HAUJAFIKA BADO WALA HAUJAWA MKAMILIFU
1)12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
Wafilipi 3:12
>> HAUJAFIKA BADO ( HAIJALISHI UPO WAPI KIROHO NA KIHUDUMA) USIJIONE UMEFIKA UTAPOTEA!
>> HAUJAWA MKAMILIFU BADO BILA KUJALI UMEKUA KIROHO KIASI GANI AU UMEKAMILISHA MANGAPI KWA AJILI YA BWANA YESU. USIJIDHANIE UMEKAMILIKA, UTAPOTEA!
>> UNACHOTAKIWA NI KUKAZA MWENDO NA KUTAZAMA MBELE (AMBAKO KUNA MENGI BADO!!) ILI KUFIKILIA THAWABU INAYOTOKANA NA WITO WAKO MKUU ULIOITIWA KATIKA KRISTO YESU
2) Wafilipi 3:13
[13]Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
Brethren, I count not myself to have apprehended: but this one thing I do, forgetting those things which are behind, and reaching forth unto those things which are before,
>> USIJIONE KWAMBA TAYARI WEWE NDO WA ROHOOOOONIIIII MPAKWA MAFUTA ULIYEKAMILIKA MSHIKA OFISI MOJA YA ZILE TANO ULIYEKAMILIKA ( KWA KIGEZO CHOCHOTE KAMA ELIMU, MATENDO MAKUU, KUNDI KUBWA, AU MAFANIKIO MENGINE YOTOTE!!!,) UTAPOTEA!!
>> TENDA NENO MOJA TU; SAHAU YOTE YA NYUMA YALIYOPITA!! SAHAU WAFU ALIOWAFUFUA BWANA KWA MKONO WAKO, MABILIONI WALIOOKOKA, VIZIWI WALISIKIA, VIPOFU WALIOONA, WAGONJWA NA WENYE MARADHI WALIOPONA, UTAJIRI NA MALI ULIZOZIPATA, UNAARUFU ULIONAO, ISHARA, MAAJABU, NA MIUJIZA ALIYOITENDA BWANA KWA MIKONO YAKO, UPAKO UNAOTENDA KAZI NDANI YAKO, MAJENGO ULIYOJENGA, MAGARI ULIYONUNUA, FEDHA ULIZOKUSANYA, N.K. SAHAU HAYA, TUPA KULE, MPE UTUKUFU YESU, BADO ANA MENGI MAPYA YA KUTAFANYA SAWASAWA NA ANDIKO HILI;
1 Wakorintho 2:9
[9]lakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)
Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
But as it is written, Eye hath not seen, nor ear heard, neither have entered into the heart of man, the things which God hath prepared for them that love him.
>> YAPO MENGI BADO AMBAYO JICHO HALIJAYAONA POPOTE, WALA SIKIO LA MWANADAMU KUYASIKIA, WALA HAYAJAINGIA MOYONI MWA MWANADAMU AWAYE YOTE, AMBAYO BWANA YESU ANAKUSUDIA KUYATENDA KUPITIA WEWE!! UTUKUFU WA MWISHO WA HUDUMA YAKO NI MKUBWA KULIKO WA MWANZO KAMA HAUTAJIVUNA, HAUTAJIINUA, HAUTAJIKWEZA, HAUTAWAPANDA WENGINE MABEGANI, NA KUJIONA WEWE NDO UNAJUA ZAIDI, WA KIROHO ZAIDI, UNA UPAKO ZAIDI, NI MCHA MUNGU ZAIDI, MSOMI ZAIDI, N.K. UTAPOTEA NA KUSAHAULIWA! MUNGU ANA WENGI WA KUWATUMIA!!
3) Wafilipi 3:14
[14]nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
I press toward the mark for the prize of the high calling of God in Christ Jesus.
>> UKIFANYA HAYO TULIYOTANGULIA KUYASEMA UNAKUWA UMEACHA KUKIMBIA MBIO HIZI MPAKA KUZIMALIZA,UMEACHA KUKAZA MWENDO UMEJIVUNA, UNATAZAMA ALIYOYAFANYA BWANA NA KUCHUKUA UTUKUFU WAKE! JIHADHARI USIPOTEZE THAWABU NA UKASHINDWA KUMALIZA MASHINDANO HAYA JUU YA FALME, MAMLAKA, WAKUU WA GIZA HILI NA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
Mithali 16:18
[18]Kiburi hutangulia uangamivu;
Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
Pride goeth before destruction, and an haughty spirit before a fall.
>> KAZA MWENDO, DUMU KATIKA UNYENYEKEVU, ENENDA KWA HOFU, MPE MUNGU UTUKUFU, UTAKUWA SALAMA
4) Wafilipi 3:15-16
[15]Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.
Let us therefore, as many as be perfect, be thus minded: and if in any thing ye be otherwise minded, God shall reveal even this unto you.
[16]Lakini, hapo tulipofika na tuenende katika lilo hilo.
Nevertheless, whereto we have already attained, let us walk by the same rule, let us mind the same thing.
>> MKAMILIFU NI YULE ANAYEJIJUA KUWA ANAENDELEA KUKAMILISHWA!!
>> MKAMILIFU ANAJIJUA ANATAKIWA KUWA MKAMILIFU VILE VILE KAMA BABA YETU ALIVYOKUWA NDANI YA MWILI AKAITWA YESU!!
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Mathayo 5:48
5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
1 Yohana 2:5
6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
1 Yohana 2:6
>> MKAMILIFU HUENENDA VILE VILE KAMA YESU!! NGUVU ZILE ZILE, UPENDO ULE ULE, HURUMA ZILE ZILE, ROHO SABA ZILE ZILE, UTUKUFU ULE ULE, UTAKATIFU ULE ULE, NA MENGINE MENGI ZAIDI!!
>> MATOKEO YAKE DUNIA HAITAONA TOFAUTI KATI YA WEWE NA YESU WA BIBLIA, NA TENA WEWE UTAFANYA KAZI KUBWA KULIKO ALIZOZIFANYA YESU
Yohana 14:12
[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Verily, verily, I say unto you, He that believeth on me, the works that I do shall he do also; and greater works than these shall he do; because I go unto my Father.
>> DUNIA ITAJAZWA NA MAARIFA YA UTUKUFU WA BWANA KUPITIA YESU ALIYEKAMILIKA NDANI YAKO! WANAFUNZI WAKO WATASIMAMA KAMA WALIVYOSIMAMA AKINA PETRO, UTAUPINDUA ULIMWENGU KAMA AKINA PAULO!! PUNGUFU NA HAPO HUO SIO UKAMILIFU BALI NI MAJIVUNO NA KUJIDANGANYA!! SISI TULIO WAKAMILIFU TUCHUCHUMILIE UKAMILIFU!! UKAMILIFU WETU NI NDANI YA YESU
Wakolosai 2:9-10
[9]Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
For in him dwelleth all the fulness of the Godhead bodily.
[10]Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.
And ye are complete in him, which is the head of all principality and power:
>> HUU NDIO UAMSHO! HII NDIYO MAANA YA UAMSHO! KUUPINDUA ULIMWENGU KAMA WALIVYOFANYA YESU NA PAULO!! KINGINE PUNGUFU YA HAPO SIYO UAMSHO NI UDANGANYIFU WA KUZIMU!!