NI ROHO YA NANI IMENENA KUPITIA KINYWA CHAKO??!! ( WHOSE SPIRIT SPOKE THROUGH YOUR MOUTH?)*
Job 26:4
[4]Who has helped you utter these words?
*And whose spirit spoke from your mouth?[* 4 Je! Umetamka maneno kwa nani? *Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?*
Ayubu 26:4]
● maneno yanayotoka kwenye kinywa chako ni "roho" inaongea ili kutaarifu, kushawishi, kuelimisha, kuhekimisha, kupotosha, kukengeusha, kujenga au kubomoa, kuinua au kushusha, kutia au kuvunja moyo, kufariji au kutia moyo, kuonya, kukaripia, kudanganya au kusema kweli, kuua au kuhuisha, kuponya au kuumiza, kusafisha au kuchafua, kutakasa au kupandikiza roho chafu, kuganga au kujeruhi, kubisha na kubishana, kupinga na kuasi, kukubali na kutii, n.k.
● utagundua roho hiyo inenayo ni ya namna gani kutegemea kama inanena sawa na au kinyume na kweli!!!
● kama ni roho ya Mungu itajenga, itafariji, itatia moyo, itahuisha, itaimarisha, italeta amani, italeta suluhu, itawapa neema wasikiao, itasuluhisha, itawapa faida wale waisikiao, italinda sifa na heshima za wasikiao, itadumisha uchaji Mungu, itadumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani, itaepuka magomvi, mabishano, na machafuko, bali italeta utulivu, maelewano, furaha, amani, na ushirika, n.k.
● Unapoamini lazima unene ulichoamini maana hiyo ndiyo roho ya imani;
2 Wakorintho 4:13
[13]Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, *Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena;*
We having the same spirit of faith, according as it is written, I believed, and therefore have I spoken; we also believe, and therefore speak;
● ULIYEOKOKA HAURUHUSIWI KUNENA CHOCHOTE NJE YA KILE ULICHOKIAMINI! Maana imeandikwa, "KWA MOYO MTU HUAMINI........KWA KINYWA MTU HUKIRI HATA KUPATA WOKOVU!!!" (RUM 10:10)
● UNAAMINI UNACHOKISEMA??!! UNAAMINI UNACHOKINENA??!! JE! HIVYO NDIVYO UNAVYOAMINI??!! KWA ANDIKO LIPI??!! KWA
MAANDIKO YAPI??!!
● MTU AKISEMA NENO KUHUSU WEWE, MKEO/MUMEO, HUDUMA YAKO, KIROHO CHAKO, WATOTO WAKO, N.K. .MUULIZE " IMEANDIKWA WAPI?" KAMA HANA ANDIKO UJUE NI roho ya shetani imeongea!!! Hajaongea anachoamini bali alichoona au kusikia!!! Muulize imeandikwa wapi mimi ni muongo? au nimepotoka? au nina hasira? au mvivu? au n.k.? Imeandikwa haturuhusiwi SISI TUNAOMWAMINI YESU kupitisha hukumu kuhusu mwingine kwa kuzingatia YALE TUYAONAYO AU TUYASIKIAYO!!!
Isaya 11:3
[3]na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; *wala hatahukumu kwa kuyafuata*! *ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake* ;
And shall make him of quick understanding in the fear of the LORD: and he shall not judge after the sight of his eyes, neither reprove after the hearing of his ears:
● KAMA YESU NDANI YAKO AMEKUFUMBUA MACHO SABA YA ROHO HUWEZI KAMWE KUTEGEMEA UONE KWANZA au USIKIE NDIPO UJUE NA KUHUKUMU KWAMBA MAMBO NDIVYO YALIVYO!!! HIYO SIYO HUKUMU YA HAKI BALI NI HUKUMU YA MACHO YA MTENDA DHAMBI ASIYEAMINI KAMA ILIVYOANDIKWA KWENYE ISAYA 11:3 HAPO JUU!!
● ALIYEOKOKA AMEOKOKA KWA NENO LA MUNGU
● TABIA ZAKE ZIKOJE? ZIKO KAMA NENO LISEMAVYO!!
● JE! UTAKATIFU WAKE, UCHAJI MUNGU, UPENDO N.K. VYA MTOTO WA MUNGU VINATEGEMEA UNACHOKIONA KWAKE AU ANAVYO-BEHAVE ANAPOKOSEA??!! AU NENO LIMESEMA NINI KUMHUSU YEYE??!!
● MTOTO WA MUNGU NI MTAKATIFU KAMA NENO LISEMAVYO, NI MPOLE KAMA NENO LISEMAVYO, SI MWEPESI WA HASIRA KAMA NENO LISEMAVYO, MWAMINIFU KAMA NENO LISEMAVYO, YUPO KAMA NENO LISEMAVYO NA SIYO KAMA UMSIKIAVYO AU UMWONAVYO!!
MFANO:
Umeiombea nyumba yako neema ya wokovu kwa andiko hili;
Matendo ya Mitume 16:30-31
[30]kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
And brought them out, and said, Sirs, what must I do to be saved?
[31]Wakamwambia, *Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.*
And they said, Believe on the Lord Jesus Christ, and thou shalt be saved, and thy house.
● LILE JIBU: " *Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako!!!"* LINA MAMBO 3:
>> MWAMINI BWANA YESU (UMEMWAMINI BWANA YESU?)
>> NAWE UTAOKOKA ( UMEOKOKA?)
>> UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO
- Umeokoka peke yako??!! HAPANA!!!
- Nimeokoka mimi pamoja na nyumba yangu!!!
- Huu ndio ukiri wangu, hili ndilo niliaminilo!! Na hii ndiyo kweli kuhusu familia yangu!! TUMEOKOKA WOTE!
● Sasa atakuja mtenda dhambi asiyeamini atakuambia:" mwanao nilimuona bar na mwanamume wanalewa na kisha wakaondoka wakaingia guest House! Nikakaa pale nikinywa kama masaa 3 hivi sikuwaona wanatoka!!
>> JIBU LANGU: MIMI SINA MTOTO MLEVI NA MWASHERATI! BALI NINA WATOTO WALIOOKOKA NA KUJAZWA ROHO KAMA MAANDIKO YASEMAVYO!! HILO LA MATENDO 16:30-31 NA HILI:
Matendo ya Mitume 2:38-39
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Then Peter said unto them, Repent, and be baptized every one of you in the name of Jesus Christ for the remission of sins, and ye shall receive the gift of the Holy Ghost.
[39] *Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili ya watoto wenu, na kwa watu wote* *walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.*
For the promise is unto you, and to your children, and to all that are afar off, even as many as the Lord our God shall call.
● HIVI NDIVYO WATENDA DHAMBI MAKANISANI WASIOAMINI WANAVYOWANENEA MABAYA WATEULE WALIOOSHWA KWA DAMU YA YESU KWA KUWA NI MACHO NA MASIKIO YAO YANAYOWAONGOZA NA KAMWE SIYO ROHO WA YESU NA NENO LAKE!!!
2 Wakorintho 5:7
[7](Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
(For we walk by faith, not by sight:)
>> ONGEA NENO KINYUME NA UYAONAYO NA UYASIKIAYO!!
>> TUBU NA UANZE KUKIRI NENO, KUTAMKA NENO, KUTABIRI NENO, KUTANGAZA NENO, N.K. KINYUME NA UYAONAYO YOTE, UYASIKIAYO YOTE, HALI ZILIZOPO KINYUME ZOTE, MAZINGIRA KINYUME YOTE!!
>> VINGINEVYO UTASUBIRI UAMSHO MPAKA MVI ZITAENEA KICHWANI BALI UTASIKIA TU KULE UAMSHO, HUKU UAMSHO, PALE UAMSHO, N.K. WEWE BAKI NA KUTOA VIBANZI HUKU UKIWA NA BONGE LA BORITI!!!