NGUVU YA KUSHINDA DHAMBI



NGUVU YA KUSHINDA DHAMBI

Biblia inasema, 

"1 Wakorintho 15:56

[56]Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 

The sting of death is sin; and the strength of sin is the law.["1 Corinthians 15:56 NIV

[56]The sting of death is sin, and the power of sin is the law."]

>>  NGUVU YA DHAMBI NI TORATI AU SHERIA 

>> YAANI, SHERIA AU TORATI NDIYO INAYOIPA AU KUITIA NGUVU DHAMBI 

>> PASIPO SHERIA AU TORATI DHAMBI IMEKUFA

Warumi 7:8

[8]Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa. 

But sin, taking occasion by the commandment, wrought in me all manner of concupiscence. For without the law sin was dead.

>> DHAMBI ILIKUWEPO KABLA YA SHERIA, LAKINI ILIPOKUJA ILE TORATI/SHERIA DHAMBI ILIPATA NAFASI IKAHUIKA MWANADAMU AKAFA

>> LAKINI DHAMBI BILA SHERIA IMEKUFA! FAIDA YA SHERIA ILIKUWA NI KUNISAIDIA KUTAMBUA DHAMBI LAKINI SI KUIONDOA DHAMBI

7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani. 

Warumi 7:7

8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa. 

Warumi 7:8

>> HII NDIO MAANA TORATI IKAFUATIWA NA NEEMA!!

17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. 

Yohana 1:17

>> MUSA ALITULETEA TORATI, YESU AKATULETEA NEEMA NA KWELI

14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. 

Warumi 6:14

>> DHAMBI HAIWEZI KAMWE MILELE YOTE KUKUTAWALA IKIWA UPO CHINI YA NEEMA YAKE KRISTO YESU MWOKOZI!!

Tito 2:11

[11]Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 

For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men,

>> NEEMA YA MUNGU NDIYO INAYOOKOA WANADAMU WOTE (SAVING GRACE)

Tito 2:12

[12]nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 

Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world;

>> NEEMA HIYO INATUFUNDISHA PIA, SIYO KUOKOA TU PEKE YAKE, BALI: (INSTRUCTING GRACE) 

1. KUKATAA UBAYA WOTE NA TAMAA ZOTE  ZA KIDUNIA

2. KUISHI MAISHA YA UTAUWA (GODLY LIVING)

3. KUISHI MAISHA YA KIASI (SELF-CONTROLLED LIVING)

4. KUISHI MAISHA YA HAKI ( RIGHTEOUS LIVING)

>> HII NDIYO MAANA UKIWA CHINI YA NEEMA DHAMBI HAINA NAFASI KWAKO!! UNAISHI MAISHA YA USHINDI DHIDI YA DHAMBI

>> LAKINI HUWEZI KUPOKEA NEEMA YA KRISTO PASIPO KUMWAMINI YESU KRISTO/PASIPO KUMPOKEA YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO BINAFSI/ PASIPO KUAMINI KUWA YESU NI KRISTO/ PASIPO KUZALIWA MARA YA PILI/ PASIPO "KUAMINIIII!!!"

>> Waefeso 2:8-9

[8]Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 

For by grace are ye saved through faith; and that not of yourselves: it is the gift of God:

[9]wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 

Not of works, lest any man should boast.

>> HATUOKOKI KWA MATENDO MEMA

>> TUNAOKOLEWA KWA NEEMA KWA NJIA YA IMANI

>> ILI UPOKEE NEEMA YA WOKOVU LAZIMA UMWAMINI YESU!!

>> UKISHAKUMWAMINI YESU NA KUOKOKA LAZIMA UENDELEE KUISHI KWA IMANI YA YESU ILI UZIDI KUPOKEA NEEMA JUU YA NEEMA KAMA MAANDIKO YANENAVYO:

16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. (Yohana 1:16)

John 1:16

[16]For out of His fullness (abundance) we have all received [all had a share and we were all supplied with] one grace after another and spiritual blessing upon spiritual blessing and even favor upon favor and gift [heaped] upon gift.

>> MAISHA YA WOKOVU TUNAISHI KWA NEEMA KADIRI TUNAVYOISHI NA KUENENDA KWA IMANI

16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. 

Warumi 1:16

17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. 

Warumi 1:17

>> HAKI YA MUNGU INADHIHIRISHWA NDANI YAKO TOKA IMANI HATA IMANI! KULE KUSEMA IMANI HATA IMANI MAANA YAKE UNAZIDI KUJAA NENO UNALOLIAMINI AMBALO LINAKUWA SEHEMU YA WEWE KATIKA ROHO.YAANI, LILE NENO LINAUNGANIKA NA WEWE NA KUWA ROHO MOJA NA WEWE!! KIVIPI???!!! BIBLIA INASEMA,

John 6:63

[63]It is the Spirit who gives life; the flesh profits nothing. The words that I speak to you are spirit, and they are life.

63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. 

Yohana 6:63

>> MWILI HAUFAI KITU

>> ROHO NDIYE ATUPAYE UZIMA/ MAISHA YA MUNGU KWENYE NENO LAKE

>> MANENO YA KRISTO YESU YOTE NI MANENO YA MUNGU, NAYO NI UZIMA/ MAISHA (life), NA TENA NI roho/spirit!

>> MAISHA YETU TULIOOKOKA YAMO NDANI YA NENO

>> NENO LA KRISTO NI ROHO 

>> HII MAANA YAKE NENO UNALOLIAMINI LINAKAA NDANI YAKO KAMA "roho" NA KUKUPA "maisha ya hiyo roho" ILI UYAISHI KWA NGUVU ZA HIYO "roho"

>> Ukiamini neno la kusamehe linakupa ndani yako/ moyoni mwako/ rohoni mwako roho ya kusamehe yenye nguvu za Mungu za kusamehe nayo ndiyo inayokuwezesha kusamehe!!

>> Ukiamini neno la utoaji linakupa roho na maisha ya utoaji, ambapo nguvu za utoaji za hiyo roho zinakuwezesha kutoa pasipo kuombwa au kulazimishwa au kuhimizwa saaana!!

>> Neno la upendo lina roho, nguvu na maisha ya upendo kukuwezesha wewe kupenda pale unapoliamini hilo neno

>> Neno la utii lina roho, nguvu, na maisha ya utii kukuwezesha wewe kutii pale unapoliamini hilo neno

>> Neno la kuchukia uovu lina roho, nguvu, na maisha ya kuchukia uovu kukuwezesha wewe kuchukia uovu pale unapoliamini hilo neno!

>> Neno la utakaso lina roho, nguvu, na maisha ya utakaso kukuwezesha wewe kujitakasa pale unapoliamini hilo neno!

>>  Neno la uponyaji lina roho, nguvu, na maisha ya uponyaji kukuwezesha wewe KUPONA NA KUPOZA wagonjwa kwa jina la Yesu pale unapoliamini hilo neno!

>> neno ni roho, neno ni uzima, neno ni maisha ya mtakatifu!! Kwa maana neno hilo ni takatifu!! Na hiyo roho ya hilo neno ni takatifu!!

>> Yohana 6:63 anaposema maneno hayo ni roho na tena ni uzima au maisha analenga roho yako iliyozaliwa mara ya pili!! Kuamini neno kunapelekea roho ya hilo neno kuunganika na roho yako na wewe kushiba na kunenepa kiroho! Unakuwa roho moja na hilo neno uliloliamini!!

>>  NEEMA NI [ NENO + ROHO YA HILO NENO ULILOLIAMINI + NGUVU YA HIYO ROHO]

NEEMA =  [NENO + ROHO YA NENO + NGUVU ZA HIYO ROHO] ZIKITENDA KAZI NDANI YAKO, NA PIA KUPITIA WEWE KWA WENGINE UNAOWAHUDUMIA

>> KUTOAMINI NI KUJINYIMA

1) roho ya hilo neno

2) maisha ya hilo neno ama uzima wa hilo neno

3) kila baraka iliyomo ndani ya hilo neno

>> KUTOAMINI NI KUJINYIMA NEEMA YA MUNGU MAISHANI MWAKO 

>> NA PASIPO NEEMA YA MUNGU HUWEZI KUFANYA LOLOTE LA MUNGU 

>> KWA SABABU MAPENZI YA MUNGU YANAFANYWA KWA NEEMA YA MUNGU AMBAYO NI ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE ZA HILO NENO ULILOLIAMINI!!

>> DAUDI ALISEMA,

Zaburi 119:11

[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, 

Nisije nikakutenda dhambi. 

Thy word have I hid in mine heart, that I might not sin against thee.

>> HII INAMAANISHA DAUDI ALIJAA ROHO YA HILO NENO ALILOLIPENDA/ALILOLIHESHIMU/ALILOLIKUBALI/ALILOLIPOKEA MOYONI MWAKE/ ALILOLITUNZA ROHONI MWAKE, NA NGUVU ZAKE ILI ASIMTENDE MUNGU DHAMBI 

>> ROHO NA NGUVU ZA NENO NDIZO NGUVU ZA KULIISHI NA KULITENDA NENO NA HAYO NDIYO MAISHA YA UTAKATIFU!!

>> TOBA YA MTAKATIFU NI TOBA YA UTAKASO ILI KUZIDI KUJAA KWA LENGO KIKOMBE CHAKO KIFURIKE!! KIKOMBE NI ROHO YAKO! KIKOMBE NI MOYO WAKO!! JAA NENO LA IMANI MOYONI MWAKO, MAANA KWA MOYO MTU HUAMINI!!! KISHA TAMKA, SEMA, ONGEA, KIRI, SHUHUDIA, TANGAZA NENO ILI MUNGU ATUKUZWE!! MAANA KINYWA CHA MTU HUNENA YAUJAZAYO MOYO WAKE!

Waefeso 5:18

[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 

And be not drunk with wine, wherein is excess; but be filled with the Spirit;

>> JAZWA ROHO KWA KUJAZWA  NENO UNALOLIAMINI!! WENGI HAWAJAI ROHO KWA SABABU HAWAAMINI NA/AU HAWAENDELEI KUKUA NA KUONGEZEKA KIIMANI!!

>> KUONGEZEKA KIIMANI KUNAONEKANA UNAPOLITENDEA KAZI NENO LILILOMO TAYARI NDANI YAKO KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU!!

>> WAEFESO 5:18 MUNGU ANAKUTAKA UENDELEE KUJAZWA ROHO KWA NJIA HII :

Wakolosai 3:16

[16]Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 

Let the word of Christ dwell in you richly in all wisdom; teaching and admonishing one another in psalms and hymns and spiritual songs, singing with grace in your hearts to the Lord.

Psalms 119:11 (NLT)  I have hidden your word in my heart, that I might not sin against you.

11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. 

Zaburi 119:11

>> UKIJAA NEEMA YAKE KRISTO YESU, YAANI,  NENO LAKE, ROHO WAKE, NA NGUVU ZAKE HUWEZI KAMWE KUTENDA DHAMBI  NA SHETANI HANA KITU KWAKO!!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post