*MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA* *(1Kor 15:33)*
MTU A: Nimekutana na mungu!
MTU B: Umekutana na mungu??!! Wapi?!
MTU A: Nimekutana na mungu hapo mtaa wa majungu!
MTU B: Huyo mungu akakuambiaje?
MTU A: Mengi! Kaniambia kuna mchungaji katenda dhambi haingii mbinguni, kuna mzee wa kanisa kazaa nje ya ndoa haingii mbinguni, kuna wanandoa hawaongei, hivyo hawaingii mbinguni, kuna mwalimu anafundisha uongo haingii mbinguni,...! (MTU B KAINGILIA!)
MTU B : Hebu subiri kidogo, huyo mungu alikuhakikishia kabisa kwamba amewakataa na hata wakitubu toba zao hatazipokea na kuwasamehe??!!
MTU A: Aaah, hilo sikumuuliza!
MTU B: Wewe si unajua Mungu ni mwingi wa rehema, si mwepesi wa hasira, naye husamehe makosa na dhambi kwa wote wanaorejea kwake kwa toba?! Halafu isitoshe si imeandikwa heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake???!!!! Yeye angekuwa Mungu wa miungu angalikuhakikishia kuwa hao mwisho wao wote ni jehanamu!! Kwa kuwa yeye huutangaza mwisho tokea mwanzo!!
MTU B: Basi yule hakuwa Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, bali alikuwa mungu wa dunia hii, shetani! YEYE SIKUZOTE ANASHIKILIA BANGO DHAMBI NA MAKOSA YA WATAKATIFU NA WALA HAZUNGUMZII REHEMA NA MSAMAHA VYA MUNGU KWA WATU WAKE!
MTU A: Ndio, hiyo ni kweli kabisa maana kuna andiko linasema tusihukumu kwa kufuata tunayoyasikia au kuyaona!!! " *3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;*
Isaya 11:3
>> YESU AKIWA NDANI YAKO NA WEWE UTAFANYA KAMA YEYE! HII INA MAANA WENGI HATUNA YESU, BALI TUNAMTUMIKIA SHETANI KWA MIOYO NA VINYWA VYETU!!
MTU B: Imeandikwa pia *"4 Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu; Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara."*
Mithali 17:4
>> LAZIMA AWEPO MTENDA MABAYA ILI UOVU USIKILIZWE, UKUBALIWE, UPOKEWE MOYONI, NA UENEZWE KWA KINYWA!
>> PIA LAZIMA AWEPO MWONGO ILI ASIKILIZE HABARI MBAYA KUHUSU WENGINE, HABARI ZENYE KUCHAFUA MAJINA NA KUHARIBU SIFA ZA WENGINE NA KISHA KUZIPOKEA MOYONI MWAKE, NA KISHA KUZIENEZA!! HABARI MBAYA HUENEZWA NA WABAYA KUPITIA VINYWA VYAO, MITANDAO YA JAMII, N.K. TUBU UACHE KUSAMBAZA UBAYA NA USAFISHE MOYO WAKO MBAYA AMBAO UNAHIFADHI MABAYA!!
34 *Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.*
Mathayo 12:34
35 *Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.*
Mathayo 12:35
36 Basi, nawaambia, *Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.*
Mathayo 12:36
37 *Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.*
Mathayo 12:37