MAPUNGUFU YA KIBINADAMU HAYAZUILII MWAMINI KUWA MTAKATIFU



MAPUNGUFU YA KIBINADAMU HAYAATHIRI UTAKATIFU WA MWAMINI BALI HUMSAIDIA KUKUA KUELEKEA UKAMILIFU

Upungufu wa kibinadamu ni hali ya mwili wake pamoja na utu wake wa mwilini  kushindwa na/au kutoweza kabisa KUYAKUBALI, KUYAELEWA, KUYAPOKEA, KUYAFAHAMU, KUYAZINGATIA, KUYATAFUTA, KUYAFIKIRI, KUYAWAZA, KUYAISHI, NA KUYATENDA MAMBO YA MUNGU ALIYE ROHO (mambo ya Roho) KAMA YALIVYOFUNULIWA KATIKA NENO LAKE, PASIPO MSAADA WAKE YEYE MWENYEWE KWA ROHO WAKE MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE PALE UNAPOMWAMINI YESU KRISTO NA KISHA UKAMPOKEA AKAWA BWANA NA MWOKOZI WAKO BINAFSI!! "..........pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote!" (Yoh 15:5C)

Warumi 8:3-9

[3]Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 

For what the law could not do, in that it was weak through the flesh, God sending his own Son in the likeness of sinful flesh, and for sin, condemned sin in the flesh:

>> UDHAIFU MWILI ULIMFANYA MWANADAMU ASHINDWE KUITII TORATI, MPAKA IKAJA NEEMA!!

[4]ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. 

That the righteousness of the law might be fulfilled in us, who walk not after the flesh, but after the Spirit.

[5]Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 

For they that are after the flesh do mind the things of the flesh; but they that are after the Spirit the things of the Spirit.

[6]Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 

For to be carnally minded is death; but to be spiritually minded is life and peace.

[7]Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 

Because the carnal mind is enmity against God: for it is not subject to the law of God, neither indeed can be.

[8]Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. 

So then they that are in the flesh cannot please God.

[9]Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 

But ye are not in the flesh, but in the Spirit, if so be that the Spirit of God dwell in you. Now if any man have not the Spirit of Christ, he is none of his.

>> UDHAIFU WA MWILI NA MAPUNGUFU YA KIBINADAMU YANAMEZWA NA KUTOWESHWA NA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE ROHONI NDANI YAKO UNAPOMPOKEA NA KUANZA KUISHI NA KUENENDA UKIONGOZWA NAYE

>> ROHO MTAKATIFU NDIYE ROHO WA UUNGU WETU NDANI YA MWILI ULIO DHAIFU

2 Petro 1:3-4

[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 

According as his divine power hath given unto us all things that pertain unto life and godliness, through the knowledge of him that hath called us to glory and virtue:

>> NGUVU ZAKE ZA UUNGU ZIMETUPATIA VITU VYOTE VYENYE KUTUWEZESHA, SISI TULIOAMINI NA KUJAZWA ROHO, KUISHI MAISHA YAKE YA UUNGU NA UTAUWA KWENYE MWILI HUU WA DAMU NA NYAMA

2 PET 1:4

[4]Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. 

Whereby are given unto us exceeding great and precious promises: that by these ye might be partakers of the divine nature, having escaped the corruption that is in the world through lust.

>> AMETUKIRIMIA PIA AHADI KUBWA MNO NA ZA THAMANI KWENYE NENO LAKE ILI KWAMBA, KWA HIZO, TUPATE KUWA WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU (PARTAKERS OF THE DIVINE NATURE)! HAKUNA MAPUNGUFU YA KIBINADAMU KWENYE UUNGU MAANA SI WEWE UNAYEISHI BALI KRISTO YU HAI NDANI YAKO (GAL 2:20)

>> HAMNA KISINGIZIO MAANA MUNGU AMETUPA KILA KINACHOTAKIWA ILI TUISHI NA KUENENDA KAMA miungu KATIKA MWILI WA DAMU NA NYAMA!!

1) YESU MWANA WA MUNGU ALIKUWA MUNGU KATIKA MWILI

2) LEO HII YESU NDANI YETU AMETUFANYA SISI KUWA WANA WA MUNGU NA miungu KATIKA MIILI YA DAMU YA NYAMA WASIO NA MAPUNGUFU YOYOTE BALI WAKAMILIFU KAMA BABA YETU WA MBINGUNI ALIVYO MKAMILIFU!

>> TUENDELEE KUKUA KUELEKEA HUKU KWENYE MIISHO YA KIMAANDIKO 

>> Mathayo 5:48

[48]Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. 

Be ye therefore perfect, even as your Father which is in heaven is perfect.

>> Wakolosai 2:9-10

[9]Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. 

For in him dwelleth all the fulness of the Godhead bodily.

[10]Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. 

And ye are complete in him, which is the head of all principality and power:[ NAMI/NAWE NIME/UME TIMILIKA NDANI YAKE YEYE....]

>> NDANI YA YESU WEWE NI MKAMILIFU NA MTIMILIFU MACHONI PAKE!! LAKINI LAZIMA UENDELEE KUKUA NA KUJITAKASA

13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; (Waefeso 4:13)

>> TUNAKUA HADI TUNAKAMILIKA!!

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 

Waefeso 4:14

15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 

Waefeso 4:15

>> LAZIMA TUKUE HADI TUMFIKIE YESU KATIKA MAMBO YOTE

1 Yohana 2:6

[6]Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. 

He that saith he abideth in him ought himself also so to walk, even as he walked.

>> LAZIMA DUNIA YOTE IMUONE YESU AKIISHI NA KUENENDA NDANI YAKO VILE VILE KAMA YESU ALIVYOENENDA NYAKATI ZA BIBLIA 

>> KAMA KUNA MAPUNGUFU LEO BASI NI KUTOKUWA KAMA YESU

2 Petro 3:18

[18]Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele. 

But grow in grace, and in the knowledge of our Lord and Saviour Jesus Christ. To him be glory both now and for ever. Amen.

>>  NDIYO MAANA LAZIMA TUKUE KATIKA NEEMA NA KATIKA KUMJUA YESU!!!

>> SAFARI HII INAANZA NA KUENDELEA KWA KUENENDA KWA ROHO MTAKATIFU SIKU ZOTE!!

>> 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 

Wagalatia 5:16

>> MAPUNGUFU YANAJIONYESHA KUPITIA TAMAA ZA KIMWILI ZINAZOWATAWALA WASIOMFUATA ROHO MTAKATIFU 

24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 

Wagalatia 5:24

25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. 

Wagalatia 5:25

>> miungu wanaishi na kuenenda kwa Roho Mtakatifu!! miungu hawana mapungufu kwa sababu ya neema tele iliyo juu yao na maishani mwao!!

>> tazama watakatifu kwa macho saba na kamwe hutaona mapungufu!!

Isaya 11:3

[3]na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; 

And shall make him of quick understanding in the fear of the LORD: and he shall not judge after the sight of his eyes, neither reprove after the hearing of his ears:

>> YESU KAMWE HAHUKUMU KWA KUFUATA YALE ANAYOYAONA NA ANAYOYASIKIA!! HUKUMU YA MACHO NA MASIKIO NI HUKUMU YA KIMWILI! NI HUKUMU YA WATOA VIBANZI WASITOA BORITI ZAO WENYEWE (MATH 7:1-5) AMBAO YESU ALIWAITA WANAFIKI!! MUNGU HAHUKUMU HIVYO, JIFUNZE HUKUMU YA HAKI!! HAUTAENDELEA KUONA MAPUNGUFU YA MWILI WA KRISTO!! UTAANZA KUSEMA KWA IMANI NA KUBADILI WATU NA HALI KWA KINYWA CHAKO NA SIYO KUHARIBU KWA KUTOAMINI KWAKO!!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post