NINI HII BASHASHA KUHUSU MWAKA MPYA?! TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO VINGINEVYO.....!
>> VIPI HALI YA NDOA YAKO? AKIRUDI YESU SASA HIVI UTAONDOKA? MAMBO YAKO SHWARI NA MKEO AU MUMEO? UNASHEHEREKEA MWAKA MPYA WA UASI??!!
>> VIPI UTAKATIFU WAKO, HAUNA LAWAMA MBELE ZA MUNGU? UNAPATA HELA ZA HALALI? HAUCHEZI DILI HARAMU? HAUTOI RUSHWA? HAUFANYI BIASHARA HARAMU KIMAANDIKO?! HAUTAPELI WATU? HAUGHUSHI KAZINI KWAKO? HAUDHULUMU AU KUPUNJA WENGINE? HAUNYIMI WATU HAKI ZAO? ULIOWAAJIRI KAZINI NA NYUMBANI NA KANISANI UNAWALIPAJE NA KUWATENDEAJE? FEDHA YAKO NI FEDHA HALALI? HAITOKANI NA MAOMBEZI YA MITUME NA MANABII WA UONGO?! UNAFANYA UKAHABA ILI KUTAJIRIKA?
>> VIPI UHUSIANO WAKO NA WAZAZI WAKO WA KIROHO NA WA KIMWILI? HAMJAGOMBANA? UNA UHUSIANO MZURI NAO? WANAKUFURAHIA ADABU, HESHIMA NA HUDUMA ZAKO KWAO??!! AU WANAUGUA MIOYONI MWAO KWA AJILI YAO?
>> MAHUSIANO YAKO MENGINE YAKOJE?! KUNA WATU HUONGEI NAO, SIYO? MMENUNIANA, SIYO? KUNA WATU HUTAKI HATA KUWAONA, SIYO? KUNA WATU UMEAPA KUTOWASAIDIA KAMWE HATA WAWE NA SHIDA GANI, SIYO? KUNA WATU UNA KISASI NAO, SIYO? YAANI, KUNA WATU HUJAWASAMEHE NA HUTAKI KUWASAMEHE, SIYO? JE! UNALIPA KISASI? JE! UNALIPA BAYA KWA BAYA AU JEMA KWA BAYA? UNAFANYA HAYA YALIYOANDIKWA HAPA CHINI??!!
Warumi 12:17-21
[17]Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
Recompense to no man evil for evil. Provide things honest in the sight of all men.
[18]Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
If it be possible, as much as lieth in you, live peaceably with all men.
[19]Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Dearly beloved, avenge not yourselves, but rather give place unto wrath: for it is written, Vengeance is mine; I will repay, saith the Lord.
[20]Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Therefore if thine enemy hunger, feed him; if he thirst, give him drink: for in so doing thou shalt heap coals of fire on his head.
[21]Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Be not overcome of evil, but overcome evil with good.
>> JE! UNAWAPENDA ADUI ZAKO? KAMA HUWAPENDI ADUI ZAKO UNAMFUATA SHETANI KINYUME NA NENO LA MUNGU
27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
Luka 6:27
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
Luka 6:28
29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Luka 6:29
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
Luka 6:30
31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
Luka 6:31
32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
Luka 6:32
33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
Luka 6:33
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
Luka 6:34
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
Luka 6:35
>> KUNA WEWE UNAONA FAHARI KUTOKA NJE YA NDOA, SIYO? HUNA HOFU YA MUNGU HATA KIDOGO UNAPOTENDA DHAMBI UKIDHANI UTAKUWA SALAMA MWAKA 2024 NA MILELE YOTE PASIPO KUGUSWA NA MUNGU WALA MWANADAMU, SIYO? NDIVYO, UNAVYOFIKIRI HIVI, SIYO?
>> KUNA WEWE UNAABUDU MAHALI FULANI, KWENYE DINI FULANI, NA DHEHEBU FULANI, UNATENDA MEMA HUKU NA KULE, MICHANGO MBALIMBALI HUKOSI, UNAONEKANA MTU WA DINI SANA, INAWEZEKANA NI KIONGOZI HAPO UNAPOABUDU, AU MTU MUHIMU, LAKINI HUJAOKOKA, NA MNAPINGA KUOKOKA WAKATI MUNGU AMEMTUMA MWOKOZI ULIMWENGUNI, NA UNASEMA HAKUNA MKAMILIFU WALA MTAKATIFU!! JINSI GANI UMEDANGANYWA? UNATAKA KUTUBU UKIWA JEHANAMU??!! MAANDIKO YANASEMA BAADA YA KUFA INAFUATA HUKUMU!! ( WAEBRANIA 9:27)! KUOKOKA NI SASA HAPA DUNIANI!!
2 Wakorintho 6:2
[2](Kwa maana asema,
Wakati uliokubalika nalikusikia,
Siku ya wokovu nalikusaidia;
tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)
(For he saith, I have heard thee in a time accepted, and in the day of salvation have I succoured thee: behold, now is the accepted time; behold, now is the day of salvation.)
HAKUNA ATAKAYEINGIA MBINGUNI KWA SABABU YA MATENDO MEMA UYATENDAYO PEKE YAKE!!! LAZIMA UOKOKE KWANZA KISHA MATENDO HAYO MEMA YATAKUWA KAMA VAZI KWAKO NA UTAPEWA THAWABU NA BWANA YESU MBINGUNI BAADA YA UNYAKUO!! KORNELIO ANAKUZIDI SANA KWA SIFA ZAKO HIZO (Matendo ya Mitume 10:1-2) LAKINI ALIKUWA HAJAOKOKA!! MUNGU AKAMHURUMIA, AKAMTUMIA MALAIKA ILI AMWITE MHUBIRI AJE KWAKE AISIKIE INJILI, AMBAYO ILIPELEKEA YEYE NA NYUMBA YAKE KUOKOKA!! NA WEWE LAZIMA UOKOKE ILI MATENDO MEMA YAKO YAWE NA FAIDA KWAKO!! VINGINEVYO UTAPOTEA NA MATENDO MEMA YAKO YOTE!! YESU NDIYE ANAYEOKOA NA SI MATENDO MEMA YAKO!!
Mathayo 1:21
[21]Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
And she shall bring forth a son, and thou shalt call his name JESUS: for he shall save his people from their sins.
>> NIMESEMA NA WEWE UNAYESHEHEREKEA MWAKA MPYA UKIWA MUASI BADO! UNASHEHEREKEA KUKATAA KUMTII MUNGU, UNASHEHEREKEA KUKATAA KUITII KWELI, UNASHEHEREKEA KUMKATAA MWOKOZI!!
>> BAADA YA KUMKATAA UMETABIRIWA MAFANIKIO NA WATUMISHI WA SHETANI ILI UENDELEE DHAMBINI, SIYO? BIBLIA HAISEMI HIVYO!! INASEMA;
16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
Isaya 1:16
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Isaya 1:17
18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Isaya 1:18
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Isaya 1:19
20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
Isaya 1:20
>> UKIKATAA NA KUASI HAYO ULIYOYASIKIA KUNA KUANGAMIA KWA UPANGA WA NENO HILO!!! WANAOASI HUWA WANAYAITA MAANGAMIZO NA SIYO MAFANIKIO!! TUBU!!
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
Mathayo 6:31
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
Mathayo 6:32
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Mathayo 6:33
>> UNAYOYATAKA YA MWILINI NI ZIADA UTAKAYOZIDISHIWA BAADA YA KUUPATA KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE!! PONYA ROHO NA NAFSI YAKO KWANZA!!
>> MWAKA MPYA KIUMBE KIPYA!
2 Wakorintho 5:17
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Therefore if any man be in Christ, he is a new creature: old things are passed away; behold, all things are become new.
>> JE! UTAENDELEZA JITIHADA ZAKO ZA KUITAFUTA JEHANAMU ILI UKAJUTE MILELE, UKATESEKE MILELE, UKALIE MILELE, UKASAGE MENO MILELE, KWA SABABU KIBURI CHAKO KILIKUZUIA KUNYENYEKEA NA KUTUBU NA KUOKOKA??!!
>> HERI YA MWAKA MPYA 2024, MWAKA WA KUMCHA BWANA!!