UDHAIFU NA MAPUNGUFU YAKO HAVIKUZUII KUWA MTAKATIFU



HAKUNA UDHAIFU WALA MAPUNGUFU YA KIBINADAMU YANAYOWEZA KUATHIRI UTAKATIFU WA MWAMINI-2

Warumi 6:5-7

[5]Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 

For if we have been planted together in the likeness of his death, we shall be also in the likeness of his resurrection:

>> KWA IMANI TWAJUA ALIPOKUFA MSALABANI NASI TULIKUFA PAMOJA NAYE 

>> VIVYO HIVYO TWAJUA ALIPOFUFUKA SISI NASI TULIFUFULIWA PAMOJA NAYE!!

[6]mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 

Knowing this, that our old man is crucified with him, that the body of sin might be destroyed, that henceforth we should not serve sin.

>> HAUWEZI KUFA PASIPO KUSULUBIWA! HIVYO KILICHOSULUBIWA NI UTU WETU WA KALE/UTU WETU WA DHAMBI/ UBINADAMU WETU UNAOHARIBIKA WENYE MAPUNGUFU NA UDHAIFU MWINGI!

>> BAADA YA KUSULUBIWA HUKU MWILI WA DHAMBI UMEBATILIKA NA HATUTUMIKII DHAMBI TENA, NA TUMEKUWA WATUMWA WA HAKI, KATIKA UTUMISHI WA UTII

18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki. 

Warumi 6:18

19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. 

Warumi 6:19

20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. 

Warumi 6:20

21 Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. 

Warumi 6:21

UTAKATIFU 22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. 

Warumi 6:22

>> TUMETAKIWA KUJUA KWAMBA HILI NI JAMBO LILILOTENDWA TAYARI NA KUKAMILIKA, NASI TUNATAKIWA TU KUAMINI NA KUPOKEA KULE KUSULUBIWA, KUFA, NA KUFUFUKA, ILI NGUVU ZA MUNGU ZITENDE KAZI KWA NJIA YA NEEMA YAKE KUTUWEZESHA KUISHI KATIKA NGUVU ZA UFUFUO. WA YESU KRISTO (RESURRECTION POWER OF JESUS CHRIST)

>> UDHAIFU WANGU NA WAKO WA KIBINADAMU ULISULUBIWA MSALABANI!! WEWE UNA NGUVU ZILIZOMFUFUA YESU KUTOKA KWA WAFU ZIKITENDA KAZI NDANI YAKO!! UNAISHI MAISHA YA UFUFUO (RESURRECTION LIFE)

>> UNA NGUVU, UNAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE AKUTIAYE NGUVU ( WAFILIPI 4:13)

[7]kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. 

For he that is dead is freed from sin.

>> UKIFA UNAKUWA UMEHESABIWA HAKI MBALI NA DHAMBI!! LAZIMA UFE!! JE! UNAAMINI KWAMBA UTU WAKO WA KALE ULISULUBIWA PAMOJA NA KRISTO???!!! (RUM 6:6) KAMA UNAAMINI ULISULUBIWA PAMOJA NA KRISTO LAZIMA UAMINI ULIKUFA PAMOJA NAYE, UKAFUFULIWA PAMOJA NAYE, NA SASA UNAISHI PAMOJA NAYE KATIKA NGUVU ZA UFUFUO NA SI KATIKA UDHAIFU TENA!! 

1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 

Wakolosai 3:1

2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 

Wakolosai 3:2

3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 

Wakolosai 3:3

4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. 

Wakolosai 3:4

5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 

Wakolosai 3:5

6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. 

Wakolosai 3:6

7 Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. 

Wakolosai 3:7

KUAMINI KUNAKUONDOA KWENYE KUTAZAMA KWA MACHO YA DAMU NA NYAMA HII NYUMBA YETU YA UDONGO NA KUTAZAMA INAVYOCHOKA, INAVYOZEEKA, ISIVYO NA NGUVU ZA KUTOSHA, INAVYOSHAMBULIWA NA MAGONJWA, N.K. BALI UNAPOAMINI UTAMTAZAMA YEYE ALIYE HAI AISHIE NDANI YAKO!!

20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. 

Wagalatia 2:20

>> UTU WA KALE ULIOSULUBIWA NA KUFA NDIO ULIOBEBA UDHAIFU NA MAPUNGUFU YOTE YA KIBINADAMU!! KAMA UMO NDANI YAKE WEWE SI DHAIFU!! ALIYE DHAIFU ASEME MIMI HODARI!! ANAYESHAMBULIWA MAGONJWA ASEME KWA KUPIGWA KWAKE YESU MIMI NIMEPONA, MASKINI ASEME MIMI NI TAJIRI NILIYEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO YESU,  NA BARAKA HIZO ZIMENITAJIRISHA KWA UTAJIRI WOTE, ALIYE MNYONGE ASEME BWANA AMENIINUA KUTOKA MAVUMBINI KWENYE UNYONGE, NA KUTOKA JALALANI KWENYE UHITAJI, NA AMENIKETISHA JUU PAMOJA NA WAKUU, ANAYESHINDWA SHINDWA NA ASIYEWEZA NA ASEME, NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU, MWENYE MKE MSUMBUFU, MGOMVI, MKOROFI MKOROFI, ANAYEJIBU MAJIBU YA KUUMIZA ASEME NINA MKE MCHA MUNGU, MPOLE, MKIMYA, MNYENYEKEVU,  MTULIVU, ANAYENITII NA KUNIHESHIMU SIKUZOTE, NA TUNAELEWANA, TUNAPENDANA, TUNACHUKULIANA, TUNASAMEHEANA, TUNATENDEANA MEMA, N.K. N.K. SIKUZOTE!! N.K. HIZO NI NGUVU ZA KUFUFUKA KWAKE YESU, HAMNA UNYONGE TENA, HAMNA KUSHINDWA TENA, HAINA MAKWAZO TENA, NA YAKIJA NI MWENDO WA KUYASHINDA KWA NEEMA YAKE , HALELUYA!! HAKUNA UDHAIFU, BALI KUNA KUMZALIA MUNGU MATUNDA, TUMEUVUA UTU WA KALE PAMOJA NA MATENDO NA MAWAZO YAKE MABAYA, NA TUMEUVAA UTU MPYA ULIOUMBWA KWA SURA NA MFANO WAKE KATIKA HAKI NA UTAKATIFU WA KWELI!! MADHAIFU YA KIBINADAMU YALIKOMESHWA NA YESU KWENYE MWILI HUU!! 17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. 

Mathayo 8:17

>> YESU MWENYEWE ALIUTWAA UDHAIFU WETU WOTE PALE JUU MSALABANI........! SISI SI DHAIFU BALI TUMEJAA NGUVU!! Biblia inasema, 

1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. (Warumi 8:1)

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. (Warumi 8:2)

>> SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI NI SHERIA YA UDHAIFU, SHERIA YA 

3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 

(Warumi 8:3)

4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. 

Warumi 8:4

>> BWANA YESU ALIIHUKUMU DHAMBI KWENYE MWILI!!

>> BWANA ALIUVAA MWILI ILI ATUSHINDIE UDHAIFU WOTE WA KIMWILI ULIOKUWA KAMWE HAUWEZI NA HAUTAKI KUITII SHERIA YA MUNGU

>> BAADA YA YESU KUIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI NDIPO, MAAGIZO YOTE YA TORATI YAKATIMIZWA NDANI YETU SISI TUNAOISHI NA KUENENDA KWA ROHO

>> HAKUNA TENA KISINGIZIO CHA HAKUNA MKAMILIFU, HAKUNA ASIYE NA MAPUNGUFU, NJOO KWA YESU UMWAMINI,  KISHA USULUBIWE PAMOJA NAYE,  UFE PAMOJA NAYE, NA KISHA UFUFULIWE PAMOJA NAYE, UTAONA NENO LA MSALABA, AMBALO NI NGUVU ZA MUNGU KWAKO WEWE UNAYEAMINI, LIKITENDA KAZI MAISHANI MWAKO KUKUWEZESHA KUMZALIA MUNGU MATUNDA KWA KUENENDA KWA ROHO SIKUZOTE!!! IT TAKES FAITH AND NOT HUMAN EFFORTS!! INAHITAJI IMANI NA SIYO JUHUDI AU BIDII ZOZOTE ZA KIBINADAMU!!! INAHITAJI KUAMINI NA SIYO KUTOA SANA AU KUFUNGA SANA N.K. MAANA HAUFI KWA KUFUNGA KAMA VILE USIVYOOKOKA KWA KUFUNGA BALI NI KWA KUAMINI TU!! UTU WAKO WA DHAMBI, UTU WAKO WA KALE, UBINADAMU WAKO DHAIFU WENYE MAPUNGUFU ULISULUBIWA!! JE! UTAMVAA YESU AU MAUTI YA MAPUNGUFU NA MADHAIFU YA KIBINADAMU??!!!

9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; 

Wafilipi 3:9

10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 

Wafilipi 3:10

11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. 

Wafilipi 3:11

>> NATAKA: (OMBA SANA NA AMINI SANA NA KIRI SANA NENO HILI)

1) NATAKA NIMJUE YESU

2) NATAKA NIUJUE UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE/ NIZIJUE NGUVU ZILIZOMFUFUA YESU

3) NATAKA NIUJUE KWENYE MAISHA HALISI USHIRIKA WA MATESO YAKE

29 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; 

Wafilipi 1:29

4) NATAKA NIFANANISHWE NA KUFA KWAKE, niifie dhambi, niufie udhaifu wa mwili, niifie dunia hii na tamaa zake, n.k.

5) ILI NIWEZE KUFIKIA KIYAMA YA WAFU, KWA KIINGEREZA HII NI RESURRECTION OF THE DEAD, YAANI, UFUFUO WA WAFU AMA UFUFUO WA WENYE HAKI!!

28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 

Yohana 5:28

29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu. 

Yohana 5:29

>> ULIYEOKOKA UNAYEMWAMINI YESU UMEFUFULIWA KUTOKA MAUTINI, USIKAE TENA MAUTINI!!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post