WINGI AKIWA AMEJAA NDANI YA MWILI WAKE UNAONDOA WATENDA DHAMBI AMBAO YESU ALIWAITA WANAFIKI (MT 7:1-5) AMBAO KAZI YAO KUU NI KUSHUGHULIKA NA VIBANZI VYA WENGINE HUKU BORITI ZAO HAWAZIGUSI KAMWE!! BORITI NI GIZA MOYONI! NI roho ya unafiki ya shetani!! Tubu!