*LAZIMA UISIKIE SAUTI YA MUNGU*

 


*LAZIMA UISIKIE SAUTI YA MUNGU* 


Yohana 10:2-3

[2]Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 

But he that entereth in by the door is the shepherd of the sheep.

[3]Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 

To him the porter openeth; and the sheep hear his voice: and he calleth his own sheep by name, and leadeth them out.

>> KONDOO WA YESU, MCHUNGAJI MWEMA, HUWA WANAISIKIA SAUTI YAKE

>> KUISIKIA SAUTI YA YESU SIYO UPENDELEO (PRIVILEDGE) WA WATU WACHACHE TU!!

>> YESU HUWAITA KWA MAJINA YAO NAO HUMFUATA PALE ANAPOWATOA NJE NA KUWAONGOZA!!

>> MCHUNGAJI MWEMA HUINGIA NDANI YAKO KUPITIA MOYO WAKO UNAPOMWAMINI, KUMSIKIA, NA KUMFUNGULIA MLANGO

>> ZIPO SAUTI HUJA KUPITIA MAWAZO NAFSINI MWAKO, LAKINI HIZO SI SAUTI ZA MCHUNGAJI MWEMA

Yohana 10:4

[4]Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 

And when he putteth forth his own sheep, he goeth before them, and the sheep follow him: for they know his voice.

>> KUMFUATA YESU KUNAHITAJI UIJUE SAUTI YAKE

Yohana 10:5

[5]Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. 

And a stranger will they not follow, but will flee from him: for they know not the voice of strangers.

>> ZIPO SAUTI ZA WAGENI AMBAZO SI ZA MCHUNGAJI MWEMA YESU 

>> HIZO SAUTI KONDOO HAWAZIJUI  BALI WANAIJUA SAUTI MOJA TU YA MCHUNGAJI MWEMA YESU

>> KONDOO WA YESU HUWAKIMBIA WAGENI NA KAMWE HAWAWAFUATI

Yohana 10:9

[9]Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 

I am the door: by me if any man enter in, he shall be saved, and shall go in and out, and find pasture.

>> KAMA WEWE NI KONDOO LAZIMA UWE UMEOKOKA KWELI KWELI MAANA YESU NDIYE MLANGO PEKEE WA WOKOVU

>> UKIWA UMEOKOKA LAZIMA UTAKUWA UNAPATA MALISHO KWA YESU NA UNASHIBA MAANA YEYE NI MCHUNGAJI MWEMA ANAYEKUCHUNGA NA KUKULISHA SIKUZOTE 

>> Yohana 10:8

[8]Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. 

All that ever came before me are thieves and robbers: but the sheep did not hear them.

>> SHETANI NA WATUMISHI WAKE KAZI YAO NI KUJARIBU KUIBA NA KUNYANG'ANYA KONDOO, LAKINI HILO HALIWEZEKANI MAANA KONDOO WA YESU WANAIJUA SAUTI YAKE 

>> UKIJIKUTA UNAHAHA NA KUHANGAIKA HUKO NA KULE KUTAFUTA MALISHO, UPONYAJI, BARAKA, N.K. NI DHAHIRI KWAMBA WEWE UMEKATAA KUWA KONDOO WA YESU, KWA MAANA VITU VYOTE NA MAMBO YOTE VINAPATIKANA KWAKE YESU NA KWA UTELE!! LAKINI WEWE BADO UNAHAHA!!!!!

IMEANDIKWA;

1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. 

Zaburi 23:1

>> KWA YESU WANGU SIPUNGUKIWI CHOCHOTE WALA KUHITAJI KITU, YESU ANATOSHA

2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. 

Zaburi 23:2

>> SIONI NJAA WALA KIU NIKIWA NA YESU, MAANA NAKULA NA KUYWA WAKATI WOTE

3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 

Zaburi 23:3

>> NAFSI YANGU ANAIPA UHAI NA UZIMA UTOKAO KWAKE, ANANIPA AMANI NA KUNIONGOZA KUTENDA HAKI SIKUZOTE 

>> KAMA UKO NA WEZI NA WANYANG'ANYI UTAKUWA BADO UNATENDA DHAMBI, UNA FADHAA TELE, UNA MASUMBUFU YA MAISHA, MAHANGAIKO TELE, HUNA AMANI, BADO UNA NJAA NA KIU YA KUTENDA DHAMBI, N.K.

4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. 

Zaburi 23:4

>> SINA HOFU NIKO NA YESU NA UWEPO WAKE UMENIWEKA SALAMA NA ANANIFARIJI KILA WAKATI

5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. 

Zaburi 23:5

>> YESU ANANIBARIKI NA KUNIINUA, NAFAIDI VINONO NA VITAMU MEZANI PAKE HUKU ADUI ANAONA NA KUSAGA MENO MAANA HAWEZI KUFANYA LOLOTE KUZUIA BARAKA NA VINONO  VYA YESU KWANGU

6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. 

Zaburi 23:6

>> MATOKEO YA KUMFUATA HUYU YESU NI UHAKIKA NILIONAO KWAMBA WEMA NA FADHILI ZINAFUATANA NAMI SIKUZOTE ZA MAISHA YANGU!!

SAUTI YAKE 

>> HAYA YOTE NI MAZAO YA KUISIKIA SAUTI YAKE!! HUWEZI KUISIKIA SAUTI YAKE KAMA HAUISHI KWA IMANI TAKATIFU YESU KRISTO YA WOKOVU!! MAANA IMEANDIKWA, "Warumi 10:17

[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. 

So then faith cometh by hearing, and hearing by the word of God."

>> CHANZO CHA IMANI NI KUSIKIA!!!

>> NA HUKO KUSIKIA HUJA KWA NJIA YA NENO LA KRISTO! KIVIPI??!! NABII EZEKIELI ANAELEZA; "Ezekieli 2:1-2

[1]Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe. 

And he said unto me, Son of man, stand upon thy feet, and I will speak unto thee.

[2]Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami. 

And the spirit entered into me when he spake unto me, and set me upon my feet, that I heard him that spake unto me."

1) MUNGU ALISEMA NA NABII EZEKIELI 

2) ALIPOSEMA NAYE roho ILIMWINGIA

3) ILE roho ILIYOMWINGIA NDIYO ILIYO KUWA NA NGUVU ZA KUMSIMAMISHA NABII EZEKIELI 

4) NDIPO EZEKIELI NABII AKAMSIKIA YEYE ALIYESEMA NAYE!

>> roho ya neno la Mungu ilimwingia nabii aliyekuwa amefungua moyo wake

>> hiyo roho ndiyo iliyomfanya nabii amsikie Yeye aliyesema naye baada ya kuingiwa na kusimamishwa kwa nguvu  za hiyo roho

>> Nabii Ezekieli alimsikia Mungu katika roho

>> Imani inazaliwa pale roho ya neno inapounganika na roho yako iliyozaliwa mara ya pili, na ndipo tunasema umemsikia Yeye aliyesema nawe!!

2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. 

Waebrania 4:2

>> Neno lililonenwa halina faida wala manufaa yoyote kwako lisipochanganyika na imani ndani yako!!

>> Yaani, lile neno linabaki ni neno tu au andiko tu na wala ile roho ya neno lile haijakuingia rohoni mwako na kuwa mmoja nawe, na hivyo tunasema haujamwamini Mungu na sababu ni kuwa haujamsikia Mungu!

>> Kuamini kunauunganisha na Mungu (Neno) katika roho! Yohana 6:63 inasema; 63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. 

Yohana 6:63

>> MANENO YA KRISTO YESU YOTE ni roho, TENA ni uzima (life)

>> Neno la Kristo linakuwa roho na uzima rohoni mwako pale unapoliamini, NA NDIPO TUNASEMA UMEMSIKIA MUNGU!! Kamwe huwezi kuasi kama umemsikia Mungu kweli katika roho!! KUSIKIA NI KUAMINI NA KUAMINI NI KUSIKIA

>> KUSIKIA KUNAKUJAZA ROHO NA KUAMINI HALIKADHALIKA KUNAKUJAZA ROHO

>> KUSIKIA KUNAKUUNGANISHA NA MUNGU KATIKA ROHO HALI KADHALIKA KUAMINI NAKO!

>> KUSIKIA NI KUISIKIA KWA ROHO YAKO SAUTI YA MUNGU KUPITIA ILE ROHO YA LILE NENO LAKE, YAANI, KUSIKIA KATIKA ROHO!!!

>> TUNABATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU ILI TUENDELEE KUJAZWA ROHO KUPITIA NENO LAKE TUNALOENDELEA KULIAMINI

>> KUAMINI NI KUJAZWA ROHO YA MUNGU NA NGUVU ZAKE ZA KULITENDA NA KULIISHI HILO NENO LA KRISTO ULILOLIAMINI,  NA NDIYO MAANA IMANI YA KWELI INAONEKANA KWENYE UTENDAJI WA NENO!!

>> UKIAMINI UNAKUWA UMEPOKEA SAUTI YA MUNGU NDANI YAKO KUPITIA ILE ROHO ILIYOKUINGIA YA LILE NENO ULILOLIAMINI!! KUJAA IMANI NI KUJAA SAUTI YA MUNGU NA NGUVU ZAKE ZA KUTENDA YOTE ISEMAVYO SAUTI HIYO

>> HUWEZI KUMWAMINI YESU HALAFU USIFANYE ASEMAVYO! HUO NI UONGO KWA MAANA HAPO HUJAAMINI BADO WALA SAUTI YAKE HUNA MOYONI MWAKO

>> HUKU NDIKO KUSIKIA KUNAKOPELEKEA IMANI MOYONI MWAKO 

>> WEWE ANZIA HAPA:

16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 

Wakolosai 3:16

>> ZINGATIA SANA HILI MAANA IMEANDIKWA PIA,

11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. 

Zaburi 119:11

>> NENO LA MUNGU NI TAKATIFU NA HIVYO KUJAA ROHO YA HILI NENO NI KUJAA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE ZA KUKUPELEKEA KUISHI MAISHA MATAKATIFU!!! KWA MAANA MAISHA HUTOKA KWA HUYO ROHO (YOHANA 6:63)

>> NDIYO NI BORA KUJAA NENO MOYONI KULIKO KILA KITU KINGINE

23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. 

Mithali 4:23

>> KWA MAANA,

Ayubu 26:4

[4]Je! Umetamka maneno kwa nani? 

Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako? 

To whom hast thou uttered words? and whose spirit came from thee?

>> MTU ANAPONENA HUWA KUNA ROHO INAONGEA KUTOKA ROHONI (MOYONI) MWAKE 

>> KAMA HASEMI NENO BASI KUNA ROHO AMBAYO SI ROHO MTAKATIFU INAONGEA! AKISEMA NENO KWA UNYOOFU NA UAMINIFU BASI;

2 Samweli 23:2

[2]Roho ya BWANA ilinena ndani yangu, 

Na neno lake likawa ulimini mwangu. 

The Spirit of the LORD spake by me, and his word was in my tongue.

>> HUWEZI KUONGEA NENO LISILOKUWEMO MOYONI MWAKO!! KUMBUKA; 11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. 

Zaburi 119:11

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post