KWA YESU NJIA NI HII, HAMNA NJIA YA MKATO!!
*UTANGULIZI*
Huwa inasemwa sana kuwa
>> YESU NI JIBU,
>> YESU NI SULUHISHO, na
>> YESU NI UTATUZI, na NDIVYO ILIVYO KWELI SIKUZOTE, MAHALI POTE, NA KATIKA HALI NA MAZINGIRA YOTE!! LAKINI KIVIPI??!! Yesu ni jibu kivipi, Yesu ni suluhisho kivipi, Yesu ni utatuzi kivipi kwenye ndoa yangu iliyosambaratika??!! Kwenye biashara yangu iliyokwama??!! Kwenye huduma yangu isiyokua wala kuendelea kwa miaka mingi??!! Kwenye mahusiano yangu yaliyovunjika na yenye kulegalega??!! Kwa mke wangu anayenisumbua??!! Kwa mume wangu anayenitesa na/au kunisumbua??!! Kwa watoto wangu wasiosikia na wasiotii??!! Kwenye umaskini wangu wa miaka na miaka??!! Kwenye washirika wangu wasiokua kiroho/wasiopendana/wavivu/wasio watoaji/n.k??!! Kwenye taifa langu lisiloendelea??!! KWENYE TATIZO LANGU HILI HAPA NA SASA HIVI HAPA??!! KWENYE MATATIZO YETU HAYA SASA HAPA TULIYONAYO??!! HUYU YESU ANANISAIDIAJE MIMI??!!!! NINATOKAJE HAPA??!! TUNATOKAJE HAPA??!!
>> Katika somo hili nakusudia, kwa kadiri ya neema ya Mungu, kukuonyesha hatua saba ZA UTATUZI na UFUMBUZI mkamilifu wa shida, tatizo, mateso, au ugumu wowote uliokutana nao, unaokukabili, uliokushinda, unaokutesa HIVI SASA MAISHANI MWAKO!! Nataka upate SULUHISHO LA MILELE KATIKA KRISTO YESU KUANZIA SASA!! Imeandikwa, Waebrania 13:8
[8]Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.
Jesus Christ the same yesterday, and to day, and for ever.
YESU NI JIBU LA, SULUHISHO LA, NA UTATUZI WA MATATIZO YAKO YOTE YALIYOANZIA JANA YAKO, YA LEO (SASA YAKO) , NA KESHO YAKO PIA!! KARIBU TUANZE SAFARI YETU YA UTUKUFU KWA ROHO HUYU WA UTUKUFU TULIYENAE!!
1)HATUA YA KWANZA
(LAZIMA UANZE NA NENO)
Biblia inasema; “Mithali 13:13
[13]Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu;
Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu.
Whoso despiseth the word shall be destroyed: but he that feareth the commandment shall be rewarded.”
>> Mwanadamu huwa sikuzote anajiletea yeye mwenyewe uharibifu maishani mwake kwa sababu ya KULIDHARAU NENO, AU KUTOLITENDA NENO (YAKOBO 1:22-25), KUTOLIJUA NENO NA HIVYO KUISHI NA KUENENDA PASIPO HILO (HOSEA 4:6a)! Kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa Neno la Mungu (Mwanzo 1:26-28), na mpango wa Mungu ni kuwa mwanadamu aishi kwa neno hilo!! (Mwanzo 2:7,15-17) MATATIZO, SHIDA, ADHA, MATESO, UGUMU, KUSHINDWA, KUUGUA, KUFA, MAHUSIANO KUVUNJIKA, N.K. VILIINGIA BAADA YA MWANADAMU KUTENDA DHAMBI, YAANI, KULIASI NENO LA MUNGU KWA KUWA IMEANDIKWA, DHAMBI NI UASI (1 YOHANA 3:4)
>> Mungu alikuwa ameumba KILA KITU CHEMA SANA KWA AJILI YA MWANADAMU NA UUMBAJI WOTE! (MWANZO 1:31)
>> Dhambi ilisababisha shetani aharibu, aibe, na kuua kila jema na kila chema kilichoumbwa kwa kumtumia mwanadamu aliyeasi na hivyo kila kitu kikawa KIBAYA SANA NA KIOVU SANA!! Mabaya huwa yanakuja kwako na huwa yanakuwa na NGUVU, UHALALI, na HAKI ya kukupata UNAPOKUWA KINYUME NA AU NJE YA NENO LA MUNGU!!
>> UKIWA KINYUME NA NENO AU NJE YA NENO LAZIMA UWE DHAMBINI
>> KWA HIYO MATATIZO YAKO NI SAWA NA KIWANGO CHAKO CHA KUWA NJE YA AU KINYUME CHA NENO
>> MATATIZO YAKO NI SAWA NA KIWANGO CHAKO CHA KUTOMWAMINI MUNGU
>> KWA WEWE ULIYEMWAMINI YESU HUNA MATATIZO NA HUWEZI KUWA NA MATATIZO KAMA KWELI UNAAMINI!!! KAMA HAUAMINI UTAKUWA NA MATATIZO MENGI SANA MAANA UNAENENDA KWA KUONA NA SI KWA IMANI!! HIVYO HAYO YOTE UYAONAYO MAISHANI MWAKO KWAKO NI MATATIZO YALIYOSIMAMA MAISHANI MWAKO!! HILI TUTALIANGALIA HAPO MBELE KWENYE SOMO HILI!! ILA KIMSINGI HICHO KINACHOITWA MATATIZO KWA ALIYEAMINI NI SEHEMU YA MAJARIBU YA IMANI YAKE!! NA PIA NI MASHAMBULIZI YA KUZIMU NA MAUTI! AKISHINDWA KUAMINI BASI NDIPO YANAKUWA MATATIZO KWELI KWELI!!
>> NENO LA MUNGU LIMEBEBA KILA SULUHISHO UNALOLITAKA, NA PIA LIMEBEBA KILA UTATUZI UNAOUTAKA, NA KILA UFUMBUZI UNAOUTAFUTA!! LIMEJAA HEKIMA, MAARIFA, UFUNUO, KICHO, USHAURI, NGUVU, UFAHAMU, UGUNDUZI, N.K.
>> YESU KRISTO MWANA WA MUNGU NI NENO LA MUNGU ALIYE HAI KWA ULIMWENGU! MUNGU AMESEMA NA ULIMWENGU KATIKA SIKU ZA MWISHO KUPITIA MWANAWE PEKEE YESU!!!
“Waebrania 1:1-2
[1]Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,
God, who at sundry times and in divers manners spake in time past unto the fathers by the prophets,
[2]mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Hath in these last days spoken unto us by his Son, whom he hath appointed heir of all things, by whom also he made the worlds;”
>> YESU KRISTO NI NENO TAKATIFU LA MUNGU KWA ULIMWENGU WOTE KATIKA SIKU ZA MWISHO
>> HII INA MAANA UKIMWAMINI YESU UMEMWAMINI YEYE ALIYEMTUMA!!
>> HUWEZI KUMWAMINI MUNGU PASIPO KUMWAMINI YESU!!
>> NA HUWEZI KUMWAMINI YESU HALAFU USIOKOKE!!
》》》“Yohana 1:1
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.”
》》》”Yohana 1:3
[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
All things were made by him; and without him was not any thing made that was made.”
>> NAYE NENO ALIKUWA MUNGU
>> PASIPO YEYE HAKIKUFANYIKA CHOCHOTE KILICHOFANYIKA........!!!
>> KILA KITU KILIUMBWA AMA KUFANYWA KWA NENO LA MUNGU
>> HATA SASA KILA KITU BADO KINAFANYIKA KWA NENO LA MUNGU
>> KWA SABABU YA DHAMBI YOTE YANAYOFANYIKA LEO PASIPO NENO LA MUNGU NI UASI, NI UHARIBIFU, NI MAUTI!! Yaani, Mungu hayumo ndani yake!!! Humu ndimo yanazaliwa matatizo ya mwanadamu!!! Matatizo yako hayawezi kwisha katika ulimwengu wa roho pasipo Yesu kukuosha moyo wako na kukupa moyo mpya, roho mpya, na lugha mpya!!(lugha ya maandiko/lugha ya neno)[ Ezekiel 36:25-26, Marko 16:17b)
>> Matatizo yako yataondolewa kwa Neno! Jibu lako limo kwenye neno! Utatuzi wako umo kwenye neno! NA HUYO NENO NI YESU
>> Pasipo Neno dhambi inatawala! Pasipo Yesu dhambi itakutawala! Dhambi inamzuia Mungu kufanya kazi maishani mwako! KUMBUKA DHAMBI NI UASI WA NENO!! Ni kiasi kile hulipendi Neno, ni kiasi kile hulitaki neno, ni kiasi kile hulithamini neno, ni kiasi kile hulihitaji neno, ni kiasi kile hulitumainii neno, ni kiasi kile hulitamani neno, ni kiasi kile hulijui neno, ni kiasi kile unalidharau neno, ni kiasi kile unalipuuza neno, ni kiasi kile hulifurahii nenonini kiasi kile huoni umuhimu wa kujifunza neno, ni kiasi kile unajiona tayari umelijua neno, ni kiasi kile huna hofu na neno, ni kiasi kile unapingana na neno, ni kiasi kile haulitendi neno,ni kiasi kile humuoni Yesu kwenye neno, ni kiasi kile humsikii Yesu kwenye neno, ni kiasi kile hulikimbilii neno upatapo tatizo au ugumu au changamoto kwenye maisha!! HAYA YOTE NI KIWANGO CHA MOYO WAKO USIVYOMWAMINI YESU NA ULIVYO MBALI NAYE!!NI KIWANGO CHAKO CHA MOYO WAKO KUTOKUWA SAFI!!! DAUDI ALINENA;
“Zaburi 119:11
[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi.
Thy word have I hid in mine heart, that I might not sin against thee.”
>> USIKIMBILIE KUJAZA NENO KWA KULIKARIRI, NENO LAZIMA LIKAE MOYONI KWA NJIA YA IMANI!! KWA MOYO MTU HUAMINI....!!! LAZIMA UMWAMINI YESU ILI NENO LIKAE KAMA ROHO MOYONI MWAKO!! YESU NDIYE ROHO WA NENO (1 KOR 15:45) NA NDIYE AKUPAYE UZIMA WA MILELE NA MAISHA TELE (YOHANA 6:63 & 10:10)
>> UNA SHIDA? UNA TATIZO? UNA MATESO? ANZA NA NENO!! PEKUA BIBLIA UKUTANE NA NENO MAHSUSI LA KUKUFAA!! ANZIA HAPO KISHA TWENDE HATUA YA PILI!! TUKUTANE SEHEMU YA PILI!!