Kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake
Mathayo 12:34
[34]Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
O generation of vipers, how can ye, being evil, speak good things? for out of the abundance of the heart the mouth speaketh.
● HUWEZI KAMWE KUNENA MEMA KAMA MOYO WAKO UMEJAA MABAYA!
● HUWEZI KAMWE KUNENA MEMA KUHUSU KANISA, WATAKATIFU, WATUMISHI WA MUNGU, TAIFA, RAIS, N.K. HUKU MOYONI MWAKO UMEJAZA MABAYA KUHUSU WAO
● MOYO MBAYA WA KUTOAMINI HAUWEZI KUWA NA MEMA NA SIKU ZOTE UTAKUWA UNATAFUTA MAKOSA YA WENGINE UKOSOE, ULAUMU, ULALAMIKE, UNUNG'UNIKE, ULAUMU, UPINGE, UHUKUMU, UBOMOE, UCHAFUE, USHINDANE ILI KUONEKANA BORA ZAIDI, UTAFUTE SIFA ZAKE BINAFSI, N.K.
● MWAWEZAJE KUNENA MEMA MKIWA WABAYA!! MTU AKIJA KWAKO NAYE ANANENA MABAYA KUHUSU WENGINE MUULIZE
1. LENGO LAKO NI NINI?
2. KWA NINI UNAMNENEA MABAYA HAYO KWANGU?
3. UNANIAMBIA HAYO ILI NIFANYEJE? NIMCHUKIE??!! NIMDHARAU??!! NIMKIMBIE??!! AU NIFANYEJE??!!
4. NA WEWE UNAFAIDIKA NINI UNAPOELEZA UBAYA WA MWINGINE??!!
5. AU YESU ANAFAIDIKA NINI WEWE UNAPOHARIBU SIFA ZA WENGINE??!!
6. UFALME WA MUNGU UNAFAIDIKAJE PALE UNAPONENEA MABAYA WENGINE??!!
7. UKINENA MABAYA MAANA YAKE ULISHAWAZA MABAYA, JE! HUO NDIO UTAKATIFU??!!
8. JE! UTAKATIFU NI KUPROVE KWAMBA MWINGINE NI MBAYA AU AMEKOSEA??!!
9. WAOVU NA WABAYA "SIKUZOTE HUKAA UPANDE WA MABAYA" (ALWAYS DWELL ON THE BAD SIDE!!)
10. THE BAD SIDE, IF ANY, WAS FOR THE TRUE SAINT TO PRAY AND INTERCEDE ABOUT BEFORE THE THRONE OF GRACE! EVIL MEN CANNOT APPROACH THE HOLY THRONE OF GOD!! ( UPANDE WA MABAYA, KAMA KWELI UPO, NI KWA AJILI YA WATAKATIFU WA KWELI KULIA NA KUOMBOLEZA MBELE ZA MUNGU/ KITI CHA NEEMA KWA AJILI YA HAO WAKOSEAO!!) ILA WATU WAOVU HAWAWEZI KUKIKARIBIA KITI CHA NEEMA!!
11. HIVYO YESU ANASEMWA VIBAYA KILA SIKU, ANADHALILISHWA, ANABISHIWA, ANAPONDWA, ANADHARAULIWA, ANAPUUZWA, N.K. TENA NA HAO WANAOJISEMA WANAMWAMINI!!! KWA SABABU LOLOTE UMFANYIALO AU KUMTENDEA MTEULE WA YESU " UNAMTENDEA YESU!!" NA KAMA HUMWONI YESU NDANI YA MTEULE BADO UKO MWILINI!!! AU NI MTENDA DHAMBI!! YESU ALIAGIZA;
■ 12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Wakolosai 3:12
13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Wakolosai 3:13
14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Wakolosai 3:14
NA TENA AKAAGIZA
■ 2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.
Wafilipi 2:2
3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
Wafilipi 2:3
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Wafilipi 2:4
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
Wafilipi 2:5
TAHADHARI
1 Wakorintho 15:33-34
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Be not deceived: evil communications corrupt good manners.
[34]Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.
Awake to righteousness, and sin not; for some have not the knowledge of God: I speak this to your shame.
Proverbs 18:2 (NLT) Fools have no interest in understanding; they only want to air their own opinions.